Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

WANAKILOSA WATAKIWA KUHIFADHI MAZINGIRA KUEPUKA MAFURIKO

$
0
0
Kufuatia mafuriko yaliyotokea tarehe 11 hadi 19 Januari mwaka huu wilayani Kilosa  na kusababisha athari kwa nyumba 384 kubomoka, nyumba 2,216 kuingiliwa na maji, Kaya 2,542 zenye watu 9,479 kuathirika. Baraza la maafa la wilaya  hiyo limebainisha moja ya sababu kubwa ya mafuriko hayo ni uharibifu wa Mazingira.

Akiongea mara baada ya kutembelea maeneo yaliyoathirika na maafa ya mafuriko wilayani Kilosa, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora, alibainisha kuwa baada  ya  kujionea athari hizo na kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maafa wilayani humo ambayo ilibainisha sababu tano  za kutokea  mafuriko wilayani humo, sababu hizo zote zimeonekana  msingi wake  ni uharibifu wa Mazingira.

“Nimeelezwa hapa Shughuli za kibinadamu ikiwa ni pamoja na makazi, Kilimo kando kando ya mto mkondoa zimechangia mafuriko, pia mto Mkondoa  kubadilisha uelekeo na kubomoa tuta, lakini pia kujaa mchanga katika mto na kupunguza kina cha maji pamoja na bwawa la Kidete lilokuwa likitumika kuhifadhi na kupunguza kasi ya maji ya mto mkondoa kuharibika, niwasihi wanakilosa wahifadhi mazingira kuepuka haya” Alisema Kamuzora.

Kamuzora aliongeza kuwa Halmashauri hiyo haina budi kuzingatia sheria za maafa na mazingira  kwa kuwaelimisha wanakilosa umuhimu wa kuhifadhi mazingira. Aidha aliishauri halmashauri hiyo  kuandaa mfumo wa tahadhari za awali utakao wawezesha wananchi hao kuweza kupata taarifa za awali za mvua kunyesha kutoka katika maeneo ya jirani ili waweze kujiandaa na kukabili maafa ya mafuriko.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akifafanua kwa baadhi ya wajumbe wa Baraza la maafa wilayani Kilosa, umuhimu wa kuhifadhi mazingira kama njia ya kuepuka maafa,  wakati alipotembelea maeneo yaliyoathirika  na  maafa ya mafuriko wilayani humo yaliyotokea tarehe 11 hadi 19 Januari mwaka huu.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora (katikati) akiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Adamu Mgoyi  kutembelea makazi hatarishi ya maafa ya mafuriko ambayo wakazi wa maeneo hayo  wameamuliwa kuhama kwa Amri halali Na KLS/03/208   ya Mkuu wa wilaya hiyo na kugawiwa viwanja 1204 kwenye makazi mapya na salama.
Muonekano wa Sehemu ya Reli ya kati wilayani Kilosa   ilivyoathirika na maafa ya mafuriko yaliyotokea tarehe 11 hadi 19 Januari mwaka huu, baada ya mto mkondoa  kubomoa tuta na kubadili mwelekeo na kumega sehemu ya ardhi ya reli hiyo.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

HAMAD RASHID AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA KILIMO WA CHINA

$
0
0
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohammed akizungumza na Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Mhe. Dkt. QU DONGYU walipokutana katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijijni Dar es Salaam tarehe 26 Januari, 2018 kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikino katika sekta ya kilimo na uvuvi kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na China. Mhe. Dkt. QU DONGYU yupo nchini kwa ziara ya kikazi. 
Mazungumzo kati ya Mhe. Hamad Rashid na Mhe. Dkt. QU DONGYU yakiendelea huku wajumbe wa China na Tanzania wakifuatilia. 
Mhe. Hamad Rashid na Dkt. QU kwa pamoja wakipitia baadhi ya nyaraka za ushirikiano 
Picha ya pamoja kati ya Mhe. Hamad Rashid na Dkt. QU DONGYU pamoja na wajumbe wengine walioshiriki kikao hicho. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki 
Mhe. Hamad Rashid akiagana na Dkt. QU DONGYU mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. 

AZAM FC WASEMA WATAIFUNGA YANGA KESHO

$
0
0
Na Agness Francis, Blog ya Jamii.

MSEMAJI Mkuu wa Azam FC Jaffary Iddy Maganga amesema licha ya Yanga wameshawahi kuutumia Uwanja wa Azam  Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam lakini wanaamini timu yao itaibuka na ushindi na kuchukua pointi tatu ambazo ni muhimu kwao na wamejiandaa vizuri.

Kauli ya Maganga inakuja kuelekea mtanange utakaopigwa kesho kwa kuzikutanisha timu hizo kesho saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex.Azam FC ndio mwenyeji wa mchezo huo."Yanga wameshawahi kuutumia uwanja wetu  kwa ajili ya mechi zao za kirafiki lakini Azam FC ni mara ya kwanza kucheza na kikosi hicho katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,"amesema Maganga.

Akiwa katika Makao Makuu ya Azam, Maganga amesema "Tumejipanga  vizuri na tunaimani tutashinda kwa kunyakua pointi 3 dhidi ya mabingwa watetezi  Yanga,"amesema Maganga.Kwa upande wa Nahodha wa Azam FC, Himid Mau amesema ushindi  kwao ni muhimu japokuwa kikosi cha Yanga kiko vizuri na ni timu kubwa hapa nchini na wanauwezo wa kucheza kabumbu la kiufundi zaidi.

Aidha Kocha Msaidizi AzamFc Iddy Cheche amesema kikosi chake kitaibuka na ushindi kwani maandalizi ni mazuri na wachezaji wako fiti kiakili na kiafya na wapo tayari kupambana kwenye mchezo huo."Tunaitaji ushindi wa pointi 3 ili kukaa kileleni  kumshusha Mnyama Simba,"amesema Cheche.
 Msemaji Mkuu Azam Fc, Jaffary Iddy Maganga akizungumza na waandishi wa habari  katika kuelekea mtanange wa kesho dhidi ya AzamFc na Mabingwa watetezi YangaSC, leo katika Makao makuu ya Azam Chamazi Jijini Dar es Salaam.
 Kocha Msaidizi Azam Fc, Iddy Cheche akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wao wa kesho na wanamatumaini kuwa Ushindi ni wao.
 Nahonda wa kikosi cha AzamFc, Humid Mau Mkami akizungumzia jinsi walivyojipanga vizuri kukabiliana na mechi yao dhidi ya Yanga SC hapo kesho Katika makao makuu ya Azam Chamazi leo Jijini Dar es salaam.
 Beki wa kati wa AzamFc, Agray Mourris akizungumza  na waandishi wa habari kuwa wamejipanga vema dhidi ya mchezo wa kesho, katika makao makuu ya AzamChamazi Complex  leo Jijini Dar es Salaam.

TAASISI ZA SERIKALI KUPEWA MUDA MWAKA MMOJA KUACHA MATUMIZI YA KUNI NA MKAA

YANGA SC KUIVAA AZAM BILA WACHEZAJI WAKE SABA

$
0
0
Na Agness Francis, Globu ya Jamii

MABINGWA Watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC  kesho kukutanaa uso kwa uso na AzamFc  katika  kukamilisha mzunguko  wa kwanza,mchezo utakaochezwa Uwanja  wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza Msemaji Mkuu  wa Yanga SC  Dismas Ten leo Katika Makao makuu yao amesema wachezaji wapo fiti kuelekea mpambano huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki  kuwa wamejipanga kuondoka na ushindi  dhidi ya Azam FC  kuachilia mbali kuwa watakuwa wageni wa mchezo huo mashambulizi yatakuwa ya kutosha katika kuonesha uwezo mkubwa walionao. 

Aidha amesema kikosi hicho kitawakosa wachezaji wake nyota  katika mtanange huo ambao ni Thabani Kamusoko, Amiss Tambwe, Yoana Mkomola, Pato Ngonyani, Donald Ngoma, Abdalah Shaib  ambao wako majeruhi pamoja na Pius  Biswita ambaye anatumukia adhabu ya kadi 3 za njano.  

Pia Msemaji Huyo amesema kuwa "katika mchezo wao wa kesho watamkosa Kocha Msaidizi  shedrack  Nsajigwa ambaye amepa msiba,"amesema Dismas. 

Pia Dismas amesema kwa siku ya kesho Kocha Mkuu George Lwandamina atarejea katika benchi la ufundi kuongoza kikosi chake kama ilivyokuwa hapo awali ikiwa kibali chake kipo hatua za mwisho kukamilika

Mzambia huyo alikuwa akikaa jukwaani wakati wa mechi za Mabingwa hao zikichezwa kwa sababu ya  kumalizika kwa  muda wa kibali chake cha kufanya kazi hapa nchini.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR NA BOHARI YA DAWA (MSD) WASAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO

$
0
0
WIZARA ya Afya ya Zanzibar na Bohari ya Dawa (MSD) wamesaini makubaliano ya ushirikiano wa MSD kuipatia wizara hiyo huduma ya kuwasambazia dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kupitia Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar (CMS)

Hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuhakikisha wananchi wake wanapata dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara.Akizungumza wakati wa hafla hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Asha Abdulla amesema changamoto ya upatikanaji wa dawa ilikuwa kubwa, zikipatikana kwa gharama ya juu na kiwango kidogo walichohitaji ilikuwa inaleta shida wanapoagiza wenyewe.

Ameongeza kuwa hatua hiyo ni muungano shairi,na kuipongeza Bohari ya Dawa (MSD) na Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar (CMS) kwa kutekeleza taratibu zote kwa haraka hadi kufika kusaini makubaliano hayo.Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Rugambwa Bwanakunu amewahakikishia kuwa watawapa huduma nzuri,zenye viwango na kwa wakati na bei nafuu kutokana na kushuka kwa bei ya dawa kwani wananunua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji.

Ameongeza kuwa pamoja na maboresho ya kiutendaji yanayoendelea kufanyika MSD,taasisi hiyo pia imeteuliwa kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa Jumuiya ya nchi za Ukanda wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) hivyo huduma zake zinakubalika kimataifa,hasa katika mnyororo mzima wa ugavi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa CMS Zanzibar , Zahran Ali amesema licha ya makubaliano yaliyofikiwa na kusainiwa, wamekuwa wakishirikiana na MSD kwa huduma mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutoa watalaam wa kuwasaidia kuboresha mnyororo wa ugavi na masuala ya maoteo sahihi ya mahitaji ya wateja.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Rugambwa Bwanakunu (kulia), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Asha Ally Abdullah wakisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano mjini Zanzibar leo. Wengine wanaoshuhudia ni wanasheria wa taasisi hizo mbili.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Rugambwa Bwanakunu, akielezea namna MSD ilivyojipanga kwenye majukumu yake.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Rugambwa Bwanakunu, akimkabidhi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Asha Ally Abdullah , mpango mkakati wa MSD, 2017-2020, ripoti ya maboresho ya MSD na kitini cha bei za bidhaa za MSD (MSD price catalogue)
Kabla ya kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Rugambwa Bwanakunu (kulia) na timu yake walitembelea ghala la kuhifadhi dawa la Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar (CMS)

STEVE NYERERE AMSHUKURU RAIS MAGUFULI

DC SHINYANGA AUNGANA NA WANANCHI KUZUIA MAJI BWAWA LA MWALUKWA YASITOROKE

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Ijumaa Januari 26,2018 ameungana na wananchi wa kijiji na kata ya Mwalukwa iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Vijijini) kuziba ukingo wa bwawa la Mwalukwa ambao umebomoka na kusababisha maji yatoroke.

Matiro aliyekuwa ameambatana na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bahati Kasinyo Mohammed pamoja na baadhi watendaji wa halmashauri akiwemo Injinia wa maji Silvester Mpemba aliungana na wananchi kuziba sehemu ya ukuta/ukingo wa bwawa iliyobomoka na kusababisha maji yavuje/yatoroke.

Bwawa hilo lililojengwa kwa nguvu ya wananchi kati ya mwaka 1941- 1951 linahudumia wananchi wa kata ya Mwalukwa yenye vijiji vinne ambavyo ni Ng’hama,Bulambila,Mwalukwa na Kadoto B lakini pia kijiji cha Mwamadilanha kilichopo katika kata ya Pandagichiza.

Akizungumza wa zoezi hilo la kuziba sehemu ya bwawa inayovuja,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro aliwataka wananchi kutunza bwawa hilo wakati serikali inaendelea na utaratibu wa kufikisha huduma ya maji ya mradi wa Ziwa Victoria katika vijiji ambavyo havijafikiwa na mradi huo.

“Nimekuja hapa kuungana nanyi kuongeza nguvu ya kuzuia maji yasitoke,niwapongeze pia kwa kuja,naomba mtunze bwawa hili kwani kuna maeneo mengine wanatamani kuwa na bwawa kama hili,maafisa watendaji ,viongozi wa sungusungu na viongozi ngazi za vijiji na kata wekeni utaratibu wa kutunza hili bwawa kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo yenu”,alisema Matiro.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (kulia) akiwa amebeba karai la udongo aliouchimba kwa ajili ya kuziba ukingo/ukuta wa bwawa la Mwalukwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (wa tatu kushoto) akiangalia maji yaliyoroka katika bwawa la Mwalukwa lililopo katika kata ya Mwalukwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Kulia ni wananchi wa kijiji cha Mwalukwa wakiweka mchanga kwenye mifuko ili kuzuia maji yasitoroke katika bwawa hilo.
Sehemu ya bwawa la Mwalukwa.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WANANCHI WAPEWA MIEZI SITA KUTOA MAZAO NDANI YA HIFADHI YA RELI

$
0
0
Serikali imetoa miezi sita kwa wananchi wanaolima ndani ya eneo la hifadhi ya reli inayopita Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kuhama eneo hilo baada ya kuvuna mazao yao ili kuhifadhi miundombinu ya reli na kupunguza uharibifu wa miundombinu hiyo.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ua Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake alipotembelea kukagua ukarabati wa reli iliyopo eneo la Kilosa, Morogoro na Gulwe, Dodoma lenye umbali wa kilomita mia moja baada ya kuharibika kwa mvua na Serikali kusitisha usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa mbali mbali na nchi za jirani.


Nditiye amesema kuwa uharibifu wa eneo hilo ni wa kiwango kikubwa kwa kuwa katika kipande cha umbali wa kilomita mia moja zilizoharibika kwa mvua baadhi ya maeneo reli imebomoka, kuhama kwenye njia yake na ardhi husika kuliwa na maji ya mvua yaliyojaa kwenye mto Mkondoa ambao unapita pembezoni mwa reli hiyo. 


Ameongeza kuwa uharibifu huo unasababishwa na shughuli za kibinadamu ambapo wananchi wanaishi na kulima ndani ya mita thelathini upande wa kulia na kushoto mwa reli ambapo ni hifadhi ya miundombinu ya reli na wananchi hawaruhusiwi kutumia eneo hilo kwa shughuli yeyote.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akipanda kiberenge kwenda kukagua ukarabati wa reli iliyoharibika kwa mvua katika eneo la umbali wa kilomita mia moja lililopo kati ya Kilosa, Morogoro na Gulwe, Dodoma.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Bwana Masanja Kaodogosa (wa pili kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) kazi ya kukarabati reli ikiendelea unaofanywa na wafanyakazi wa Shirika hilo baada ya kuharibika kwa mvua wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati huo katika kijiji cha Mkadage kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akishuka kwenye tingatinga inayojaza udongo kwenye eneo lililopo katika kijiji cha Munisagala kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro baada ya kukagua kazi inayoendelea ya kujenga na kurejesha miundombinu ya reli iliyoharibika na mvua wakati wa ziara yake kwenye eneo hilo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Bwana Masanja Kadogosa.
 Kazi ya kujaza udongo kwenye eneo la ukubwa wa mita 170 lililopo katika kijiji cha Munisagala kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro ikiendelea kwa ajili ya kujenga na kurejesha miundombinu ya reli iliyoharibika na mvua.

Mhandisi Mkuu Ujenzi wa TRL Mhandisi Nelson Ntejo akimuonesha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano (kulia) uharibifu wa miundombinu ya reli uliotokea kutokana na mvua wakati wa ziara yake ya kukagua uharibifu huo na ukarabati unaoendelea kati ya Kilosa, Morogoro na Gulwe, Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Bwana Masanja Kadogosa.



HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


RPC TABORA AWAOMBA WADAU KUSAIDIA UJENZI NYUMBA ZA MAKAZI YA POLISI.

$
0
0


Na Tiganya Vincent

JESHI la Polisi Mkoa wa Tabora linakabiliwa na uhaba wa nyumba za kuishi Askari wake jambo linalowafanya wengi kupanga uraini ambapo sio salama kulingana na shughuli zao.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) Wilbroad Mtafungwa wakati wa hafla fupi ya sifa na zawadi kwa askari Polisi vyeo mbalimbali mkoani humo waliotumia Jeshi hilo kwa weledi na nidhamu.

Alisema kuwa ambazo wanaishi Maaskari ni kongwe na chakavu ambapo zinahitaji ukarabati mkubwa na kujengwa mpya ambazo zitasaidia Askari waliopanga uraiani kuondoka huko na kuisha katika nyumba hizo.

SACP Mtafungwa alisema kuwa Askari wanaoishi kambini hivi sasa ni 327 na waliopo uraiani ni 853 na hivyo kufanya Askari wengi kuwa uraiani.Kufuatia hali Kamanda huyo wa Mkoa aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia Jeshi la Polisi ili liweze kupata makazi katika maeneo yao maalum ili waweze kufanyakazi kwa ufanisi wa hali ya juu zaidi.

Alisema kuwa kama wanavyochangia katika Ujenzi wa Vituo mbalimbali vya Polisi ni vema wakachangia pia ujenzi wa nyumba kwa ajili ya makazi ya Polisi ili kuondoa tatizo la ukosefu wa nyumba kwao.

HAKIKISHENI WALIMU WANAPANDA MADARAJA - WAZIRI JAFO

$
0
0
Na Nteghenjwa Hosseah, TAMISEMI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo ameitaka Tume ya Utumishi wa Walimu(TCC) kusimamia na kuhakikisha Walimu wote wanapanda madaraja kwa wakati na kwa mujibu wa Elimu zao ili kupunguza Malalamiko ya Walimu wetu Nchini.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wajumbe wa Kamati ya Tume za Utumishi wa Walimu za Wilaya kwa Mikoa ya Dodoma, Morogoro na Singida uliofanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kilichopo Mkoani Dodoma mapema leo Tarehe 26/01/2017.

Waziri Jafo alisema kuwa kumekuwa na malalamiko, manunguniko na masononeko ya muda mrefu toka kwa Walimu kuhusu suala hili ya Upandaji wa madaraja halifuati taratibu aliyeajiriwa mwaka 2000 na anaweza kuwa sawa na yule aliyeajiriwa mwaka 2008 na wengine wamejiendeleza Kielimi lakin hakuna mabadiliko yoyote madaraja yao.

‘Tume hii ifanye kazi ya kurudisha hadhi ya Walimu, iwajengee heshima na thamani yao katika Jamii, shughulikieni malalamiko yao ya Msingi madaraja yao yapande kwa kuzingatia muda waliokaa kazini, elimu yao na Utendaji wao wa kazi; Hilo lisitegemee “favour” ya Katibu wa Watumishi wa Tume waliopo katika eneo husika’
 Waziri WA Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo akifungua Mkutano wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.
 Katibu wa Tume ya Walimu (kushoto aliyesimama) Mwl. Winifrida G. Rutaindurwa  akiwasilisha taarifa ya Tume katika Mkutano wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bw.Oliva Paul Mhaiki akitoa neon la utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano wa wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.
 Baadhi ya wajumbe wakifuatilia Mkutano wa wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.

Waziri WA Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(Aliyekaa katikati) katika Picha ya Pamoja na Sekretariet ya Mkutano wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YATILIANA SAINI MAKUBALIANO NA BOHARI YA DAWA TANZANIA

$
0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo  .

WIZARA  ya Afya Zanzibar imetiliana saini makubaliano ya ushirikiano na Bohari ya Dawa Tanzania (msd) katika masuala ya uagiziaji dawa na vifaa Tiba kutoka viwandani moja kwa moja na hatua hiyo itaiwezesha Zanzibar kupunguza gharama kubwa ya kuagiza dawa kutoka katika makampuni.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Abdalla Juma alitia saini kwa upande wa Wizara hiyo na Mkurugenzi  Mkuu Laurean Rugambwa Bwanakunu aliiwakilishi Bohari kuu ya Dawa Tanzania katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Zanzibari Mnazimmoja.

Akizungumza baada ya kutiliana sani Bi. Asha Abdalla alisema ushirikiano huo utaisaidi Serikali na wananchi kwa jumla kuwa na uhakika wa upatikanaji dawa na kupunguza mzigo wa kutumia gharama kubwa kuagiza dawa.Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhakikisha  dawa zote zinapatikana  bila usumbufu katika Hospitali na vituo vya afya na kufanikisha  malengo yake ya kuwapatia wananchi  huduma bora za afya.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya ameshauri mashirikiano yaliyoanzishwa baina ya Bohari  Kuu ya Dawa Zanzibar na Bohari Kuu ya Tanzania yawe endelevu na kuwa mfano kwa Taasisi nyengine za pande mbili za Muungano na ukanda mzima wa Afrika Mashariki.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Abdalla Juma na Mkurugenzi Mkuu wa  Bohari ya Dawa Tanzania Laurean Lugambwa Bwanakunu wakitia saina makubaliano ya ushirikiano kati ya Wizara ya Afya  Zanzibar na Bohari Kuu ya Dawa Tanzania katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi Asha Abdalla Juma na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania Laurean Lugambwa Bwanakunu wakibadilisha hati za makubaliano baada ya kutiliana saini makubaliano hy katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania Laurean Lugambwa Bwanakunu akizungumza  baada ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano na Wizara ya Afya Zanzibar.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Abdalla Juma akitoa shukrani zake kwa Uongozi wa Bohari ya Dawa Tanzania  baada ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano kati yao. Picha na Abdalla Omara Maelezo - Zanzibar

RAIS KARIA ATEULIWA NA CAF KUSIMAMIA MECHI YA CHAN KESHO

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Wallace Karia ameteuliwa kwa mara nyingine na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF kuwa kamishna wa mechi ya Morocco na Namibia kwenye fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN itakayochezwa kesho Jumamosi Januari 27, 2018.

Mbali na Rais Karia, Waamuzi watakaochezesha mchezo huo namba 22 utakaochezwa kwenye Uwanja wa Mohamed V Casablanca ni Mahamadou Keita  kutoka Mali  atakuwa mwamuzi wa katikati akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja kutoka Msumbiji Arsenio Chadreque Maringula na mwamuzi msaidizi namba mbili akitokea Burkina Faso  Seydou Tiama wakati mwamuzi wa akiba ni Ghead Grisha  akitokea Misri.

Hii ni mara ya tatu kwa Rais Karia kuteuliwa kuwa kamishna wa mechi zinazoendelea za fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN.

Aliteuliwa kuwa kamishna wa mechi ya ufunguzi ambapo Morocco walicheza na Mauritania Januari 13, 2018 na kisha akateuliwa tena kuwa kamishna wa mechi ya Namibia dhidi ya Zambia ambayo ilichezwa Januari 22, 2018

RWEGASIRA AIAGIZA TBA KUMALIZA UJENZI NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA KWA WAKATI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira (wapili kushoto) akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Askari Magereza, Mhandisi Khadija Salum, alipokua anamuonyesha Katibu Mkuu huyo maeneo mbalimbali ya ujenzi wa nyumba hizo zilizopo Ukonga, jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu huyo aliiagiza TBA kumaliza ujenzi huo kwa muda wa miezi mitano kuanzia sasa.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira ameiagiza Wakala wa Majengo Nchini (TBA) ambao wanajenga nyumba za askari wa Jeshi la Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam, kuukamilisha mradi huo ndani ya miezi mitano kama walivyoahidi.

Katibu Mkuu huyo alitoa agizo hilo, jijini Dar es Salaam jana, wakati alipokua akizungumza na Maafisa wa TBA pamoja na wa Jeshi la Magereza mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mradi huo katika eneo zinapojengwa nyumba hizo, akiwa na lengo la kujua ujenzi ulipofikia mpaka sasa.

“Licha ya maelezo yenu mlioyatoa jinsi mradi huu wa ujenzi unavyoendelea, nimeyasikiliza vizuri, na pi nimeona hatua ya mradi huo ulipofikia, ila fanyeni juu chini muhakikishe mradi huu unakamilika ndani ya miezi hiyo mitano mlioisema hapa nyie wenyewe, muongeze nguvu zaidi katika kuukamilisha mradi huu kwa wakati,” alisema Rwegasira.

Mradi huo una thamani ya shilingi bilioni 10 ambazo zilitolewa na Rais John Magufuli mara baada ya kufanya ziara yake Ukonga mwishoni mwa mwaka juzi na kutoa maelekezo wa ujenzi wa nyumba za makazi ya askari hao katika eneo hilo.

Aidha, kutokana na agizo alilolitoa Katibu Mkuu huyo ambaye ndio msimamizi mkuu na mwenye mradi huo na kukubaliana na TBA katika maelekezo hayo, hivyo ifikapo mwezi Juni mwaka huu, mradi huo unatarajiwa kukamilika.

Ujenzi huo ulianza rasmi mwanzoni mwa mwaka jana 2017, mara baada ya Desemba 19 mwaka juzi 2016, Mtendaji Mkuu wa TBA pamoja na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, walikutana na kusaini mkataba wa makubaliano wa kuanza kwa ujenzi wa nyumba hizo.

DKT TULIA ACKSON APOKEA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE YA WALEMAVU KATUMBA MKOANI MBEYA

$
0
0
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson akipokea Msaada wa kofia kwa ajili ya Watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaosoma katika shule ya Walemavu Katumba kutoka kwa Mkurugenzi wa Human Relief Foundation  Sheikh Khalid Butchery.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson,akipokea Msaada wa Karatasi kwa ajili ya watu wasioona kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa Quintex International Shafiq Dhalla ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya ya Human Relief Foundation .
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson, akipokea Baiskeli ya Walemavu kutoka kwa Meneja wa Miradi wa Human Relief Fondation Mustafa Bunamay  wakati tasisi hiyo ilipokuwa ikikabidhi msaada kwa ajili ya shule ya Maalum Katumba.
  Mkurugenzi wa Human Relief Foundation  Sheikh Khalid Butchery, akimkabidhi alama ya tasisi hiyo Mjumbe wa bodo wa Human Relief Tanzania Mohamed Bahaswan(Big Bon).
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson,akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Taasisi ya Human Relief  Tanzania .


SERIKALI YAWATOA HOFU WAKULIMA MKOANI RUVUMA UHABA WA MBOLEA

$
0
0
Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania TFRA imewatoa hofu wa kulima wa mkoa wa ruvuma, baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika maghala ya kuhifadhia mbolea SONAMCU ,na kukuta shehena ya mbolea ikiwa ya kuridhisha kama anavyobainisha Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya mbolea Lazaro Kitunda.  

MME ATUHUMIWA KUMUUA MKE NA MTOTO WAKE WILAYANI CHATO

$
0
0
Na Joel Maduka-Chato. 

Mkazi wa kijiji cha Minkoto Wilaya ya Chato Mkoani Geita Bw Hoja Kasumbakabo ( 25) anatuhumiwa kumuua mke wake Spensioza Petro (22) kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali mwilini na kisha kumnyonga mtoto Brison Hoja mwenye umri wa miezi mitatu kisha kutokomea kusikojulikana.

Mwenyekiti wa kijiji hicho leo Nkwabi amesema tukio hilo limetokea Januari  24,2018 kuamkia Januari 25 ,kwenye kijiji hicho ambapo ilibainika miili kuonekana chini ya Sakafu ndani ya chumba walichokuwa wanaishi huku mwili wa mwanamke huyo ukiwa na majeraha sehemu ya kooni, mgongoni na tumboni huku utumbo ukiwa nje.

Mzazi wa marehemu Mzee Petro Lusaga ameelezea kusikitisha na tukio hilo na kwamba hakuwahai kuwaona marehemu na mumewe wakiwa na ugomvi kwani kwa kipindi chote walikuwa wakiishi kwa amani bila ya kuwa na malumbano wala kelele zozote ndani ya familia yao. 
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye eneo ambalo kumetokea tukio. 
Jirani wa Familia ambapo kumetokea mauaji Bi,Mariam Shija akizungumza na waandishi wa habari kwa masikitiko juu ya tukio hilo. 
Diwani wa Kata Minkoto , Bw Geroge Magezi akiwasisitiza wananchi kushiriana na jeshi la Polisi kwenye suala la ulinzi na usalama. 
Dk Masanja Mchanganya anayetokea kituo cha afya cha Bwanga akielezea namna ambavyo wamebaini mwili wa marehemu majeraha yaliyopo baada ya kufanya uchunguzi.



Ndoto ya Ujenzi ofisi za walimu yaanza kutimia-Makonda

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa fikira ya kutaka kuwa na ofisi bora za walimu katika mkoa wa Dar es Salaam imeanza kutimia kwa baadhi ofisi kufikia hatua ya upauaji.

Akizungumza leo katika uzinduzi ofisi ya walimu wa shule ya msingi Mapinduzi, Makonda amesema sasa anapata usingizi kuona ndoto yake inanitimia ya kuwapa ofisi nzuri za wanafunzi.

Makonda amesema kuwa wakati alipikuja na wazo hilo alijua hali ni kazi ngumu lakini kutokana na msukumo wa sasa chini ya Serikali ya Dk. John Pombe Magufuli ya elimu bure inatimia.Amesema maendeleo yeyote kwa watoto wa kitanzania yanaanza kwa walimu ambao ndio wataweza kuzalishwa watoto hao kupata elimu na kuinuka kiuchumi.

“Mtu mwenye umasikini hana nyumba ambayo haina bati kamwe hawezi mtu kuwa na nyumba ya bati ili aweze kuwa na nyumba hiyo lazima apate elimu”amesema.Katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa huyo amesema wanaonunua maeneo ya shule ni kukamatwa pamoja na wanaonunua wakamatwe ambapo mtu mmoja Ajay Shohan amekamatwa kwa kununua eneo la shule ya msingi Mapinduzi.

Katika hafla ya uzinduzi wa upauji wa shule msingi Mapinduzi kampuni ya simu za mkononi ya Halotel imetoa mchango wa fedha taslim Shilingi milioni Hamsini (50,000,000) kwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni moja ya utekelezaji wa kampuni hiyo katika kuunga mkono jitihada za serikali na ofisi hiyo katika kuboresha sekta ya elimu Tanzania, kupitia ujenzi wa ofisi za walimu kwa shule 402 kati ya hizo shule 295 ni za elimu ya awali/msingi na shule 107 ni za sekondari zilizoko mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipokea Hundi ya Milioni 50 kutoka kampuni ya Hallotel kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za walimu 402 Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika uzinduzi wa kukamalika kwa ujenzi wa ofisi ya walimu wa shule ya msingi Mapinduzi, leo jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Solomon Urio akitoa taarifa ya hatua za mbalimbali za ujenzi wa ofisi za walimu leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa upauaji wa ofisi ya walimu shule ya msingi Mapinduzi leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipaua jengo la ofisi ya walimu katika shule msingi Mapinduzi leo jijini Dar es Salaam.

WATU WASIYOJULIKANA WACHOMA MOTO BANDA LA VIJANA KIKUNDI CHA KUJIKOMBOA GROUP PEMBA

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba Abeid Juma Ali akikagua banda la vijana wa kikundi cha Kujikomboa Group kiliopo shehia ya Gando Ziwengi Wilaya ya Wete lililoteketezwa kwa moto na watu wasiyojuilikana usiku wakuamkia leo Januari 26, 2018
 Mkuu wa Wilaya ya Wete Abeid Juma Ali akizungumza na vijana wa kikundi cha Kujikomboa Group cha shehia ya Gando Ziwengi alipofika kuwafariji.

Eneo la shamba la matunda na alizeti linaloshughulikiwa na kikundi cha Kujikomboa Group cha Gando Ziwengi.Picha na Makame Mshenga Pemba.

Donald Trump atuma salamu kwa viongozi wa Afrika

$
0
0
Rais wa Marekani Donald Trump amemuomba Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kufikisha salamu zake kwa viongozi wengine wa mataifa wanachama wa AU.

Viongozi hao wawili wamekutana mjini Davos, Uswizi pambizoni mwa mkutano wa viongozi na watu mashuhuri kuhusu uchumi na biashara duniani.

Mkutano huo wa Kagame na Trump umetokea wiki chache baada ya kiongozi huyo wa Marekani kuyaeleza mataifa ya Afrika kama "machafu" au mataifa ya "mabwege".

Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali na viongozi wa AU na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama vile Botswana na Ghana.Bw Trump amekanusha kwamba alitumia neno hilo kuyaelezea mataifa ya Afrika.

Hata hivyo alikiri kwamba alitumia maneno makali akiyaeleza mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador alipokuwa anazungumzia wahamiaji wanaoingia Marekani.

Lakini katika mkutano wake na Kagame pambizoni mwa Mkutano wa Uchumi wa Dunia mjini Davos, Trump hajaonyesha dalili zozote za majuto kuhusu tamko lake la awali kuhusu Afrika.

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images