Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110095 articles
Browse latest View live

UNNewsKiswahili: Habari mbalimbali za leo duniani


SENSEI RUMADHA FUNDI NA GOJU RYU KARATE PART 1

MAGAZETI YA IJUMAA LEO JANUARY 26,2018

LUKUVI AWAPOZA WANANCHI WA KIGOTO, KABUHORO MWANZA

$
0
0
Na Baltazar Mashaka, Mwanza.

WANANCHI wanaomiliki nyumba 664 katika mitaa ya Kigoto na Kabuhoro katika Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza wametakiwa kuwa na subira wakati serikali ikitafuta ufumbuzi wa mgogoro uliopo kati yao na Jeshi la Polisi.

Pia wamezuiwa kujenga nyumba zingine mpya kwenye maeneo ya mitaa yao na badala yake wawe walinzi na kuonya watakaothubutu kujenga hawatalipwa fidia ambapo awali walitakiwa kuondoka na kupisha eneo hilo baada ya kuandikiwa ilani ya siku saba na jeshi la polisi.

Akizungumza na wananchi hao Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alisema serikali imesikia kilio chao na hivyo amekuja chunguza mgogoro huo ili ifanye uamuzi wa kuutatua.

 Alisema serikali inataka kufahamu mahitaji ya wananchi na polisi na kuonya wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo wasithubutu kujenga (kuongeza) majengo mengine zaidi ya yaliyopo sasa na watakaokaidi hawatalipwa fidia.

“Nimekuja kuangalia mgogoro huu na kuchungumza jambo hili ili serikali ifanye uamuzi. Msidhani nina majibu, majibu yatatolewa ndani ya mwaka mmoja lakini msituhubutu kuongeza nyumba zingine zaidi, kuweni walinzi wa maeneo haya na tunataka muwe maeneo mzuri ili tuwarasimishie,”alisema Lukuvi.

Waziri huyo wa ardhi alisisitiza baada ya uchunguzi atamshauri vizuri Rais John Magufuli namna ya kumaliza mgogoro huo baina ya wananchi na taasisi hiyo ya serikali.

Lukuvi alieleza eneo la Kigoto ambalo Polisi inadai inataka kujenga Chuo cha Polisi wanamaji, nyumba za askari na  gati la boti na meli za doria zinaweza kujengwa popote lakini eneo hilo lazima lipangwe upya hata kama matumizi yakibadilishwa kwa kuwa haiwezekani watu waishi kwenye nyumba za ovyo ovyo.

“Miaka 70 hadi leo kwa nini ujenzi haukuzuiwa,hakuna viongozi hapa na kama mngewashirikisha wangewasaidia kuzuia.Je, upembuzi yakinifu ulifanyika kwenye eneo mnalotaka kujenga mdomo huo wa gati la boti za polisi?

Aidha akizungumza kwa niaba ya wenzao ,Ferdinand Mtundubalo alimweleza Waziri kuwa hawana tatizo na ujenzi wa gati la boti za polisi isipokuwa warasimishiwe makazi yao ili waondokanane na mgogoro huo.

Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi aliwataka wataalamu wa wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela waainishe eneo la Uwanja wa Ndege wa Mwanza na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha Ihale ili kila mmoja alinde eneo lake.

Pia alishauri eneo la Nyamwilolelwa litakalobaki baada ya kutengwa la uwanja wa ndege na JWTZ lipimwe wapewe wananchi wa eneo wapatao 1,961 na kuhusu barabara ya Mwanza –Igombe uamuzi wa Rais Magufuli ubaki ulivyo na uheshimiwe. 
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza jambo amlipozuru kwenye eneo la Kigoto lenye mgogoro kati ya wananchi na polisi. 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi akimfafanulia jambo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipozuru eneo la Kigoto Ilemela ambalo lina mgogoro baina ya wananchi na jeshi la polisi. Kushoro wa kwanza ni Meya wa Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga, wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.
Waziri wa  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akimuuliza Meneja majengo na Mkaguzi wa polisi, Daud Mwakalobo (kulia) kama eneo wanalotaka kujenga gati la boti na nyumba za askari polisi liko kwenye ramani. PICHA ZOTE NA BALTAZAR MASHAKA

MWILI WA MAREHEMU LULU SYLVESTER MATTUNDA LEMA WAWASILI KIJIJINI NRONGA KWA MAZISHI

$
0
0
Marehemu Lulu Sylvester Mattunda Lema.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu, Lulu Sylvester Mattunda Lema mara baada ya kuwasili nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi,Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro Januari 25, 2018. Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo Ijumaa Januari 26, 2018. 
Sylvester Mattunda Lema (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na watoto wake mara baada ya kuwasili Nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Hai kwa taratibu za mazishi yatakayofanyika Leo Saa Nane Mchana, Januari 26, 2018 katika makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo
Mwinjilisti wa Usharika wa Nronga, Donald Lema akizungumza jambo baada ya mwili wa marehemu, Lulu Sylvester Mattunda Lema ulipowasili katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro .

MKURUGENZI HALMASHAURI WILAYA YA MBULU AKAGUA UJENZI WA MIUNDOMBINU SHULE YAEDA CHINI MBULU

$
0
0
Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imepokea Tsh 281,500,000 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaenda Chini na shule ya Msingi Domanga. Fedha hizi ni sehemu ya Zaidi ya Tsh 17 Bilioni zilizotolewa na Serikali kwa baadhi ya Halmashauri nchini kuboresha miundo mbinu ya shule za msingi na sekondari!

Ni lengo la Serikali ya awamu ya tano chini Rais Dr. John Pombe Magufuli kuondoa kero katika sekta ya elimu nchini. Tumeshaanza maandalizi ya ujenzi na kukamilisha kwa wakati ufanisi wa hali ya juu katika shule hizo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga akiongozana na Diwani kata ya Yaeda Chini (CCM) Bryson, wakati Mkurugenzi huyo alipokagua ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaeda Chini na shule ya Msingi Domanga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga akiongozana na Afisa Elimu Wilaya ya Mbulu ,Ludovic Longino kulia na Afisa ugavi wilaya ya Mbulu Faustine Safari kushoto, wakati Mkurugenzi huyo alipokagua ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaeda Chini na shule ya Msingi Domanga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu  Hudson Kamoga akiongozana na Afisa Elimu Wilaya ya Mbulu Ludovic Longino kulia na Afisa ugavi wilaya ya Mbulu Bw. Faustine Safari kushoto wakati Mkurugenzi huyo alipokagua ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaeda Chini na shule ya Msingi Domanga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa maafisa wa Wilaya ya Mbulu wakati Mkurugenzi huyo alipokagua ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaenda Chini na shule ya Msingi Domanga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akishiriki katika ujenzi wa Msingi wa shule wakati alipokagua ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaenda Chini na shule ya Msingi Domanga

RC MAKONDA AZINDUA JENGO LA UPASUAJI WAJAWAZITO HOSPITALI YA MWANANYAMALA

$
0
0

IMG-20180125-WA0078
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda jana  amezindua Jengo la Upasuaji katika Hospital ya Rufaa ya Mwananyamala yenye thamani ya zaidi ya Million 420, inayoenda kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto wakati wa kujifungua.

Jengo hilo la kisasa lenye Gorofa Moja limepewa jina la HON. PAUL MAKONDA OBSTETRIC THEATRE kama sehemu ya kuenzi jitihada za RC Makonda kuboresha Sekta ya Afya kwa kumtafuta mfadhili GSM Foundation aliekubali kujenga Jengo hilo bila kutumia pesa ya Serikali.

RC Makonda aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo hilo mnamo March 13 ,siku ambayo ndio aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa na sasa jengo limekamilika likiwa na Vyumba Viwili vya Upasuaji vyenye uwezo wa kufanya upasuaji kwa wakati mmoja na kuhudumia Wagonjwa 20 kwa siku.

RC Makonda amesema kabla ya kujengwa kwa jengo hilo Wagonjwa walikuwa wakisongamana kusubiri kufanyiwa upasuaji kitendo kilichokuwa kikisababisha Maumivu Makali na Vifo vya Mama na Mtoto, lakini kupitia jengo hilo vifo vinaenda kupungua.

Makonda ameishukuru GSM Foundation kwa kufanikisha Ujenzi wa Jengo hilo ambapo inakadiriwa Hospital ya Mwananyamala inapokea Wagonjwa kuanzia 1,500 hadi 2,000 kwa siku na Kati ya hao ni Wajawazito wanaohitaji huduma ya Upasuaji.

RC Makonda amesema hadi sasa zaidi ya Kinamama 55 wamejifungua salama ndani ya jengo hilo na linaendelea kupokea kinamama Wajawazito kila kukicha. 

Baadhi ya Kinamama waliofanyiwa upasuaji wamemshukuru RC Makonda kuwajengea jengo zuri la upasuaji linalowawezesha madaktari kufanya kazi yao pasipokuwa na usumbufu na wanafurahia kuona huduma za upasuaji zinaenda vizuri. 

Viongozi waliohudhuriwa uzinduzi huo akiwemo Mkuu wa wilaya ya kinondoni, Mstahiki Meya wa Kinondoni, watendaji wa Afya na wananchi wamempongeza RC Makonda kwa jitiada kubwa anazofanya kuboresha sekta ya Afya Dar es salaam.

Dk.Shein Akutana na Sheikh Saud Bin Saqr Katika Makaazi Yake

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza Mtawala wa Ras-Al-Khaimah Mtukufu Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi na kufanya nae mazungumzo yaliolenga kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya pande mbili hizo.

Mazungumzo hayo yaliofanyika katika makaazi ya Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi mjini Ras-Al-Khaimah, ambapo viongozi hao kwa pamoja walieleza haja ya kuendeleza uhusiano na kuimarisha mashirikiano katika kuinua sekta za maendeleo ikiwemo sekta ya mafuta na gesi asilia. 

Aidha, viongozi hao walizungumza juu ya hatua zinazoendelea katika suala zima la utafiti wa mafuta na gesi asilia ambapo katika mazungumzo hayo walieleza haja ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa pamoja ili kufikia lengo la kuipaisha Zanzibar kiuchumi na kimaendeleo.

Katika maelezo yake, Dk. Shein alitoa shukrani kwa kiongozi huyo kutokana na juhudi zake za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar na kumpongeza kiongozi huyo kwa mafanikio yaliopatikana nchini humo katika kipindi kifupi.

Rais Dk. Shein alimueleza kiongozi huyo kuwa Zanzibar ina mengi ya kujifunza kutoka kwa ndugu zao wa Ras Al Khaimah na iko tayari kupanua wigo wa maendeleo kutoka nchini humo kwani inatambua mafanikio yaliopatikana kutokana na mikakati iliyowekwa.

Pamoja na hayo, viongozi hao kwa pamoja walizungumzia hatua zaidi zinazohitajika katika kuimarisha ushirikiano kati ya Zanzibar na Ras Al Khaimah katika sekta za maendeleo ikiwa ni pamoja na kupanga mipango madhubuti katika malengo yaliokusudiwa ya hapo baadae.

Nae Kiongozi huyo alieleza kuwa Ras Al Khaimah itaendeleza uhusiano na ushirikiano wake na Zanzibar hasa katika sekta hizo za maendeleo na kusisitiza kuwa uhusiano na ushirikiano huo utaletea maendeleo makubwa Zanzibar hasa kwa kutambua kuwa jambo hilo limo kwenye dhati ya moyo wake.


Umoja wa Mataifa Tanzania wachagua vijana watakaoiwakilisha Tanzania Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC) 2018 jijini New York

$
0
0
Umoja wa Mataifa Tanzania wachagua vijana watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC) 2018 jijini New YorkRahma Mwita Abdallah na Paschal Masulu wamechaguliwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC) jijini New York. 

Wawili hao walichaguliwa kupitia shindano lililoendeshwa na Umoja wa Mataifa kupitia mitandao ya kijamii ambapo walitakiwa kupakia video ya dakika moja wakieleza kwanini wachaguliwe kuwawakilisha vijana wa Tanzania kwenye Baraza la ECOSOC. 
Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) akiongea na vijana Rahma Mwita Abdallah na Paschal Masul waliochaguliwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC) jijini New York kabla ya kuwakabidhi bendera ya Tanzania na Umoja wa Mataifa.

 Baraza hilo linakutanisha vijana viongozi kutoka ulimwenguni kwote kujiunga na waunda sera kujadili changamoto mbalimbali zinazowakumba vijana katika nchi wanazotoka na jinsi ya kuzitatua. Pia Mkutano huo unatoa fursa kwa vijana kutoka nchi balimbali kubadilishana ujuzi wa namna ya kutatua changamoto za vijana katika nchi zao.Mkutano huo utafanyika kuanzia Jumatatu ya Januari 30 hadi 31 na unaweza kupata tarifa za safari ya Rahman na Paschal kwa kufuatilia akaunti za Umoja wa Mataifa katika Twitter @UnitedNationsTZ na Instagram @unitednationstzBw. Rodrguez akiwakabidhi vijana mfano wa hundi kama mchango wa Umoja wa Mataifa Tanzania ili kuwawezesha vijana hao kuhudhiria Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC).Bw. Rodrigues akiwakabidhi Rahma na Paschal bendera za Tanzania na Umoja wa Mataifa kama utambulisho wao kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC).Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez katika picha na Rahma pamoja na Paschal wakiwa wameshika bendera ya Umoja wa Mataifa Tayari kuwawakilisha vijana wa Tanzania kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC).

Rais Shein Atembelea Kisiwa na Utalii Cha Al Marjan Nchini Ras Al Khaimah.

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mkurugenzi wa Kisiwa cha Utalii cha Al Marjan Ras Al Khaimah, Abdullah Al Abdouli wakitembelea katika moja ya Hoteli zilizo jengwa katika kisiwa hicho cha Kitalii Nchini Ras Al Khaimah. Rais wa Zanzibar akiendelea na ziara yake katika Nchi za Falme za Kiarabu UAE.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mama Mwanamwema Shein na Viongozi wa Serikali wakipata maelezo ya picha ya majengo ya mahoteli ya Kitalii yaliojengwa katika eneo la kisiwa  hicho cha Al Marjan Nchini Ras Al Khaimah kulia Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Kisiwa cha Al Marjan Abdullah Al Abdouli, wakisikiliza maelezo ya picha za majengo yaliojengwa katika kisiwa hicho.




MOJA ya majengo ya Mahoteli ya Kitalii yaliojengwa katika eneo hilo ka kisiwa hicho cha Al Marjan Nchini Ras Al Khaimah kama linavyoonekana


UJUMBE wa Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakitembelea moja ya hoteli ya kitalii katika Kisiwa cha Kitalii cha Al Marjan Nchini Ras Khaimah katika ukanda wa kisiwa hicho

WAZIRI UMMY AIPIGA 'JEKI' KLABU YA AFRICAN SPORTS

$
0
0
MBUNGE wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu amekabidhi chakula na vifaa vyengine kwa ajili ya kuisaidia timu ya African Sports ya Jijini Tanga kujikimu katika kambi yao iliyopo maeneo ya Donge Tanga.

Msaada huo umefika wakati muafaka ambapo timu hiyo inajiandaa kuelekea michezo yao miwili iliyobakia ya ligi ya Taifa Daraja la Pili inayomalizika ndani ya wiki mbili.Miongoni mwa vitu alivyokabidhi ni pamoja na Mchele kg 100,Unga wa ngano kg 50,Unga wa sembe kg 100,Maharage kg 50,sukari kg 50,mafuta ya kupikia lita 20,chumvi,sabuni na dawa za meno ambavyo vilikabidhiwa na Khatibu Kilenga kwa niaba ya Waziri Ummy.


Akizungumza mara baada ya kukabidhi kwa niaba ya Waziri Ummy ,Kilenga aliwaambia wametakiwa heri katika michezo miwili iliyosalia kwenye michuano hiyo.Aidha pia ni matumaini yake kwamba katika michezo hiyo timu hiyo itaweka bidii kubwa kuhakikisha inashinda .Naye kwa upande wake,Katibu wa timu ya African Sports,Ismail Masoud alimshukuru Waziri Ummy kwa sapoti kubwa anayoionyesha na kwamba sasa wachezaji wamepata hari na nguvu ya kushinda mechi mbili zilizobakia.

Alisema mipango ya kushinda michezo hiyo iliyobakia ni mizuri ili kuhakikisha hawashuki daraja huku akiwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia timu hiyo kwani ni ya wananchi."Tanga ina enye ,na enye ni sisi,Shime wana Tanga'Tanga Kwanza.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Mwakilishi wa MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu,Khatibu Kilenga kushoto akimkabidhi unga nahodha wa timu ya African Sports ambapo kiongozi huyo alitoa mchele kg100,unga wa sembe kg 100,Ngano kg 50,maharage kg 50,sukari kg 50,mafuta ya kupikia lita 20,chumvi ,sabuni na dawa za meno

Sehemu ya vitu vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu

Katibu wa Klabu ya African Sports,Ismail Masoud katika aliyeshika funguo akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo ambapo alimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo ambao utakuwa chachu ya timu hiyo kumaliza ligi wanayoshiriki kwa ushindi 

MILIONI 20 ZATUMIKA KAMPENI UPANDAJI MITI WILAYANI IGUNGA

$
0
0
NA TIGANYA VINCENTRS-TABORA

JUMLA ya shilingi milioni 20 zimetuma katika kampeni ya upandaji miti katika maeneo mbalimbali wilayani Igunga.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Revocatus Kuuli wakati wa uzinduzi wa upandaji miti kwa wanachuo wa Chuo cha Sayansi za Afya Nkinga uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora

Alisema kuwa fedha hizo zimetumika katika ununuzi wa miche ya miti, uoteshaji wa miche na zoezi zima la upandaji katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kurudisha uoto wa asili.

Kuuli alisema kuwa kutokana na zoezi hilo kutumia fedha za Halmashauri hiyo zinazotokana na vyanzo vyake wataendelea kupambana na watu wote wanaoenesha uharibifu katika mistu, vyanzo vya maji na wanachunga mifugo katika maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria ili kuhakikisha matunda ya fedha hizo yanaonekana.

Akiongea katika nyakati tofauti na Wanachuo wa Ndala, Nkinga na Kitongo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema kuwa kundi hilo la wasomi ni kundi muhimu sana katika kampeni zinazoendelea Mkoani humo.

Alisema kuwa kundi hilo haliwezi kubaki kuwa watazamaji katika zoezi la upandaji miti linapaswa kuwa sehemu ya mradi huo unaoendelea maeneo mbalimbali mkoani humo ili nao wabakize alama kama waliwahi kukaa na kupata elimu na hatimaye kushirikia katika utunzaji mazingira.

Mwanri alisema kuwa hatua hiyo itabaki katika kumbukumbu zao binafisi na za Mkoa wa Tabora.Alisema kuwa ni jukumu la Wakufunzi kuhakikisha kila mwanachuo kama ilivyo katika Shule za Msingi na Sekondari anakuwa na mti mmoja ambao atautunza katika siku zote ambazo yuko masomoni.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Nkinga Dkt. Yohana Masonda akisoma taarifa ya Chuo cha sayansi za Afya Nkinga alimpongeza Mkuu huyo wa Mkoa kwa uamuzi wake wa kutumia wanachu mbalimbali kupanda miti katika maeneo yao nay ale ya jamii.

Alisema kuwa wao katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuu ya ile ya Mkoa katika suala la uhifadhi wa mazingira tayari wameshapanda miti maji 200 na wanatarajia kuongeza mingine 600 ili kuifanya Igunga kuwa ya kijani.

BREAKING NEWZZZZ:ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TBC TIDO MHANDO AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU LEO

$
0
0
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la utangazaji TBC, Tido Mhando, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Azam Media akiwa katika ukumbi wa wazi  wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akisubiri kusomewa mashtaka yanayomkabili.Habari zaidi inakuja.

Updates kutoka Mahakama ya Kisutu

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Wa shirika la Utangazaji nchini, Tido Mhando, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtka ya uhujumu uchumi.


Mhando ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Azam Media anakabiliwa na mashtaka manne ya matumizi mabaya ya madaraka na shtaka moja la kuisababishia TBC hasara  ya zaidi ya sh. Milioni 887.

WATAALAM MASUALA YA MAAFA WAKUTAKANA

$
0
0
 Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig. Jen. Mbazi Msuya akifungua kikao cha Wataalam wa Maandalizi  wa Kikao cha Baraza la Usimamizi wa Maafa Tanzania kilichofanyika Januari 25, 2018 katika Ukumbi wa Mikutano  Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
 Mratibu wa Maafa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Charles Msangi akiwasilisha mada wakati wa kikao cha Wataalam wa Maandalizi  wa Kikao cha Baraza la Usimamizi wa Maafa Tanzania kilichofanyika Januari 25, 2018 katika Ukumbi wa Mikutano  Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
 Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Tafiti) Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu akichangia hoja wakati wa Kikao cha Wataalamu wa masuala ya Maafa kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
 Afisa Kilimo Wizara ya Kilimo (Idara ya Usalama wa Chakula) Bw.Robert Dimoso akiuliza swali wakati wa Kikao cha Wataalamu wa masuala ya Maafa kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
 Mhandisi Mwandamizi kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bi. Kalunde Malale akichangia hoja wakati wa Kikao cha Wataalamu wa masuala ya Maafa kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
 Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Wataalamu wa masuala ya Maafa wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kutoka kwa Mratibu wa Maafa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Charles Msangi (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Wataalamu wa masuala ya Maafa kilichofanyika Januari 25, 2018 Dodoma.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig. Jen. Mbazi Msuya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kikao cha Wataalamu wa masuala ya Maafa kilichofanyika Januari 25, 2018 Dodoma.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU - DODOMA)

ZIMAMOTO NCHINI YAPATA TUZO YA UTENDAJI BORA YA MWAKA 2017

$
0
0
 Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (katikati) akiongea na Waandishi wa habari wa radio Times Fm wakati akitoa taarifa ya Mafanikio ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ya mwaka 2017, kabla ya kukabidhiwa Tuzo na Cheti cha heshima kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kushoto) kwa kutambua utendaji kazi wa Jeshi hilo, Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.
 Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kushoto) akitoa pongezi na shukrani kwa Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (katikati) wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo na cheti cha heshima kwa kutambua utendaji kazi wa jeshi hilo (kulia) ni Mkurugenzi wa vipindi Times Fm Bw. Amani Misana wakati wa Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.
 Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kushoto) akimkabidhi Cheti cha heshima Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (katikati) kwa kutambua utendaji kazi wa Jeshi hilo wakati wa Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.
 Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko akipokea Tuzo ya heshima toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa kutokana na utendaji kazi wa Jeshi hilo kwa jamii na Taifa kwa ujumla (kulia) ni Mkurugenzi wa vipindi Times Fm Bw. Amani Misana wakati wa Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.
Picha ya Pamoja, Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (wa nne kulia) akiwa na Viongozi Waandamizi wa Jeshi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kulia kwake) na (kushoto kwake) ni Mkurugenzi wa vipindi Times Fm Bw. Amani Misana Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

JPM na Mama Janeth wampa Wastara msaada wa pesa za matibabu tabata Sanene jijni Dar leo

$
0
0
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwasilisha mchango wa shilingi milioni 15 kwa mwigizaji Wastara  kutoka kwa Rais Dkt Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli kwa ajili ya matibabu. SHILAWADU ndio waliomuibua mwigizaji huyo kiasi hata ugonjwa wake uliwagusa wengi pamoja na JPM na mkewe.

Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwa na mwigizaji Wastara pamoja na SHILAWADU baada ya kumkabidhi msaada wa 15m/- kutoka kwa Rais Dkt Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli kwa ajili ya matibabu. Pia aliwasilisha mchango wa sh milioni moja na laki tisa toka kwa wasaidizi wa Rais. SHILAWADU ndio waliomuibua mwigizaji huyo kiasi hata ugonjwa wake uliwagusa wengi pamoja na JPM na mkewe.

ESRF, PROF. JIN SANG LEE WAANDAA MHADHARA KUBADILISHANA UZOEFU NYANJA YA SAYANSI, TEKNOLOJIA

$
0
0
Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Profesa Jin Sang LEE kutoka Chuo Kikuu cha New York – Korea (SUNY Korea) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) waliandaa mhadhara wa kubadilisha uzoefu ili kuweza kufikia malengo ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Mhadhara huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF na kufunguliwa na Mheshimiwa Anthony Mtaka – Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Akizungumza katika mhadhara huo, Mheshimiwa Mtaka alisema, nchi yetu imejipanga kufikia uchumi wa kati kwa kuwa na sera na mikakati mbalimbali.
 Aliongeza kwa kusema kilichobakia ni kuendelea kuitekeleza sera na mikakati hiyo ili kutimiza ndoto ya kuwa na uchumi wa kati. Kwa upande wake, Dkt. Tausi Kida- Mkurugenzi Mtendaji ESRF alisema, mhadhara huo umekuja wakati muafaka kwa kuwa nchi yetu imedhamiria kufikia Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, ambapo sekta binafsi itakuwa injini ya ukuwaji wa uchumi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mheshimiwa Anthony Mtaka ofisini kwake kabla ya ufunguzi wa warsha ambayo ilijadili mafanikio ya Korea Kusini katika viwanda na nini kinaweza kuigwa na watanzania kufikia uchumi wa kati mwaka 2025 iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Profesa Jin Sang LEE katika Mhadhara wake alianza kubadilishana uzoefu kwa kuelezea mapinduzi ya uchumi katika Korea ya kusini kuanzia miaka ya 1960. Alisema katika miaka hiyo Serikali ya Korea ya Kusini iliweka vipaumbele kadhaa ikiwamo kuondoa umaskini na kukuza viwanda. Katika miaka hiyo serikali ilijikita katika uchumi wa viwanda vidogo vidogo na wakijitahidi kuuza ndani na nje bidhaa ndogondogo. Katika miaka ya sabini Korea ilipiga hatua nyingine kwa kupanua techonoljia ili kuongeza tija katika viwanda vyake, Hayo yalikuwa yakifanywa kwa ushirikiano wa serikali na sekta binafsi. 
Katika miaka ya themanini, nchi ilizidi kujikita katika sayansi, teknolojia na ubunifu, waliweza kuwafundisha watu wake ili kuwa na wataalamu wengi ambao watasaidia katika kubuni mambo muhimu ya maendeleo. Katika miaka ya tisini, Korea Kusini ilinza kujikita katika kujiimarisha katika teknolojia ambayo iliyohitajika kimataifa kama vile teknolojia ya Tehama. Na katika miaka ya 2000, nchi ilieweza kuwa na mapinduzi makubwa ya viwanda vya kubuni bidhaa mbalimbali kama vile simu za mikononi, komptuta, magari n.k.
 Hayo yote ni matokeo ya uzalendo, kusomesha wataalamu, kuanzisha na kusimamia masuala ya utafiti na maendeleo, kufanyakazi kwa bidii kwa wananchi wa Korea Kusini. Masuala ya Utafiti na Maendeleo ni nguzo imara katika kuendesha sekta mbalimbali katika nchi. Alisisitiza pia , ushirikiano kati ya serikali na vyuo vikuu amboko ndio sehemu ambayo kutafumbuliwa na kukuzwa kwa sayansi, teknolojia na ubunifu. Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF Bi. Margareth Nzuki (kulia) akiongozana na mgeni mzungumzaji Profesa Jin-Sang LEE kutoka Chuo Kikuu cha New York-( SUNY)- Korea (katikati) kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Profesa Lee alisema katika upande wa viwanda Tanzania inatakiwa kuwa na viwanda vya msingi, masoko na kuwa na uelewa wa soko la kimataifa. Aidha kama taifa linatakiwa kuwa na nadharia zinazofaa kwa ajili ya kubeba mfumo huo wa viwanda kama Pia vyuo vikuu vinatakiwa kutengeneza wataalamu wa ngazi za juu watakaoweza kusaidia sekta mtambuka kwenye masuala ya sayansi na teknolojia kufanyakazi. Aidha ameshauri serikali kujenga uwezo wa viwanda nchini kwa kuviwezesha kushindana huku ikitilia maanani soko la ndani na nje. Katika hilo inatakiwa kukuza ujasirimali kwa kuwezesha maarifa katika menejimenti, kujiamini na kutengeneza ushirika na makampuni ya kigeni 
 Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mheshimiwa Anthony Mtaka akitoa neno fupi la ufunguzi wa warsha ambayo ilijadili mafanikio ya Korea Kusini katika viwanda na nini kinaweza kuigwa na watanzania kufikia uchumi wa kati mwaka 2025 iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Aidha alihimiza uzalendo na kujitosa huku mtu akiwa na mawazo, maono na mikakati ya kusonga mbele huku utekelezaji wa mambo kuelekea katika ustawi wa viwanda ukiambatana na sera .

Profesa Lee aliyasema hayo katika warsha ambayo ilijadili mafanikio ya Korea Kusini katika viwanda na nini kinaweza kuigwa na watanzania kufikia uchumi wa kati mwaka 2025. Alikuwa akizungumza kama mgeni mwalikwa katika warsha iliyoshirkisha wataalamu mbalimbali nchini Tanzania kutoka serikali na sekta binafsi

Akizungumzia sekta binafsi alitaka, kuchukua pale ambapo serikali itakuwa imeishia katika kutengeneza mifumo ya kuwezesha uchumi mkubwa kwa kuwa na utaratibu wa kuwezesha sayansi, teknolojia katika kukuza shughuli zao.
 Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kabla yakumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mheshimiwa Anthony Mtaka kufungua warsha ambayo ilijadili mafanikio ya Korea Kusini katika viwanda na nini kinaweza kuigwa na watanzania kufikia uchumi wa kati mwaka 2025 iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Naye mtaalamu wa Maendeleo ya Sekta binafsi Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) Ernest Salla akizungumza wakati wa kufunga warsha hiyo alisema kwamba ipo haja ya watanzania kuwa wazalendo na kuhakikisha wanatimiza ndoto ya nchi ya viwanda kwa kuwekeza zaidi.

Aidha alisema kutokana na kuwapo kwa maendeleo makubwa ya teknolojia na sayansi Tanzania inaweza kutumia nafasi hiyo kusonga mbele kwa kasi kuelekea sekta ya viwanda

Alitaka kwa sasa sekta binafsi kuhakikisha inatumia fursa zilizopo kuleta maendeleo badala ya kuwa na woga na hofu kutokana na vikwazo vya hapa na pale. Mgeni mzungumzaji Profesa Jin-Sang LEE kutoka Chuo Kikuu cha New York-( SUNY)- Korea akielezea jinsi Korea Kusini ilivyofanikiwa katika uchumi wakati wa warsha ambayo ilijadili mafanikio ya Korea Kusini katika viwanda na nini kinaweza kuigwa na watanzania kufikia uchumi wa kati mwaka 2025 iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT MAGUFULI NA MAMA JANETH MAGUFULI WACHANGIA SH. MILIONI 15 KWA AJILI YA MATIBABU YA MWIGIZAJI WASTARA JUMA

$
0
0

 

  Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwasilli kumkabidhi mwigizaji wa filamu za Bongo movie Wastara Juma shilingi milioni 15 zilizotolewa na Rais John Pombe Magufuli na Mama Janeth Magufuli kwa ajili ya matibabu nyumbani kwake Tabata Sanene jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 26, 2018. Bw. Samike alimkabidhi Wastara shilingi milioni moja na laki tisa zilizocahngwa na wasaidizi wa Rais. Msanii huyo maarufu, ambaye alionekana na Rais kupitia kipindi cha Clouds TV cha SHILAWADU akiomba msaada wa pesa ili kurudi hospitali ya Sifael nchini India, kwa  matibabu chini ya uangilizi wa hospital hiyo, amemshukuru Rais kwa kuwajali wananchi wake.     
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi mwigizaji wa filamu za Bongo movie Wastara Juma shilingi milioni 15 zilizotolewa na Rais John Pombe Magufuli na Mama Janeth Magufuli kwa ajili ya matibabu nyumbani kwake Tabata Sanene jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 26, 2018. Bw. Samike alimkabidhi Wastara shilingi milioni moja na laki tisa zilizocahngwa na wasaidizi wa Rais. Msanii huyo maarufu, ambaye alionekana na Rais kupitia kipindi cha Clouds TV cha SHILAWADU akiomba msaada wa pesa ili kurudi hospitali ya sifael nchini India, kwa  matibabu chini ya uangilizi wa hospital hiyo. 
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike na waendesha kipindi cha Clouds TV cha SHILAWADU wakimsikiliza mwigizaji wa filamu za Bongo movie Wastara Juma  akishukuru kwa kupokea shilingi milioni 15 zilizotolewa na Rais John Pombe Magufuli na Mama Janeth Magufuli kwa ajili ya matibabu yake nyumbani kwake Tabata Sanene jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 26, 2018. Bw. Samike pia alimkabidhi Wastara shilingi milioni moja na laki tisa zilizocahngwa na wasaidizi wa Rais. Msanii huyo maarufu, ambaye alionekana na Rais kupitia kipindi cha Clouds TV cha SHILAWADU akiomba msaada wa pesa ili kurudi hospitali ya sifael nchini India kwa  matibabu chini ya uangilizi wa hospital hiyo, amemshukuru Rais kwa kuwajali wananchi wake.  
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike na ujumbe alioongozana nao pamoja na  waendesha kipindi cha Clouds TV cha SHILAWADU wakiwa katika picha ya kumbukumbu na mwigizaji wa filamu za Bongo movie Wastara Juma  baada ya kumkabidhi  shilingi milioni 15 zilizotolewa na Rais John Pombe Magufuli na Mama Janeth Magufuli kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo nyumbani kwake Tabata Sanene jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 26, 2018. Bw. Samike pia alimkabidhi Wastara shilingi milioni moja na laki tisa zilizocahngwa na wasaidizi wa Rais. Msanii huyo maarufu, ambaye alionekana na Rais kupitia kipindi cha Clouds TV cha SHILAWADU akiomba msaada wa pesa ili kurudi hospitali ya Sifael nchini India kwa  matibabu chini ya uangilizi wa hospital hiyo, amemshukuru Rais kwa kuwajali wananchi wake.  

mvua iliyoambatana na upepo yaezua paa za nyumba 30 tanganyika mkoani Katavi

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika,Salehe Muhando (Mwenye miwani pichani juu na chini) akikagua athari ya  Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha jana na kusababisha kuezua mapaa ya nyumba 30 na kuharibu mazao hasa migomba katika kijiji cha Mwese Kata ya Mwese.Muhando alisema kuwa kutokana na athari hiyo, lakini wanamshukuru Mungu hakuna mtu aliyepoteza maisha.

WAFANYAKAZI KAMPUNI YA UDALALI KORTINI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

$
0
0
Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

WAFANYAKAZI wa kampuni ya udalali ya Tambaza jijini Dar es Salaam, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa ya Sh. 40,000 kwa mwendesha pikipiki( bodaboda).

Washitakiwa hao, Christopher Mbiku na Deus Warioba ambao wamesomewa mashitaka yao leo mahakamani hapo na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), Leornad Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa,

Imedaiwa Januari 23 mwaka huu, maeneo ya Daraja Salender Bridge wilayani Ilala, Dar es Salaam washtakiwa walishawishi kupewa rushwa ya Sh.40,000.

Alidai kuwa washitakiwa walishawishi fedha hizo kutoka kwa Abul Malenda ambae ni dereva wa bodaboda kwa madai kwamba hawatamchukulia hatua za kisheria kutokana na kosa la kutokuwa na kadi na kibali cha kuendesha pikipiki mjini kitendo ambacho ni kinyume na taratibu.
Pia alidai Januari 23, mwaka huu maeneo hayo hayo, washtakiwa hao walipokea rushwa ya Sh.40,000 kutoka kwa Malenda kwa madai wasingemchukulia hatua za kisheria kwa kutokuwa na kadi na kibali cha kuendesha pikipiki na mjini.

Katika mashitaka ya tatu inadaiwa, Januari 23, mwaka huu maeneo hayo ya daraja la Salander wilayani Ilala, washitakiwa wote kwa pamoja walijipatia sh. 40,000 kwa njia ya udanganyifu kwa kujitambulisha kuwa wao ni watumishi wa Kampuni ya  udalali ya Tambaza kitu ambacho si kweli.

Washitakiwa walikana mashitaka na wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.  

Kesi imeahirishwa hadi Februari 23 mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa shauri hilo umekamilika ambapo upande wa mashitaka umeomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.
Viewing all 110095 articles
Browse latest View live




Latest Images