Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MAHAKAMA YAZUIA UGONJWA WA BOSI IPTL KUSEMWA MARA KWA MARA,KESI YAAHIRISHWA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, imeiahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabiki mmiliki wa IPTL, Harbinder Singh Sethi na mfanyabiashara James Rugemarila hadi Machi 2, mwaka huu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Leornad Swai kudai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi wakili Swai ameomba kesi hiyo iahirishwe kwa kuwa bado wanafuatilia hatua ya upelelezi.Kutokana na taarifa hiyo, Wakili wa utetezi, Michael Ngalo aliiomba Mahakama waelezwe upelelezi umefikia wapi ili wajue kipi kinaendelea.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi, ameiomba Mahakama kutoruhusu suala la ugonjwa wa washtakiwa kuwa linasesemwa semwa mahakamani hapo kwa kuwa hilo ni suala la kitaaluma zaidi, (Kitabibu).

Amedai, masuala ya ugonjwa ni la mtu binafsi linapaswa kujadiliwa nje ya Mahakama isipokuwa pale tu Mahakama inapotakiwa kutoa amri na si vinginevyo."Mahakamani hapa si mahali sahihi sana pa kuleta masuala ya ugonjwa, kwanza watakuwa hawawatendei haki wateja wao,amedai Kishenyi kutokana upande wa mashtaka mara kwa mara kesi hiyo inapokuja kwa ajili ya kutajwa kuwa wanalalamikia afya za wateja wao.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 2, mwaka huu. Kwa pamoja washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh.Bil 309.

BENKI YA TPB,SATF ZAUNGANA KUENDESHA MRADI WA DOLA MILIONI MOJA

$
0
0
BENKI ya TPB imeungana na taasisi ya Savings at the Frontier (SatF), kwenye mradi utakaogharimu kiasi cha dola Milioni Moja. 
 
Mradi huo unaoitwa “Digitalizing Informal Savings Mechanisms” utaendeshwa kwa kipindi cha miaka mitatu (3) ambapo TPB inatarajia kuwaunganisha kwenye mfumo rasmi wa kifedha wateja wapya laki Mbili na nusu hadi kufikia mwaka 2020, Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Bank, Bw. Sabasaba Moshingi amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Februari 16, 2018.

Kitangaza mradi huo mbele ya waandisahi wa habari, Bw. Moshingi alisema, mradi huo utaanzia Mkoa wa Ruvuma, na baadae kupelekwa Mikoa ya Mtwara, Lindi, Njombe, Iringa na Morogoro.

“Watanzania wengi waishio kwenye mikoa ya pembezoni, hususani wenye vipato vidogo wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa huduma za kifedha. Kupitia ushirikiano huu na SatF, TPB itawawezesha wananchi kupitia makundi au mtu mmoja mmoja, kujiwekea akiba kupitia teknolojia rahisi na salama isiyowalazimu kwenda kwenye tawi la benki ili kupata huduma hizo za kifedha. Njia hii itawawezesha wananchi kutatua changamoto zao mbalimbali za kifedha na pia kuwaingiza kwenye mfumo rasmi wa kiuchumi.

Akifafanua zaidi Bw. Moshingi alisema, Benki ya TPB ni benki ya kwanza hapa nchini kuanzisha utoaji wa huduma za kibenki kwa makundi kupitia simu za mkononi, maarufu TPB POPOTE. Hivi sasa, wateja kupitia vikundi vyao wanaweza kuweka akiba na hata kukopa kupitia simu zao za mkononi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KANALI NDAGALA AKABIDHI MABATI 280 KWA WALIMU 14 WALIOSTAAFU KAKONKO

$
0
0

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amekabidhi mabati 280 kwa wastaafu 14.

Amekabidhi mabati hayo kwa niaba ya kamati tendaji ya Chama cha Waalimu Tanzania(CWT)Wilaya ya Kakonko ambayo ni zawadi kwa kufanya kazi iliyotukuka kwa kipindi chote cha utumishi wao.

Akikabidhi mabati hayo juzi kwa wastaafu katika ofisi za CWT wilayani Kakonko Kanali Ndagala aliwapongeza wastaafu hao na kuwasisitiza kutumia zawadi waliyopewa kukamilisha nyumba zao au kuanzisha biashara itakayowasaidia kuendeleza maisha yao.

Amesema kila mhsataafu amepewa mabati 20 kama zawadi za pongezi kutokana uadilifu.Pia pamoja na kujituma wakati wakiitumikia Serikali katika sekta ya elimu ambapo chama hicho kimetambua utendaji wao uliotukuka.

“Niwapongeze kwa kumaliza salama muda wenu, mnapoenda kuanza maisha mapya na mazuri, huu ni mwanzo mzuri kama hujamalizia kibanda kamalizie."Kama tayari ni vizuri kujenga kibanda cha biashara au kufuga ilikuweza kujikimu kwa kipindi hiki maana kuna maisha baada ya kustaafu,”, amesema Kanali Ndagala.
 MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikabidhi mabati 280 kwa mmoja wa wastaafu kati ya 14.Ndagaka amekabidhi mabati hayo kwa niaba ya kamati tendaji ya Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Kakonko ambayo ni zawadi kwa kufanya kazi iliyotukuka kwa kipindi chote cha utumishi wao.

Baadhi ya Wastaafu hao hao wakimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali (hayupo pichani),Hosea Ndagala mara baada ya kuwakabidhi mabati 280.

DK. KALEMANI AAGIZA MKANDARASI KUMALIZA HARAKA MRADI WA UMEME WILAYANI KISHAPU

$
0
0
Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi
Waziri wa Nishati, Mh. Dk. Medard Kalemani Februari 15 mwaka amefanya ziara wilayani Kishapu ambapo amezindua ujenzi wa miradi ya kusambaza umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Akiwa kwenye vijiji vya Negezi na Mwamashele, Dk. Kalemani alimuagiza mkandarasi anajenga mradi huo kukamilisha kwa wakati na kuviunganisha vitongoji vyote kwa umeme bila kuruka nyumba.
Alimuagiza kufikia Aprili mwaka huu kazi ya kusambaza nishati hiyo iwe imekamilika ili wananchi wanufaike na huduma hiyo na hivyo kuweza kuutumia kwa shughuli za maendeleo.
“Mkandarasi ongeza kasi hakuna kulala kumaliza mradi huu hatutaki wananchi wakwame na tunahakikisha vijiji vyote 118 vinapata huduma ya umeme, nakuagiza ndani ya siku 40 hapa Mwamashele umeme uwe umewaka,” alisema.
Dk. Kalemani aliwataka wananchi hao kuutumia umeme huo kwa ajili ya shughuli za kiuchumi zikiwemo kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili kujipatia kipato.
Pia aliwahimiza kuwa tayari kupokea nishati hiyo katika nyumba zao kwa kutandaza nyaya na kuwataka kuitunza miundombinu inayosambaza umeme ikiwemo, nguzo, nyaya na transifoma ili isaidie kutokatika kwa huduma hiyo.
 Waziri wa Nishati, Mh. Dk. Medard Kalemani akizungumza na wananchi katika kijiji cha Negezi ambako aliwasha umeme katika taasisi ya Serikali ambako tayari mradi huo ulijengwa awamu iliyopita. 
 Mbunge wa Kishapu, Seleman Nchambi akizungumza katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati kijiji cha Negezi. 
 Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio kwenye shughuli hiyo.
 Sehemu ya nguzo zikiwa tayari zimewasili kijiji cha Negezi kwa ajili ya kuanza kusimikwa wakati wa ujenzi wa mradi huo vijiji mbalimbali.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MADALALI WA MAHAKAMA WATAKIWA KUWA NA CHETI CHA UMADHUBUTI WA KAZI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MAHAKAMA nchini Tanzania, imewataka madalali wa Mahakama kuwa na cheti cha umadhubuti katika kazi hiyo toka Chuo cha Uongozi wa Mahakama ama Taasisi inayotambuliwa na kamati ya uteuzi.

Jaji kiongozi wa Mahakama ya Tanzania, Frerdnand Wambali amesema haya leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kongamano la wadau mbalimbali wa Mahakama wanaoratibu na kusimamia utekelezaji wa amri za mahakama wakiwamo madalali.

Lengo la kongamano hilo ni kujadili rasimu ya mtaala maalumu wa kutolewa mafunzo kwa watu wanaofanya shughuli za udalali na usambazaji wito na amri za Mahakama.

Kongamano hilo limeratibiwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Rushoto kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania lengo ni kujadili rasimu ya mtaala maalum wa kutolewa mafunzo kwa watu wanaofanya shughuli za udalali na usambazaji wito na amri za Mahakama.

Akizungumza, Jaji Wambali amesema Mahakama inatambua madalali wa Mahakama na wale wanaopaswa kupelekwa hati za kuitiwa kwenye mashauri wanawajibu wa kuhakikisha amri mbalimbali zinazotolewa na mahakama hasa katika mashauri ya madai zinatekelezwa kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa.

Introducing "Waambie" (Official video& audio) by Papii Kocha

NEC YAJIBU HOJA 6 ZA CHADEMA

$
0
0
Jana 16/02/2018 baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe, walifika ofisi za Tume ya Taifa kuwasilisha malalamiko yao kadhaa ambayo walikuwa wanahitaji ufafanuzi kutoka NEC kuhusu uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam. 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya kupitia hoja za Chadema, inapenda kutoa ufafanuzi wa hoja hizo: 

Hoja ya kwanza, kwamba, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Uchaguzi la Kinondoni amekaa kuwaapisha mawakala wa ziada wa upigaji kura kutoka CHADEMA ambao ni asilimi kumi na tano (%15) ya Mwakala wote wanaohitajika kwenye vituo 613, na kuwa utaratibu huu umekuwa unatumiwa katika Chaguzi zilizopita. 

Ufafanuzi, kwa mujibu wa kifungu cha 57(1)(2) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, kila Chama cha Siasa kilichopata ridhaa ya kuweka wagombea, kinaweza kuteua wakala mmoja wa upigaji kura kwa kila kituo ndani ya jimbo. 

Aidha, Kanuni ya 48(2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za mwaka 2015 inakitaka kila Chama cha Siasa kinachoshiriki katika Uchaguzi siyo zaidi ya siku saba (7) kabla ya siku ya Kupiga Kura kiwe kimewasilisha kwa maandishi kwa Msimamizi wa Uchaguzi majina ya Mawakala, anwani zao na vituo walivyowapangia. 

Vilevile, kifungu cha 57(3) cha Sheria tajwa, kimeweka utaratibu na mazingira ambayo wa Chama kilichosimamisha Mgombea kuweka wakala mbadala wa upigaji kura. 

Tunashauri CHADEMA kuzingatia matakwa ya kifungu cha 57(3) cha Sheria husika pale patakapohitajika uwepo wa mawakala mbadala. 

Hoja ya pili, kwamba, Msimamizi wa Uchaguzi amekataa kuwaruhusu na Viongozi wa CHADEMA kuwa Mawakala wa upigaji kura, kwa maana hiyo atakichagulia chama mawakala wa upigaji kura, na kwamba, orodha ya viongozi hao watambuliwe na kuapishwa kuwa Mawakala wa upigaji kura. 

Ufafanuzi, kifungu cha 57(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 kikisomwa pamoja na Kanuni ya 48(2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za mwaka 2015 vimeweka utaratibu wa muda wa kuwasilisha orodha ya mawakala na muda wa kuwaapisha kuelekea siku ya Uchaguzi. 

KWANDIKWA : WATENDAJI WA TAASISI ZA WIZARA TIMIZENI WAJIBU WENU KUFANIKISHA TANZANIA YA VIWANDA.

$
0
0
Na Ismail Ngayonga
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa amewataka Watendaji wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo kutumia weledi, maarifa na ujuzi walionao ili kufanikisha adhma ya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati kupitia uchumi wa viwanda.

Akizungumza katika kikao cha majumuisho ya Zaira yake ya kukagua miradi ya sekta ya ujenzi Mkoani Tanga na Watendaji wa Wizara hiyo, jana Alhamisi Februari 15, 2018, Naibu Waziri Kwandikwa amewataka Watendaji hao kubuni mipango na mikakati mbalimbali itayoweza kulisaidia Taifa.
Alisema  Watendaji wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo ikiwemo Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) na Wakala wa Ufundi na Umeme Serikalini (TEMESA) wana wajibu mkubwa wa kutimiza matarajio hayo yaliyowekwa na Serikali katika kufikia nchi ya kipato cha kati.
Kwa mujibu wa Kwandikwa alisema, Wizara hiyo imekuwa na watalaamu wa kutosha na wenye weledi ambao wamekuwa tegemeo kubwa katika Taifa, hivyo ni wajibu wa Watendaji hao kufanya kazi kwa bidii kwa kutumia vipaji vyao badala ya kuacha ujuzi na maarifa waliyonayo yakipotea bila ya kuinufaisha.
“Wizara hii, imekuwa tegemeo katika sekta zote za kiuchumi, hususani wahandisi tulionao katika Taasisi zetu, hivyo ni vyema tuhakikishe kuwa utaalamu huu unaweza kuleta matokeo chanya katika Taifa letu ikizingatia kuwa Tanzania ya Uchumi wa Viwanda itagemea sana Wataalamu wengi kutoka Wizara yetu” alisema Kwandikwa.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akisalimiana na Watendaji wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo ikiwemo TBA, TANROADS na TEMESA wakati wa mkutano wa majumuisho ya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya sekta za ujenzi inayosimamiwa na Wizara hiyo jana Alhamisi Februari 15, 2018. Kulia kwake ni Meneja wa TANROAD Mkoa wa Tanga, Mhandisi Alfred Ndumbaro.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akizungumza na Watendaji wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo ikiwemo TBA, TANROADS na TEMESA wakati wa mkutano wa majumuisho ya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya sekta za ujenzi inayosimamiwa na Wizara hiyo.


WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU WAKOSA SOKO LA UHAKIKA LA KUUZIA ZAO HILO

$
0
0
Na Jumbe Ismailly 
WAKULIMA wa zao la tumbaku katika Halmashauri ya Itigi, wilayani Manyoni, Mkoani Singida hawana soko la uhakika la kuuzia zao hilo kutokana na Makampuni yaliyokuwa yakinunua zao hilo kushindwa kuendelea kwa sababu ya madeni makubwa yanayovikabili vyama vya msingi vinavyolima tumbaku katika Halmashauri hiyo.
Afisa Maendeleo ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri hiyo Renatusi Mtatina aliyasema hayo kwenye mkutano maalumu wa Barazaa la Madiwani wa Halmashauri hiyo wakati akijibu swali la diwani wa kata ya Rungwa,Charles Machapaa ambaye alitaka kufahamishwa shilingi milioni 477 zitapatikanaji kwenye zao la tumbaku wakati serikali imeshusha ushuru wa mazao kutoka asilimia 5 hadi 3.
Aidha Mtatina alithibitisha kwamba ni ukweli usiopingika kwamba Halmashauri ya Itigi kwa mwaka huu bado haaijapata mnunuzi wa tumbaaku wala kampuni yeyote ile itakayonunua zao hilo na badala yake wakulima wataendelea kulima zao hilo na kwenda kuuza sehemu nyingine.
“Nia tunataraji kwamba watakuwepo wakulima ambao watalima lakini wanaweza wakauza sehemu nyingine lakini kwa Halmashauri ya Itigi hatujapata mnunuzi kwa hiyo patakuwa na changamoto kubwa katika kilimo cha tumbaku.”alisisitiza afisa huyo wa kilimo,umwagiliaji na ushirika.
Kwa mujibu wa Mtatina suala la matatizo ya vyama vya ushirika bado halijatatuliwa kwa sababu bado wana madeni makaubwa na ndiyo maana hawajapata mnunuzi wa zao hilo la tumbaku.
Katika swali lake la msingi,diwani wa kata ya Rungwa,Charles Machapaa alionyesha hofu ya kutofikiwa kwa malengo ya makusanyo ya mapato ya Halmashauri hiyo ya shilingi milioni 477 kutokana na serikali kushusha ushuru wa aina mbali mbali ya mazao,ikiwepo tumbaku,ushuru wa pamba pamoja na ushuru wa mazao mengineyo.
Kwa upande wake Mweka hazina wa Halmashauri hiyo,Charles Mnamba akitetea hoja hiyo alisisitiza kwamba katika msimu ujao uzalishaji wa kilimo cha zao la tumbaku utaongezeka zaidi ikilinganishwa na wa mwaka uliopita na utaweza kufidia kiwango cha ushuru wa asilimia mbili kilichopunguzwa na serikali.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi, wilayani Manyoni, Mkoani Singida, Ally Minja(wa pili kutoka kushoto) akiongoza mkutano maalumu wa baraza la madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Kijiji cha Songambele.
 Mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi, Yahaya Masare akichangia baadhi ya hoja kwa kutoa ufafanuzi kwa wajumbe wenzake wa mkutano huo.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Manyoni,Jumanne Ismaili akiwasilisha salamu za chama kwa madiwani na watendaji wa Halmashauri ya Itigi, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Kijiji cha Songambele,tarafa ya Itigi, wilayani Manyoni.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
  Baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Itigi, wilayani Manyoni Mkoani Singida wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa Kijiji cha Songambele, wakati wa mkutano maalumu wa baraza la madiwani.
Marobota ya tumbaku yaliyohifadhiwa kwenye moja ya ghala la chama cha Msingi Mitundu,tarafa ya Itigi, wilayani Manyoni wakati wa uzinduzi wa soko la tumbaku lililofanyika hivi karibuni katika Kijiji cha Mitundu.

NEC YARIDHISHWA MAANDALIZI YA VITUO 46 VYA KUPIGIA KURA KATA YA ISAMILO -MWANZA

MAFUNZO YA UONGOZI KWA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI YAFANYIKA JIJINI DAR

$
0
0
 Afisa Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kutoka Manispaa ya Kinondoni,Saleh Hijja Mohamed (aliyesimama) akizungumza kabla ya kumalizika kwa semina ya siku tatu ya mafunzo ya uongozi kwa walimu wa shule za msingi na sekondari wa Jiji la Dar es Salaam leo. Semina hiyo imefanyika katika Kituo cha Walimu cha Mzimuni kilichopo Magomeni Mapipa. Kulia wanaoshuhudia ni Afisa Mkuu wa Miradi wa Shirika lisilo la Kiserikali la British Council,Atiya Sumar na Meneja Miradi wa Shirika hilo,Ephraim Kapungu. Picha na Elisa Shunda
 Afisa Mkuu wa Miradi wa Shirika lisilo la Kiserikali la British Council, Atiya Sumar akizungumza katika ufungaji wa semina hiyo.
 Meneja Miradi wa Shirika Lisilo la Kiserikali la British Council, Ephraim Kapungu (katikati) akielezea utendaji kazi wa shirika hilo katika uwezeshaji wa masuala mbalimbali yahusuyo elimu jinsi shirika hilo linavyofanya kazi zake kwa kushirikiana na serikali kupitia wizara ya elimu.
 Mmoja kati ya wakufunzi wa semina hiyo Ndg.Edwin Shunda akiwa katika majukumu yake ya ufundishaji na uwezeshaji wa uongozi kwa walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari wa Jiji la Dar es Salaam.
Mgeni rasmi, Afisa Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kutoka Manispaa ya Kinondoni,Saleh Hijja Mohamed (katikati) akiwa na viongozi wa shirika la British pamoja na walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa semina ya siku tatu ya mafunzo ya uongozi kwa walimu hao wa Jiji la Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI YAWATAKA WATUMISHI WA UMMA NCHINI KUFANYA KAZI KWA UADILIFU

$
0
0
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa katika kikao kazi na waumishi hao kwa lengo kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi hususani haki na wajibu wa mtumishi wa Umma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Bw. Ng’wilabu N. Ludigija akitoa neno la utangulizi kumkaribisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - UTUMISHI Dkt. Laurean Ndumbaro kuzungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo masuala ya kiutumishi hususani haki na wajibu wa mtumishi wa Umma.
 Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) katika kikao kazi na waumishi hao chenye lengo kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI KUJENGA KITUO CHA UZAAJI MADINI NCHINI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WIZARA ya Madini imetangaza kuanzia sasa mnada wa madini yote utafanyika hapa nchini badala ya nje ya nchi kama ulivyokuwa unafanyika awali.

Lengo ni kuizesha Serikali kupata mirabaha yake pamoja na wachimbaji kuwa na uhakika wa soko la madini.

Uamuzi huo umetokana na mnada wa madini uliofanyika nchini Ubelgiji ambapo jumla ya karati 54,094.47 ziliziuzwa kwa dola za Kimarekani 13,607,858.72 sawa na Sh.bilioni 30.6.Mnada huo ni watatu wa madini ya Almasi ya mgodi wa Mwadui mkoani Shinyanga .

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Naibu  Waziri wa Madini,  Dotto Biteko amesema mnada huo kufanyika hapa nchini utailetea nchi faida katika mapato yatokanayo na madini .

Amezitaja faida ni kuongezea nchi mapato yatakayotakana na wageni kuja kwenye mnada huo wa madini pamoja na kuikuza nchi kwenye sekta ya madini.

Amesema hapo awali mnada ulipokuwa unafanyika nchini Ubeligiji, Taifa lilikuwa linapoteza fedha nyingi kutokana na makampuni mengi ya madini kufanya udanganyifu kwenye uuzaji wa madini.

Biteko amesema amesema ujenzi wa ukuta kwenye mgodi wa Mererani mwenye urefu wa kilomita 24.5 ambao upo hatua za mwisho kukamilika.

Pia, Serikali imesema Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa kushirikiana wataalam wa Wizara ya Madini wataanza kutoa vitambulisho vya uraia kwa wananchi wa eneo la Mererani ambao ni wachimbaji wadogowadogo wa madini ili waweze kufanya uchimbaji kama sheria inavyotaka.
Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mnada wa madini uliofanyika nchini Ubelgiji na serikali kuweza kupata mauzo mazuri leo jijini Dar es Salaam.

WASHINDI 36 WA PROMOSHENI YA NYAKA NYAKA BONUS WAZAWADIWA.

$
0
0

Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kulia) akimkabidi Mariam Akida (kati) mkaazi wa Tabata jijini Dar es Salaam zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 36 walipata zawadi za simu janja kutoka Tigo katika promosheni hiyo inayoendelea. Kushoto ni Mtaalam wa Usambazaji wa Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza. 
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (wa pili kushoto) pamoja na Mtaalam wa Usambazaji wa Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza (kushoto) wakiwa pamoja na baadhi ya washindi wa zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 walizoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 36 kutoka sehemu mbali mbali nchini walipata zawadi za simu janja kutoka Tigo katika promosheni hiyo inayoendelea. 
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (wa pili kushoto) pamoja na Mtaalam wa Usambazaji wa Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza (kushoto) wakiwa pamoja na baadhi ya washindi wa zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 walizoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 36 kutoka sehemu mbali mbali nchini walipata zawadi za simu janja kutoka Tigo katika promosheni hiyo inayoendelea.
Kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TBL YATAKIWA KUMLIPA DAVID MGWASSA SH. BILIONI MOJA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

TUME Usuluhishi na Uamuzi (CMA) imetoa tuzo kwa aliyekuwa Meneja wa Konyagi David Mgwassa ya kulipwa dola za Kimarekani 200, 000 ndani ya siku 14 kuanzia leo kama gharama za usumbufu baada ya kuachishwa kazi isivyo halali na Kampuni ya Tanzania Brewaries (TBL)

Pia  TBL inatakiwa kumlipa Mgwassa Sh.milioni 412   kama fidia ya kusitishwa kwa haki zake  na pia ilipe mkopo wa gari lenye thamani ya  Sh.milioni 94 ambalo lilikopwa na Mgwasa akiwa kazini.

Uamuzi huo umetolewa na Mwamuzi, Alfred Massay katika shauri la mgogoro wa kazi  lenye kumbukumbu namba CMA/DSM/ILALA/R.49/16,   ambapo Mgwassa alifungua madai mbalimbali dhidi ya TBL,  Sabmiller Africa na Sabmiller PLC-London. 

Mgwassa pamoja na mambo mengine mbali mbali, alikuwa akilalamikia kuachishwa kazi isivyohalali na kuomba alipwe mishahara ya miezi 36 kama fidia na pamoja na malipo ya bonasi kwa miezi mitatu ambayo ni sawa na zaidi ya Sh.milioni 261.5.

Mgwassa aliajiriwa na TBL kati ya Februari mwaka 1982 na Juni mwaka  2015 na katika kipindi cha kusitishwa kwa mkataba wake wa ajira alikilipwa mshahara wa Sh. 17,191,451.88 kwa mwezi.

Hata hivyo, ajira kati ya TBL na Mgwassa ilifikia mwisho Juni 25 mwaka  2015 baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya mkataba wa kustaafu mapema

baada ya uamuzi huo kutolewa,Mgwassa aliyekuwa akiwakilishwa na Wakili Alex Mshumbusi alisema ameridhishwa na uamuzi huo.

Aliyepewa msaada wa bajaji na Rais Magufuli aonyesha maajabu

Lady in Red Farewell after party kufanyika Jumapili ukumbi wa Next Door Masaki jijini Dar es salaam

$
0
0
Mbunifu nguli wa mitindo Bi. Asya Idarous-Khamsin ameandaa After party (pool party) ya Lady in Red Farewell siku ya Jumapili Februari 18, 2018 kuanzia saa 10 jioni katika ukumbi wa Next Door Masaki jijini Dar es salaam kuwaaga rasmi washirika na mashabiki wake baada ya kutamba kama Mama wa Mitindo nchini Tanzania kwa zaidi ya miongo miwili.

​WANANCHI KWIMBA WAMKATAA MKUU WA WILAYA MBELE YA WAZIRI MKUU

$
0
0
WANANCHI wa wilaya ya Kwimba wamemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aondoke na mkuu wa wilaya hiyo Bw. Mtemi Msafiri  (pichani) baada ya kutoridhishwa na utendaji wake. 
Wametoa ombi hilo leo (Ijumaa, Februari 16, 2018) walipozuia msafara wa Waziri Mkuu alipowasili katika Ofisi za Halmashauri ya wilaya Kwimba zilizopo Ngudu kwa ajili ya kuzungumza na watumishi akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza. 
Wananchi hao walimkataa mkuu wao wa wilaya Bw. Msafiri kupitia ujumbe wa mabango 17, ambapo Waziri Mkuu amewataka wananchi hao wawe watulivu wakati Serikali inafanyia kazi malalamiko yao. 
Wananchi hao wanadai kwamba Mkuu huyo wa Wilaya anatabia ya kuamrisha polisi wawakamate kwa kisingizio cha uzururaji na kisha wanawekwa mahabusu, ambapo baada ya muda wanatolewa na kwenda kulima kwenye shamba lake. 
Waziri Mkuu amesema Serikali inahitaji kila mtumishi atambue majukumu yake na ayatekeleze. “Hakuna atakayeonewa, haki zenu zote tunazitekeleza nanyi mnatakiwa kutenda haki kwa kuwatumikia wananchi.” 
Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka Mkuu huyo wa wilaya Bw. Msafiri, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kwimba Bibi Pendo Malebeja na wakuu wote wa Idara wajitathmini kama kweli wanatekeleza majukumu yao ipasavyo na kuwatumikia wananchi. 
“Mkurugenzi katika kipindi chako chote cha utendaji kuanzia mwaka 2013 hadi leo, fedha nyingi za Serikali zilizoletwa Kwimba zimepotea na hazijulikani zilipo huku miradi mingi bado haijakamilika na muda wote huo Halmashauri imekuwa inapata hati chafu.” 
Pia Waziri Mkuu amewataka watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Kwimba wabadilishe mienendo yao na wawatumikie vizuri wananchi pamoja na kuishi nao vizuri.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, FEBRUARI 16, 2018.

ASLAY, NANDY WAULA AIR TANZANIA

MAJALIWA AKAGUA MASHAMBA BORA YA PAMBA KATIKA VIJIJI VYA KILYABOYA NA SOLWE WILAYANI KWIMBA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga (watatu kulia) kuhusu zao la pamba lililostawi vizuri wakati alipotembelea shamba darasa  katika kijiji cha Kilyaboya wilayani Kwimba Februari 16, 2018. Wanne kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella na kushoto ni Afisa Kilimo wa wilaya ya Kwimba, Magreth Kavalo. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shamba la pamba la Bw. Dotto Masomi  (kushoto) katika kijiji cha Solwe wilayani Kwimba Februari 16, 2018, Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mtemi Simon Msafiri.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shamba la pamba la Bw. Dotto Masomi  (kushoto) katika kijiji cha Solwe wilayani Kwimba Februari 16, 2018, Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mtemi Simon Msafiri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza, Dotto  Masomi baada ya kutembelea shamba la pamba la mkulima huyo katika kijiji cha Solwe wilayani Kwimba na kufurahishwa na ubora wa shamba hilo Februari 16, 2018. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images