Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

WAGOMBE 27 WATEULIWA MAJIMBO 2 KATA 4

$
0
0
Hussein Makame-NEC

WAGOMBEA 27 wa ubunge na udiwani wameteuliwa kugombea nafasi hizo katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Februari 17, mwaka huu katika majimbo mawili ya ubunge na kata nne.


Katika uteuzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki,  mgombea udiwani kupitita CCM katika kata ya Kimagai iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya  Mpwapwa mkoani Dodoma, amepita bila kupingwa.


Mbali na uteuzi huo, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi katika kata sita za Tanzania Bara wanatarajia kuteua wagombea wa udiwani wa kata hizo siku ya Jumatano ya tarehe 24 Januari, 2018 kukamilisha kata 10 zilizopangwa kushiriki Uchaguzi Mdogo wa Februari 17, 2018.


Akizungumzi uteuzi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Hamis Mkunga amesema mgombea huyo wa CCMa amepita bila kupingwa baada ya mgombea wa CHADEMA kushindwa kurejesha fomu za uteuzi.


Amesema katika uteuzi wa wagombea Jimbo la Kinondoni, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo amewateua wagombea 12 ambao ni ambao ni Godfrey Maliza  kutoka chama cha TLP, Johnson Mwangosya  (SAU) na  Mwajuma Milambo kutoka UMD.

Mkunga amewataja wagombea wengine walioteuliwa kuwa ni John January Mboya  (Demokrasia Makini), Maulidi Mtulia (CCM), na Mary Mpangala wa DP.

Wengine ni Salim Mwalimu  (CHADEMA), Rajabu Salum (CUF), Mohamed Majaliwa (NRA), George Christian (CCK),  Ally Omari Abdallah (ADA THADEA) na Ashiri Kiwendu wa AFP 


Kuhusu uteuzi wa wagombea ubunge katika Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro, Mkunga amewataja wagombea wanne walioteuliwa kuwa ni Dk Godwin Mollel (CCM) Mdoe Azania Yambazi (SAU), Tumsifuheri Mwanry (CUF) naElvis Christopher MosiwaCHADEMA.


Katika kata tatu zilizobaki, Mkunga amevitaja vyama vya siasa vilivyopitisha wagombea ambao waliteuliwa katika kata ya Isamilo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza kuwa ni Chama cha CUF, DP, UDP, CCM, na CHADEMA.
Amevikumbusha vyama na wagombea kuheshimu maadili ya uchaguzi katika kipindi hiki cha kampeni kwani vyama vyote vimekubaliana kuheshimu maadili hayo na kuwaomba wananchi wajitokeze kwa wingisiku ya kupiga tarehe 17 Februari mwaka 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



WANAVYUO WATAKIWA KUTUMIA NAFASI ZAO KULINDA NA KUHIFADHI MAZINGIRA

$
0
0
Na Tiganya Vincent

WANAVYUO Mkoani Tabora wameagizwa kuhakikisha kuwa wanatumia elimu wanayopata kuwa mabalozi watakaosaidia katika kuzuia uharibufu wa mazingira na kuwahimiza jamii kujenga utamaduni wa kupanda miti mipya na kulinda iliyopo kwa ajili ya manufaa yao ya sasa na baadae.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati alipowaongoza wanavyuo kutoka Vyuo mbalimbali katika upandaji miti ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhakikisha kila mtu anashiriki katika zoezi hilo.

Alisema kuwa wasomi kama wanavyuo wakiwa mstari wa mbele katika utoaji wa elimu katika maeneo yao yanayowazunguka na sehemu za baadae watakazopangiwa kazi ipo nafasi ya kuzuia uharibifu wa mazingira ikiwemo mistu kuendelea kuharibiwa.

Mwanri alisema kuwa jamii inawategemea sana wasomi katika kutoa elimu katika hatua ya awali ya kuzuia uharibifu kabla ya masuala mengine kama matumizi ya nguvu za dola hayafanyika katika kuzuia uharibifu usiendelee.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa kitendo cha wanachuo hao kuomba kuweka alama katika Mkoa wa Tabora kinapaswa kuwa mwanzo kwao katika katika kupeleka elimu hiyo katika maeneo mbalimbali ya jamii inayowazunguka ili wananchi wengi waweze kutambua umuhimu wa kutoharibu mazingira na vyanzo vya maji.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tabora Idd Moshi aliwataka Wanachuo kuunga mkono juhudi za Mkuu huyo wa Mkoa wa kutaka kuigeuza sehemu ya kijana kwa kupanda miti miti na kurudisha uoto wa asili.

Alisema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora anafanyakazi nzuri ya kuhakikisha anasimamia agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha mikoa yote hapa nchini inapanda miti mingi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Moshi alisema kuwa wanachuo na jamii kwa ujumla wanalojukumu la kuhakikisha kuwa wanaunga mkono viongozi kwa kupanda miti sio katika maeneo ya umma katika maeneo wanayoishi.

Alisema kuwa wao wakiwa vijana wa CCM mkoa wa Tabora wameshapanda miti katika Wilaya ya Igunga , Nzega, Sikonge na Urambo katika kuunga mkono juhudi za viongozi wa Mkoa na Kitaifa.

SAIDA KAROLI KUPAMBA TAMASHA LA 15 LA SAUTI ZA BUSARA 2018

$
0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Msanii wa nyimbo za asili Saida Karoli anatarajia kutuimbuiza katika tamasha la busara 2018 linalotarajia kuanza Februari 8, 2018 Ngome Kongwe mjini Unguja, Zanzibar.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Yusuf Mohamed alisema tamasha linazingatia Zanzibar na Tanzania sehemu mbalimbali duniani kwa kuwa linavutia mapromota wa kimataifa na kutoa fursa adhimu kwa wanamuziki wa Afrika Mashariki kuupeleka duniani kote.

Bw. Yusuf alisema kuwa wanamshukuru Mungu kwakuweza kukutana na msanii Saida Karoli ambaye amekubali kushiriki tamasha la sauti za Busara 2018 kwa vile sasa ni miaka 13 tokea ameweza kushiriki tamasha hilo.

Alisisitiza kuwa, orodha ya mwaka 2018 ni bora kuwahi kutokea kwa miaka yote 15 ya uhai wa tamasha hilo. "Ndani ya majukwaa matatu kwa siku nne, tamasha litakuwa na naonyesho 46 yenye hadhi ya kimataifa ambayo kwa asilimia 100 yatapigwa mubashara.

"Tamasha litawaleta pamoja wanamuziki wadogo na wakubwa kutoka katika viunga vyetu na hata nje ya nchi, likibeba dhumuni moja, huku tukisimama pamoja kupitia kaulimbiu ya Kuunganishwa na Muziki," alisema Yusuf.

Msanii wa nyimbo za asili Saida Karoli (pichani) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ushiriki wake katika tamasha la busara 2018 ambapo yeye mwenyewe alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kuweza kushiriki tokea mwaka 2005. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud, Balozi wa Uswizi nchini Tanzania, Mhe. Florence Tinguely Mattli.
Waandishi wa Habari wakifuatilia.

NHIF kuimarisha na kuboresha huduma za matibabu nchini

$
0
0
Na Grace Michael, Geita
MKUU wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel ameupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa namna ulivyojipanga na unavyoshirikiana na Uongozi wa Mikoa mbalimbali kwa lengo la kuimarisha na kuboresha huduma za matibabu nchini.
Pongezi hizo amezitoa leo wakati akipokea msaada wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Mfuko katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu. 
“NHIF nawapongeza sana kwa namna ambavyo mmekuwa tayari wakati wote kuhakikisha huduma za matibabu zinakuwa bora zaidi na niwahakikishie tu kwamba Mkoa umejipanga kutoa huduma kwa wananchi ambazo ni za kiwango cha juu kwani kama viongozi tuna deni la kuwatumikia Watanzania,” anasema.
Injinia Gabriel aliutaka Mfuko kutochoka kutoa misaada kama hiyo ambayo inalenga kuwanufaisha wananchi moja kwa moja.
Alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. Pombe John Magufuli imedhamiria kusogeza huduma kwa wananchi hivyo Mkoa unatekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za matibabu ili kuondokana na changamoto za huduma za afya.
Akikabidhi msaada huo, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Bi. Anjela Mziray alisema jukumu kubwa la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ni kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa Watanzania kupitia mfumo wa bima ya afya.
 Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bi. Anjela Mziray akionesha vifaa vya msaada vilivyotolewa na Mfuko huo katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel akipokea vitanda 20, magodoro 20 na mashuka 80 msada ambao umetolewa na NHIF.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel akikalia kitanda kwa lengo la kukagua ubora wake.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel akichunguza kitanda hicho na kuangalia ubora wa mashuka yaliyokabidhiwa.
 Baadhi ya Watumishi wa Hospitali hiyo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa katika hafla ya kukabidhiwa kwa vifaa hivyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

POWER ON FITNESS GYM KUUKARIBISHA MWAKA MPYA KWA STYLE YA KIPEKEE

$
0
0
Power on Fitness Gym iliyopo Mwenge, Kinondoni Jijini Dar es salaam imeandaa siku maalumu kwa ajili ya kujumuika pamoja, kufanya mazoezi na kuukaribisha mwaka mpya wa 2018.

 Shughuli hiyo itafanyika siku ya Jumamosi January 27, 2018  katika viwanja vya Posta vilivyopo Sayansi,  Kijitonyama. Shughuli hii itanzaa saa 12 asubuhi mpaka usiku.

Siku hiyo kutakuwa na mazoezi ya kukimbia(Jogging) ambayo itaanza alfajiri ya saa 12, na kufuatiwa na mazoezi ya Aerobics, Steps, Zumba, Mpira wa miguu, na michezo mingine kama kuvuta Kamba, Kukimbiza Kuku nk.

Baada ya mazoezi, kutakuwa na burudani kabambe ya muziki itakayoongozwa na bendi ya Skylight bila kusahau burudani ya muziki itakayoporomoshwa na Ma DJ wakali wa hapa nchini.
Siku hiyo pia kutakuwa na Nyama choma itakayoandaliwa kiufundi na wapishi waliobobea, Supu bila kusahau vinywaji vya kila aina. 

Wadahamini wa shughuli hiyo ni Kampuni ya JSP Marketing Link Limited ikishirikiana na Msouth Company, Dagaa Microfinance Limited, Simba Makini Group, Jaina Ice Cubes, Micgen Insurance Brokers, TTCL na wenyeji Power on Fitness Gym.

MADAKTARI WA INDIA WATOA HUDUMA YA MATIBABU HOSPITALI YA J.P.M

$
0
0
 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

HOSPITALI ya J.PM  imesema ujio wa madaktari wa India katika hospitali hiyo kumesaidia wananchi wa Jiji Dar es Salaam kuonana na madaktari hao, kupata vipimo na dawa kwa gharama nafuu.

Akizungumza Dar es Salaam,Mkurugenzi hospitali hiyo, Dk. Ameir Binzoo amesema huduma iliyofanyika katika hospitali hiyo kati ya Januari 19 na 20 mwaka huu imeleta matumaini kwa wananchi kuonana na madaktari wabobezi katika magonjwa mbalimbali.

Amesema madaktari hao walijikita kutoa huduma ya matibabu ya magonjwa ya moyo, mifereji ya mikojo na magonjwa ya wanawake.

Binzoo amesema  wananchi wengi walijitokeza kupata huduma mbalimbali katika Hospitali ya J.P.M  na kuongeza wataendelea kufanya utaratibu huo kila mara ili Watanzania wengi kupata huduma hiyo.


Mkurugenzi wa Hospitali ya J.P.M , Dk. Ameir Binzoo akizungumza na waandishi habari kuhusu huduma waliotoa kwa ushirikiano na madaktari wa India ,jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Hospitali ya J.P.M, Dk. Ameir Binzoo akionesha kifaa kitakachotumika kutoa huduma za afya kwa masafa kati mgonjwa na daktari akiwa nchini India, jijini Dar es Salaam.
 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

HOSPITALI ya J.PM  imesema ujio wa madaktari wa India katika hospitali hiyo kumesaidia wananchi wa Jiji Dar es Salaam kuonana na madaktari hao, kupata vipimo na dawa kwa gharama nafuu.

Akizungumza Dar es Salaam,Mkurugenzi hospitali hiyo, Dk. Ameir Binzoo amesema huduma iliyofanyika katika hospitali hiyo kati ya Januari 19 na 20 mwaka huu imeleta matumaini kwa wananchi kuonana na madaktari wabobezi katika magonjwa mbalimbali.

Amesema madaktari hao walijikita kutoa huduma ya matibabu ya magonjwa ya moyo, mifereji ya mikojo na magonjwa ya wanawake.

Binzoo amesema  wananchi wengi walijitokeza kupata huduma mbalimbali katika Hospitali ya J.P.M  na kuongeza wataendelea kufanya utaratibu huo kila mara ili Watanzania wengi kupata huduma hiyo.


Mkurugenzi wa Hospitali ya J.P.M , Dk. Ameir Binzoo akizungumza na waandishi habari kuhusu huduma waliotoa kwa ushirikiano na madaktari wa India ,jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Hospitali ya J.P.M, Dk. Ameir Binzoo akionesha kifaa kitakachotumika kutoa huduma za afya kwa masafa kati mgonjwa na daktari akiwa nchini India, jijini Dar es Salaam.

YANGA NI TIMU NZURI, TUTAINGIA KWA UMAKINI MKUBWA- KOCHA AZAM

$
0
0
KOCHA Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba amesema mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Yanga utakuwa mgumu na watacheza kwa umakini ili waibuke na ushindi.

Azam FC watakuwa wenyeji wa Yanga SC Jumamosi wiki hii Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam wakitoka kushinda 2-0 ugenini dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Jumapili.

Cioaba amesema Yanga ni moja ya timu kubwa nchini ikitoka kutwaa ubingwa wa ligi msimu uliopita na kudai kuwa wataingia uwanjani na kuonyesha uwezo mkubwa.

“Mechi itakuwa Chamazi, hautakuwa mchezo mwepesi nitakuwa na muda wa siku tatu wa maandalizi kwa kuwa nina safari ndefu sana na wachezaji wanauchovu kidogo lakini siku hizo tatu nitawaunganisha vema wachezaji na kujaribukufanya vizuri dhidi ya Yanga Chamazi, sihitaji kupoteza mchezo wowote hapo baadaye,”amesema.

Hadi sasa ikiwa imecheza mechi 14 za ligi, Azam FC imefanikiwa kuwa rekodi bora baada ya kutopoteza mchezo hata mmoja, ikiwa imeshinda mechi nane na sare sita ikiwa kileleni kwa pointi zake 30 ikiizidi mechi moja Simba ambayo ipo nafasi ya pili ikijikusanyia 29.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AKUTANA NA WATENDAJI WA ASASI YA INTERNATIONAL YOUTH FELLOWSHIP JIJINI DAR

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiteta jambo Ofisini kwake  na Maafisa Watendaji wa Asasi ya International Youth Fellowship(IYF), leo Januari 23, 2018 walipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza ambapo Watendaji wa Asasi hiyo wamewalisha mada kuhusu mafunzo yanayolenga mabadiliko ya mitizamo kwa wafungwa katika kuachana na tabia za kihalifu mara wamalizapo vifungo magerezani.  
 Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya International Youth Fellowship (IYF),  Jeon Hee yong akitoa mada mbele ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) kuhusiana na mabadiliko ya mitizamo kwa wafungwa katika kuachana na tabia za kihalifu mara wamalizapo vifungo vyao magerezani
 Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa umakini mada kutoka kwa Watendaji wa Asasi ya International Youth Fellowship (IYF) katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza(wa kwanza kushoto) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila..
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akitoa taarifa fupi kabla ya  Watendaji wa Asasi ya International Youth Fellowship (IYFkuwasilisha mada yao katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo Januari 23, 2018.
 Kikundi cha Kwaya cha Asasi ya International Youth Fellowship ambacho kinaundwa raia kutoka nchini Korea kikitumbuiza kabla ya uwasilishaji wa mada kama inavyoonekana katika picha.
 Wataalam wa Jeshi la Magereza wakifuatilia Mada kuhusu mabadiliko ya mitizamo kwa wafungwa katika kuachana na tabia za kihalifu.
Kamishna Jenaerali wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Asasi ya International Youth Fellowship walioketi(wa kwanza kushoto) ni  Mkurugenzi Mkazi wa Asasi hiyo Bw. Jeon Hee yong(wa kwanza kulia) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila. Wengine waliosimama mstari wa nyuma ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza, leo Januari 23, 2018 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

SERIKALI KUENDESHA MNADA WA HADHARA WA MENO YA VIBOKO JANUARI 29 JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Hamza Temba - WMU- Dodoma

*Wanunuzi wataruhusiwa kuyakagua (Januari 25 na 26) kabla ya mnada
*Watakaovuruga mnada kukiona cha mtemakuni

SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) itafanya mnada wa hadhara wa meno ya viboko vipande 12,467 vyenye uzito wa kilo 3,580.29.

Mnada huo utakaosimamiwa na Wizara ya Fedha na Mipango umepangwa kufanyika tarehe 29 Januari, 2018 kuanzia saa nne asubuhi katika Jengo la Mpingo, Barabara ya Nyerere Jijini Dar es Salaam, zilipokuwa  ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii (Ivory Room).

Kupitia taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dk. James Wakibara amesema  mnada huo utawahusisha wafanyabiashara wa Nyara waliopewa leseni ya Nyara Daraja la Kwanza mwaka 2017.

Amesema wafanyabiashara hao wataruhusiwa kukagua meno hayo kati ya tarehe 25 na 26 Januari, 2018 kuanzia saa nne asubuhi hadi saa tisa na nusu jioni kabla ya siku ya mnada huo.Aidha, amesema wanunuzi watakaoshinda mnada huo watatakiwa kulipa asilimia 25 ya malipo yote papo hapo na asilimia 75 itakayosalia itatakiwa kulipwa ndani ya siku kumi na nne zijazo baada ya mnada huo.

“Mtu yeyote atakayekuwa ametamka bei ya juu, kisha akashindwa kulipa asilimia 25 ya bei aliyotamka, atachukuliwa kuwa ni mwenye kutaka kuvuruga mnada na hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake,” ameonya Mkurugenzi huyo.

Amesema meno hayo yatauzwa kwa wastani wa uzito wa nusu kilo bila kugawanywa au kuchambuliwa wakati wa mnada na wanunuzi wataruhusiwa kuondoa bidhaa kwenye eneo la mnada baada ya kulipia ada na kodi husika kikamilifu na kupewa hati ya kumiliki nyara hizo.

Mnada huo utafanyika katika Jengo hili la Mpingo (Mpingo House) ambalo awali lilikuwa Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii kabla ya kuhamia Makao Makuu ya Nchi mjini Dodoma. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Dk. James Wakibara (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya 15 ya Jeshi Usu kwa kwa Maafisa wa Wanyamapori 87 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania– TAWA, Shirika la Hifadhi za Taifa – TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro hivi karibuni Mkoani Katavi. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Rachel Kasanda.

SIMBA SC WAREJEA DAR KWA RAHA ZAO

$
0
0
Na Agness Francis, Globu ya Jamii.

KIKOSI cha Wekundu wa Msimbazi Simba SC kimewasili leo jijini Dar es Salaam kikitokea mkoani Kagera kilikokuwa na mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar.

Mchezo huo uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Kaitaba ambapo Simba wameibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Akizungumza na Michuzi Blog baada ya kuwasili leo,jijini Dar es Salaam katika uwanja kimataifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Kocha Msaidizi wa Simba Massoud Djuma amesema kuwa anawashukuru wachezaji wake kwa kufanya vizuri kwenye Ligi kuu Tanzania Bara.

Amesema anaamini watafika mbali wakiendelea kucheza kwa kumsikiliza Mwalimu. Aidha Mwalimu huyo amewapongeza wachezaji kwa jinsi wanavyojituma." Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu tumerejea salama, pia niwapongeze wachezaji wangu kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu, naimani tukicheza kwa ushirikiano tutazidi kufanya vizuri zaidi na zaidi,"amesema Masoud 

Wakati huohuo mchezaji Shomari Kapombe baada ya takribani miezi sita aliyokuwa akiumwa jana amepata nafasi ya kucheza na ameonesha kiwango kikubwa katika mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar na kutengeneza nafasi ya goli la pili ililofungwa na John Bocco dakika ya 79.

Kapombe amesema kuwa anamshuru mwalimu (Massoud Djuma) kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kucheza mchezo wa jana na anaamini ataendelea kufanya vizuri katika Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.


 Mchezaji wa wekundu wa Msimbazi SimbaSc Shomari Kapombe akizungumza na waandishi wa habari alipowasili leo Jijini Dar Es Salaam katika uwanja wa Mwalimu J.K. Nyerere.
Kocha Msaidizi  wa Simba Massoud Djuma akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwa sili leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa kimataifa Mwalimu J.K. Nyerere akiwapongeza wachezaji ea Kikosi hicho kwa kufata maelekezo yake  na kufanya vizuri.

RC MASENZA AZIPIGA JEKI SHULE TANO MKOANI IRINGA

$
0
0
Na Fredy Mgunda,Kilolo

MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ametoa jumla ya shilingi milioni nne (4,000,000) kwa ajili ya kuchochea manendeleo ya ujenzi majengo kwenye shule nne za sekondari ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa wanafunzi wa shule hizo wanasoma bila kuwa na usumbufu wowote ule.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa shule mpya za sekondari zilizopo tarafa ya Mazombe mkuu wa mkoa Amina Masenza alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila kulipia kitu mchango wowote ule utakaochangishwa na walimu.

“Mimi nimetumwa na Rais kusisimamia ila ya chama cha mapinduzi kuhakikisha inatendewa haki katika kuleta maendeleo hivyo ni lazima nihakikishe wanafunzi wanakwenda shule na sio vinginevyo maana bila wanafunzi kwenda shule Rais hawezi kunielewa nitakuwa sijatimiza malengo ya kutoa elimu bila malipo” alisema Masenza

Masenza alisema kuwa atachangia shilingi milioni moja kwa kila shule za sekondari za tarafa hiyo ambazo zipo kwenye ujenzi na shule hizo ni Ibumu na Nyanzwa ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma na kuwapunguzia umbali wa kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kuifuata shule.

“Naombeni tuzikamilishe shule hizi kwa wakati ili kuwapunguzia umbali wa kusoma watoto wetu haiwezekani wanafunzi hadi kuikuta shule moja ni umbali wa zaidi ya kilometa kumi na tatu ,jamani hawa ni watoto zetu na maisha yao yanategemea elimu hivyo ni lazima tuwekeze kwenye elimu” alisema Masenza
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari ambayo inajengwa kwa nguvu za wananchi na serikali kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu mkoani Iringa
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua vyoo vya shule ya Nyanzwa 
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua vyoo katika sekondari ya Ibumu
Na hili ni moja ya jengo ambalo linajengwa kwa ajili ya maabara za shule ya sekondari ya Ibumu.

CAF YAJA TANZANIA UKAGUZI MFUMO WA LESENI KWA VILABU

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF litafanya ukaguzi wa mfumo wa leseni kwa vilabu (Club Licencing) kwenye upande wa miundo mbinu.

CAF watafanya ukaguzi huo wa kutembelea na kutazama miundo mbinu ili kuhakikisha mfumo huo unatekelezeka ipasavyo kwa kuanzia na mtazamo wa vigezo vya miundo mbinu.

Wakati wa miaka kadhaa ya kuzindua mfumo huo wa leseni kwa vilabu ni wazi changamoto kubwa kwenye Bara la Africa imekuwa ni vigezo vya miundo mbinu ambayo kwenye baadhi ya viwanja vinavyotumika wakati wa mashindano imekuwa ikitoa taswira isiyo nzuri kwa mashindano ya CAF.

Kwa mwaka huu 2018 wameandaa ukaguzi kutembelea klabu zote zitakazoshiriki hatua ya makundi kwenye mashindano ya vilabu ya CAF wakijielekeza kwenye kiwango na ubora wa viwanja vya kucheza mechi na viwanja walivyochagua kwa mazoezi.

Caf watachagua kundi la wakaguzi watakaotembelea kwenye klabu za kila mwanachama wake ili kukusanya ripoti itakayowasilishwa na moja kati ya ripoti hiyo ni miundo mbinu ya Uwanja,ripoti itakayothibitisha kama uwanja umefikia kwenye mahitaji ya juu ya kutumika kwa mechi za CAF.

Viwanja ambavyo havitakidhi mahitaji hayo ya juu hautaidhinishwa kutumika kwa mashindano na hautatumika kwa mchezo wowote wa hatua hiyo ya makundi kwa mashindano ya klabu kwa mwaka huu 2018.

UKAGUZI WA VIWANJA KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM VITATU KUTOTUMIKA HATUA YA RAUNDI YA TATU

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF limefanya ukaguzi wa viwanja vinavyotumika kwa kombe la Shirikisho na kuzuia viwanja vitatu kutumika kwa mechi zinazofuata za hatua ya raundi ya tatu.

Viwanja ambavyo havitaweza kutumika kwa raundi hiyo ya tatu ni pamoja na Uwanja wa Nachingwea unaotumiwa na Majimaji Rangers ambao watalazimika kwenda Ilulu Lindi kucheza mchezo wake na Mtibwa Sugar kwenye raundi hiyo.

Uwanja mwingine ni uwanja wa CCM Mkamba Morogoro unaotumiwa na timu ya Shupavu nao hautatumika kwa raundi hiyo na badala yake Shupavu watautumia Uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa mchezo wake na Azam FC.

Nayo timu ya Ihefu ya Mbarali haitatumia Uwanja wake kwa raundi ya tatu dhidi ya Yanga na badala yake mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Mbeya.

INTRODUCING Nzaya Don Ngosha ft Mirror - Achana na Mimi

SABA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUIBA NYAYA ZA UMEME

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

WATU saba wakazi wa sehemu tofauti jijini Dar es Salaam,wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kuiba roli nne za waya za umeme zenye thamani ya Dola za Marekani 52268.78 sawa na Sh.116,872,813 mali ya  Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco).

Mwendesha mashtaka wakili wa Serikali, Herieth Lopa amewataja washtakiwa hao kuwa ni Mbatia Mhando (35), Abdallah Tambwambwa (39),  Willy Mgimbudzi (32), Francis Nchimbi (50), Ally Mohammed (42), Hassan Haji (29) na Misana Selestine (27).

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu mkazi Mkuu, Huruma Shaidi Wakili Lopa amedai, Desemba 16 mwaka 2017 huko Tabata Kinyerezi washtakiwa hao waliiba roli hizo nne za nyaya za umeme zenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Wakili huyo wa Serikali alidai katika kipindi hicho,washtakiwa kwa vitendo vyao na kwa makusudi walisababisha hasara ya Sh 116,872,813 mali ya Tanesco.Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa hao hawakuruhusiwa kuzungumza chochote kwa sababu Mahakama haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.

Kesi imeahirishwa  hadi Februari 7, mwaka 2018.Katika kesi nyingine, Peter Mdegera na Ali Mayumba wamefikishwa mahakamani hapo,kujibu tuhuma za kukutwa na kilo 192.46 za dawa za kulevya aina ya bangi.Wakili wa Serikali, Lopa amedai mbele ya Hakimu Shaidi kuwa  Septemba 7, mwaka 2017 katika Mtaa wa Tarangile Mbezi Beach washtakiwa hao walikuwa wakiwa bangi hizo.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, washtakiwa hao hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu ya Tanzania.Hata hivyo baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, mshtakiwa Ali alieleza mahakamani hapo kuwa anaumwa mguu kwa kuwa alipigwa na askari na kwamba kutokana na kipigo hicho sehemu zake za siri za kiume azisimami hivyo anahitaji msaada wa matibabu.

Mbali na Ali na mshtakiwa mwenzake Peter anaye alilalamika kuwa naye alipigwa.Baada ya kuwasikiliza washtakiwa hao, Hakimu Shaidi aliwaeleza wakipelekwa gerezani watapatiwa matibabu na kama hawatapatiwe tarehe ijayo watoe taarifa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februairi 7,2018 washtakiwa walipelekwa rumande.  

BALOZI WA UFILIPINO AKUTANA NA IGP SIRRO

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro (kulia),  akizungumza na Balozi wa Ufilipino hapa nchini Mhe.Uriel Norman R. Garibay, mwenye Makazi yake Nairobi nchini Kenya aliyefika Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam leo kwa lengo la kujitambulisha tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo ambapo pia wamejadiliana masuala mbalimbali ikiwamo Usalama pamoja na kuendeleza ushirikiano. Picha na Jeshi la Polisi.
 IGP Simon Sirro, akiwa katika picha na Balozi wa Ufilipino hapa nchini Mhe.Uriel Norman R. Garibay, mwenye Makazi yake Nairobi nchini Kenya pamoja na ujumbe alioongozananao Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam leo kwa lengo la kujitambulisha tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo ambapo pia wamejadiliana masuala mbalimbali ikiwamo Usalama pamoja na kuendeleza ushirikiano.. Picha na Jeshi la Polisi.
Balozi wa Ufilipino hapa nchini Mhe.Uriel Norman R. Garibay (kushoto), mwenye Makazi yake Nairobi nchini Kenya, akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, wakati alipofika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa lengo la kujitambulisha tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo ambapo pia ametumia fursa hiyo kujadiliana masula ya Kiusalama. Picha na Jeshi la Polisi.

WIKI YA SHERIA KUFANYIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA

Uongozi wa Kampuni ya iSAtech ya Ujerumani Watembelea ubalozi wa Tanzania mjini berlin

$
0
0
Kampuni ya isatech Water  Watengenezaji wa mita za maji za kutumia LUKU kwa ajili ya matumizi mbali mbali kama Water Kiosk kwa matumizi ya community , Domestic meter kwa makazi na  meter kubwa kwa ajili ya viwanda na taasisi. 
Katika mazungumzo yao  Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dkt. Abdallah  Possi ameelea kufurahishwa na technolojia hiyo ambayo amesema inaweza kusaidia ukusanyaji wa mapato hususani maeneo ya vijijini ambako miundombinu ya maji bado ni tatizo. 
Mhe Balozi Dr Possi ameshauri kampuni ya iSatech Water watumie  fursa iliyopo na  kuingia katika soko la Tanzania .
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa iSatech water Berlin,Mr  Emmanuel Mey, Balozi wa Tanzania Ujerumani  Mh Balozi DKt. Abdallah  Possi, Mwakilishi wa Kampuni ya iSATECH Water Tanzania Bw.  Peter Kazaura na Bi. Hanna Jass kutoka iSatech water Berlin.

CLEMENT SANGA EXCLUSIVE:MSANII WA FILAMU IRINGA ATANGAZA KUUZA FIGO ILI KUTENGENEZA FILAMU KUELIMISHA VIJANA

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 23.01.2018

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images