Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

TAA YARUDISHIWA KIWANJA CHA NDEGE KAHAMA

0
0
KAMPUNI ya madini ya ACACIA yenye kumiliki migodi ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyahulu imekirudisha serikalini Kiwanja cha Ndege cha Kahama kwa ajili ya kuchochea maendeleo kwa ujumla.

Awali mwaka 2005 kiwanja hicho kilikabidhiwa kwa makabidhiano maalum kati ya serikali na iliyokuwa kampuni ya madini ya Barrick walioomba ili kurahisisha shughuli zao za migodini ikiwemo ya kutumia ndege kusafirisha wafanyakazi wao na vifaa. 

Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika jana mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela aliiomba serikali kusaidia kurefusha barabara ya kutua na kuruka kwa ndege kutoka Km. 1.5 hadi kufikia Km 2, ili kufanikisha utuaji wa ndege kubwa ikiwemo ya Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Q400. 

“Tunashukuru wenzetu wa ACACIA kwa kurudisha tena serikalini kiwanja hiki, lakini bado tunaimani tutaendeleza ushirikiano baina yetu, lakini ombi langu kwa serikali ni kuongeza urefu wa barabara ya kutua na kuruka kwa ndege ili ndege kubwa zaidi ziweze kutua ninaimani zitachochea shughuli za kilimo, biashara na madini na uchumi wananchi utaimarika zaidi,” alisema Bw. Mayongela. 
Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (wanne kulia), Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack (Mwenye ushungi) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (watatu kulia), jana wakikagua miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Kahama kabla ya makabidhiano ya kurudishwa serikalini na Kampuni ya Madini ya ACACIA.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainabu Telack akihutubia wananchi waliofika kushughudia makabidhiano ya Kiwanja cha Ndege cha Kahama yaliyofanyika jana baina ya Kampuni ya Madini ya ACACIA na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (watatu kulia), akisaini nyaraka za makubaliano ya kurudishwa Kiwanja cha Ndege cha Kahama kwa serikali kutoka kwa Kampuni ya Madini ya ACACIA, ambapo wa pili kulia ni Meneja wa migodi ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyahulu, Bw. Benedict Busuzu na wakwanza kulia ni Mwanasheria wa ACACIA, Bi Diana Wamuza, huku Naibu Waziri Sekta ya Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa (mwenye miwani) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack wakishughudia


Waziri Ummy Mwalimu afungua CT-Scan hospitali ya Bugando

0
0
Na WAMJWW.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB)  ameahidi kuwaletea mashine ya uchunguzi ya MRI katika hospitali ya rufaa ya kanda ya ziwa Bugando mwaka huu.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati akifungua mashine ya  CT-scan ambayo itakua inapima magonjwa mbalimbali iliyogharimu shilingi za kitanzania bilioni 1.6 ambazo zinetokana na vyanzo mbalimbali vya mapato vya hospitali hiyo.
Aidha,Waziri Ummy ameahidi ndani ya miaka mitatu kuanzisha taasisi ya moyo ili kuweza kupunguza gharama kwa wananchi wa kanda ya ziwa na magharibi wanaopata matatizo ya moyo kwenda kupata vipimo na matibabu kwenye taasisi ya moyo ya  JKCI ya jijini Dar es Salaam.
 Waziri Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria ufunguzi wa  CT-Scan kwenye hospitali ya Bugando,kulia ni Baba Askofu wa Kanisa katoriki jimbo la Geita Flavian Kasala na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.

Mashine ya CT-scan iliyogharimu shilingi za kitanzania bilioni 1.6
 Waziri Ummy mwalimu akiongea na watumishinwa hospitali ya rufaa ya kanda ya ziwa ya bugando wakati wa uzinduzi wa mashine ya CT-scan.
 Mkurugenzi wa hospitali ya rufaa ya bugando dkt.Abel Makubi akitoa shukrani mara baada ya uzinduzi wa mashine hiyo.
 Mtaalamu wa Mionzi wa hospitali ya Bugando akimpatia maelezo Waziri wa Afya mara baada ya ufunguzi wa mashine hiyo
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) akiwajulia hali wagonjwa waliofika hospitalini hapo kupata matibabu.
 Waziri Ummy Mwalimu akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa Hospitali hiyo kwenye kitengo cha Saratani hospitalini hapo.
 Waziri Ummy Mwalimu akiongea na Mzee Juma Salumu kutoka tabora aliyefika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu ya masikio.Waziri amewahakikishia serikali ipo mbioni kuboresha huduma za kibingwa katika hospitali ya mkoa ya Tabora ili kupunguza gharama kwa wananchi

WAZIRI MAKAMBA AONGOZA SHUGHULI ZA UPANDAJI MITI DODOMA

0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba akihutubia wakati zoezi la upandaji miti kuendeleza programu ya kuifanya Dodoma iwe ya kijani  iliyofanyika mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba akipanda mti wakati wa zoezi la upandaji miti kuendeleza programu ya kuifanya Dodoma iwe ya kijani  iliyofanyika mjini Dodoma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Kangi Lugola akishiriki katika zoezi la upandaji miti katika kuendeleza programu ya kuifanya Dodoma iwe ya kijani.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akifurahia jambo na Wajumbe wa kamati ya bunge ya viwanda , biashara na Mazingira katika siku ya zoezi la programu ya  upandaji wa miti na kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.
 Sehemu ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais waliohudhuria katika zoezi hilo wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani)
Pichani Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakitumbuiza wakati wa zoezi hilo la upandaji miti.

Wizara ya Maliasili na Utalii kuikarabati nyumba ya Nyerere Magomeni-Dk Kigwangalla

0
0
Wizara ya Maliasili na Utalii kuikarabati nyumba ya Nyerere Magomeni-Dk Kigwangalla Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla (MB) mapema leo Januari 26,2018,amefanya ziara maalum katika Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda Namba 62, ambayo aliishi hapo miaka ya 1950's .

Dk. Kigwangalla ameweza kujionea mambo mbalimbali ndani ya makumbusho hayo huku pia akipokea maoni ya namna ya kufanyiwa maboresho ya kituo hicho ikiwemo ufinyu wa eneo la ofisi na maegesho ya wageni wanaotembelea hapo.

"Nimefika hapa leo kujionea Kituo hichi ambacho ni kielelezo kikubwa cha Mwasisi wa Taifa letu. Hapa pana hazina kubwa na kituo hiki kina mambo mengi sana ya kumuenzi Baba wa Taifa. Kwa hali tuliookuta kwa kweli tutakaa na timu yangu kuona tunafanya maboresho makubwa kabisa ili kiwe kama maeneo mengine yenye Wahasisi wa Mataifa yao, tumeona kama eneo alilozaliwa Mzee Mandela kule Afrika Kusini, nyumba yake imehifadhiwa vizuri na imekuwa na wageni wengi.Kwa hapa kwetu na sisi tutakaa na wenzetu kutatua changamoto hizi. 

Hapa tutajenga Maktaba ambapo watu watakuja kusoma vitabu vya Mwasisi wetu na kuona mambo aliyokuwa akifanya. Lakini pia tutaonana na Viongozi wa Halmashau ri ya Kinondoni kuona namna ya kupaboresha mahala hapa ikiwemo miundombinu ya Barabara ya kuingia na kutoka eneo ili" alieleza Dk. Kigwangalla.
  
Muhifadhi Mkuu wa Makumbusho nyumba ya Nyerere iliyopo Magomeni Jijini Dar es Salaam,Bi. Neema Mbwana akisoma taarifa za kituo hicho kwa Waziri Dk Kigwangalla alipotembelea kituoni hapo mapema leo Januari 26,2018.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Kigwangalla akisaini kitabu cha Wageni alipowasili kituoni hapo
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Kigwangalla akitambulishwa wafanyakazi wa kituo hicho
Dk. Kigwangalla akitazama baadhi ya vitabu vya Mwalimu Nyerere ambavyo vimehifadhiwa nyumbani hapo
Dk. Kigwangalla akitazama baadhi ya picha mbalimbali za Baba wa Taifa ambazo zipo nyumbani hapo.

Kumbukumbu ya miaka 12 ya kifo cha Chipembele Said Chipembele

0
0
 Ni miaka 12 sasa tangu uage Dunia mpendwa wetu Chipembele Said Chipembele, tunaona ni Kama Jana!
Mwenyeezi Mungu aendelee kuipumzisha Roho yako mahala Pema Peponi.
AMIN
 Chipembele Said Chipembele enzi za uhai wake ambapo alikuwa mmoja wa wapiga drum mahiri nchini na nchi za nje kwenye bendi mbalimbali za muziki

Watoto wa Kituo cha Tumaini la Maisha Muhimbili Wapatiwa Msaada

0
0
Watoto wenye saratani ambao wanamekuwa wakihudumiwa na Kituo cha Tumaini la Maisha  kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)wamepatiwa msaada wa fedha kwa ajili ya kupatiwa huduma mbalimbali ikiwamo na lishe bora.
Kampuni ya Simu ya Vodacom leo imetoa msaada wa Sh. 30 milioni kwa kituo cha ikiwa ni jitihada za kuiunga serikali mkono katika mipango yake za kutoa huduma bora kwa wagonjwa wa kundi hilo.
Mkurugenzi wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru ameishukuru kampuni hiyo simu kwa kuwasaidia watoto hao na ameiomba iendelee kuwaisaidia watoto hao ili kuwajengea uwezo wa kuwa na afya bora.
“Napenda kutoa shukrani kwa Vodacom kwa miaka kadhaa kuendelea kusaidia Tuamaini la Maisha,” amesema Profesa Museru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akipokea mfano wa hundi ya Shilingi 30 milioni ambazo zimetolewa na Kampuni ya Simu ya Vodacom kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye saratani. Kutoka kulia ni Mkuu wa Uhusiano na Mawasilino wa Kampuni ya Vodacom, Jackline Materu, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tumaini la Maisha, Dkt. Trish Scanlan na Zuhura Mawona ambaye amemwakilisha Mkurugenzi wa Uuguzi Muhimbili.
Watoto wenye saratani wakifurahia jambo kabla ya kupatiwa msaada wa Shilingi 30 milioni. 

UNNewsKiswahili: Hii ndio hali halisi ya kazi za walinda amani wa UN

0
0
Tahir na askari wenzake wanajiandaa kwenda katika doria kaskazini mwa Mali eneo lililotawaliwa na vikundi vya magaidi na pia wanamgambo wa Boko Haram. Swali !!! je yeye na wenzake watarudi salama? #MINUSMA,#PEACEKEEPER kwa habari mbalimbali tembelea http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/

VOA Swahili: Duniani Leo 26th January 2018


JK AFURAHIA SOMO LA MKIKITA KUHUSU KILIMO BORA CHA MAPAPAI

0
0
Na Richard Mwaikenda, Msoga.

.RAIS mstaafu Dk.Jakaya Kikwete amefurahishwa na elimu ya kilimo cha kisasa cha Papai chenye gharama nafuu aliyopatiwa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Living green)

Elimu hiyo ilitolewa hivi karibuni nyumbani kwake Msoga, Chalinze, mkoani Pwani na Ezra Machogu Mtaalamu wa Kilimo wa Kampuni ya Awino Farm ambayo ni mwanachama wa Mkikita.

Kikwete alifurahi kuambiwa kwamba kampuni hiyo inaweza kuzalisha papai lenye ubora kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye gharama nafuu hivyo kumfanya mkulima apate faida kubwa wakati wa mauzo.

Ezra anasema kuwa unaweza kupunguza gharama kwa kuacha kuchimba mashimo badala yake unalima shamba mara tatu kwa kutumia trekta, hivyo kuufanya udongo kuwa tifutifu kitendo kitakacho kurahisishia kupanda miche ya papai bila matatizo.

Anasema ukitumia njia hiyo itakuondolea gharama ya kuchimba mashimo 1200 katika heka moja ambayo jumla ni sh. mil. 6 ikiwa kila shimo itakuwa sh. 500 wakati kulima mara tatu heka moja kwa trekta ni sh. 150,000.

Ezra anamweleza Dk. Kikwete kuwa unaweza pia kupunguza gharama ya mbolea kwa kila shimo kuweka majagi mawili badala ya debe moja.Pia alimweleza kuwa katika umwagiliaji papai halihitaji maji mengi, hivyo unaweza kutumia lita 10,000 kwa siku kumi badala ya siku nne.
 Rais mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete akifurahi kuona papai alililopelekewa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Livinggreen) walipokwenda kumpa elimu kuhusu kilimo bora cha zao hilo nyumbani kwake Msoga, Chalinze mkoani Pwani. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange.
 Dk. Kikwete akishukuru kwa mafunzo hayo yaliyotolewa na Mwanachama wa Mkikita  Mtaalamu wa Kilimo cha Papai kutoka Kampuni ya Awino Farm, Ezra Machogu. Kulia ni Adam Ngamange.
 Meneja  Kilimo wa Mashamba ya Dk. Kikwete, Justine (kushoto) akiwa na  Mkurugenzi wa Kampuni ya Awino, Martine Wamaya (kulia) na Mtalaamu wa kilimo cha Papai,  Ezra Machogu walipokuwa wakitoka kuchuma papai kutoka kwenye shamba darasa la Kampuni ya Awino eneo la Msata tayari kumpelekea Rais mstaafu, Dk. Kikwete.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 26.01.2018

Minja brings better medical imaging technology to homeland of Tanzania

0
0
Most people, at some point in their lives, have had an x-ray. It’s a common practice. In fact, today at Yale-New Haven Hospital alone, every year more than 70 radiologists perform more than one million x-ray, ultrasound, CT and MRI imaging studies to diagnose and monitor the treatment of various health conditions for more than 500,000 people. Typically, once an image is taken, it is digitized and can be immediately shared electronically with the patient’s general practitioner and other medical specialists, enabling them to make a quick diagnosis and provide care in a timely manner. 
Dr. Frank Minja, M.D.In many countries, however, operating an effective medical imaging program is much more challenging. Many imaging programs worldwide still use hard-copy film, which is expensive, frequently in short supply, and not as easily and quickly shared as digitized images. 
Dr. Frank Minja, M.D.
To help remedy this, Dr. Frank Minja, assistant professor of radiology and biomedical imaging at Yale School of Medicine, traveled to Tanzania, Africa in 2014 to implement a Picture Archiving and Communication System (PACS), a medical imaging technology that provides economical storage and convenient access to medical images including x-rays, ultrasounds, CTs, and MRIs.
Minja is no stranger to Tanzania. He was born and raised in the former Tanzanian capitol of Dar es Salaam, and traveled to the United States for college and medical school at Harvard University. Minja came to Yale School of Medicine in 2004 for a fellowship in diagnostic radiology residency and neuroradiology; he joined the Yale faculty in the Department of Radiology and Biomedical Imaging in 2009.
Even before completing his Neuroradiology Fellowship, Minja had already begun collaborating with radiology colleagues at the Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) in Dar es Salaam, who were establishing the first Diagnostic Radiology residency training program in Tanzania.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama akutana na Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini

0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mh. Nkurlu leo amekutana na Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro na kufanya mazungumzo kuhisu maendeleo na changamoto na fursa zilizoko Kahama.
Mr. Alvaro amemhakikishia Mh. Nkurlu kusaidia sekta za elimu, ajira kwa vijana na mimba za utotoni. Bw. Alvaro na timu yake watazuru Kahama mwezi February mwaka huu ili kujionea fursa zilizopo.

msaada tutani: mdau apotelewa na binti yake dar es salaam

0
0
Nimepotelewa na binti yangu kwa  jina anafahamika kama KHADIJA ALLY mwenye umri wa miaka 14, mkaazi wa Kinondoni Vijana, Dar es salaam. 
Ametoweka katika mazingira ya kutatanisha tangia aage aende shule hatujamuona tena yapata wiki moja sasa, tangia Ijumaa iliyopita hajaonekana  nyumbani. 
Tafadhali atakaemuona atoe taarifa polis au anaweza kuwasiliana na namba zifuatazo:
shukran sana - Mdau wa Globu ya Jamii

MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO JANUARY 27,2018

maonesho ya kitalii kufikia kilele jumapili jijini new york

0
0
Mkurugenzi wa East point hotel, ndugu Rashid Adam, na Pia ni Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni ya ZARA TOURS akiwa kwenye maonesho ya kitalii nchini marekani New York times travel show. Watu ni wengi na maonesho ni makubwa New York times travel Sambamba na Balozi wa Tanzania nchini Marekani,Wilson Masilingi, wapo pia Tanzania Tourist Board ngorongoro crater pamoja na Tanapa. Maonesho hayo yanatarajiwa kufikia kilele siku ya Jumapili


DKT. MWANJELWA AISHUKURU CHINA KUONESHA NIA KUISAIDIA TANZANIA

0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa ameishukuru Serikali ya China kwa kuonyesha nia ya kusaidia eneo la utafiti na maendeleo hususan kwenye kuendeleza zao la minazi na mihogo kupitia Kituo cha Utafiti wa Mazao cha Mikocheni JIJINI Dar es Salaam.

Dkt Mwanjelwa amemshukuru Serikali ya China kupitia Naibu Waziri wa Kilimo wa China Dkt Qu Dongyu mara baada ya kufanya ziara katika Kituo hicho mapema leo.


Katika Wasilisho lake kwa ugeni wa Waziri huyo wa Kilimo kutoka China, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti Mikocheni Dkt Fred Tairo amesema Kituo kimekuwa kikiendesha tafiti mbalimbali zenye lengo la kuzuia na kukabiliana na magonjwa hatari ya minazi na mihogo lakini kikwazo kikubwa kimekuwa teknolojia hafifu na uzoefu mdogo katika nyanja hiyo.


Mara baada ya wasilisho hilo Naibu Waziri wa Kilimo wa China ambaye anataaluma ya kilimo amesema Serikali ya China ipo tayari kuisaidia Tanzania kwenye maeneo ya utafiti wa kuzuia magonjwa ya mazao kwenye minazi na mihongo na kutoa wito kwa Watafiti wa Tanzania kuongeza juhudi katika kubunia teknolojia mbazo zitakuwa rahisi na rafiki kwa Wakulima wa Tanzania ili iwe rahisi kuziuza na baadae pato lake lisaidie Kituo hicho kujiendesha.

Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akimweleza mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu namna ambavyo Kituo cha Utafiti Mikocheni kinavyochangia kwenye kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya Kilimo kushoto kwa Dkt. Mwanjelwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dkt. Thomas Kashillilah

Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu katika moja ya maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni

Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Magonjwa ya Mimea Dkt. Deusdeth Mbanzibwa katika moja ya maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni

Aina za mbegu mbalimbali za mihogo ambazo ni Sehemu ya matokeo ya tafiti zinazoendeshwa na Kituo cha Utafiti Mikocheni ambazo Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu walipata nafasi ya kujionea

Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Mikocheni Dkt Aloyce Kulaya ambaye amewaeleza faida za mbegu za mahindi ziligunduliwa Kituoni hapo kupitia Mradi wa WEMA

Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Dkt. Christopher Materu Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Wadudu na Magonjwa kutoka Kituo cha Utafiti Mikocheni namna nzuri ya kudhiti magonjwa ya mimea kwa kutumia wadudu marafiki.

RAIS WA FIFA KUSHUHUDIA FAINAL YA NDONDO SUPER CUP

0
0
Baada ya kufanyika michuano ya Sports Xtra Ndondo Cup kwa mafanikio katika mikoa ya Mwanza na Mbeya sasa yaongeza wigo kwa mabingwa wa mikoa.

jana jijini Mbeya kamati ya mashindano hayo imetangaza rasmi uwepo wa mashindano ya Ndondo Super Cup itakayofanyika jijini Dar es salaam mwezi  februari kwa kushirikisha mabingwa wa mikoa ilipofanyika Sports Xtra Ndondo Cup.

Mwenyekiti wa kamati ya Ndondo Cup Shaffih Dauda amewaambia waandishi wa habari kuwa uwepo wa mashindano hayo ni hitimisho la msimu wa Ndondo Cup 2017 kabla ya kuzinduliwa msimu mpya mwezi wa tatu. "Mashindano hayo yatashirikisha timu nne na kutakua na michezo minne itakayofanyika tarehe 17, 18, 20, na 21 mwezi februari jiji Dar es salaam" amesema Dauda.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya Ndondo Super Cup Gipson George amesema hili ni jambo lingine kubwa kutoka Clouds Media kama support ya wanamichezo wa Tanzania na ulimwenguni kote kwa ujumla hususani ujio wa viongozi wa FIFA nchini. "Hakuna asiyejua Rais wa FIFA atakuwepo hapa, hii ni heshima kubwa tuliyopewa Duniani lazima na sisi tuwaoneshe kuthamini ujio wao"

"Shaffih Dauda amewasiliana na TFF kuona namna ya kushirikiana kutusaidia kuwezesha kumpata rais wa FIFA kuja kwenye fainali ya Ndondo Super Cup ndio maana tumepanga iwe tarehe 21" amesema Gipson.

Gipson ameongeza kuwa mashindano hayo yanaendana na agenda ya Rais wa sasa wa FIFA ya kurudi chini kabisa (grassroot) mpira unapochezwa na watu wa kawaida wenye vipaji vya hali ya juu. Msafara wa FIFA ukiongozwa na Rais Infantino unatarajiwa kuwasili nchini tarehe 21 na siku inayofuata watakua katika mkutano utakaofanyika hapa nchini. 

 Mwenyekiti wa kamati ya Ndondo Cup Shaffih Dauda akifafanua jambo kwenye mkutano huo uliofanyika mapema jana jijini Mbeya.

SERIKALI YAMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUMALIZIA MAJENGO YA CHUO.

0
0
NA WAMJW-MTWARA

SERIKALI Kupitia Wizara ya Afya imeagiza Kampuni ya Ujenzi na Uhandisi Nadhra kumalizia kazi ya kurekebisha kasoro zilizotokana na ujenzi katika majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara ( NTC) na Chuo cha Maafisa Tabibu mkoani humo (COTC) ili kuweza kudahili wanafunzi wengi zaidi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Castro Simba wakati wa ukaguzi wa majengo hayo mkoani Mtwara.

“Majengo haya yalimalizika Desemba 2016 tukatoa kipindi cha mwaka mmoja kujiridhisha na ubora wake lakini kuna baadhi ya maeneo hayajakidhi ubora hivyo mkandarasi anatakiwa kurekebisha ndani ya mwezi mmoja” alisema Bw. Simba.

Aidha Bw. Simba amesema kuwa mradi huo wa kupanua, kukarabati na kujenga majengo hayo yanafanyika katika vyuo vitano nchini ikiwemo Hospitali ya Kairuki Dar es salaam, Bagamoyo, Chuo cha Uuguzi Mtwara (NTC), Chuo Cha Maafisa Tabibu (CoTC) na Chuo cha St. Bakhita cha Sumbawanga.
Mshauri elekezi wa mradi wa upanuzi na ujenzi katika Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc Arch. Benjamini Kasiga aliyevaa fulana ya bluu akiwakilisha mada katika kikao kifupi kilichofanyika chuoni hapo wakati wa ukaguzi wa majengo ya chuo hiko uliofanywa na jopo la Wakaguzi kutoka Wizara ya Afya Mkoani Mtwara.
Mkandarasi kutoka kampuni ya Ujenzi na Uhandisiz Nandhra wa kwanza kushoto akiwapa maelezo baadi ya wakaguzi wa jengo hilo kutoka Wizara ya Afya wakati wa ukaguzi wa majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc uliofanyika leo mkoani humo. 
aimu Mkurugenzi wa kitengo cha kusanifu Majengo Wizara ya Afya Arch. Daniel Mwakasungura aliyevaa shati jekundu akiangalia moja ya sehemu ya jengo la Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc wakati wa ukaguzi wa majengo ya chuo hiko uliofanyika leo mkoani humo, katikati ni Mratibu wa ujenzi huo Dkt. Joachim Catherine na kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Wizara ya Afya Bw. Castro Simba.
engo la wagonjwa Kutoka nje la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini ambalo lipo kwenye ujenzi bado ambapo limegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1. 7 za Kitanzania na lengo la ujenzi wa Hospitali hiyoni kuweza kutoa huduma za kibingwa.Picha Na Wizara ya Afya-MTWARA

SERIKALI YAIPATIA TAASISI YA MOI BILIONI 16 KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA KWA JAMII

0
0
Na WAMJWW. DSM.

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ajali na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) shilingi Bilioni 16 ikiwa ni jitihada za Serikali katika kuboresha huduma zinazotolewa na taasisi hiyo kwa wananchi,

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika ziara yake ya kukagua Ubora wa Huduma zinazotolewa kwa wananchi na taasisi hiyo.

“Serikali imewapa fedha, Bilioni 16 ya kununua vifaa vyakutumika kwenye jingo lao jipya, watafunga mashine mpya za kisasa pamoja na CT-Scan na MRI, Thieta pamoja na kufungua kitengo cha zarura jambo litalopunguza usumbufu kwa wananchi wanaohitaji huduma”, alisema Dkt. Ndugulile.

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile ameahidi kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo katika kuhakikisha wanaiwezesha zaidi ili kuweza kufanya upasuaji mkubwa ndani ya nchi jambo litakalopunguza usumbufu kwa mwananchi mwenye kipato cha chini.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wananchi waliofika kupata huduma katika Taasisi ya Mifupa MOI, katika ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifuatilia idadi ya Dawa katika mfumo wa Kompyuta katika Taasisi ya Mifupa ya MOI.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua utunzwaji na uhifadhi wa dawa, katika Taasisi ya Mifupa ya MOI wakati alipofanya ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (Wakwanza) akiteta jambo na viongozi wa Taasisi ya Mifupa ya MOI wakati alipofanya ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo, wakatika ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Boniface.

WAVUVI WAASWA KUZINGATIA SHERIA,TARATIBU ZA UVUVI KUZILINDA RASILIMALI ZIWA VICTORIA

0
0
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ameteketeza Nyavu haramu 242 zenye thamani ya Sh Mil.242 baada ya wavuvi kuzisalimisha wenyewe katika kisiwa cha Zilagula kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayni Sengerema mkoani Mwanza.

Akizungumza wakati wa uteketezaji wa nyavu hizo, Ulega aliwapongeza wavuvi hao kwa hatua hiyo walioichukua huku akikazia msimamo wa serikali wa kupambana na uvuvi halamu. Pamoja na kuwapongeza huko,Ulega aliwasisitiza wavuvi hao kuzingatia sheria na taratibu za uvuvi ili kuzilinda rasilimali hiyo, ambayo ilikuwa inaelekea kutoweka.

"Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa samaki, wazazi walikuwa wamebaki asilimia nne, wenye hadhi ya kuvuliwa kwa maana ya sentimita 50 hadi 85 wamebaki asilimia tatu na wachanga wamebaki asilimia 93, na kama uvuvi huu ungeendelea maana yake ziwa lingebaki jangwa," alisema Ulega

Waziri Ulega aliwataka wavuvi hao kununua nyavu zinazokubalika kwenye viwanda ambavyo vinauza nyavu hizo,  badala ya kuendelea kutumia nyavu zisizoruhusiwa kwani watapata hasara kwa kuteketezewa na wengine kushtakiwa kwa mujibu wa sheria.

kwa upande wake kiongozi kazi maalumu mkoa wa kioparesheni Sengerema, Charles Lwekaza alisema baada ya kufanya operesheni hiyo iliyoanza mapema Januari mwaka huu, baadhi ya wavuvi waliamua kuzisalimisha nyavu hizo wenyewe bila shuruti.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega  akiongoza shughuli za kuteketeza Nyavu haramu 242 zenye thamani ya Sh Mil.242  baada ya wavuvi kuzisalimisha wenyewe katika kisiwa cha Zilagula  kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza
 .Wavuvi wakisogeza  Nyavu haramu 242 zenye thamani ya Sh Mil.242  eneo la kuchomea  baada ya kuzisalimisha wenyewe katika kisiwa cha Zilagula  kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wavuvi  katika kisiwa cha Zilagula  kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.Picha na Emanuel Massaka.

Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images