Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

MTULIA ASEMA SHIDA ZA WANANCHI KINONDONI NI ZAKE, ATAJA ATAKAYOANZA NAYO AKIWA MBUNGE

$
0
0


Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MGOMBEA ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Abdallah Mtulia ameendelea kuomba kura huku akiwaambi wananchi yeye hana tofauti na wao.

Pia shida za wananchi ni shida zake, matatizo yao ni matatizo yake pia na kuongeza yeye in mtoto wa kimaskini.tulia amesema hayo kwa nyakati tofauti kwenye mikutano yake ya kampeni kwenye uchaguzi huo wa jimbo hilo.Hata hivyo wakati Mtulia akiomba kura  kwa wananchi hao wa Kinondoni, mgombea ubunge wa Chadema Salum Mwalimu naye ameendelea kuomba kura.

Mwalimu amekuwa akitoa Sera mbalimbali zenye lengo kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo na kwamba anaamini yeye ndio mgombea sahihi ,hivyo wamchague alete maendeleo.Wakati wagombea hao kila mmoja akiomba kura  za wananchi hao ,kwa Mtulia yeye ameendelea kusisitiza changamoto za jimbo hilo anazijua na anao uwezo wa kuzitatua.

"Niliguswa na matatizo yenu ya kubomolewa nyumba nikaenda Mahakamani kuzuia bomoabomoa nikafanikiwa."Nilipambana kuhakikisha watu waliobomolewa wanapata hifadhi Magomeni. Nimekuja CCM kuhakikisha hilo linatimia," amesema Mtulia. Ameongeza kuwa "Niliacha ubunge, mshahara, posho na kiinua mgongo changu kwa sababu nawajali wana Kinondoni. Ukiwa jiongozi wa upinzani hauwezi kufanya lolote.

"Maendeleo hayapatikani kwa kutukana, kukashifu, matusi. Maendeleo huja kwa ushirikiano na mahusiano mema," amesema.Amefafanua zaidi  ni kweli anampenda Rais,Dk.John Magufuli  na kuuliza ataachaje Rais ambaye anajenga reli ya kisasa, kununua ndege za kisasa, ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme. Rais mkweli na muwazi.
MGOMBEA ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Abdallah Mtulia ameendelea kuomba kura huku akiwaambi wananchi yeye hana tofauti na wao.
Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni jana jioni katika viwanja vya Vegas,Makumbusho,Kinondoni jijini Dar. 
Baadhi ya Wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakiwa wamekusanyika kwenye kampeni katika viwanja vya Vegas,Makumbusho Kinondoni jijini Dar
Baashi ya Wananchi wakishangilia yaliyokuwa yakijiri kwenye kampeni hizo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SINE TAMER YATILIA MKAZO AGIZO LA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

Kampuni ya Sine Tamer imedhamiria kuhakikisha inatilia mkazo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli la kuwa katika uchumi wa kati wa  viwanda kwa mwaka 2025.

Hayo yamesemwa katika mkutano na wadau mbalimbali wa masuala ya nishati hususani katika viwanda, makampuni binafsi, mahospitali, mabenki na mashirika mbalimbali.

Mkurugenzi wa Sine Tamer nchini Tanzania Dotto Ibambasi amesema ndani ya miezi 7 tokea Juni 2017 wameweza kusambaza kifaa hicho kwa hospitali ya Muhimbili na wameweza kuonyesha mafanikio baada ya kuanza kukitumia ikiwemo kupungua kwa gharama za ufundi wa vifaa vilivyokuwa vinaharibika mara kwa mara.

"Kifaa hiki kimeweza kutumika katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili na wameonesha mafanikio makubwa sana baada ya kuanza kukitumia kifaa hicho kwani wameweza kupunguza gharama za ufanyaji wa ukarabati wa mara kwa mara,"amesema Ibambasi.
 Rais wa Sine Tamer Tim Chima (wa kwanza kulia) akiwa sambamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanfas Ndaki Munyeti pamoja na Mkurugenzi wa Sine Tamer Tanzania Dotto Ibambasi kwenye picha ya pamoja wakati wa hafla maalumu ya kukitambulisha kifaa maalumu cha kudhibiti umeme.
Akielezea kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda, Ibambasi amesema kuwa mikakati yao mikubwa ni kuhakikisha wanashirikiana na viwanda kwenye matumizi ya kifaa hicho kwa ajili ya kusaidia upunguzaji wa gharama za matumizi ya ukarabati wa mitambo kwani baadhi ya vifaa vingine hususani Balbu zinaungua kutokana na umeme kuja mchafu.

Ibambasi amesema kuwa mpaka sasa ni kampuni ya NMB imeweza pia kutumia kifaa hicho na wameweza kuona umuhimu wa kifaa hicho ambapo wamekiweka kwenye vituo vyao mbalimbali.

Kifaa hicho kimetambulishwa leo kwa wadau na wameaswa kukitumia ili kuweza kupunguza gharama za ukarabati wa mashine, mashine kuwa sawa pia kupunguza matatizo ya kuhangaika kupata vipuli vya mashine pindi vinapoharibika.
Mkurugenzi wa Sine Tamer nchini Tanzania Dotto Ibambasi akizungumzia kifaa hicho na kuelekezea namna kilivyoweza kusaidia kwenye kudhibiti uharibifu wa vifaa vya umeme pamoja na gharama za matengenezo.
Wadau mbalimbali waliojitokeza katika hafla hiyo.

PICHA ZA MATUKIO WAZIRI MKUU BUNGENI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Mkoa wa Geita Upendo Penezanje ya jengo la utawala la Bunge Mjini Dodoma, Februari 7, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, bungeni mjini Dodoma Februari 7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

TANZIA

$
0
0
Mfanyabiashara maarufu mkoani Kigoma, Carole P. Mtei amefariki tarehe 04/02/2018 katika hospitali ya Rabininsia, Tegeta jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa ykimsumbua. Mwili wa Marehemu Mtei unatarajiwa kuagwa leo Alhamisi 08/02/2018 katika Hospitali ya Lugalo na baadaye kusafirishwa kwenda kijijini kwao Marangu, Moshi kwa Mazishi yatakayofanyika siku ya Jumamosi 10/02/2018. habari ziwafikie Ndugu, Jamaa na Marafiki wote wa Familia ya Mtei popote pale walipo.

Neno: 

2 Timotheo 4: 7 
Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda.

Mungu ailaze mahala pema roho ya Marehemu - Amin

UTUMIAJI WA ISOTOPU ZA KINUKLIA KATIKA UTIBABU: VIPI INAWEZEKANA?

$
0
0
Kama kawaida maneno kama “kinuklia” au “mionzi” yanatisha ikiwa yanatumika katika nyanja za afya na maisha marefu. Hata hivyo, haiwezekani kufikiria utibabu za siku hizi bila ya teknolojia mpya inayotumia radioisotopu za kinuklia.
Duniani watu wanajua juu ya utumiaji wa mionzi na radioisotopu katika utibabu hasa kwa ajili ya utambuzi na utibabu ya magonjwa magumu mbali mbali. Katika nchi zilizoendelea, ambapo robo ya watu wote wa dunia wanaishi, mtu mmoja wa watu watano anatumia utibabu za utambuzi za kinuklia kila mwaka.
Lakini swali muhimu ni vipi dawa za kinuklia na radioisotopu (dawa zenye mionzi) zinafanya kazi na vipi zinaweza kuleta faida kwa Watanzania?
Kwanza, mionzi ni ufungaji wa nishati tu. Kama taa ya mwanga atomu za mionzi zinazalisha nishati inayotumika kwa ajili ya utibabu. Dawa za mionzi zinaingizwa katika mwili wa mgonjwa na sindano, kwa kumeza au kwa kuvuta pumzi.Ukubwa wa mionzi unaotumiwa ni mdogo sana. Mwilini radioisotopu zinatoa vyembe fupi (alpha au beta) ambavyo vinapoteza nishati yao yote katika umbali mfupi sana, kwa hivyo vinaathiri sana seli zilizoharibiwa. Kwa ujumla dawa za mionzi zinatumika kama matibabu: uharibifu wa seli za kansa, upungufu wa maumivu ya kansa ya mifupa na arthritis.
Kwa kutumia technolojia hizi za kinuklia wataalamu wa matibabu wanaweza kutambua na kutiba magonjwa mengi mbali mbali kwa njia salama na bila ya maumivu. Matibabu ya kinuklia yanawawezesha wataalamu kutambua kwa usahihi habarimbali mbali za afya ambazo hazipatikani kwa njia nyingine, zinahitaji upasaji au utumiaji wa kupima nyingine. Taratibu hizo zinatambua ukosefu ambapo ugonjwa unaendelea – mapema zaidi sana kabla ya testi za kawaida zinaweza kuutambua. Utambuzi mapema huo unawawezesha madaktari kuanza matibabu mapema zaidi, kwa hivyo tangazo zuri linawezekana.
Matibabu ya kinuklia inaweza kutambua magonjwa mengi mbali mbali. Yanatumika kwa kutambua mwilini vidonda visivyo vya kawaida bila ya upasuaji. Taratibu hizo pia zinapatia madaktari nafasi ya kutambua viungo vya mwili vikifanya kazi ipasavyo. Kwa mfano, matibabu ya kinuklia inaweza kutambua moyo ikipampu damu ipasavyo na bongo ikipata damu ya kutosha na kadhalika.
Utumiaji wa matibabu ya kinuklia si kitu kipya kabisa kwa Tanzania. Kwa kutumia teknolojia za kinuklia katika utibabu madaktari wenyeji wanafaulu zaidi katika utoaji wa utibabu mzuri kwa watu wenye magonjwa magumu kama kansa au magonjwa ya moyo na damu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TANZIA: MWANASIASA TAMBWE HIZZA AFARIKI DUNIA

$
0
0
Mwanasiasa maarufu nchini, Tambwe Hizza amefariki Dunia leo alfajiri nyumbani kwake Mbagala Kizuiani, jijini Dar es salaam.

Inaelezwa kuwa Marehemu Tambwe Hizza amefikwa na mauti hayo akiwa usingizini, kwani jana mpaka usiku alionekana kuwa mzima na hana dalili zozote za kuumwa.

Taarifa za msiba huu zimethibitishwa na Msemaji wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tumaini Makene.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu, Hizza huko Mbagala Kizuiani, Jijini Dar es salaam.

Mungu ailaze mahapa pema roho ya Marehemu Tambwe Hizza - Amen.

Tatu Mzuka yazidi kuwaneemesha Watanzania,wengi waendelea kujizolea mamilioni

$
0
0


Mwakilishi wa Kampuni ya inayochezesha mchezo wa kubahatisha,TatuMzuka,Kemilembe Mbeikya (katikati),akizungumza mbele ya Wanahabari mapema jana wakati wa kuwatambulisha washindi wa TatuMzuka,ambao kulia ni Abraham Kisiri kutoka Mkwajuni Kinondoni aliyejishindia million 60 pamoja na Ummy Abraham kutoka Wazo hill, Tegeta alijishindia million 5.



Kemi alisema kuwa Tatu Mzuka jackpot ya wiki iliyopita imetoa jumla million 80 kwa washindi wa nne,wakiwemo wawili pichani na wengine ni Mathew Mtoni kutoka Songea aliyejishindia milioni 10 pamoja na Selemani Mkoko kutoka Nachingwea aliejishindia millioni 5.

Tatu Mzuka hadi leo imetoa billion 14 na kutengenza washindi million 6. Hawa washindi ni thibisho tosha kuwa Tatu Mzuka inabadilisha maisha ya watu.Kama unavyojua, Tatu Mzuka inakupa nafasi ya kushinda kila lisaa hadi million 6, na sasa hivi kwenye msimu wa Valentine, wewe na mpendanao mnaweza kushinda million kumi kila silku na bado una nafasi ya kushinda million 60 jumapili hii.
Ummy Abraham amabae ni wa Wazo hill, Tegeta jijini Dar Es Salaama akieleza namna alivyojishindia kitita cha shilingi million 5.Amesema kwa sasa fedha hizo zitamsaidia kuendelea kumsadia katika Matibabu ya Mumewe ambaye ni mgonjwa na pia Fedha nyingine amepanga kumaliza ukarabati wa nyumba zake mbili ili ziendelee kumuingizia kipato.Aidha Ummy ameishukuru TatuMzuka kwa kuleta mchezo ambao kwake umekuwa kama mkombozi kwa wakati aliokuwa nao kwa sasa.
Abraham Kisiri kutoka Mkwajuni Kinondoni jijini Dar,ambaye ni Dereva wa taasisi ya UVCCM alijishindia milioni 60.Abraham ameishukuru Tatu Mzuka kwa kuuleta mchezo huo kwa Wananchi,kwani umekuwa na manufaa makubwa kwa baadhi yao kiasi hata ya kuyabadilisha maisha yao,anasema kwa sasa fedha hizo atazitumia kujiimarisha zaidi kiuchumi .
Mwakilishi wa Kampuni ya inayochezesha mchezo wa kubahatisha,TatuMzuka,Kemilembe Mbeikya (katikati),akiwa na Washindi wa washindi wa TatuMzuka,ambao kulia ni Abraham Kisiri kutoka Mkwajuni Kinondoni aliyejishindia million 60 pamoja na Ummy Abraham kutoka Wazo hill, Tegeta alijishindia million 5 wakiwa sambamba na mfano wa hundi zao.

Airtel yawazawadia washindi 2,000 wa promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti

$
0
0
Kampuni ya simu za mkokoni Airtel Tanzania leo imewazadia washindi 2,000 wa kwanza wa promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti kwenye droo ambayo imechezesha jijini Dar es Salaam.

Promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti ilizunduliwa mapema wiki hii ambapo kuna washindi 1,000 wakila siku ambao wanajishindia bando ya 1GB pamoja na zawadi nyingine zikiwepo wakishinda simu za kisasa za smatiphone na moden.Akiongea baada ya droo hiyo, Meneja Uhusiani Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema wateja wa Airtel 2000 wameweza kujishindia bando ya 1GB.

Kama mnvyoona hapa leo droo ya promosheni yetu ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti inafanyika kwa uwazi kabisa na washindi. Ni ya promosheni hii ni kutoa shukrani kwa wateja wa Airtel kwa kuonyesha uaminifu wao kwa kuendelea kutumia mtandao bora kabisa hapa nchini, alisema Mmbando.

Ni muhimu kufahamu kuwa mteja haitaji kujisajili kwa ajili ya promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti. Kile anachotakiwa kufanya ni kupiga *149*99# halafu changua namba 5 Yatosha SMATIKA Intaneti, hapo atanunua bando aidha ya siku, wiki au mwezi na kuwa mmoja wa washindi wa zawadi zetu kambambe, alisema Mmbando.

Mmbando aliongeza kuwa promosheni ya Shinda na Yatosha SMATIKA intaneti ilizinduliwa mwanzo mwa wiki na itakuwa ni ya siku 30 huku kukiwa na droo 3 kila wiki – Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Kwa droo za kila siku, wateja 1000 watajishindia bando ya intaneti yenye 1GB kila mmoja wakati kwenye droo kubwa kutakuwa na washindi 10 huku watano wakishinda simu za smatiphone na 5 wakijishindia moden.
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akionesha moja namba ya washindi wakati wakuchezesha droo ya SHINDA NA SMATIKA Intanetiambapo washindi 2000 kila mmoja alijishindia 1GB za SMATIKA Yatosha Intaneti. Kushoto ni ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Abdallah Hemedy na Afisa Masoko Airtel Nassoro Abubakar
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea na mmoja kati ya washidi wakati Airtel Ilipochezesha droo ya SHINDA NA SMATIKA Intanetiambapo washindi 2000 kila mmoja alijishindia 1GB. Kushoto ni ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Abdallah Hemedy na Afisa Masoko Airtel Nassoro Abubakar


HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA YABOMOA NYUMBA YA SERIKALI

$
0
0

Na Emanuel Madafa-Mbeya 

HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya, imetoa siku saba kwa mkandarasi anayejenga nyumba ya serikali iliyoamuliwa na mahakama kuu kujengwa, kuibomoa baada ya kubainika kujengwa chini ya kiwango.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake , Afisa habari wa halmashauri hiyo, John Kilua, amesema ofisi kupitia idara ya majengo ilitembelea eneo la nyumba hiyo inayojengwa kwa amri ya mahakama kuu na kubaini changamoto mbalimbali za ujenzi.

Amesema, kutokana na changamoto hizo wahusika wanaojenga nyumba hiyo wametakiwa kuibomoa na kuanza upya kwa kufuata kanuni za ujenzi na kwamba zoezi la kubomolewa kwa jengo hilo la nyumba linatakiwa kufanyika ndani ya siku saba.Nyumba hiyo yenye namba 1103/5 ambayo ipo katika eneo la Mafiat Jijini hapa, ilifunguliwa kesi namba 63 ya mwaka 2007 katika mahakama

Muonekano wa Nyumba yenye namba 1103/5 ambayo ipo katika eneo la Mafiat Jijini Mbeya , ilifunguliwa kesi namba 63 ya mwaka 2007 katika mahakama ya Wilaya Mbeya. 

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UJUMBE WA SHIMUTA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika  ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMUTA) mjini Dodoma.

Akizungumza baada ya kikao na Makamu wa Rais, Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Khamis Mkanachi alisema wamekutana na Makamu wa Rais na kumkabidhi ripoti ya mashindano ya mwaka 2016-2017 na 2017-2018.

Pamoja na kumkabidhi Ripoti hiyo, pia walimueleza Makamu wa Rais ambaye ni Mlezi wa Shirikisho, changamoto na mipango mbali mbali ya kuboresha shirikisho hilo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania kwenye makazi yake Kilimani mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Khamis Mkanachi ambaye aliongozana na Uongozi na Wajumbe wa Shirikisho kukutana na Makamu wa Rais kwenye makazi yake, Kilimani mjini Dodoma. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Shirikisho la Michezo la Mashirika ya umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania mara baada ya kumaliza mazungumzo kwenye makazi yake Kilimani, mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

YANGA KUIFUATA MAJIMAJI SONGEA 16 BORA YA KOMBE LA FA

$
0
0
 Raundi ya nne ya michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara (Azam Sports Federation Cup) imefanyika leo kwa timu 16 zimehusika katika droo hiyo.

Miongoni mwa timu hizo ni ile ya Buseresere FC ambao ni mabingwa wa mkoa wa Geita (Timu pekee ya ligi daraja la tatu) ambao wao wamepangwa kucheza na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Taifa Kahama uliopo mkoani Shinyanga.

Yanga ambao walikuwa mabingwa wa msimu wa 2015/16 wamepangwa kucheza Wanalizombe timu ya soka ya Majimaji katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Wakati huo huo Dodoma Fc inarejea tena mkoani Shinyanga na mara hii amepangwa kucheza na Stand United katika uwanja wa CCM Kambarage, ikumbukwe katika raundi ya tatu timu ya Dodoma FC inayoongozwa na Julio waliwatoa Mwadui FC.

Ratiba kamili. 
Stand United Vs Dodoma FC - CCM Kambarage, Shinyanga.

JKT Tanzania SC Vs Ndanda FC - Mbweni, Dar.

Kiluvya United Vs Tanzania Prisons - Filbert Bayi, Pwani.

KMC Vs Azam - Uhuru, Dar.

Majimaji Vs Young Africans SC - Majimaji, Ruvuma.

Singida United Vs Polisi Tanzania - Namfua, Singida.

Njombe Mji Vs Mbao FC - Sabasaba, Njombe.

Buseresere FC Vs Mtibwa Sugar - Taifa Kahama, Shinyanga.

Mechi hizo za hatua ya 16 bora zimepangwa kuchezwa Kati ya Februari 22 hadi 25 ambapo washindi watakwenda moja kwa moja katika hatua ya robo fainali na baadae nusu fainali.

Ikumbukwe mpaka sasa hakuna bingwa mtetezi kwani waliokuwa mabingwa Simba SC walitolewa mapema katika hatua ya pili ya mashindano hayo na timu ya Green Warriors ambao nao waliishia mikononi mwa Singida United. Bingwa wa michuano hiyo ataliwakilisha Taifa katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.

KESI YA WEMA SEPETU KUUNGURUMA FEBRUARI 26 MWAKA HUU

$
0
0
 Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Shahidi wa pili wa Upande wa Mashtaka katika kesi ya kutumia dawa za kulevya  inayomkabili msanii Wema Sepetu ameieleza  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa aliijaza fomu ya kupima sampuli ya mkojo wa Wema, kabla hajamfanyia vipimo.

Aidha Shahidi huyo, Inspekta Wille, alidai kuwa hajawahi kupeleka sampuli za mkojo  za washtakiwa Angelina Msigwa  na Matrida Seleman Abbas ambao ni wafanyakazi wa Wema kwenda kuchunguzwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kuhusu kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi.

Shahidi ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alipokuwa akihojiwa na Wakili wa upande wa utetezi, Albert Msando baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake.

Alipoulizwa muda gani alipeleka sampuli hiyo kwa Mkemia, alidai kuwa aliijaza fomu ya kupeleka sampuli ya mkojo wa Wema saa nne kamili asubuhi akiwa ofini kwao na kuandika maneno kuwa sampuli hiyo ya mkojo iko kwenye chupa ya plastiki lakini alikuwa bado hajampima mshtakiwa.

Alipoulizwa kama alijaza fomu hiyo kwa kuhisi tu, alidai, alijaza hivyo kwa kutumia uzoefu wake wa miaka 15 katika jeshi la polisi kwani alikuwa anajua taratibu za upimqaji ukifika katika ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali mkojo unakuwa katika chupa ya plastiki.

Aliendelea kudai kuwa Februari 8, mwaka jana alifika katika ofisi za Mkemia Mkuu wa Serikali  saa tano asubuhi na kumkabidhi Mchunguzi Elia Mulima kichupa cha plastiki ambacho ndani kilikuwa na mkojo.

Wakili Msando alimuuliza shahidi ulikuwapo wakati sampuli ya mkojo uliokuwamo ndani ya kichupa cha plastiki  unaodaiwa kuwa ni wa Wema ulipochukuliwa ambapo Inspekta Wille alidai kuwa hakuwapo.

Wakili Msando alimuuliza Inspekta Wille anaweza kusema kuwa unajua kwa uhakika kilichokuwa ndani ya chupa ya plastiki kuwa ni mkojo na je ni mkojo wa Wema? Alijibu kuwa hajui.

Msando alimuhoji Inspekta Wills kuwa walikaa kwa muda gani katika Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Inpekta Wille alidai kuwa hakumbuki.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

LIVE: MKUTANO WA KAMPENI ZA UBUNGE CCM JIMBO LA KINONDONI LEO

MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI JANUARI UMEBAKI KUWA ASILIMIA 4.0-NBS

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MFUMUKO  wa bei wa Taifa  wa Januari 2018 umebaki kuwa asilimia 4.0 kama ilivyokuwa mwezi Desemba 2017 kwa ujumla inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2018 imekuwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka. 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa  Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Epharaim Kwesigabo amesema  kubaki kwa mfumko huo kunatokana na bidhaa na huduma kuendelea bei ileilie ya mwezi Desemba.
Amesema baadhi ya bidhaa za vyakula vilivyochangia kupungua kwa mfumuko wa bei huo ni  Mahindi kwa asilimia 8.0, Maharage 4.3. Ndizi ya kupika asilimia 9.0, Samaki kwa asilimia 9.0 kwa upande mwingine baadhi ya bei za bidhaa zisizo za Chakula zilizochangia mfumuko wa bei ya mwezi Januari 2018 ni pamoja na sare za shule kwa asilimia 2.3, Huduma za afya kwenye Hospitali Binafsi  kwa asilimia 10.0, Mkaa asilimia 9.4, Vitabu vya shule kwa asilimia 2.7 na gharama za malazi asilimia 3.2.
Kwesigabo amesema mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unafanana na nchi nyingine Afrika Mashariki ambapo Kenya Mfumuko wa bei wa mwezi Januari 2018 umeongezeka hadi asilimia 4.83 kutoka asilimia 4.50 kwa mwaka ulioishia Desemba 2017, Uganda Mfumuko wa bei umepungua hadi kufikia asilimia 3.0 kutoka asilimia 3.3 kwa mwaka ulioishia wa mwezi Desemba 2017.
Aidha amesema Mfumuko wa bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.
Kwesigabo amesema NBS ni Taasisi ya Umma  iliyoanzishwa kwa sheria ya kufanya uratibu upatikanaji wa takwimu rasmi.
 Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa  Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Epharaim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari juu mfumuko wa bei wa Mwezi Januari 2018 leo jijini Dar es  Salaam.

WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO KAZINI

$
0
0
Wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Machinga,akisafisha vikombo katika Barabara ya Morogoro Shekilango jijini Dar es Salaam.

Kijana akipima chupa za plastiki anazozikusanya  mtaani na kuziuza jijini Dar es Salaamu,kilo moja huuza kati ya shilingi 300 hadi 400. 

Wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Machinga, wakitembeza bidhaa zao wakati wakisaka wateja katika foleni ya magari, Barabara ya Morogoro,eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam jana. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

DIAMOND NA HAMISA WAMALIZA TOFAUTI ZAO

$
0
0

Na Karama Kenyunko , Globu ya Jamii
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul “Diamond Platzum” mapema leo asubuhi amefika katika viunga vya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Ustawi wa Jamii kwenye mahakama ya watoto kwa ajili ya usuluhishi juu ya matunzo ya mtoto wake aliyezaa na mlimbwende Hamisa Mobeto.

Alianza kuingia Diamond akafuatiwa na Hamisa baada ya muda kidogo ambapo walikaa kwa zaidi ya saa moja.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza usuluhushi huo, Diamond alisema,

“Kiasi cha pesa tunavyoviandika kama kama hivi, tunazungumza tu, lakini watoto hawahitaji mahitaji mengi, wakati mwingine mtoto wako una uwezo wa kumpa hadi Shilingi milioni 100 na huwezi kusema simpi kwa sababu niliandikisha nitampa Laki Moja haimsaidii”.

Alisema wao kama wazazi wameweka mazingira mazuri ya kumlea mtoto wao kwa kadri ya uwezo wataokapata, kiasi kitakachomfanya akue katika malezi bora wakipata watakula nae wakikosa watalala.
Alipohojiwa baada ya kumalizika kwa usuluhishi, wakili wa Hamisa Mobeto,Walter Goodluck amesema, "leo tulikuja kwa usuluhishi na wamesuluhishwa Ila sasa wamesuluhishwa nini na nini hilo tutalijua badae", amesema

Msanii wa Bongo Fleva, Nasbu Abdul ‘Diamond Platinumz’ akifika katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaajili ya usuruhisho wa matunzo ya mtoto wao aliyezaa na Hamisa Mobeto.

Hamisa Mobeto akiwa
mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Msanii wa Bongo Fleva, Nasbu Abdul ‘Diamond Platinumz’ akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoka ustawi wa jimii kwa ajili ya kwaajili ya usuruhisho wa matunzo ya mtoto wao aliyezaa na Hamisa Mobeto leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAMBO YA SERIKALI MTANDAO: NDANI YA TCRA

RITA SASA KUTOA CHETI CHA KUZALIWA SIKU MOJA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA) imefanya maboresho ya Kanzidata na mfumo wa usajili wa vizazi na kifo kupitia mradi wa maboresho ya miundombinu ya  Tekknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).


Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa  Sifuni Mchome amesema kuwa lengo kuu la maboresho ni kuwezesha matukio ya vizazi na vifo kufanyika kwa ufanisi zaidi na kuwa karibu na wananchi katika  kuimarisha miundombinu ya usajili, krahisisha usafirishaji taarifa, uhifadhi wa taarifa pamoja na matumizi ya taarifa za ndani na nje ya Wakala.


“Maboresho ya mfumo wa usajili yamezingatia mahitaji ya mkakati wa kitaifa wa usajili wa matukio muhimu ya binadamu wenye lengo la  kuboresha usajili wa matukio muhimu” amesema.

Amesema maeneo yaliyolengwa katika mradi huo ni kama yafuatavyo ni kuboresha miundombinu ya kanzidata , kuweka vituo 60 vya majaribio na madawati manne ya usajili  wa RITA  katika Makao Makuu , Maboresho ya mfumo wa kielektronikI wa usajili ,maboresho ya mfumo wa utafutaji wa taarifa za zamani na kuweka mfumo maalum wa kutoa namba za kuzaliwa.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome akizungumza na Waandishi wa Habari Juu ya mfumo mpya wa usajili  wa Wakala wa Usajili, ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kutumia TEHAMA wakati alipofanya ziara katika wakala huo leo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili ,ufilisi na Udhamini (RITA), Emmy Hudson akitoa ufafanuzi juu ya mfumo wa usajili wa vizazi na vifo kupitia mradi wa maboresho ya Miundombinu wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome  alipofanya ziara katika wakala huo leo jijini Dar es Salaam.
Watendaji na Waandishi wa habari wakifatilia Mkutano  wa  Wakala wa Usajili, ufilisi na Udhamini (RITA) leo jijini Dar es Salaam.

Simba Sc, Gendarmerie Nationale Nani Mbabe.

$
0
0
Na Agness Francis Globu ya jamii 

VINARA  wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba Sc  wanaendelea kujifua vikali kukabiliana na mchezo wao  kimataifa dhidi ya Gendarmerie Nationale FC  ya nchini Djibouti katika kuwania Kombe la Shirikisho  la CAF.

Mtanange huo utakaorindima Februari 11 katika Dimba la Uwanja wa Taifa Jijini  Dar es  salaam Majira ya Saa 10:00 jioni . 
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam katika Makao Makuu ya Timu ya    SimbaSc' Mnyama'  Msemaji  Mkuu wa Timu ya  Simba, Hajji Manara  amesema kuwa katika mchezo huo atahudhuriwa na   Rais Mstaafu wa Awamu ya  Pili  Dk.  Ali Hassan Mwinyi akiwa kama Mgeni rasmi katika mchezo huo. 

"Timu yetu ipo vizuri na kikosi kipo kinaendelea na mazoezi na vijana wapo fiti kabisa ukizingatia wachezaji wetu tayari wawili Saidi Nduda pamoja na Salimu Mbonde wanaendelea vizuri na  wamesharejea kikosini kuendelea na  na Mazoezi"amesema Manara. 

Hata hivyo katika mtanange huo wataendelea kumkosa nyota wao  kutoka Rwanda  Haruna Niyonzima ambaye hivi karibuni ataelekea Nchini India kwa ajili ya matibabu . 

"Tutaendelea kumkosa Mchezaji wetu mahiri Haruna Niyonzima ambaye hivi karibuni ataelekea Nchini India kwa ajili ya matibabu ya maradhi yanayomsumbua, ila mpaka kufikia  mwezi ujao atarejea kikosini"amesema Manara. 
Aidha Manara amesema kuwa Timu ya Gendarmerie  Nationale FC watawasili Jumamosi saa 7:00 Usiku  ambapo  msafara wao utakuwa ni wa watu 18 na Viongozi  wakiwa ni 8.

Katika Mtanange huo Manara amewasaa  mashabiki kuhudhuria kwa wingi katika mchezo huo ambapo viingilio vitakuwa ni  Sh,30,000 kwa VIP A, Sh.20,000 kwa VIP B, Viti vya rangi ya Chungwa 'Orange'  Sh.10,000 na Sh.50,00 kwa vitu vya Mzunguko.

Serikali Yahamasisha Kilimo cha Mazao Makuu Matano ya Biashara.

$
0
0
 Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Serikali inaendelea na mpango wa kuhamasisha ulimaji wa mazao makuu matano ya Pamba, Korosho, Tumbaku, Kahawa na Chai nchini ili kuongeza uzalishaji wa mazao hayo.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameyasema hayo leo Bungeni Mjini Dodoma wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Sumve Mhe. Richard Ndassa juu ya namna Serikali ilivyojipanga na utafutaji wa masoko ya Pamba kutokana na mwitikio mkubwa wa kulima zao hilo mwaka huu.

"Miongoni mwa mikakati ya kuendeleza mazao hayo ni pamoja na kulima kisasa na kutafuta masoko ndani na nje ya nchi," alisema Waziri Mkuu.

Amesema, mwezi huu anatarajia kukutana na watumiaji wa zao la Pamba hapa nchini ili kuweka mfumo endelevu wa ununuzi wa zao hilo. Aidha, Wizara ya Kilimo inafanya kazi ya kutafuta masoko nje ya nchi.

Pia, Mhe. Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Liwale Mhe. Zuberi Kuchauka juu ugawaji wa pembejeo za korosho kwa mwaka huu amesema, Serikali ilitoa pembejeo ya Salfa bure mwaka jana kwa wakulima wa korosho ili kufanya hamasa kwa zao hilo baada ya wakulima kutelekeza zao hilo kutokana na kukosa pembejeo hiyo.

"Baada ya ugawaji wa pembejeo hiyo ya Salfa zao hilo limevunwa kwa kiwango cha juu kwa mwaka jana, hivyo kutokana na fedha walizozipata wakulima wa zao hilo watatatikiwa kuchangia gharama za Salfa kwa mwaka huu," alisema Mhe. Majaliwa.

Wakati huo huo, Mhe. Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Urambo Mhe. Margaret Sitta juu ya migogoro ya mipaka ya mapori na misitu, amesema Serikali imeiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikisha wanavijiji na viongozi wa kijiji wakati wa uwekaji wa mipaka hiyo.

Hata hivyo amesema ikiwa kijiji kitaonekana kiko ndani ya mipaka ya msitu au pori, tathimini itafanyike na baadae watapewa elimu ya kutoingia ndani ya mipaka ya misitu na mapori ya Serikali Kuu.

Misitu yote ya Serikali Kuu inahifadhiwa kisheria na mipaka hiyo inaonekana ili kuondoa migogoro na wananchi.
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images