Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

YANGU MACHO JIMBO LA KINONDONI MAANA HUKU MTULIA...KULE MWALIMU

$
0
0

Na Said Mwishehe

KWA heshima na taadhima, naomba nitumie nafasi hii kuwasalimia wananchi wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Natoa salamu zangu kwenu nikitambua kuwa pamoja na shughuli nyingine za ujenzi wa nchi yetu , pia mpo kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.Sababu za kufanyika za uchaguzi huo unatokana na uamuzi wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) Maulid Mtulia kuamua kujiuzulu ubunge.Baada ya kujiuzulu akaondoka CUF na kujiunga CCM.

Sioni umuhimu wa kurudia sababu ambazo amezitoa Mtulia wakati anatangaza kujiondoa CUF.Hata hivyo moja ya sababu amedai alipokuwa CUF alijikuta akiwa kwenye wakati mgumu kutokana na mpasuko uliopo.Tunafahamu ndani ya CUF hakuko sawa kutokana na tofauti ya misimamo na mitazamo baina ya vingozi wa juu wa chama hicho.Hivyo Mtulia akaona bora ajiweke kando.Ndio sababu ambayo ameitoa.

Pia akasema juhudi za Rais ,Dk.John Magufuli za kuleta maendeleo zimemfanya aone haja ya kuunga mkono kwa kujiunga na CCM.Najua kila mtu anayo nafasi ya kuchambua na kupima anachosema Mtulia.Kwa sasa Mtulia anagombea tena ubunge wa Kinondoni kwa tiketi yaCCM.Kampeni zinaendelea Kinondoni na Mtulia ni miongoni mwa wanaomba kura kwa wananchi.
Katika uchaguzi huo ushindani upo kati ya Mtulia na mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema Salimu Mwalimu.Ni ushindani haswa na kila chama kilipozindua kampeni rasmi walitoa tambo nyingi.Tunasubiri mwisho wa tambo hizo utakuaje.

Kila mmoja anaamini ataibuka na ushindi.Chadema wanaamini Kinondoni ni ya Salumu Mwalimu na hivyo hivyo CCM nao wanaamini Kinondoni ni ya Mtulia.Sawa yupo mgombea wa TLP ,Dk.Godfrey Malisa ambaye naye anawania jimbo hilo.Najua wapiga kura ndio wenye kuamua nani awe mbunge wao baada ya kila mmoja kupita na kutoa sera za chama chake kuhusu nini watafanya kwenye jimbo hilo.

KUSOMA ZAIDI MAKALA HII BOFYA HAPA


KIPINDI MAALUM CHA MAENDELEO YA UJENZI WA RELI NCHINI

Bamiza Music Chart 3rd February, 2018

NEC YARIDHIA KUHAMISHWA KWA VITUO 46 VYA KUPIGIA KURA KINONDONI

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeridhia kuhamishwa kwa vituo 46 vya kupigia Kura katika kata tatu za jimbo la Kinondoni zitakazofanya Uchaguzi mdogo wa Ubunge Februari 17 mwaka huu.

 Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Ramadhani Kailima ameeleza kuwa uamuzi wa NEC kuridhia kuhamishwa kwa vituo hivyo, umetokana na makubaliano yaliyofikiwa katika Mkutano wa Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Kinondoni na Vyama vya siasa juu ya kuhamishwa kwa vituo hivyo vilivyokuwa kwenye nyumba za Ibada, Zahanati na maeneo ya majengo ya watu binafsi.
 Amesema Tume imeridhika na uamuzi huo kwasababu hatua zilizochukuliwa ni sahihi kwa mujibu sheria na kanuni namba 21 ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambayo inaeleza kuwa ; Vituo vya Kupigia Kura havitakiwi kuwekwa katika majengo ya nyumba za Ibada, kambi za jeshi, nyumba za watu binafsi na ofisi za vyama vya siasa.
“ Tumejiridhisha kuwa baadhi ya vituo vya Kupigia Kura katika Kata ya Kigogo vilikuwa katika Zahanati na nyumba za Ibada na vingine kuwa katika maeneo yenye ufinyu wa nafasi hivyo tumeridhia vituo hivyo vihamishwe na kupelekwa katika majengo ya umma”. alisema Kailima. Amesema kuwa baadhi ya vituo vya kupigia Kura vilivyokuwa katika majengo ya umma ikiwemo Zahanati vimehamishwa katika shule za msingi za umma zilizo katika kata hizo ili kuondoa usumbufu kwa wagonjwa. 
 Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Mwananyamala Bi. Barima Omari ameeleza kuwa Kata ya Mwananyamala ina vituo vya kupigia kura 65 na wapiga kura 27,589 na kuongeza kuwa vituo nane (8) vilivyokuwa katika shule ya Sekondari Kambangwa mtaa wa msisiri A vimehamishwa. Kati ya hivyo 6 vimehamishiwa katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa ya Msolomi na 2 kuhamishiwa uwanja wa kwakopa. 
 Naye Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Kijitonyama Elizabeth Minga ameeleza kuwa Kata ya Kijitonyama ina jumla ya vituo vya kupigia Kura 101, kati ya hivyo vituo 22 vimehamishwa.
 Akifafanua kuhusu vituo hivyo amesema vituo 6 vilivyokuwa katika shule ya Sekondari Kenton vimehamia shule ya Msingi Mapambano na vituo 5 vilivyokuwa nje ya Ofisi ya serikali ya Mtaa wa Bwawani vimehamishiwa mbele ya ofisi hiyo. 
 Aidha, vituo 6 vilivyokuwa nje ya soko la Makumbusho vimehamia ndani ya Ofisi ya Meneja wa Soko hilo na vituo 5 vilivyokuwa katika Ofisi ya Serikali za mitaa kijitonyama vimehamishiwa katika shule ya msingi kijitonyama. 

 Kwa upande wake Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Kigogo Bw. Singoro Mdegela ameeleza kuwa Kata yake ina idadi ya Wapiga kura 27,000 na Vituo vya Kupigia Kura 59. Amesema katika Kata hiyo vituo 16 vimehamishwa ambapo vituo 5 vilivyokuwa eneo la Kiwenge kwenye Msikiti wa Shiha vimehamia Uwanja wa People na Vituo 6 vilivyokuwa kwenye Zahanati ya Kigogo vimehamishiwa katika Shule ya Msingi Kigogo ili kuruhusu shughuli za matibabu kwa wagonjwa kuendelea.
 Aidha, vituo 5 katika ofisi ya serikali ya mtaa wa Mkwajuni vimehamishiwa katika shule ya secondari Kigogo.

Ratiba rasmi ya mazishi ya Mzee Kingunge Ngombale Mwiru (Baba Kinje)

$
0
0
Jumapili tarehe 4/2/2018
- Saa 10:00 jioni mwili kutoka Hospitali kuelekea nyumbani Victoria/Makumbusho Kingunge street, Dar es salaam. 
-Saa 11:00 Jioni mwili kuwasili nyumbani na taratibu za ibada mila na desturi kuendelea usiku mzima(mkesha)
******************************
Jumatatu tarehe 5/2/2018
- Saa 1:00 Asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani Kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.
- Saa 2:00 Asubuhi mpaka saa 3:30 asubuhi Kupata kifungua kinywa/Chai Kwa waombolezaji wote
- Saa  4:00  Asubuhi mpaka saa 5:00 misa nyumbani Kwa marehemu
- Saa 6:00 Mchana mwili kuwasili Karimjee hall kwa shughuli ya kuagwa
- Saa 6:00 Mchana  9:00 Alasiri kuaga mwili wa marehemu
- Saa 9:00 Alasiri mpaka 9:30 Alasiri msafara wa kuelekea makaburini Kinondoni
- Saa 9:30  Alasiri mpaka 11:30 Jioni maziko
- Saa 11:30 Jioni 12:30 Jioni kuelekea nyumbani kwa marehemu kwa chakula cha jioni kwa waombolezaji wote
1:30 mpaka  2:45  Usiku chakula cha usiku waombolezaji wote
3:00 Usiku-Hitimisho la shughuli ya Mzee wetu kwa waombolezaji wote.

Tunawashukuru sana waombolezaji wote kwa ushiriki wenu wa Hali na mali katika wakati huu mgumu. Mungu awazidishie.
Bwana ametoa, na bwana ametwaa.
Jina lake na lihimidiwe - AMINA

Imetolewa na:
Omary A. Kimbau
Mwenyekiti wa kamati ya mazishi

MAGAZETI YA JUMAPILI LEO FEBRUARY 4,2018

RC Wangabo awaibaini wakwepa kodi, atoa siku 7 wajirekebishe kabla ya Msako.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim wangabo amesikitishwa na kitendo cha wafanyabiashara kutumia mbinu mbalimbali za kukwepa kulipa kodi serikalini jambo linalorudisha nyuma maendeleo, hivyo kutoa siku saba za kujirekebisha kabla ya Mamlaka ya mapato kuanza msako mkali na kuwatia nguvuni. 

Amesema kuwa katika kipindi cha mitatu kuanzia Oktoba hadi Disemba, 2017 Mamlaka ya Mapato Rukwa imekusanya shilingi bilioni 2.2 kiasi ambacho hakiendani na uhalisia na kuongeza kuwa Mamlaka hiyo inaweza kufanya vizuri zaidi endapo itapambana na vipingamizi vilivyopo.

“Kuna vipingamizi kadhaa moja ni wafanyabiashara kutokuwa na EFD, pili, baadhi ya wafanyabiashara kutotoa risiti, kuna wenye EFD mbili, iliyosajiliwa na isiyosajiliwa, na wao hutumia isiyosajiliwa na wengine kuwa na vitabu viwili vya stakabadhi na kutumia kile chenye mapato madogo kupiga mahesabu ya serikali, yote hii ni mianya ya kukwepa kodi ya serikali,na wengine kuuza kwenye magari bila ya risiti,” Alisisitiza.

Pia amebainisha kuwa kuna wafanyabiashara 316 ambao wamelipia mashine za EFD lakini hadi leo hawajapewa mashine hizo na kusababisha kuvuja kwa mapato ya serikali, ameyasema hayo katika mkutano wa Baraza la Biashara la Mkoa. Katika kubainisha changamoto za wafanyabiashara mkoani humo Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ,Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Rukwa Sadrick Malila amesema kuwa wafanayabiashara mkoani humo wamekuwa na wakati mgumu kutokana na utitiri wa kodi na kutokuwa na mahusiano mazuri na Mamlaka ya mapato Tanzania na kushauri kurudishwa kwa Jukwaa la walipa Kodi kwani lilikuwa na manufaa.

“Tulikuwa na jukwaa la walipa kodi, amabapo tulikuwa tunakaa na kujadili, lakini hili jukwaa limefutwa na kutoka pale imekuwa ubabe na wakati ule TRA walikuwa wanavuka malengo kuliko hali ilivyo hivi sasa,ambapo hawavuki malengo”Alisema .Tuhuma hizo zilikanushwa na Meneja wa Mamlaka ya Mapato TRA Mkoani Rukwa Fredrick Nyariri nae kutoa takwimu zilizobainisha kuvuka kwa malengo kulingana na viwango walivyopangiwa.

“Si kweli kwamba hatuvuki malengo kwa mfano mwezi Novembea tulipangiwa Shilingi Milioni 801 tukapata Milioni 928 na Mwezi Disemba tulipangiwa kukusanya Shilingi Milioni 908 na tukapata Milioni 996, nasikitika kusema kwamba taarifa ya mwenyekiti TCCIA imejaa upotoshaji,” Alimalizia. Na kuongeza kuwa Mamlaka ya Mapato imejipanga kuuza mashine za EFD na kuepukana na kuwa na wakala mmoja wa kusambaza mashine hizo ndani ya Mkoa wa Rukwa. 
 Mkuu wa MKoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo katika Baraza la Biashara la Mkoa akiwa na katibu Tawala wa Mkoa Benard Makali (wa kwanza kushoto) pamoja na Wenyeviti wa Halmashauri za Kalambo na Nkasi (Kulia)

KATIBU MKUU UVUVI ATEKETEZA NYAVU HARAMU ZA BILIONI 2.6 MWANZA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha akishiriki kwenye zoezi la kuteketeza nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara zikiteketezwa kwa moto kulia mwenye suti ni Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba akishuhudia,Picha na John Mapepele.

Na John Mapepele, Mwanza. 

Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba ametaifisha na kuteketeza zaidi ya tani mia mbili za shehena ya nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara .

Mbali na kuteketeza zana hizo haramu, Serikali pia imekusanya zaidi ya shilingi bilioni tano kama sehemu ya adhabu kwa wavuvi na wafanyabiashara waliokutwa na zana haramu pamoja na makosa ya utoroshaji mwani, samaki na mazao yake nje ya nchi.
 
Shehena ya nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara zikiteketezwa kwa moto,Picha na John Mapepele.

Akizungumza na mamia ya wavuvi wakati wa kuteketeza nyavu hizo leo, katika dampo la Buhongwa nje kidogo ya jiji la Mwanza, Dkt. Budeba amesema hatua hizo kali zinazochukuliwa na Serikali dhidi ya uvuvi haramu hazilengi kuwaonea wafanyabiashara au wavuvi wanyonge bali zimelenga kuwatengenezea maisha bora ya kizazi cha sasa na baadae ili kiweze kunufaika na rasilimali zilizoko ziwani. Aidha Dkt. Budeba amesisitiza kuwa kikosi hicho kitaendelea na operesheni hiyo bila kuchoka hadi hapo uvuvi haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi utakapokwisha ndani ya ziwa hilo.

Pia aliwaonya wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara wanaotengeneza na kuuza nyavu hizo ambapo amesema Serikali ikiwabaini itawachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafutia leseni zote za biashara zao. Alisema rasilimali zilizopo ndani ya ziwa hili ni mali ya wananchi viongozi wamepewa dhamana ya kuongoza kazi ya ulinzi tu na endapo uvuvi haramu utakomeshwa wananchi ndiyo watakaonufaika.
 
Shehena ya nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara zikiteketezwa kwa moto,Picha na John Mapepele.

Pamoja na kuteketeza nyavu hizo haramu, Dkt Budeba alieleza hali ya upatikanaji wa samaki aina ya sangara katika Ziwa Victoria ambapo alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) mwaka 2017 unaonesha kuwa samaki waliochini ya sentimita 50 ni asilimia 96.6 hivyo samaki hawa ni wachanga na hawarusiwi kuvuliwa ambapo samaki walio zaidi ya sentimita 85 ni asilimia 0.4 tu ambao ni wazazi na hawarusiwi kuvuliwa pia. Samaki wa sentimita 50 mpaka 85 ambao ndio wanafaa kuvuliwa ni asilimia 3 tu.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Fatma Sobo amesema Idara itaendelea kutumia Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 pamoja na Sheria nyingine za Mazingira ili kudhibiti Uvuvi haramu nchini. 
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba aliyevaa suti akishirikiana na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana,Mary Tesha zoezi la kuteketeza nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara ,Picha na John Mapepele 

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha alisema Serikali ya Wilaya hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za kupambana na uvuvi haramu na kuwachukulia hatua stahiki kuwataka wananchi kuendelea kuwafichua wavuvi haramu ili kulinda rasimali hiyo muhimu waliyopewa na Mungu.

Kwa upande wao baadhi ya wavuvi walimuomba Dkt. Budeba kuwasiliana na Wizara ya Viwanda na Biashara, ili kuona namna ya kudhibiti nyavu zisizoruhusiwa ambazo zinatengenezwa viwandani na baadae kuuziwa wavuvi.

Hivi karibuni watendaji wakuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na kikosi kazi kilichoundwa na Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi wameweza kukamata nyavu haramu, meli za uvuvi kutoka nje ya nchi zinazovua bia kufuata taratibu na mazao ya uvuvi yanayotoroshwa nje ya nchi ikiwemo mwani na samaki yenye mabilioni ya fedha huku Waziri Mwenye dhamana ya sekta hiyo Luhaga Mpina kuahidi kuwa operesheni hizo zitakuwa za kudumu hadi uuvi haramu utakapokoma.

VIJANA WA MOROGORO WANUFAIKA NA AJIRA UJENZI RELI MWENDO KASI ‘SGR’

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( wa kwanza kulia) asikiliza maelezo ya mtaalamu wa Kampuni ya Uhandisi ya MotaEngil Afrika - Tanzania ya ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) eneo la Ngerengere kutoka kwa Mpima ardhi wa Kampuni hiyo , Juma Sospeter , wakati wa ziara yake na wajumbe wa kamati ya ulinzi na salama ya mkoa na wilaya ya Morogoro alipotembelea eneo la ujenzi wa kambi ya kampuni hiyo na njia ya reli ya kisasa ya “SGR “ katika kata ya Ngerengere , wilayani humo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( wa pili kulia) asikiliza maelezo ya mtaalamu wa Kampuni ya Uhandisi ya MotaEngil Afrika - Tanzania ya ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) ambaye ni Mpima ardhi , Juma Sospeter , wakati wa ziara yake na wajumbe wa kamati ya ulinzi na salama ya mkoa na wilaya ya Morogoro alipotembelea eneo la ujenzi wa kambi ya kampuni hiyo na njia ya reli ya kisasa ya “SGR “ eneo la kata ya Ngerengere , na ( kutoka kushoto) ni mkuu wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo akizungumza jambo na Mhandisi mwendeshaji wa kampuni hiyo , Filipe Ataide. ( Picha na John Nditi).
Baadhi ya wataalamu wa Kitanzania wa Kampuni ya Uhandisi ya MotaEngil Afrika - Tanzania ya ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) wakiendelea na kazi zao za hatua ya awali ya ujenzi huo eneo la Ngerengere wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe na wajumbe wa kamati ya ulinzi na salama ya mkoa na wilaya ya Morogoro walipotembelea eneo la ujenzi wa kambi ya kampuni hiyo na njia ya reli ya kisasa , “SGR “ katika kata ya Ngerengere , wilayani humo.

Na John Nditi, Morogoro

MKUU wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ameitaka Kampuni ya Uhandisi ya MotaEngil Afrika  - Tanzania  ya ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) kuhakikisha inawatumia wafanyakazi wa kitanzania waliopo katika  maeneo ya ujenzi wa mradi kwenye  ajira zisizo hitaji utaalamu zaidi. Dk Kebwe  alisema hayo alipokuwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa  na wilaya ya Morogoro  wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa kambi  ya kampuni hiyo  na njia ya reli ya kisasa  inayotarajiwa  kujengwa ,kata ya Ngerengere , wilayani humo.

Mkuu huyo wa mkoa alisema , suala la ajira katika miradi kama hiyo mara nyingi limeleta  tatizo kubwa , lakini  kutokana na maelezo ya uongozi wa Kampuni pamoja na wa Serikali za kijiji na Kata ya Ngerengere kuwa upo utaratibu mzuri wa kushirikisha viongozi hao kuwapata wafanyakazi kwenye kazi zisizo na utaalamu.

 “ Hatuja pata matatizo na   wanaendelea vyema na kukamilishaji wa ujenzi wa kambi na kuanza njia ya reli ya SGR “ alisema Dk Kebwe .

Pamoja na hayo aliitaka Kampuni hiyo kuweka kipaumbele cha ajira  kwa  wakazi wa maeneo ya mradi na si  kuchukua  watu wa mbali ,  na kwamba kutokana na utaratibu uliowekwa kwa kushirikisha viongozi wa serikali za vijiji na kata utaondoa  malalamiko na hiyo  ni miongoni mwa sera ya kampuni. Mkuu huyo wa mkoa , aliitaka kampuni hiyo kutekeleza majukumu yake ya ujenzi wa reli ya kisasa kama mkataba ulivyo  na kwa kuzingatia kauli ya Rais  Dk John Magufuli wakati wa uzinduzi  wa ujenzi wa mradi huo ya kuwapata kukamil;ishaji uwe ndani ya miezi 24.

Pia  aliwataka  viongozi wa vijiji  na kata vilivyopo jirani na eneo  hilo   kushirikiana na wananchi ili kuhakikisha mradi huo unalindwa kwa lengo la kumwezesha mkandarasi kumaliza kwa wakati.

“ Wale wezi wa mafuta , vipiri na vitu vingine vya mradi huu washughulikiwe kikamilifu wanaponainika “ aliangiza Dk Kebwe kwa viongozi wa Serikali za vijiji vya kata ya Ngerengere.

Kwa upande wao ,Mpima ardhi  wa Kampuni hiyo , Juma Sospeter  pamoja na msimamizi wa maeneo ya ujenzi wa kambi hiyo Erick Mtasiwa ka nyakati tofauti wakitoa maelezo  kwa niaba ya kampuni, walisema zaidi ya vijana 50 kutoka vijiji vya tarafa ya Ngerengere, wamenufaika na ajira za mkataba za  kufanya kazi mbaimbali. Walisema ,  kampuni imezingatia maelekezo na miongozo inayotolewa na serikali kuyataka makampuni yanayo fanyashughuli mbalimbali ikiwemo ujenzi kuhakikisha inawatumia wafanyakazi wa kitanzania hususani katika ajira zisizo hitaji utaalam zaidi.

Awali, Mhandisi mwendeshaji wa kampuni ya MotaEngil  Afrika - Tanzania  ,  Filipe Ataide alisema  mpaka sasa hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza na wamepenga  kukamilisha mradi huo kuzingatia makubaliano yaliyomo ndani ya mkataba na kwa ushauri wa Rais. Ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) kwa  awamu  kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro  inatarajiwa kukamilika Oktoba 2019, ikiwa na urefu wa kilometa 300 na steshani sita  na inajengwa na Kampuni ya Uhansisi ya Mota-Engil  Afrika – Tanzania.

MICHUZI TV LIVE: FUATILIA HAPA IBADA YA KUMUWEKA WAKFU REV. CAN. JACKSON SOSTHENES JACKSON KUWA ASKOFU WA TANO WA DAYOSISI YA DAR ES SALAAM

KUTOKA KUUZA MAJI HADI KUWAVALISHA YANGA,DIAMOND PLATINUMZ NA BAKHARESA

$
0
0
Jeffrey Jessey anaishi ndoto ambayo kila kijana wakitanzania angependa kuishi hivyo. Akiwa na ari ya kuja kuwa na mafanikio Jeffrey alianza shule hadi kufika Chuo kikuu cha Dar es salam ambako alisoma masomo ya biashara huku akisaidia wanafunzi wenzake kupunguza nguo kubwa na kuzifanya kuwa “modo“.

Jeffrey ambaye maisha yake ya nyuma yalikuwa na changamoto nyingi ambazo zilipelekea kuuza maji ili kuifanya familia ijikimu. Kwa uhakika mafanikio yake ya leo yanachangiwa sana na makuzi yake yaliyomtayarisha kupambana na kufanikiwa.

Baada ya kumaliza shahada yake ya chuo kikuu, Jeffey hakutaka kuajiriwa bali kujiajiri kama mshonaji wa nguo kupitia chapa yake ya Speshoz. Hadi sasa ameajiri watu wengi na kufanikiwa kutengeneza jezi za Yanga, kuwavesha Diamond Platnumz, Mfanya biashara maarufu Bakhresa, Wabunge , Mawaziri na Maharusi wengi.


Simulizi ya Jeffrey imo kwenye kipindi maalum cha kukuza Ujasiriamali chenye kulenga zaidi vijana kiitwacho Extra Mile Show ambacho kimezinduliwa leo jijini Dar es salaam.Wakieleza mkakati wao Extra Mile Show walisema vipindi hivi vinavyopatikana kwenye mitandao na youtube, facebook, instagram na twitter kinalenga kuwawezesha vijana kutambua fursa na kubadilishana uzoefu.

Wote waliolima,kuchoma mkaa msitu malangali wakamatwe mara moja-RC Wangabo

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameagiza kuwasaka na kuwakamata wananchi wote waliokiuka amri ya mahakama ya kutoutumia msitu wa hifadhi ya Malangali kwaajili ya matumizi ya kibinadamu.

Amesema kuwa pamoja na kukamtwa, wananchi hao wasimamiwe kuhakikisha kuwa wanapanda miti maeneo ambayo wameyaharibu na kusisitiza kusakwa kwa wale wote waaofanya shughuli za kibinadamu kando ya vyanzo vya maji huku akitaja bonde la mto lwiche.

“Mpite shamba kwa shamba, kamateni watu wote ambao wamevamia kule, ule msitu uache kama ulivyo, vyanzo vyetu vya maji vitakauka, Mkurugenzi fanya msako wa bonde lote hilo kwa wale wote ambao wameanza kufyeka na kulima, kamata. DC simamia hili, tunataka kukomesha uharibifu wa mazingira wa aina yoyote ile,” Alisisitiza.

Ametoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara alioufanya baada ya kutembelea msitu huo wa malangali uliopo kata ya Malangali, Wlayani Sumbawanga na kujione namna wananchi hao walivyoharibu msitu huo uliojaa miti ya miombo ambayo inakatwa na kugeuzwa mkaa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa agizo la kukamatwa kwa waliokiuka amri ya mahakama na kufanya shughuli za kibinadamu kwenye msitu wa Malangali Mjini Sumbawanga
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa agizo la kukamatwa kwa waliokiuka amri ya mahakama na kufanya shughuli za kibinadamu kwenye msitu wa Malangali Mjini Sumbawanga katika Mkutano wa hadhara.


Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu akiwasilisha taarifa ya msitu wa Malangali uliopo Sumbawanga Mjini Kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo.

MNEC SALIM ASAS KULA SAHANI MOJA NA WATENDAJI WATAKAOKWAMISHA JUHUDI ZA RAIS

$
0
0

MJUMBE wa Halmashauri kuu CCM Taifa (NEC )Salim Abri amesema kuwa CCM Mkoa wa Iringa itamshughulikia mtendaji yeyote wa Serikali atakayeonyesha dalili ya kukwamisha juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.

Kauli hiyo aliitoa mwishoni mwa mwiki alipokuwa akiongea na wananchma wa CCM Manispaa ya Iringa katika maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa CCM ,alisema Mtu yeyote ndani ya serikali ya mkoa wa Iringa atakayeonyesha dalili za kuhujumu au kwa makusudi, serikali ya chama cha mapinduzi haita muacha na lazima itamshughulikia.

“Nasema hatuta kubali kuona mtu yeyote atakaye onyesha kukwamisha juhudi wakati rais na mwenyekiti wetu wa Taifa tutapambana nae,Rais amejitoa kwa wananchi wake alafu mtu atokee tu na kuvuruga utaratibu lazima haiwezekani na tutapambana nae”alisema MNEC

Alisema Wakuu wa Wilaya wanapaswa kuwaambia viongozi wao wa serikali kuwa kofia na nguo za kijani ndiyo wanaosimama kwenye majukwaa kuwatete wao,hivyo si haki CCM tubebe lawama kwa ajili ya hao watendaji wazembe wenye nia ovu kwa serikali ya kukwamisha maendeleo ili wengine wapande jukwaani wakitukane chama Tawala.

hivyo aliwataka viongozi wa chama hicho kujua majukumu yao ya kuhakikisha CCM inasimammia Serikali na si wengine wanasimama kutetea uozo wa watendaji hao ambao nia yako ni mbaya lakini kama watendaji wangejua thamani ya CCM basi ingekuwa vigumu kuwepo mtendaji wa serikali ambae ni mpinzani.

Abri ( ASAS ) aliongeza kuwa Ilani inataka yaale mambo yaliyaidiwa kwa wananchi yanatekelezwa kwakuwa wakati wa kuomba kura ni wanaCCM ndiyo waliosimama kuomba kura na si taasisi za serikali au Mkurugenzi wa Halmashauri,hivyo hatuna budi kuhakikisha Ciongozi wa CCM wanafuatilia utekelezaji wa Ilani kwani hata pale yasipotekelezwa wananchi halaumu chama tawala na si watendaji wa serikali.

WAZIRI JENISTA MHAGAMA : WCF KUFUNGUA OFISI KWA AWAMU MIKOANI KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA ZAKE

$
0
0
KUANZISHWA kwa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni hatua muafaka katika mazingira ya sasa ambapo kuna ongezeko la maeneo ya uzalishaji hususan viwanda kunakokwenda sambamba na ongezeko la matukio ya athari zinazotokana na ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amewaambia wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa warsha ya kujenga uelewa kwa wabunge kuhusu majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), mjini Dodoma Februari 3, 2018.

Mhe. Mhagama alisema warsha hiyo ni utekelezaji wa ombi lililotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kutaka wabunge wajengewe uelewa wa shughuli za Mfuko huo. Akifafanua zaidi Mhe. Waziri alisema Mfuko uliundwa Julai 2015 chini ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, sura 263 marejeo ya mwaka 2015 ili kulipa Fidia stahiki kwa mfanyakazi aliyeumia, kupata maradhi au kifo wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kwa mujibu wa mkataba. 

Alisema, Serikali ilianzisha Mfuko huo kwa lengo la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata Mafao bora ya Fidia tofauti na Sheria ya zamani ya Fidia kwa Wafanyakazi ambayo viwango vyake vya Mafao ya Fidia vilikuwa vya chini mno. “Mathalan viwango vya juu vya Fidia kwa Mfanyakazi aliyepata ajali kazini ilikuwa ni shilingi 108,000/= huku Mfanyakazi aliyefariki katika ajali ama ugonjwa kutokana na kazi anayofanya kwa mujibu wa Mkataba wa ajira yake ilikuwa ni shilingi 83,000.” Alibainisha Mhe. Waziri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (MB), akizungumza kwenye warsha ya siku moja ya kuwajengea uelewa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni mjini Dodoma Februari 3, 2018. Kulia ni Mwenyekiti Mwenza wa Bunge, Mhe. Andrew Chenge, na katikati ni Mwenyekiti wa Warsha hiyo, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamatui ya Bunge ya Katiba na Sheria na Mwenyekiti Mwenza wa Bunge, Mhe. Najma Giga.
Mhe. Najma Giga(katikati), akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo. Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, iliishauri serikali juu ya umuhimu wa waheshimiwa wabunge kukutana nna wataalamu kutoka WCF ili kuwajengea uelewa wa shughuli za Mfuko. 
Mhe. Andrew Chenge, akizunhgumza kwenye warsha hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa mada juu ya uelewa wa jumla kuhusu utekelezaji wa Matakwa ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, sura 263 marejeo ya mwaka 2015 mjini Dodoma leo Februari 3, 2018.
Baadhi ya waheshimiwa wabunge na viongozi wa WCF wakifuatilia warsha hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DK. Shein aongoza Kikao cha Kamati Maalum ya halmashauri kuu ya CCM Taifa (zanzibar)

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein leo Februari 4, 2018 ameongoza Kikao cha kawaida cha siku moja cha  Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar.

Hiki ni Kikao cha kwanza tangu Wajumbe wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) walipochaguliwa  kupitia Mikutano Mikuu ya Mikoa, Jumuiya na Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi uliofanyika mwaka jana katika Uchaguzi wa Chama.

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika ukumbi wa mkutano baada ya kuwasili na kupokelewa na Wajumbe wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar, kulia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Juma Mabodi.(Picha na Ikulu)
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiongoza Kikao cha kwanza cha Kamati Maalum ya CCM kilichofanyika katika Ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM kisiwandui Zanzibar, baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa CCM uliofanyika mwaka jana Dodoma.(Picha na Ikulu).

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza wakati wa Mkutano wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Juma Mabodi.(Picha na Ikulu)

WAJUMBE wa Mkutano wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua mkutano huo wa kwanza wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM kisiwandui Zanzibar.(Picha na Ikulu) .


KAMISHNA MKUU WA TRA AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA TRA MKOA WA MARA

$
0
0

Na: Veronica Kazimoto-Bunda, 

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere amemsimamisha kazi Meneja wa TRA Mkoa wa Mara Ndg. Nicodemus Mwakilembe kutokana na uzembe wa kutosimamia vizuri matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kwa wafanyabiashara wa mkoani kwake. 

Uamuzi huo umetokana na ziara ya kushtukiza ya kukagua matumizi ya EFD aliyoifanya Kamshina Mkuu wa TRA kwenye baadhi ya maduka ya biashara Wilayani Bunda Mkoa wa Mara. Akizungumza mara baada ya ziara yake, Kamishna Mkuu Kichere alisema Meneja huyo ameonyesha uzembe wa hali ya juu kwani kuna wafanyabishara wengi mkoani kwake ambao walishalipa fedha kwa ajili ya kupata mashine za EFD lakini mpaka sasa hawajapatiwa mashine hizo. 

"Katika ziara yangu nimegundua kwamba, wapo wafanyabiashara ambao walikwisha kulipia mashine tangu mwaka 2013, 2014 na 2015 lakini mpaka sasa bado hawajapatiwa mashine za EFD na wamekuwa wakitumia mwanya huo kama kinga ya kutochukuliwa adhabu na TRA wakati Meneja wa Mkoa yupo na hachukui hatua zozote. Huu ni uzembe uliopitiliza na kamwe siwezi kuuvumilia," alisema Kichere. 

Kutokana na uzembe huo, Kamishna Mkuu Kichere amewaagiza Mameneja wote wa TRA nchi nzima pamoja na majukumu mengine, kuhakikisha wanasimamia kikamilifu matumizi ya mashine za EFD katika mikoa yao na amesema hatasita kumuwajibisha Meneja yeyote atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akimsisitizia jambo Mfanyabiashara wa duka la nguo Wilayani Bunda Mkoani Mara kuhusu suala la umuhimu wa kutumia mashine ya Kielektroniki ya Kutolea Risiti (EFD) mara alipofanya ukaguzi wa mashine hizo katika baadhi ya maduka Wilayani hapo 3 Februari, 2018.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akikagua taarifa ya mauzo ya siku ya Mashine ya Kielektroniki ya Kutolea Risiti (EFD) toka kwa Wafanyabiashara wa duka la vifaa vya nyumbani Wilayani Bunda Mkoani Mara mara alipofanya ukaguzi wa mashine hizo katika baadhi ya maduka Wilayani hapo 3 Februari, 2018.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (aliyekaa mbele) akiongea na kutoa maagizo kwa Meneja wa TRA Wilaya ya Bunda Mkoani Mara pamoja na wafanyakazi wengine wa Mamlaka hiyo kuhusu ukusanyaji wa mapato ya Serikali mara alipotembelea ofisi ya TRA Wilayani hapo ili kujionea namna ukusanyaji mapato unavyofanyika mapema 3 Februari, 2018.

NHIF TANGA WAENDELEA KUHAMASISHA MPANGO WA TOTO AFYA KADI KWA WAKAZI WA JIJI LA TANGA

$
0
0

Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Sophia Shabani kushoto akitoa elimu ya mpango wa Toto Afya kadi kupitia kipeperusi kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda lao kwenye viwanja vya Tangamano ambapo walikuwa wakihamasisha mpango wa Toto Afya kadi
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Sophia Shabani kushoto akimsikiliza kwa umakini mmoja wa wananchi waliotembelea banda lao kwenye viwanja vya Tangamano ambapo walikuwa wakihamasisha mpango wa Toto Afya kadi

Mmoja kati ya wakazi wa Jiji la Tanga katikati akimsikiliza kwa umakini afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga kuhusu umuhimu wa mpango wa Toto Afya kadi
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Sophia Shabani kulia akitoa elimu ya namna ya kujiunga na mpango wa Toto Afya kadi kwa watoto mkazi mmoja wa Jiji la Tanga ambaye aliwatembelea kwenye banda lao eneo la Tangamano 

Mwakyembe apongeza TBC kwa kuongeza Usikivu maeneo ya Mipakani mwa Tanzania

$
0
0

Na Anitha Jonas – WHUSM 

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe ameupongeza uongozi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kuongeza usikivu katika maeneo mbalimbali ya mipakani mwa nchi. 

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa pongezi hizo alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika hilo uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam ambapo katika mkutano huo walijadili mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya bajeti na mwenendo wa shirika hilo. 

“Ninafuraha kubwa kupata taarifa ya kuimarika kwa usikivu katika maeneo ya mipakani yaliyokuwa na yanasumbua kwa muda mrefu kama maeneo ya Tarakea,Kibondo,Longido,Tarime na Mbababey na pamoja na maeneo ya Mtwara na Nachingwea,”Dkt.Mwakyembe. 

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo Mheshimiwa Waziri Mwakyembe aliendelea kupongeza uongozi wa TBC kwa kufanya maamuzi ya kutumia mafundi mitambo wa ofisi yao kwa ajili ya kufunga mitambo hiyo pamoja na kufanya matengenezo pia aliwapongeza mafundi mitambo waliofanya kazi hiyo kwa uaminifu na uzalendo huku akiomba uongozi wa shirika hilo kuwapeleka bungeni mafundi hao wakati wa bunge la bajeti. 

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Rioba alieleza kuwa mpaka sasa Wilaya ya Geita tayari kumeshafungwa mitambo mipya inayosaidia kuboresha usikivu kwa uhakika na kazi hiyo imefanywa na mafundi wazalendo wa shirika hilo. 

Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufundi kutoka TBC Bw. Joseph Kambanga alieleza kuwa mpaka sasa kazi ya kububoresha usikivu inaendelea na baadhi ya mafundi walikuwa Tarime wakiendelea na kazi hiyo na kwa mwezi ujao wanategemea kuongeza usikivu kwa Mkoa wa Mtwara na Nachingwea . 

Pamoja na hayo Waziri Mwakyembe ameuagiza uongozi wa TBC pia kufichua uovu uliyoko katika jamii kwani serikali ya awamu ya tano inapiga vita ufisadi na matendo maovu katika jamii hivyo wasibaki nyuma katika kuyaangazia hayo pale wanapohabarisha umma. 


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe akiwapongeza viongozi na watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania kwa kuongeza usikivu kwa maeneo ya mipakani  (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam,kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Rioba.



Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt.Ayoub Rioba akitoa taarifa ya upanuzi wa usikivu   wa matangazo ya Shirika  hilo nchini kwa  Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (Kushoto) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe(aliyeketi wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mafundi mitambo wa Shirika la Utangazaji Tanzania baada ya ufunguzi wa mkutano wa baraza la wafanyakazi uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu kutokana na kufurahiswa na kazi waliyoifanya  ya kupanua usikivu kwa maeneo mbalimbali nchini,aliyeketi watatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Rioba na wapili kutoka kulia aliyeketi ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufundi TBC Bw.Joseph Kambanga.



Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe(aliyeketi wanne kutoka kulia)  mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa baraza la wafanyakazi wa shirika hilo jana jijini Dar es Salaam aliyeketi watatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Rioba

Leo ni Siku ya Saratani Duniani (World Cancer Day).

$
0
0
Hapa nchini, tatizo la Saratani limekuwa likiongezeka kila mwaka. Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa, kila mwaka wagonjwa wapya wapatao 50,000 hugundulika na saratani za aina mbalimbali Tanzania. 

Na kati ya hao ni *wagonjwa 13,000 tu, sawa na 26% ndio wanaofanikiwa kufika katika Hospitali zetu kuweza kupata matibabu*. 

Aidha, *wagonjwa walio wengi (takribani asilimia 70) hufika Hospitalini kwa ajili ya matibabu wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa (hatua ya 3 na ya 4)*, hali ambayo hupunguza uwezekano wa wagonjwa kuweza kupona maradhi hayo.

Takwimu za mwaka 2016/2017 kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonyesha kwamba Saratani zinaoongoza nchini ni: 
1. Saratani ya Kizazi ​(32.8%)
2. Matiti ​(12.9%)
3. Ngozi (Kaposis Sarcoma)  ​(11.7%)
4. Kichwa na Shingo ​(7.6%)
5. Matezi ​(5.5%)
6. Damu ​(4.3%)
7. Kibofu cha Mkojo ​(3.2%)
8. Ngozi (Skin)  ​(2.8%)
9. Macho ​(2.4%)
10. Tezi Dume ​(2.3%)

Katika kuadhimisha Siku ya Saratani Duniani *ninatoa wito na kuhimiza kila mmoja wetu kupima ugonjwa wa Saratani. *Saratani inatibika endapo itagunduliwa mapema*. 

Serikali ya Awamu ya 5 inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli itaendelea na jitihada za kuongeza uelewa  wa wananchi juu ya vyanzo mbalimbali vinavyosababisha saratani ili kila mmoja wetu aweze kujikinga. Vyanzo hivi ni pamoja na *Mtindo wa kimaisha (Life Style) kama vile Uvutaji wa sigara, ulaji wa vyakula usiofaa (kula vyakula vyenye mafuta mengi, kutokula matunda na mboga mboga za kutosha), matumizi ya pombe kupita kiasi, matumizi ya dawa za kulevya na kutofanya mazoezi*.

Mahakama ya Afrika kuhamasisha wadau Jamhuri ya Demokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi (SADR)

$
0
0
Arusha, 4 February, 2018-Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) inaendelea kuimarisha juhudi zake za kuitangaza kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika(AU) pamoja na wadau mbalimbali ili waweze kuitumia kikamilifu kupeleka mashauri yaliyotimiza vigezo katika Mahakama hiyo.

Katika kufanikisha juhudi hizo, AfCHPR inafanya ziara ya kikazi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi (SADR) ili kukutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali.

Katika ziara hiyo inayofanyika kuanzia Februari 05 hadi 07 mwaka huu,wajumbe wa Mahakama hiyo wakiwemo majaji 3 wataendesha semina kwa wadau husika na pia watakutana na Rais wa nchi hiyo pamoja na Spika wa bunge la SADR.

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu,Jaji Sylvain Ore’,amesema semina hiyo inalenga kukuza uelewa wa wadau hao juu ya uwepo wa Mahakama hiyo hivyo, kuleta hamasa kwa nchi nyingi za Umoja wa Afrika kuridhia itifaki iliyoanzisha AfCHPR na kutoa tamko rasmi la kutambua na kukubali mamlaka ya Mahakama hiyo kuweza kupokea kesi za watu binafsi na Mashirika yasiyo ya kiserikali(NGO’s).

“Ili Mahakama iweze kufanikisha malengo yake na pia kuimarisha mfumo wa haki za Binadamu barani Afrika,nchi nyingi za Umoja wa Afrika hazina budi kuridhia itifaki iliyounda Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu kwa mujibu wa kifungu cha 34(6)” alisema Rais huyo wa AfCHPR.

Tangu mwaka 2010,Mahakama hiyo ya Afrika imefanikiwa kuendesha programu mbalimbali zinazolenga kutoa elimu ya uwepo wa Mahakama hiyo pamoja na shughuli zake katika baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Chad,Ethiopia,Afrika ya Kusini,Ghana,Malawi,Kenya,Uganda,Zambia na Ivory Coast.

Mahakama ya Afrika ilianzishwa kwa mujibu wa kifungu namba 1 cha itifaki ya mkataba ulioanzisha Mahakama hiyo ambapo Itifaki hiyo ilikubaliwa Juni 09,1998 nchini Burkina Faso na ikaanza kutumika Januari 25,2004 na ilianza shughuli zake rasmi Novemba 2006.

Aidha hadi Desemba mwaka jana,jumla ya maombi 155 ya mashauri yalipokelewa na Mahakama hiyo na kesi 32 zimekamilishwa.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images