Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 211 | 212 | (Page 213) | 214 | 215 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Davis Mosha "The CEO", Deo Temba "Mayor wa LA" na milionea Jimmie Maggette wakiwa katika Supper Club Hollywood jana usiku kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa tajiri Jimmie ambaye ni mdogo wa mcheza basketball maarufu na tajiri Corey Maggette. MC wa party alikuwa mwanamuziki maarufu J Cole. Wamarekani weusi wanajisikia proud sana wanapokutana na successful people kutoka Afrika.

  The CEO Davis Mosha, D. Temba, Jimmie Maggettte na Alex King

   Deo Temba "Mayor wa L.A." katikati ni Mlinzi (BodyGuard) wa Davis Mosha " The CEO"

  Baada ya The CEO Davis Mosha kukubali mwaliko wa Jimmie Maggette alitumiwa mlinzi maalum (Body Guard) wa kumlinda, maana sehemu hiyo hawaendi watu wa kawaida, lazima uwe na mlinzi. Hapa Boss Mosha akiteta jambo na Body Guard wake.

     Mayor wa L.A. Deo Temba akikaribishwa kwenye gari na Boss Mosha

  Ricardo Emmanuel Brown Rapper maarufu na aliyewahi kuwa Excutive Vice President wa Death Row records, jina la kisanii  Kurupt aka Kurupt tha Kingpin, aka Kurupt young Gotti au Young Gostra, ni member wa kundi kali la hip-hop la Tha Dogg Pound na HRSMN akiwa na The CEO Davis Mosha katika birthday party ya Jimmie Maggette Super Club, Hollywood Los Angeles.


    Deo Temba "L.A Mayor," Davis Mosha" The CEO" na Comedian Maarufu Funny Man Red Grant

  Alex King na tajiri na mmiliki wa Kiota maarufu cha R n B LIVe Hollywood. L.A.

   Bathroom ina kila aina ya perfumes, zote expensive ukiingia lazima utoke na unyunyu mpya na pipi za bei ghali.

   Alex king akiwa na Bodyguard wa Davis Mosha Super club L.A.
  PICHA ZOTE NA SWAHILI TV 
  kwa picha zaidi tembelea www.swahilitv.blogspot.com


  0 0

  http://mvuto.com/ ni Mtandao (social network) mpya na wa kipekee wenye lengo la kuwauunganisha watanzania wote waliopo nje na ndani ya Tanzania. Sifa na malengo yake ni kama yale ya facebook, tofauti ni kwamaba Mvuto umelenga kuunganisha watu wa jamii moja zaidi.
  Tunaamini kwamba tukiwa pamoja ni rahisi kutatua matatizo ya kijamii na kiuchumi tuliyonayo. 
  Kujiunga ni bure na karibu sana.
  Tunatanguliza shukrani zetu za 
  dhati kwa ushirikiano wako
  Wadau Finland

  0 0

  Na Enock Nyanda 
  Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe Sofia Mjema amesema manispaa ya Temeke inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na uhaba wa  vitendea kazi vya kuhakikisha hali ya usafi inaimalika katika wilaya hiyo.
   Mhe Mjema pia ameeleza kwamba Manispaa ya Temeke ni moja kati ya manispaa ambazo zipo mbele kabisa katika ukusanyaji wa mapato, ambapo ni wilaya pekee hapa Tanzania ambayo inakusanya kodi kwa wingi na kwa wakati muuafaka kutoka kwa walipa kodi wake. 
   Amesema swala la ukusanyaji wa taka ngumu limepewa kipaumbele hasa ukizingatia manispaa hiyo inazalisha ujazo wa tani 138,000 (elfu moja na therasini na nane elfu) kwa siku. 
  "Tunaponunua vifaa kama hivi sasa tunahitaji kununua tena vfaa vingine ambavyo vitakuwa na uwezo wa kutenganisha takataka za chupa,taka ngumu na zile za karatasi. 
  "Mkakati wa halmashauri ni kuongeza magari mengi zaidi ili kuweza kuendana na kasi ya kuwahudumia wananchi wake kwa kuhakikisha kwamba takataka zote zinazolewa kwa muda muafaka na haziachwi zikazagaa", alisisitiza Mhe. Mjema.
  Naye Kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw. Photidas Kagimbo akitoa ripoti ya maendeleo ya usafi kwa mkuu wa wilaya alisema, halmashauri ya manispaa ya Temeke imeamua kununua magari matatu kuongeza ufanisi katika swala zima la ukusanyaji wa taka. 
  Amesema Magari hayo yana thamani ya tsh.324 millioni ambayo yataongeza uvushaji wa taka ngumu kutoka 48% ambayo ni sawa na tani 455 kwa siku na kufikia 56% ambazo ni sawa na tani 515 kwa siku. 
   Ili kufanikisha zoezi hili manispaa pia imenunua magari mengine madogo yenye thamani ya tsh 102 millioni kwa ajili ya shughuri za usimamizi wa usafi,afya na mazingira hiyo yote ni katika kutekeleza maagizo ya mkuu wa mkoa wa dare s salaam ambaye aliwataka viongozi kushirikiana na watendaji wa kata na mtaa katika kuhakikisha wanaweka mazingira ya jiji kuwa safi.
  Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Photidas kagimbo akitoa ripoti ya maendeleo ya usafi kwa mkuu wa wilaya Bi Sophia Mjema (kati) kulia ni Meya wa manispaa ya temeke mhe. Maabad Suleimani Hoja
  Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe.Sophia Mjema akikata utepe kuzindua rasmi magari madogo mawili ambayo yamenunuliwa sambamba na magari ya kuondoshea taka ngumu katika manispaa ya Temeke
  Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Sophia mjema akizindua rasmi moja ya magari yaliyonunuliwa na manispaa ya temeke kwa shughuli ya uondoshashi wa taka,uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya manispaa ya temeke
  Mkuu wa wilaya ya Temke Mhe Sophia Mjema akisisitiza jambo wakati wa kuzindua magari ya uondoshaji taka katika manispaa ya Temeke


  0 0
 • 07/31/13--12:24: Article 17


 • 0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawa Mhe. Pindi Hazara Chana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. William Ngeleja wakiendesha kikao cha kupokea maoni ya wadau mbalimbali kuhusu muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba sura ya 83(2012) katika Ofisi ya Bunge, Dar es Salaam, leo.
  Wajumbe na wadau kutoka Asasi mbalimbali (zikiwemo WLAC, TAWLA, LHRC, TANLAP, TUCTA na TLS) waliohudhuria kikao hicho.
  Mhe. Tundu Lisu, Mjumbe wa Kamati akitoa ufafanuzi wa vifungu vya sharia.
  Mwanasheria wa Mtandao wa Utoaji wa Msaada wa Kisheria Bi. Sarah Mkenda (TANLAP) akiwasilisha mapendekezo ya Asasi yake.
  Mjumbe wa Kamati Mhe. Nyambali Nyangwini akichangia wakati wa mjadala na wadau.
  Mjumbe kutoka The Tanganyika Law Society (TLS) akiwasilisha mapendekezo ya Asasi hiyo.Picha na Prosper Minja - Bunge.

  0 0

  Three lectures on art history
  16.30-18.30
  For Nafasi Visual Artists and interested visual artists
  Elvira van Eijl, renowned art Historian and Curator will host three (visual) lectures about contemporary art history at Nafasi Art Space. The lectures are open to all Nafasi members and interested visual artists

  Lecture 1: The influence of African Art on the development of Western Modern Art - Date: 7 August 2013

  Lecture 2: International Contemporary Art with a focus on African Art part I with, among others: What is happening in the international visual art world What is happening in contemorary African Art world - Date: 12 August 2013 

  Lecture 3: International Contemporary Art with a focus on African Art part II with, among other topics How does Applied and Fine arts come together
  - Date: 13 August 2013

  These lectures are open to all Nafasi members and interested visual artists, and other people who are interested in the arts. Please share the lectures info with your artists friends. Especially for Nafasi members, Elvira, will hold in the week from 6-13 August one on one meetings to discuss individual portfolios, she can help with writing, advising and editing of art statements, CV's, portfolio pictures etc.
  If you are interested in the one-on-one support, please reply to this message and we can set up time and date

  About Elvira Van Eijl
  Elvira van Eijl was born in Enschede Netherlands. Her parents were both sculptors. She studied history of art in Amsterdam. She worked for 25 years in ArtEZ Academy of Fine Art and Design in Enschede, 15 years in a gallery of modern art in Amsterdam and owned her own gallery for 13 years in Enschede. Next to that she is the director of an antiquarian art bookstore in Amsterdam and Enschede. 
  Elvira gives lectures about modern and contemporary art in Holland and Germany, writes articles for catalogues and makes speeches for openings of exhibitions. She is a member of many cultural advisory committees (of the province / city) and the founder and organizer of AKI Festival (7 editions) a one-week cultural event in the city center of Enschede. She organizes interventions and interactions between artists and the public. She has been a curator of exhibitions in Holland and Poland (recently Poznan) and is the founder and curator of the Art Brut Biennale Holland

  0 0

  Balozi wa Uingereza hapa nchini Bibi Dianna Melrose akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa International Inspiration awamu ya pili leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga.Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetiliana saini ya makubaliano na Serikali ya Uingereza katika utekelezaji wa mradi huo.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga na Balozi wa Uingereza hapa nchini Bibi Dianna Melrose kushoto wakiweka saini kwenye mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa International Inspiration leo jijini Dar es Salaam.Mradi huu unatekelezwa hapa nchini kwa ushirikia.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga na Balozi wa Uingereza hapa nchini Bibi Dianna Melrose kushoto wakionesha kwa waandishi wa habari hati za makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa International Inspiration baada ya kumaliza zoezi la utiaji wa saini leo jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga akiwa na baadhi ya wawakilishi wa wanafunzi wanaonufaika na mradi wa International Inspiration wakimskiliza Balozi wa Uingereza hapa nchini Bibi Dianna Melrose kushoto alipokuwa akifafanua jambo baada ya kumaliza hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa mradi huu leo jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija.

  0 0

   Waziri Mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra akiteremka kwenye ndege katika Uwanja wa Ndege wa Seronera, Serengeti, leo na kulakiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
   Waziri Mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
   Waziri Mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra akisalimiana na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti William Mwakilema mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
   Waziri Mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra akisindikizwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki (kushoto) na Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu (kulia) mara baada ya kuwasili Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

  0 0

  Waziri wa Fedha, , Dk. William Mgimwa amenukuliwa kwenye magazeti ya HNIPASHE na HabariLeo matoleo ya leo akisema kuwa Serikali sasa imekubali kuwa kodi mpya ya laini ya simu ni mgogoro na hivyo inakusudia kurejesha muswada wa sheria ulioazisha kodi hiyo wenye mkutano wa Bunge mwishoni mwa mwezi wa Agosti kwa mjadala zaidi na ufumbuzi kutoka kwa Wabunge.

  Wiki iliyopita Rais Jakaya Kikwete alikutana na Wizara hiyo, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wajumbe wa MOAT (Chama cha Wamiliki wa Kampuni za Simu -  TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel)  Ikulu kusikia pamoja na mambo mengine, kuondolewa kwa kodi ya simu kutakavyokwaza maendeleao ya sekta ya mawasiliano na kuwataka MOAT kutoa mapendekezo ya jinsi serikali itapata kiasi cha Sh. bilioni 178 zilizopangwa kupatikana katika bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2013/14 kutokana na kodi ya simu.

  Kodi hizo za Shilingi 1,000 kwa mwezi ambazo Waziri Dk Mgimwa akiwasilisha makaridio ya mapato na matumzi kwa Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2013/14 Bungeni mwezi Juni tarehe 13, mwaka hu, alisema:

  1. Zilianza kutozwa na serikali mwanzoni mwa Julai, mwaka huu hivyo kuwalazimu wamiliki wa simu nchini kuingia gharama zaidi kwa asilimia 14.5 ili kuongeza mapato. 

  2. Serikali inakusudia kutoza ushuru kwenye huduma zote za simu za mkononi, kama chanzo kipya cha mapato ya  badala ya muda wa maongezi peke yake.

  3. Asilimia 2.5 ya mapato ya kodi hiyo yatatumika kugharimia elimu nchini kwa kuzingatia mapendekezo ya Kamati Maalumu ya Spika ya Kushauri kuhusu mapato na matumizi ya Serikali.

  4. Inaanzishwa kodi ya zuio ya asilimia 10 ya kamisheni ya usafirishaji wa fedha kwa njia ya simu za mkononi ambazo zitakusanywa na kampuni za simu kutoka kwa Wakala wanaotoa huduma hizo kupitia simu za mkononi.

  5. Mapendekezo hayo ni utekelezaji wa ushauri wa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), itafute vyanzo vipya vya kodi ili kuongeza mapato ya Serikali. 

  0 0

  JUMLA ya warembo 15 kutoka katika vitongoji vinne vya wilaya ya Ilala, wameanza mazoezi ya kujiandaa na kumsaka mrembo wa wilaya ya Ilala ‘Redd’s Miss Ilala 2013’ yanayofanyika katika ukumbi wa klabu Billicanas uliopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

  Shindano hilo litafanyika katika ukumbi wa Golden Jubilee Tower tarehe 16 Agosti mwaka huu, kati ya hao warembo watatu ndio wanaowania nafasi ya kushiriki shindano la Redds Miss Tanzania, shindano linalotarajia kufanyika baadae mwezi Septemba.

  Warembo hao ambao wanatoka katika vitongoji vya Mzizima, Tabata, Ukonga na Dar City Centre wamekuwa wakijifua na kufanya onesho hilo kuwa la kuvutia zaidi, tofauti na miaka iliyopita.

  Maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri na wamepania kuonesha vipaji vyao kwa kufanya shindano la kuoesha vipaji ambalo linatarajiwa kufanyika wiki ijayo.

  Sisi kama kamati tunaowaomba wadau wa urembo kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia muonekano mpya wa mashindano ya urembo, lakini pia kuangalia jinsi Ilala ilivyosheheni warembo watakaoleta ushindani mkubwa Redds Miss Tanzania 2013.

  Warembo waliopo katika kambi ya Miss Ilala ni pamoja na Alice Isaac, Clara Poul,Anna Johnson,Iren Mwelolo, Munira Mabrouk,Rehema Mpanda, Shamim Mohamed, Martha Gewe, Diana Joackim, Natasha Mohamed, Dorice Mollel, Pendo Lema, Kazumbe Mussa na Kabula Kibogoti.

  Hadi sasa kampuni zilizojitokeza kudhamini ni Redd’s, Dodoma wine,CXC Tours,Chilly Will,Tanzania Daima,Jambo Leo,Clouds FM,Tanzania Daima,City Lounge na Times FM.

  0 0


  Brothers and sisters asalaam aleikum! 
  Ramadhan is running fast, please join us to our last community iftar 
  at Al Baqi Islamic Center 
  148 Fort Pleasant Avenue, Springfield, 
  Mass 01108
   on
   Saturday August 3rd 2013 from 8pm-11pm. 
  Please pass this message to others. 
  Shukran! 
  Ramadhan kareem.

  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye  akifuturu pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk.Amani Kaborou,Katibu wa CCM Mkoa wa Kigoma Mohamed Nyawenga na Mbunge wa Manyovu Albert Obama.
   Baadhi ya Mabalozi wa nyumba kumi na wakazi wa Kigoma mjini wakifuturu leo 31Julai 2013 katika ofisi za CCM wilaya ya Kigoma Mjini.
   Baadhi ya Mabalozi na wakazi wa Kigoma mjini wakipata futari
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza machache baada ya kufuturu na Mabalozi wa nyumba 10 ambapo alisisitiza Watanzania kutunza amani waliokuwa nayo.
   Sheikh Mustafa Halfan Kiumbe akisema maneno machache kabla ya kumkaribisha Sheikh Mkuu wa Kigoma
   Katibu wa NEC itikadi na Uenezi akishiriki dua iliyoongozwa na Sheikh Hassan Idd Kiburwa leo baada ya kufuturu na mabalozi wa nyumba 10 wa Kigoma mjini.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya mabalozi wa nyumba 10 kutoka Kigoma mjini ambao alifuturu nao pamoja.
  Wajumbe wa kamati ya utekelezaji kutoka wilaya ya Kigoma mjini wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kufturu .

  0 0

   Na Mwandishi Maalum
  Wakati watanzania wakiwa  bado hawajawasahau mashujaa wao Saba waliopoteza maisha wakati wakitekeleza jukumu la  ulinzi wa  Amani ya kimataifa katika jimbo la Darfur, nchini Sudan,   Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, limetoa wito kwa walinzi wa Amani kudhibiti  mashambulizi yanayoelekezwa dhidi yao.

  Wito huo wa Baraza Kuu la Usalama  umo ndani ya  Aya  zipatazo 30 za Azimio namba 2113 la mwaka 2013 ambalo limeongeza  muda wa   Mamlaka (   Mandate)  ya  Misheni ya Mseto ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika inayolinda Amani katika  Jimbo la Darfur maarufu kama    UNAMID.


  Katika kikao chake kilichofanyika siku ya  jumanne,  wajumbe 15 wanaounda  Baraza  Kuu la Usalama  walipitisha kwa kauli moja  Azimio hilo linaloongeza mamlaka ya UNAMID kwa  miezi 13 hadi  Agosti 31, 2014.

  Miongoni mwa  Aya hizo 30 zipo aya zinazoelezea  kwamba ingawa kumekuwa na hali ya utulivu tangu  Misheni ya UNAMID ilipopelekwa   Darfur lakini pia  limeeleza kusikitishwa  kwake na uwepo wa matukio ambayo yanaelekea kudhoofisha hali ya amani na usalama na vile vile  kuvuruga shughuli za ulinzi wa amani na upelekaji wa misaada ya kibinadamu  kwa wananchi wanaokubwa na machafuko hayo.

   Baraza  Kuu kupitia Azimio hilo  pamoja na mambo mengine limelaani  vikali matukio ya kushambuliwa kwa  walinda Amani wa UNAMID,  likiwamo tukio la hivi karibuni    la Julai 13,  ambapo walinda amani   saba walipoteza maisha na wengine 14 akiwamo polisi kujeruhiwa katika shambulio la kushitukiza.

   Azimio hilo pia limesititiza   mamlaka ya    UNAMID ambayo  yapo  ndani ya  Sura ya    VII ya Katiba ya Umoja wa Mataifa, na kutoa wito kwa walinzi hao wa amani  kuzuia  vitisho vyovyote dhidi yao ikiwa  ni pamoja na kuwalinda wananchi  walio hatarini  bila kuathiri wajibuwa wa serikali wa kuwalinda  wananchi wake.  

  Aidha  Baraza Kuu limesisitiza kupitia Azimio hilo   haja na umuhimu  kwa walinzi wa Amani  wa siyo tu kuwa tayari kukabili vitisho dhidi yao, bali limevitaka vyombo vinavyohusika kuhakikisha kuwa walinzi hao wanapewa zana na vifaa vitakavyowawezesha  kutekeleza mamlaka waliyopewa.

  Vile vile kupitia Azimio hilo Baraza  limerejea tena wito wake wa kutaka uchunguzi wa kina ufanyike kuhusu tukio la Julai 13, na kwamba  ni matumaini yake kuwa  serikali ya Sudan itashiri kikamilifu kama ambavyo imekwisha kuahidi. Na aidha   Baraza limeyataka  makundi mengine kutoa ushirikiano   huku likisisitiza kwamba hujuma dhidi ya walinzi wa amani ni jambo ambalo halikubaliki

  Katika muktadha huo, na kupitia Azimio hilo, Baraza Kuu la usalama limezitaka pande  husika na  hasa  makundi  yenye    silaha na ambayo hayajatia saini  Nyaraka za   Doha kuhusu amani  ya Darfur , kuacha mara moja  vitendo vyovyote  vinavyolenga kuvuruga Amani na  kukomesha unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu, mauaji holela.

  Vile vile na  makundi hayo yametakiwa  kushiriki bila ya kuchelewa na bila masharti katika  mazungumzo ya kuteta Amani.

  Aidha  Azimio hilo linamtaka  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika kuendelea  kupitia utekelezaji wa Mamlaka ya UNAMID  ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa  Baraza hilo kila baada ya siku tisini.

  Kupitia Azimio  hilo  Baraza  Kuu limezishukuru  nchi zote ambazo zimetoa wanajeshi wake na polisi kushiriki katika operesheni ya kulinda amani  kupitia UNAMID na limeyaomba  mataifa mengine kuendelea kuchangia kwa hali na mali ili hatimaye  UNAMID iweze kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu na kufanya Darfur kuwa mahali salama.

  Wakati huo huo  akizungumza baada ya  Azimio hilo kupitishwa,   Muwakilishi wa  Jamhuri ya Sudan katika Umoja wa Mataifa, Bw. Daffa-Alla-Elhag Ali Osman, amelihakikishia Baraza  Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwamba serikali yake itashiriki kikamilifu katika kuwasaka  wale wote waliohusika na tukio la  Julai 13.  0 0

  The International African Festival Tübingen 2013 will take place in Tübingen, Germany from 8th to 11th August.

  It will feature Africa’s top bands including Ngoma Africa Band - a German based Tanzanian band, Susubilibi – a West African band, Osumare Band from Nigeria, Richard Amougou from Cameroon and Wamali Percussions from Senegal. David Presna from Haiti will also perform.

  The festival will also feature a huge market with more than 70 traders selling beautiful African artefacts, children’s programs, exotic African culinary and Gospel music.


  Ms. Susan Muyang Tatah, CEO of the International African Festival Tübingen

  Business and social forums will provide guests with information on business opportunities in Africa.

  At least 10 African Ambassadors in Germany have confirmed their participation at the festival together with dignitaries from the city of Tübingen.

  For more information about the International African Festival Tübingen 2013, please visit:www.afrikafestival.net  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa rasmi kwenye mkutano wa "High Level Group" na Dr. Sheila Tlou, Mkurugenzi wa UNAIDS Regional Support Team kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika katika siku ya pili ya mkutano huo unaofanyika jijini Gaberone nchini Botswana tarehe 31.7.2013.
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akifunga rasmi mkutano wa High Level Group uliokuwa unafanyika kwenye hoteli ya Lasmore nchini Botswana tarehe 31.7.2013.
  Baadhi ya wajumbe wa mkutano wakisoma jarida linalochapishwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, huku wakiendelea na mkutano.  

  0 0
 • 07/31/13--21:17: --none--


 • 0 0
 • 07/31/13--22:35: Article 4
 • Kampuni ya Glitz Entertainment imeandaa Toto Party kwa ajili ya watoto wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake linayotarajiwa kufanyika katika Art Gallery iliyopo Mbezi Beach siku ya Iddi Mosi.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam muandaaji wa tamasha hilo, Deniss Ssebo alisema kuwa hii ni mara ya nne kuandaa TOTO PARTY kwa ajili ya watoto, na wanatarajia kuanza kulipeleka na mikoani.
  Katika Tamasha hilo, watoto watapata nafasi ya kushiriki katika michezo mbalimbali kama soka, kuogelea, kusaka hazina (Treasure hunt) na kujipaka rangi usoni (Face painting) na mengine mengi.
  Aidha watoto hao pia wataweza kukutana na wenzao wanaoishi katika mazingira magumu.
  Mbali na watoto kucheza na kufurahi michezo mbalimbali pia wazazi wao watachuana katika mchezo wa kuvuta kamba ambapo washindi katika michezo hiyo watazawadiwa zawadi mbalimbali na viingilio ni Sh 3,000 kwa watoto na wakubwa Sh 7,000.

  0 0

    Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Bw. Hassani Mkivanga (aliyesimama) akiwasilisha maoni kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba mbele ya Wajumbe wa Tume hiyo kutoka kulia Bi. Kibibi Hassan, Joseph Butiku   na Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume, Bw. Mubarak Saleh. Mkutano huo ulifanyika jana Jumatano (Julai 31, 2013) katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Green Bird kilichopo Wilayani humo. 

    Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Joseph Butiku akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro (hawapo pichani) wakati wa kufunga mkutano wa Baraza hilo jana Jumatano (Julai 31, 2013) katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Green Bird kilichopo Wilayani humo. Kulia ni Mjumbe wa Tume hiyo, Bi. Kibibi Mwinyi Hassan.

   Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Bi. Christina Kasaga akichangia hoja wakati wa mkutano wa kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika  mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Green Bird kilichopo Wilayani humo jana Jumatano (Julai 31, 2013).

  1.       Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya yua Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Bw. Thomas Edward akichangia akichangia hoja wakati wa mkutano wa kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika  mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Green Bird kilichopo Wilayani humo jana Jumatano (Julai 31, 2013).

  1.       Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Bw. Hamza Mwanga akiwasilisha maoni ya wajumbe wa kundi lake kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika  mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Green Bird kilichopo Wilayani humo jana Jumatano (Julai 31, 2013). Picha na Tume ya Katiba

  0 0

   Mkazi wa Makumbusho Isabela Edwad Msemo akipokea funguo ya Bajaji akiwa mwenye furaha kutoka kwa Meneja Chapa wa Tigo, Wiliam Mpinga  mara baada ya kujishindia  kupitia Promosheni ya Miliki Biashara yako na Tigo ambapo washindi wa wiki ya pili  wamekabidhiwa zawadi zao jana Jijini Dar es Salaam. 
    Evelyn Elisalia Massawe-(22) Mkazi wa Kimara akipokea funguo za Bajaji mpya aliyojishindia kupitia Promosheni ya Miliki Biashara yako na tTgo kutoka kwa Meneja Chapa wa Tigo Wiliam Mpinga ambapo washindi wa wiki ya pili ya Promotion hiyo wamekabidhiwa zawadi  zao jana Jijini Dar es Salaam.
   Evelyn Elisalia Massawe-(22) Mkazi wa Kimara akishuka ndani ya bajaji yake aliyokabidhiwa na Tigo  baada ya kujishindia kupitia Promosheni ya Miliki Biashara yako na Tigo, kushoto ni  Meneja Chapa wa Tigo Wiliam Mpinga.

   Mkazi wa Mabibo Khalid Jafari Gomani akikagua Bajaji  mpya aliyojishindia kupitia Promosheni ya Miliki Biashara yako na Tigo ambapo washindi wa wiki ya pili ya wamekabidhiwa zawadi zao jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo Wiliam Mpinga.

  0 0
 • 07/31/13--23:54: KUMBUKUMBU
 • Joseph Mturi Mahemba 1955-2012

  Hatimaye siku, Miezi imepita hadi hii leo ambapo imetimia Mwaka mmoja(1) tangu ulipofariki usiku ule wa siku ya jumatano ya tarehe moja ya Mwezi Agosti ,2012. Japokuwa haupo nasi hapa duniani lakini tupo nawe kiroho kwa kuendeleza mema yote uliyotufundisha na kutuasa.

  Tunakukumbuka kwa Upole, Upendo, Busara na Ukarimu uliokuwa nao kwa familia na Marafiki.

  Daima unakumbukwa sana na Mkeo Rose Joseph, dada zako Theresia, Karaghita, Wankuru na Mnaga, wanao wapendwa Michael, Mkami, Niwa, Sagana, Mary, Geofrey, Nyakaho, Lecardia na Pricilla, na wajukuu zako wote .

  Ibada Maalum ya Maombi itafanyika tarehe 04/08/2013 Saa 2.00 asubuhi kwenye kanisa katoliki la Mt Maurus Kurasini, Dar es Salaam. 

  Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake libalikiwe.

older | 1 | .... | 211 | 212 | (Page 213) | 214 | 215 | .... | 3272 | newer