Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

NEC YATOA UFAFANZI TUHUMA ZA CHADEMA


INTRODUCING Phillz - Brown Shuga (Official music)

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAJUMUISHO YA ZIARA YAKE MKOANI IRINGA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa mkoa wa Iringa kushirikiana ili kuweza Kuwasaidia wananchi.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kutoa majumuisho ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Iringa.

Makamu wa Rais alitembelea wilaya ya Iringa, Kilolo na Mufindi ambako kote alishiriki shughuli za kimaendeleo ikiwa kuzindua Vituo vya Afya Kising’a wilaya Iringa, Jengo la Utawala na Madarasa katika Shule ya Sekondari Kilolo, 
Pia aliweka jiwe la msingi katika Ujenzi wa Maabara na Madarasa katika shule ya sekondari Mgololo na kuweka jiwe la Msingi katika upanuzi wa Kituo cha Afya cha Ihongole kilichopo Mafinga.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao wakati wa majumuisho ya ziara yake mkoani Iringa, Wengine pichani ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza (kushoto) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bw. Salim Abri Asas. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Iringa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kumaliza kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Iringa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

YANGA, MAJIMAJI KUSHUKA DIMBANI KESHO TAIFA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) Yanga, kesho wanashuka dimbani kuvaana na kikosi cha Majimaji ya Songea " Wanalizombe" katika mchezo wa raundi ya 18 kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.

Mechi hiyo itakayoanza majira ya saa 10 alasiri unatarajiwa kuwa wa ushindani kwa pande zote mbili,Yanga wakitaka kupata ushindi ili kuzidi kujiweka kwenye mazingira ya kutetea ubingwa wao huku Majimaji wakitaka kujinasua kutoka kwenye nafasi ya tatu kutoka chini.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa mkoani Songea kwenye Uwanja wa Majimaji Yanga walilazimishwa sare ya 1-1 wakisawazisha goli hilo kupitia kwa mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka Zimbabwe Donald Ngoma.

Akizungumza na Globu ya jamii Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanga Dismas Ten amesema timu imeendelea  na mazoezi yake kama kawaida na kesho kitashuka dimbani kikiwakosa wachezaji watatu ambao hawajaanza kujumuika na wenzao kwenye mazoezi.

Amewataja wachezaji hao ni Amidi Tambwe, Donald Ngoma na Yohana Mkomola ambao wapo chini ya uangalizi wa daktar wakiuguza majeraha yao.

" Wachezaji watakaokosekana kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Majimaji ni watatu ambao hawajaanza mazoezi na wenzao ni Donald Ngoma, Amisi Tambwe na Yohana Mkomola wakiwa chini ya uangalizi wa daktari," amesema Ten.

Yanga watashuka dimbani wakiwa na alama 34 wakishika nafasi ya pili nyuma ya vinara wa VPL Simba wakiwa kileleni kwa alama 38.

WAZIRI MKUU AZINDUA MPANGO MKAKATI AFYA MOJA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Blogu ya jamii
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha Tanzania inakuwa mahala salama na penye afya bora huku akielezea jitihada zinazochukuliwa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na matukio hatarishi kwa wananchi.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam, wakati anazindua Mpango Mkakati wa Afya Moja na Dawati la Kuratibu Afya Moja nchini huku akisisitiza uzinduzi huo ni muhimu hasa kupindi hiki ambacho kumekuwepo na muingiliano mkubwa kati ya binadamu, wanyama na mazingira.

Amesema dhana ya dhana ya Afya Moja inafaa kutumika zaidi katika nchi zinazoendelea kwani inatoa fursa kwa wadau mbalimbali kushirikana katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

"Mpango huu wa Afya Moja ni ajenda ambayo ipo kwenye nchi mbalimbali duniani na kwa Tanzania ni mpango ambao tunaamini utasaidia kukabiliana na magonjwa ya mlipuko yatokanayo na binadamu, wanyama na mazingira,"amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Ameongeza mkakati wa kukabiliana na maradhi yatokanayo na wanyama na mazingira ni muhimu kwa nchi nyingi za Afrika kwani zipo kwenye hatari zaidi.

Amesema katika Bara la Afrika kuna maeneo mengi yenye mapori makubwa ,hivyo ni rahisi kuwepo kwa magonjwa ya kuambukizwa yanayotokana na binadamu, wanyama na mazingira,hivyo Afya Moja imekuja wakati sahihi.

Ametoa mfano wa mapori makubwa yaliyopo kwenye Bonde la Mto Kongo, ambalo mazingira yake yamekuwa ni kitovu cha magonjwa ya mlipuko kama vile Ebola, Homa ya Bonde la Ufa (RVF), Marburg na mengineyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

HOJA YA HAJA: HUU NI UPUUZI MKUBWA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
 Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 

 Tangu Jumapili tarehe 11/02/2018 nilishtushwa na habari iliyoandikwa na mwandishi aitwaye David Ng’ang’a kupitia mtandao uitwao “Business Insider” ikiwa na kichwa cha habari kisemacho “Marry two or more women to reduce prostitution among ladies – Magufuli to Tanzanian men” ikiwa na maana Rais Magufuli amewaambia wanaume wa Tanzania waoe wake wawili au zaidi ili kupunguza umalaya kwa wanawake. 
 Kwanza habari yenyewe imejaa uongo na uzandiki wa hali ya juu. Ina takwimu za uongo kuwa Tanzania ina wanawake milioni 40 na wanaume milioni 30, yaani jumla Tanzania ina watu milioni 70??
Uongo na upuuzi mkubwa, kwamba Rais Magufuli alikuwa akizungumza na wanaume 14,000 waliokuwa mafunzoni? Uongo wa kupigiwa mfano, kwamba wanawake wa Tanzania wanalia kukosa wanaume?? Uongo na udhalilishaji wa hali ya juu, kwamba serikali itatoa ruzuku kwa wanaume watakaooa wanawake wawili au zaidi?? 
Uongo na uchochezi wa hali ya juu, na kwamba Tanzania ina viwango vya juu vya umalaya Afrika Mashariki?? Uongo na udhalilishaji usiovumilika. 
 Nilishtushwa kwa sababu kauli hizi haziwezi kutamkwa na kiongozi tena kiongozi mwenyewe akiwa ni Rais Magufuli ambaye ameaminiwa na Watanzania na anayetosha kwa sifa za kiongozi makini, asiye na ubaguzi, mwenye upendo, mpigania wanyonge na mwenye maono ya kuifikisha Tanzania katika neema. 
Sijawahi kumsikia mahali popote Rais Magufuli akitamka maneno hayo na kwa utamaduni wa kitanzania na viongozi watokanao na Chama Cha Mapinduzi hizi sio kauli za kiungwana. Nilipofuatilia nikabaini kuwa mwandishi wa makala hii ni wa nchi jirani, nilipofuatilia zaidi nikabaini kuwa makala hii inachochewa na kushabikiwa na wanasiasa za upinzani nchini Tanzania. Kwa kifupi nikabaini kuwa hapa kuna mbinu za kumchafua Rais Magufuli kutoka nchi jirani na pia wanasiasa wanataka kupata maslahi ya kisiasa kwa kupambisha upuuzi huu. 
 Nimeona niandike kumjulisha aliyepika uongo huu kuwa takataka alizoandika hazina maana yoyote na kamwe hazitarudisha nyuma juhudi za Rais Magufuli na Watanzania kujenga nchi yao. 
 Nimeona nimjulishe kuwa Watanzania wanamjua Rais wao na dunia inajua kuwa Tanzania kuna Rais Magufuli wa mfano kwa Marais wote wa Afrika, kuna Rais Magufuli ambaye ameamua kwa dhati kupigana na rushwa na anafanikiwa sana, kuna Rais Magufuli ambaye amesema hakuna atakayeendelea kuinyonya Tanzania, kuna Rais Magufuli ambaye hakubaliani na danganya toto iliyosababisha Tanzania kuwa shamba la bibi, kuna Rais Magufuli ambaye ameanza kutekeleza miradi mikubwa, anakuza uchumi na anasimamia utendaji kazi katika ofisi za umma na hataki mchezo dhidi ya vitendo vyote vya kuirudisha nyuma Tanzania na kuwanyanyasa Watanzania hasa wanyonge. 
 Nimejua kuwa kinachowasumbua wengi ni mwangwi wa mafanikio ya muda mfupi aliyoyapata Rais Magufuli katika miaka miwili ya tangu Serikali anayoiongoza ya Awamu ya Tano iingie madarakani. Na hiki ni kipimo cha kuwajua wanaoitakia mema Tanzania, na kwa namna yoyote wasioitakia mema Tanzania lazima wataponda kazi zinazofanywa na Rais makini Dk. Magufuli. 
 Wapo walioumizwa na kuanza kujengwa kwa reli ya kati (Standard Gauge) kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro na baadaye kuendelea hadi Dodoma na Isaka, wamekasirika zaidi waliposikia taarifa za ghafla kuwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame amekubaliana na Rais Magufuli kuunganisha reli ya Standard Gauge kutoka Isaka hadi Kigali nchini Rwanda. 
Wanajua kuwa sasa bandari zao zinakwenda kukosa mizigo ya Rwanda. Kabla yake waliumizwa na makubaliano ya Rais Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Museveni kuhusu kuunganisha reli ya kati hadi Kampala ili mizigo yote ya Uganda itumie bandari ya Dar es Salaam. 
 Pia wameumizwa baada ya kuona Tanzania imeshinda mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Rwanda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania, wanajua kuwa sasa mabilioni ya dola za mradi huu mkubwa yatatua Tanzania na Watanzania lukuki watapata ajira na kuongeza vipato. 
 Wamekasirika zaidi kusikia habari za Tanzania kuanza kujenga mradi mkubwa wa kuzalisha megawatts 2,100 katika mto Rufiji (Stieglers’ Gorge), wanajua kuwa matarajio yao ya kuuza umeme Tanzania yamepotea, wanajua kuwa upepo wa wawekezaji ambao walishindwa kuja Tanzania na kwenda nchi mwao sasa utabadili mwelekeo na kuvumia Tanzania. 
 Wamechukia kwamba kwa hatua ambazo Tanzania inazichukua kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji ikiwemo kuondoa urasimu katika uwekezaji, kupambana na rushwa na kuusimamia vizuri uchumi kutaifanya Tanzania kuwa nchi itakayoongeza kasi isiyoshikika ya ukuaji wa uchumi ambao hata sasa inaongoza kwa Afrika Mashariki kwa ukuaji wa asilimia 6.8, na kuwa ya nchi tatu kwa ukuaji barani Afrika. 
 Wamenuna sana kuona utekelezaji wa azma ya ujenzi wa viwanda ukienda kwa kasi kubwa, imewaudhi sana kusikia ndani ya miaka miwili viwanda 3,500 vimejengwa na sasa Tanzania inazungumza kununua bidhaa za ndani kwa wananchi wake. 
 Hawana amani kabisa wanaposikia Rais Magufuli na Serikali yake wameanza kufufua shirika la ndege la Taifa (ATCL) kwa kununua ndege sita ikiwemo ndege kubwa yenye uwezo wa kuruka moja kwa moja hadi Ulaya, China na Marekani, na ndege nyingine zitakazoruka ndani ya bara la Afrika na hivyo kukuza uchumi kupitia utalii na biashara. Wanajua kuwa hii ina madhara makubwa kwenye uchumi wao. 
 Hawapendi kabisa kuona washirika wa maendeleo wanazidi kuongeza imani na kuongeza fedha katika miradi mbalimbali ya kujenga uchumi na kuhudumia wananchi. 
Walitarajia kuona baada ya Rais Magufuli kuchukua hatua alizochukua pengine wadau wa maendeleo wangesusia lakini ndio kwanza Benki ya Dunia imeongeza pesa, Benki ya Maendeleo Afrika imeongeza pesa, achilia mbali nchi mbalimbali ambazo zinatoa misaada kila uchao zikiwemo China, Marekani, Uingereza, nchi za Uarabuni na nyinginezo nyingi. 
 Unaweza kusema mengine lakini hali ndio hii, na hata wale waliokuwa wanabeza na kujiona wao ni bora, sasa wanaumbuka kutokana na mambo kuwaendea kombo. Hizi ni salamu nzito sana. Na kwa wanasiasa wa ndani ya Tanzania nawakumbusha msemo maarufu “kama huwezi kushindana nae, ungana nae” cha ajabu madiwani wengi wamelijua hili mapema na wanazidi kumiminika kuhama kutoka siasa za upinzani na kujiunga na chama tawala, hapa somo ni moja tu wamegundua kama kweli kiongozi ana nia ya kuwapigania wananchi dawa ni kuungana na Rais Magufuli kupigania watu wake. 
 Wameshtuka kuwa yale ambayo Rais Magufuli na Serikali wanayasimamia ndio yale ambayo vyama vyao vya siasa viliyahubiri kwa miaka mingi na sasa vyama hivyo havitaki tena kuyasema na kuyapigania na badala yake waliotuhumiwa kuiangamiza nchi na kuwaumiza wananchi wamekaribishwa kwenye vyama vya upinzani na wamekaa meza za mbele (hightable). 
 Hivi sasa imekuwa ndio siasa za upinzani kwa viongozi wake kupinga kila anachokifanya Rais, wamegawana majukumu ya kumdhohofisha bila mafanikio. Ukigeukia huku utamkuta Freeman Mbowe anamshambulia Rais, ukigeuka kule utamkuta mgonjwa Tundu Lissu anaacha kushughulika na matibabu yake anamshambulia Rais, Zitto Kabwe kasahau hata chama chake cha ACT kinachopukutika amejipa kazi ya kumshambulia Rais, Julius Mtatiro amekuwa mwanamitandao maarufu wa kumshambulia Rais na Mawaziri. 
 Kazi ni hiyo hiyo kwa wengine ambao Watanzania wamewapuuza akina Godbless Lema, Mchungaji Peter Msigwa, Halima Mdee, Ester Bulaya na wabunge wengine wa chama cha CHADEMA na viongozi wao wa chama. Napata wasiwasi kuwa upinzani Tanzania umeishiwa mbinu za kufanya siasa na sasa unatukana tu, unashambulia personalities za viongozi na kupika taarifa ili kuleta taharuki. 
Wengine wanachokoza vyombo vya dola ili wapate umaarufu wa kukamatwa na kulalamika kuwa wanaonewa. Hata hawashtuki kwa nini wanayemshambulia hawajibu? Hawajiulizi Watanzania wanawaonaje? Hawajiulizi kwa haya wanayofanya ikitokea siku wao wakashika nchi watafanya hayahaya ama itawalazimu kubadilika na kuwapa Watanzania haya anayowapa Rais Magufuli. 
 Kwa ninavyomjua Rais Magufuli, wanachofanya nchi jirani na wanasiasa za upinzani Tanzania ni patapotea, na kizuri ni kwamba Watanzania wanaelewa na wanakwenda kwa mwendo wa Rais Magufuli. 

 Naamini wamesoma andiko hili na ujumbe umefika 
 Alamsiki 
 Fabian Mdondolelo 
 13 Februari, 2018 
 Dar es Salaam

Introducing "Ni Wewe" (Official Video) by Iddi Singer, Landan Balla, Lovince Mckenzie

$
0
0


Roya Entertainment & Hourglass254 Presents

Slay Queen Official Video
Audio Produced by Teknixx
by Iddi Singer & Landan Balla
Styling & Accessories by HourGlass254
Video by Eddie Juma & Elle Elle Motion Pictures
Make Up by Dansons Make Up 

Logistics by HourGlass254 -- 

KAMATI YA NIDHAMU YAMFUNGIA JUMA NYOSO

$
0
0
Kamati ya Nidhamu iliyokutana Jumamosi Februari 10, 2018 pamoja na mambo mengine pia ilipitia shauri la mchezaji wa Kagera Sugar Juma Nyoso lililofikishwa kwenye kamati akituhumiwa kwa utovu wa nidhamu kwenye mechi namba 112 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Kagera Sugar dhidi ya Simba Sports Club iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Juma Nyoso alituhumiwa kumpiga shabiki baada ya kumalizika mchezo huo kinyume cha kanuni ya 36 ya ligi Kuu inayozungumzia uchezaji wa kiungwana pamoja na Ibara 50(1)(2) na (5) ya katiba ya TFF toleo la 2015.
Kamati ilipitia ripoti ya kamishna wa mechi ambayo imeeleza tukio hilo la Juma Nyoso kupishana na shabiki aliyekuwa amebeba vuvuzela  na ndipo Nyoso aliposimama na kuanza kumpiga na kiatu na kutumia goti mpaka askari wa jeshi la Polisi walipoingilia kumuokoa na kumshikilia mchezaji huyo wakati shabiki akipatiwa huduma kwenye gari la huduma ya kwanza.
Juma Nyoso katika utetezi wake alikana malalamiko dhidi yake akidai kitendo alichofanya ni kukunjana na shabiki.
Kamati kupitia ripoti ya kamishna wa mchezo huo imemtia hatiani Juma Nyoso kupitia kanuni ya 36 ya kanuni ya Ligi kuu na Ibara ya 50(1)(2) na (5) ya katiba ya TFF.
Kamati pia ilipokea taarifa za nyuma za nidhamu za Juma Nyoso ambayo rekodi inaonesha aliwahi kufungiwa kwa makosa ya kinidhamu .

Kupitia kifungu cha 37(10)cha kanuni za ligi Kuu kamati imemtia hatiani Juma Nyoso na imemfungia kutocheza mechi Tano(5) na faini ya Shilingi milioni moja(1,000,000). Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Tanzania yawa Mwenyeji ya Mkutano wa Baraza la Wakimbizi Duniani

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuisaidia Tanzania kutokana na mchango mkubwa wa kuwahudumia wakimbizi ambao imekuwa ikiutoa kabla na baada ya uhuru, licha ya uchumi mdogo ilio nao. 
Waziri Mahiga ametoa wito huo leo Jijini Dar Es Salaam katika kikao cha Baraza la Wakimbizi Duniani (World Refugees Council-WRF) kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia jana kwenye Hoteli ya Hyatt Regecy, Kilimanjaro.

Waziri Mahiga alieleza kuwa Tanzania ilipokea wakimbizi kutoka Poland wakati wa vita ya pili ya dunia na mwaka 1959 ilipokea wakimbizi kutoka nchi ya Rwanda. Aidha, baada ya uhuru, Tanzania imekuwa ikipokea wakimbizi mara kwa mara na wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Tanzania ilipokea wakimbizi wengi zaidi duniani.
Aliendelea kueleza kuwa athari zinazotokana na kupokea wakimbizi wengi ni nyingi na kubwa hivyo, ni jukumu la Jumuiya ya Kimataifa kuzisaidia nchi zenye wakimbizi wengi, hususan zile zenya uchumi mdogo.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari kuhusu dhamira ya kuanzishwa kwa Baraza la Wakimbizi Duniani ambalo yeye ni Mwenyekiti Mwenza. Kushoto kwake ni  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akiongea na waandishi wa habari kuhusu msimamo wa Tanzania kujitoa katika Mpango wa kutafuta suluhu ya kudumu ya tatizo la wakimbizi duniani.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea katika kikao cha Baraza la Wakimbizi Duniani kinachofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini DAr es salaam.
Kwa habari kamili BOFYA HAPA

Serikali na TFF yakutana na Wahariri wa Michezo kujadili Maandalizi ya Ujio wa Rais wa FIFA na CAF

$
0
0
 Mjumbe wa CAF na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Bw.Leodger Tenga (katikati) akizungumza na Wahariri wa Habari za Michezo kutoka vyombo mbalimbali nchini (hawapo pichani) kuhusu mambo ambayo uongozi wa FIFA utapenda kujua katika soka la Tanzania ambapo moja wapo ni Maendeleo ya Soka la Wanawake,Kushoto ni  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe na Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Wallace Karia  (katikati) akitoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa waandishi watakao shiriki kuripoti habari wakati wa ujio wa Rais wa FIFA na CAF nchini kwa Wahariri wa Habari za Michezo kutoka vyombo vya habari nchini (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, Kushoto ni  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe na Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
Seehemu ya Wahariri wa Habari za Michezo kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia kikao cha maandalizi ya ujio wa rais wa FIFA NA CAF mwezi huu nchini kilichokuwa kikiendeshwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Wahariri wa Habari za Michezo kutoka vyombo mbalimbali nchini (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam  kuhusu utaratibu wa ujio wa Rais  FIFA na CAF nchini mwezi huu kwa ajili ya kufanya mkutano wa kujalili agenda za mkutano mkuu wa FIFA,na Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
Na Anitha Jonas – WHUSM

Dkt. Kalemani afanya ziara Chato, Atoa wiki moja kwa mkandarasi kukamilisha usambazaji umeme

$
0
0
Na Greyson Mwase, Chato
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani  leo  tarehe 13 Februari, 2018 amefanya ziara katika wilaya ya Chato mkoani Geita lengo likiwa ni kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na  Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Akizungumza kwa nyakati tofauti  na wananchi katika vijiji vya Iparamasa na Kalembela vilivyopo wilayani Chato mkoani Geita, Dkt. Kalemani ameitaka kampuni iliyopewa kazi ya kujenga miundombinu ya umeme katika vijiji husika, ya White City JV Guandong kukamilisha kazi  iliyopewa ndani ya  wiki moja  katika kijiji cha Iparamasa na  siku tatu katika kijiji cha Ilembela ili wananchi waanze kunufaika na huduma ya umeme wa uhakika.
“ Wananchi hawa wamechoka na adha ya kukosa  huduma ya umeme kwa muda mrefu, ninatoa wiki moja kwa mkandarasi kuhakikisa kijiji cha  Iparamasa kinapata umeme wa uhakika na siku tatu kwa kijiji cha Kalembela wanapatiwa huduma ya umeme kwa kuwa tayari nguzo zimefika katika vijiji husika,” alisema Dkt. Kalemani
Waziri Kalemani aliendelea kusema kuwa Serikali kupitia  Wizara ya Nishati, imepanga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025 asilimia ya 75 ya watanzania wanapata huduma ya umeme ambao ni wa uhakika na kuchangia nchi kutoka kwenye orodha ya nchi masikini na kuingia kwenye orodha ya nchi za kipato cha kati
Alisisitiza kuwa, kwa kutambua mchango wa nishati kwa ukuaji wa uchumi wa viwanda, Wizara ya Nishati imepanga mikakati ya kuhakikisha miradi ya REA inatekelezwa kwa wakati kwa kutenga fedha za kutosha, na usimamizi  makini ili wananchi wote wanufaike na huduma ya umeme.
Aidha, katika hatua nyingine Dkt. Kalemani aliwataka wananchi  wa vijiji husika kujiandaa na huduma ya umeme kwa kutandaza nyaya kwenye nyumba zao (wiring) au kuweka  Kifaa Maalum cha Umeme Tayari (UMETA) ili waunganishwe na huduma ya umeme  mapema.
Pia  Waziri Kalemani aliwataka wananchi kuchangamkia fursa zitakazojitokeza mara baada ya upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika kama vile uanzishwaji wa viwanda vya kusindika nafaka, mashine za kuchomea vyuma na kuondokana na umaskini.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akielezea matumizi ya Kifaa Maalum cha Umeme Tayari (UMETA) kwa wananchi wa kijiji cha Iparamasa (hawapo pichani) wilayani Chato mkoani Geita.
 Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Kalembela kilichopo wilayani Chato mkoani Geita, wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kalembela kilichopo wilayani Chato mkoani Geita.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akitoa maelekezo kwa mkandarasi, wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika  kijiji cha Kalembela kilichopo wilayani Chato mkoani Geita.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akisalimiana na mmoja wa wananchi mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kalembela kilichopo wilayani Chato mkoani Geita.

MAENEO YANAYOTUMIKA KUPITISHA DAWA ZA KULEVYA NCHINI YATAJWA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 
 SERIKALI imebaini kwamba maeneo ya bandari, bahari kuu,vituo vya mabasi na viwanja vya ndege  bado yanatumika kupitisha dawa za kulevya nchini. Hata hivyo imeelezwa kuwa wafanyabiashara, wasambazaji na watumiaji wa dawa za kulevya wameendelea kukamatwa, lengo ni kuhakikisha biashara hiyo inamalizika kabisa. 
Hayo yamesemwa leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akikabidhi gari kwa Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers Siyanga. 
 Amefafanua mbali na kukamata meli, pia Serikali imewakamata wasambazaji pamoja na kundi kubwa la wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya sambamba na watumiaji, lengo ni kuhakikisha Tanzania inakuwa salama na kizazi chenye uwezo wa kuzalisha mali. 
 "Serikali imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya dawa za kulevya na hivi karibuni imekamata meli nyingi, moja ilikiwa inatokea pwani ya Msumbiji na ilikamatiwa maeneo ya Mtwara ikiwa na dawa nyingi za kulevya.
 "Niwakati wa Serikali kuendelea kuiwezesha Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na leo hii tunawakabidhi gari hili jipya kabisa ili kuendelea na utekelezaji wa majukumu yake ipasavyo. 
 "Watanzania wenye tabia ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya kuacha ikiwa ni pamoja na kazi ya kusambaza, kuzalisha na kutumia na watakaokamatwa wakijihusisha nayo watachukuliwa hatua kali za kisheria,"amesema.
 Ameongeza kwa sasa Serikali inajenga maabara ambayo itatumiwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa dawa wanazozikamata. 
 Waziri Mkuu amesema wananchi wanatakiwa kushirikiana na Serikali katika vita dhidi ya dawa za kulevya kwa kutoa taarifa mara wanapowabaini wafanyabiashara, watumiaji na wasambazaji wa dawa hizo. 
Pia wahakikishe wanawalinda vijana ili wasijihusishe na dawa za kulevya. Kwa upande wake Siyanga ameishukuru Serikali kwa kuipatia mamlaka hiyo gari, ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi waachane na biashara ya dawa za kulevya.  Pia amesema jamii iache kuwanyanyapaa watu ambao wameathirika na matumizi ya dawa za kulevya na kushauri kuwa walioathirika na dawa za kulevya wanastahili kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu ya huduma za methadone.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo (Jumanne, Februari 13, 2018) amekabidhi gari kwa Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers Siyanga kwa ajili ya Mamlaka hiyo. Makabidhiao hayo yamefanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

JUKWAA LA NISHATI TANZANIA KUTOA SEMINA KWA WABUNGE

$
0
0

Na Mwandishi Wetu
JUKWAA la Nishati Tanzania linatarajia kutoa semina kwa wabunge ili wapate uelewa wa nishati na changamoto zake, watakapokuwa wanajibu maswali ama kuuliza wafanye hivyo kwa manufaa ya taifa.
Mratibu wa Jukwaa hilo nchini ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Hudson Nkotagu alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shughuli wanazozifanya.
Profesa Nkotagu alisema wanaamini wabunge wakipata uelewa kuhusu nishati pale watakapokuwa wakijadili masuala hayo bungeni watakuwa na uelewa mpana, na maamuzi yake yatakuwa kwa manufaa ya taifa.
Pia alisema semina hizo zitatolewa kwa viongozi wakuu, watendaji wa serikali kutoka sekta za viwanda, mazingira, serikali za mitaa, wawekezaji pamoja na wafanya biashara mbalimbali.
Alisisitiza kuwa wananchi wengi hawana uelewa wa nishati kwamba kuna za aina mbili, aina ya kwanza inatokana na vyanzo vya nishata ambavyo vikitumika vinapoisha havirudi tena mfano gesi, mafuta, mkaa wa mawe pamoja na urani.
Na aina nyingine ni ile inayotokana na vitu ambavyo vinajiendeleza vyenyewe kiasili kwa mfano nishati ya sola, upepo, maji, mawimbi ya bahari na kuni.
“Nishati hizi zinajiendeleza kiasili. Kwa bahati nzuri zote tunazo katika nchi yetu. Tanzania imejaliwa kuwa na vyanzo vyote vya nishati, vinahitajika tu kuendelezwa,” alisema.
Alisema jukwaa hilo linashirikisha UDSM, Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT), Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), pamoja na vyuo vikuu vine kutoka nchini Uholanzi ambavyo ni Twente, Ultreacht, Hanze na Delft.

MKAPA AONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA MFUKO WA UDHAMINI KUDHIBITI UKIMWI

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

RAIS Mstaafu Benjamin Mkapa amewataka wadau mbalimbali na wananchi kuendelea kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo nchini ambapo zaidi ya sh.milioni 200 zilipatikana.

Mkapa alitoa ombi hilo wakati akiongoza harambee ya kuchangia mfuko huo iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, wawakilishi wa mashirika ya nje na ndani pamoja na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.

"Ni wajibu kwa kila mwananchi na wadau mbalimbali kuendelea kuchangia mfuko huu ili kusaidia mapambano ya Ukimwi hapa nchini na kuwa mapmbano hayo si ya mtu mmoja" alisema Mkapa. Katika hatua nyingine Rais Mstaafu Mkapa ameiomba Serikali kuendelea kutenga fedha za Ukimwi katika bajeti zake.

Akizungumza katika harambee hiyo Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama alisema kwamba Serikali itaendelea kusimamia Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) katika matumizi ya fedha hizo.

Mhagama alisema asilimia 60 ya fedha hizo zitatumika kununulia madawa, asilimia 25 itatumika katika kutoa huduma za kinga pamoja na kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi mapya ya Ukimwi na asilimia 15 zitatumika kwa ajili ya uwezeshaji na ufuatiliaji wa programu za Ukimwi.
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa akitoa zawadi ya picha iliyonunuliwa kwa sh. milioni moja katika harambee hiyo.
Rais Mkapa akimkabidhi picha Salama Mussa kutoka Benki ya NBC baada ya kuinunua katika harambee hiyo. Kulia ni Waziri Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama na wa pili kushoto ni Mdau Teddy Mapunda mratibu wa harambee hiyo.
Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa akimkabidhi picha Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez baada ya kuinunua katika harambee hiyo.
Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa akimkabidhi picha ya simba Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Hoteli ya Serena, Bw. Seraphin Lusala baada ya kuinunua kwenye harambee hiyo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Geita Gold Mine (GGM), Bw. Tenga B. Tenga akimkabidhi Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa mfano wa hundi yenye thamani ya sh.milioni 100 zilizo tolewa na mgodi huo kuchangia mfuko huo.



MRADI WACUJENZI MAHAKAMA KUU-KANDA YA MSOMA WAENDELEA,WANANCHI WAUPOKEA KWA SHANGWE

$
0
0

Na Mary Gwera 

KAMA ilivyo kwa huduma nyingine katika jamii, huduma ya upatikanaji wa HAKI ni miongoni mwa huduma ambazo wananchi wanahitaji kwa wakati bila longolongo, kufuatia uhitaji huu wa Wananchi, Mahakama ya Tanzania imekuwa na inaendelea katika jitihada za kuboresha huduma ya upatikanaji wa haki kwa kujenga na kukarabati miundombinu bora na wezeshi ya kutolea haki. 

Tukiangazia Mkoa wa Mara ambapo kwa kipindi kirefu wananchi wake wamekuwa na wanaendelea kupata shida hususani katika upatikanaji wa huduma ya haki kwa ngazi ya Mahakama Kuu ambapo Mwananchi mwenye kesi anatakiwa kusafiri kwa kilomita zipatazo 218 kwenda Mahakama Kuu Mwanza ili kutafuta haki yake. 

Kulingana na uhitaji mkubwa wa huduma ya Haki nchini, Mahakama ya Tanzania imekuwa ikifanya ujenzi na matengenezo ya majengo yake kwa awamu kulingana na hali ya bajeti, kwa sasa Mahakama ya Tanzania imeanza ujenzi wa Mahakama Kuu katika mikoa miwili ambayo ni Mara na Kigoma. 

Katika mahojiano maalum na Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma, Bibi. Zilliper Geke yaliyofanyika ofisini kwake Mahakama ya Mkoa-Musoma, Februari 13, Bi. Zilliper anasema kuwa ujenzi wa Mahakama Kuu unaoendelea katika Kanda hiyo umeleta faraja na ukombozi mkubwa kwa wananchi wa Mkoa wa Mara kwani wamekuwa wakisumbuka kwa muda mrefu kusafiri kilometa kadhaa kwenda mkoani Mwanza kutafuta haki zao kwa ngazi ya Mahakama Kuu. 

“Kwakweli wananchi wa Mkoa huu na hata wateja wanaokuja katika Mahakama ya Mkoa, wanaonekana kufurahia ujenzi wa Mahakama Kuu Musoma ambapo pindi itakapokamilika itawaondolea usumbufu wa kusafiri hadi Mwanza kupata huduma” alieleza Mtendaji huyo. 
Mtendaji-Mahakama ya Hakimu Mkazi-Musoma, Bi. Zilliper Geke akiongea jambo katika mahojiano maalum. (Picha na Mary Gwera, Musoma-Mara) 
Muonekano wa sehemu ya jengo la Mahakama Kuu-Musoma likiendelea kujengwa. 
Mafundi wakiendelea na ujenzi. 
Wahandisi wa Mradi huo wakitoa maelezo ya hatua ya ujenzi waliyofikia kwa katika ujenzi wa jengo hilo. 


BBC DIRA YA DUNIA

BIL 23.061 KUTUMIKA MATENGENEZO YA BARABARA PWANI 2018/2019

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani 

KIASI cha sh. bilioni 23.061 zimepangwa kutumika kutoka mfuko wa barabara kwa ajili ya miradi ya matengenezo mbalimbali ya barabara ,mkoani Pwani, katika kipindi cha mwaka 2018/2019 . 

Aidha katika kipindi hicho kiasi cha shilingi bilioni 10.4 zimepangwa kutumika kwa ajili ya matengenezo ya kilometa 518 za barabara kuu madaraja madogo 23 na makubwa mawili. 

Hayo yamesemwa mjini Kibaha na meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Pwani, Mhandisi Yudas Msangi wakati wa kikao cha bodi ya barabara ya mkoa huo. 
Pamoja na hayo ,alisema kiasi cha shilingi bilioni 14 zitatumika kutengeneza barabara zinazounganisha maeneo muhimu ya kiuchumi ili kurahisisha mawasiliano kwenye maeneo hayo. 

Hata hivyo ,Msangi alielezea shilingi bilioni 12.5 zitatumika kwenye matengenezo ya barabara za mkoa huo . 
“Matengenezo ya kawaida lami kilometa 501.7 yametengewa shilingi bilioni 3.1, matengenezo maalumu lami kilometa 15.6 yametengewa kiasi cha shilingi bilioni 7 huku matengenezo ya sehemu korofi 0.7 kilometa yametengewa kiasi cha shilingi milioni 57.9,”alifafanua Msangi. 

Alibainisha matengenezo madogomadogo ya madaraja 23 yametengewa kiasi cha shilingi milioni 74 na matengenezo makubwa ya madaraja mawili yametenegewa kiasi cha shilingi milioni 200.4. 
Nae mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ,alisema katika kuelekea kwenye ukanda wa viwanda ,ni lazima miundombinu ya barabara iboreshwe na kujengwa ili kuvutia wawekezaji. 

Aliitaka Tanroads kutekeleza miradi hiyo kama ilivyoomba ili kutatua changamoto ya miundombinu ya barabara. 
Ndikilo ,aliwaasa pia wananchi kulinda na kuacha kuharibu alama zinazowekwa barabarani . 
Wakati huo huo mbunge wa Kibaha Mjini Silvestry Koka ,aliomba ufafanuzi juu ya ujenzi wa barabara ya kutoka Kwamatias hd Nyumbu. 

Meneja wa TANROADs Pwani ,alimtoa hofu Koka kuwa barabara hiyo itajengwa mita 300 kwa mil.200.9 na ujenzi utaanza wakati wowote kuanzia sasa.
Meneja wa wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) Mkoani Pwani ,mhandisi Yudas Msangi akizungumza jambo ofisini kwake ,kuhusiana na masuala ya barabara Mkoani hapo ( picha na Mwamvua Mwinyi) 

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo(University of Bagamoyo UB) Profesa Costa Mahalu mara baada ya kufanya nae mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo(University of Bagamoyo UB) Profesa Costa Mahalu mara baada ya kufanya nae mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni mtoto wa Profesa Mahalu ambaye ni Mwanasheria wa Kujitegemea Jaji Costa Mahalu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mtoto wa Profesa Mahalu ambaye ni Mwanasheria wa Kujitegemea Jaji Costa Mahalu mara baada ya kumaliza mazungumzo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo(University of Bagamoyo UB) Profesa Costa Mahalu Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

SIXTUS MAPUNDA AMNADI KWA KISHINDO MTULIA, KINONDONI SHAMBA

$
0
0
Mbunge wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda (kushoto) akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni, Said Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo Feb 13, 2018, katika Kata ya Kinondoni Shamba jijini Dar es Salaam
Mbunge wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni, Said Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo Feb 13, 2018, katika Kata ya Kinondoni Shamba jijini Dar es Salaam
Mbombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo jimbo la Kinondoni Sad Mtulia akiomba kura kwa wananch katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Kinondoni Shamba jijini Dar es Salaam, leo Feb 213, 2018
Baadhi ya Wabunge wakiwa jukwaaani kumuombea kura mgombea ubunge wa CCM Said Mtulia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo katika Kata ya Kinondoni Shamba, leo Feb 13, 2018.

WAKULIMA WA KOROSHO PWANI WANEEMEKA

$
0
0

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha 

Wakulima wa zao la korosho Mkoa wa Pwani wamefanikiwa kupata kiasi cha sh. bilioni 57.7 kutokana na mauzo ya zao la korosho ,msimu huu. Mafanikio hayo yametokana na mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umetumika miaka mitatu iliyopita tangu kuanzishwa kwenye Mkoani hapo. 

Hayo yalisemwa mjini Kibaha na mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC). Alisema fedha hizo zimepatikana kutokana na minada sita hadi kufikia Januari mwaka huu ambapo minada hiyo ilianza Novemba mwaka jana. 

Ndikilo alifafanua ,kilo zilizouzwa ni 20,399,325 za daraja la kwanza ni kilo 11,554,380 na daraja la pili ni kilo 8,814,945. “Kilo hizo kwa daraja la kwanza ziliingiza kiasi cha shilingi bilioni 35.8 na daraja la pili shilingi bilioni 21.4 kwa wakulima wa mkoa huo” 

“Wilaya ya Mkuranga imeweza kuongoza kwa kuuza na kupata mapato makubwa ikiwa imeingiza kiasi cha bilioni 13 ikiwa imeuza kilo milioni 4.1, Kibiti waliingiza bilioni 4 kwa kuuza kilo milioni 4,Rufiji bilioni 2.8 kwa kuuza kilo milioni 1.5,” alisema Ndikilo. Awali katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji Shangwe Twamala alieleza, bei ya juu kwa korosho daraja la kwanza ilikuwa ni shilingi 3,817 kwa kilo na daraja la pili ni shilingi 2,950. 
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza na wajumbe wa kikao cha ushauri cha mkoa huo (RCC)kuhusiana na mipango na mkakati mbalimbali ya kuendeleza maendeleo ya kimkoa.(Picha na Mwamvua Mwinyi) .

Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images