Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 212 | 213 | (Page 214) | 215 | 216 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake kutoka nchi za Maziwa Makuu, wakati walipokuwa katika Mkutano wa Viongozi wa Nchi za Maziwa Makuu, alipoiwakilisha Tanzania katika majadiliano ya mkutano huo uliofanyika Jijini Nairobi, nchini Kenya jana Julai 31, 2013.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mkewe Mama Asha Bilal, (wa pili kulia) Balozi wa Tanzania Nchini Kenya, Dk. Batrida Burian, na viongozi wengine wakati alipowasili Jijini Nairobi juzi Julai 30, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu, uliofanyika Jiji humo jana Julai, 31, 2013. Makamu anaondoka leo Jijini Nairobi kurejea nchini baada ya kumalizika kwa majadiliano hayo. Picha na OMR

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameiwakilisha Tanzania katika mkutano wa Wakuu wa nchi za Maziwa Makuu uliofanyika jijini Nairobi Kenya, jana Jumatano ya tarehe 31, 2013. 

  Mkutano huu ulihudhuriwa na Mwenyeji wa Mkutano huo, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Mwenyekiti wa nchi za Maziwa Makuu na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, Katibu Mtendaji wa Kamisheni yas Nchi za Maziwa Makuu Prof.Ntumba Luaba, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika, wawakilishi wan chi za DRC, Zambia, Afrika Kusini, Rwanda na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa.

  Mkutano huo umepokea taarifa kutoka kwa Mawaziri wa Ulinzi kutoka katika nchi za Maziwa Makuu ambayo imepokelewa na kisha kujadiliwa. Pia ripoti kutoka kwa Kamati ya Kimataifa inayoshughulikia suala la Mazungumzo kati ya Serikali ya Kongo (DRC) na wapiganaji wa kikundi cha M23 kinachojihusisha na upingaji wa serikali ya DRC kikifanya machafuko katika Mashariki mwa Kongo (DRC) imepokelewa kujadiliwa na kisha kupitishwa mapendekezo ambayo nchi washiriki zimeyasaini.

  Wakati wa uzinduzi wa mkutano huo, nchi washirika walisisitiza kutaka kuona amani inapatikana katika nchi za Maziwa Makuu na hasa DRC, Afrika ya Kati na Sudan. Wawakilishi hao walielezea kusikitika kwao kutokana na machafuko ya amani katika nchi hizo na wakawataka viongozi mbalimbali wanaotajwa kuhusika na machafuko haya kutambua kuwa athari inayotokana na machafuko haya ni kubwa na inaathiri wananchi wengi.

  Viongozi hao walisema, nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu zinahitaji utulivu na kwamba mgogoro wa uvunjaji amani katika Kongo DRC unaotokana na kuwepo kwa kikundi cha M23, lazima upewe tiba ya kudumu ili eneo hilo libakie tulivu na watu wake waweze kupata fursa ya utulivu utakjaowasaidia kushiriki katika kazi zao za kila siku.

  Akifunga mkutano huo kwa niaba ya Mwenyekiti Yoweri Museveni, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema ni wakati sasa nchi za Maziwa Makuu kutambua na kuazimia kwa kauli moja kuwa amani inahitajika katika nchi zote za ukanda huu. Akifafanua zaidi Mheshimiwa Rais Kenyatta alisema wananchi wa ukanda huu wanataka ajira na sio mapigano.

  “Hata vijana wanaotumika katika mapigano, tukumbuke kuwa baada ya mapigano watakachohitaji ni ajira. Akina mama na watoto wanataka kuona maisha yao yanaboreshwa na sio vionginevyo. Kwa namna nilivyoona tukishiriki katika mkutano huu ni dhaihiri tumeonesha nia ya dhati ya kuhakikisha maeneo yetu yanakuwa na amani. Tudumishe nia hii nzuri,” alisema Rais Kenyatta.

  Makamu wa Rais na msafara wake wanarejea nyumbani leo Alhamisi Agosti Mosi, 2013 tayari kuendelea na majukumu mengine ya kitaifa.

  Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
  Nairobi, Kenya
  Agosti 01, 2013

  0 0

  IMG_1445
  Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Stella Vuzo akielezea jukumu lao kubwa wao kama Unic ni kuelimisha jamii ambapo kwa kufanya hivyo wamehamasika kuanzisha vilabu vya kujisomea kwa shule za msingi vitakavyowajengea watoto msingi mzuri wa kupenda kujisomea ili kufahamu mambo mengi zaidi yanayoendelea duniani katika nyanja ya Sayansi, Teknolojia na habari.
  IMG_1488
  Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha ( wa tatu kushoto) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Soma Book Café , mshiriki katika kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kujisomea mashuleni Mama Demere Kitunga ( wa nne kushoto) wakikabidhi vitabu vya kujisomea kwa walimu na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
  Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) kwa kushirkiana na Soma Book Café walihamasisha kuanzishwa kwa Klabu za Kujisomea katika shule tatu za msingi ambazo ni Hananasif, Kumbukumbu na Oysterbay ili kujenga tabia ya kujisomea kwa watoto tangu utotoni. Klabu ya Kujisomea ya Shule ya Msingi Oysterbay imezinduliwa rasmi jana tarehe 31 Julai 2013 kwa kukabidhiwa mashelfu na vitabu vilivyotolewa na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Soma Book Café pamoja na Book Aid International kupitia Maktaba Kuu ya Taifa.


  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Waziri Mkuu wa Thailand kwa maafisa waandamizi mbalimbali wa serikali wakati wa kumsindikiza mgeni huyo aliyehitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini mchana huu. Hapo akipeana mkono na Mkumbwa Ally wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa
   Akisalimiana na Dr Laurent Ndumbaro
   Akisalimiana na Dr Hamisi Mwinyimvua
   Akisalimiana na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bw. Omar Mjenga
   Akiagana na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki
   Akiagana na Kamanda wa Mkoa maalumu wa kipolisi wa Dar es salaam Suleiman Kova.PICHA NA IKULU.

  0 0


  0 0

  Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA wakiwa nje ya jingo la Makao Makuu ya Shirika la Utangazaji la Afrika ya Kusini (SABC). Kutoka kushoto ni Festo Sikagonamo (ITV), Phinias Bashaya (Mwananchi), Lilian Shirima (TBC 1), Alex Magwiza (TBC Taifa), Maxmilian Bushoke mtanzania anayeishi Johannesburg na Albano Midelo (Nipashe).
  Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya SABC Mike Arareng (kushoto) akiongea na washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA walipomtembelea ofisini kwake.
  Meneja Uhusiano wa TANAPA Pascal Shelutete akifanya mahojiano katika Studio za SABC.
  Lilian Shirima wa TBC 1 ambaye ni mshindi wa Tuzo za Habari za TANAPA akiwa katika studio za SABC.
  Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA katika picha ya pamoja ndani ya chumba cha habari cha SABC na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili Mike Arareng( wa kwanza kushoto) na mtangazaji wa SABC kutoka Kenya Christina ( wa tatu kushoto).

  0 0

   
  Familia ya marehemu Ramadhani Mwinshehe na Familia ya marehemu Kiembe binti Ndugumbi wanasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao mpendwa Bw. Sababu Ditopile Mzuzuri (pichani) kilichotokea tarehe 31/Julai/2013 katika Hospitali ya Regency,Dar es Salaam
  Msiba utakuwa nyumbani kwao mtaa wa Tunduru,Ilala,nyumba namba 5.Mazishi yatafanyika tarehe 2 Agosti,2013 baada ya swala ya Ijumaa Kinyerezi,Dar es Salaam. Habari ziwafikie ndugu,jamaa na marafiki.
  Innalillah wa Innaillahi rajjiun

  Kwa mawasaliano
  Bw. Tahadhari .S. Ditopile + 255 653 222220
  Bw. Ramadhani Ditopile     +255 712 659757

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Bi. Juliet Kairuki akitoa mada kwa wafanyabiashara kutoka nchini Thailand jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) akiwaelezea fursa mbalimbali za kiuwekezaji zilizopo hapa nchini wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Thailanda Bi. Yingluck Shinawatra aliyeambatana na ujumbe wa wafanyabiashara hapa nchini hivi karibuni.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Bi. Juliet Kairuki (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyabiashara kutoka nchini Thailand Bw. You, muda mfupi mara baada ya Rais Jaskaya Kikwete kumaliza kuzungumza na wafanyabiashara wa nchi hiyo na wale wa Tanzania, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra aliyeambatana na ujumbe wa wafanyabiashara hapa nchini hivi karibuni.

  0 0


  0 0

  Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge akipata maelezo kuhusu miradi ya maji wilayani Same kutoka kwa mhandisi wa maji wilaya ya Same Musa Msangi.
  Naibu waziri wa maji Dk Binilithi Mahenge akiangalia moja ya vilula vilivyojengwa katika kijiji cha Miombo wilayani Same.
  Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge akiongea na wananchi wa kijiji cha Miombo wilayani Same ambao hata hivyo walidai tangu uhuru hawakuwahi kumuona waziri aliyefika katika kijiji hicho.
  Mwenyekiti wa kijiji cha Mteke wilayani Same Samson Kimbuta akiongea wakati wa mkutano mdogo wa wananchi wa kijiji hicho na naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge aliyetembelea kijiji hicho.
  Diwani wa kata ya Mhezi katika kijiji cha Mteke wilayani Same Allen Mbaga kiongea wakati wa mkutano mdogo wa wananchi wa kijiji hicho na naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge aliyetembelea kijiji hicho.
  Dk Binilith Mahenge akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mteke wilayani Same wakati wa ziara yake kutembelea miradi ya maji katika wilaya hiyo. Picha na Dixon Busagaga waglobu ya jamii Moshi.

  0 0

  Klabu ya Rotary ya Jijini Dar Es Salaam leo imekabidhi rasmi wodi ya watoto wenye saratani kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Wodi hiyo imejengwa na Klabu hiyo kwa kiasi cha Shilingi Billioni 1.2 ikiwa ni gharama za ujenzi, samani, na vifaa tiba vya wodi hiyo. Wodi hiyo ni ya kwanza kwa ubora Kusini mwa Jangwa la Sahara. Tafadhali fuatilia katika picha yaliyojiri wakato wa ufunguzi
  Hii ndiyo wodi iliyojengwa na Klabu ya Rotary kwa kushirikiana na wadau wengine. Ni sakafu moja ya juu ambayo imewekwa bango.
  Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, akifuatiwa na Mgeni rasmi Dr. Jane Goodall aliyeko kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Sr. Agnes Mtawa wote kwa pamoja wakipokea ufunguo wa wodi hiyo kutoka kwa watoto wanaougua saratani.

  wageni mbalimbali wakifuatilia kwa karibu hotuba mbalimbali wakati wa ufunguzi.
  Wageni wakitembelea wodi kuona ilivyojengwa.

  0 0
  0 0

  HABARI NZURI KWA WALE WATEJA WETU VIBONGE aka PLUS SIZE NI KWAMBA MZIGO UMESHAFIKA DUKANI. 
  KWA WALE KAKA ZETU MNAO TAKA RABA ZA MTOKO ORIGINAL CONVERSE, TOMS NA VANS PIA ZINAPATIKANA. 
  WALE WA SIZE NDOGO PIA KUNA NGUO NZURI SANA ZINAPATIKANA.
  WAZAZI WAPENDEZESHE PIA WATOTO WAKO NA ZuRii KIDS COLLECTION.
  KARIBUNI MJIPATIE VITU VYA SIKUKUU, MAKAZINI, MITOKO NA KANISANI. 
  NGUO NZURI, QUALITY NZURI NA BEI NAFUU. 
  LOOK GOOD, FEEL GOOD WITH ZuRii FASHION & BEAUTY BOUTIQUE. 
  TUNAPATIKANA SIZA LEGHO, NYUMA YA ROMBO GREEN VIEW HOTEL (KUNA KIBAO BARABARNAI PIA). TUPIGIE +255659189769 or WHATSAPP +447404332910 (BUSINESS ONLY). 
  NGUO ZA PLUS SIZE ZINAZOPATIKANA NI SIZE 14-20 (UK).  NA SIZE NDOGO NI 8-14 (UK).
  KARIBUNI SANA.

   
   

   

   

  0 0

  Salam Kaka Michuzi na Watanzania wote
   Naomba niwekee hizi picha nne za Watanzania wawili waliojeruhiwa vibaya na kikundi cha watu wapatao 20 hadi sasa haijajulikana ni akina nani kama ni Waalbania au Ni vishoka wengine au Wagiriki. Tukio limetokea jana usiku wakati walipopita karibu na watu hao waliowajeruhi ambao wanasema walikuwa wamevunja gari za watu kuiba sasa inaonekana kuwa walifikiria wataita polisi ndipo walipowavamia
   Ahsante - Mdau Ugiriki


  0 0
 • 08/01/13--12:36: mambo ya gado


 • 0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais SMZ Fedha, Mipango na Uchumi Mh. Omar Yusuf Mzee  hapo tarehe 29/7/13 alifanya ziara ya kikazi nchini Oman.

  Wakati ya ziara hiyo Mh. Waziri Omar Yusuf Mzee(wa kwanza kushoto) alikutana na kufanya mazungumzo na Mh Yusuf bin Alawi bin Abdulla, Waziri anaeshughulika na Mambo ya Nje wa Oman(wa pili kushoto) huko nyumbani kwa mwenyeji wake katika mji wa Salalah katika Mkoa wa Dhofar kusini mwa Oman.

  Mazungumzo hayo ambayo yaliyofuatiwa na karama ya Iftar, yaliyohusu masuala ya ushirikiano kati ya Zanzibar na Oman pia yalihudhuriwa na Balozi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania nchini Oman, Mh. Ali Ahmed Saleh(wa kwanza kulia) "

  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na madiwani wa CCM na Wajumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Buhigwe.
   Madiwani na Wajumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Buhigwe waliohdhuria kikao kilichoongozwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
   Katibu wa NEC Itikadi  na Uenezi Nape Nnauye akivishwa skafu alipowasili katika ofisi za CCM wilaya ya Kibondo.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni katika za ofisi za CCM wilaya ya Kibondo sanjali na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk.Amani Kaborou.
   Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wilaya ya Kibondo wakiwa wamefurika katika ofisi za wilaya ya Kibondo kumsalimia Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati mkutano na madiwani na wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya Kibondo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Aisha Omari (kushoto) Mama wa watoto wawili waanga wa mlipuko wa Bomu la Arusha, Sharifa Jumane (9) na Fatuma Jumanne (8) waliolazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Mama huyo alifika kuzungumza na Makamu akiwa jijini Nairobi leo asubuhi, Agosti 1, 2013 kuelezea hali ya watoto, ambapo pia alitoa shukrani zake kwa Serikali inayoendelea kuwahudumia watoto hao. Katikati ni Balozi wa Tanzania, nchini Kenya, Batrida Buriani.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Aisha Omari, Mama wa watoto wawili waanga wa mlipuko wa Bomu la Arusha, Sharifa Jumane (9) na Fatuma Jumanne (8) waliolazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Mama huyo alifika kuzungumza na Makamu akiwa jijini Nairobi leo asubuhi, Agosti 1, 2013 kuelezea hali ya watoto, ambapo pia alitoa shukrani zake kwa Serikali inayoendelea kuwahudumia watoto hao. 

  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu na Mshauri Mwelekezi katika Mradi wa Utengenezaji Kofia Ngumu katika Gereza Kuu la Ukonga, Bw. Alpherio Nchimbi(kushoto)akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo na Mifugo, Eng. Christopher Chiza(kulia)namna Kofia hizo zilivyo na ubora alipotembelea Banda la Magereza leo Agosti 01,2013(wa tatu toka kulia) ni Kamishna wa Magereza anayeongoza Divisheni ya Urekebishaji, Deonice Chamulesile. Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.
  Waziri wa Kilimo na Mifugo, Mhe. Eng. Christopher Chiza akiangalia Kiatu cha ngozi kilichotengenezwa katika Kiwanda cha Magereza kilichopo Gereza Karanga, Moshi leo Agosti 01, alipotembelea Banda la Magereza katika Viwanja vya Nzuguni, Mkoani Dodoma
  0 0
 • 08/01/13--15:08: --none--


older | 1 | .... | 212 | 213 | (Page 214) | 215 | 216 | .... | 3272 | newer