Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

DKT.MABODI AMTUMIA SALAMU ZA RAMBI RAMBI DKT.MAGUFULI

$
0
0
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ ametuma salamu za rambi rambi kwa familia ya mtumishi wa Chama hicho Zanzibar Marehemu Bi. Nakia Khamis Abdalla aliyefariki leo Januari 25,2018.

Bi. Nakia amefariki dunia akiwa nyumbani kwake mtaa wa Sogea Zanzibar baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Katika Salamu zake Dk. Mabodi amesema CCM Zanzibar imepokea taarifa ya kifo cha mtumishi huyo kwa Mshutuko, Majonzi na Simanzi kubwa, kwani Marehemu enzi za uhai wake alikuwa Mwadilifu aliyefanya kazi kwa bidii na ubunifu wa hali ya juu katika utumishi wake.

Pamoja na hayo alitoa pole kwa familia Wanachama, Viongozi na Watendaji Wote wa CCM, Marafiki pamoja na Jamaa wa karibu walioguswa na msiba huo, na kuwaomba waendelee kuwa na uvumilivu katika kipindi chote cha msiba huo.

“ Marehemu alikuwa ni mfano wa kuigwa enzi za uhai wake hasa kwa kujitolea na kukipigania Chama cha Mapinduzi muda wote wa uhai wake, hivyo tumepoteza mtu muhimu sana ndani ya Chama na Taifa kwa ujumla.

Pia nawaomba watumishi na wanachama na Familia ya Marehemu kuwa na Subra katika kipindi hiki kigumu cha Msiba huo, na tuendelee kumuombea dua mwenzetu ili Mwenyezi Mungu amuweke pahala pema peponi Amin.”, alieleza Dk. Mabodi.


SHIRIKA LA CSI LAPANIA KUOKOA MAISHA YA MAMA MJAMZITO

$
0
0
*Mkurugenzi aelezea namna wanavyotoa elimu ya  kuokoa maisha ya mama mjamzito

*Wapania kumfanya mwanamke mjamzito kuwa malkia, mwanamke shujaa na mwenye thamani 
*Aprili 6 mwaka huu Rais Mstaafu , Dk.Jakaya Kikwete  mgeni rasmi sherehe ya miaka mitano  ya uwepo wa CSI.

 Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

NGUVU ya mwanamke na iheshimiwe, itukuzwe maana imeshafanya mapinduzi mengi duniani na yoyote mwenye kumdharau au kumuumiza mwanamke hafai kutambulika kama binadamu mwenye kujitambua.

Ukweli ni kwamba mwanamke ni malkia na maisha yake ya sasa na baadae yanahitaji heshima kubwa. Pamoja na hayo mheshimu mwanamke maana wewe umetoka ndani yake, na unamwita mama.

Mwanaume ili aitwe baba anahitaji mwanamke. Mwanaume mwenye akili  timamu huhitaji mapenzi ya kweli na hayo hayapatikani kwingine zaidi ya kwa mwanamke. Mwanamke ni maisha.

Unaweza kujiuliza kwanini nimeanza kwa kueleza yote hayo. Kabla sijajibu sababu ya kuelezea hayo kwa kina niongeze tu mwanamke ni kiumbe mwenye thamani  mbele ya viumbe vilivyopo chini ya jua .

Kwanini? Jibu ni kwamba pamoja na sababu nyingine nyingi lakini Mungu amempa kazi moja ambayo ni muhimu katika maisha ya mwanadamu. Mwanamke ndio mwenye uwezo wa kuleta  mtu mpya duniani.

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA UJUMBE WA RAIS KAGAME, AMUAGA BALOZI WA ZIMBABWE

$
0
0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea  na Dkt Donald Kaberuka, Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame (kushoto kwa Rais),  katika mazungumzo yaliyohudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Mhe. Dotto James na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Uwekezaji Profesa Adolf Mkenda Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 25, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Dkt. Donald Kaberuka, Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 25, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Dkt. Donald Kaberula, Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame  na ujumbe wake pamoja na  na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Mhe. Dotto James na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Uwekezaji Profesa Adolf Mkenda Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 25, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Dkt. Donald Kaberuka, Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, huku Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akishuhudia baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 25, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Balozi wa Zimbabwe aliyemaliza muda wake nchini Mhe. Edzai A.C. Chimonyo aliyefika kumuaga rasmi Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 25, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Balozi wa Zimbabwe aliyemaliza muda wake nchini Mhe. Edzai A.C. Chimonyo aliyefika kumuaga rasmi Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 25, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza  Balozi wa Zimbabwe aliyemaliza muda wake nchini Mhe. Edzai A.C. Chimonyo aliyefika na kumuaga rasmi Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 25, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Zimbabwe aliyemaliza muda wake nchini Mhe. Edzai A.C. Chimonyo aliyefika kumuaga rasmi Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 25, 2018.


PICHA NA IKULU

RWEGASIRA AKAGUA UJENZI WA NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA UKONGA, JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira (wapili kushoto) akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Askari Magereza, Mhandisi Khadija Salum, alipokua anamuonyesha Katibu Mkuu huyo maeneo mbalimbali ya ujenzi wa nyumba hizo zilizopo Ukonga, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Moja ya jengo la Makazi ya Askari Magereza likionekana hatua iliyofikia. Nyumba hizo zilizopo Ukonga jijini Dar es Salaam, zinajengwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA-B) na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira akiwafafanulia jambo wajenzi wa Nyumba za Askari Magereza zilizopo Ukonga jijini Dar es Salaam, ambao ni Wakala wa Majengo nchini (TBA-B).  Kushoto (meza kuu) ni Kaimu Meneja wa Mkoa wa Dar es Salaam (TBA-B), Manasseh Slekelaghe, anaefuata ni Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba hizo, Mhandisi Khadija Salum, na kushoto ni Mhandisi wa Mradi huo, Peter Kikwati. Kulia ni Msimamizi wa Mradi wa huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, Cosmas Mtambala. Katibu Mkuu alizikagua nyumba hizo leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira akiwafafanulia jambo wajenzi wa Nyumba za Askari Magereza zilizopo Ukonga jijini Dar es Salaam, ambao ni Wakala wa Majengo nchini (TBA-B), pamoja na wasimamizi wa mradi huo ambao ni Maafisa wa Jeshi la Magereza.  Kushoto (meza kuu) ni Kaimu Meneja wa Mkoa wa Dar es Salaam (TBA-B), Manasseh Slekelaghe. Katibu Mkuu alizikagua nyumba hizo leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira akimsalimia Kaimu Meneja wa Mkoa wa Dar es Salaam, Wakala wa Majengo nchini (TBA-B), Manasseh Slekelaghe (Kushoto), mara baada ya Katibu Mkuu huyo kumaliza ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa nyumba za askari Magereza, zilizopo Ukonga, jijini Dar es Salaam leo.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MKOA KASKAZINI PEMBA WENYEJI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI (MEI MOSI).

$
0
0
Katibu Tawala Mkoa Kaskazini Pemba Ahmed Khalid Abdalla akiwakaribisha wageni katika Mkutano wa kujadili madhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani yanayotarajiwa kufanyika katika Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman akifungua Mkutano wa kujadili madhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani yanayotarajiwa kufanyika katika Mkoa wake.
Katibu Mkuu Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) Khamis Mwinyi Mohammed (aliesimama) akitoa maelezo juu ya mchakato na ufanikishaji wa Madhimisho ya Mei mosi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba.
Afisa kutoka Wizara ya Kazi Zanzibar Amin Ali Amin akichangia kitu katika Mkutano huo uliofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba.

Picha na Makame Mshenga Pemba.

DC MJEMA AKAGUA UKARABATI SEKONDARI YA JANGWANI, AZANIA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

MKUU wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, Sophia Mjema amefanya ziara ya kukagua ukarabati wa majengo unaofanyika kwenye Sekondari ya Wasichana Jangwani na Sekondari ya Wavulana Azania ambapo ukarabati huo umegharimu zaidi ya Sh.bilioni 3.

Amefafanua kiasi hicho cha fedha pia kinahusisha ukarabati wa sekodari ya Pugu na unafanywa na Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania(TBA).

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, akiwa Jangwani ambayo alisoma kidato cha tano na sita, Mjema amesema amefanya ziara hiyo kuangalia maendeleo ya ukarabati huo.

"Nitumie nafasi hii kuwapongeza Wakala wa Majengo kwa kazi nzuri wanayoifanya.Pia naomba ukarabati huu uende kwa haraka kama ambavyo imeagizwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,"amesema.

Amefafanua ukarabati huo umeleta mabadiliko makubwa katika shule hiyo hasa walipokarabati vyoo vya wanafunzi wenye ulemavu  ambavyo hapo awali havikuwepo Jangwani.

"Kwa ukarabati huu hata wanafunzi wenye uhitaji maalumu wanaweza kuendana na mazingira ya shule kwani yatakuwa rafiki kwao,"amesema.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akikagua Milango ya Choo cha Shule ya Sekondari ya Wasichana Jangwani ambayo inakarabatiwa katika mpango maalum wa ulitolewa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Dk John Magufuli ya ukarabati wa shule kongwe ambapo ukarabati huo  umegharimu Shilingi Bilioni 3 za kitanzania.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema, akikagua Mabweni  ya Shule Sekondari ya Wavulana ya Azania ambayo inakarabatiwa na Wakala wa Majengo TBA
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema, akizungumza na Wasichana  wa shule ya Sekondari ya jangwani juu ya kujiepusha ngono wakiwa shuleni ili wasipate Mimba.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo  akisalimiana na Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Azania Sekondari Goodlove Kapufi kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa ukarabati wa shule hiyo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema  akikagua mazingira ya shule ya sekondari ya Jangwani,Kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Ilala Ndugu Edward Mpogolo.

SERIKALI YASITISHA SHUGHULI ZA WAKALA BINAFSI WA HUDUMA ZA AJIRA WALIOKIUKA SHERIA

$
0
0
Serikali yasitisha Shughuli za Kampuni Tatu (3) za Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira hapa Nchini kutokana na kukiuka matakwa ya sheria ya Huduma za Ajira Na.9 ya mwaka 1999 na Kanuni zake.

Akitoa tamko la Serikali kuhusu Kusitishwa kwa Shughuli za Kampuni hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi na wadau mbalimbali kuhusu utaratibu unaotumiwa na baadhi ya Wakala Binafsi wa huduma za Ajira nchini.

Kampuni zilizofutiwa usajili baada ya kukiuka sheria ni pamoja na  Sasy Solution Company Ltd, Bravo Job Centre Agency na Competitive Manpower International Ltd ambapo Kampuni hizo haziruhusiwi kujihusisha na shughuli za Uwakala  Binafsi wa Ajira  nchini.

Akifafanua Mhe. Mhagama amesema kuwa uchunguzi umebaini  ukiukwaji wa taratibu za usajili ambapo baadhi ya Mawakala wamekuwa wakitumia nyaraka zilizopatikana kwa njia isivyo halali katika kujipatia leseni za uwakala hali iliyowawezesha kukwepa kodi na kujipatia faida.

Aliongeza kuwa ukiukwaji wa taratibu za kisheria umeleta athari mbalimbali kwa wafanyakazi hasa kwa wale wanaoenda kufanya kazi Mataifa ya Nje ambapo wafanyakazi hao wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ubaguzi na unyanyasaji katika ajira, malipo ya mishahara na stahiki mbalimbali.

Aidha, Mhe. Mhagama amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imesitisha mara moja shughuli za Mawakala Binafsi wa huduma za Ajira zinazohusika na kuwatafutia kazi wafanyakazi nje ya nchi (cross border placement) hadi hapo Serikali itakapoleta mfumo wa kusimamia jambo hili na kutoa taarifa kwa umma.

Vile Vile, Waziri Mhagama amemwagiza Kamishna wa Kazi kuhakikisha kuwa ndani ya wiki mbili kuzifanyia uhakiki Wakala zote zilizosajiliwa kuona kama wametimiza na kuzingatia Sheria na Kanuni zinazosimamia Wakala Binafsi za Ajira, Pia aliiasa Timu ya wakaguzi itakayoundwa na Wizara ikikiuka miiko ya ukaguzi na kuficha udhaifu wa mawakala hao hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa Mujibu wa Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akitoa tamko la Serikali leo mjini Dodoma kuhusu Kusitishwa kwa Shughuli za Kampuni zinazotoa huduma ya Uwakala Binafsi wa Ajira baada ya kukiuka sheria ni pamoja na Sasy Solution Company Ltd, Bravo Job Centre Agency na Competitive Manpower International Ltd ambapo Kampuni hizo haziruhusiwi kujihusisha na shughuli za Uwakala  Binafsi wa Ajira  nchini, Januari 25, 2018.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama leo mjini Dodoma wakati akitoa tamko la Serikali kuhusu Kusitishwa kwa Shughuli za Kampuni zinazotoa huduma ya uwakala binafsi wa Ajira baada ya kukiuka sheria Huduma za Ajira Na.9 ya mwaka 1999 na Kanuni zake.

Wataalamu Ujenzi,Uchukuzi SMT na SMZ wakutana kuboresha sekta hiyo

$
0
0
 Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Bi. Elizabeth Tagora akifungua rasmi kikao cha ushirikiano na uboreshaji masuala ya sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Khatib Mohamed akifafanua jambo katika kikao cha ushirikiano na uboreshaji masuala ya sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Barabara Kuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Light Chobya akielezea majukumu ya idara hiyo katika kikao cha ushirikiano na uboreshaji masuala ya sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wajumbe wa kikao cha ushirikiano na uboreshaji masuala ya sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia mjadala kuhusu uboreshaji wa sekta hiyo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Msajili wa Bodi ya Wahandisi Tanzania (ERB), Eng. Patrick Barozi akiwasilisha mada kuhusu utendaji wa Bodi hiyo katika kikao cha ushirikiano na uboreshaji masuala ya sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo jijini Dar es Salaam. 
Wajumbe wa kikao cha ushirikiano na uboreshaji masuala ya sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

MAVUNDE,NDEJEMBI WAZINDUA KAMPENI UPANDAJI MITI KONGWA

$
0
0

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde leo amezindua kampeni ya upandaji miti milioni moja katika kijiji cha Ibwagwa,Wilayani Kongwa Dodoma ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya KIJANISHA DODOMA iliyozinduliwa na Mhe. Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

Waziri Mavunde amewataka wananchi wa Kongwa kuhakikisha wanatunza mazingira kwa kupanda miti mingi zaidi na kuwataka kuacha tabia ya kukata miti ambayo hali inayosababisha uharibifu wa mazingira mkubwa.

Aidha Mavunde ametumia nafasi hiyo kuutaka uongozi wa Wilaya ya Kongwa kuhakikisha kwamba unasimamia utekelezaji wa sheria na kanuni mbalimbali za Mazingira ili kuinusuru wilaya hiyo na uharibifu wa Mazingira.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mkuu wa Wilaya wa Kongwa Mhe. Deogratious Ndejembi amemuhakikishia Naibu Waziri Mavunde kwamba kama watahakikisha miti yote iliyopandwa inastawi ili kufikia lengo la kui-KIJANISHA DODOMA na pia ameahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaobainika kuharibu mazingira hasa kwa ukataji miti na uchomaji wa misitu.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti milioni moja katika kijiji cha Ibwagwa,Wilayani Kongwa Dodoma
Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratious Ndejembi akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti.
Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratious Ndejembi akipanda mti katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akiwa ameshika miche kwa ajili ya kupanda.
Miti inayopandwa katika wilaya ya Kongwa 

ZIDANE AKALIA 'KUTI KAVU' REAL MADRID

$
0
0
Na Agnes Francis, Globu ya Jamii

KOCHA Mkuu wa kikosi cha Real Madrid, Zinedine Zidane ameendelea kusakamwa na matokeo mabaya anayoyapata baada ya jana kuondolewa kwa jumla ya mabao 2-2 dhidi ya Leganes.

Matokeo hayo yameifanya Madrid kuondolewa katika michuano ya Kombe la Mfalme(Copa del Rey).Mtanange huo uliopigwa Uwanja wa Santiago Bernabeu, Madrid imeondolewa kwenye michuano hiyo licha ya ushindi walioupata wakiwa ugenini wa bao 1 - 0 wakati jana Madrid walipokea kichapo cha bao 2 - 1 bila ya nyota wake Christian Ronaldo na Gareth Bale. 

Mabao ya Leganes yalipachikwa nyavuni na Javier  Eraso na la pili  lilifungwa na  Gabriel Appelt Pires dakika ya 55,wakati mshambuliaji  wa Real Madrid  Karin Benzema alipatia timu yake bao dakika ya 47.

Hivi karibuni kabla ya mechi hiyo Kocha Zidane amekuwa akisakamwa na baadhi ya viongozi wake kutokana na mwenendo mbovu wa klabu hiyo siku za usoni.

DK. KIGWANGALLA ATAJA ORODHA WATUHUMIWA UJANGILI LEO MJINI DODOMA

$
0
0
Na Hamza Temba - Dodoma

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla leo Januari 25, 2018 mjini Dodoma ametaja majina ya watuhumiwa wa ujangili ambao wengi wao ni wamiliki na washirika wa Kampuni za uwindaji wa kitalii na kuwapa siku saba wawe wamefika kwa hiari yao wenyewe katika ofisi za Wizara hiyo Mjini Dodoma, Swagaswaga House kwa ajili kutoa maelezo kwanini wasichukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kujibu tuhuma hiyo na nyingine nyingi zinazowakabili mbele ya kamati atakayoiunda.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Dk. Kigwangalla ametaja baadhi ya tuhuma hizo ambazo ziko kinyume cha sheria na taratibu za uwindaji wa kitalii kuwa ni uwindaji haramu, uhawilishaji wa umiliki wa vitalu vya uwindaji pasipo kufuata sheria, udanganyifu kwenye kujaza fomu za uangalizi,  rushwa, uhalifu dhidi ya rasilimali za wanyamapori na uhujumu uchumi.

Alitaja tuhuma zingine kuwa ni ukiukwaji wa kanuni za uwindaji (kupiga wanyama usiku, kuwinda wanyama bila kujali umri, kupiga wanyama nje ya maeneo waliyopewa), kukutolipa tozo mbalimbali za maendeleo za jamii kwenye vijiji jirani na maeneo wanaoendesha biashara ya uwindaji, kushindwa kuendesha ipasavyo shughuli za kuzuia ujangili.


Dk. Kigwangalla aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni ndugu Pasanis na wenzake ambao wanamiliki kampuni ya Berlette Safari Corporation Ltd na Ngugu Shein Ralgi na wakurugenzi wenzake wa kampuni ya Game Frontiers of Tanzania Ltd.


Wengine ni Ndugu Howel na wakurugenzi wenzake wa kampuni ya Mkwawa Hunting Safaris Tanzania Ltd, Ndugu Thomas Fredikin na wenzake wa Kampuni ya Mwiba Holdings Ltd, Wengert Windrose Safaris Tanzania  Ltd na Tanzania Game Trackers Safaris Ltd, na Ndugu Awadh na wenzake ambao wanamiliki kampuni ya Uwindaji wa Greenmiles Safaris Ltd.


Aliwataja washirika wengine kuwa ni Ndugu ni Kwizema, Ndugu Robert, Ndugu Solomon Makulu, Ndugu Siasa Shaban, Ndugu Hamis Abdul Ligagabile na mtumishi wa Wizara Wizara ya Maliasili na Utalii, Alex Aguma.


Katika hatua nyingine Dk. Kigwangalla ametoa Ilani ya siku 30 kwa watu mbalimbali ikiwemo Mawaziri Wakuu Wastaafu waliovamia kiwanja chenye hati namba 4091 kilichopo Njiro Jijini Arusha wafike kwa Kamishna Mkuu wa Ardhi waweze kuhakikiwa na kuthibitisha umiliki wao halali ama sivyo wavirejeshe Serikalini viweze kumilikishwa kwa mmiliki wake halali.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara hiyo Mjini Dodoma leo. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki.
 Dk. Kigwangalla akizungumza katika mkutano huo leo mjini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DC MJEMA AWAKUMBUSHA WAZAZI UMUHIMU WA KUWATUNZA WATOTO WA KIUME

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya Ilala,Sophia Mjema akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhimbili wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Tumkumbuke Mtoto wa kiume, inayoendeshwa na Tasisi ya Dahuu Foundation  inayotoa elimu ya kuwakinga watoto wa kiume wasikumbwe na majanga mbalimbali.
  Mkuu wa Wilaya Ilala,Sophia Mjema, akicheza na wanafunzi wa  Kiume wa shule ya msingi Muhimbili wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Tumkumbuke Mtoto wa kiume inayoendeshwa na Tasisi ya Dahuu Foundation
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhimbili wakiwa katika Maandamano yenye mabango ambao walipita mbele ya mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema Kuonesha hisia zao.
 Mkurugenzi wa Dahuu Foundation, Husna Abdul akizungumza kabla ya kumkaribisha mkuu wa Wilaya kufanya uzinduzi wa kampeni ya Tumkumbuke Mtoto wa kiume inayoendeshwa na Tasisi ya Dahuu Foundation

WAMILIKI NYUMBA 59 KIPUNGUNI A WAPEWA SIKU SABA WAHAME

$
0
0
JOPO la maofisa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), limefanya utambuzi wa nyumba 59 zilizopo eneo la Kipunguni A, jijini Dar es Salaam na kutoa notisi ya siku saba kwa wakazi wake kuhama.Nyumba hizo ni zile ambazo serikali tayari ililipa wakazi wake stahiki zao mwaka 2014 kufuatia uthamini uliofanyika mwaka 1997, lakini bado wanachi hao waliendelea kuishi eneo hilo linalohitajika na Serikali kwa ajili ya matumizi ya shughuli za Mamlaka ya Viwanja vya N dege.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa shughuli hiyo ya utambuzi iliyofanyika leo Januari 25, Ofisa Ardhi mkuu wa TAA, Cecilia Mwing'uri amesema jopo hilo lilijumuisha watumishi kutoka TANESCO,  Polisi, TAA kitengo cha sharia na Mahusiano,  na wajumbe wa eneo hilo waliowawakilisha wananchi.

"Tulizitambua nyumba husika na kuziwekea alama ya X na kutoa notisi ili wakazi ambao bado wapo eneo hilo la Kipunguni wahame ndani ya siku saba kuanzia leo."Kwa bahati nzuri kuna ambao wamehama na wengine wanaendelea na ubomoaji wa kistaarabu wa nyumba zao isipokuwa wachache ambao waliuziwa nyumba  na maeneo huku wamiliki wa kwanza wakijua fika, eneo hilo ni mali ya serikali na walishalipwa fedha zao," amesema.

Kwenye zoezi hilo Bi  Cecilia alisema watumishi wa Shirika la Umeme (TANESCO), kutoka mkoa wa kihuduma wa Gongo la Mboto walitoa siku tatu kuanzia kesho na kwamba baada ya hapo wataanza zoezi la kuondoa miundombinu ya umeme kwenye nyumba husika ili kurahisisha zoezi la ubomoaji.

Mwishoni mwa mwaka jana, wakati wa ziara ya Naibu waziri wa mawasiliano na uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye kwenye makao makuu ya TAA, alikutana na hoja hiyo na kuagiza Mamlaka hiyo ya Viwanja vya Ndege kuhakikisha waliolipwa fidia na bado wapo Kipunguni A wanaondoka ndani ya siku 30.

Amesema kwa kuwa serikali tayari imekamilisha jukumu lake kwa nafasi yake, hakuna budi watu hao wakahama ili nia ya serikali kwenye eneo hilo kama ni upanuzi wa kiwanja cha ndege au shughuli nyingine itekelezwe kwa nafasi.

Katika mazungumzo yake na watumishi wa TAA akiwemo Mkurugenzi Mkuu, Richard Mayongela, Mhandisi Nditiye aliahidiwa kuwa mamlaka hiyo itahakikisha wakazi ambao tayari wamelipwa fidia katika awamu iliyohusisha nyumba 59 inatekelezwa, kama ambavyo TAA imeanza kufanya leo.
 Mhandisi Astelius John kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania akitoka kuweka alama ya kuondolewa kwa moja ya nyumba zilizolipwa fidia eneo la Kipunguni A.
 Moja ya  Nyumba zilizoanza kubomolewa na mwananchi mwenyewe katika eneo la Kipunguni A.

Afisa ardhi Mkuu kutoka Mamlaka ya viwanja Vya Ndege Bi Cecilia Mwing’uri  akisaidia  zoezi la kuweka alama ya kuondoa nyumba hiyo  kati ya nyumba 59  zinazotakiwa kubomolewa.  

MHALIFU ATAINGIA DAR AKIWA SALAMA LAKINI HATATOKA SALAMA-MAMBOSASA

$
0
0
*Asema wamedhibiti uhalifu, azungumzia Panya road 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAMANDA wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema iwapo kuna mhalifu yoyote na wa kutoka sehemu yoyote anaweza kuingia Dar es Salaam salama lakini ajue hatatoka salama.

Amefafanua kutoka na kujipanga vema kulinda usalama wa raia na mali zao kwa Jiji la Dar es Salaam wamefanikiwa kukomesha uhalifu na hata waliokuwa wanajiita Panya Road na makundi mengine ya kihalifu sasa imebaki historia huku akifafanua jeshi hilo halipo tayari kuchezewa.

Mambosasa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea tuzo maalumu iliyotolewa na uongozi wa Redio Times Fm na kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu kama sehemu ya kutambua mchango wanaoutoa katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama wakati wote.Tuzo hiyo ilitolewa na Mkurugenzi .

Mtendaji wa redio hiyo Rehule Nyaula.Amesema tuzo hiyo imewatia moyo polisi Kanda Maalumu kwani imekuwa ni kawaida kusikia tu wakilaumiwa lakini Redio Times wanatambua kazi ambayo wanafanya na kuomba wengine kuiga mfano huo wa kuthamini kazi zinazofanywa na taasisi mbalimbali nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Radio Times FM, Rehule Nyaulawa(aliyesimama)akizungumza leo akiwa katika Ofisi za Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa kabla ya kukabidhi tuzo maalum ambayo inalenga kutambua mchango wa Polisi katika kulinda usalama wa raia na mali zao. 
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akionesha tuzo maalum ambayo wamepewa na Radio Times FM.Tuzo hiyo ni kutambua mchango wa Polisi katika kulinda usalama wa wananchi wa Dar es Salaam kwa mwaka 2017
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa(aliyesimama) akizungumza leo kabla ya kupokea tuzo maalum ya kutambua mchango wao katika suala la ulinzi na usalama iliyotolewa na uongozi wa Radio Times FM wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Rehule Nyaula(aliyekaa kushoto) .




DKT. KIGWANGALLA AKITAJA ORODHA WATUHUMIWA WA UJANGILI


mvua iliyoambatana na upepo yaezua paa za nyumba 30 tanganyika mkoani Katavi

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika,Salehe Muhando (Mwenye miwani pichani juu na chini) akikagua athari ya  Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha jana na kusababisha kuezua mapaa ya nyumba 30 na kuharibu mazao hasa migomba katika kijiji cha Mwese Kata ya Mwese.Muhando alisema kuwa kutokana na athari hiyo, lakini wanamshukuru Mungu hakuna mtu aliyepoteza maisha.

Wanafunzi saba wafanya mtihani na kufaulu kupandishwa madaraja ya mkanda mweusi wa Goju Ryu karate

$
0
0
 Na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii
Wanafunzi waandamizi saba wa  shule za Karate (dojo) mtindo wa Okinawa Goju Ryu  za  Kaizen na Hekalu la Kujilinda  za jijini Dar es salaam na Dodoma wamefanya mitihani na kufaulu kupandishwa madaraja ya mkanda mweusi chini ya Sensei Rumadha Fundi  (BOFYA HAPA KUMJUA) usiku wa Jumatatu Januari 22, 2018.
Wanafunzi hao kutoka Kaizen dojo  iliyopo Shule ya Sekondari ya Jamhuri na dojo dada ya Hekalu la Kujilinda iliyopo katika shule ya msingi ya Zanaki ni pamoja na ma-Senpai Yusuf Kimvuli, Abdulwahud Aghfoul, Bilali Mtenga na Seif Soud ambao wamepanda kutoka mkanda mweusi daraja la kwanza (1st Dan)  kwenda la daraja la pili (2nd Dan) lijulikanalo kama "Nidan".
Wakati ma-Senpai Kimvuli, Maghfoul na Mtenga wanatoka dojo la Kaizen, Senpai Seif Soud anatoka Hekalu la Kujilinda.
Wanafunzi wengine watatu waliofaulu na kupanda daraja la kwanza (1st Dan) ama "Shodan" kutoka mkanda wa kahawia ni ma-Senpai Abdulmajid Khan wa Hekalu la Kujilinda pamoja na  Shaaban Yusuf na Galant Swai ambao wanatoka katika tawi la Hekalu la Kujilinda lililopo mjini Dodoma kwa jina la Miyagi dojo.
Hii ni mara ya kwanza kwa  Sensei Rumadha Fundi  mwenye Dan 4,“Yondan” na  mwenye uzoefu mkubwa wa  mafunzo ya Goju Ryu chini ya walimu wakuu wengi maarufu toka Okinawa, Japan, kuwafanyia mitihani na kuwapandisha madaraja wanafunzi wa Tanzania.
Sensei Rumadha, ambaye alianza mafunzo ya Okinawa Goju Ryu miaka 38 iliyopita  katika Hekalu la Kujilinda la Zanaki amesema anajisikia furaha na fahari kutimiza hilo jukumu lake kwa mara ya kwanza, na kwamba hajutii kufunga safari hii kutoka Houston, Marekani, anakoishi na kuja kuwasaidia ndugu zake.
Na hilo liliwezakana baada ya mwaka jana huko  nchini Poland  Sensei Rumadha kufanya  na kufaulu vizuri mitihani wake wa kupanda ngazi toka Dan ya tatu "Sandan" kwenda ngazi ya nne "Yondan"  chini ya waamuzi (masters) toka Okinawa wakiongozwa na Sensei Yoshihiro Kancho Miyazato, ambaye ni Master au mwalimu mkuu wa Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu Karate-Do huko Okinawa.
Tokea hapo Sensei  Rumadha amekuwa na mamlaka ya kuwasaidia wanafunzi wake wa Tanzania na kuwafanyia mitihani na kuwapa wanafunzi  "Dan" hadi ngazi ya pili " Nidan" sababu katika Goju Ryu Karate  kuanzia Dan ya 3 na kuendelea hutolewa na Master Miyazato pekee.
"Hawa waliofaulu na kupanda daraja la pili hivi sasa wana mamlaka ya kufungua shule zao chini ya uangalizi wangu na wakiendelea kufanya vyema nitatoa idhini ya wao kuwa waalimu ("Sensei") wanaotambulika Okinawa  baada ya muda si mrefu ujao" amesema Sensei Rumadha.
Hakusita kutoa shukran zake nyingi kwa mlezi wake wa mafunzo tokea utotoni,  "Sensei Magoma Nyamuko Sarya akisema chini ya uongozi wake kitengo cha watoto kilichoitwa "Bomani Brigade"  kilichobuniwa  na mwanzilishi wa Okinawa Goju Ryu nchini Tanzania mwaka 1973,  hayati Sensei Nantambu Camara Bomani. 
Alitoa shukurani za pekee kwa viongozi wa sasa wa Hekalu la Kujilinda - Sensei Mohamed Murudker, Sensei Wilfred Melkia, Sensei Geofrey Sawayael “Shoo” na Sensei Rashid Almasi ambao amesema moyo wao wa  kuendeleza Goju Ryu bila kutetereka pale Zanaki ni wa kusifika, na kwamba anawapongeza sana.
Sensei Rumadha pia ameeleza kuwa kabahatika mwaka huu kualikwa kuiwakilisha Tanzania ambayo pamoja na na Angola ni nchi pekee za Afrika zilizoalikwa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 65 tangu kuanzishwa kwa chama cha "Jundokan" na Master Eiichi Miyazato Sensei huko Naha City, Okinawa, mwezi wa Novemba 1918. 
Chama hicho kwa sasa kinaongozwa na mwanawe Yoshihiro Kancho Miyazato, ambaye pia ni Mwenyekiti mkuu dunia wa chama hicho na mwanae Master Eiichi Miyazato, ambaye amewafanyia mitihani ya mkanda mweusi zaidi ya walimu 15 toka ngazi ya pili" Nidan" hadi ngazi ya saba "Nandan". 
Kwa mujibu wa Sensei Rumadha, ngazi hizo zote kwa utamaduni wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu Karate huchukua miaka mingi sana kupandishwa ngazi  tofauti na mitindo mingine. 
 Sensei Rumadha Fundi akiwafanyisha mazoezi wanafunzi saba hao kabla ya kuanza kufanya mtihani wao wa kupanda daraja katika Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam Jumatatu usiku Januari 22, 2018
Viongozi wakuu wa  Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam  wakishuhudia  wanafunzi saba wakifanya mazoezi kabla ya mtihani Jumatatu usiku Januari 22, 2018. Kutoka kulia ni Sensei Wilfred Malekia, Sensei Mohamed Murudker na Sensei Rashid Almasi
  Sensei Rumadha Fundi akiendelea kuwafanyisha  mazoezi wanafunzi saba hao kabla ya kuanza kufanya mtihani wao wa kupanda daraja katika Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam Jumatatu usiku Januari 22, 2018
Sensei Rumadha Fundi akiendelea kuwafanyisha  mazoezi kwa vitendowanafunzi saba hao kabla ya kuanza kufanya mtihani wao wa kupanda daraja katika Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam Jumatatu usiku Januari 22, 2018
 Sensei Rumadha Fundi akitoa mwongozo akiwa na uongozi wa dojo kabla ya  mtihani  wa kupanda daraja wa wanafunzi saba  katika Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam Jumatatu usiku Januari 22, 2018
 Kutoka kushoto Ma-Senpai Abdulmajid Khan wa Hekalu la Kujilinda pamoja na  Shaaban Yusuf na Galant Swai ambao wanatoka katika tawi la Hekalu la Kujilinda lililopo mjini Dodoma kwa jina la Miyagi dojo wakifuatiwa na ma-Senpai Yusuf Kimvuli wa Kaizen dojo na Senpai Seif Soud wa Hekalu la Kujilinda.
Wanafunzi watatu waliofaulu na kupanda daraja la kwanza (1st Dan) ama "Shodan" kutoka mkanda wa kahawia ni  kutoka kushoto ma-Senpai Abdulmajid Khan wa Hekalu la Kujilinda pamoja na  Shaaban Yusuf na Galant Swai ambao wanatoka katika tawi la Hekalu la Kujilinda lililopo mjini Dodoma kwa jina la Miyagi dojo.

MICHUZI TV ! ON 1 GOSSIP: ALIKIBA ADONDOSHA MZIGO MPYA SOKONI NA KUNYAKUWA TUZO.

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 25.01.2018

VOA SWAHILI: Duniani Leo 25th January 2018

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images