Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

MAGUFULI AMEWATENDEA HAKI WANARUFIJI KURIDHIA UJENZI WA STIEGLER'S GORGE RUFIJI - MCHENGELWA

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Rufiji
MBUNGE wa jimbo la Rufiji,mkoani Pwani,Mohammed Mchengelwa amesema Rais Dkt.John Magufuli hakukosea kuridhia kujengwa kwa mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (stiegler's gorge) kwani utafungua milango ya kibiashara ,uchumi ,ajira na maendeleo wilayani humo.
Aidha ameeleza ataendelea kupigania kujengwa kwa barabara kutoka Nyamwage-Utete kwa kiwango cha lami , ili kuondokana na adha wanayoipata watumiaji wa barabara hiyo .
Akizungumzia utekelezaji na namna anavyoendelea kusimamia changamoto zinazowakabili wakazi wa Rufiji,katika mkutano wa wanaCCM Utete na mkoa,Mchengelwa alisema hatokata tamaa kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo .
Alisema nishati ya umeme haijafika kwenye baadhi ya maeneo lakini kutokana na ukubwa wa mradi wa stigglers gauge utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 2,100 za umeme.
"Nampongeza Rais Dk.Magufuli kwa kuridhia na kuelekeza ujenzi huo ujengwe katika wilaya hii,itakuwa mkombozi mkubwa kwetu ,Na uhakika utafungua fursa nyingi za kimaendeleo na kiuchumi " alisema Mchengelwa
 Mbunge wa  jimbo  la  Rufiji ,Mkoani Pwani ,Mohammed Mchengelwa akielezea utekelezaji katika uongozi wake katika kipindi cha miaka  miwili kwa  baadhi ya wanachama wa  Chama Cha Mapinduzi na wananchi Utete ,wakati walipotembelewa na uongozi wa  CCM Mkoani humo.
Mbunge wa  jimbo  la  Rufiji ,Mkoani Pwani ,Mohammed Mchengelwa akimjulia hali mgonjwa katika hospital ya Utete wilayani Rufiji .
(Picha na Mwamvua Mwinyi) Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

DC SHINYANGA AFUNGUA KIKAO CHA TAHOSA, ATOA TAHADHARI KWA WAKUU WA SHULE

$
0
0
 Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine MatiroMatiro amewatahadharisha wakuu wa shule za sekondari wilayani humo kutothubutu kuchangisha pesa kwa wazazi na wanafunzi kwa ajili ya mitihani ya shule na shule kwani ni kwenda kinyume cha agizo la rais John Pombe Magufuli linalokataza michango shuleni.
Matiro ametoa tahadhari hiyo leo Jumatano Februari 7,2018katika kikao cha kwanza kwa mwaka 2018 cha Umoja wa wakuu wa shule za sekondari Tanzania (TAHOSA) halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Vijijini) kilichofanyika  katika ukumbi wa Mwalimu House Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wakuu wa shule 27 za sekondari zilizopo katika halmashauri hiyo. 
Aidha aliwataka wakurugenzi wa halmashauri za wilaya kutumia mapato ya ndani na juhudi za wafadhili au wadau wa elimu kufanikisha mitihani ya wilaya badala ya kuchangisha wazazi na wanafunzi. 
"Naomba mitihani mnayofanya ya Interschool Examination isihusishe michango yoyote kutoka kwa wazazi na wanafunzi, tukihusisha michango tunakuwa tumekwenda kinyume na kanuni, taratibu na matamko yanayotolewa na viongozi wetu”,alisisitiza . 
"Hakikisheni pia pesa za serikali zinatumika kulingana na kanuni na utaratibu uliopangwa,zisipotumika vizuri maana yake mmeshindwa kufanya kazi mtawajibishwa”,alieleza. 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua kikao cha Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSA) halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Vijijini) . Kushoto ni mwenyekiti wa TAHOSA wa halmashauri hiyo Leonard Laurent. Kulia ni Kaimu mkurugezi wa halmashauri hiyo Stewart Makali. 

Wakuu wa shule za sekondari katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Matiro aliwasisitiza wakuu hao wa shule kuwachukulia hatua watu wanaowapa mimba wanafunzi na kuhakikisha wanatoa elimu kuhusu madhara ya ndoa na mimba za utotoni. 

RAIS DKT MAGUFULI NA MAKOMANDOO WA JWTZ

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya askari wa vikosi maalumu (makomandoo) wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) baada ya kufungua kituo cha mafunzo maalumu ya kijeshi huko Mapinga wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Februari 6, 2018. Kushoto kwake ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo.Picha na IKULU

MWINYI ASHIRIKI KUPANDA MITI NA ROTARY INTERNATIONAL CLUB JANGWANI SEKONDARI

$
0
0
RAIS Mteule wa Rotary International, Barry Rassin akikata utepe kuashiria uzinduzi wa zoezi kupanda miti kwenye Shule ya Wasichana Jangwani kushiriki zoezi la kupanda miti kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. Wanaoshuhudia ni Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi (kulia kwake) District Governor, Bwana Kenneth Mugisha (kulia), Mkewe Esther (wa pili kulia) Pamoja nao ni wanafunzi wa shule hiyo. #RIPEinD9211. 
District Governor Kenneth Mugisha akipanda mti kwenye Shule ya Wasichana Jangwani kushiriki zoezi la kupanda miti kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. Wanaoshuhudia (kulia kwake) ni Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (wa pili kulia) na Mke wa Rais Rassin, Esther (kulia) Pamoja nao ni wanafunzi wa shule hiyo. #RIPEinD9211
RAIS Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (kushoto) akiagana na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi baada ya kushiriki zoezi la upandaji miti kwenye shule hiyo. Katikati ni District Governor, Kenneth Mugisha. 
RAIS Mteule wa Rotary International, Barry Rassin alipowasili kwenye Wodi ya watoto wenye mahitaji maalum iliyodhaminiwa na Rotary Clubs kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa ziara yake hospitalini hapo.

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YATEKELEZA MWONGOZO HUDUMA KWA WATUMISHI WA UMMA WENYE ULEMAVU

$
0
0
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Bw. Abbas Mpunga kabla ya kumkabidhi Bajaji ili kumwezesha mtumishi huyo kutekeleza majukumu yake.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na watumishi wa ofisi yake wakati wa tukio la kumkabidhi Bajaji kwa mmoja wa watumishi wa ofisi yake
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akikabidhi nyaraka za umiliki wa Bajaji kwa Bw. Abbas Mpunga.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akikata utepe kabla kumkabidhi Bajaji mmoja wa mtumishi wake Bw. Abbas Mpunga.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

POLE POLE AMTAKA MKURUGENZI HALMASHAURI ILALA KUTOA UFAFANUZI MIKOPO WANAYOTOA

$
0
0
Na David John

KATIBU wa Nec Itikadi na uenezi Taifa wa Chama cha Mapinduzi, Humphrey Polepole ameuagiza uongozi wa Chama hicho wilaya chini ya Ubaya Chuma kumuita mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala na wasaidizi wake ili kupata ufafanuzi kuhusu mikopo wanayotoa.

Amesema kuwa pamekuwepo na malalamiko mengi juu ya eneo hilo hivyo lazima viongozi hao wachama Wilaya kuwaita viongozi hao wa Halmashauri ili waje kueleza.

Polepole ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashuri kuu aliyasema hayo katika kongamano la Maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa Chama hicho. Ambapo pamoja na mambo mengine alisema viongozi hao wa Halmashauri waitwe ili waseme fedha hizo wanamkopesha nani.

"Hapa kuna Malalamiko mengi sana kuhusu mikopo hii nani anapewa sasa ndugu Mwenyekiti mwiteni mkurugenz na watu wake muulizeni hizo fedha anapewa nani "amesema Polepole .Nakuongeza kuwa wanachama hawa wa Chama cha Mapinduzi hawapati mikopo,wanamchi.maana hata kwenye maeneo ambako madiwani wa vyama vingine fedha zinakwenda kwa watu wao.

JINSI YA KUANDAA NA KUTAYARISHA LISHE MAALUMU YA ASILI YA KUONGEZA UZITO NA KUNENEPESHA MWILI

$
0
0
Je,   umekonda  na  kudhoofika   mwili kwa  sababu  mbalimbali kama  vile  kuugua  maradhi au  msongo  wa  mawazo ( stress)?
Uzito wako umepungua  kupita  kawaida ? Unahitaji  kuongezeka uzito  wako kwa  kutumia lishe  maalumu  na  vyakula  vya  asili ?
 Unahitaji  kunenepa   na  kurejea  katika  afya  yako  ya  kawaida   kwa kutumia  lishe maalumu  na  vyakula  vya a sili?
Kama  jibu  lako  ni  NDIO  basi  hii  ni  HABARI  NJEMA  SANA  KWAKO. Unacho takiwa  kufanya  ni   kufahamu  jinsi  ya  kuandaa na  kutayarisha  Lishe  maalumu  ya  Asili ambayo  husaidia  kuongeza uzito wa  mwili pamoja  na  kunenepesha  mwili. 
Kufahamu  kuhusu  namna  na  jinsi  ya  kuandaa, kutayarisha  na  kutumia  lishe  hii maalumu tembelea: https://neemaherbalist.blogspot.com/2018/02/jinsi-ya-kuandaa-na-kutayarisha-lishe.html

PASIPOTI MPYA NI SALAMA ASILIMIA 100 - UHAMIAJI

$
0
0
Na Mwandishi Wetu. 
IDARA ya uhamiaji nchini imewataka watanzania kupuuza habari zinazozagaa kuhusu uvumi wa pasipoti mpya kuwa zimechakachuliwa.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dkt. Anna Makakala amesema wananchi wanatakiwa kupata taarifa sahihi kila mara juu ya kila jambo linalohusu maendeleo yao na mambo yanayoletea ustawi wa Taifa letu,sisi ndio wenye taarifa sahihi zinazohusu Mchakato mzima wa Pasipoti Mpya za Kielektroniki.

Hivi karibuni Rais Dkt. John Magufuli wakati akizindua hati mpya za kusafiria alisema kumekuwapo na wahujumu wa mchakato huo ambao hawakufanikiwa kuiba sh. bilioni 400.Amesema kumekuwapo kwa watu waliozunguka kila kona na kutumia kila njama zote kupiga vita mchakato huo wakidhani watafanikiwa kuhujumu serikali.

Dkt. Anna Makakala amesema hatua hizo za kutoa na kueneza taarifa zisizo sahihi zinawaletea mkanganyiko wananchi na kudhoofisha mawazo na fikra chanya kwa Taifa lao.Amesema ni vyema jamii kutambua kuwa mchakato wa Pasipoti mpya ya kidigitali ni hatua kubwa kwa Taifa hili na si vyema kuutolea Taarifa zisizo sahihi, amewasihi wanahabari kupata taarifa kutoka katika vyanzo sahihi na kuzifikisha kwa walaji ambao ni Wananchi," 

Amesisitiza hatua ya mafanikio ya matumizi ya hati hizo hazitarudi nyuma kwa sababu ya kuwapo na taarifa zisizo sahihi zenye lengo la kupotosha ukweli wa mchakato huo.“Ni vyema jamii kuelewa kazi ya hati hizo ni kulinda usalama wa nchi yetu hivyo Uhamiaji tutaendelea kudhibiti mipaka ya Tanzania na kulinda usalama wa nchi kwa kuwezesha jamii na raia wa kigeni kufuata taratibu katika utokaji,ukaaji na uingiaji wa kila mmoja,” amesema Dkt. Makakala.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dkt. Anna Makakala akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

SIMBA SC YAIBAMIZA AZAM FC BAO 1 - 0, MKUDE GUMZO...

MAGAZETI YA ALHAMIS LEO FEBRUARY 8,2018

MPINA APANGUA HOJA ZA WABUNGE NAMNA WIZARA YAKE INAVYOPAMBANA KUTOKOMEZA UVUVI HARAMU NCHINI

$
0
0
Na John Mapepele, Dodoma

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amepangua hoja zilizotolewa na wabunge kuhusu namna Wizara yake inavyopambana kutokomeza uvuvi haramu ili kunusuru kupotea kabisa kwa samaki na kuchochea kufa kwa viwanda vya samaki na kusababisha kupungua kwa ajira nchini.

Waziri Mpina alitoa ufafanuzi huo wakati akijibu hoja za baadhi ya wabunge bungeni Mjini Dodoma ambao walikosoa hatua zinazochukuliwa na Wizara hiyo katika kupambana na uvuvi haramu hususan katika Ziwa Victoria pamoja na kudhitibi utoroshaji wa samaki na mazao yake nje ya nchi.

“Mimi na Wizara yangu tutahakikisha hili tunalisimamia kwa nguvu zote, hizi ni rasilimali za taifa na haziwezi kugawanwa kwa ukanda, rasilimali hizi zinapashwa kunufaisha nchi nzima kwa hiyo kama Wizara inayosimamia Sheria zilizopitishwa na Bunge hili tutahakikisha kwamba hakuna kabisa uvuvi haramu katika nchi yetu, hakuna mfanyabishara atakayejihusisha na kuuza wala kusambaza nyavu haramu, hakuna kiwanda kitakachochakata samaki wasioruhusiwa, hakuna mtu yoyote atakayevua kwa vyavu haramu wala kufanya biashara haramu ya mazao ya uvuvi ni lazima mali zetu tuzilinde kwa nguvu zote” alisisitiza.
Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, Injinia Arcard Mutalemwa (Mwenye shati jeupe), kufanya tathmini ili kujua uwekezaji uliopo katika Ranchi za Taifa (NARCO) akikabidhi ripoti ya kazi hiyo jana kwa Waziri Mpina na viongozi wakuu wa Wizara hiyo. Mhe. (Picha na John Mapepele)
Picha ya pamoja baina ya Kamati iliyoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (mwenye suti nyeusi na miwani) kufanya tathmini ili kujua uwekezaji uliopo katika Ranchi za Taifa (NARCO) kushoto kwake ni Injinia Arcard Mutalemwa, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Maria Mashingo Katibu Mkuu wa Mifugo, kulia ni Naibu Waziri Abdalah Ulega na Mtendaji Mkuu wa NARCO,Profesa Philemoni Wambura
Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, Injinia Arcard Mutalemwa (aliyesimama), kufanya tathmini ili kujua uwekezaji uliopo katika Ranchi za Taifa (NARCO) akisoma na kuwasilisha ripoti ya kazi hiyo jana kwa Waziri Mpina na Viongozi wakuu wa Wizara hiyo.
Mtendaji Mkuu wa NARCO,Profesa Philemoni Wambura akichangia hoja kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, kwenye kikao cha kukabidhi taarifa ya kamati ya kufanya tathmini ya uwekezaji uliopo katika Ranchi za Taifa (NARCO) jana.(Picha na John Mapepele) .



JUKWAA LANGU Feb 5 2018 Pt 2 TANO LADIES

$
0
0
Katika sehemu ya pili ya kipindi cha Jukwaa Langu Jumatatu hii tumetembelewa na TANO LADIES.
"Wadada" walioamua kuwa sehemu ya msukumo wa maendeleo ya wanawake na mabinti zetu.
Wamezungumzia (pamoja na mambo mengine) nafasi na mchango wao kama Diaspora kwa Tanzania, na pia wanavyopanga kuadhimisha siku ya kimataifa ya Wanawake duniani.
Unaweza ona sehemu ya video yao hapa
https://vimeo.com/253461804

JUKWAA LANGU ni kipindi kinachoijadili TANZANIA YA SASA NA ILE TUITAKAYO. *Tanzania katika jicho la DIASPORA.*
Ungana na Mubelwa Bandio, Dj Luke Joe, Eddie Fundi na waalikwa wengine kujadili mambo mbalimbali kuhusu siasa, afya, uchumi, utamaduni nk.
Usikose.
Ni Jumatatu na kila Jumatatu kuanzia saa 12 kamili jioni mpaka 2 kamili usiku kwa saa za Marekani Mashariki (6:00 - 8:00pm ET)
Ni kupitia Kwanza Radio kwenye TuneIn
http://tun.in/sfwyf ama 202-683-4570
**********************************************
PANEL: Mubelwa Bandio, Dj Luke Joe, Eddie Fundi

PRODUCER: Mubelwa Bandio

BBC DIRA YA DUNIA: Marekani na Uturuki zatoleana macho

WENGI WAJITOKEZA KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA KILIMO BIASHARA CHA PAPAI SALAMA

$
0
0
Na Seleman Msuya

ZAIDI ya wanachama 500 wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), wanatarajiwa kushiriki mafunzo maalum ya kufungua msimu wa kilimo cha Papai salama.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mkikita, Adam Ngamange wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.Ngamange alisema mafunzo hayo yatafanyika Februari 24 mwaka huu yatabeba ujumbe 'Papai salama open speech' kwa lengo la kuunganisha walaji, wazalishaji na wataalam wa kilimo hicho.

Alisema baada ya tafiti kufanyika wamegundua mkanganyiko mkubwa wa taarifa hivyo kupitia mafunzo hayo ni wazi mabadiliko katika kilimo cha Papai yatatokea."Tafiti zinaonesha watalaam wanatofautiana kwenye idadi ya miche, uchimbaji wa mashimo, umwagiliaji maji na utiaji mbolea hivyo mafunzo haya yataweka washiriki kwenye mstari ili kukidhi ubora na ulinganifu wa soko la ndani na nje," alisema.

Mkurugenzi huyo alisema mafunzo hayo yatawakutanisha wabobezi na watendaji mbalimbali katika kilimo hicho kipya cha Papai salama yatakuwa na awamu tatu tofauti ili kujenga misingi imara katika kuleta unafuu wa uzalishaji papai.Alisema Mkikita imejipanga kikamilifu katika kuhakikisha wakulima wa Tanzania hasa wanaolima papai, mchaichai, mhogo na pilipili kichaa.

Aidha, Ngamange alisema pamoja na mafunzo hayo wanatarajia kupokea ugeni kutoka nchini Uturuki kutambua fursa za zao la papai nchini.Pia alisema wanachama wa Mkikita wanatarajia kufanya ziara ya mafunzo Nchini Israel kuanzia Machi 11 mwaka huu na kugharimu dola za Marekani 2,000.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange (kulia), akibadilishana hati za makubaliano ya ushirikiano na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema), Askofu Edger Mwamfupe katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Spice leo makutano ya Mitaa ya Narung'ombe na Lumumba Dar es Salaam leo.Taasisi hizo zitashirikiana katika nyanja za teknolojia na Kilimo kwa lengo la kuunganisha nguvu za umoja ili kuwapunguzia wananchi umasikini. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema), Askofu Edger Mwamfupe akizungumza katika mkutano na wanahabari na kuelezea ni kwa nini wameamua kuingia ushirikiano na Mkikita kuwakomboa wananchi masikini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui S. Kissui na Adam Ngamange.

Ngamange akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya semina ya mafunzo ya Kilimo biashara cha Papai Salama.

Kipindi cha JUKWAA LANGU: SARATANI

$
0
0
Katika sehemu ya kwanza ya kipindi cha Jukwaa Langu, tumezungumzia kuhusu siku ya SARATANI DUNIANI iliyoadhimishwa  Feb 4.
· Takwimu za maradhi haya zinaonyesha kwamba kifo 1 kati ya 6 hutokana na maradhi haya.
· Wajua, namna yanavyoathiri nchi zinazoendelea? Ni 20% tu zenye takwimu sahihi kuwezesha kupambana na maradhi haya.
Unajua ni tabia gani maishani zinaweza kuondoa 30% ya Saratani?
· Unafahamu harakati zinazofanywa na Diaspora katika kupambana na maradhi haya?
· Tulikuwa na Mwanasayansi na Mtafiti wa aina mojawapo ya Saratani, pamoja na mwanaharakati kujadili haya.
......
JUKWAA LANGU ni kipindi kinachoijadili TANZANIA YA SASA NA ILE TUITAKAYO. *Tanzania katika jicho la DIASPORA.*
Ungana na Mubelwa Bandio, Dj Luke Joe na waalikwa wengine studioni kujadili mambo mbalimbali kuhusu siasa, afya, uchumi, utamaduni nk.
Usikose.
Ni Jumatatu na kila Jumatatu kuanzia saa 12 kamili jioni mpaka 2 kamili usiku kwa saa za Marekani Mashariki (6:00 - 8:00pm ET)
Ni kupitia Kwanza Radio kwenye TuneIn
http://tun.in/sfwyf ama 202-683-4570
**********************************************
PANEL: Mubelwa Bandio, Dj Luke Joe, Eddie Fundi

PRODUCER: Mubelwa Bandio

INTRODUCING DASHIE FT RUBY MPUTA (OFFICIAL VIDEO)

JKCI yafanya semina ya afya ya moyo,magonjwa yasiyoambukiza kwa Wabunge mjini Dodoma.

$
0
0
Wazazi wametakiwa kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo
zote zinazotakiwa ili waweze kuepukana na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo.

Rai hiyo imetolewa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia
wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiongea na wabunge
waliohudhuria semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza
iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo
ilifanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.

Waziri Ummy aliwaomba wabunge hao kila wanapokutana na wananchi
kupitia mikutano ya hadhara wawasisitize umuhimu wa kuwapeleka watoto
wao katika vituo cha afya ili wakapate chanjo zinazohitajika kwa
wakati.

Aidha Waziri huyo alisema kuwa matibabu ya moyo pamoja na magonjwa
mengine yasiyoambukiza ni ya gharama kubwa na kuwaomba wabunge hao
kuwahimiza wananchi kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambao
utawasaidia kupata matibabu katika Hospitali zote nchini ikiwemo JKCI
na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Katika hatua nyingine Mhe. Ummy aliwataka wakurugenzi wa Taasisi
zingine kuiga mfano wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete Prof. Mohamed ambaye kupitia uongozi wake na jitihada zake
binafsi Taasisi hiyo imeweza kutoa huduma bora na kuwahudumia wananchi
vizuri katika matibabu ya moyo na hivyo kuokoa maisha ya watanzania
wengi.
 Mbunge wa Lupa Mhe. Victor Mwambalaswa akiwasisitiza wabunge wenzake umuhimu wa kupima afya zao hasa tezi dume kwa wanaume wakati wa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana  katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.

 Mbunge wa  Bunda mjini  Mhe. Ester Bulaya akieleza jinsi anavyoridhishwa  na huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na JKCI ambayo ilifanyika jana  katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akielezea mpango wa Serikali kupitia Hospitali za mikoa wa kusomesha madaktari bingwa wengi ili kuweza kukabiliana na uhaba wa wataalam  hao wakati wa  semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana   katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na Daktari wa Bunge Jeminian Temba mara baada ya kumalizika kwa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana   katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma. Katikati ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Yona Gandye.

SERIKALI YAANDAA ENEO KWA VIJIJI VILIVYOATHIRIWA NA MVUA MKOANI DODOMA

KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe,Mohamed Aboud Mohamed kulia akibadilishana mawazo na Waziri wa Fedha na Mipango Dk,Khalid Salum Mohammed ndani ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi lililoanza jana chukwani mjini Zanzibar.
Muakilishi wa Jimbo la Chakechake Suleiman Sarahan Saidi akichangia Mswada wa sheria ya kufuta Sheria ya kusimamia mwenendo wa Biashara na kumlinda mtumiaji Namba 2 ya mwaka 1995 na kutunga sheria mpya ya ushindani halali wa Biashara na kumlinda mtumiaji kuweka masharti bora zaidi pamoja na mambo mengine yanayohusiana na hayo ndani ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi lililoanza jana Chukwani mjini Zanzibar.
Muakilishi wa Jimbo la Kijito upele Ali Suleiman Ali(Shihata) akichangia Mswada wa sheria ya kufuta Sheria ya kusimamia mwenendo wa Biashara na kumlinda mtumiaji Namba 2 ya mwaka 1995 na kutunga sheria mpya ya ushindani halali wa Biashara na kumlinda mtumiaji kuweka masharti bora zaidi pamoja na mambo mengine yanayohusiana na hayo ndani ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi lililoanza jana Chukwani mjini Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

PESA ZA MAENDELEO HAZINA CHAMA-SALUM MWALIMU

$
0
0
 Mgombea Ubunge wa CHADEMA, Salum Mwalimu akihutubia katika Mkutano wa Wananchi uliofanyika katika Kata ya Kigogo akiomba kura hili aweze kupata ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni katika Uchaguzi Mdogo wa Marudio utakaofanyika February 17, 2018
 Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akumuombea Kura Mgombea Ubunge wa CHADEMA Salum Mwalimu katika Mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Raound abot ya Kigogo .
 Waziri Mkuu Mstaafu, na Kampeni Meneja wa Mgombea Ubunge wa Chadema , Fredrick Sumaye akihutubia Wananchi wa kata ya Kigogo katika Mkutano uliofanyika Kigogo.
 Mgombea Ubunge wa CHADEMA, Salum Mwalimu , akiwa Juu ya gari  na kuwapungia mkono wakazi wa Kigogo mara baada ya kumaliza mkutano wake wa kuomba kura kwa Wananchi
Sehemu ya Wananchi wa kata ya Kigogo waliojitokeza kwa wingi katika Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Salum Mwalimu.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>