Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 213 | 214 | (Page 215) | 216 | 217 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Vazi NI DUKA LA NGUO, VIATU, VIPODOZI, NA FASHION ACCESSORIES.


  FIKA dukani  Vazi Ujipatie  mavazi  ya watoto yenye ubora wa uhakika  kutoka  Ulaya na marekani kwa bei za kawaida.

  Mavazi hayo ni kama vile; Suruali na kaptula Kali za Kadet, Mashati, Tshits, magauni  Sketi na blouse.

  Zaidi ya Nguo za Watoto!
  Dukani Vazi Utajipatia Vitu mbali mbali kama vile

  Make up za Sleek; Viatu; Tops na Blouse, Body Splash  na Lotions za Victoria’s Secret

  pamoja na

   vipodozi vya aina Mbalimbali


  KUONA BIDHAA MBALI MBALI ZINAZOPATIKANA VAZI na Maelekezo Kufika Dukani TEMBELEA blog WWW.vazitz.blogspot.com

  KUMBUKA! Vazi utapata bidhaa Zenye Ubora wa Uhakika kwa bei za Kawaida.

   DUKA LA Vazilipo barabara ya Mwai Kibaki   KATIKATI YA SHOPPERS PLAZA NA ZANTEL MAKAO MAKUU, DUKA LINATAZAMANA NA GHOROFA LA NHC, LILILOPO PEMBENI YA INTERNATIONAL COMMERCIAL BANK

  Kwa Mawasiliano piga 


  0658 286 555


  0 0
 • 08/01/13--15:15: --none--
 • Welcome to the screening of “PAN’S LABYRINTH," this coming Tuesday August 6th Slipway at the Slipway Cinema Studio, 7.30 pm.

  5000 TZS for one day membership. 
  Movie ticket and voucher will enable you to get a FREE drink from the Waterfront!

   A FILM by GUILLERMO DEL TORO.........
  In the fascist Spain of 1944, the bookish young stepdaughter of a sadistic army officer escapes into an eerie but captivating fantasy world.

  ‘‘So breathtaking in its artistic ambition, so technically accomplished,so morally expansive,so fully realized that it defies the usual critical blather.’’

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taassisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye (kushoto) akizungumza na wajumbe wa kamati maalumu ya taasisi hiyo inayoshughulikia uharakishwaji wa upatikanaji wa hati ya umiliki rasilimali ardhi na majengo (Land Title Deeds) jijini Dar es Salaam. Kulia ni afisa wa TPSF Bw. Adam Gahhu
  ------------------------------------------
  TAASISI ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), imesema kukosekana kwa umiliki wa raslimali ardhi na majengo (Land Title Deeds) miongoni mwa watanzania wengi kutarudisha nyuma uharakishwaji wa kujipatia maendeleo hapa nchini.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Bw. Godfrey Simbeye alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha kamati cha taasisi hiyo kilichokuwa kikijadili umuhimu wa kuwa na hati ya umiliki wa raslimali hiyo kuwa ni asilimia tatu tu ya watanzania mpaka sasa ndiyo wenye hati za umiliki huo.
  “Tunashindwa kupata maendeleo kutokana na kwamba hatuna hati hizi ambazo zinatumika kuombea mikopo katika taasisi za fedha,” alisema Bw.Simbeye na kuongeza kuwa raslimali isiyohamishika  ndiyo inayokubarika zaidi katika kupata mikopo.
  Alisema kikao walichofanya kilikuwa ni mwendelezo wa vikao vinavyoendelea kufanyika kwa ajili ya  kuungana  na vile vinavyofanywa na sekta ya umma katika mbinu za kutaka kurahisisha upatakanaji na kutaka kuboresha mazingira ya biashara.
  Alisema pia viwango vya Benki ya dunia vinaonyesha Tanzania ipo nyuma sana, hivyo kuna kila sababu ya kuhakikisha maboresho yanafanyika haraka ili kila mtu aweze kuwa na hati ya umiliki wa ardhi na majengo bila usumbufu.
  Alisem mchakato wa raslimali hizo kutakiwa kuwa na hati za umiliki ulianzishwa mwaka 2009 na ilipofika mwaka 2010 serikali ilikubali lakini utekelezaji wake umekuwa wa kiwango cha chini sana.
  “ Kwa sasa kamati yetu inajadili viwango vilivyowekwa na Benki ya Dunia na taarifa ya serikali ya utekelezaji wa mpango kazi wa maboresho ya mazingira ya biashara na uwekezaji (ROADMAP) katika kipindi cha robo mwaka ya tatu na nne ya mwaka wa fedha 2012/13,” alisema.
  Alisema pia kamati hiyo imejichimbia kujadili kwa kina vikwazo mbalimbali vilivyopo katika kutekelezaji wa makubaliano hayo ili kuja na mapendekezo ya kuisukuma serikali kuharakisha swala hilo kwa maslahi ya taifa na watu wake.
  Alifafanua kwamba sekta binafsi inahitaji kuona mtu anayetaka kuanzisha kiwanda hapa nchini anaanzisha bila ya kuchukua muda mrefu kupata umiliki wa ardhi.
  Alisisitiza kwamba serikali inahitajika kuiwezesha Wizara ya Ardhi ili iweze kuwa na uwezo mkubwa wa upimaji ardhi na utoaji vibari vya umiliki ardhi na pia kuwa na mipango ya matumizi ya ardhi endelevu.
  Alisema Millenium Challenge Corporation kutoka Marekani imetenga dola milioni 800 za kimarekani ambapo sehemu ya fedha hizo zitatumika katika maswala ya ardhi ikiwemo kupima na kutoa hati za umiliki.
  Mshauri wa, maswala ya wajasirimali TPSF, Dkt. Donath Olomi alisema mrorongo wa kuandikisha usajiri wa majengo na ardhi ni mgumu na mazingira hayo ndiyo yanarudisha nyuma maendeleo ya nchi.
  “Pia  mfumo mzima wa utoaji wa vibari kwa mtu anayetaka kufanya tathimini ya ardhi au jengo, survey ya ardhi, kubadilisha hati ya umiliki ardhi au jengo na usanifu wa majengo bado unaukiritimba mkubwa,” ambao kikosi kazi chao kitakuja na mapendekezo ya kuitaka serikali kuondoa hali hiyo.
  Alisema nchi ikifikia viwango vya kimataifa vya utoaji wa hati za umiliki ardhi na majengo na vibari mbalimbali umasikini utapungua kwa asilimia kikubwa.   0 0

  IMG_1445
  Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Stella Vuzo akielezea jukumu lao kubwa wao kama Unic ni kuelimisha jamii ambapo kwa kufanya hivyo wamehamasika kuanzisha vilabu vya kujisomea kwa shule za msingi vitakavyowajengea watoto msingi mzuri wa kupenda kujisomea ili kufahamu mambo mengi zaidi yanayoendelea duniani katika nyanja ya Sayansi, Teknolojia na habari.
  IMG_1488
  Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha ( wa tatu kushoto) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Soma Book Café , mshiriki katika kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kujisomea mashuleni Mama Demere Kitunga ( wa nne kushoto) wakikabidhi vitabu vya kujisomea kwa walimu na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
  Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) kwa kushirkiana na Soma Book Café walihamasisha kuanzishwa kwa Klabu za Kujisomea katika shule tatu za msingi ambazo ni Hananasif, Kumbukumbu na Oysterbay ili kujenga tabia ya kujisomea kwa watoto tangu utotoni. Klabu ya Kujisomea ya Shule ya Msingi Oysterbay imezinduliwa rasmi jana tarehe 31 Julai 2013 kwa kukabidhiwa mashelfu na vitabu vilivyotolewa na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Soma Book Café pamoja na Book Aid International kupitia Maktaba Kuu ya Taifa.
  IMG_1498
  Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Stella Vuzo akishiriki zoezi hilo la kukabidhi vitabu kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Oysterbay wakihamasisha wanafunzi kujenga tabia ya kujisomea tangu wakiwa wadogo.
  IMG_1494
  Afisa Habari wa UNIC Usia Nkhoma Ledama naye alishiriki zoezi hilo.
  IMG_1508
  Mwalimu Salome Makanza (kushoto) akitoa shukrani kwa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) kwa msaada huo ambapo waliahidi kuleta mabadiliko ya maendeleo kwa wanafunzi wao kujijengea tabia ya kujisomea na hata kuongeza ufaulu kwa matokeo ya darasa la saba shuleni hapo. Katikati ni Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Soma Book Café , mshiriki katika kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kujisomea mashuleni Mama Demere Kitunga.
  IMG_1398
  Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha akitoa ushauri wa namna ya upangaji vitabu kwa Msimamizi wa Maktaba ya shule hiyo Mwl. Veronica Kassidy.
  IMG_1401
  Unic team wakijikumbushia baadhi ya vitabu walivyowahi kuvisoma walipokuwa shule za msingi.
  IMG_1415
  Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay wakichagulia vitabu vya kujisomea katika maktaba ya shule yao.
  IMG_1513
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Soma Book Café , mshiriki katika kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kujisomea mashuleni Mama Demere Kitunga na Afisa Habari wa UNIC Stella Vuzo wakiteta jambo na baadhi ya wanafunzi wa shule mara baada ya kumaliza zoezi la kukabidhi vitabu wanafunzi hao.

  0 0

  Maonyesho ya 20 ya Siku ya Wakulima Tanzania (NaneNane) yameanza rasmi jana Agosti 1 katika viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.Maonyesho hayo ambayo yapo chini ya Udhamini Mkubwa wa TIB Development Bank,yanaendelea kwa kasi mpaka hapo itakapofikia kilele chake Agosti 8,2013.
  Sehemu ya Ngoma za asili zikiendelea kutumbuiza katika ugunguzi wa Maonyesho hayo ya 20 ya Siku ya Wakulima Tanzania (NaneNane) yanayoendelea kwenye viwanja Nzuguni mjini Dodoma.
  Baadhi ya Wageni na Viongozi wakifatilia Burudani hiyo ya ngoma.
  Muonekano wa Jengo la Mdhamini Mkuu wa Maonyesho hayo mwaka huu wa 2013.

  0 0

  Mkufunzi toka taasisi ya Risxcel, Sunny Ahonsi akitoa mada kuhusu Governance and Parliament kwa viongozi wa Bunge.Naibu Spika Job Ndugai (kwanza kushoto), Wenyeviti wa Bunge (Mhe Zungu na Mhe Mohamed Seif Khatib) wako Dubai katika mafunzo maalum kwao kama viongozi wa Bunge wakiongezewa uwezo katika maeneo ya Uongozi Bora, Uendeshaji wa Vikao na Mikutano na tathmini ya mifumo na uongozi wa kibunge duniani.Mafunzo hayo yanatolewa na jopo la wataalamu toka Uingereza kupitia taasisi ya Risxcel.
  Mhe Job Ndugai akitoa maelezo kwa wenzake juu 'Leadership Values', Mafunzo hayo ambayo ni ya vitendo zaidi ni sehemu ya mipango ya Ofisi ya Bunge kuongeza ujuzi kwa wabunge na viongozi wake.
  Mhe Zungu akichangia katika moja ya mijadala kwenye mafunzo hayo.
  Viongozi wa Bunge wakiwa katika mazoezi ya vitendo juu ya Uongozi.Kushoto ni Bi.Maria toka Uingereza akiendesha zoezi la 'Leading by Example. Picha na Saidi Yakubu.

  0 0

  The General Public is hereby informed that pursuant to the powers conferred upon him by section 4(1) of the Tourism Act No. 29 of 2008, the Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Sued Kagashek has appointed the following as members of the Tourism Technical Advisory Committee for a period of three years with effect from 1st July, 2013:
  1. Dr. Wineaster Anderson – Chair person (Department of Marketing, University of Dar es Salaam).
  2. Mr. Charles Dobbie ( Selou Safari)
  3. Mr. Mbaraka Islam ( Journalist)
  4. Hon. Mustafa Akunaay (Executive Secretary, Tanzania  Association of Tour Operators)
  5. Mr. Donatius M.K.Kamamba   (Director of Antiquities)
  6. Mr. Allan Kijazi (Director General Tanzania National Parks)
  7. Mr. Bruno Kawasange (Ag. Conservator,  Ngorongoro Conservation Area Authority)
  8. Mr. George Msumi (Ag. Manager, Marine Parks and reserves Unit- MPRU)
  9. Prof. Alexander Songorwa ( Director of Wildlife Management)
  10.  Ms. Latifa Sykes ( Executive  Secretary, Hotel Association of Tanzania)
  11.  Dr. Alois Nzuki ( Director General, Tanzania Tourism Board)
  12.  Mr. Richard Rugimbana (Executive  Secretary, Tourism  Confederation of        Tanzania)
  13.   Eng. T.Baya ( Director General, National Environment Management Council – (NEMC)
  14.  Mr. Bavoo Junus (Representing Attorney General)
  15.  Mr. Haji Y. Janabi (Representing  Ministry of Home Affairs)

  N. H. M. Millao
  AG. PERMANENT SECRETARY
  1st August, 2013

  0 0

  Na Mwandishi Wetu Dodoma

  MPANGO wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora umeshauri kuwa ili kuboresha mazao ya kilimo na vyema sera na mikakati inayoendelea kutekelezwa na Serikali ikalenga zaidi kuwafikia wananchi walio wengi.

  Hayo yamesemwa mjini hapa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa APRM Tanzania, Bw. Hassan Abbas alipokuwa akizungumza kuhuru matokeo ya utafiti wa APRM kuhusu masuala mbalimbali ya utawala bora nchini.

  “Ripoti ya APRM pamoja na kuangalia masuala mengine ya siasa na utawala bora pia imeangalia namna nchi yetu inavyotekeleza sera na mikakati mbalimbali ya kukuza maisha ya watanzania ikiwemo kilimo.

  “Ripoti ya APRM inayo mapendekezo yanayogusa sekta ya kilimo hususani umuhimu wa kuboreshwa sera na uwekezaji katika kilimo ili kukuza uzalishaji wa mazao lakini pia kuwawezesha wakulima kujinasua kutoka lindi la umaskini,” alisema katika Banda la Taasisi hiyo kwenye Maonesho ya Wakulima, Nane Nane yanayoendelea mjini hapa.

  Bw. Abbas alisema Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zilizopiga hatua katika kuweka mikakati ya kuboresha kilimo na akasem a Ripoti ya wataalamu wa APRM imeguswa na Mkakati wa Serikali wa Kilimo Kwanza kuwa ni hatua nzuri ya kufikia mapinduzi ya kilimo.

  Hata hivyo alionya kuwa kwa mujibu wa misingi ya utawala bora ni vyema sera na mikakati iliyopo vikatekelezwa kwa kuwshirikisha wakulima na wadau wengine ipasavyo.

  “Kwa kuwa moja ya malengo ya Mpango wa APRM Afrika nzima ni kueneza dhana ya utawala bora hasa utawala shirikishi, nasi tunatumia fursa hii ya Maonesho ya Nane Nane kusisitizia kuwa kilimo chetu kitapiga hatua iwapo wananchi watashirikishwa katika kila mikakati na pia wakipewa fursa ya kutoa mrejesho wa sera na mikakati hiyo kwa nia ya kuboresha,” alisema.

   APRM ni Mpango wa viongozi wa Afrika ulioanzishwa mwaka 2003 kwa lengo la kuhakikisha kuwa nchi za Afrika zinawashirikisha wananchi wao katika kubaini na kuzitatua changamoto za kiutawala bora.

  Bw. Abbas alisema kuwa Tanzania ilijiunga na Mpango huo mwaka 2004 na imekuwa ikitekeleza hatua za Mpango huo kiufanisi. Alisema kuwa Ripoti ya APRM inayoainisha masuala mbalimbali nchini itazinduliwa Oktoba mwaka huu.

  0 0

  Mhe.  Michael Chilufya Sata, Rais wa Zambia ameonesha kukwerwa Na Unene wa askari Polisi wa Jeshi la Zambia na kuhoji kama kweli ni wakakamavu (Physical Fitness). Aidha, amemwagiza Bibi Stella Libongani, Inspekta Jenerali wa Jeshi hilo kuhakikisha kuwa kuna ukakamavu katika jeshi hilo. Mhe Rais Sata aliyasema hayo katika Ikulu ya nchi hiyo alipokuwa anamwapisha Kamishna Malcolm Mulenga kuwa Mkuu wa Polisi wa Jimbo ya Luapula, nchini Zambia. Kazi kwa Jeshi  Letu la Tanzania.
   
   

  0 0


   Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akiwakabidhi msaada wa vyakula watoto yatima wanaolelewa katika Kituo cha Dar Alqaama Tandika katika sherehe ya kutoa misaa kwa vikundi mbalimbali vya yatima, Dar es Salaam hivi karibuni.
                                          Akiwakabidhi watoto wa Kituo cha Hiyari Chang'ombe

  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali, Said Mwema (kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uturuki, Zeki Catalakaya (katikati) wakisaini hati ya ushirikiano wa kuchunguza matukio ya uhalifu kati ya Tanzania na Uturuki. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akilishuhudia tukio hilolililofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam leo.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akiwashukuru kwa furaha ujumbe kutoka nchini Uturuki baada ya kukabidhi gari maalumu ya kuchunguza matukio ya uhalifu nchini kwa Jeshi la Polisi. Gari hilo ambalo linavifaa vyote vya kuchunguza matukio ya uhalifu nchini lilikabidhiwa leo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akiliwasha gari maalumu la kuchunguza matukio ya uhalifu mara baada ya kukabidhiwa ufunguo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uturuki, Zeki Catalakaya. Gari hilo ambalo linavifaa vyote vya kuchunguza matukio ya uhalifu nchini lilikabidhiwa leo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (watatu kutoka kulia-waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka nchini Uturuki pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi nchini mara baada ya kusaini hati ya ushirikiano wa uchunguzi wa matukio ya uhalifu kati ya nchi ya Tanzania na Uturuki. Jeshi la Polisi Uturuki tayari limekabidhi ya gari maalumu la kuchunguza hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0
 • 08/02/13--04:15: Article 19


 • 0 0  0 0

  Announced a few days ago by FORBES AFRICA, a 21-year-old Angolan model Maria Borges makes the tops Forbes Africa's Magazine Model List for 2013 making her the hottest item of the moment in the catwalk.

  The magazine will hit stands on August 1st, so grab your copy for the list where other African models that came close to snatching the title for number 1 include Ajak Deng from Sudan, Grace Bol from Sudan, Candice Swanepoel of South Africa, Liya Kebede of Ethiopia, Katryn Kruger of South African and Miss Universe competitorFlaviana matata.

  Maria-Borges-Forbes-Africa-Top-Model-BellaNaija-July2013-8-400x600
  Maria Borgas
  Flanianamatata

  0 0
 • 08/02/13--08:00: Article 16


 • 0 0


   Mpiganaji Davis Mosha, Edgar D. Mosha, Mayor wa L.A. Deo Temba (Katikati nyuma) na Army Nando
    Mpiganaji Davis Mosha akimpa ushauri Army Nando kuwa asahau yaliyopita na aangalie ya mbele na kumweleza kuwa hiyo ilikuwa ni mchezo tu (It was just a game)

   Nancy Assenga ( Mama wa Army Nando), Army Nando, na Deo Temba L.A. Mayor
   Mayor wa L.A. Deo Temba, Army Nando, Nancy Assenga (Mama na Meneja) na Mkurugenzi mtendaji wa Swahili TV Bwana Alex Kassuwi mara baada ya kumpokea Nando Los Angeles, California.
   Juliet Luangisa, Army Nando na Nancy Assenga (Mama na Meneja wa Nando)


  Mkurugenzi Mtendaji Swahili TV Bwana Alex Kassuwi, Army Nando, Walter Minja, Deo Temba na Nancy Assenga-Meneja wa Nando wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kumpokea Army Nando Marekani.

  MPIGANAJI DAVIS MOSHA "THE CEO" BAADA YA KUONANA NA WATANZANIA WAISHIO  L.A.  AMWANDALIA HAFLA (BASH) NZITO YA HADHI YA KISTAA (CELEB STATUS) ARMY NANDO KATIKA HOTELI GHALI YA YARD HOUSE L.A. MAREKANI.
   

   Mpiganaji "THE CEO" Davis Mosha katika msafara aliwakaribisha pia chakula cha jioni watanzania zaidi ya ishirini katika hoteli ya bei ghali L.A. Yard House ambayo ipo Downton katikati ya Uwanja wa Lakers (Staples Center) na JW Marriott Hoteli.

   Army Nando na Nancy Assenga (Mama mzazi na Meneja wake) wakifurahia chakula katika Yard House Hoteli Downtown L.A.
  Juliet Luangisa na Walter Minja wakiburudika kwa misosi ya Yard House.
  USIKOSE KUANGALIA EXCLUSIVE INTERVIEW NA SWAHILI TV

   

   

   

   
     USIKOSE KUANGALIA INTERVIEW HII ENDELEA KUANGALIA SWAHILI TV   www.swahilitv.blogspot.com

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga(kulia) akibadilishana hati za makubaliano ya mikataba ya ushirikiano na Mwanzilishi wa kikundi cha kimataifa cha Vijana kutoka Korea(IYF) Mchungaji Mwandamizi Ock Soo Park (kushoto) leo jijini Dar es Salaam. Mchungaji Mwandamizi huyo ambae ametia saini kwa niaba ya kikundi cha IYF(International Youth Fellowship) . Hafla hiyo pia ilishuhudiwa na Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara(katikati).
  Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Dkt, Elisante Ole Gabriel (kulia)akiongea katika hafla ya kutiliana saini mikataba ya ushirikiano leo jijini Dar es Salaam baina ya Wizara yake na Kikundi cha Kimataifa cha Vijana kutoka Korea (IYF).Pichani aliekaa katikati ya bendera ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni naMichezo Mh,Dkt. Fenella Mukangara.( kulia aliokaa) Ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bibi Sihaba Nkinga. (kushoto) Mwanzilishi wa IYF , Mchungaji Mwandamizi Ock Soo Park kutoka kanisa la Good News Gangnam. Seoul Korea.
  Baadhi ya vijana wa kikundi cha IYF kutoka korea wakiohudhuria katika hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo.Mh. Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akipokea Tuzo kutoka kwa Mwanzilishi wa IYF ya Korea Ock Soo Park , ambae pia ni Mchungaji Mwandamizi wa Kanisa laGood News Gangnam.Dhumuni ya tuzo hiyo ni kwaajili yakumpongeza Mh,Waziri huyo kwa jitihada za kazi zake .


  0 0

  Na Anna Nkinda- aliyekuwa Gaborone,  Botswana

  Watanzania waishio nchi za nje wametakiwa kuwalea watoto wao katika misingi bora ya malezi yanayofuata mila, desturi  na utamaduni wa mtanzania ili waendane  na maadili ya kitanzania ya kuishi kwa unyenyekevu, upendo, ushirikiano na kuheshimu watu.

  Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mke wa Rais  Mama Salma Kikwete wakati wa futari ya pamoja iliyoandaliwa na chama cha watanzania waishio nchini Botswana (ATB) katika hoteli ya Grand Palm mjini Gaborone nchini humo.

  Mama Kikwete alisema kuwa ni vizuri watoto wawe na tabia njema inayokubalika na jamii ya kitanzania kuliko kulelewa katika mazingira yatakayowafanya wajue mila na tamaduni za nchi zingine kwani nyumbani ni nyumbani na ili  waendane na  hilo ni lazima walelewe kama  wazazi wao walivyolelewa.

  “Ninawapongeza kwa  kuwa na umoja imara na wenye nguvu na ushirikiano ambao unawafanya kuwa kitu kimoja na pale ambapo jambo lolote linatokea liwe zuri au baya mnaweza kukabiliana nalo kwani  umoja ni nguvu na mahali penye upendo chuki hujitenga”, alisema Mama Kikwete.

  Alisema ni jambo la kufurahisha kuona kuwa ndani ya  umoja huo kuna umoja wa kinamama ambao lengo lao ni  kuwaweka watoto pamoja na kuwafundisha mila na utamaduni wa mtanzania na kuwaomba wanawake ambao hawajajiunga na umoja huo waweze kujiunga  ili wajenge mshikamano ambao ni silaha kubwa ya watanzania.


  0 0

  Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Prof. Palamagamba Kabudi (wa pili kulia|) akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Pwani leo Ijumaa (Agosti 2. 2013) wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Halima Kiemba (kushoto), Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Bertha Swai (wa pili kushoto). Wajumbe wa Tume walifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kupokea taarifa za maandalizi ya Mikutano ya Mabaraza ya Katiba katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani humo, kulia ni Mjumbe wa Tume, Mhe. Al-shaymaa Kwegyir.
  Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi akuizungumza na Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo (Ijumaa Agosti 2, 2013) katika uykumbi wa Shule ya Sekondari ya Kilangalanga iliyopo Wilayani humo.
  Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, Bi. Fediria Swai akichangia hoja kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katika katika mkutano uliofanyika leo( Ijumaa Agosti 3, 2013) katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Kilangalanga iliyopo Wilayani humo.
  Mjumbe wa Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, Jenifer Hassani akichangia hoja kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutanop uliofanyika leo Ijumaa (Agosti 2, 2013) katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Kilangalanga iliyopo Wilayani humo.
  Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwa ni katika mkutano uliofanyika leo Ijumaa (Agosti 3, 2013) katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Kilangalanga iliyopo Wilayani humo.
  Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto), Al- Shaymaa Kwegyir (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Pwani wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Halima Kiemba (wa pili kulia) na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bi. Bertha Swai mara baada ya Wajumbe wa Tume kupokea taarifa ya Maandalizi ya Mikutano ya Mabaraza ya Katiba katika Halmashauri za Wilaya na Miji ya Kibaha.

  0 0

  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Angela Kairuki (katikati-mstari wa kwanza) akifuatana na Balozi wa Vietnam alimaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Nguyen Duy Thien (kulia), Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Mhe. Balozi Juma Khalfan Mpango (kushoto mstari wa nyuma), Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Balozi Bertha Semu-Somi na Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Asia na Australasia, Bw. Omar Mjenga walipokuwa wanawasili katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro kwa ajili ya hafla fupi ya kumuaga Balozi Thien.
  Mhe. Kairuki akizungumza kuhusu uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Vietnam wakati wa hafla  hiyo huku Balozi Thien na Mkewe wakimsikiliza.
  Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Omar Mjenga akiwakaribisha wageni waalikwa kwenye hafla ya kumuaga Balozi Thien ambaye amemaliza muda wa kazi hapa nchini. Wengine katika picha ni Balozi Mpango na Balozi Semu-Somi.
  Mhe. Balozi Nguyen Duy Thien na Mkewe wakimsikiliza Bw. Mjenga (hayupo pichani).
  Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini Balozi Mpango nae akizungumza machache wakati wa hafla hiyo huku Mhe. Kairuki, Balozi Thien na wageni wengine waalikwa wakimsikiliza.
  Mhe. Kairuki akimkabidhi Balozi Thien na Mkewe zawadi ya picha ya kuchora ya Mji Mkongwe wa Zanzibar kama kumbukumbu yao kwa Tanzania.Picha na Reginald Philip.

older | 1 | .... | 213 | 214 | (Page 215) | 216 | 217 | .... | 3348 | newer