Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live

SHOW YA MIC TATA KUTIKISA UKUMBI WA DAR LIVE MBAGALA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
RADIO Uhuru imeandaa show  MIC TATA itakayowashirikisha wasanii mbalimbali nchini itakayofanyika Februari 24 katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Michuzi Blog, Afisa Uhusiano , Sheila Simba  amesema kuwa show siyo ya kukosa kutokana na wasanii walivyojipanga katika kukutanisha wasanii mbalimbali .
Sheila amesema kuwa radio uhuru kufanya show hiyo  ni mwendelezo wa show zingine ikiwa ni kukutanisha wasanii mbalimbali kutoa burdani kwa mashabiki wao.Wasanii watakaotumbiza katika Mic Tata ni Joe Makini , Inspekta Haruni , Manifongo , Dulla Makabila  na Amigo wa Tarabu  huku kiingilio ikiwa ni sh. 5000
Afisa Uhusiano wa Radio Uhuru, Sheila Simba akizungumza na Michuzi Blog kuhusiana na Radio hiyo kuandaa show Mic Tata itakayofanyika Februari 24 katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam, Mtayarishaji wa Vipindi, Richichard Ricomoco


MADINI YA RUBY KUENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI LONGIDO

$
0
0
Na Veronica Simba – Loliondo
Serikali imewaahidi wakazi wa Kata ya Mundarara katika Wilaya ya Longido kuwa itahakikisha madini ya Ruby ambayo yanapatikana katika eneo hilo yanaendelea kuwanufaisha na siyo kuwadidimiza.
Ahadi hiyo ilitolewa jana, Februari 13 na Naibu Mawaziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Dotto Biteko baada ya kufanya ziara katika Mgodi unaojishughulisha na uchimbaji wa madini hayo na kisha kuzungumza na wananchi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Nyongo na Biteko waliwataka wananchi wa Mundarara kuondoa hofu kuwa neema ya madini hayo yanayopatikana katika maeneo yao haitawanufaisha tena kutokana na kile wanachodai kuwa sheria mbalimbali zilizowekwa na Serikali zinasababisha kupungua kwa Soko lake.
Akizungumza na wananchi hao, Naibu Waziri Biteko aliwaambia kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini inaandaa mwongozo maalum utakaobainisha utaratibu unaopaswa kutumika katika biashara ya kila aina ya madini hapa nchini ili yaweze kuwanufaisha wananchi na Taifa ipasavyo.
“Nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha rasilimali zote zinazopatikana nchini yakiwemo madini, zinalinufaisha Taifa kwa kiwango kinachostahili. Kwa muda mrefu tumekuwa tukiibiwa sana na watu wengine kunufaishwa na rasilimali zetu wenyewe ilhali sisi tunazidi kuwa maskini. Sasa tumeamua kuwa hatutaki kuibiwa tena,” alisisitiza.
Akifafanua zaidi, Biteko alisema kwamba, mwongozo huo unaoandaliwa na Serikali utasaidia hata wananchi wanaozungukwa na Migodi ya Madini kunufaika zaidi.
Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza na wananchi wa Kata ya Mundarara Wilaya ya Longido, baada ya kufanya ziara katika Mgodi unaochimba madini ya Ruby eneo hilo Februari 13 mwaka huu. Biteko aliambatana na Naibu Waziri Stanslaus Nyongo (hayupo pichani)
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza na wananchi wa Kata ya Mundarara Wilaya ya Longido, baada ya kufanya ziara katika Mgodi unaochimba madini ya Ruby katika eneo hilo, Februari 13 mwaka huu. Nyongo aliambatana na Naibu Waziri Dotto Biteko (hayupo pichani)
Sehemu ya umati wa wananchi wa Kata ya Mundarara wilayani Longido, wakiwa katika Mkutano wa Naibu Mawaziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Dotto Biteko (hawapo pichani), walipofanya ziara katika Mgodi unaochimba madini ya Ruby katika eneo hilo, Februari 13 mwaka huu na kuzungumza nao.
Naibu Mawaziri wa Madini Dotto Biteko na Stanslaus Nyongo wakizungumza na wawekezaji wa Mgodi wa Madini ya Ruby katika Kijiji cha Mundarara wilayani Longido, Februari 13 mwaka huu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Benki ya CRDB yaboresha maslahi ya wafanyakazi wake

$
0
0
Benki ya CRDB yasaini mkataba wa hali bora kwa wafanyakazi wake na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya Ramada Encore iliyopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Menejimenti ya Benki ya CRDB na Viongozi wa TUICO.

Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei alisema mbali na kusaidia kuongeza morali na motisha ya utendaji kazi kwa wafanyakazi, mkataba huo wa hali bora utakwenda kusaidia kuongeza ustawi kwa wafanyakazi na familia zao na hivyo kuboresha maisha yao kwa ujumla.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (katikati) pamoja na Mkuu wa Sekta ya Fedha -TUICO Tanzania, Willy Kibona (kushoto) wakisaini Mkataba wa Makubaliano wa hali bora za Wafanyakazi kati ya Benki ya CRDB na Taasisi ya Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO) katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es salaam leo Februari 15, 2018. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB, Dorah Ngaliga.

"Ustawi wa wafanyakazi ni muhimu sana kwetu na tunajitahidi kuhakikisha tunatoa kipaumbele katika hili. Mkataba huu utakuwa ni wa kipindi cha miaka mitatu tangu tarehe ya utiaji saini ambapo kuna mambo 19 ambayo kwa pamoja tumeyaridhia na kuyapitisha”, alisema Dkt. Kimei.

Dkt. Kimei alisema katika mkataba huo wa hali bora kwa wafanyakazi, Benki ya CRDB imetoa kipaumbele katika kuboresha afya za wafanyakazi wake. “Benki ya CRDB imekuwa ikichangia asilimia 100 katika huduma za matibabu kwa wafanyakazi wake, tunajivunia sana kwa hilo. Kutokana na mafanikio na umaarufu wa mpango huu tunaoutumia, tumeamua kuboresha zaidi ahadi yetu kwa wafanyakazi wetu mara nyingine tena, "alisema Dkt. Kimei.
Dkt. Kimei alisema kwa upande wa huduma za afya, wafanyakazi wa Benki ya CRDB sasa wameongezewa huduma nyingine ikiwamo huduma za macho na miwani pamoja na huduma ya matibabu kwa wastaafu na wategemezi wao kupitia Shirika la Bima ya Afya ya Taifa (NHIF). Hii inamaanisha kuwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB wataendelea kutibiwa kama bado wapo kazini pindi wakistaafu.

Baadhi ya mambo mengine ambayo yaliridhiwa katika mkataba huo wa hali bora kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB ni pamoja na utaratibu mpya wa uthibitishwaji wa wafanyakazi kazini, utaratibu ulioboreshwa wa kushughulikia migogoro ya kikazi, utaratibu wa likizo ya ugonjwa, utaratibu wa likizo ya uzazi, utaratibu wa mazishi ambapo sasa Benki hiyo itagharamia mazishi ya wazazi wa mfanyakazi, mtoto wa kuzaliwa wa mfanyakazi, au aliyeasiliwa pamoja utaratibu wa utoaji tuzo kwa wafanyakazi wa Benki hiyo.

Akimalizia hotuba yake Dkt. Kimei alisema Benki CRDB pia imeanzisha Kamati za Ustawi wa Wafanyakazi katika matawi yake yote kwa ajili ya kubuni na kuratibu programu na shughuli mbalimbali zinazolenga kukuza ustawi wa wafanyakazi na familia zao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akibadilishana Mkataba wa makubaliano na Mkuu wa Sekta ya Fedha -TUICO Tanzania, Willy Kibona (wa pili kushoto) hali bora za Wafanyakazi kati ya Benki ya CRDB na Taasisi ya Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO) katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Ramada, jijini Dar es salaam leo Februari 15, 2018.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza jambo katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es salaam leo Februari 15, 2018.
Baadhi washiriki 

Attorney General Dr Adelardu Kilangi pays courtesy call on African Court in Arusha

$
0
0
Tanzania’s Attorney General Dr Adelardu Kilangi admires the just-released first volume of the African Human Rights Yearbook at the African Court in Arusha, Tanzania, today 15th February 2018. Left is the President of the Court Hon. Justice Sylvain Oré and in the middle is the Registrar of the Court, Dr Robert Eno. Dr Kilangi paid a courtesy on the president and to familiarise with the court’s activities.

Tanzania’s Attorney General Dr Adelardus Kilangi today 15th February 2018 paid a courtesy call on the President of the African Court Hon. Justice Sylvain Oré (r) in Arusha, Tanzania, to familiarise with its activities.

MICHUZI TV LIVE: MKUTANO WA KAMPENI ZA UBUNGE CCM JIMBO LA KINONDONI LEO TAREHE 14/02/2018 MAGOMENI DUNGUMBI

RAIS MAGUFULI AMUAPISHA LUTENI JENERALI YAKUBU HASSAN MOHAMED KUWA MNADHIMU MKUU WA JWTZ

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha cheo kipya Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed ambapo awali alikuwa na cheo cha Meja Jenerali kabla hajamuapisha kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed akizungumza mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati Maafisa Mbalimbali wastaafu wa (JWTZ) walipokuwa wakizungumza mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed pamoja na Maafisa wengine wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi ambao wamepandhishwa vyeo kutoka Cheo cha Brigedia Jenerali na kupewa cheo kipya cha Meja Jenerali Ikulu jijini Dar es Salaam. 
PICHA NA IKULU

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

HUKUMU KESI YA MASOGANGE KUTOLEWA FEBRUARI 21 MWAKA HUU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Februari 21 mwaka huu, inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Video Qeen Agnes Gerald  'Masogange'

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ndio atakayesoma hukumu hiyo baada ya upande wa mashtaka uliowakilishwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula kuwaita mashahidi watatu kutoa ushahidi dhidi ya Masogange na kuufunga huki mshtakiwa akijitetea mwenyewe.

Kabla ya kutolewa kwa tarehe ya hukumu, Masogange akiongozwa na Mawakili wake, Nehemiah Nkoko na Ruben Simwanza,  ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imuachie huru kwa sababu hana kosa lolote.

Akitotoa utetezi wake,Leo mahakamani hapo Masogange  anayekabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam, amedai yeye hajawahi kutumia dawa za kulevya hata siku moja.

Amedaimbali ya kuwa Video Qeen yeye alikuwa ni mfanyabiashara wa nguo.

Alidai Februari 14, mwaka jana polisi walipoenda nyumbani kwake, yeye hakuwepo, alikuwepo dada yake, yeye alikuwa amempeleka mjomba wake kununua vitu Ocadeco.

Alidai, Polisi hao walimuweka chini ya ulinzi dada yake na kumtaka ampigie simu na ajifanye anaumwa ili arudi nyumbani lakini baada ya kupigiwa simu, alirudi nyumbani Kwake saa 12 jioni.

Ambapo alipofika getini kabla hajashuka kwenye gari alimuona mlinzi amekaa na watu wanne, aliwasalimia na kuingia ndani.

Aliendelea kudai ilipofika ndani alimkuta dada yake na askari wa kike na askari wawili wa kiume, walimueleza wanasubiri yeye na wakajitambulisha kuwa wao ni polisi ambao walimuuliza kuwa wamekwenda kufanya upekuzi,

Alidai baada ya upekuzi huo, alichukuliwa na kupelekwa kituo cha polisi cha kati na walipofika mapokezi akaandikisha jina na wakampeleka rumande ambapo alikaa siku tisa.

Alidai baada ya mahojiano polisi alipelekwa Mwananyamala ambapo alioneshwa picha mbili za wanaume wawili, akaulizwa kama anawafahamu na kuwaeleza kuwa hawafahamu.

Alidai baada ya hapo alipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kupimwa mkojo akiwa chini ya ulinzi wa askari wa kike, afande Judy na baadae akarudishwa Polisi.

" Mheshimiwa Mimi sijawahi kutumia dawa za kulevya hata siku moja nipo tayari hata mahakama yako ijiridhishe kwa kunipima." alieleza Masogange.

Katika kesi hiyo  Masogange anadaiwa kati ya February 7 na 14,mwaka  2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).

Pia anadaiwa kati ya February 7 na 14, mwaka 2017 alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam

KAMATI YA MASHINDANO YAWAADHIBU KASEKE, DIHILE

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KAMATI ya Mashindano ya TFF imewafungia Deus Kaseke na Shaban Dihile kwa makosa ya utovu wa nidhamu waliyoyafanya katika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho la Azam (FA).

Tukio hilo walilifanya wote kwa pamoja wakati wa mchezo wao kati ya Green Warriors na Singida United uliofanyika kwenye dimba la Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Kikao cha Kamati ya mashindano kilichokutana Februari 13 mwaka huu pamoja na mambo mengine iliweza kupitia  taarifa za mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam kati ya Green Warriors na Singida United ambapo wachezaji Deus Kaseke wa Singida United na Shaban Dihile wa Green Warriors wamefungiwa mechi tatu (3) na faini ya Sh.500,000 kila mmoja kwa kosa la kutoingia uwanjani na timu zao na hawakuwepo wakati timu hizo zikipeana mikono kwenye mchezo uliozikutanisha timu hizo Januari 31,mwaka 2018 mchezo namba 73 uliochezwa Azam Complex Chamazi.

Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya ASFC(1) ambayo inaelekeza kutumika kanuni ya ligi husika na hivyo kanuni iliyotumika ni 37(7d).

Mbali na hilo, mchezaji wa Singida United Kambale Salita amepelekwa kwenye Kamati ya nidhamu ya TFF kwa kosa la kumpiga mchezaji wa timu pinzani kwenye mchezo huo

REHMTULAH: NIMEANZISHA KIWANDA NDANI YA MIAKA 10

$
0
0
Na Agness Francis, Globu ya jamii 
MBUNIFU wa mavazi nchini Ally Rehmtulah ameweka wazi mafanikio na changamoto alizopitia ndani ya miaka 10 katika   kuendeleza sanaa ya ubunifu hapa nchini.. 

Akizungumza nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Rehmtulah amesema Mama wa mitindo nchini Asia Idarous ndiye aliyeng'arisha nyota yake  kwa kumshika mkono kwa kumpa fursa ya kwanza kuonesha shoo ya mavazi yake kwa watanzani katika tamasha la Lady in read. 

"Baada ya hapo watanzania walianza kunikubali  ndio nikaanza kufanya shoo zangu sehemu mbalimbali ikiwepo kusafiri nje ya nchi nilihangaika sana kuanza kushona nguo.

 "Naenda Kariakoo kutafuta vitambaa na mafundi popote pale wa kushona nguo, vile vile pia nilifanikiwa kufanya kazi Landani fashion week,Rwanda, Uganda na Kenya.Hiyo yote ni kuhangaika tu kutafuta soko sehemu tofauti tofauti,"amesema Rehmtulah. 

Aidha amesema tokana na changamoto hizo imemfanya kufungua kampuni yake ya kiwanda cha utengenezaji wa nguo kwa kuona anapata oda nyingi kutoka nje ambapo haikuwa na uwezo wa kuweza kukamilisha oda hizo kutokana na ukosefu wa viwanda hapa nchini. 

"Nimeamua kuanzisha kiwanda kidogo ilikuweza kukamilisha ubora wa  oda nazopata kutoka soko la nje.

"Na hadi mpaka sasa naimeajiri watu 11 unafanyanao kazi nawalipa kwa wakati nalipa kodi na hata NSSF kwa kila mfanya kazi wangu,"amesema  Rehmtulah.
Mwanamitindo Ally Rehmtulah akizungumzia mafanikio na changamoto aliyoyapitia ndani ya mika 10 ya tasnia ya ubuni wa mavazi leo Nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam..

WAKALA VYUO VIKUU VYA NJE AIOMBA SERIKALI KUANGALIA MFUMO HATI YA KUSAFIRIA KWA WANAFUNZI

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Wakala  ya Vyuo Vikuu vya Nje ya Darwin, Joseph Makungu amesema mfumo mpya wa hati ya kusafiria unapaswa kuwangalia wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya nje ambao hawana sifa ya kupata hati hiyo kutokana kutofikisha miaka 18 ya kuweza kupata hati hizo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi huyo amesema mamlaka zinazotoa vitambulisho ni vema kuangalia kundi hilo ili kupata hati ya kusafiria pale wanapohitaji kwa ajili ya masomo katika vyuo vikuu vya nje.

Amesema hati ya kusafiria ambayo imeanza kutolewa ni ya viwango vya kimataifa ambapo Tanzania imeweza kuthubu katika kwenda na wakati.

Makungu amesema wakala wa vyuo vikuu vya nje  kutokana na mfumo wa hati ya kusafiria kwa idara ya uhamiaji kuweza kuwapa elimu juu ya mfumo wakaulewa ili mbele ya safari wasipate usumbufu kwa wanafunzi pale wanapotaka kusafiri kwa masomo katika vyuo vikuu vya nje.
Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Uwakala wa Vyuo Vikuu vya Nje, Joseph Makungu akizungumza na waandishi habari kuhusiana na mfumo wa Hati ya Kusafiria, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mahiga afanya mazungumzo na Wabunge wa EALA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe. Balozi Dkt.Augustine Mahiga akizungumza na Wabunge
wa EALA (hawapo pichani)
Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA)  leo wamekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt.Augustine Mahiga Wizarani mjini Dodoma. Wabunge wa EALA wamewasili mjini Dodoma wakiwa katika ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya Jumuiya inayotekelezwa na nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Masharaiki. 
                         
Katika ziara hii Wabunge wanatembelea miradi inayotekelezwa katika ushoroba wa kati (central corridor) sambamba na kubaini changamoto zinazoikabili miradi hiyo na namna inavyorahisha utoaji huduma kwa wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Katika mazungumzo yao na Waziri Mahiga, Wabunge wa EALA wameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utekelezaji mzuri wa miradi inayotokana na makubaliano ya Jumuiya kama vile ujenzi wa mizani za kisasa sambamba  na kupunguza idadi ya mizani hiyo ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa, hudumu na watu ndani Jumuiya.

Hadi sasa Tanzania kwa upande wa ushoroba wa kati imefanikiwa kupunguza idadi ya vituo vya mizani kutoka  vituo saba hadi vitatu.

Kwa upande wake Waziri Mahiga, amewapongeza Wabunge wa EALA kwa kuona umuhimu wa kutembelea miradi ya Jumuiya inayotekelezwa na nchi Wanachama ambayo inagusa maisha ya wananchi moja kwa moja. Aidha amesema katika ziara hii Wabunge wataweza kubaini changamoto zinazowakabili wananchi, hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kutatua changamoto hizo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao Bungeni.

Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari walipotembelea ofisi za Wizara mjini Dodoma. Kulia ni  Mhe. Wanjiku Muhia  kutoka Kenya ambaye pia ni kiongozi wa msafara wa ziara hiyo
Mhe. Adam Kimbisa Mbunge wa EALA (Tanzania) akizungumza wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari.



Mkutano ukiwa unaendelea

WAUZAJI WA PIKIPIKI WA WATAO MSAADA KWA MAJERUHI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Kampuni ya King Lion imetoa msaada wa waendesha bodaboda  waliopata ajali na wamelazwa katika Hospitali Taifa ya Muhimbili

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukakabidhi  msaada huo Afisa Uhusiano na Masoko, Erasto Baragamba amesema kuwa kama kampuni inatambua umuhimu wa waendesha bodaboda  hivyo wanatoa mchango ambao utasaidia kujisitili.

Msemaji wa waendesha bodaboda Wilaya ya Ilala, Abdallah Bakari amesema wanashukuru kinglion kwa msaada walioutoa.

Amesema waendesha bodaboda wazingatie sheria za usalama barabarani ili kuweza  kuepukana na ajali zinazotokana na makosa ya kibinadamu.
 Msemaji wa waendesha bodaboda wa Manispaa ya Ilala, Abdallah Bakari akizungumuza  na waandishi  habari kuhusiana msaada kwa waendesha bodaboda waliopata ajali na wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Msemaji wa waendesha bodaboda wa Manispaa ya Ilala, Abdallah Bakari  akikabidhiwa msaada kutoka kwa Afisa Uhusiano na Masoko, Erasto Baramamba.

MAJALIWA AZINDUA MADARASA SHULE YA SEKONDARI NYEHUNGE WILAYANI SENGEREMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua madarasa ya Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Secondari ya Nyehunge wilayani Sengerema Februari 15, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Watatu kushoto ni Waziri wa Kilimo , Dkt. Charles Tizeba na wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, Dkt. Anthony Diallo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua darasa wakati alipozindua madarasa ya Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Secondari ya Nyehunge wilayani Sengerema, Februari 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Dkt. Flavian Kassala baada ya kuweka jiwe la msing la hospitali ya Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Februari 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vitanda wakati alipokagua Bweni lililopewa jina la Dkt.John Pombe Magufuli katika Shule ya Secondari ya Nyehunge wilayani Sengerema Februari 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MGODI WA ACACIA BULYANHULU WAENDELEA KUSHIRIKIANA NA JAMII MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu umezindua na kukabidhi maktaba iliyogharimu shilingi milioni 22.6 kwenye shule ya sekondari Bulyanhulu iliyopo katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani wa Shinyanga kwa lengo la kusaidia wanafunzi na walimu katika kuboresha ubora wa elimu inayotolewa.

Maktaba hiyo imezinduliwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Msalala Bw , Simon Berege na kuhudhuriwa na kaimu Meneja mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu,Elias Kasitila.

Akizungumza wakati uzinduzi huo, Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi Bulyanhulu,Elias Kasitila alisema wakati wakitafakari namna ya kuinua taaluma ya wanafunzi waliona ni vyema wakaimarisha usomaji wa wanafunzi kwa kuwekeza kwenye maktaba ambayo itasaidia kuboresha upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi kutoka kwa jamii inayouzunguka mgodi huo.

Alisema kupitia mpango wa Acacia wa maendeleo ya jamii wameamua kushirikiana na shirika la kimataifa la Read International kuboresha jengo moja la shule hiyo na kuliwekea samani kwa ajili ya matumizi ya maktaba ambayo itawasaidia wanafunzi na walimu kwa kiasi kikubwa.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala ,Simon Berege akikata utepe kuzindua rasmi jengo la maktaba katika shule ya sekondari Bulyanhulu. Kaulia ni kaimu Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Elias Kasitila.Na katikati ni Mwakilishi wa shirika la Read International ,Esther Kalwinzi .
Muonekano wa jengo la maktaba katika shule ya sekondari Bulyanhulu lililoboreshwa na mgodi wa Bulyanhulu kwa kushirikiana na Read International . 
Mwakilishi wa shirika la Read International ,Esther Kalwinzi akionesha sehemu ya kuangalia orodha ya aina za vitabu vilivyopo katika maktaba kwa mkurugenzi wa halmashauri ya msalala , Simon Berege . 

KWANDIKWA AKAGUA MIRADI YA UJENZI MKOANI TANGA

$
0
0
Diwani wa Kata ya Mombo, Halima Mussa akizungumza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa (wa pili kulia) wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya sekta ya ujenzi ikiwemo barabara katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Mombo ikiwemo stendi ya Mombo jana Jumatano Februari 14, 2018. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyan
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (katikati) akiongozwa na Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani (wa pili kulia) na Diwani wa Kata ya Mombo, Halima Mussa (kushoto) kukagua kipande cha barabara kilichopo katika stendi ya Mombo ikiwa ni sehemu yake ya kukagua miradi ya barabara katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tanga jana Jumatano Februari 14, 2018.
Diwani wa Kata ya Mombo iliyopo Korogwe Mkoani Tanga, Halima Mussa akimpa maelezo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (kulia) kuhusu kuharibika kwa mtaro wa kupitisha maji machavu na uchakavu wa miundombinu ya barabara katika eneo la soko lililopo katika stendi ya Mombo Wilayani Korogwe jana Jumatano Februari 14, 2018. Wa pili kushoto ni Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani.


MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA MAJENGO YA MAHAKAMA MKOANI MARA

$
0
0
Pichani ni muonekano wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Robanda lililopo Serengeti wilayani Mugumu, jengo hili lilijengwa kwa nguvu za wananchi na kumaliziwa na Mahakama ya Tanzania lilikabidhiwa rasmi tayari kwa matumizi Januari 26, 2018, uwepo wa jengo hili utasaidia kuwapunguzia wananchi aza ya kusafiri kilomita zipatazo 40 kwenda Mahakama ya Mwanzo Serengeti kutafuta haki zao.
Maafisa Tawala wa Mahakama mkoani Mara wakionyesha baadhi ya ofisi za jengo hilo; hapo ni sehemu ya ukumbi wa Mahakama hiyo ‘court room’ ambayo ina ukubwa wa kutosha wa kuwawezesha wananchi wenye kesi kusikiliza kesi zao bila usumbufu.
Muonekano wa Ukumbi wa Mahakama ‘court room’

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN MGEMI RASMI KWENYE MAHAFALI YA 13 YA SUZA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Dk. Ali Mohamed Shein pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) akihutubia wakati wa hafla ya Mahafali ya 13 ya Chuo hicho yaliofanyika katika ukumbi mpya wa SUZA wa Dk Ali Mohamed Shein.(Picha na Ikulu).

BAADHI ya Wakufunzi na Wahitimu wa Mahafali ya 13 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) (Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar(SUZA) Dk. Ali Mohamed Shein, akimtunuku Shahada ya Uzamivu ya Kiswahili Salma Omar Hamad, wakati wa hafla ya Mahafali ya 13 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar ( SUZA) jumla ya wahitimu watano wametunukiwa Shadaha hiyo.
WAHITIMU wa Shahada ya Uzamivu ya Kiswahili wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) wakati akihutubia na kutowa nasaha zake kwa wahitimu wa mahafali ya 13 ya SUZA.

MKAZI WA SOMBETINI MOHAMEDI HAMISI ANAOMBA MSAADA.

$
0
0
 Mohamed Hamisi ni mkazi wa Sombetini. Ana umri wa miaka 24. Ni mtoto wa marehemu Hamisi Faustine. Ni mlemavu wa miguu na mkono mmoja pia una shida. Hapendi kuomba, anapenda kujishughulisha. Kwa sasa anafanya vikazi vidogo vidogo vya kuweka tinted kwenye magari lakini anakabiliwa na changamoto kadhaa.

  Anatamani  kuwa na biashara nyingine ndogo ili aweze kuongeza kipato kuwasaidia wadogo zake watano ambapo mdogo kabisa ana miaka minne.
   Anaomba msaada afungue ofisi yake ili achanganye kazi zake ya kuweka tinted (maana sasa anafanya kwa mtu) na pia ofisi hiyo ataweza kuongeza biashara nyingine ya kuuza na kuburn VCD, kuuza mitumba vocha na kadhalika. Pia baiskeli yake ni nzito, ni ya mbao na chuma hasa ukizingatia anatumia mkono mmoja zaidi.

Ombi langu kwenu.
 
Tumkopeshe mungu kupitia kijana huyu tukiamini ni jukumu letu kama jamii kumsaidia. Namba yake ni +255768924516 inapokea M-pesa na jina la YUKI HAMISI. Pia mnaweza kumpigia kumsikiliza zaidi.🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼


RAIA WA KIGENI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA BAADA YA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Na Dixon Busagaga,Moshi.

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania ,Kanda ya Moshi ,imemuhukumu kifungo cha maisha jela ,Christina  Biskasevskaja (26) raia wa nchi ya Lithuania baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin na Hydrochloride kinyume cha sheria .

Hukumu hiyo imetolewa jana Mahakama kuu ya Tanzania ,Kanda ya Moshi  na Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu ,Aishieri Sumari ambapo upande wa utetezi ulikuwa ukiwakilishwa na Mawakili Patrick Paul na Gwakisa Sambo huku upande wa jamhuri ukiwakilishwa na Jopo la Wanasheria wa serikali wakiongozwa na Tamari Mndeme .

Akisoma hukumu ,Jaji Sumari alieleza kuwa mahakama imejiridhisha kupitia ushahidi usio na shaka uliowasilishwa na mashahidi wapatao saba wa upande wa Jamhuri unlimtia hatiani mshtakiwa huyo ambao ulieleza kukutwa na Dawa hizo zikiwa na uzito wa gramu 3775.26 na thamani ya sh za kitanzania Mil 169,886,700.

Biskasevskaja ambaye pia anatajwa kuwa msanii wa Muziki  alikamatwa Agosti ,28 mwaka 2012  majira ya saa 9:16 za mchana katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) wakati akijiandaa kuelekea katika mji wa Brussels Ubelgiji kupitia Addis Ababa Ethiopia.

 Christina  Biskasevskaja (26) raia wa nchi ya Lithuania akiwa chini ya Ulinizi baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin na Hydrochloride kinyume cha sheria .


MSCL KUDHIBITI MAPATO KIELEKTRONIKI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameitaka kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kuhakikisha inafunga kamera katika maeneo mbalimbali ya ukaguzi ili kudhibiti vitendo vya hujuma katika mifumo ya kampuni hiyo hususani kwenye Mapato. 

Ametoa rai hiyo jijini Mwanza mara baada ya kuzindua mfumo mpya wa ukatishaji tiketi kwa njia ya kielektroniki katika Meli ya MV Clarias na kusisitiza kuwa matumizi ya mfumo huo mpya yaende sambamba na elimu stahiki kwa watumishi wanaoutumia mfumo huo katika kukatisha tiketi. 

“Niwapongeze sana kwa hatua hii ya kuingia kwenye mfumo wa kielektroniki katika utoaji huduma lakini niwatake sasa kuongeza kamera kwenye maeneo yote unapofanyika ukaguzi ili kudhibiti mianya yote inayoweza kujitokeza ya kuhujumu mapato ya kampuni” amesema Prof. Mbarawa. 

Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuwekeza kwenye shirika hilo ili liweze kupata faida na liweze kujitegemea na kuagiza kuwa kwa sasa kila fedha inayopatikana itumike vizuri sababu Shirika limeanza kupata faida. 

Aidha, Prof. Mbarawa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao (eGA), kutengeneza mfumo kama huo kwa ajili ya Shirika la Reli Nchini (TRL), ili kudhibiti uvujaji wa mapato. 
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mfumo wa ukatishaji wa tiketi kwa njia ya kielektroniki katika Meli ya MV. Clarias inayotoa huduma kati ya Mwanza na Ukerewe.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akikata tiketi ya kieletroniki mara baada ya kuzindua mfumo wa tiketi hizo katika Meli ya MV Clarias, mkoani Mwanza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamis, wakati akikagua ukarabati wa Meli ya MV. Clarias, mkoani Mwanza.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live




Latest Images