Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

KIPINDI CHA DIRA YA DUNIA BBC.


MRADI WA KOICA KUWAWEZESHA MABINTI WAFANYA MKUTANO

$
0
0
WADAU wa mradi wa kuwawezesha mabinti na wanawake vijana katika sekta ya elimu wamekutana katikati ya wiki kujadili mpango kazi wa utekelezaji wa mradi wa UNESCO kwa kushirikiana na UNWomen pamoja na UNFPA unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Korea (KOICA). 

Mradi huo ambao umelenga kuondoa vikwazo vya elimu kwa wasichana na wanawake kwa kuangalia sera, sheria na kanuni zinazowezesha maendeleo kwa wanawake kwa kuzingatia matakwa ya Umoja wa Mataifa na makubaliano ya kimataifa ambayo Tanzania imetia saini ulianza mwaka 2016. 

Mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kwa kusimamiwa na Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN Women) na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya Watu ( UNFPA) unatarajia kuiwezesha Tanzania kuwezesha elimu kwa kutumia mbinu mtambuka kwa kutambua watu wa pembezoni.Kaimu Mkuu wa ofisi na Mkuu wa kitengo cha Elimu ofisi ya Unesco Dar es Salaam, Faith Shayo akitoa neno la utangulizi wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa wa Kitaifa anayeshughulikia Elimu ya Afya na Ukimwi ofisi za Unesco Dar es Salaam, Mathias Herman.

Mradi huo unatarajiwa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kuwa na uwezo wa kuingia katika utuuzima bila kuvurugwa utaratibu wa upatikanaji wa elimu.

Mradi huo unatekelezwa katika wilaya nne za Ngorongoro, Sengerema, Kasulu na Mkoani huko Pemba.Mkutano huo wa kamati ya ufundi ya mradi ulilenga kutoa ratiba ya utekelezaji wa mradi baada ya mada mbalimbali kuwasilishwa za utafiti uliofanyika na hali halisi iliyopo nchini kuhusu wasichana na wanawake kwa kuangalia sharia zilizopo, utamaduni na tabia. 
Akizungumza katika mkutano huo Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) Kitivo cha Elimu, Dk. Felix Mulengeki alisema kwamba mradi huo utafanikiwa kutokana na ukweli kuwa sharia na katiba za nchi zipo vizuri huku sera nazo zikitambua haki ya kusoma.Ofisa wa Kitaifa anayeshughulikia Elimu ya Afya na Ukimwi ofisi za Unesco Dar es Salaam, Mathias Herman akiwasilisha taarifa ya mwaka 2017 ya mradi huo wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.

Wakati mradi unabuniwa ilionekana kwamba kutoeleweka kwa katiba na sheria zilizopo zinazomlinda mtoto wa kike, uelewa hafifu umekuwa ukikwamisha maendeleo kielimu kwa watoto wa kike.Dk. Mulengeki alisema kwamba hali ya sera na sheria nchini Tanzania ni salama zaidi kilichobaki utekelezaji wa mradi huo umelenga kukusanya pia takwimu kwa ajili ya kutumika kutengeneza sera. 

  Katika mradi huo unatarajiwa kuongeza uelewa zaidi wa elimu ya afya ya uzazi na kutengeneza mifumo ya kuelimisha watu.Mada mbalimbali zilizojadiliwa ziliwezeshwa kupata muda wa utekelezaji wa vipengele mbalimbali ambavyo vilipaswa kufanyika ili kuondokana na tabia mbaya ambazo zinamnyima binti wa Kitanzania kukamilisha elimu yake.Washiriki wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu wakifuatilia ripoti ya mwaka 2017 ya mradi huo iliyokuwa ikiwasilisha Mathias Herman kwenye mkutano uliofanyika katika ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.

WANAWAKE MILIONI 3 KUPIMWA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI NA MATITI KUFIKIA DESEMBA 2018

DKT. NCHEMBA: UMAKINI UNAHITAJI KATIKA USAJILI WA WANANCHI KATIKA VITAMBULISHO VYA TAIFA.

$
0
0

NA TIGANYA VINCENT -RS TABORA

SERIKALI imewataka Watendaji wanaosimamia zoezi la usajili wananchi kwa ajili ya vitambulisho vya taifa kufanyakazi kwa umakini, uzalendo na kwa ushirikiano na jamii ili kuepuka kuandikisha na kuwapa watu wasio stahili vitambulisho vya raia.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Tabora na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt.Mwigulu Nchemba wakati uzinduzi wa zoezi la usajili wananchi kwa ajili ya vitambulisho vya kitaifa mkoani humo.

Waziri huyo wa Mambo ya Nchi alisema kuwa miaka ya nyuma ambapo Watanzania walikuwa hawana vitambulisho vya Uraia, wapo wageni kutoka katika baadhi ya nchi waliweza kutumia mwanya huo kunufaika na huduma za jamii kama vile elimu ambazo zilipaswa kutolewa kwa Watanzania.

Alisema watu hao walipomaliza masomo walirudi kwao na kunufaisha nchi zao huku wakiwa wametumia pesa za Watanzania kujinufaisha wao na nchi zao na kusema zoezi hilo linahitaji umakini na uaminifu ili kubaini wageni na raia kwa ajili ya kuhakikisha kila kundi lisajiliwe kwa hadhi yake.

Dkt. Nchemba alisema kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake na kuhakikisha hakuna mgeni anayepenya kupewa Kitambulisho cha uraia kwa njia za udandanyifu. Aidha Waziri huyo alisema zoezi la uandikishaji na utoaji wa vitambulisho hivyo ni bure , mwananchi hapaswi kulipa chochote wakati wa ufuatiliaji na kuongeza kuwa isitokee mtua akalipa pesa.

Alisema kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali watendaji au viongozi watakaobainika kuwanachangisha wananchi wakati wa zoezi zima la kusajili na utoaji wa vitambulisho vya uraia. Dkt.Nchemba alitoa wito kwa wananchi waliofikia umri wa miaka 18 na kuendelea kujitokeza mapema kwa wingi katika muda ulipangwa ili wasajiliwe na kupewa vitambulisho vya uraia.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KATAMBI ATAJA SABABU KUYUMBA KWA UPINZANI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Blogu ya jamii

KADA mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi ameeleza sababu zinazochangia kudhoofika kwa vyama vya upinzani nchini.

Amesema kuyumba kwa vyama hivyo kunachangiwa na ubinafsi waviongozi wake ambao wengine wageuza Chama ni mali yao na kutoamaamuzi ambayo si shirikishi.
 
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,Katambi amesema kuwa tanguameondoka Chadema ambako alikuwa Mwenyekiti wa Vijana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho amekuwa kimya muda mrefulakini ameona ni vema akasema mambo kadhaa kuhusu hali ya kisiasa nchini.

Kuhusu vyama vya siasa kuyumba, Katambi amesema zipo sababuambazo zimekuwa zikichangia vyama hivyo kushindwa kuwa imara namatokeo yake kubaki kulalamikia kila jambo ambalo linafanywa naSerikali hata liwe lenye maslahi kwa nchi.
 
"Upinzani umeshindwa kujenga chama taasisi kwani hivi sasa kilachama ni cha mtu.vyama vingi ni vya watu na si taasisi.Dhana yataasisi ni kwamba sheria ,kanuni na taratibu lazima zifuatwe"Kama mtu anadharau katiba na misingi iliyowekwa basi huo niudikteta. Wapinzani kabla ya kukimbilia kugombea udiwani na ubunge wajikite kwanza kujenga taasisi, kama wameshindwa kuheshimu katiba za vyama vyao wanapate uhalali wa kudai Katiba,"amesema.

MICHUZI BEAT: Angalia Ajira iliyojificha yenye kuingiza fedha nyingi kwa Mtanzania

WARIOBA: Ngombale Mwiru alifanya kazi nzuri sana na Chama

IMETOSHA YASHIRIKI SIKU YA KANSA DUNIANI KWA KUPIMA WATOTO WENYE UALBINO

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Imetosha, Henry Mdimu amesema kuwa watoto wenye ualbino kati ya watano  hadi saba wanafariki kwa mwezi  katika Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na Kansa ya ngozi.

Mdimu ameyasema hayo  wakati wa upimaji wa kansa kwa watoto wenye ualbino katika Hospitali ya  0cean Road katika Maadhimisho ya Siku ya Kansa Duniani  ambayo huadhimishwa Februari 3 kila mwaka.

Amesema  kambi ya upimaji huo wameshirikiana na Hospitali ya Ocean Road na Chama cha Watu Wenye Ualbino (TAS)  katika kuhakikisha kila mtoto mwenye ualbino anapata vipimo.

Amesema kambi ya upimaji hiyo itaendelea  mikoani ambayo watapima madaktari wa Ocean Road ili kujua hali ya tatizo  ya Kansa kwa watoto wenye Ualbino na baada ya kupimwa na kuonekana kuanza kupatiwa matibabu.

“Mimi Mkurugenzi wa Imetosha naona nina wajibu wa kuwa moja kwa moja na watu wenye ualbino kuhakikisha maisha ya watoto yanaokolewa nikifanya mimi na mwingine atafanya”amesema Mdimu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Imetosha, Henry Mdimu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na maadhimisho ya siku ya Kansa Duniani ambayo Taasisi ya Imetosha imeratibu upimaji wa watoto leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Watu wenye ualbino wakiandisha  kwa ajili ya upimaji katika Hospitali ya Ocean Road leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watu wenye ualbino wakiwa  wamekaa  kwa ajili ya kwenda kupata taraibu za upimaji katika Ocean Road leo jijini Dar es Salaam (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii )

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AIPA POLE FAMILIA YA ALIYEKUWA RUBANI WA NDEGE ZA SERIKALI MAREHEMU DOMINIC BOMANI

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitia saini katika kitabu cha maombolezo kwenye msiba wa aliyekuwa rubani wa ndege za serikali, marehemu Dominic Bomani nyumbani kwa marehemu, Kinyerezi jijini Dar es salaam Februari 3, 2018.Bomani alifariki dunia katika ajali ya ndege ndogo iliyotokea Zanzibar Feb. 1 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na mmoja wa wanafamilia wa msiba wa aliyekuwa rubani wa ndege za serikali marehemu Dominic Bomani nyumbani kwa marehemu, Kinyerezi jijini Dar es salaam Februari 3, 2018.Marehemu Bomani alifariki dunia katika ajali ya ndege ndogo iliyotokea Zanzibar Feb. 1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa pole kwa familia ya aliyekuwa rubani wa ndege za serikali, marehemu Dominic Bomani nyumbani kwa marehemu, Kinyerezi jijini Dar es salaam Februari 3, 2018.Bomani alifariki dunia katika ajali ya ndege ndogo iliyotokea Zanzibar Feb. 1 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DKT.NCHEMBA: VITAMBULISHO VYA TAIFA VITAONDOA MAPINGAMIZI YA URAIA KATIKA CHAGUZI

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT-RS TABORA

Vitambulisho wa uraia vitasaidia kuwa na utambuzi wa wananchi utakao ondoa ile tabia ya baadhi ya watu kutilia mashaka wakati wa shughuli mbalimbali ikiwemo kipindi kushiriki katika zoezi la uchaguzi wote wote.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Tabora na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt.Mwigulu Nchemba wakati uzinduzi wa zoezi la usajili wananchi kwa ajili ya vitambulisho vya kitaifa mkoani humo.

Alisema kuwa mara nyingi mtu anapogombea nafasi yoyote hapa nchi au kunapokuwepo na migogoro ya kugombania mashamba ndio suala la kusema kuwa huyo sio raia linapojitokeza.

Dkt. Nchemba alisema wananchi wenye sifa kuchangamkia zoezi la usajili na upataji wa vitambulisho vya uraia ili kuepuka matatizo kama vile migogoro ikiwemo ya mapingamizi wakati chaguzi mbalimbali na kuiweza Serikali kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo kwa ajili ya wananchi wake

LSF YAKUTANA NA WADAU WA WATOA HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA, JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Mwenyekiti wa Muda wa Asasi ya kiraia ya Legal Services Facilities (LSF) Dkt. Benson Bani , akitoa neno la ufunguzi wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria.
Mkurugenzi wa Asasi ya kiraia ya LSF Bw. Kees Groenendijk akitoa mada yake ambapo alizungumzia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuelezea malengo, mambo mbalimbali yaliyofanyika kwa mwaka 2017 pamoja na mwelekeo kwa mwaka 2018, wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria.
Meneja Miradi wa LSF Bw.Ramadhani masele akielezea kiundani juu ya utendaji , mrejesho na nini kifanyike wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria.

Makundi mbalimbali ya ya wakurugenzi pamoja na wajumbe wa bodi za wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria wakijadili mambo mbalimbali na namna watakavyofanya kazi na LSF kwa mwaka 2018.

RAIS DK.MAGUFULI AWATUNUKU KAMISHENI MAOFISA WAPYA 192 JWTZ,WAMO PIA WA NCHI MARAFIKI

$
0
0

 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatunuku Kamisheni Maafisa wapya 192 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania pamoja na Maafisa kadhaa kutoka nchi marafiki katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi wakivalishana vyeo mara baada ya Kutunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi wakila Kiapo cha Utii kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika viwanja vya Ikulu mara baada ya kutunukiwa Kamisheni.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi pamoja na baadhi kutoka nchi marafiki kabla ya kuwatunuku Kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli (TMA) Meja Jenerali Paul Peter Masao katika picha ya pamoja  na Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi pamoja na baadhi kutoka nchi marafiki mara baada ya kuwatunuku Kamisheni.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma wakati Bendi ya Jeshi la Ulinzi ilipokuwa ikitoa burudani katika viwanja vya Ikulu mara baada ya kuisha kwa shughuli za Kutunuku Kamisheni.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kutunuku Kamisheni katika Viwanja vya Ikulu
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kutunuku Kamisheni kwa maafisa wapya wapatao 192 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi pamoja na baadhi kutoka nchi marafiki. PICHA NA IKULU

VULLU ACHANGIA MIFUKO YA SARUJI UJENZI NYUMBA YA MGANGA, ZAHANATI YA KIJIJI CHA KOMA

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga.

MBUNGE wa viti maalum Mkoani Pwani,Zainab Vullu amekabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji pamoja na malumalu vipande 500 ,vilivyogharimu sh .milioni 1.6,katika halmashauri ya Mkuranga.

Kati ya vifaa hivyo mifuko 50 ya saruji ni mchango katika ujenzi wa nyumba ya mganga zahanati ya Kijiji cha Koma na mifuko mingine 20 ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Kisiju Pwani.

Vullu alielekeza ,Malumalu (tiles)zipelekwe shule ya msingi Kisiju Pwani,katika ujenzi wa vyoo lakini aliomba kipaombele kipewe kwenye vyoo vya wanafunzi wa kike ili kujihifadhi wakati wakiwa katika hedhi .Aidha alisema anahamasisha ujenzi wa nyumba ya mganga na aliwataka wadau wengine waunge mkono jitihada za serikali ,halmashauri ,mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega aliyechangia mifuko 100 ya saruji .

Hata hivyo,Vullu alisema kilichomgusa kuchangia pia ni ilani ya Chama Cha Mapinduzi inaelekeza kusimamia maisha na maslahi ya mtanzania .
“Kijiji cha Koma hakina zahanati ,kutokana na suala hilo niliona nguvu za Mbunge ,halmashauri na ndipo Jan 1 ,nikwenda kuona hali ilivyo ,nimeona nitoe fedha za mfukoni mwangu nichangie mifuko ya saruji ujenzi wa nyumba ya mganga .” 
KAIMU mkurugenzi halmashauri ya Mkuranga, Mkoani Pwani,ambae pia ni afisa maendeleo ya jamii,Safina Msemo akimshukuru mbunge wa viti maalum Mkoani Pwani, Zainab Vullu (kushoto aliyesimama)kwa kuchangia baadhi ya mifuko ya saruji kati ya mifuko 70 na malumalu vipande 500 vilivyogharimu zaidi ya mil.1.6
MBUNGE wa viti maalum Mkoani Pwani, Zainab Vullu, akimkabidhi kaimu mkurugenzi halmashauri ya Mkuranga, Mkoani Pwani,ambae pia ni afisa maendeleo ya jamii,Safina Msemo (mwenye gauni la kitenge) baadhi ya mifuko ya saruji kati ya mifuko 70 na malumalu vipande 500 alivyochangia ambapo vimegharimu zaidi ya mil.1.6.Picha na Mwamvua Mwinyi.

UTENDAJI KAZI BODI YA FILAMU WAWAKUNA WAENDESHA BIASHARA ZA UTALII

$
0
0
 Katibu Mtendaj wa Bodiya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo akifafanua jambo wakati wa kikao kazi na wadau wa sekta ya Filamu ambao pia ni Wanachama wa Chama Cha Waendeshaji wa Biashara ya Utali Tanzania (TATO) jana Jijini Arusha. Lengo la kikao hicho ni kuwajengea uelewa wadau hao wa filamu kuhusu taratibu mbalimbali za kuzingatia pindi wanapojihusisha na masuala ya filamu. Kulia ni Afisa Maendeleo  ya Filamu Benson Mkenda.
  Afisa Maendeleo  ya Filamu kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Benson Mkenda akifafanua jambo wakati wa kikao kazi na wadau wa sekta ya Filamu ambao pia ni Wanachama wa Chama Cha Waendeshaji wa Biashara ya Utali Tanzania (TATO) jana Jijini Arusha. Lengo la kikao hicho ni kuwajengea uelewa wadau hao wa filamu kuhusu taratibu mbalimbali za kuzingatia pindi wanapojihusisha na masuala ya filamu. Kushoto ni Katibu Mtendaj wa Bodiya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo
 Mhasibu kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Adrian akitoa ufafanuzi kuhusu namna  wanavyoshughulikia malipo ya wadau wanapowasilisha maombi ya vibali vya filamu katika  ofisi yao  wakati wa kikao kazi na wadau wa sekta ya Filamu ambao pia ni Wanachama wa Chama Cha Waendeshaji wa Biashara ya Utali Tanzania (TATO) jana Jijini Arusha. Lengo la kikao hicho ni kuwajengea uelewa wadau hao wa filamu kuhusu taratibu mbalimbali za kuzingatia pindi wanapojihusisha na masuala ya filamu. 
 Katibu Mtendaj wa Bodiya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo akionyesho kanuni zinazotumika katika sekta ya filamu nchini wakati wa kikao kazi na wadau wa sekta ya hiyo ambao pia ni Wanachama wa Chama Cha Waendeshaji wa Biashara ya Utali Tanzania (TATO) jana Jijini Arusha. Lengo la kikao hicho ni kuwajengea uelewa wadau hao wa filamu kuhusu taratibu mbalimbali za kuzingatia pindi wanapojihusisha na masuala ya filamu. Kulia ni Afisa Maendeleo  ya Filamu Benson  Mkenda.
  Katibu Mtendaji wa Chama Cha Waendeshaji wa Biashara ya Utali Tanzania (TATO) Sirili Akko akichangia hoja wakati wa kikao kazi na wadau wa sekta ya filamu ambao pia ni Wanachama wa Chama Cha Waendeshaji wa Biashara ya Utali Tanzania (TATO) jana Jijini Arusha. Lengo la kikao hicho ni kuwajengea uelewa wadau hao wa filamu kuhusu taratibu mbalimbali za kuzingatia pindi wanapojihusisha na masuala ya filamu.
 Mmoja wa washiriki wa kikao baina ya Bodi ya Filamu Tanzania na Chama Cha Waendeshaji wa Biashara ya Utalii Tanzania (TATO)  ambaye pia ni mmiliki wa Kampuni ya African Environments Bw. Richard Beatty akichangia hoja wakati wa kikao hicho jana Jijini Arusha. Lengo la kikao hicho ni kuwajengea uelewa wadau hao wa filamu kuhusu taratibu mbalimbali za kuzingatia pindi wanapojihusisha na masuala ya filamu.
  Mmoja wa washiriki wa kikao baina ya Bodi ya Filamu Tanzania na Chama Cha Waendeshaji wa Biashara ya Utali Tanzania (TATO)  ambaye pia ni mmiliki wa Kampuni ya Jevas Hotel Bw. Leopald Kabendera akichangia hoja wakati wa kikao hicho jana Jijini Arusha. Lengo la kikao hicho ni kuwajengea uelewa wadau hao wa filamu kuhusu taratibu mbalimbali za kuzingatia pindi wanapojihusisha na masuala ya filamu. 
Baadhi ya washiriki wa kikao baina ya Bodi ya Filamu Tanzania na Chama Cha Waendeshaji wa Biashara ya Utali Tanzania (TATO)  wakifuatilia mada wakati wa kikao hicho jana Jijini Arusha. Lengo la kikao hicho ni kuwajengea uelewa wadau hao wa filamu kuhusu taratibu mbalimbali za kuzingatia pindi wanapojihusisha na masuala ya filamu. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO)

Wateja wa Zantel waendelea kuzoa zawadi promosheni ya Jero yako

$
0
0
 Mmoja wa washindi  wa droo ya wiki ya promosheni ya ‘Jero yako tu’ ya kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Mwinjuma Mdoe (kushoto), akipokea zawadi ya simu ya kisasa aina ya Moto C 4G toka Zantel kutoka kwa Mtaalamu wa Data na Masoko wa Zantel, Hamid Mohamed jijini Dar es Salaam jana. Mteja wa Zantel  akiongeza muda wa maongezi kuanzia shs mia tano hujipatia nafasi kushiriki na kujishindia Zawadi za pikipiki, baiskeli, simu na pesa taslimu. Katikati ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Bi. Rukia Mtingwa. 
 Mmoja wa washindi  wa droo ya wiki ya promosheni ya ‘Jero yako tu’ ya kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Mohamed Salum (kushoto), akipokea zawadi ya simu ya kisasa aina ya Moto C 4G toka Zantel kutoka kwa Mtaalamu wa Data na Masoko wa Zantel, Hamid Mohamed jijini Dar es Salaam jana. Mteja wa Zantel  akiongeza muda wa maongezi kuanzia shs mia tano hujipatia nafasi kushiriki na kujishindia Zawadi za pikipiki, baiskeli, simu na pesa taslimu. Katikati ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Bi. Rukia Mtingwa.
Meneja Masoko wa Zantel Tanzania, Bi. Rukia Mtingwa, Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemedy (kushoto) na Mtaalam wa Data na Masoko wa Zantel, Hamid Mohamed, wakichezesha droo ya wiki ya promosheni ya ‘Jero yako tu’ ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Mteja wa Zantel  akiongeza muda wa maongezi kuanzia shs mia tano hujipatia nafasi kushiriki na kujishindia Zawadi za pikipiki, baiskeli, simu na pesa taslimu.



SERIKALI KUIMARISHA MASOKO YA MAZAO-MAJALIWA

$
0
0

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inataka kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kupata tija.

Aliyasema hayo jana (Februari 2, 2018) wakati akikagua Kampuni ya Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), iliyoanzishwa kwa lengo la kuimarisha masoko.

Alisema kupitia Wizara ya Kilimo, Serikali imedhamiria kuimarisha masoko  ya mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kujikwamua kiuchumi.

“Kupitia Wizara ya Kilimo tunataka kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini. Wakati umefika kwa wakulima nchini kuona tija ya mazao wanayolima.”

Alitoa mfano wa zao la pamba ambalo wakulima walikuwa wanaingia mikataba na wanunuzi, mfumo ambao ulikuwa unawanyonya badala ya kuwanufaisha.

Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa TMX, Bw. Godfrey Malekano alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba wamejipanga vyema kuanza minada ya mazao.

“Tutaanzia na zao la ufuta mwezi Mei 2018 na kuendelea na mazao mengine kwa kadiri ya misimu ya mazao hayo ilivyo.”

Alisema kufanikiwa kwa Soko la Bidhaa na Mfumo wa stakabadhi ghalani kunategemea sana msaada wa Serikali.  “Soko la Bidhaa la Ethiopia linalotajwa sana kwa mafanikio, limefikia malengo yake kutokana na mkono wa Serikali.”

Bw. Malekano alisema kutokana na umadhubuti wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli wanamatumaini makubwa kwamba soko hilo  litatimiza malengo yake.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAMOSI, FEBRUARI 3, 2018.

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MWANASHERIA MKUU, NAIBU WAKE NA MAJAJI WAWILI LEO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha  Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya, Dkt. Adelardus Kilangi  Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha  Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Paul Joel Ngwembe Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha, Mhe. Gerson J. Mdemu kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania   Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza,  Mhe. George Mcheche Masaju  akiongea machache baada ya kumwapisha kuwa Jaji wa Mahakama kuu Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaangalia wakila kiapo cha maadili ya viongozi kutoka kulia  ma-Jaji wa Mahakama kuu  Mhe. George Mcheche Masaju na Mhe. Gerson J. Mdemu, wakifuatiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya Dkt. Adelardus Kilangi na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Paul Joel Ngwembe baada ya kuwaapisha  Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Mhe. Gerson J. Mdemu akiongea machache baada ya kumwapisha kuwa Jaji wa Mahakama kuu   Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya Dkt. Adelardus Kilangi  akiongea machache baada ya kumwapisha   Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018 .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Naibu  Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya Mhe. Paul Joel Ngwembe akiongea machache baada ya kumwapisha   Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018 .
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mhe. Gerson J. Mdemu baada ya kumuapisha kuwa Jaji wa Mahakama Kuu  Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018. Kushoto ni  Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya Dkt. Adelardus Kilangi  na kulia ni  Jaji wa Mahakama kuu  Mhe. George Mcheche Masaju    Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mama Samia suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, waziri wa katiba na sheria Profesa Palamagamba Kabudi,  Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika picha ya kumbukumbu na walioapishwa  ma-Jaji wa Mahakama kuu  Mhe. George Mcheche Masaju na Mhe. Gerson J. Mdemu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya Dkt. Adelardus Kilangi na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Paul Joel Ngwembe baada ya kuwaapisha  Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 3, 2018.

Picha na IKULU

NEC YARIDHIA KUHAMISHWA KWA VITUO 46 VYA KUPIGIA KURA KINONDONI.

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeridhia kuhamishwa kwa vituo 46 vya kupigia Kura katika kata tatu za jimbo la Kinondoni zitakazofanya Uchaguzi mdogo wa Ubunge Februari 17 mwaka huu.

Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Ramadhani Kailima ameeleza kuwa uamuzi wa NEC kuridhia kuhamishwa kwa vituo hivyo, umetokana na makubaliano yaliyofikiwa katika Mkutano wa Msimamizi  wa Uchaguzi wa  jimbo la Kinondoni na Vyama vya siasa juu ya kuhamishwa kwa vituo hivyo vilivyokuwa kwenye nyumba za Ibada, Zahanati na maeneo ya majengo ya watu binafsi.

Amesema Tume imeridhika na uamuzi huo kwasababu hatua zilizochukuliwa ni sahihi kwa mujibu sheria na kanuni namba 21 ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambayo inaeleza kuwa ;  Vituo vya Kupigia Kura havitakiwi kuwekwa katika majengo ya nyumba za Ibada, kambi za jeshi, nyumba za watu binafsi na  ofisi za vyama vya siasa.

“ Tumejiridhisha kuwa baadhi ya vituo katika Kata ya  Kigogo vilikuwa katika nyumba za Ibada na vingine kuwa katika maeneo yenye ufinyu wa nafasi hivyo tumeridhia vituo hivyo vihamishwe na kupelekwa katika majengo ya umma” Amesema.

Amesema kuwa baadhi ya vituo vya kupigia Kura vilivyokuwa katika majengo ya umma ikiwemo Zahanati vimehamishwa katika shule za msingi za umma zilizo katika kata hizo  ili kuondoa usumbufu kwa wagonjwa.

Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Mwananyamala Bi. Barima Omari ameeleza kuwa kata ya Mwananyamala ina vituo vya kupigia kura 65 na wapiga kura 27,589 na kuongeza kuwa vituo nane (8) vilivyokuwa katika shule ya Sekondari Kambangwa mtaa wa msisiri A vimehamishwa. Kati ya hivyo 6 vimehamishiwa katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa ya Msolomi na 2 kuhamishiwa uwanja wa kwakopa.

Naye Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi  Kata ya Kijitonyama Elizabeth Minga ameeleza kuwa Kata hiyo ina jumla ya vituo vya kupigia Kura 101, kati ya hivyo vituo 22 vimehamishwa.

Akifafanua kuhusu vituo hivyo amesema vituo 6 vilivyokuwa katika shule ya Sekondari Kenton vimehamia shule ya Msingi Mapambano na vituo 5 vilivyokuwa nje ya Ofisi ya serikali ya Mtaa wa Bwawani vimehamishiwa mbele ya ofisi hiyo. 

Aidha, vituo 6  vilivyokuwa nje ya soko la Makumbusho vimehamia ndani ya Ofisi ya Meneja wa Soko hilo na vituo 5 vilivyokuwa  katika Ofisi ya Serikali za mitaa kijitonyama vimehamishiwa katika shule ya msingi kijitonyama.

Kwa upande wake Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Kigogo Bw. Singoro Mdegela ameeleza kuwa kata yake ina idadi ya Wapiga kura 27,000 na Vituo vya Kupigia Kura  59.

Amesema katika Kata hiyo vituo 16 vimehamishwa ambapo vituo 5 vilivyokuwa eneo la Kiwenge kwenye Msikiti wa Shiha vimehamia Uwanja wa People na Vituo 6 vilivyokuwa kwenye Zahanati ya Kigogo vimehamishiwa katika Shule ya Msingi Kigogo ili kuruhusu shughuli za matibabu kwa wagonjwa kuendelea.

Aidha, vituo 5 katika ofisi ya serikali ya mtaa wa Mkwajuni vimehamishiwa katika  shule ya secondari Kigogo.

MAVUNDE ASISITIZA ELIMU ZAIDI JUU YA TATIZO LA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA

$
0
0

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde amesisitiza kuwepo kwa kampeni kubwa ya nchi nzima juu Elimu ya tatizo la Usugu wa vimelea vya dawa.

Mavunde ameyasema hayo leo wakati akihitimisha kampeni ya Elimu ya Tatizo la Usugu wa vimelea vya dawa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana-Msalato,Dodoma ambapo ametumia fursa hiyo kuwataka wadau na taasisi mbalimbali za umma na binafsi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Chama cha Wanafunzi Wafamasia Tanzania(TASPA) ambao wamejitolea kutembea nchi nzima kutoa elimu.

“Najua moja kati ya sababu nyingi zinazosababisha usugu wa vimelea vya madawa ni ubora hafifu wa dawa na utoaji wa dawa pasipo cheti cha daktari”amesema Mavunde.Kufuatia hali hiyo, Mavunde ametumia nafasi hiyo kwa kuzitaka Taasisi za TFDA na Baraza la Wafamasia Tanzania kuchukua hatua kali na stahiki kwa wale wote wanaovunja sheria na miongozo iliyowekwa katika kusimamia masuala yote ya dawa na tiba.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi, Rais wa TASPA Erick Venant ameeleza kwamba kampeni hiyo ya kujitolea wamefanya nchi nzima kwa mikoa 23 na Shule za Sekondari 123 na wamewafikia takriban watanzania 6 milioni.

Venant amesisitiza kwamba tatizo hili ni hatari kuliko hata ugonjwa wa UKIMWI kwa kuwa takribani watu 700,000 wanafariki kila mwaka kutokana na tatizo hilo na ikisiwa ifikapo 2050 jumla ya watu 10 milioni watakufa kwa mwaka.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akihitimisha kampeni ya Elimu ya Tatizo la Usugu wa vimelea vya dawa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana-Msalato,Dodoma

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akiwa na wanafunzi wa shule ya Wasichana Msalato katika kampeni ya Elimu ya Tatizo la Usugu wa vimelea vya dawa.

Chama cha Wanafunzi Wafamasia Tanzania(TASPA) wakiwa katika uhitimishaji wa kampeni ya Elimu ya Tatizo la Usugu wa vimelea vya dawa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana-Msalato,Dodoma

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Wasichana Msalato wakiwa katika kampeni ya Elimu ya Tatizo la Usugu wa vimelea vya dawa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana-Msalato,Dodoma

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akipanda mti katika Shule ya Sekondari ya Wasichana-Msalato,Dodoma

COASTAL UNION YAPOKEWA KISHUJAA,WAZIRI UMMY,RC SHIGELLA WAONGOZA MAPOKEZI

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiwasalimia wakazi wa Mji wa Pongwe mara baada ya kuwasilia na timu ya Coastal Union ikitokea mkoani Morogoro ambapo iliweza kupanda daraja baada ya kuifunga Mawenzi ya Morogoro mabao 2-0 kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella kulia akizungumza wakati alipoipokea timu ya Coastal Union mara baada ya kupanda daraja kucheza Ligi kuu msimu ujao mapokezi hayo yalifanyika kwenye eneo la Pongwe Jijini Tanga kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akizungumza katika mapokezi hayo
 Wapenzi wa soka mkoani Tanga pamoja na wananchi wakiwa wamezingira barabara ya Tanga kwenye mikoani eneo la Pongwe wakiilaki timu ya Coastal Union leo.
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akizungumza katika mapokezi hayo akizungumza katikani ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella
 Mwenyekiti wa timu ya Coastal Union,Steven Mguto katikati akimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa kamati ya usaji wa klabu hiyo Ahmed Aurora kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Tanga(TRFA) Saidi Soud
Mfungaji wa moja ya mabao yaliyoipandisha timu ya Coastal Union Athumani Iddi Chuji akizungumza kwenye mapokezi hayo leo (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images