Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA JUMATANO YA MAJIVU KANISA LA ST. JOSEPH JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

Bi Hellen Stephan akisoma somo la pili katika ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Februari 14, 2018

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  na mkewe Mama Janeth Magufuli  wakiwa  na waumini wengine katika ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Februari 14, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipakwa majivu pajini wakati wa ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Februari 14, 2018

Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam baada ya kujiunga na waumini wengine katika ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Februari 14, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiagana na waumini wenzao baada ya ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Februari 14, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisindikizwa na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Padri Venance Tegete baada ya kujiunga baada ya ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Februari 14, 2018.
Kwa Picha zaidi BOFYA HAPA

Naibu Waziri awasha Umeme Gongolamboto

$
0
0
Na Zuena Msuya, Dar es salaam 

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewasha umeme katika kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Gongolamboto chenye uwezo wa MVA 65 na hivyo kuimarisha upatikanaji wa umeme katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar s Salaam, Mgalu alisema Kituo hicho kinapokea umeme kutoka katika mitambo ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi katika line ya 132 kV. Mgalu alifafanua kuwa kukamilika kwa kituo hicho kumewezesha uboreshaji wa upatikanaji wa umeme katika maeneo ya Kurasini, Kipawa, Kitunda, Chanika na Kisarawe, Ubungo, Mbagala na GongolaMboto.

“Kwa sasa hali ya kukatika kwa umeme mara kwa mara katika maeneo yaliyokuwa yakisambaziwa umeme kutoka katika kituo hiki haitakuwepo tena, hivyo Serikali itaendelea na juhudi kuwasha umeme katika vituo vingine vilivyosalia,” alisisitiza Mgalu.

Kituo cha Gongolamboto ni miongoni mwa vituo 19 vya kupoza na kusambaza umeme nchini vilivyo katika mradi wa uboreshaji wa vituo hivyo unaofadhiliwa na TEDAP ambapo Jiji la Dar es salaam lina vituo 11, Arusha vituo Sita (6) na Kilimanjaro vituo viwili (2
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (aliyekaa) akiwasha umeme katika kituo cha Gongolamboto kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa njia ya Kompyuta. 
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wa pili kushoto) akipata maelezo ya  uendeshaji wa kituo cha Gongolamboto , kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James,(mbele) wakati akikagua mitambo ya kituo hicho kabla ya kuwasha kwa mtambo huo.kushoto ni Kaimu Meneja Miradi , Mhandisi Emmanuel Manirabona. 
Baadhi ya watendaji katika kituo cha Gongolamboto, wakikamilisha kazi kabla ya kuwasha umeme katika kituo hicho. 
Transfoma iliyofungwa mwaka 57, ( kulia) iliyokuwa ikifanya kazi ya kusambaza umeme katika kituo cha Gongolamboto,na mpya zilizowekwa sasa( kushoto). 
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wapili kushoto) akizungumza na mkandarasi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mbagala. kushoto Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James 

KWANDKWA: SERIKALI KUIMARISHA SEKTA YA UJENZI NA UCHUKUZI MKOA WA TANGA

$
0
0
Na Ismail Ngayonga -MAELEZO 

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa amesema Serikali imekusudia kuimarisha sekta ya ujenzi na uchukuzi katika Mkoa wa Tanga ikiwemo Ujenzi wa Daraja kubwa lenye urefu wa Mita 550 katika Wilaya ya Pangani, hatua inayolenga kufungua fursa na kuinua pato la kiuchumi kwa wanachi wa Mkoa huo. 

Akizungumza katika mkutano wake na Mkuu wa Mkoa huo, Martin Sheghela jana Jumanne Februari 12, 2018, Naibu Waziri Kwandikwa aliyopo katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya barabara Mkoani humo, alisema lengo la Serikali ni kuimarisha miundombinu ya barabara, bandari na uwanja wa ndege katika Mkoa wa Tanga. 

Kwandikwa alisema katika bajeti ya mwaka 2017/18 Serikali imekusudia kuanza ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani-Saadani-Bagamoyo yenye urefu urefu wa kilometa 242, ambapo tayari kazi ya usanifu wa barabara hiyo tayari umeaanza, ambapo wakati wowote kutoka sasa Serikali inatarajia kutangaza zabuni ya ujenzi wa barabara hiyo. 

“Kwa kipande cha barabara ya Tanga-Pangani ambayo imekuwa kilio cha wananchi wa Pangani kwa kipindi kirefu, tayari tumeanza hatua ya usanifu wa barabara hiyo, ambapo Serikali imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 4.3 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo” alisema Kwandikwa. 
Meneja wa TANROAD Mkoa wa Tanga, Mhandisi Alfred Ndumbaro akitoa maelezo ya ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (wa pili kulia)kuhusu ujenzi wa Daraja kubwa lenye urefu wa kilometa 550 linalotarajia kujengwa na Serikali katika Mto Pangani wakati wa ziara yake Wilayani humo jana Jumanne Februari 13 2018. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Bi. Zainab Issa. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akipata maelezo kuhusu ufafanisi wa utendaji kazi wa kivuko cha MV Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya barabara na vivuko katika Wilaya ya Pangani na Mkoa wa Tanga kwa ujumla katika ziara yake jana Jumanne Februari 13 2018. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme Serikalini (TEMESA), Mhandisi Magreth Ginna. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akishuka katika kivuko cha MV Tanga iliyopo Pangani wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya barabara na vivuko katika Wilaya za Mkoa wa Tanga jana Jumanne Februari 13, 2018. Anaongoza nao Diwani wa Kata ya Pangani Magharibi, John Semhande na Meneja wa TEMESA Mkoa wa Tanga, Mhandisi Magreth Ginna na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Zainab Issa. (PICHA NA MAELEZO 

Tanzia

$
0
0
Familia ya wanakifungilo wanasikitika kutangaza kifo cha mama yao mpendwa na mlezi wao Sr. Mary Fidesta Rimisho C.P.S., aliyepata kuwa mkuu wa shule ya Kifungilo kianzia mwaka 1981 hadi 2000, kilichotokea ghafla Jumanne asubuhi tarehe 13 Feb. 

Mazishi yanatarajiwa kufanyika Arusha siku ya Jumamosi tarehe 17 Feb kuanzia saa 4 asubuhi USA River. Habari ziwafikie wanafunzi wote wa Kifungilo, popote pale walipo duniani, wazazi, ndugu, jamaa na marafiki.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu MAMA yetu

Barclays hosts an economic forum for its corporate clients

$
0
0
Barclays Corporate and Investment Banking (CIB) clients were invited for an evening hosted by the bank, whereby the main agenda for the evening was to present the banks 2017 financial performance, future ambitions and the 2018 economic outlook for Tanzania. 

Speaking during the event, which took place at the Serena Hotel, Barclays Managing Director, Abdi Mohamed said “We had a tremendous year in 2017, and look forward to exceeding our own expectations in 2018. Our ambition is to create a business that is modern, agile and fit for purpose. 

Our focus will still be on ensuring we make our customers’ and clients’ lives easier by simplifying our business processes to better serve our customers and clients, by sustainably reducing costs and improving efficiencies. Our continued investment in people, our technology and digital innovation will still be a key component to our success and our commitment to our communities in which we serve will continue to be an area of focus”

In 2017, Barclays was awarded the Best Commercial Bank in Tanzania by the Banker Africa. Abdi continued, “The award received was based on ‘peer voting’, and such, we were proud of this recognition by the industry in Tanzania”.
 Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (left), addresses participants during the bank’s Economic Forum hosted for its corporate and investment banking clients in Dar es Salaam over the weekend. Far from right are Absa Capital economic researcher, Samantha Singh, Barclays Tanzania CFO, Obedi Laiser and banks Corporate Director, Esther Maruma. 
 Barclays Bank Tanzania Chief Financial Officer, Obedi Laiser (left), highlights the BBT performance during the bank’s economic forum hosted for its corporate and investment banking clients.
 Barclays Bank Tanzania Marketing and Communications Manager, Joe Bendera (right), chats with South Africa’s Absa Capital economic researcher, Samantha Singh (left), during the bank’s economic forum hosted for its corporate and investment banking clients in Dar es Salaam. Second left is BBT Corporate Director, Esther Maruma and the bank’s Marketing Officer, Nasikiwa Berya.
Barclays Bank Tanzania senior officials exchange views during the forum. From left: Head of Marketing and Corporate Relations, Aron Luhanga, Chief Financial Officer, Obedi Laiser and Marketing and Communications  Manager, Joe Bendera.


JALADA KESI YA MHASIBU ANAYEDAIWA KUWA NA UTAJIRI WA KUTISHA LAPELEKWA KWA DPP

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, jalada la kesi inayomkabili Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai anayedaiwa kuwa na utajiri wa kutisha kwa kumiliki mali zenye thamani ya Sh.bilioni 3 ambazo haziendani na kipato chake limepelekwa (DPP)ili kulipitia na kulitolea uamuzi.

Wakili wa Serikali, Wankyo Simon amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba. Ksi hiyo ilipofika kwa ajili ya kutajwa

Wankyo alieleza awali jalada hilo lilipelekwa kwa DPP ambapo alilipitia na kulirejesha Takukuru na kuelekeza baadhi ya maeneo yafanyiwe uchunguzi zaidi."Maeneo hayo yamekwishafanyiwa kazi na jalada limerejeshwa tena kwa DPP kwa ajili ya kulipitia na kulitolea maamuzi", amesema Wankyo.

Baada ya kudaia hayo aliiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe nyingine ili waweze kueleza hali ya upelelezi ikoje.Mshtakiwa Gugai aliiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo kwa siku saba kwani mpaka sasa wamefikisha siku 90 wakiwa wako rumande na upelelezi bado.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 21, mwaka huu, pia ameutaka upande wa mashtaka uhakikishe wanalifanyia kazi jalada hilo kwa kuwa limeanza kuwa zee.Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasini Katera

Washtakiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka 43 yakiwemo 20 ya utakatishaji fedha haramu, kumiliki mali zisizoendana na kipato na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika maeneo mbalimbali.

Gugai na wenzake wanasota mahabusu kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya utak

WAHIFADHI WAIOMBA SERIKALI KUCHEPUSHA BARABARA YA LAMI INAYOPITA NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA MIKUMI (TANZAM) ILI KUNUSURU HIFADHI HIYO

$
0
0

Na Hamza Temba-WMU-Morogoro
................................................................
Serikali inafikiria namna bora ya kubadilisha uelekeo wa eneo la kilometa hamsini za barabara ya lami inayopita ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi au kutoza kodi ya utalii kwa watu wanaotumia barabara hiyo ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazosabishwa na barabara hiyo kwenye uhifadhi.

Hayo yamesemwa mkoani Morogoro na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kufuatia ombi la uongozi wa hifadhi hiyo la kuiomba Serikali kuchepusha barabara hiyo kutokana na athari mbalimbali za kimazingira zinazosabishwa na uwepo wa barabara hiyo ndani ya hifadhi hususan vifo vya mara kwa mara vya wanyamapori, ujangili na ukosefu wa mapato ya Serikali.

Awali akiwasilisha taarifa ya hifadhi hiyo mbele ya Waziri Kigwangalla, Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Gerald Mono alisema licha ya barabara hiyo kuwa na fursa nyingi za kimaendeleo imekuwa na changamoto nyingi kwenye uendeshaji wa shughuli za uhifadhi.


Alisema wastani wa mnyamapori mmoja hugongwa na gari kila siku katika barabara hiyo ambapo takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2014 idadi ya wanyamapori waliogongwa walikuwa 351, mwaka 2015 walikuwa 361 na mwaka 2016 walikuwa 218.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua maziringira ya jengo lililoungua moto la Mikumi Wildlife Lodge ambalo linalofanyiwa ukarabati wakati wa ziara yake ya kikazi katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi jana mkoani Morogoro ambapo amemtaka muwekezaji aliyepewa hoteli hiyo kuikarabati ndani ya muda aliopewa ama sivyo atanyang’anywa kibali alichepewa. Kushoto kwake ni Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Gerald Mono. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa  na Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Gerald Mono kukagua mazingira ya hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi katika hifadhi hiyo jana mkoani Morogoro. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo  kutoka kwa Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Gerald Mono wakati wa ziara yake ya kikazi katika hifadhi hiyo jana mkoani Morogoro.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia mazingira mwanana ya  Hifadhi ya Taifa ya Mikumi wakati wa ziara yake ya kikazi katika hifadhi hiyo jana mkoani Morogoro.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MALAWI YAONESHA NIA KUPATA GESI KUTOKA TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amekutana na Ujumbe wa Mawaziri wawili kutoka Malawi na kuzungumza kuhusu uwezekano wa Malawi kupata Gesi Asilia kutoka Tanzania na Uendelezaji wa pamoja wa Bonde la Mto Songwe kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo uzalishaji umeme.

Ujumbe wa Malawi uliongozwa na Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini, Aggrey Masi na Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii, Henry Mussa ambao waliambatana na Balozi wa Malawi nchini, Hawa Ndilowe na wataalam kutoka Taasisi mbalimbali zilizo chini ya wizara zao.

Waziri Kalemani alikutana na ujumbe huo Februari 12, 2018 katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam ambapo alielezwa dhumuni la ziara hiyo ya Mawaziri hao wawili kutoka nchini Malawi.

Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Nishati wa Malawi, Aggrey Masi alisema kuwa Malawi inaupungufu mkubwa wa nishati ya umeme na kwamba jitihada mbalimbali zinafanyika kuhakikisha kiwango cha uzalishaji umeme kinaongezeka.
 Mawaziri kutoka Malawi mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam kwa ajili ya majadiliano kuhusu masuala ya Nishati na mwenyeji wao Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani). Kushoto ni Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini, Aggrey Masi na Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii, Henry Mussa.
 Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya Nishati na Mawaziri kutoka Malawi (hawapo pichani).
 Ujumbe wa Mawaziri kutoka Malawi ukiendelea na majadiliano wakati wa mkutano na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani). Kutoka kulia ni Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini, Aggrey Masi, Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii, Henry Mussa na Balozi wa Malawi nchini, Hawa Ndilowe.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akizungumza jambo wakati wa mkutano na Mawaziri kutoka Malawi. Kulia ni Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini wa Malawi, Aggrey Masi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA



ALIYOYASEMA KAMISHNA USTAWI JAMII WAKATI WA HAFLA YA MAKABIDHIANO YA ZANA ZITAKAZOTUMIKA KUKUSANYA,KUTOA TAARIFA ZA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA HATARISHI.

BIL. 161.9 ZIMETUMIKA KUBORESHA VITUO VYA AFYA 170-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetumia sh. bilioni 161.9 kuboresha vituo vya afya 170 nchini pamoja na kugharamia huduma ya Afya ya Mama na Mtoto kwa lengo la kuokoa maisha yao.

Amsema Serikali itaendelea kukarabati na kupanua miundombinu ya kutolea huduma pamoja na kununua vifaa vya kisasa katika Hospitali za Mloganzila, Benjamini Mkapa, Dodoma na Hosptali za Rufaa katika Mikoa na Kanda.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 14, 2018) wakati akizindua jengo  jipya la mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa-Amana iliyopo wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.

Jengo hilo la ghorofa mbili limejengwa kwa ufadhili wa kundi la kampuni za AMSONS na lina thamani ya sh bilioni 1.2.

Amesema uzinduzi wa jengo hilo  unakwenda sambamba na azma ya Rais Dkt. John Magufuli za kuimarisha sekta ya afya na kuifanya kuwa miongoni mwa sekta za kipaumbele.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha inasogeza huduma za afya karibu na wananchi. “Mfano, Hospitali za Rufaa za Amana, Mwananyamala na Temeke, zimeendelea kuhudumia wagonjwa kutoka Zahanati, Vituo vya Afya vya Serikali, binafsi na vya dini kutoka mikoa jirani ya Pwani, Morogoro na Lindi.

Pia amesema Serikali itaendelea kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 – 2020, kuhusu kuwapatia wananchi huduma bora za afya pamoja na kujenga hospitali nyingine za Rufaa kwa ajili ya Kanda ya Kusini, Kati na Magharibi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

UNACHOSTAHILI BAADA YA KUACHISHWA/KUFUKUZWA KAZI KIMAKOSA.

$
0
0


Na  Bashir  Yakub .


1.  NINI MAANA  YA  KUACHISHWA  KAZI  KIMAKOSA.     

Katika  ujumla  wake  kuachishwa  au  kufukuzwa  kazi  kimakosa ni  hatua  ambapo  mwajiri  anamwachisha  au  anamfukuza  kazi  mwajiriwa  wake  bila  kufuata  utaratibu  wa  sheria.  Mwajiri  asipofuata  sheria  katika  kumuondoa  mwajiriwa  kazini  ndipo  anapokuwa  amemiwachisha  kazi  kimakosa. 


Na  hapa  haiongelewi  Sheria  ya  ajira  na  mahusano  kazini  tu  inayotakiwa kuzingatiwa, bali  sheria  zote  ambazo  huhusika katika  ajira na mikataba  ikiwemo  sheria ya  mikataba  na  nyinginezo. Sheria yoyote   haipaswi  kuvunjwa  au  kukiukwa  wakati  mwajiriwa  anapotakiwa  kuachishwa  kazi.


2.   AINA  MBILI  ZA  KUACHISHWA  KAZI  KIMAKOSA.

Kuachishwa  kazi  kimakosa  kumegawanyika  mara  mbili ;

( a ) KUACHISHWA KWA KOSA AMBALO HALIPO(WRONGFUL TERMINATION).


Hii  ni  pale  ambapo  mwajiri  anamtuhumu  mwajiriwa  kwa  kosa  ambalo  hajatenda  kabisa.  Anamtungia  kosa  ili  amuondoe  kazini  kwasababu   anazojua  mwenyewe.  Au  inakuwa  ni  kweli  mwajiriwa  ametenda  kosa  lakini kosa  lile  halina  hadhi  au  uzito  wa  kumwondoa   kazini.  Sio  kila  kosa  ni  la  kumwondoa  mtu  kazini.  Makosa  mengine  ni  ya  kuonya  au  kuelekeza  tu. 


Kwahiyo  haya yakitokea  ndipo  tunaposema  kuwa mwajiriwa  ameachishwa  kazi   kimakosa.  Kimakosa  kwa  maana  kwa  kosa  ambalo  halipo  au  lipo  lakini  halitoshi  kumuachisha  mtu  kazi( not  justifiable).


( b ) KUACHISHWA KAZI KWA KOSA  AMBALO LIPO  LAKINI  BILA  KUFUATA UTARATIBU(UNFAIR TERMINATION).


Hapa  kosa  linakuwa  ni  kweli  kabisa  limetendwa.  Na  uzito  wa  kosa  lenyewe  unatosha  kabisa  kumuachisha mwajiriwa  kazi.  Tatizo  linakuja  kuwa  wakati  wa  kumuachisha  kazi  kwa  kosa  hilo  utaratibu  unakiukwa.  Kosa  sawa  lipo, lakini   utaratibu  wa  kutumia  kosa  hilo kumwondoa  mtu  ndio  uliokiukwa.


Utaratibu  ni  kama  kutopewa  taarifa(notice) , au kupewa  taarifa  lakini  katika  muda  usiostahili, kutolipwa  stahili, kutopewa  nafasi  ya  kusikilizwa, nk.  Kwahiyo utaona  tofauti  ya aina  hizi  mbili  za  kuachishwa  kazi  kimakosa.


Hata hivyo, pamoja  na  utofauti  huu bado  unachostahili  baada  ya  kuachishwa  kazi  kimakosa  ni  kilekile.  Aliyeachishwa  kwa  kosa  ambalo  halipo  na  aliyeachishwa  kwa  kosa  ambalo  lipo  lakini  kwa  kukiuka  utaratibu  wote  hustahili  stahili  sawa  kama  tutakavyoona hapa.


                           KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com


SERIKALI YAPOKEA ZANA ZITAKAZOTUMIKA KUKUSANYA NA KUTOA TAARIFA ZA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI

$
0
0
Na Beatrice Lyimo, MAELEZO- DODOMA.
Serikali imepokea zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi kwa ajili ya wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya jamii inayojumuisha kata, vijiji na mitaa.

Zana hizo zimekabidhiwa leo mjini Dodoma kwa Kamisha wa Maendeleo ya Jamii Dkt. Naftal Ng’ondi na Shirika la John Snow Inc(JSI) kushirikiana na MEASURE Evaluation na PACT Tanzania kupitia Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii(CHSSP) unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Maendeleo la Watu wa Marekani(USAID).

Wakati wa makabidhiano hayo Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi amesema kuwa ni muhimu kupeana taarifa katika utekelezaji wa mipango mbalimbali iliyopo ili kuwe na matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo hivyo zana hizo zitasaidia katika utoaji wa taarifa zilizo sahihi.

Dkt. Naftali Ng’ondi ameongeza kuwa Serikali kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha mtoto anayeishi katika mazingira hatarishi anapata huduma stahiki.

“ Zana hizi zitasadia wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya jamii katika kuwasaidia watoto waliopo katika mazingira hatarishi” alisema Dkt. Ng’ondi.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii  Dkt. Naftali Ng’ondi akikata utepe kuzindua zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi katika hafla ya makabidhiano ya zana hizo katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14, 2017  mjini Dodoma.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii  Dkt. Naftali Ng’ondi pamoja na wadau wakionesha zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi katika picha ya pamoja na wadau hao mara baada ya Kikao cha makabidhiano ya  zana hizo kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14,2017 mjini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAPOKEZI YA VIFAA VYA MATIBABU ZAHANATI YA KOMKONGA

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe akisaidiana na mganga mkuu katikati na mkuu wa Mkoa kutoa hadubini tayari kwa kuikabidhi kwa viongozi wa Komkonga.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mh. Martine Shigela(kulia) akikabidhi hadubini kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Komkonga Bw.Omary Mngazija ikiwa ni moja ya kifaa kwaajili ya kuboresha huduma za Zahanati ya Komkonga.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mh. Martine Shigela akizungumza na watumishi na wananchi wa Komkonga juu ya utunzaji wa vifaa hivyo na kupongeza uongozi wa Halmashuri kwa ujenzi wa maabara ndogo.
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe aki shukuru Rais kwa fedha alizozitoa na kufikia hatua ya kupokea Vifaa hivyo kwenye Zahanati ya Komkonga.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA




Article 0

Grace Matata @ Sauti za Busara 2018

$
0
0
Another great edition of Sauti za Busara has just ended and this year, the world known music festival 100% live, has seen the debut on its stage of Tanzanian songstress Grace Matata.

The Afro Soul/Jazz singer and songwriter dedicated her music career to develop her distinctive brand as live performer and this persistence was recognized by Festival Manager – Journey Ramadhan, as one of the criteria that has been used to select Grace among the 40+ performers of this year’s edition of the Zanzibar based festival.

The Tanzanian act was booked by the organizers to perform two gigs. On Saturday night Grace entertained a very lively crowd at the Amphitheater stage. A good portion of the attending crown took the foot of the stage to dance along the tunes and lyrics of Grace’s feel good music.

Grace hits such as “Uwe Wangu”, “Utanifaa” were perfectly executed by the band which included: Norman Bikaka (solo guitar), Wilfred Masanja (bass), Frank Nzobaza (drums) and Jonas Mwakibinga (keyboard). “One more song” was enthusiastically and repeatedly requested by the crowd at the end of her set.

The following day, Grace and her band amused a much more Zanzibari crowd at the famous Forodhani Gardens where the organizers of Busara have set a free stage for the duration of the festival. A just less than an hour set, took the audience into a soulful tour of Swahili melodies and stories.
Grace attendance at the Sauti za Busara was completed with her participation as a panelist at the Mover & Shakers forum held on Sunday at the Monsoon Restaurant.

SAUTI SOL TEAM UP WITH BURNA BOY ON A NEW HIT AFRIKAN STAR

$
0
0
Sauti Sol are thrilled to announce the release of their 3rd single ‘Afrikan Star’ from the ‘Afrikan Sauce’ LP. The new release features the versatile Nigerian mega star, Burna Boy and is currently available on all music platforms.

Teaming up with Africa’s king of vibez for this beautiful afro-pop ballad, the track speaks about the beauty of an African woman and love. Co-written by Burna boy, produced by Sauti Sol and mixed-mastered by Supersonic Africa, this song is simply infectious.

The official music video was shot and directed by Mex Films. 

“Working with Sauti Sol was nice, the vibe and mood was grand. We have become family through music.” Burna Boy said.

RAIS WA AFRIKA KUSINI, JACOB ZUMA AJIUZULU

$
0
0
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma jana jioni aliamua kujiuzulu wadhifa wake huo kufuatia kuongezeka kwa shinikizo la kumtaka afanye hivyo kutoka kwa chama chake cha ANC (African National Congress) , kinachotawala nchini humo kufuatia miaka 9 ya kukabiliwa na kashfa za rushwa, kuporomoka kwa uchumi na kushuka kwa umaarufu.

Awali kabla ya kuamua kug'atuka kwake kwenye wadhifa huo wa juu kabisa nchini humo, Rais Zuma alikilalamikia chama chake cha ANC kwa kumtaka aondoke madarakani, ikiwa ni pamoja na kumtishia kumuondoa kupitia kura ya bunge ya kutokuwa na imani naye, iliyopangwa kupigwa hii leo, Alhamisi.

Rais Zuma amesema anaheshimu maagizo ya chama chake cha ANC kwa kumtaka kujiuzulu wadhifa wake, baada ya wiki kadhaa za uvumi kuhusu mustakabali wake. Alinukuliwa akisema “nimeamua kujiuzulu kutokana na kura ya kutokuwa na Imani iliyokuwa imepangwa kupigwa siku ya Alhamisi".

Katika hotuba ya kitaifa aliyoitoa kwa dakika 30 kupitia tekevisheni mbalimbali nchini humo, Zuma alisema, hatua hiyo inaanza kutekelezwa mara moja. 

Zuma amekuwa katika mvutano wa kimadaraka na mfanyabiashara bilionea wa zamani na makamu wa rais, Cyril Ramaphosa ambaye sasa anakuwa rais wa mpito. Ramaphosa aliyeshinda nafasi ya kukiongoza chama cha ANC, baada ya kuchaguliwa mwezi Disemba, atapigiwa kura na wabunge nchini humo kuwa rais mpya wa mpito kati ya leo au kesho Ijumaa. 

WAJUMBE WANNE WA BODI YA WAKURUGENZI YA KAMPUNI YA MBOLEA NCHINI

MAANDALIZI YA UCHAGUZI JIMBO LA SIHA YAMEKAMILIKA

$
0
0
Zikiwa zimebakia siku tatu kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mdogo katika Majimbo 2 na Kata 8 za Tanzania Bara, maandalizi kwa ajili ya Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Siha na Udiwani katika Kata 3 za jimbo hilo lililopo mkoani Kilimanjaro yamekamilika.


Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo  Bwana VALERIAN MARGWE JUWAL amesema vifaa vyote kutoka Tume Makao Makuu kwa ajili ya Uchaguzi huo tayari vimepokelewa na kwamba Mafunzo kwa Watendaji wa Uchaguzi yanaendelea.

Akizungumzia kuhusu kampeni zinazoendelea kwa Vyama vinavyoshiriki Uchaguzi huo Bwana JUWAL amesema kumekuwepo na vitendo vinavyokiuka Maadili ya Uchaguzi ingawa kamati ya Maadili imekuwa ikichukua hatua kwa mujibu wa taratibu.

Ametaja baadhi ya vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani ambavyo vimewasilishwa katika Kamati ya Maadili kuwa ni pamoja na baadhi ya wanachama wa Vyama vya siasa kufanya Maandamano baada ya mikutano, baadhi ya Viongozi na Wanachama wa Vyama hivyo kutoa kauli za vitisho na lugha za maudhi dhidi ya Vyama vingine.

Msimammizi huyo wa Uchaguzi ambaye amewataka wakazi wa Jimbo la Uchaguzi la Siha kujitokeza siku ya Uchaguzi ili kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi wao na kutahadharisha watu au kikundi chochote cha watu watakaojaribu kuvuruga Uchaguzi huo.

Jimbo la SIHA mbali ya kufanya Uchaguzi wa Mbunge lakini pia linafanya Uchaguzi wa Madiwani katika kata tatu za Donyomuruwaki, Gararagua na Kashashi, Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi Februari 17 Mwaka huu sambamba na Jimbo la Kinondoni Mkoani Dar es salaam na Kata nyingine 5.

LUKUVI NA KAMPENI YA FUNGUKA NA WAZIRI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Willium Lukuvi amesema Dar es Salaam ndio inaongoza kwa migogoro mingi ya ardhi nchini.

Amesema ili kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya ardhi ameanzisha kampeni inayofahamika kwa jina la Funguka na Waziri itakayotoa fursa kwa wananchi wenye migogoro kuifikisha wizarani na hatimaye kupata ufumbuzi.

Lukuvi amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua ambazo Wizara yao inachukua kutatua migogoro ya ardhi nchini.

Amesema Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imedhamiria kushughulikia migogoro ya ardhi nchini na kwa mwaka huu yeye pamoja na Naiu Waziri wa wizara hiyo watazunguka maeneo mbalimbali nchini kuwasikiliza wananchi na kutatua migogoro iliyopo.

Kuhusu Dar es Salaam ,Lukuvi amesema ni Jiji ambalo linaongoza kwa migogoro ya ardhi nchini na kufafanua na wilaya inayoongoza ni Kinondoni hasa maeneo ya Tegeta na Mbezi.

"Siku chache zilizopita nimeshughulikia migogoro ya ardhi kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo wananchi zaidi ya 400 nimewasikiliza na kupata ufumbuzi.Na leo hii nimerudi tena Dar es Salaam ambapo kwa leo tu wananchi 420 nitawasikiliza.

"Kwa Dar es Salaam migogoro inatokana na watu kudhulimiwa viwanja, mirathi na mingine watu kuvamia viwanja vya watu wengine na kisha kujenga.Pia ipo migogoro inayoshughulikiwa na Mahakama na iliyotolewa hukumu.

"Migogoro ambayo imetolewa hukumu wizara haina uwezo wa kuishughulikia ,hivyo tunashauri warudi tena mahakamani ili kupata haki. Hivyo tutaendelea kuishughulikia kadri ya uwezo wetu.Tutafanya hivyo kwa nchi nzima,"amesema Lukuvi.

Amefafanua leo, kesho na keshokutwa atakuwa Dar es Salaam na baada ya hapo atakwenda Kagera na kisha atarudi tena Kanda ya Pwani ambapo kuna Dar es Saalam na Pwani.

Akielezea zaidi jitihada zinazofanywa na wizara yake kutatua mgogoro ya ardhi, Lukuvi amesema wakati yeye na Naibu Waziri wakiendelea kushughulikia migogoro hiyo, pia watalaamu wa ngazi mbalimbali wizarani hapo nao wanaishughulikia.

"Ipo migogoro ambayo Waziri wa Ardhi anao uwezo wa kuitafutia ufumbuzi kutokana na mamlaka niliyonayo na ndio maana nimeamua kuwa na kampeni ya Funguka na Waziri ili kusikiliza wananchi.Hivyo kwenye kampeni kuna fomu maalumu ambazo zitajazwa na wananchi na tukifika kwenye mkoa husika watajulishwa ili tuwasikilize.

"Na kwa kuwa tutakuwa tunasikiliza wananchi maeneo ya wazi ,hivyo hata wale ambao watakuwa hawajaandikwa majina nao watasikilizwa,"amesema.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images