Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

WADAU WA MITINDO, UREMBO MSIWABAGUE WENYE ULEMAVU WA NGOZI-BRIGITA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii .

MSHINDI wa Miss Tanzania mwaka 2012 Brigita Alfred ameweataka wadau wa masuala ya urembo na mitindo kuacha kubagua watu kutokana na mapungufu yao ya kimaumbile katika tasnia hiyo.

Brigita amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akitoa neno la shukrani kwa wadau wa mitindo na urembo waliofika katika onesho lake Maalum kwa watu wenye ulemavu wa ngozi lililofanyika nyumbani kwa Balozi wa Uturuki lililokwenda kwa jina la 'My Skin My Pride' na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.

" Unaweza ukaona ukadhani labda nimefanya haya maonesho kwa ajili ya tasisi yangu lakini ukweli unabaki palepale kuwa katika tasnia ya mitindo sasa tunapaswa kuwapa nafasi watu wenye matatizo ya ulemavu wa ngozi kuonesha vipaji vyao na uzuri wa ngozi yao kuliko kuwaacha wenyewe jambo linalo wafanya wajisikie tofauti"amesema Brigita.

Amesema ni jambo zuri sasa kwa waandaaji wa mashindano ya urembo na mitindo kuwajumuisha wadau hao hili nao waonekane katika majukwaa ya kimataifa.

Mkurugenzi wa Tasisi ya Brigita Foundation, Brigita Alfred akizungumza kwa kuwashukuru wadau mbalimbali waliofika wakati wa Fashion Show ya watu ya wenye ulemavu wa ngozi iliyofanyika nyumbani kwa balozi wa Uturuki Masaki jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa wana Mitindo mwenye ulemavu wa ngozi akiwa anapita jukwaani akionyesha mavazi yaliyobuniwa na wanamitindo mbalimbali
Warembo waliowahi kushika taji la Miss Tanzania nchini Nancy Sumari na Jackline Mengi wakishuhudia onesho hilo la mitindo kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.
Baadhi ya wadau wa mitindo waliofika katika Onesho la Mavazi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini lililofanyika Nyumbani kwa Balozi wa Uturuki nchini.
Mwanamitindo Nemalisa akiwa na Mmoja wa warembo wenye ulamavu wa ngozi akionyesha Vazi la nguo za jioni lililoandaliwa na kampuni ya Jackies Collection.

WAKAZI MULEBA WAIOMBA SERIKALI KUONGEZEA WATUMISHI WA UMMA

$
0
0
Na Emanuel Massaka-Globu ya jamii 

WAKAZI wa Kisiwa cha Kerebe wilayani Muleba mkoani Kagera wameomba Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais,Dk. John Maguli kuwapelekea rasilimali watu hasa upande wa afya  na elimu.

Wamesema kwa sasa wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali za kijamii kutokana na uhaba uliopo wa watumishi wa umma. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Michuzi blog juzi na jana, wakazi hao wamesema  huduma za kijamii ni changamoto kwao.

" Zimekuwa zinawaumiza hivyo wamezitaka Wizara husika kusikia kilio chao na tunaomba tujengewa hospitali na shule ili watoto na wakina mama wajazito wapate hudumu muhimu,"wamesema wakazi hao.

Pia wameomba Serikali kuwatengenezea huduma bora katika usafiri wa majini kwa kuwapatia boti kwani wamekuwa wakitumia boti za mtu binafsi ambazo si salama kwao.Hivyo wanaomba upatikane usafiri ulio bora na wa uhakika katika kulinda maisha yao.

Hata hivyo Wakazi hao Kisiwa hicho asilimia 93 wanatengemea uvuvi wa Samaki na asilimia 7 wanajishughulisha na kilimo na ufungaji, hivyo basi wameitaka Serikali kuboresha katika sekta ya uvuvi pamoja na ufungaji ili waweze kuendana na mabadiliko ya nchi kwa kupata kipato kikubwa zaidi.

Kisiwa cha Kerebe kwa sensa ya 2012 kina jumla ya wakazi  3100 lakini  idadi hiyo hupungua na kuongezeka kulingana na kilimo na upatikanaji wa samaki kwa wingi ziwani humo.Hivyo basi kutokana na Serikali ya awamu ya tano inayosema 'Hapa kazi to' itasikiliza kilio chao na kuwapelekea huduma muhimu kwani kila Wizara itakuwa ipo tayari kushirikiana na wanakijiji hao kwa kupitia Wilaya ya Muleba.Na kuongeza viongozi mbalimbali waliochaguliwa wataimarisha ushirikiano wao kwa Serikali

NAIBU MEYA ILALA AWAKUMBUSHA MADIWANI KUSIMAMIA USAFI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

NAIBU Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, amewataka viongozi na madiwani wa Manispaa hiyo kuwahimiza waanchi wao kufanya usafi katika maeneo yao ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.

Kumbilamoto amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Michuzi blog kuhusu nini kifanyike kupunguza magonjwa ya mlipuko katika baadhi ya maeneo katika Manispaa ya Ilala na Mkoa wa Dar es Salaam kwa ujumla.

"Viongozi tunatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na kuhimiza watu kufanya usafi kwani Rais wetu, Dk.John Magufuli alianza kwa kutuonesha kwa mfano nasi tunapawa kumuunga mkono kwa hali na mali ili tutokomeza magonjwa ya mlipuko ambayo mara nyingi hutokana na uchafu," amesema Kumbilamoto.

Ameongeza tangu mchakato huo wa usafi mazingira uanze kwa takribani zaidi ya mwaka sasa katika kata ya Vingunguti hakujaripotiwa kuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu hali ambayo tofauti na awali.Amefafanua kata hiyo ilikuwa sugu kwa ugonjwa huo kiasi cha kuwekwa kambi maalum ya wagonjwa muda wote .

Amesema jukumu la usafi ni la kila mmoja wetu lakini kama viongozi inatakiwa kuacha siasa za maneno na kufanya mambo hayo kwa vitendo ili tuwe mfano bora kwa wapigakura wetu. 

 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto akisukuma Toroli lenye taka kwenda kumwaga Dampo wakati wa zoezi la usafi la kila mwisho wa Mwezi lililofanyika katika Kata ya Vingunguti Jijini Dar es Salaam kama agizo la Rais  Dkt John Magufuli la kuhakikisha kila mmoja anafanya usafi katika eneo lake kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto, akishiriki kusafisha Mitaro ya kutiririsha maji ya Mvua katika Barabara ya Vingunguti Kembembuzi .
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtambani Sharif Mbulu, akichimba mchanga na kutoa taka katika mtaro wa kutiririsha maji barabara ya Vingunguti Kembembuzi.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto ,akihamasisha zoezi la usafai kwa wakazi wa Vingunguti.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto  akikabidhi Pikipiki kwa kundi la Wajasiliamali la Watoto Pori ambao aliungana nao pamoja mapema leo katika shughuli ya Usafi.

WAZIRI UMMY AENDELEA NA ZIARA KANDA YA ZIWA

$
0
0
 Waziri ummy Mwalimu akiangalia ramani ya kituo hicho cha afya ambacho kimejengwa kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Shirika la SEDA Foundation, kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Subi na kushoto ni mmoja wa Viongozi wa Shirika hilo.
Waziri Ummy Mwalimu akiangalia Ramani ya Ujenzi wa jengo la ghorofa nne la Uzazi linalojengwa hospitali ya Mkoa ya Sekoture jijini Mwanza.
.Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto akiangalia kazi inavyoendelea katika hospitali hiyo.
Waziri Ummy Mwalimu akiangalia duka la dawa lililopo kwenye hospitali ya Mkoa ya Sekoture ambapo upatikanani wa dawa kwa Mkoa wa Mwanza ni asilimia 80.
Jengo la Maabara lililojengwa kwenye kituo hicho cha afya katika mpango wa Serikali wa kuboresha huduma za dharura za uzazi kwenye vituo vya afya nchini.(Picha zote na Wizara ya Afya).

RC MAKONDA ATOKWA NA CHOZI BAADA YA KUJIONEA MAISHA YA WASTAAFU WALIODHULUMIWA NYUMBA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea na kutoa pole kwa Familia ya Wastaafu ya Bwana Edward Bejumula na Bi. Stella Bejumula walioteseka kwa Miaka Sita bila Makazi baada ya kudhulumiwa Nyumba yao ambapo ameahidi kulivalia njuga suala hilo kuhakikisha haki inatendeka bila kuvunja sheria.
RC Makonda amewatembelea wastaafu hao na kuwapatia Masada wa vitu mbalimbali ikiwemo Mchele, Unga, Sabuni, Ngano, Mafuta,Nyama,Viazi, Maharage, Sukari, Vitunguu, Ndizi, Nyanya kwaajili ya matumizi ya nyumbani baada ya familia hiyo kupoteza Mali zote. 

Habari ya wastaafu hao kudhulumiwa Nyumba waliyojenga baada ya kufanya kazi kwa Miaka 34 imemgusa RC Makonda hadi kujikuta anashindwa kuvumilia na kutokwa na machozi kutokana na namna inavyouzunisha kuona mnyonge anajituma kwenye kazi na kufanikiwa kujenga nyumba alafu anatokea mtu anatokea mtu anamdhulumu Mali yake.
Makonda amesema kazi ya kutafuta haki ya wastaafu hao inaanza Mara moja kwa kuwahoji watu wote waliohusika na sakata hilo wakiwemo Bank, Muuzaji wa nyumba, Mnunuzi, kampuni ya udalali ya Majembe, Watu wa Mahakama na watu wa ardhi.

Kwa sasa wastaafu hao wanaishi kwenye nyumba ya mfadhili mmoja aliejitolea kusitiri familia hiyo ambapo RC Makonda amemshukuru kwa moyo alioonyesha. 
Kwa upande wao Wastaafu waliodhulumiwa Mali zao wamefurahia kitendo cha RC Makonda kuona taarifa zao kwenye vyombo vya habari kisha kuwatembelea na kuwasikiliza kitendo kilichowafariji na wanaamini kwa utendajikazi wa RC Makonda wanapata haki yao.
Aidha wamemshukuru RC Makonda kwa kitendo cha kuwapelekea Chakula kwakuwa wameishi maisha ya tabu hadi kukosa vitu vya ndani ikiwemo vyakula ambapo wamemuombea kwa Mungu azidi kumpa maarifa ya kuwasaidia wananchi wanyonge. 

HAKIMU WA KWELI NI MUNGU

Dkt. Abbasi Aviasa Vyombo vya Habari Kuunga Mkono Mageuzi Yanayoletwa na Serikali

$
0
0
Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma.
Vyombo vya Habari nchini vimeaswa kuunga mkono juhudi za Serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kwa maslahi mapana ya Taifa.
Akizungumza Wakati wa ziara yake yakutembelea Vyombo vya habari leo mjini Dodoma Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo endelevu kwa kuwa misingi ya Taifa letu imejengwa katika uchumi jumuishi.

“ Kuna umuhimu kwa vyombo vya habari kushiriki kikamilifu kueleza faida za miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa kama ule wa ujenzi wa reli ya Kisasa (Standard Gauge) kwa wananchi ili nao washiriki kikamilifu katika utekelezaji wake ambapo ukishakamilika utakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo” Alisisitza Dkt. Abbasi.

Akifafanua amesema kuwa dhamira yakuwaletea wananchi maendeleo inaendelea kutekelezwa kupitia mfumo wa elimu bure, uzalishaji wa umeme wakutosha, Ujenzi wa uchumi wa Viwanda, ujenzi wa miundo mbinu kama barabara, reli na upatikanaji wa huduma muhimu kama madawa ambapo Serikali imeongeza bajeti ili kuhakiksha kuwa kila mwananchi anapata huduma muhimu na za msingi katika ubora unaotakiwa.
 Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdallah Majura (Mwenyeshati Jeupe) akimuonesha Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi Chumba cha kurushia matangazo wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma. Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimsikiliza Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdalah Majura (Mwenyeshati Jeupe) wakati wa ziara yake yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na wafanyakazi wa Radio ABM FM wakati wa ziara yake yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma. - Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdalah Majura (Mwenyeshati Jeupe) toleo Maalum la Jarida la Nchi Yetu kuhusu mafaniko ya miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Tano. Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifanya mahojiano maalum na Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdalah Majura (Mwenyeshati Jeupe) wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.

uzinduzi wa kampeni za CCM Kinondoni viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam Januari 27, 2018

MRITHI WA ALLY YANGA ANENA BAADA YA USHINDI WA YANGA SC DHIDI YA AZAM FC

$
0
0
Yanga SC iliibuka na ushindi wa bao 2 - 1 dhidi ya Azam FC, mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara uliopigwa katika Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.

DK SHEIN AREJEA NCHINI AKITOKEA NCHI ZA FALME ZA KIARABU UAE

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Nchi za Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu UAE, akivishwa shada la maua na Mtoto aliyeandaliwa.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akitokea katika ziara yake ya wiki moja katika Nchi za Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama,baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wazee wa CCM alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume baada ya kumaliza ziaya yake katika Nche za Falme za Kiarabu UAE

MAONYESHO WIKI YA SHERIA YAANZA RASMI VIWANJA VYA MNAZI MMOJA

$
0
0
Mkurugenzi wa Malalamiko na Maadili-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Happiness Ndesamburo akisikiliza malalamiko ya mmoja wa wananchi aliyetembelea katika Banda hilo lililopo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Watumishi wa Mahakama wakiendelea kuwasikiliza Wananchi waliotembelea katika Maonyesho hayo yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na nchi nzima kuanzia Januari 27-Januari 31, 2018, kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini ni Februari 01, 2018 kitaifa itafanyika jijini Dar es Salaam na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa, Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, aidha sherehe hizi zinaadhimishwa nchi nzima.


Elimu ya Sheria ikiendelea kutolewa kwa wananchi walipotembelea Viwanjani hapo mapema Januari 27, 2018 siku ambayo Maonyesho yameanza rasmi. Elimu ya Sheria inaendelea nchi nzima, pia kwa upande wa Dar es Salaam, huduma hii inatolewa katika Vituo mbalimbali kama Sinza (Simu 2000-Makmbusho), Magomeni (Manzese-Darajani), Mbezi Mwisho (ndani ya kituo), Kawe Stendi, Tegeta (Stendi Nyuki), Bunju, Mbagala Zakiem, Keko (Keko-Bora), Mjimwema-Kigamboni Stendi, Tandika mbele ya Kituo cha Polisi, Mombasa, Kitunda, Banana, Segerea, Ilala sokoni (Boma), Kariakoo-Msimbazi Polisi, Buguruni Sheli na Gerezani.

Muonekano wa Banda la Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katika Maonyesho ya Wiki ya Sheria nchini, yanayoendelea nchi nzima, Wizara ni Moja ya Taasisi za Sheria zinazoshiriki katika Maonyesho hayo, Taasisi nyingine ni: Tume Ya Utumishi Wa Mahakama, Ofisi Ya Mwanasheria Mkuu Wa Serikali (Agc), Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Mashitaka (DPP), Mkemia Mkuu Wa Serikali, TAKUKURU (PCCB), Wakala Wa Usajili, Ufilisi Na Udhamini (Rita) na nyingine nyingi.

Muonekano wa sehemu ya Mabanda ya Watoa huduma ya Sheria pamoja na wananchi walipotembelea kupata huduma.

NEC YATOA MAAMUZI RUFAA MGOMBEA UBUNGE NA RUFAA 5 ZA WAGOMBEA UDIWANI

$
0
0
Kwa kuzingatia masharti ya Kifungu cha 40(6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, ikisomwa pamoja na Kanuni za 34 na 35 za Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015, Tume ilipokea Rufaa moja (1) kutoka kwa Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) akipinga maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo kuhusu pingamizi alilomuwekea Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Aidha, kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 44 (5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, ikisomwa pamoja na Kanuni za 28 na 29 za Kanuni za Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015, Tume ilipokea Rufaa tano (5) za Wagombea Udiwani kutoka katika Kata ya Isamilo – Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakipinga Maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo. Rufaa tatu (3) ni za wagombea walioondolewa kwenye kugombea ili warejeshwe na Rufaa mbili (2) zinaomba Tume itengue uteuzi wa mgombea Udiwani aliyeteuliwa katika Kata hiyo.

Katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika tarehe 26 Januari 2018 siku ya Ijumaa, Tume ilipitia Rufaa hizo na kuamua kama ifuatavyo:

Mosi, kuhusu Rufaa ya Mgombea Ubunge, Tume imekubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi na hivyo Mgombea aliyekatiwa Rufaa wa CHADEMA anaendelea kuwa mgombea wa Ubunge Jimbo la Kinondoni.

Pili, kuhusu Rufaa za Wagombea Udiwani Kata ya Isamilo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza, kupinga kuondolewa kugombea Udiwani katika Kata hiyo, Tume imewarejesha kuwa Wagombea Udiwani wawili wa vyama vya CHADEMA na CUF.

Tatu, Tume imekubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi ya kumuondoa katika orodha ya wagombea Udiwani mgombea wa Chama cha UDP. Hivyo hatakuwa mgombea katika kata hiyo

Nne, Tume imekataa rufaa mbili zilizokuwa zinapinga uteuzi wa mgombea wa CCM aliyeteuliwa katika Kata hiyo na hivyo, mgombea wa CCM anaendelea kugombea Udiwani katika kata husika.

Taarifa rasmi za maamuzi ya Tume zimetumwa kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ili wawapatie wahusika maamuzi hayo.

Imetolewa leo tarehe 26 Januari, 2018 na,
Kailima, R.K
MKURUGENZI WA UCHAGUZI
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (katikati) akieleza jambo wakati wa Kikao cha Tume kilichokaa Ijumaa Januari 26, 2018 kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Uchaguzi Mdogo unaofanyika Februari 17, 2018.Kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mkuu Mst. wa Zanzibar, Hamid Mahmoud Hamid na kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi Hamis Mkunga na wajumbe wengine wa kikao cha Tume.Picha na Daniel Kasokola-NEC

POWER ON FITNESS GYM YAUKARIBISHA MWAKA 2018 KWA MBWEMBWE

$
0
0

Power on Fitness Gym iliyopo Mwenge, kinondoni, Jijini Dar es salaam imeukaribisha mwaka 2018 kwa style ya kipekee ambapo wadau mbalimbali wamejumuika kufanya mazoezi pamoja na kuburudika kwa chakula, Vinywaji na muziki kabambe wa Skylight Band.

Shughuli hiyo imefanyika Jumamosi January 27,2018 katika viwanja vya posta vilivyopo Sayansi, Kijitonyama. Shughuli hiyo ilianza saa 12 asb na inatarajia kumalizika usiku mnene.

Siku hiyo imepambwa na mazoezi ya kukimbia(Jogging) ambayo yameanza alfajiri ya saa 12, na kufuatiwa na mazoezi ya Aerobics, Steps, Zumba, Mpira wa miguu, na michezo mingine kama kuvuta Kamba, Kukimbiza Kuku nk.

Baada ya mazoezi kukamilika wadau wa Power on Fitness Gym wamejumuika katika burudani kabambe ya muziki iliyoporomoshwa na bendi ya Skylight na Ma DJ wakali wa hapa nchini.

Siku hiyo pia kutakuwa na Nyama choma itakayoandaliwa kiufundi na wapishi waliobobea, Supu bila kusahau vinywaji vya kila aina.

Shughuli hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya JSP Marketing Link Limited ikishirikiana na Msouth Company, Dagaa Microfinance Limited, Simba Makini Group, Jaina Ice Cubes, Micgen Insurance Brokers, TTCL na wenyeji Power on Fitness Gym.

MASAUNI AKAGUA MAKAZI YA ASKARI MAENEO YA POLISI WALIYOUZIWA WANANCHI KINYUME NA UTARATIBU MKOA WA KUSINI UNGUJA

$
0
0
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuuliza maswali Mhandisi wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Pascal MacORWA (kushoto), alipotembelea eneo la Tunguu lililovamiwa na wananchi, ambalo mmiliki halali ni jeshi la Polisi. Wakwanza kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja,Makarani Khamis na watatu kulia ni Mkuu wa mkoa huo, Hassan Khatib Hassan.Naibu Waziri yuko Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Makarani Khamis , akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, juu ya eneo la Tunguu lililoko Mkoa wa Kusini Unguja ambalo ni mali ya Jeshi la Polisi, hivi sasa likimilikiwa na wananchi kinyume cha sheria.Kushoto ni Mkuu wa mkoa huo, Hassan Khatib Hassan. Naibu Waziri yuko Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyeshwa na Mhandisi wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Pascal MacORWA, ramani ya moja ya maeneo yanayomilikiwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa ziara ya naibu waziri kukagua maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya polisi mkoani hapo.Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo,Hassan Khatib Hassan. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Khatib Hassan, akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kukagua makazi ya askari polisi yanayoonekana pichani, yaliyopo eneo la Machui, lililopo Mkoa wa Kusini Unguja.Naibu Waziri yupo Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya kukagua maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya polisi na makazi ya askari.Kulia ni Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Khatib Hassan, akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kukagua eneo yalipojengwa maduka ya biashara ambayo wamiliki wamenunua viwanja hivyo vya Jeshi la Polisi kinyume na utaratibu. Naibu Waziri yuko Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na viongozi wa Mkoa Kusini Unguja alipowasili leo mkoani hapo kwa ziara ya kikazi ya kukagua maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya polisi na makazi ya askari.Kulia ni Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

UZINDUZI KAMPENI ZA CCM UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE KINONDONI ZAWAVUTIA WENGI.

$
0
0
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba (kushoto), akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo. 
Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akiwasalimia wananchi mara baada kutambulishwa na kuitwa jukwaani kumwaga sera zake za kuomba kura wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo. 
Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akizungumza mambo mbalimbali mbele ya Wanachama wa chama hicho na Wananchi kwa ujumla mara baada kutambulishwa na kuitwa jukwaani kumwaga sera zake za kuomba kura wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kimara Chadema, Ngudu Pascal Manota akiwasalimia wananchi wa Kinondoni jioni ya leo alipokuwa akitambulishwa kwao na kurudisha kadi ya chama hicho na kujiunga na CCM,pichani kati ni Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba na kulia kwake ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Stephen Wasira
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kimara Chadema, Ngudu Pascal Manota akirudisha kadi ya chama hicho na kujiunga na CCM,Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba akiitazama kadi hiyo kwa makini
Aliyekuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Muslim Hassaanal ambaye hivi karibuni alihamia CCM,akimwombea kura za ushindi Mgombea Ubunge wa jimbo la Kinondoni ,Maulid Mtulia wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo. 
Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba akizungumza mbele ya umati wa watu waliofika kuhudhuria uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, jijini Dar es Salaam leo. 
Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo,katika viwanja vya Biafra Kinondoni jioni ya leo.
Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakisikiliza kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la uzinduzi wa kampeni Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Kinondoni,mapema leo jijini Dar.PICHA NA MICHUZI JR.

DAILY NEWS ONLINE: UKWELI KUHUSU ATHARI ZA MIONZI YA MINARA YA SIMU HUU HAPA


DAILY NEWS OMLINE: MAGAZETINI JANUARI 28, 2018: UCHUMI TANZANIA WAGUSA WANANCHI, KAMPENI ZA UCHAGUZI DAR MOTO

TANESCO yaja na mfumo wa GIS kuboresha huduma

$
0
0
                                                                      Na Yasin Silayo

Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limeandaa mfumo wa taarifa za kijiografia za wateja, maarufu kwa jina la GIS, kwa lengo la uboreshaji wa huduma za usambazaji umeme, ambapo sambamba na ujio wa mfumo huo TANESCO iliandaa  mafunzo maalumu kwa wafanyakazi wa Shirika hilo kwa Kanda ya Dar na Pwani iliyofanyika Kibaha Mkoani Pwani. Hayo yamebainishwa na Naibu Mkurugenzi mtendaji wa TANESCO Anayesimamia masuala ya Usambazaji umeme na huduma kwa wateja Bi. Joyce J Ngahyoma (pichani, aliyesimama).
Akiongea katika kikao cha tamati ya mafuno hayo Bi. Joyce alisema kuwa Mfumo huo wa uboreshaji wa huduma za usambazaji umeme (GIS) kanda ya Dar na Pwani ulibuniwa na TANESCO kwa lengo la kuboresha miundombinu ya usambazaji umeme kwa kupitia mjumuisho wa pamoja wa taarifa zote za wateja, miundombinu ya kusambaza umeme pamoja na ramani ya mifumo ya umeme yenye taarifa za wateja wote kulingana na taarifa za kijografia za maeneo yao waliyoko.
Aliongeza kuwa TANESCO Iliamua kuja na mfumo huu kama suluhisho kutokana na Kanda ya Dar es salaam na Pwani, kuwa na changamoto nyingi za kihuduma zinazotokana na ongezeko kubwa la mahitaji ya umeme kila uchwao. Ongezeko hili la mahitaji ni kutokana na ujenzi wa majengo marefu ya kibiashara pamoja na viwanda vya uzalishaji mali katika maeneo mbalimbali ya katikati ya Jiji na Mkoa wa pwani, hasa Kariakoo, Ilala, Kinondoni, Kigamboni na maeneo ya kiviwanda yaliyopo na yale mapya yanayoanzishwa katika Kanda ya Dar wa Pwani.

Aidha Bi. Ngahyoma alibainisha kuwa ni matumaini ya Uongozi wa Shirika na Serikali kwa ujumla, kuwa mafunzo hayo yanayoambatana na matumizi ya mfumo wa taarifa za kijiografia (GIS) yatasaidia Shirika kuimarisha huduma maradufu hivyo kuchochea zaidi ukuwaji wa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Baada ya kukamilika kwa mfumo huu wa GIS Katika kanda ya Dar na Pwani, lengo la TANESCO ni kupanua zaidi mfumo huu katika Mikoa mingine.
Kutokana na mafunzo yaliyotolewa katika semina hiyo na matumizi ya mfumo wa GIS, yatarahisisha na Kuboresha huduma kwa wateja na kuongeza ufanisi wenye tija katika huduma zaShirika. Maboresho yatakayojumuisha kuwafikia wateja kwa wakati na haraka zaidi yanapotokea matukio ya dharura, udhibiti wa wizi wa umeme, ukusanyaji haraka mapato ya Shirika, kuchukua vipimo vya wateja wapya wanaohitaji kuunganishwa umeme (Service line Survey) kwa haraka kupitia mfumo huu kutokea ofisini, kuimarisha usimamizi mzuri wa miundombinu ya usambazaji umeme kwa wateja huko mitaani pamoja na kurahisisha ukaguzi wa taarifa za mauzo ya Shirika na kulinda Transfoma za usambazaiji umeme zisiungue ambapo ilielezwa kuwa Shirika linatarajia mageuzi makubwa ya kihuduma kwa wateja kupitia mfumo huo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Wa TANESCO anayesimamia masuala ya Usambazaji Umeme na Huduma kwa Wateja Bi. Joyce Ngahyoma, akiongea na wafanyakazi wa TANESCO walioshiriki mafunzo ya mfumo huo mpya Wa GIS yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi za TANESCO Mkoani wa Pwani.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARi 28,2018

TANZANIA KINARA UCHUMI JUMUISHI AFRIKA

$
0
0

Usimamizi mzuri na utekelezaji wa Sera mbalimbali za kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu kujenga na kumiliki uchumi, kumeifanya Tanzania kuibuka kinara miongoni mwa nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kuwa na Uchumi Jumuishi (Inclusive Economy) unaokua duniani.

Taarifa iliyotolewa na Word Economic Forum kupitia mradi wake wa  ‘The Inclusive Development Index’, imeitaja Tanzania kushika nafasi ya kwanza kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na ya 48 kati ya nchi 103 zilizofanyiwa tathmini ya nchi zenye Uchumi Jumuishi duniani,

Katika orodha ya kumi bora, nchi zilizofuatia na nafasi ziliyoshika kidunia ni pamoja na Ghana (52), Cameron (53), Burundi (55), Namibia (56), Rwanda (57), Uganda (59), Mali (60), Senegal (61) na Nigeria (63).

Takwimu za ukuaji huu zinaakisi moja kwa moja kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amekuwa akielezea kutaka uchumi wa Tanzania umilikiwe na wananchi kwa njia mbalimbali ikiwemo kutekeleza sera ya uchumi wa viwanda ambapo watanzania wengi hivi sasa wamekuwa wakitekeleza sera hiyo kwa kuanzisha viwanda vikubwa na vidogo.

Mtaalamu Mbobevu wa masuala ya Uchumi na Mhadhiri wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Honest Ngowi ameeleza kuwa takwimu zilizotolewa na taasisi hiyo zinatafsiri kuwa uchumi wa Tanzania unaelekea kumilikiwa na watu wengi zaidi jambo ambalo litasaidia kupunguza pengo la kipato kati ya walionacho na wasionacho.

Profesa Ngowi ameeleza kuwa uchumi wa aina hiyo unawashirikisha wananchi kumiliki uchumi na kuwafanya watu wengi kufaidi matunda ya ukuaji wa uchumi wa nchi.

“Taarifa hizi ni njema kwani kitaalam tunaita broad based economy ambapo watu wengi wanashirikishwa kumiliki uchumi na wengi wanafaidi,” alieleza Profesa Ngowi na kuongeza kuwa kuna nchi zingine zinauchumi mzuri lakini unamilikiwa na watu wachache na kufanya kuwa na pengo kubwa kati ya walionacho na wasionacho.

Katika siku za hivi karibuni, Taasisi mbalimbali duniani zimekuwa zikitoa ripoti zikiielezea Tanzania kupaa kiuchumi ambapo ripoti za Shirika la Fedha Duniani (IMF), Benki ya Dunia (WB) na Taasisi ya Goldman Sachs ya Marekani hivi karibuni zilitabiri kuwa wakati uchumi wa dunia utakua kwa wastani wa asilimia 3.0 hadi 4.0, ukuaji wa uchumi wa Tanzania unatajwa kuendelea kuwa kati ya nchi tano bora za Afrika ukitarajiwa kukua kwa asilimia 6.5 hadi 7.0 katika mwaka 2018.

Dar Swim Club yatwaa ubingwa wa Tanzania kwa waogeleaji chipukizi

$
0
0
Klabu ya kuogelea ya Dar Swim Club imetwaa ubingwa wa Tanzania wa waogeleaji chipukizi wenye umri kati ya miaka saba na 14 kwa mara ya pili mfululizo baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 3,144.
Mashindano hayo yalishirikisha jumla ya timu sita, yalimalizika Jumamosi jioni kwenye bwawa la kuogelea la  shule ya Haven of Peace Academy (Hopac) jijini.
Haikuwa kazi rahisi kwa Dar Swim Club kutwaa ubingwa huo kwa mara ya pili mfululizo kutokana na ushindani mkubwa kutoka kwa klabu za Taliss na Bluefins ambao zilionyesha upinzani wa hali ya juu.
Taliss ilimaliza katika nafasi ya pili kwa kujikusanyia pointi 2,966 huku Bluefins ikimaliza ya tatu kwa kupata pointi 2,945 na Champion Rise ikishika nafasi ya nne kwa kupata pointi 329.
Nafasi ya tano ilichukuliwa na timu ya Wahoo ya Zanzibar kwa kupata pointi 222  na klabu ya Mwanza International School ikimaliza ya sita kwa kupata pointi 44 katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na kituo cha ITV, Coca Cola, Print Galore, Label Promotions, Kisima Water, IST, JNC Events Support &co limited, Kalu Photography na Knight Support.
Waogeaji wa kike wa klabu ya Dar Swim Club ndiyo waliochangia ushindi kwa kiasi kikubwa katika mashindao hayo baada ya kuwa wa kwanza kwa kujikusanyia pointi 1,706 na kufuatiwa na Taliss waliopata pointi 1,480 na  Bluefins kwa kupata pointi 1,000.
Wahoo walishika nafasi ya nne kwa upande wa wasichana kupata pointi 190 na kufuatiwa na Mwanza (44) na Champions Rise katika nafasi ya sita kwa kupata pointi 30.
Kwa upande wa wavulana, klabu ya Bluefins ilishika nafasi ya kwanza kwa kupata pointi 1,755 na kufuatiwa na Taliss (1,321) na Dar Swim Club (1,243), Champion Rise ( 329) na Wahoo katika nafasi ya tano kwa kupata pointi 32.
Katibu Mkuu wa DSC, Inviolata Itatiro aliwapongeza wachezaji na makocha wa klabu hiyo kwa kufanya vyema katika mashindano hayo na kuendelea kuwa mabingwa.
Inviolata alisema kuwa kujituma kwa wachezaji, makocha, viongozi na wazazi kumeiletea sifa timu hiyo.
Mashindano hayo yalishirikisha jumla ya waogeleaji chipukizi 182 ambao walishindana katika mita 50, 100 na 200 katika staili tano butterfly, freestyle, breaststroke, backstroke na Individual Medley (IM).
 Wachezaji wa klabu ya kuogelea ya Dar Swim Club wakifurahia  ubingwa wa Tanzania wa waogeleaji chipukizi wenye umri kati ya miaka saba na 14
 Wachezaji wa klabu ya kuogelea ya Dar Swim Club wakifurahia  kombe la ubingwa wa Tanzania wa waogeleaji chipukizi wenye umri kati ya miaka saba na 14
Wachezaji wa klabu ya kuogelea ya Dar Swim Club wakipozi na kombe la ubingwa wa Tanzania wa waogeleaji chipukizi wenye umri kati ya miaka saba na 14
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images