Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live

ekari sita za bangi zateketezwa mkoani arusha

$
0
0

Waziri wa mambo ya ndani nchini,Dkt Mwigulu Nchemba leo ameongoza oparesheni ya kuteketeza jumla ya ekari sita za bangi zilizokuwa zimelimwa katikati ya msitu ndani ya kijiji cha Engalaoni wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Mwigulu akishirikiana na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha,(RPC)Charles Mkumbo pamoja na vikosi vya askari wa jeshi la polisi mkoani hapa walilazimika kuacha magari yao njiani na kutembea umbali wa kilomita 5 milimani kufika katikati ya msitu huo ambapo wamiliki wa mashamba hayo walitokomea kusikojulikana.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo Mwigulu alisema kwamba serikali itaendelea na oparesheni pande zote za nchi na haitasita kuwakamata wahusika wote na kutaifisha magari yatakayotumika kusafirisha bangi.

Akizungumza na askari waliokuwa wakishiriki katika zoezi hilo Mwigulu mbali na kuwapongeza kwa kazi wanayofanya lakini aliwambia kwamba pamoja na kufanikiwa kuteketeza madawa ya kulevya yanayolimwa mashambani lakini waongeze juhudi pia katika kupambana na madawa ya kulevya yanayotengenezwa viwandani.
Waziri wa mambo ya ndani nchini,Dkt Mwigulu Nchemba leo ameongoza oparesheni ya kuteketeza jumla ya ekari sita za bangi zilizokuwa zimelimwa katikati ya msitu ndani ya kijiji cha Engalaoni wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Waziri wa mambo ya ndani nchini,Dkt Mwigulu Nchemba leo ameongoza oparesheni ya kuteketeza jumla ya ekari sita za bangi zilizokuwa zimelimwa katikati ya msitu ndani ya kijiji cha Engalaoni wilayani Arumeru mkoani Arusha.

MWANASHERIA MKUU AKIJITAMBULISHA KWA WAZIRI MKUU

$
0
0
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mjini Dodoma hapo jana, ikiwa ni sehemu ya ratiba yake ya kujitambulisha kwa viongozi mbalimbali mara baada ya kuapishwa Bungeni mwanzoni mwa wiki. Picha kwa hisani ya PMO.

NAIBU WAZIRI AFANYA ZIARA KUKAGUA UTEKELEZAJI MIRADI YA UMEME VIJIJINI

$
0
0
Mwishoni mwa wiki Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametembelea na kukagua utekelezaji wa Miradi ya umeme vijijini (REA II & REA III) kwenye jumla ya vijiji 18 katika wilaya za ROMBO, MWANGA NA SAME Mkoani Kilimanjaro.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri aliongea na wananchi, pia kutambulisha wakandarasi wa miradi ambapo aliwaagiza wakandarasi waepuke kurudia makosa yaliyojitokeza awali na kuhakikisha wanakamilisha kazi ndani ya muda uliopangwa.

Pia Katika ziara hiyo Mh. Naibu waziri alitembelea bwawa la kuzalisha umeme la NYUMBA YA MUNGU kujionea shughuli za uzalishaji.Naibu waziri amemaliza ziara yake Januari 26/2018 na kuelekea jijini TANGA.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwaeleza wananchi wa kijiji cha Mkisha kuhusu kifaa kijulikanacho kama UMETA (REDY BODY) kifaa hicho hutumika kama mbadala wa kusuka mifumo ya waya (wiring) ndani ya nyumba. Aliyeshika kifaa hicho ni Afisa uhusiano TANESCO KILIMANJARO Bw. Samuel Mandari.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wanakijiji na kueleza uhitaji wa huduma ya umeme.

Wanakijiji wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) akieleza uhitaji wa huduma ya umeme.Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Mkuu wa wilaya ya Same Mh. Rosemary Senyamule, Kamati ya Ulinzi na usalama wilaya, wakiwa na viongozi wa TANESCO MKOA wa Kilimanjaro walipo tembelea Kijiji cha Vunta wilayani Same.

WAVURUGA ELIMU KONDOA WAMKERA MKUU WA WILAYA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mh. Sezaria Makota amesema hatowafumbia macho wale wote wenye nia ya kuishusha wilaya ya Kondoa kielimu kwa kuvuruga kwa makusudi mikakati ya kuinua elimu wilayani humu.

Aliyasema hayo wakati wa kikao cha wadau wa elimu wa Halmashauri ya Mji Kondoa kilichofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi hivi karibuni na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu ili kujadili changamoto na  mikakati ya kuinua elimu ndani ya Wilaya ya Kondoa.

Alisema kuwa katika utawala wake hatoruhusu elimu kushuka kwani matokeo ya darasa la saba mwaka jana wilaya imeshuka kiwastani ukilinganisha na mwaka juzi ambapo wilaya ilikuwa na wastani wa asilimia 80 na mwaka jana imeshuka na kufikia asilimia 71 hivyo viongozi wajipange kusimamia elimu ili kuhakikisha ufaulu unapanda.

Aidha aliwaagiza maafisa elimu kumpelekea mipango yao ili kuona jinsi gani wanainua elimu na kutaka viongozi wa Halmashauri kuacha migogoro na kutekeleza mipango kwa vitendo ili kufikia mafanikio katika elimu.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kwapakacha Mwalimu Pantaleo akisoma barua katika kikao cha wadau wa elimu iliyoandikwa na mwanafunzi wa kidato cha pili akielezea sababu za kutaka kuacha shule.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa akimwelekeza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tungufu kupandisha ufaulu baada ya kupokea cheti cha shule yenye ufaulu duni Wilayani katika kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi hivi karibuni.
 Katibu Tawala Wilaya ya Kondoa, Winnie Kijazi akimpa zawadi mmoja ya walimu waliofaulisha kwa alama A katika mtihani wa darasa la saba mwaka 2017 kwenye kikao cha wadau wa elimu.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

JESHI LA ZIMAMOTO MKOANI ARUSHA LAMUUNGA MKONO JPM

$
0
0
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Arusha limemkabidhi vifaa vya kuzimia moto (fire extenguisher’s) sita mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya nyumba za polisi zilizojengwa mkoani humo.

Akikabidhi vifaa hivyo kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Arusha Kamanda, Kennedy Komba amesema Jeshi hilo lina wajibu wa kuhakikisha ujenzi wa nyumba za makazi unazingatia vigezo vyote vya usalama, wao kama Jeshi wanaunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika kuhakakikisha makazi ya askari polisi yanakua bora.

“Sisi kama Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Arusha tunaunga mkono jitihada za Amiri Jeshi Rais Magufuli sambamba na wadau wengine waliochangia ujenzi katika kuhakikisha nyumba hizi mpya za askari ambazo ziliungua moto miezi michache iliyopita zinakua salama kwa kuweka vizima moto katika kila nyumba kama matakwa ya usalama yanavyohitaji” alisema Kamanda Komba.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alipongeza sana jeshi hilo kwa kuonyesha moyo wa kujali jitihada za Rais Magufuli na wao kufanya kitu ambacho kinatuma ujumbe kwa jamii juu ya umuhimu wa kuzingatia usalama dhidi ya Majanga ya Moto.

“Kwakweli nimefurahi sana kupokea hizi fire extinguishers kwaajili ya nyumba zetu za polisi pia tunafurahi kuona hata taasisi za serikali zikishirikiana na Mhe Rais kufanikisha mradi huu,pia uwekaji wa vifaa hivi unatukumbusha hata sisi tunapojenga nyumba zetu ni muhimu sana kukumbuka kuweka vifaa vya tahadhari kwani kinga ni bora kuliko tiba” alinukuliwa Gambo.

Ujenzi wa nyumba hizo 31 kwaajili ya makazi ya askari polisi umetokana na janga la moto lililosababisha jumla ya kaya 13 za askari katika kituo kikuu cha Polisi mkoani Arusha kupoteza makazi na mali miezi michache iliyopita.Mradi huu wa nyumba za polisi umegharimu zaidi ya shilingi milioni 540 ambapo shilijngi milioni 260 zimetolewa na Rais Magufuli.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akipokea fire extinguisher toka kwa Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Arusha Kennedy Komba kwaajili ya nyumba za Polisi zilizojengwa mkoani humo.

Halmashauri Kishapu yaboresha huduma za elimu kupitia ushirikishaji wananchi

$
0
0
Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi.

Serikali ya Tanzania imeweka mkazo kuboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi katika kujifunza ambayo ndiyo chachu ya mabadiliko na kufanya sekta hiyo nyeti ipige hatua.

Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na ongezeko la uandikishaji, kuleta usawa wa kijinsia kwenye shule za msingi na sekondari nchini.Kumekuwa na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu na hivyo kufanya hamasa katika utendaji wa walimu ishuke na vivyo hivyo kwa wanafunzi.

Ili kukabiliana na changamoto hizo, Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa pamoja ikishirikiana na Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu (Equip-Tanzania) imewekeza katika maendeleo ya sekta hiyo.Huu ni mpango unaotekelezwa na Serikali ili kuboresha mazingira ya mwanafunzi katika kujifunza ambao kwa sasa upo katika mikoa mitano ikiwemo Shinyanga, Tabora, Dodoma, Simiyu na Kigoma.

Itakumbukwa Equip-Tanzania ilianzishwa kwa malengo ya kutoa mafunzo na utendaji kazi kwa walimu pamoja na uongozi wa shule ambao tunashuhudia unavyoendelea kutekelezwa kupitia kwa walimu wakuu.

Pia inalenga kutekeleza mipango ya usimamizi wa elimu katika ngazi ya wilaya na mkoa kupitia kwa maofisa wake wa elimu ambao wanasimamia ngazi za chini yake zikiwemo kata.Mpango huo unalenga kuhakikisha kuwa ukusanyaji wa taarifa mbalimbali, takwimu na uwajibikaji katika suala zima la elmu mashuleni unafanyika ili kuboresha sekta hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (kushoto) akiwa na wataalamu Afisa Mipango, Mang'era Mang'era na Afisa Elimu Msingi Wilaya, Sostenes Mbwilo wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Elimu Ufundi, Moshi Balele kuhusu hatua za ujenzi wa chumba cha darasa shule ya msingi Migunga unajengwa pia kupitia nguvu za wananchi.
 Mradi wa vyoo vya wanafunzi katika shule ya msingi ukikaguliwa na maafisa elimu kutoka Halmashauri ukiwa katika hatua za umaliziaji mbali ya kutumika kwa fedha za Serikali pia mradi huo umechangiwa na nguvu kazi ya wananchi.
Sehemu ya vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Migunga ikiendelea kujegwa katika shule ya msingi Migunga ikiwa ni muendelezo wa mradi wa kuboresha huduma za sekta ya elimu. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MKUU WA TAKWIMU ATOA TAKWIMU ZA BEI ZANZIBAR

$
0
0
 Mkuu wa Takwimu za Bei Zanzibar Khamis Abdul-rahman Msham akitoa maelezo kuhusiana na Takwimu za Bei ambapo zimeonekana kushuka kutoka asilimia 5.9 kwa Mwezi wa Disemba 2017 hadi asilimia 5.2 kwa mwezi wa January 2018 hafla iliofanyika Ofisi kuu ya Takwimu  Mazizini Mjini Unguja.
 Meneja wa Uchumi wa Benki ya Tanzania Tawi la Zanzibar Moto Ng'winganele Lugobi katikati akitoa ufafanuzi wa Baadhi ya maswala yaliouliza na katika hafla ya  kutoa Takwimu za Bei ambapo zimeonekana kushuka kutoka asilimia 5.9 kwa Mwezi wa Disemba 2017 hadi asilimia 5.2 kwa mwezi wa January 2018 hafla iliofanyika Ofisi kuu ya Takwimu  Mazizini Mjini Unguja.kulia yake ni Mkuu wa Takwimu za Bei Zanzibar Khmis Abdul-rahman Msham na kushoto ni Mhadhiri wa Uchumi SUZA Dk, Suleiman Simai Msaraka.
Meneja Msaidizi Uchumi Benki kuu ya Tanzania Tawi la Zanzibar Deagratias Philip Mache akijibu baadhi ya maswala yalioulizwa  katika hafla ya kutoa Takwimu za Bei katika Ukumbi wa Ofisi kuu ya Takwimu  Mazizini Mjini Unguja.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika hafla ya kutoa Takwimu za Bei katika Ukumbi wa Ofisi kuu ya Takwimu  Mazizini Mjini Unguja.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Zaidi ya Bilioni 25 kutekeleza shughuli mbalimbali Halmashauri Wilaya Njombe

$
0
0
Na Lukelo Mshaura- Njombe.

Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Njombe limepitisha mapendekezo ya rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 wilayani hapa.

Katika mapendekezo hayo baraza hilo limepitisha kiasi cha zaidi ya bilioni 25.2  kutumika katika kutekeleza shughuli mbalimbali kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019.

Akisoma mpango na rasimu ya  bajeti  kwenye kikao cha baraza la madiwani ,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Bi Monica Kwiluhya alivitaja vyanzo vya kufanikisha bajeti hiyo kuwa ni Serikali Kuu, wafadhili, mapato ya ndani, uchangiaji wa huduma za afya, uchangiaji wa ada kidato cha tano na sita pamoja na mchango wa jamii kwenye miradi ya maendeleo.

Akiainisha mchanganuo wa vyanzo hivyo  Bi Kwiluhya alibainisha kuwa Serikali kuu inatarajiwa kuchangia kiasi cha bilioni 20.179, wafadhili bilioni 2.965, mapato ya ndani halisi bilioni 1,439, uchangiaji huduma za afya  zaidi ya milioni 140, uchangiaji ada ya kidato cha tano na sita milioni 42 huku mchango wa jamii kwenye miradi ya maendeleo ukiwa ni kiasi cha milioni 520.

Bi kwiluhya alifafanua kuwa  mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri ya wilaya ya Njombe imekadiria kutumia zaidi ya bilioni tano ( 5) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye maeneo mbalimbali ya Halmashauri.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe, Bi Monica Kwiluhya akiwasilisha mapendekezo ya mpango na bajeti wa Halmshauri ya wilaya ya Njombe wa mwaka 2018/2019.
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe wakifuatilia mjadala wa mapendekezo ya  bajeti ya halmashauri hiyo ya mwaka wa fedha 2018/2019.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

BAKWATA YAGEUKA MBOGO SAFARI ZA HIJJA

ZAIDI YA BILIONI 2.1 KUKARABATI BIHAWANA NA DODOMA SEKONDARI

$
0
0
Na Ramadhani Juma, Ofisi ya Mkurugenzi .

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 2.1 kwa ajili ya kukarabati Shule za Sekondari za Bihawana na Dodoma zilizopo Manispaa ya Dodoma ikiwa ni sehemu ya utekezaji wa mpango wa Serikali wa kuzifanyia ukarabati mkubwa Shule kongwe Nchini.

Kati ya Fedha hizo, zaidi ya Shilingi Bilioni 1.2 zitatumika kukarabati Shule ya Sekondari ya Bihawana pekee na zaidi ya Shilingi Milioni 900 zitatumika katika Shule ya Sekondari ya Dodoma.

Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kazi ya ukarabati katika shule hizo jana, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA Graceana Shirima alisema kuwa, shughuli ya ukarabati ilitanguliwa na upembuzi yakinifu wa hali halisi ya mahitaji ya ukarabati uliofanywa na mtaalamu mshauri ambaye ni Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

“Baada ya upembuzi yakinifu, maeneo ya kipaumbele katika ukarabati kwa awamu hii itahusisha Madarasa, maabara, bwalo na jiko,  vyoo, na mifumo ya umeme, mifumo ya TEHAMA na mifumo na maji safi na maji taka” alisema Shirima.

Alisema  awamu hii ya ukarabati inatarajiwa  kukamilika ndani ya kipindi cha  miezi minne, na awamu nyingine za ukarabati zitatekelezwa kulingana na upatikanaji wa fedha.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Graceana Shirima (wa pili kushoto) akikagua shughuli ya ukarabati katika Shule ya Sekondari ya Dodoma baada ya kuzindua rasmi kazi hiyo. TEA imetoa zaidi ya Shilingi milioni 900 kwa ajili ya ukarabati huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi na kulia ni Mhandisi Lupakisyo Mwalwiba ambaye ni Meneja Miradi kutoka Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)  ambaye ndiyo Mtaalamu Mshauri. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA Graceana Shirima (kushoto) akikagua maeneo mbalimbali yanayofanyiwa ukarabati katika Shule ya Sekondari ya Bihawana iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma jana mara baada ya kufanya uzinduzi rasmi wa kazi hiyo. TEA imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 1.2 kwa ajili ya kuikarabati Shule hiyo.

 Ukarabati ukiendelea katika Shule ya Sekondari ya Dodoma.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

2000 WAIBUKA NA USHINDI WA 1GB PROMOSHENI SHINDA NA SMATIKA

CREATING A BETTER LIFE IN TANZANIA

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Bungeni mjini Dodoma Februari7, 2018.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge , Kazi, Vijana, Ajira na  Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiteta na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya, Bungeni mjini Dodoma Februari 7, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mbunge wa Hanang, Dkt. Mary Nagu, bungeni mjini Dodoma Februari 7, 2018. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara kuelekea kwenye jengo la utawala la Bunge Mjini Dodoma Februari 7, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kavuu, Dkt. Pudenciana Kikwembe kwenye jengo la utawala la Bunge Mjini Dodoma, Februari 7, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

UHAMIAJI YAWACHUNGUZA WATOTO WATATU RAIA WA RWANDA KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI

$
0
0
Na Jumbe Ismailly, Singida
IDARA ya Uhamiaji Mkoa wa Singida inawashikilia kwa uchunguzi watoto wa kike watatu raia wa  Rwanda wenye umri chini ya miaka 18 kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria.

Kaimu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Singida,Kamishna Msaidizi, Angela Shija amesema watoto hao wenye umri kati ya miaka 9 na 13 walikamatwa Januanri 30,mwaka 2018 wilayani Manyoni.

Amesema walikuwa  wakitokea nchini Rwanda wakielekea nchini Zambia kuwaona wazazi wao.

“Januari 30 mwaka 2018,  ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Singida ilifanikiwa kuwakamata watoto wa kike watatu raia wa Rwanda.

"Walikamatwa wilayani Manyoni mkoani Singida wakiwa kwenye basi namba T 265 BFY mali ya Kampuni ya Katagi,” amefafanua Kamishina huyo msaidizi

Kwa mujibu wa Ofisa Uhamiaji  Idara ya Uhamiaji ilifanikiwa kuwakamata watoto hao kutokana na taarifa za raia wema na watoto hao wamedai wanaelekea nchini Zambia kuwaona wazazi wao.

Hata hivyo Kamishina Msaidizi huyo wa Jeshi la Uhamiaji limeweka bayana kuwa Idara ya Uhamiaji mkoani Singida inaendelea na uchunguzi ili kubaini watu waliojihusisha na biashara hiyo ya   usafirishaji wahamiaji haramu.

Aidha Kaimu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Singida ametoa mwito kwa wananchi  kujenga utamaduni wa kutoa taarifa kwenye ofisi zao au kwenye vituo vya polisi vilivyo karibu mara wanapowaona watu wasiowafahamu.

Amefafanua kuwa taarifa hizo zitaisaisi Uhamiaji kufanyia kazi za kubaini matukio ya watu wa aina hiyo na kuwachukulia hatua za kisheria.

Amesisitiza baada ya uchunguzi kukamilika na kuwabaini waliohusika katika biashara hiyo ya kuwasafirisha,na kwa sababu wana umri chini ya miaka 18,watoto hao watarudishwa nyumbani kwa wazazi wao nchini Rwanda.
 Watoto wa kike watatu raia wa Rwanda wenye umri chini ya miaka 18 kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria wakiwa kwenye ofisi za idara hiyo Mkoa Singida
 Baadhi ya Maafisa Uhamiaji waliopo katika Ofisi za Mkoa wa Singida (Picha zote Na Jumbe Ismailly)

HYATTY REGENCY HOTEL YAJIANDAA NA VALENTINE


WAHAMIAJI WALOWEZI WATAKIWA KUJIORODHESHA UHAMIAJI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
IDARA ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imewataka  wahamiaji walowezi kujiorodheshwa Marika ofisi zao za uhamiaji  wilaya.

Lengo ni kwamba baada ya kufanya hivyo watapewa vibali ya ukaazi vitavyofanya kuishi nchini kwa mujibu wa sheria , kanuni na taratibu.

Hayo yamesemwa leo  jijini Dar es Salaam, Naibu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Petro Malima na kuwa uandikishaji wahamiaji walowezi ni la nchi nzima.

"Hivyo kwa wahamiaji walowezi lazima wajiorodheshe kwa kuwa na picha tatu za Paspoti zilizo katika wakati na wenye watoto wanatakiwa kuwa na picha tatu hizo", amesema.

Ameongeza kwa wale wataofanya hivyo watatambulika na kuendelea kuishi nchini bila kusumbuliwa kuhusu masuala ya uhamiaji na kutofautisha na wakimbizi na wahamiaji haramu.

Malima amesema wageni wote wanatakiwa kuitikia mwito huo wa Serikali pamoja na wale ambao wanaishi nchini na  kufanyakazi au biashara kinyume na sheria za nchi wanatakiwa kufika katika ofisi za wilaya ili  kuhalalisha ukaazi na kupewa vibali vinavyostahili kwa mujibu wa sheria za nchi.

Amesema  yeyote atakayejificha katika mchakato huo na baadaye kubainika anaishi kinyume cha cha sheria hatua kali zitachukuliwa.

Hatua hizo ni pamoja na kufukuzwa nchini mara moja au kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kukiuka sheria.

Aidha Malima amesema kuna matapeli wamekuwa wakiwasumbua wageni wanaoingia nchini kwa kudai wao ni askari au maofisa wa uhamiaji na wakiwa hawana hata sare.

“Viongozi wetu wanajitahidi kwa kila hali kuitangaza nchi yetu na kuvutia wawekezaji sisi uhamiaji Dar es Salaam hatuwezi kukaa kimya na kuona hii ni nia njema ya Serikali inaharibiwa na watu wachache wasiotakia mema nchi yetu.
Naibu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Petro Malima akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na wahamiaji walowezi kujisajili ili kuweza kupatiwa vibali vya  kuishi nchini , leo jijini Dar es Salaam.

TANZANIA KINARA UTAWALA BORA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Orodha ya Hali ya Demokrasia Duniani (2017 Democracy Index) iliyozinduliwa Februari 2, mwaka huu na kuchapishwa na jarida kongwe na mashuhuri duniani la The Economist imeitaja Tanzania kuwa nchi ya kwanza katika maswala ya Utawala Bora kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi alisema kuwa Tanzania kuwa nchi ya kwanza kwenye masuala ya Utawala bora imeweza kusaidia ukuaji wa Uchumi wake.

“Utawala Bora ni kigezo muhimu cha ukuaji wa uchumi na hata ustawi wa jamii, kama ambavyo Orodha ya Hali ya Demokrasia Duniani iliyotolewa na jarida kongwe na mashuhuri duniani la The Economist imeitaja Tanzania ni ya kwanza katika ukanda wa EAC, ikifuatiwa na nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na DRC. 

Pia, ripoti ya Foresight Afrika na taarifa ya Uchumi ya Benki ya Dunia vyote vimeitaja Tanzania kuwa katika nchi tano Bora za Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi katika mwaka 2018, nchi hizo ni Ghana, Ethiopia, Kodivaa , Senegali na Tanzania”.

Aidha, Dkt. Abbasi alisema kuwa ukuaji huo wa uchumi ni dhamira isiyoyumba ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha uchumi mkuu unaendelea kujiakisi katika maisha ya watanzania kupitia utoaji wa huduma kwa wananchi na kuboresha sekta mbalimbali.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ahadi mbalimbali za Serikali mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi (kulia) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ahadi mbalimbali za Serikali mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo

UTUNZAJI FEDHA BADO NI CHANGAMOTO KWA WATANZANIA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Blogu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imesema bado ni changamoto kwa watanzania walio wengi katika kutunza fedha za noti na noti ya sh.500 na noti ya Sh.1000.

Hayo yamesemwa leo mkoani Mtwara na Meneja Msaidizi Idara ya Sarafu kutoka Benki Kuu Tanzania(BoT) Dolla Abdull wakati akitoa mada kwa waandishi wa habari waliokuwa kwenye semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika taarifa sahihi za uchumi.

Akifafanua kuhusu fedha chakavu, amesema noti ya Sh.500 ndio inayochakaa zaidi ukilinganisha na noti nyingine inayofuata kwa kuchakaa ni ya Sh.1000.Amesema sababu ya fedha hizo kuchakaa haraka inatokana na kutumika zaidi kwenye mzunguko wa fedha hasa kwa kuzingatia kundi kubwa la wananchi ndio watumiaji wakubwa.

"Hii noti ya Sh.500 na ya Sh.1000 zinatumika zaidi ukilinganisha na noti ya sh 10,000. Ni fedha ambazo zipo kwenye mzunguko zaidi." Pia utunzaji wa fedha bado changamoto kubwa katika jamii na ndio maana zinachakaa mapema.Ukifuatilia zaidi utabaini hizi noti za Sh.500 wengi ambao wanazitumia hawazitunzi vizuri na wala haziwapeleki benki,"amesema Dolla.

Amefafanua sababu nyingine ya fedha hizo kuchakaa haraka inatokana na ukweli uliopo watanzania ambao wwnatunza fedha zao benki hawazidi asilimia 14.Hivyo amesema sehemu kubwa ya fedha inabaki mtaani na matokeo yake zinachakaa. "Ujue fedha nayo ina umri wake wa kuishi ambapo kwa fedha za noti ni zinaishi kati ya miezi sita hadi saba.

" Kazi yetu idara ya sarafu ni kuhakikisha tunapeleka fedha safi katika mzunguko na zile ambazo zimechakaa tunazisaga katika mashine maalumu,"amesema Dolla.

Ametoa ombi kwa Watanzania kuhakikisha wanatunza fedha hizo kwani Serikali inatumia gharama kubwa kuchapa fedha hizo huku akifafanua fedha ni moja ya alama ya nchi yetu,hivyo lazima zitunzwe vizuri.Amesititiza wananchi kutunza fedha zao benki kwani ni njia moja wapo ya kuzifanya fedha kuwa safi huku akiwakumbusha wenye fedha zilizochaa kuzipeleka benki ili zibadilishwe.

WAZIRI JAFO AWATAKA WADAU WA ELIMU KUUNGA MKONO SERA YA ELIMU BILA MALIPO

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo amewataka Wadau wote wa Elimu pamoja na jamii kwa ujumla kushirikiana na serikali  kutekeleza sera ya elimu Bila Malipo. 

Jafo ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi vifaa vya shule katika shule ya msingi Uguzi, iliyopo wilayani Chamwino, mkoani Dodoma. 

Vifaa hivyo vilitolewa na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo Dkt. Ombeni Msuya na Abdala Jacob kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma.Amewataka wadau hao wasikate tamaa kuunga mkono Serikali kuhusu Elimu. “Japo changamoto ni nyingi lakini wanafunzi wenye uhitaji maalum wanahitaji msaada wao”. alisisitiza 

Amesema wanafunzi wengi wanakosa fursa ya vitendea kazi kama madaftari na kalamu hivyo ni jambo la  msingi kwa wadau wa elimu kuendelea kusaidia watoto hao na kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutekeleza sera ya Elimu Bila Malipo.

Waziri Jafo pia alizindua mpango maalum wa kusaidia wanafunzi wenye uhitaji maalum ambao ameupa jina la “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.Waziri Jafo amesema ujumbe huo unamhusu mtoto mwenye uhitaji wa kupata elimu na kuwaomba  Watanzania kwa ujumla kuunga mkono jambo hilo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa mpango maalum wa kusaidia wanafunzi wenye uhitaji maalum ambao ameupa jina la “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo akikabidhi madaftari kwa wanafunzi  na uzinduzi wa mpango wa “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo akikabidhi madaftari kwa wanafunzi  na uzinduzi wa mpango wa “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.

VIONGOZI KAGERA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO WAKATI WA UTAFITI KAYA BINAFSI

Viewing all 110016 articles
Browse latest View live




Latest Images