Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA KUSIMIKWA KWA ASKOFU MKUU WA TANO WA KANISA LA ANGLIKANA DAYOSISI YA DAR ES SALAAM LEO

0
0
  Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Mteule Mch. Can. Jackson Sosthenes Jackson akiweka sahihi hati ya kiapo baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa  kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo leo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018

 Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Mteule Mch. Can. Jackson Sosthenes Jackson akiweka wakfu na kusimikwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini Dkt Jacob Chimeledya  kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza  Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa  kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018.
 Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Willim Mkapa akimpongeza  Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa  kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
 aji Mkuu wa Tanzania Mstaafu Mhe Augustino Ramadhani akipiga kinanda kwenye sherehe za  kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   na mkewe Mama janeth Magufuli wakikomunika kwenye sherehe za  kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   na mkewe Mama janeth Magufuli pamoja na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakishiriki katika Ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   akiongea machache baada ya kushiriki  katika Ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimpongeza  Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimsihi Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Nchini Dkt. Jacob  Chimeledya kuketi kwenya kiti alichoandaliwa yeye wakati wa kupiga  picha za pamoja wakati wa sherehe za  kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Nchini Dkt. Jacob  Chimeledya na viongozi wengine  wakati wa sherehe za  kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 

Picha na IKULU

TUME YA UCHAGUZI (NEC) YAJIBU UPOTOSHWAJI WA CHADEMA KUHUSU KUHAMISHA VITUO JIMBO LA KINONDONI

0
0
Hussein Makame, NEC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema uamuzi wa kuhamisha vituo 46 vya kupigia kura katika jimbo la Kinondoni umezingatia matakwa ya kanuni za Uchaguzi kwa kuvishirikisha vyama vyote vya siasa ikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani jijini Dar es Salaam, kufuatia taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya magazeti zinazodai kuwa Chadema hakikushirikishwa katika uamuzi wa kuhamisha vituo hivyo.

Alisema kabla ya uamuzi wa kubadilisha vituo hivyo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni iliitisha mkutano na vyama vya siasa tarehe 30 Januari, 2018 na wawakilishi 26 walishiriki kwenye mkutano huo wakiwemo wawakilishi wa Chadema.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushirikiana na vyama vya siasa katika kikao kilichofanyika tarehe 30 mwezi Januari mwaka huu walikubaliana kuhamisha vituo 46 na katika vituo hivyo vituo 16 viko kata ya Kigogo, vituo 8 viko kwenye kata ya Mwananyamala na vituo 22 viko kwenye kata ya Kijitonyama” alisema Kailima.

Alifafanua kuwa kwa mujibu wa kifunga cha 21 (1) cha kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, vituo vya kupigia kura havitakiwa kuwa kwenye maeneo ya watu binafsi, nyumba za mashabiki wa vyama vya siasa au maeneo ya majeshi na ibada.

“Nimesikitishwa na kauli ya Chadema eti hawakushirikishwa, nimesikitishwa kwa sababu kumbukumbu za mikutano zilizopo tarehe 30 Januari mwaka huu, chama cha Chadema kiliwakilishwa na Mwenyekiti wa Wilaya Bw. Mustafa Muro pamoja na Katibu wa Wilaya Bw. Shabani Kirita” alibainisha Kailima.

Rasimu ya Katiba Mchezo wa Ngumi ya kabidhiwa kwa Waziri Mwakyembe

0
0

Na Anitha Jonas – WHUSM-Dar es Salaam

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameipongeza Kamati iliyoandaa rasimu ya katiba ya mchezo wa ngumi nchini kwa kumaliza kazi hiyo kwa wakati.

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa kauli hiyo alipokuwa akikabidhiwa rasimu ya katiba hiyo jana jijini Dar es Salaam mara baada kukamilika kwa kuandaliwa kwake na kamati maalum iliyokuwa na wajumbe 13 wakuteuliwa ambao walifanya kazi ya kuzunguka kwa wadau wa ngumi na kukusanya maoni.

“Nitateuwa watu wasaba kutoka katika kamati hii iliyounda rasimu watakao uungana na Baraza la Michezo la Taifa kuboresha rasimu hii ili tuweze kuitisha kikao kikubwa cha wadau wote wa mchezo wa ngumi na tuweze kuipitisha rasimu hii,”Dkt.Mwakyembe.

Akiendelea kuzungumza katika makabidhiano hayo Waziri Mwakyembe alieleza kuwa ataendelea kupokea maoni ya wadau hao ndani ya miezi mitatu kwa kuzingatia sheria ili kufanikisha kikao cha kupitisha rasimu hiyo ambacho kitaitishwa kwa mujibu wa sheria ili kufanikisha lengo la kuboresha sekta ya mchezo wa ngumi nchini.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na wadau wa ngumi (hawapo pichani) kuhusu mchakato wa kukamilisha rasimu ya katiba ya kusimamia mchezo wa ngumi nchini maara baada ya kukabidhiwa jana jijini Dar es Salaam,kulia kwake ni Msajili wa Vyama vya Michezo Nchini kutoka Baraza la Michezo la Taifa Bw. Ibrahim Mkwawa.
Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw.Mohamed Kiganja (kulia) akitoa taarifa kuhusu mchakato wa kuundwa kwa rasimu ya katiba ya mchezo wa ngumi kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) kabla ya makabidhiano ya rasimu hiyo jana jijini Dar es Salaam,wapili kulia ni Msajili wa Vyama vya Michezo Nchini kutoka Baraza la Michezo la Taifa Bw Ibrahim Mkwawa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kuunda rasimu ya Katiba ya kusimamia mchezo wa Ngumi nchini Bw.Emmanuel Salehe akikabidhi rasimu ya katiba hiyo kwa Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe () jana jijini Dar es Salaam katikati ni Katibu Mtendaji  Baraza la Michezo la Taifa Bw.Mohamed Kiganja.

WANA CCM MUHEZA WAADHIMISHA MIAKA 41 KUSHRIKI MSARAGAMBO UJENZI WA HOSPITALI

0
0


Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu kulia akiwa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo,Desderia Haule kushoto wakishirikiana na wananchi na wanachama wa chama hicho kushiriki msaragambo wa ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo 
Sehemu ya wananchi wakishriki kwenye zoezi la kubeba maji kwa ajili ya kushiriki Msaragambo wa Ujeniz wa Hospitali ya wilaya ya Muheza 
Sehemu ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wakishiriki kwenye kuchanganya zege
Sehemu ya wana CCM na wananchi wakishirikiana kubeba zege tayari kuimwaga kwenye msingi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza wakati waliposhiriki Msaragambo ambao uliongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu .

WANANCHI BOMBABILI WAPEWA SOMO UPIMAJI WA ARDHI

0
0
Na David John

WANANCHI wa mtaa wa Bombambili Kata ya Kivule wamepewa somo kuhusu suala zima la upimaji wa ardhi, huku wakielezwa umuhimu wa kurasimisha ardhi yao kwa lengo la kuzifikia huduma mbalimbali za kiserikali

Akizungumza katika mkutano wa wananchi wa mtaa huo ambao uliitishwa na ofisi ya Serikali hiyo. Adolph Milunga ambaye ni mtalaamu mpimaji kutoka chuo cha ardhi mkoani Morogoro aliwaeleza wananchi hao umuhimu wa kupima ardhi na faida Zake.

Amesema hata kuchagua watalaamu kutoka chuo cha Ardhi Morogoro hawajafanya Makosa Kwani ni uhakika kwamba serikali ndio inasimamia ambapo kupimwa kwa ardhi kunakufanya kuondoka kwenye umasikini.

Ameongeza kuwa kupimwa kwa ardhi kunakuwezesha kupata dhamana Mahakamani na mambo mengine kama mirathi. Lakini pia mikopo kwa urahisi tofauti na kuwa na ardhi ambayo haijapimwa.

" wao kama watalaamu wa serikali wanafanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa mno na kwenye mtaa huu tumetoa ofa ya 160,000 na ofa hii itadumu kwa wiki moja. "alisema . Pia amesema baada ya kumalizika kwa wiki moja hakutakuwa tena kwa maana ahadi tena ya ofa hata hivyo watakwenda kuchungulia na kuona kuna nini kipo huko Benki.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Wilaya Tano Zitakazofanya Vizuri Ujenzi wa Vituo vya Afya Kupata Vyeti.

0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amesema wilaya tano zitakazofanya vizuri katika ujenzi wa vituo vya afya unaoendelea hapa nchini zitapewa vyeti na kutangazwa.

Jafo aliyasema hayo alipokuwa akifunga mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa wilaya yaliyofanyika Mkoani Dodoma mwanzoni mwa mwezi huu.

“Nendeni mkashindane mpate matokeo makubwa, kufikia Aprili 30 mwaka huu tuone vituo vya afya vimekamilika. Wilaya Tano zitakazo fanya vizuri zaidi katika ujenzi wa vituo vya afya zitapewa zawadi na kutangazwa,” alisema Jafo.Aliendelea kusema kuwa Wilaya 10 zitakakofanya vibaya zitatangazwa pia, aidha amesema ni imani yake kuwa wilaya zote zitafanya vizuri katika ujenzi huo.“Lakini hata kama wilaya zote zitafanya vizuri basi zitatangazwa kuwa zimefanya vizuri,” alifafanua Jafo.

Jafo ameuelezea ujenzi huo kuwa ni ujenzi mkubwa kufanyika nchini tangu nchi ipate uhuru ambapo zaidi ya vituo vya afya 200 vinajengwa nchi nzima. Vituo hivyo vinatarajiwa kukamilika ifikapo Aprili 30 mwaka huu vikiwa na lengo la kupunguza vifo vya kina mama na watoto hasa maeneo ya vijijini.

Hivyo basi Jafo amewataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi hao kupitia mafunzo ya uongozi waliyoyapa wakatekeleza kwa vitendo usimamizi wa ujenzi wa vitu hivyo ili viweze kukamilika kwa wakati na wananchi waweze kupata huduma za matibabu haraka iwezekanavyo.

WAZIRI MAHIGA AHITIMISHA ZIARA NCHINI KOREA KUSINI, AAHIDI USHIRIKIANO WENYE TIJA KWA MAENDELEO YA WANANCHI WOTE

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga ameahidi kusimamia uimarishwaji wa uhusiano wa kiuchumi na biashara kati ya Tanzania na Korea Kusini ili wananchi wa pande zote mbili wapate manufaa. 

Waziri Mahiga ameyasema hayo alipokuwa anahitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu ambapo siku ya mwisho aliitumia kikamilifu kukutana na taasisi za umma za biashara na viwanda, Benki ya Exim ya Korea pamoja na makampuni binafsi yanayojipanga kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania. 

Amesema kuwa miaka 25 ya kwanza ya uhusiano wetu na Jamhuri ya Korea ilijikita kwenye kuweka misingi imara ya uhusiano wa kidiplomasia ambapo nchi zetu zilikuwa zinajiimarisha kama mataifa huru. “Sasa ni wakati wa kushamiri kiuchumi tuone sekta binafsi zinavyoshiriki katika kukuza uchumi, wananchi wa Tanzania waje kwa wingi nchini Korea kujifunza masuala ya teknolojia, uhandisi na hata usanifu na ubunifu. Huu ndio uhusiano wenye tija kwa mataifa yetu”. Mheshimiwa Waziri alisema.

Akizungumza na Bw. Chang Yaong Hun, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim ya Korea, Mheshimiwa Mahiga mbali na kuishukuru taasisi hiyo kwa kuendelea kutoa mikopo na misaada nchini Tanzania, Waziri Mahiga alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ya Mheshimiwa John Pombe Magufuli sasa imejikita kwenye mapambano dhidi ya rushwa na ujenzi wa viwanda ili kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wetu. Kwasasa Benki hiyo inatekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umeme na maji mikoa mbalimbali ya Tanzania ukiwemo Mkoa wa Dar es Salaam. 
Mheshimiwa Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa kwenye mazungumzo na Bw. Chang Yaong Hun, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim ya Korea Kusini. Viongozi hao wawili walikutana kwenye ofisi za Benki hiyo Jijini Seoul Korea Kusini wakati wa ziara ya kikazi ya siku tatu ya Waziri Mahiga nchini humo.
Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa na ujumbe wake kwenye mazungumzo na Bw. Chang Yaong Hun, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim ya Korea Kusini. Viongozi hao wawili walikutana kwenye ofisi za Benki hiyo Jijini Seoul Korea Kusini.
Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa kwenye picha ya pamoja na Bw. Jundong Kim, Makamu Mwenyekiti wa Korea Chamber of Commerce and Industries (KCCI). Mwingine pichani ni Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Korea Mheshimiwa Matilda Masuka. 
Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa na ujumbe wake kwenye mazungumzo na Bw. Jundong Kim, Makamu Mwenyekiti wa Korea Chamber of Commerce and Industries (KCCI). 
Mheshimiwa Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akimkabidhi zawadi ya majani ya chain a kahawa za Tanzania Bw. Choi Jong-won, Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Dong Myeong ya Korea Kusini. 



MICHUZI BEAT: Ajira iliyojificha lakini yenye kuingiza fedha nyingi kwa Mtanzania


WCB KUTAMBULISHA WASANII KWA 'STYLE' HII....

KAMISHNA MKUU WA TRA AENDELEA KUHIMIZA MATUMIZI YA EFD

TBA - UKARABATI WA SHULE KONGWE YA SEKONDARI KIGOMA

ALICHOSEMA MBOSSO BAADA YAKUTAMBULISHWA NA WCB, TEMEKE

msanii Issa Mussa "Cloud 112" film yake nchini Denmark Machi 31, 2018

TATUMZUKA YACHANGIA VIFAA VYA SHULE NA MATANKI YA MAJI WILAYA YA UBUNGO.

0
0
 Katibu Tawala wilaya ya Ubungo ,James Mkumbo akizungumza na Waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuhusu wilaya hiyo kupokea msaada wa baadhi ya vifaa Vya shule,kama vile Madawati 25,Vitabu 131 pamoja Matanki makubwa mawili  ya kuhifadhia maji kutoka kwa wachezeshaji wa Mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka.Kulia ni Mwakilishi wa TatuMzuka,Bi Patronela. Mkumbo alisema kuwa wamepewa msaada wa vifaa hivyo kutokana na mkazi wa wilaya hiyo ya Ubungo,aitwaye Catherine Tryphone kushinda kitita cha Milioni 60 kupitia mchezo huo wa TatuMzuka.
 Mwakilishi wa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka,Bi.Patronela akikabidhi Vitabu 131 kwa ajili ya shule za Wilaya hiyo kwa  Katibu Tawala wilaya ya Ubungo ,James Mkumbo,kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya  hiyo,Ally Juma Ally akishuhudia tukio hilo.
 Mwakilishi wa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka,Bi.Patronela akikabidhi madawati 25 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo,Ally Juma Ally,pichani kati anaeshuhudia ni Katibu Tawala wilaya ya Ubungo ,James Mkumbo.Pichani nyuma kulia ni moja ya tanki lililokabidhiwa kwa viongozi hao wa Serikali.

taarifa ya maadhimisho ya 19 kumbukizi ya prof Kairuki

0
0
  

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Herbert Kairuki Memorial, Prof. Chales Mgone akiongea na waandishi wa habari kwenye mkutano nao uliohusu maadhimisho ya Kumbukizi ya Mwasisi na Mmiliki wa Shirika la Elimu Kairuki (KHEN), Chuo Kikuu cha Kumbukumbuku ya Hubert Kairuki (HKMU), Hospitali ya Kairuki (KH)  na Shule ya Uuguzi Kairuki (KSN). Mkutano huo umefanyika Dar es Salaam leo Februari 4 2018. Kushoto ni Makamu Mkuu wa HKMU (Taaluma), Prof. Ntabaye Moshi na Mkurugenzi wa chuo hicho, Dkt. Asser Mchomvu. (Na Robert Okanda Blogs)
Mkurugenzi wa chuo hicho, Dkt. Asser Mchomvu, akiongea na waandishi wa habari kwenye mkutano uliohusu maadhimisho ya Kumbukizi ya Mwasisi na Mmiliki wa Shirika la Elimu Kairuki (KHEN), Chuo Kikuu cha Kumbukumbuku ya Hubert Kairuki (HKMU), Hospitali ya Kairuki (KH)  na Shule ya Uuguzi Kairuki (KSN). Mkutano huo umefanyika Dar es Salaam leo Februari 4 2018. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Herbert Kairuki Memorial, Prof. Charles Mgone na Makamu Mkuu wa HKMU (Taaluma), Prof. Ntabaye Moshi. 

MAADHIMISHO YA 19 YA KUMBIKIZI YA PROF. HUBERT KAIRUKI

0
0
Marehemu Prof. Hubert Clemence Mwombeki Kairuki na mkewe Mama Kushubila Kairuki;  mwanzilishi mwenza wa Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN)
Utangulizi: 
Hospital ya Kairuki (KH), Shule ya Uuguzi Kairuki (KSN) na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), kwa pamoja vitashiriki katika maadhimisho ya 19 ya kumbukizi ya Marehemu Prof. Hubert Clemence Mwombeki Kairuki, muasisi wa taasisi mama inayosimamia taasisi hizo yaani Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN). 


Kumbukizi hiyo itafanyika kwa juma moja kuanzia tarehe 1 Februari 2018 na kufika kilele chake tarehe 6 Februari 2018, kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama ifuatavyo: 

* Kuweka jiwe la Msingi kwenye kituo cha kusaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida Bunju. 
 *Kuanzisha kliniki ya mama, baba na mtoto. 
 *Kutoa huduma za afya bila malipo kwa wananchi. 
 *Uchangiaji Damu/Blood Donation.
 *Mhadhara wa Tisa wa Kitaaluma wa kumbukizi ya Prof. Hubert Kairuki. 
 *Mashindano ya kitaaluma baina ya wanafunzi wa HKMU na KSN. 

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Herbert Kairuki Memorial, Prof. Chales Mgone akiongea na waandishi wa habari kwenye mkutano nao uliohusu maadhimisho ya Kumbukizi ya Mwasisi na Mmiliki wa Shirika la Elimu Kairuki (KHEN), Chuo Kikuu cha Kumbukumbuku ya Hubert Kairuki (HKMU), Hospitali ya Kairuki (KH)  na Shule ya Uuguzi Kairuki (KSN). Mkutano huo umefanyika Dar es Salaam leo Februari 4 2018. Kushoto ni Makamu Mkuu wa HKMU (Taaluma), Prof. Ntabaye Moshi na Mkurugenzi wa chuo hicho, Dkt. Asser Mchomvu. 

Mkurugenzi wa chuo hicho, Dkt. Asser Mchomvu, akiongea na waandishi wa habari kwenye mkutano uliohusu maadhimisho ya Kumbukizi ya Mwasisi na Mmiliki wa Shirika la Elimu Kairuki (KHEN), Chuo Kikuu cha Kumbukumbuku ya Hubert Kairuki (HKMU), Hospitali ya Kairuki (KH)  na Shule ya Uuguzi Kairuki (KSN). Mkutano huo umefanyika Dar es Salaam leo Februari 4 2018. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Herbert Kairuki Memorial, Prof. Charles Mgone na Makamu Mkuu wa HKMU (Taaluma), Prof. Ntabaye Moshi. Picha na Robert Okanda

INTRODUCING "BONGO.COM" BY Dj TozB Ft DarClvn x Neo Ndawo x Prince & Kadafi

MAGAZETI YA JUMATATU LEO FEBRUARY 5,2018

WAZIRI MKUU KATIKA HAFLA YA CHAKULA CHA MCHANA NA WATU WENYE ULEMAVU

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, katika hafla ya chakula cha mchana kwa ajili ya watu wenye ulemavu, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee. Februari 4, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na muimbaji wa muziki wa kizazi kipya, Saida Kalori, katika hafla ya chakula cha mchana kwa ajili ya watu wenye ulemavu, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee. Februari 4, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi walioshiriki katika hafla ya chakula cha mchana kwa ajili ya watu wenye ulemavu, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee. Februari 4, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpatia chakula mtoto Mwahija Hassan, katika hafla ya chakula cha mchana kwa ajili ya watu wenye ulemavu, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee. Februari 4, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpatia chakula mtoto Ibrahim Shaibu, katika hafla ya chakula cha mchana kwa ajili ya watu wenye ulemavu, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee. Februari 4, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

CCM PWANI YAPOKEA WAPINZANI 31,WANACHAMA WAPYA 331 RUFIJI NA MKURANGA

0
0

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

VIGOGO 27 kutoka chama cha wananchi (CUF) na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)waliotikisa uchaguzi mkuu 2015,maeneo mbalimbali wilayani Rufiji Mkoani Pwani ,wamevihama vyama vyao na kukimbilia CCM.

Aidha wanachama wapya 120 wamejiunga na CCM wilayani Rufiji huku wengine 211 wamejiunga na chama hicho wilayani Mkuranga.Hayo yalijiri katika msafara wa Chama Cha Mapinduzi mkoani Pwani ,kuadhimisha miaka 41 ya CCM katika wilaya hizo ambapo pia walishiriki katika shughuli za kimaendeleo.

Akiongea kwenye maadhimisho hayo ,Utete ,mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rufiji ,Kaswakala Mbonde alisema wapambe na baadhi ya viongozi hao wa upinzani wamekikubali chama tawala kutokana na mabadiliko ya maendeleo na uchumi yanayofanywa na serikali yake .

Alisema serikali ya awamu ya tano imefanya mambo mengi makubwa katika sekta ya miundombinu ,afya,elimu,uwekezaji hivyo wapinzani hawana la kukosoa.Pamoja na hayo ,Mbonde alieleza wapo wanachama wengine wapya 255 waliojiunga na jumuiya ya wanawake (UWT) na 25 wamejiunga jumuiya ya wazazi Rufiji .

Mwenyekiti Wa kitongoji cha Nyangwai kata ya Chemchem aliyekuwa (CUF) Jafar Mpunjo alisema ,wapinzani kazi yao kukosoa na kubeza lakini kwasasa wanakosa la kukosoa .Mwingine aliyehamia CCM Ashura Sultan alisema ,upinzani ukifika 2019-2020 utakuwa umekufa .
 ALIYEKUWA mwenyekiti  wa  serikali ya kitongoji cha Nyangwai Kata ya Chechem wilayani Rufiji ,mkoani Pwani mwenye  miwani nyeusi ,ameiacha nafasi hiyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa  maadhimisho ya miaka  41 ya CCM huko Utete ,ambapo msafara wa  CCM Pwani ,ulipokea wapinzani 27 na wanachama wapya 120 katika maadhimisho hayo.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
 WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Utete wilayani Rufiji wakisheherekea baada ya kupokelewa wapinzani 27 waliotikisa uchaguzi mkuu 2015 wilayani hapo,katika mkutano wa  maadhimisho ya miaka  41 ya CCM ,ambapo msafara wa  CCM Pwani ,ulipokea pia wanachama wapya 120 katika maadhimisho hayo.
 MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Pwani Ramadhani Maneno akikabidhi kadi kwa  wanachama wapya katika mkutano wa  maadhimisho ya miaka  41 ya CCM huko Utete ,pia alipokea wapinzani 27 na wanachama wapya 120 katika maadhimisho hayo
Wakila kiapo.

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images