Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110126 articles
Browse latest View live

TAASISI MSICHANA INITIATIVE YAZINDUA KITABU KUZUNGUMZIA HAKI ZA WATOTO

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

TAASISI ya Msichana Initiative imezindua kitabu kidogo kinachozungumzia haki mbalimbali za watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa mtoto wa kike.

Uzinduzi wa kitabu hicho umefanyika leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa tasisi hiyo Rebeca Gyumi amesema ni vema watanzania wakakitumia kitabu hicho kilichoandaliwa na timu ya mawakili kwani kimeandikwa kwa lugha rahisi zaidi kuhusu maamuzi  yote yanayotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania Julai 8 mwaka 2016.

“Mahakama Kuu, kupitia Majaji wake katika kesi hii waliona kuwa vifungu hivi haviendani na Katiba ya nchi.Pia vinabagua haki za watoto wa kike ukilinganisha na haki za watoto wa kiume."Vifungu hivyo vinaruhusu mtoto wa kiume kuoa katika umri wa miaka 18 na mtoto wa kike kuoelewa katika umri wa miaka 14 na 15 kwa ruhusa ya Mahakama na wazazi,"amesema Gyumi.

Amesema vifungu hivyo vinachochea kwa kiasi kikubwa suala la ndoa za utotoni hasa kwa watoto wa kike na kutaja Tanzania ni moja ya nchi yenye asilimia kubwa ya tatizo la ndoa za utotoni ikilinganishwa na nchi zingine za ukanda wa Afrika Mashariki ukiacha Uganda.Ameongeza wasichana wawili kati ya watano huolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18 na wasichana hao hukumbwa na changamoto nyingi wanapoingia katika ndoa.

"Wanaolewa wakiwa na mri mdogo wanapopata mimba wakati wa kujifungua wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kupoteza maisha kwa sababu via vyao vya uzazi bado ni vichanga.Pia huwanyima haki yao ya kupata elimu,"amesema.

Gymi amesema kupitia kitabu hiki chenye maamuzi ya Mahakama Kuu, jamii itaelewa na kutambua zaidi namna ambavyo vifungu hivyo kandamizi kwa watoto wa kike na kuona haki ambazo zimetambuliwa kisheria kupitia hukumu hiyo,  pia madhara ya ndoa za utotoni .

Amefafanua Msichana Initiative pamoja na wadau wengine wanaamini suala la ndoa za utotoni litakoma endapo jamii itakuwa tayari kuwashika mkono watoto wa kike kwa kuwalinda na kutetea haki zao msingi.


Mkurugenzi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akiwa katika picha ya pamoja wageni waalikwa wakiwa wameshika kitabu kidogo kinachozungumzia haki na mambo mbalimbali ya haki za watoto.

Mkurugenzi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kitabu Kidogo kinachozungumzia haki na mambo mbalimbali y watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Mkurugenzi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akiwa katika picha ya Pamoja na wadau wakati wa uzinduzi wa Kitabu Kidogo kinachozungumzia haki mambo mbalimbali za watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike. 


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Bharti Airtel receives Regulatory approval to acquire operations of Millicom in Rwanda

$
0
0

·         Merged entity to have largest customer base of 5.9 million subscribers
·         Merger to result in the only negative ebitda OpCo joining other 13 positive ebitda OpCos in Africa
·         Merged entity to have Rwanda’s largest sales and distribution network
Bharti Airtel Limited (“Airtel”) a leading global telecommunications services provider with operations in 16 countries across Asia and Africa, today announced that it has received an approval for the acquisition of Tigo Rwanda Limited (“Tigo Rwanda”), a subsidiary of Millicom International Cellular S.A. ("Millicom") from the Rwanda Utilities Regulatory Authority (RURA).
The merged entity will have the largest customer base in Rwanda with 5.9 million subscribers. The combined networks of the two companies will serve customers with voice/ data services, global roaming and mobile banking services. It will also have Rwanda’s largest sales and distribution network.
The merger will result in the only negative ebitda OpCo joining other 13 positive ebitda OpCos in Africa.
On completion, the acquisition will undergo seamless integration, both on the customer as well as the network side and further strengthen Airtel’s market position in Rwanda. 
Airtel thanked the Rwanda Utilities Regulatory Authority (RURA) for their support during the merger process.

With a presence in 14 countries across Africa, Airtel is one of the largest telecom service providers on the continent in terms of geographical reach, and had close to 84 million customers at the end of quarter ended December 30, 2017. Globally, Airtel is ranked as the third largest mobile services provider in terms of customer base.


MWALIMU COMMERCIAL BANK PLC YAZINDUA BIDHAA KWA AJILI YA KUBORESHA MAISHA YA WATANZANIA.

$
0
0

Mwalimu Commercial Bank PLC (MCB) imezindua bidhaa iitwayo MCB Salary Advance, ikiwa ni moja ya mkakati wake katika kuboresha maisha ya Watanzania kwa ujumla. 

Akizungumzia Kuhusu bidhaa hii mpya ya mkopo wa ‘MCB Salary Advance’, Mkuu wa kitengo cha ukuzaji biashara na masoko, Bwana Valence Luteganya alisema, mteja ataweza kuchukua mkopo huu pale anapouhitaji, Nia ni kuwezesha mteja wetu kuyakabili mahitaji ya dharura yanayojitokeza wakati wowote. 

Alisema, bidhaa ya salary advance inayowalenga wateja wafanyakazi wanaopitishia mishahara yao katika Benki ya Mwalimu, “Mkopo huu unariba nafuu na unapatikana kwa urahisi na haraka, Lengo ni kutoa mkopo wa bei nafuu utakao wasaidia wateja wetu kupunguza ukali wa Maisha”. 

Aliongeza “Kupitia huduma ya Salary advance mfanyakazi anayepitisha mshahara MCB, ataweza kupata hadi asilimia 50 ya mshahara wake kwa riba nafuu. Kupata huduma hii mteja anatakiwa kutembelea tawi la benki au kutuma meseji kupitia whatsapp kwa kuandika neno ‘mshahara wangu’ kwenda namba 0629331755. 

Akiendelea Ndg Luteganya alisema “Hivyo benki hii ya biashara ya Mwalimu imekuja na mikakati ya kutoa bidhaa nzuri zinazokidhi matakwa ya watanzania ili kuisaidia jamii kupunguza na/ama kuondokana na shida ambazo zinaweza kutatuliwa kwa urahisi. 

Naye Mkuu wa kitengo cha huduma kwa njia ya mitandao Ndg. John Mhina aliongeza kwa kusema “Huu ni mwendelezo wa mchakato maalum kuhakikisha tunatimiza mahitaji ya wateja wetu mwaka 2018, na ni ishara kuwa Benki ya Mwalimu imejipanga vyema katika kutoa bidhaa na huduma zinazolenga maslahi ya watanzania hivyo kuufanya mwaka huu kuwa wa neema kwa wateja wetu. Tunakaribisha Watanzania wote kuja kufungua akaunti na kuweza kufaidi huduma na bidhaa zetu.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za kibenki kwa njia ya Mitandao wa Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), John Mhina (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya ‘MCB Salary Advance’ ambayo wateja wanaopitishia mishahara yao katika benki hiyo wataweza kupata mikopo ya hadi nusu ya mishahara yao kuwawezesha kutatua mahitaji yao ya dharura. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Mikopo, Isaya Hagamu, Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko, Valence Luteganya na Meneja Masoko wa benki hiyo, Rahma Ngassa. 
Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko wa Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), Valence Luteganya (wa tatu kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya ‘MCB Salary Advance’ ambayo wateja wanaopitishia mishahara yao katika benki hiyo wataweza kupata mikopo ya hadi nusu ya mishahara yao kuwawezesha kutatua mahitaji yao ya dharura. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Mikopo, Isaya Hagamu, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa njia ya Mitandao, John Mhina na Meneja Masoko, Rahma Ngassa. 
Baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakirekodi tukio la uzinduzi wa huduma ya ‘MCB Salary Advance’ ambayo wateja wanaopitishia mishahara yao katika benki hiyo wataweza kupata mikopo ya hadi nusu ya mishahara yao kuwawezesha kutatua mahitaji yao ya dharura jana katika ukumbi wa tawi la benki hiyo Barabara ya Samora jijini Dar es Salaam.

DK.SHEIN AENDELEA NA ZIARA YAKE UAE

$
0
0
ZANZIBAR na Sharjah zimekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano wao uliopo katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo zikiwemo elimu na biashara,  

Katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makaazi ya Mtukufu Dk. Sheikh Sultan Mohammed Al Qasimi mjini Sharja, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na kiongozi huyo wote kwa pamoja walisisitiza haja ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo kwa lengo la kuimarisha sekta hizo muhimu za maendeleo.


Rais Dk. Shein kwa upande wake alimpongeza Dk. Sultan kwa hatua zake za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha miradi ya maendeleo ukiwemo mradi wa maji.


Pamoja na hayo, viongozi hao walizungumza jinsi ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano katika kuimarisha sekta ya elimu hasa ikizingatiwa kuwa Sharjah imeweza  kupata mafanikio katika sekta hiyo kutokana na kuwa na miundombinu mizuri ya elimu vikiwemo vyo vikuu.


Aidha, Dk. Shein alieleza haja kwa Sharjah kutoa ushirikiano wake kwa Zanzibar katika sekta ya elimu kupitia Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), jambo ambalo Dk. Sheikh Sultan Mohammed Al Qasimi ameliunga mkono.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizunguma na Mtukufu Dk. Sheikh Sultan Bin Mohammed Al Qasimi alipofika katika makaazi yake kwa mazungumzo akiwa katika ziara yake katika Nchi za Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAWAKALA TIGO PESA KANDA YA ZIWA,NYANDA ZA JUU KUSINI WAZAWADIWA

$
0
0

 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Tigo-Tanzania Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh1 milioni Wakala wa Tigo Pesa, Asha Ramadhani kutoka Mkoani Ruvuma baada ya kuibuka mshindi kwa kufanya vizuri kwenye huduma ya TigoPesa katika droo inayochezeshwa na kampuni hiyo. Hafla hiyo ilifanyikia Makao Makuu ya Ofisi za Tigo Kanda hiyo zilizopo Uhindini Jijini Mbeya.

 Mwakilishi wa mshindi wa Tigo pesa wakala David Lucas,Joyce David(wa pili kushoto) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Joseph Mutalemwa(kulia), wakati wa hafla ya kuwapa zawadi mawakala waliofanya vizuri kwenye miamala ya Tigo pesa iliyofanyika jijini Mwanza jana, kushoto ni Mratibu wa Tigo wa Masoko na Biashara kanda ya Ziwa Abraham Mchau akishuhudia.

Mwakilishi wa mshindi wa Tigo pesa wakala kutoka Kahama mkoani Shinyanga Asha Athuman,Daud Kilonzo akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Joseph Mutalemwa(kushoto), wakati wa hafla ya kuwapa zawadi mawakala waliofanya vizuri kwenye miamala ya Tigo pesa iliyofanyika jijini Mwanza jana, kulia ni Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Kaskazini Daniel Mainoya akishuhudia.

Meneja MKuu wa Shamba la Kiwanda cha Maziwa atoa Maelezo kwa Rais wa Zanzibar

$
0
0
Meneja Mkuu wa Shamba hilo Dk. Ahmed Eltigani Al Mansour alimueleza Rais Dk. Shein na ujumbe wake jinsi ya shamba hilo linavyofuga ngombe kwa kutumia teknolojia ya kisasa ikiwemo kuwawekea viyoyozi na mafeni maalum kutokana na mazingira ya hali ya hewa ya ukanda huo.

Kwa mujibu wa maelezo ya Dk. Ahmed shamba hilo lina ng'ombe 12,500 ambapo kwa kila ngombe mmoja kwa siku hutoa lita 60 za maziwa na kutoa lita 250,000 kwa siku huku akitumia fursa hiyo kueleza siri ya mafanikio hayo ikiwa ni pamoja na utafiti mkubwa walioufanya kabla ya kuazisha ufugaji huo.

Dk. Ahmeda alieleza kuwa ufugaji wanaoufanya ni ufugaji bora duniani na pia ni eneo lililopata mafanikio makubwa ikifananishwa na ufugaji unaofanyika katika maeneo mbali mbali zikiwemo nchi za Afrika na hata nchi zilizoendelea ikiwa ni pamoja na kutoa ajira kwa wingi.

Akimaliza ziara yake katika eneo hilo, Rais Dk. Shein aliuhakikishia uongozi wa Al Rawabi kuwa Zanzibar itakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mashirikiano yanakuwepo katika sekta hiyo ya ufugaji ikiwa ni pamoja na kupanua wigo na kujifunza jinsi ya mafanikio hayo yalivyopatikana.

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIWETE YAPEWA TUZO MAALUM

$
0
0

*Profesa Janab amesena alipopata taarifa ya kupewa tuzo hiyo hakuamini kwani...

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, Profesa Mohamedi Janabi ameupongeza uongozi wa Redio Times Fm kwa kutambua mchango wa taasisi hiyo katika kutoa huduma bora za matibabu ya moyo nchini.

Prof. Janab amesema hayo jijini Dar es Salaam baada ya uongozi wa Redio Times FM wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Rehule Nyaula kufika katika taasisi hiyo kwa lengo la kukabidhi tuzo maalum kama ishara ya kutambua mchango wao wa kizalendo wa kuokoa maisha ya watanzania.

Akizungumzia tuzo hiyo, Prof. Janab amesema baada ya kupata taarifa kuwa uongozi wa radio hiyo wanataka kutoa tuzo kwao hakuamini kwani uzoefu unaonesha mgonjwa akitibiwa na kupona hawezi kusema ahsante na utamuona tena akiumwa na kuja hospital kwa matibabu. 

"Tunashukuru Radio Times kwa kutambua kazi ambayo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete inafanya katika kuwahudumia wa Watanzania kwa kuhakikishia tunaokoa maisha yao. "Tuzo hii ni ishara ya ninyi kutambua huduma nzuri ambazo tumekuwa tukizitoa. Malengo yetu ni kuendelea kuhudumia wagonjwa wengi wenye magonjwa ya moyo na ikiwezekana mwaka huu tuhudumie hata wagonjwa 70,000 au 80,000 kwani uwezo tunao, amesema Profesa Janab. 

Kuhusu huduma za matibabu ambazo wanazitoa katika Taasisi hiyo amesema zipo katika ubora wa hali ya juu na kwa Bara la Afrika Kwan nchi za Sub Saraha wanashika nafasi ya pili na ya kwanza ni Afrika Kusini. 

WAZIRI LUKUVI KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI JIJINI MWANZA

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo, William Lukuvi ameanza ziara mkoani Mwanza kwa lengo la kusikiliza wananchi wenye kero na changamoto mbalimbali katika eneo la ardhi. 

Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo inaeleza kuwa Waziri Lukuvi atafanya ziara wilayani Ilemela na Nyamagana na akiwa huko atakagua eneo la Polisi Kigoto lililovamiwa na wanachi. 

Pia atakagua maeneo ya Ilemela Mahakamani, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), na Uwanja wa Ndege. 

"Waziri Lukuvi atakuwa kwenye kuanzia leo Januari 25 hadi 27 mwaka guy ambapo atakagua maeneo kadhaa yenye migogoro ya ardhi, "imesema taarifa hiyo. 

Waziri Lukuvi pia atasikiliza kero za wananchi kuhusu mchakato wa urasimishaji wa makazi, Buguku katika kata ya Buhongwa.

Pia kuhamasisha kwa kutoa hati na kusikiliza kero za wananchi kuhusu urasimishaji eneo la Nyasaka wilayani Ilemela. 

Serikali yaendela kupambana na uvuvi haramu

$
0
0

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiongoza shughuli ya kuteketeza nyavu haramu zenye thamani ya zaidi shilling milioni 100,a zilizo salimishwa na zilizokamatwa katika kisiwa cha Kerebe mkoa wa Kagera jana.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wanaoishi katika kisiwa cha Kerebe mkoa wa Kagera, juu ya kutumia zana  sahihi za uvuvi na kuacha kutumia zana haramu.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akishuka kwenye boti huku akiwa ameambatana na viongozi wa kikosi maalum cha kupambana na uvuvi haramu wakiwasiri katika kisiwa cha Kerebe mkoa wa Kagera kwa usafiri wa boti.Picha na Emmanuel Massaka.

MIGOGORO YA ARDHI BADO CHANGAMOTO CHALINZE

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

MBUBGE wa Jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete(CCM),amesema migogoro ya ardhi ni moja ya Changamoto kubwa inayotukabili wana Chalinze.

Akizungumza leo na Michuzi Blog amesema kutokana na changamoto hiyo jana ameamua kufanya ziara katika Kijiji cha Kwamduma, Kata ya Kibindu kuangalia athari za migogoro baina ya kijiji na Hifadhi ya Uzigua. 

Amesema katika ziara hiyo ameona hitaji la kukaa chini na watu wa hifadhi kwa lengo la kujadili suala la mipaka inayotembea." Tumekubaliana na Serikali kuingilia hili jambo mara moja na imekubali kulishughulikia ndani ya kipindi kifupi,"amesema Ridhiwan. 

Ameongeza kuwa ataendelea kushirikiana na viongozi wa ngazi mbalimbali na wananchi wa Chalinze ili kupata ufumbuzi wa migogoro ya ardhi ndani ya jimbo hilo.

"Kazi zinazoacha alama, Chalinze ni kazi tu,CCM ni kazi tu, Magufuli ni kazi tu, Kwamduma ni kazi tu na Kibindu ni kazi tu,"amesema Ridhiwan baada ya kufanya ziara hiyo na kuongeza ataendelea kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ya Chalinze.
 
Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete akiangalia mipaka katika kijiji cha Kwamduma jana akiwa na baadhi ya viongozi wa kijiji .

WANANCHI WAZIDI KUJIZOLEA MAMILIONI YA TATUMZUKA,WAZIDI KUNG'ARISHA MAISHA YAO.

$
0
0
  Meneja Mawasiliano kampuni ya michezo ya kubahatisha ya TatuMzuka,Sebastian Maganga alisema kuwa wanayo furaha kubwa ya kuwatambulisha washindi wawili wa Tatumzuka waliopatikana tarehe 21 Januari 2018, jumapili iliyopita kupitia Mzuka Jackpot ambayo pia ilirushwa moja kwa moja kupitia vituo vya ITV, Clouds TV na TV1.

Maganga aliwataja washindi hao kuwa ni Mzee Emmanual Shayo kutoka Pugu Dar es Salaam ambaye alijishindia milioni 27,Mshindi mwingine alikuwa ni Britony Mtalemwa ambaye ametokea Songea,ambaye alijishindia milioni 40.

"Washiriki wa wiki hii walichukua jumla ya milioni 134 kwa pamoja. Washindi wengine wa wiki hii walikuwa ni Gibson Erasmas kutoka Mwanza aliyeondoka na milioni 40 na Andrew Kagoma kutoka Arusha aliyejinyakulia milioni 27'alisema Maganga..

Amesema Tatu Mzuka inawawezesha Watanzania wengi zaidi kutoka sekta mbalimbali na mikoa tofauti kuliko mchezo mwingine wowote. Kama Tatu Mzuka, amini kwamba tunatafuta njia zaidi kukupa fursa ya kuwa milionea kwa kiwango cha chini kabisa cha shilingi 500.Kila saa ndani ya siku, Tatu Mzuka inakupa fursa ya kushinda hadi milioni 6.Kila siku, siku sita za wiki kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi tuna droo ya milioni 10 inayoitwa ‘Mzuka Deile’.

"Na Jumapili ya wiki hii, tuna milioni 60 ambayo inatafutiwa mshindi,Nafasi hizi zote zinapatikana kwako kwa kiasi cha shilingi 500 tu''alimaliza kusema Maganga.



Meneja Mawasiliano kampuni ya michezo ya kubahatisha ya TatuMzuka,Sebastian Maganga akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani,mapema jana jijini Dar wakati wa kuwatambulisha washindi wawili wa Tatumzuka waliopatikana mwishoni mwa wiki Jumapili Januari 21 2018, kupitia Mzuka Jackpot ambayo pia ilirushwa moja kwa moja kupitia vituo vya ITV, Clouds TV na TV1.Pichani kulia ni Mzee Emmanual Shayo kutoka Pugu Dar es Salaam ambaye alijishindia milioni 27. na kushoto ni Britony Mtalemwa kutoka Songea,ambaye alijishindia milioni 40.
Meneja Mawasiliano kampuni ya michezo ya kubahatisha ya TatuMzuka,Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi Ndugu Britony Mtalemwa kutoka Songea,ambaye alijishindia milioni 40.
Meneja Mawasiliano kampuni ya michezo ya kubahatisha ya TatuMzuka,Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundiMzee Emmanual Shayo kutoka Pugu Dar es Salaam ambaye alijishindia milioni 27

TAKUKURU YAKAMILISHA UPEPELZI KESI YA MALINZI, WENZAKE

$
0
0
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania( Takukuru) wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kwa upande wao wamekwisha kamilisha upelelezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa rais Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) Jamali Malinzi na wenzake.

Mbali na Malinzi wengine ni, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine(46) na Mhasibu wa TFF,  Nsiande Isawayo Mwanga(27).

Wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Leonard Swai amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba,leo mahakamani hapo kuwa upelelezi katika shauri hilo kwa Takukuru umeishakamilika na hadi Jumatatu jalada la kesi hiyo litakuwa limekwisha rejeshwa   (DPP).

Awali, Swai alidai mahakamani hapo jalada la kesi hiyo lilipelekwa kwa DPP ambapo alilipitia na kurirejesha Takukuru kwa maelekezo ambapo wamekwisha yafanyia kazi.Kutokana na taarifa hiyo, Hakimu Simba ameahrisha kesi hiyo hadi Februari 8, mwaka huu.

Washtakiwa hao,       walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Juni 29, mwaka 2017, wakikabiliwa na mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha dola za Marekani 375,418. 

Rais Shein Atembelea Kiwanda Cha Samaki Sharjah East Fishing Prosessing

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo K.V.Thomas jinsi ya kuhifadhi samaki na ufanyaji wa peki kwa ajili ya kusafirisha
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo ya utayarishaji wa Kambo hadi kupekiwa kwa ajili ya kusafirishwa nje ya Nchi na katika Soko la ndani akiwa katika ziara yake katika Nchi za Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu UAE 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo ya picha katika gazeti la kiwanda hicho kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Sharjah East Fishing Processing K.V.Thomas , akiwa katika ziara ya Kiserikali katika Nchi za Umoja wa Nchi za Kiarabu UAE 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo ya picha katika gazeti la kiwanda hicho kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Sharjah East Fishing Processing K.V.Thomas , akiwa katika ziara ya Kiserikali katika Nchi za Umoja wa Nchi za Kiarabu UAE
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa mfano Jahazi na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Sharjah East Fishing Processing K.V.Thomas, baada ya kumaliza ziara yake kutembelea kiwanda hicho.


RAIS WA SIMBA FC ALAZWA MUHIMBILI

$
0
0
* Mahakama yaelezwa anasumbuliwa na Figo

MWENDESHA Mashtaka Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa ,(Takukuru) , Leonard Swai ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva amelazwa Hospital ya Taifa ya Muhimbili akisumbuliwa na Figo.

Aveva ambaye ni mshtakiwa wa kwanza shtakiwa mwingine katika kesi ya uhujumu uchumi anashtakiwa pamoja na Makamu rais wa klabu ya Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' ambaye alikuwepo mahakamani hapo

Wakili Swai amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Amedai, walishachukua maelezo ya mshtakiwa wa pili na kwamba wanaangalia jinsi ya kupata maelezo ya mshtakiwa wa kwanza ambaye kwa sasa ni mgonjwa.Baada ya kueleza hayo Hakimu Nongwa ameaihirisha kesi hiyo hadi February 8,2018 kwaajili ya kutajwa.

Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha Dola za kimarekani 300,000.

MRISHO MPOTO ATOA MSAADA KWA YATIMA, AWAPA MSINGI WA MAISHA

$
0
0
 Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto kwa kushirikiana na team yake ya Mpoto Foundation alitembelea kituo cha watoto yatima cha  Mwandaliwa na madrasa ya Tidaiya iliyopo Tandale.
 Akizungumza na waandishi wa habari wakati akikabidhi zawadi hizo, Mpoto alisema lengo kubwa la kutoa zawadi hizo ni kusaidia malezi ya watoto katika vituo hivyo ili wakue wakiwa katika maadili mazuri.
“Nimeamua kugawana na watoto kidogo nilichojaliwa nacho ili waweze kufurahi lakini pia kuwasaidia katika makuzi hasa kwenye suala zima la kidini na maadili.” alisema Mpoto.

Aidha Mpoto aliongeza kuwa kutokana na mambo mengi yanayoendelea kwa sasa nchini na duniani kote, kuna uwezekano kwa watoto kukua bila misingi mizuri ya dini, heshima na uzalendo kama wasipoandaliwa mazingira mazuri.

Ili kuhakikisha hilo halitokei, Mpoto amesema imekuwa sababu kubwa iliyompelekea kujitolea zawadi hizo ambapo kwa yeye ni kuufungua mwaka 2018 akiwa na thawabu kutoka kwa watoto.

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI,MALIASILI NA MAZINGIRA YAVUTIWA NA UBUNIFU WA HIFADHI YA TAIFA YA ZIWA MANYARA.

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa),Allan Kijazi akizungumza kwenye kikao cha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira iliyofanya ziara ya kikazi kwenye Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara mkoa wa Arusha,kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga. 
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Millanzi akizungumza kwenye kikao na kamati hiyo,kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo,Kemilembe Lwota akifatilia kwa makini. 
Mbunge wa jimbo la Sumve mkoa wa Mwanza,Richard Ndassa(kushoto),Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga(katikati) na Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete wakiwa ndani ya Hifadhi hiyo. 
Meneja Ujirani Mwema wa Tanapa,Hemed Mbugi akitembea juu ya daraja linalo ‘bembea’ ambalo ni moja kivutio kwa watalii wa nje na ndani. 
Mbunge wa jimbo la Mtama mkoa wa Lindi akifurahia daraja linalo ‘bembea’ ambalo ni moja kivutio kwa watalii wa nje ya nchi na ndani. 

KORTINI KWA KUTAMKA UONGO KIASI CHA FEDHA ZA KIGENI ALIZOKUWANAZO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

MFANYABIASHARA Boniface Mbilinyi (32) amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka kutamka uongo wa kiasi cha fedha alichokuwa nacho.

Mbilinyi anadaiwa kutamka kuwa na dola za Kimarekani 40,000 huku akiwa na dola 123,000. 

Mwendesha mashtaka wakili wa Serikali Mwandamizi, Awamu Mbagwa amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi kuwa Januari 13, mwaka huu,  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Jk Nyerere uliopo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar Es Salaami mshtakiwa alitenda kosa.

Amedai wakati mshtakiwa huyo akisafiri  kutoka nje ya Tanzania alitoa tamko la uongo kuhusiana na kiasi cha fedha alichokuwa nacho kwa kudai kuwa alitamka  kuwa ana kiasi cha dola 40,000 wakati ukweli alikuwa na dola 123,000.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulidai upelelezi umekamilika na wapo tayari kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali (PH).

Wakili wa mshtakiwa huyo, Ndigwako Joel alieleza mahakama kuwa hawajajiandaa kwa leo kusikiliza PH, hivyo aliomba wapewe tarehe ya karibu.

Pia aliiomba Mahakama impatie mteja wake kwa sababu shtaka linalomkabili linadhaminika kwa mujibu wa sheria.

Wakili Mbagwa alidai wao kama upande wa mashtaka hawapingi dhamana ila aliikumbusha Mahakama wakati ikitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa huyo izingatie kifungu cha 148(5)(e) kinachoelekeza mshtakiwa anayetuhumiwa na kiasi cha fedha kinachozidi Sh 10 milioni ni lazima alipe nusu ya kiasi hicho cha fedha.

Pia aliomba kiasi hicho cha fedha kilichopo katika hati ya mashtaka kisitumike kama sehemu ya dhamana kwa mshtakiwa huyo.

Baada ya kuwasilishwa kwa hoja hizo, Hakimu Shaidi alisema kwa kuwa fedha hizo zipo mikononi kwa Serikali, aliamuru mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua na kitambulisho na fedha hizo zitasimama kama bondi.

Kesi imeahirishwa hadi Februari 7, 2018.

BILIONI 499 ZIMIDHINISHWA KUTEKELEZA MIRADI YA UMEME PEKEE – MGALU

$
0
0
Na Veronica Simba – Dodoma

Serikali imebainisha kuwa jumla ya shilingi bilioni 499 zimeidhinishwa na Bunge kwa ajili ya kutekeleza miradi ya umeme nchini kote katika mwaka huu wa fedha unaoendelea.

Hayo yalisemwa jana, Januari 24 na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwa katika ziara katika maeneo mbalimbali ya Dodoma Mjini kwa ajili ya kujionea hali ya upatikanaji wa nishati hiyo muhimu pamoja na kuzungumza na wananchi.

Naibu Waziri Mgalu, ambaye aliambatana na Mbunge wa Dodoma Mjini, Antony Mavunde aliwaambia wananchi wa maeneo aliyotembelea kuwa, kiasi hicho cha fedha ni kikubwa na kitawezesha utekelezaji wa miradi hiyo ya umeme katika vijiji vyote 7873 vilivyosalia nchi nzima.

“Tunamshukuru Mheshimiwa Rais John Magufuli pamoja na Bunge la Jamhuri kutuidhinishia kiasi hicho cha fedha. Kazi yetu sisi wasaidizi wake katika Wizara ya Nishati ni kuhakikisha tunatekeleza jukumu alilotutuma la kuwapelekea wananchi kote nchini nishati ya umeme wa uhakika. Tunaahidi hilo litafanyika kwa ukamilifu.”
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Chisichili Kata ya Mkonze mkoani Dodoma wakati wa ziara yake kujionea hali ya upatikanaji wa umeme.
Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde (aliyesimama), akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (wa pili kutoka kulia), kujionea hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo mbalimbali ya Dodoma Mjini.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (kulia) akibadilishana mawazo na wananchi wa Mtaa wa Chisichili, Kata ya Mkonze mkoani Dodoma wakati wa ziara yake kujionea hali ya upatikanaji wa umeme. Kulia kwake ni Mbunge wa Dodoma Mjini Antony Mavunde.
Wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri Subira Mgalu (hayupo pichani) wakati wa ziara yake kujionea hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo mbalimbali ya Dodoma Mjini.
Wananchi wakiuliza maswali na kutoa maoni mbele ya Naibu Waziri Subira Mgalu (hayupo pichani) wakati wa ziara yake kujionea hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo mbalimbali ya Dodoma Mjini.


MENEJA HIFADHI YA CHAKULA MKOA WA RUVUMA AKAMATWA

$
0
0
Kauli ya kukamatwa kwa wafanyakazi wa hifadhi ya chakula pamoja na mmiliki wa ghala binafsi linakuja baada ya kufanya ziara ya kushtukiza na kukuta shehena ya mahindi ya serikali yaliyoibiwa na kuhifadhiwa kwenye ghala binafsi kiasi ambacho hadi sasa hakijaulikana.

WAZAZI NA WALEZI HANANG WATAKAOKWAMISHA MPANGO WA ELIMU BILA MALIPO KUKIONA

$
0
0


Na. Jumbe Ismailly, Hanang 

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Bryceson Kibassa amepiga mafuruku walimu wa shule za msingi kuwatoza wazazi na walezi wa watoto michango ya aina yeyote ile na kuwahakikishia kwamba hakuna mtoto wa wilaya hiyo atakayetakiwa kukosa elimu kwa kisingizio cha kutolipa michango.

Mkurugenzi huyo alitoa tahadhari hiyo kwenye mkutano maalumu wa Baraza la madiwani lililokutana kupitisha mapendekezo ya makisio ya mpango na bajeti ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Akifafanua kuhusu mpango wa elimu ya msingi bila malipo Kibassa alisisitiza kwamba kusiwepo na mtoto yeyote Yule wa Hanang ambaye atashindwa kwenda kusoma shule kwa kisingizio wa mchango wa aina yeyyote ile.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo michango inayoruhusiwa ni ile tu ya kijamii wanayokubaliana kwa ajili ya kuboresha miundombinu bila kugusa ile michango ambayo kwenye waraka inatajwa kwamba msichangishe,isiwe kikwazo cha kuzuia mtoto yeyote kwenda shuleni.

“Tunataka watoto wote wa Hanang kwa agizo na Mheshimiwa Rais na agizo la serikali ya awamu ya tano watoto wote wawepo shuleni na kusijekuwa na mchango wa aina yeyote unaozuia mtoto wa Hanang kwenda shuleni.”alifafanua Mkurugenzi huyo.

Viewing all 110126 articles
Browse latest View live




Latest Images