Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA


RIDHIWAN KIKWETE ASIKITISHWA INSTAGRAM YAKE KUINGILIWA, ATOA UFAFANUZI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

MBUNGE wa Chalinze mkoani Pwani, Ridhiwan Kikwete(CCM)amesem amesikitishwa na kitendo cha watu kuingilia instagram yake na kisha kuandika maneno hajawahi na wala hawezi kuyasema.

Ridhawani ameiamba Michuzi Blogu kwa njia ya simu kuwa watu walioingilia instagram yake kabla ya kuandika maneno mabaya walizuia yeye asiingie. 

"Nimesikitishwa sana na hili jambo lililotokea leo.Watu wameingilia ukurasa wangu wa Instagram na kunizuia nisiingie kwenye account yangu. "Lakini jambo baya zaidi wanalolifanya ni kuandika vitu au maneno ambayo hata sijawahi na sitamani kuyasema.

"Nimeshangazwa sana na hili na sijui nia ya kufanya hivyo ni nini? Malengo yenu hamtafanikiwa,"amesema Ridhiwan. Amefafanua yeye yupo katika vikao vya halmashauri kupanga bajeti za Halmashauri yao ya Chalinze. 

Amesema hayo maneno na matukio hata hayajawahi tokea na anaomba utulivu wakati wataalamu wanafanya kazi ya kurudisha ukurasa huo mikononi mwake.

RC MNYETI AWASHUKIA MAHAKIMU MANYARA

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti amewataka mahakimu wa mkoa huo kutekeleza wajibu wao ipasavyo wakati wanaposikiliza kesi na kutoa hukumu kwa haki ili kuepuka malalamiko yanayotolewa na wananchi. 

Akizungumza kwenye ziara yake ya kwanza ya siku saba katika Wilaya ya Simanjiro, Mnyeti alisema kupitia nafasi yake ya Mwenyekiti wa kamati ya maadili, hatakubali kuona wananchi wanalalamikia kukosa haki. 

Mnyeti alisema baadhi ya mahakimu wanajigeuza kuwa miungu watu na kushindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo hivyo kusababisha malalamiko kwa wananchi. "Hatuwezi kukubali kuona mambo kama hayo, yakifanyika kama kuna mtu anaona kuna mahakimu siyo waadilifu wanakula rushwa na kushindwa kutoa haki nijulisheni," alisema Mnyeti. 

Awali, mkazi wa mtaa wa Njiro, Theopista Paulo alisema amekuwa akinyanyasika wakati akidai haki yake. Theopista alisema mmoja kati ya mahakimu wa eneo hilo alikuwa anamwambia hata kama akimkataa na kesi yake kuhamishwa kwenye mahakama nyingine hawezi kushinda chochote. 

Hata hivyo, Mwanasheria wa ofisi ya mkuu wa mkoa huo, Peter Mangala alisema mwananchi yeyote ana haki ya kumkataa hakimu endapo atakuwa na sababu za msingi. Mangala alisema endapo mwananchi akiwa na hoja za msingi anazozipinga anaweza kumkataa jaji au Hakimu atakapobaini kuwa hawezi kutendewa haki. 
 Wananchi wa Mji mdogo wa Orkesumet Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakitoa kero kwa Mkuu wa Mkoa huo Alexander Pastory Mnyeti. 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Pastory Mnyeti akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Orkesumet Wilayani Simanjiro. 

BILIONI TATU ZILIZOTOLEWA NA SERIKALI MKOANI GEITA KUBORESHA MIUNDOMBINU VITUO SABA VYA AFYA

$
0
0

NaJoel Maduka-Geita.

Jumla ya Sh Bilioni 3 zilizotolewa na serikali Mkoani Geita zinatarajiwa kuboresha miundombinu katika Vituo saba vya afya .

Mganga mkuu wa Mkoa wa Geita Dkt Japhet Simeo alisema lengo kuu la hizo fedha ni kuboresha miundo mbinu kwa maana ya chumba cha upasuaji kujenga wodi ya watoto,wakina mama ,maabara na chumba cha kuhifadhia maiti na kwamba wanatarajia kuona fedha hizo zinafanyika kuboresha mandhari ya kituo kwa maana ya bustani na majengo ambayo yamechakaa.

Simeo alizitaja wilaya ambazo zimepatiwa fedha hizo ni wilaya 5 ikiwemo halmashauri ya wilaya ya Geita ambayo imepewa kiasi cha sh ,Milioni 500 kwenye kituo cha afya cha Nzera na kwamba hadi sasa wameshajenga majengo manne ambayo yamekaribia kukamilika , Mbogwe milioni 800 ambazo zimegawa kwenye vituo viwili vya afya, Bukombe milioni 400 kwaajili ya kituo cha afya cha uyovu , Chato wamepatiwa fedha kwaajili ya vituo viwili ambvyo ni Bwanga Milioni 500 na Karumwa milioni 400 na Wilaya ya Nyang’hale milioni 400 kwaajili ya kituo cha afya cha Nyang’hale.

Juma Mabura ni moja kati ya wananchi wa Wilaya ya Mbongwe ambapo ameelezea kuwa kumekuwape na changamoto kubwa ya upungufu wa majengo na kwamba kukamilika kwa baadhi ya majengo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma ya afya.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi amesema kuwa majengo yaliyo kwenye hatua ya renta na maboma yakikamilika watakuwa kwenye asilimia 55 kwa maana ya zahanati 262 na kwamba nyingine wameanza ujenzi .

Aidha amesisitiza kuwa lengo la serikali ni kuondoa kero ya kimiundombinu kwenye sekta ya afya ili kuwawezesha watanzania kupata huduma bora za afya.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki kuchimba msingi kwenye kituo cha afya cha Masumbwe Wilayani Mbongwe. 
Wananchi wakishiriki kwenye ujenzi wa msingi kwenye kituo cha afya cha Masumbwe Wilayani Mbongwe. 
Mkuu wa Wilaya ya Mbongwe ,Mathar Mkupasi akizungumza na wananchi ambao walikuwa wamejitokeza kuunga mkono jitihada za serikali za ujenzi wa jengo la kupasulia kwenye kituo cha afya cha Masumbwe. 
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM,Wilayani Mbongwe Johari Juma akisisitiza wanachama wa chama hicho kuwa mstari wa mbele kushiriki katika shughuli za maendeleo. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi akisisitiza namna serikali ilivyojipanga kupunguza changamoto ya huduma za afya Mkoani humo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mbongwe. 

NIPO TAYARI KUNYIMWA KURA KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA 2020-MBUNGE MGIMWA

$
0
0
Na Fredy Mgunda-Iringa

Wananchi wa jimbo la Mufindi kaskazini wametakiwa kuwapeleka watoto wao shule kwa lazima kwa kuwa elimu inatolewa bure na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Mafuli kwa lengo la kuhakikisha kila mwanafunzi wote waweze kupata elimu na kuondoa ujinga na kuleta maendeleo kwa taifa.

Hayo yamesemwa na mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miundombinu ya shule zilizopo katika jimbo hilo ili kuweza kuzitatua changamoto zilizopo katika maendeo hayo.

Akiwa bado yupo kwenye ziara hiyo mbunge huyo aligundua kuwa wazazi wengi wamekuwa kikwanzo cha kuwapeleka shule watoto,hivyo akawataka viongozi wote wa serikali za vijiji kuwa chukulia hatua wazazi ambao hawatawapekeka shule watoto wao.

Mgimwa alisema kuwa yupo tayari kunyimwa kura na wananchi ambao atawachukulia hatua za kisheria kwa kutowapeleka shule watoto wao kwa ajili ya faida ya maisha yao.

“Nasema kweli nitakubali kuachia ngazi ya kuwa mbunge kwa kunyimwa kura za wananchi wasiopenda maendeleo ya watoto wao,hadi sasa shule zimefungua lakini wazazi hawawapeleki shule watoto nitahakikisha wanachukuliwa hatua za kisheria” alisema Mgimwa
Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa aikiongea na baadhi ya walimu wa shule za sekondari na shule za msingi jinsi gani ya kutatua kero zilipo shuleni ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi
Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa akiwakabidhi zawadi ya mbuzi kwa walimu wa shule za msingi waliofanya vizuri katika moja ya kata iliyopo jimboni kwake.


OLE NASHA AAGIZA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA KUFUNGWA VIFAA VYA KISASA NDANI YA WIKI NNE

$
0
0
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha ameuagiza uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) uwe umefunga vifaa vya kisasa vyenye thamani ya Sh 14 bilioni ndani ya wiki nne badala ya siku 67 ili vianze kutumika mara moja.

Ametoa agizo hilo kwenye mahafali ya tisa ya wahitimu 465 wa fani mbalimbali za ufundi jijini hapa kuwa ukarabati na upanuzi wa karakana ufanyike ndani ya muda alioutoa ili vifaa hivyo vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.

"Nilipotembelea Chuo hiki Desemba 2,mwaka jana nilitoa maagizo mharakishe ujenzi na ukarabati wa miundombinu itakayotumika kufunga vifaa hivyo kutoka Austria,nafarijika kusikia kuwa utaanza mara moja kwani Wizara ilishatoa kibali cha kutumia watalaam wenu wa ndani na fedha mnayo,"alisema Ole Nasha

Alisema sekta ya elimu ya ufundi kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2015 inatarajiwa kuleta maendeleo ya haraka ya rasilimali watu walioelimika na kupenda kujielimisha zaidi ili kulifanya taifa lipate maendeleo.Ole Nasha aliongeza kuwa elimu ya ufundi ina mchango mkubwa katika kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda na nchi zilizoendelea kama Japan na China zimefikia hapo zilipo kwa kutilia mkazo elimu ya ufundi.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya tisa ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) 
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha(wa pili kuli) akiwapongeza wanafunzi wahitimu waliofanya vizuri zaidi katika kozi walizosomea 
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha(katikati),Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Masudi Senzia(wa pili kulia),Makamu Mkuu wa Chuo,Utawala,Fedha na Mipango,Dk Erick Mgaya pamoja na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wasichana. 


MGALU ARIDHISHWA NA KASI YA MKANDARASI SENGEREMA

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi-Bagamoyo

NAIBU Waziri Wa Nishati Subira Mgalu, ameridhishwa na kasi na kazi anayoendelea nayo ,mkandarasi wa mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya III, Sengerema huko kijiji cha Kongo na kata ya Yombo wilaya ya Bagamoyo ,Mkoani Pwani.

Aidha amelitaka shirika la umeme (Tanesco) wilaya ya Bagamoyo, kukimbizana na wakati kwa kuwapa wananchi fomu za kujaza ili kupatiwa umeme wakati zoezi la kuweka nguzo likiendelea katika baadhi ya vijiji.

Aliyasema hayo wakati alipokwenda kutembelea kijiji cha Kongo ,kata ya Yombo na Visezi kata ya Vigwaza na kujiridhisha na kazi ya mradi huo inavyoendelea .Mgalu alisema mkandarasi huyo ameahidi kumaliza kazi hiyo mwanzoni mwa mwezi ujao na kwa uhakika anakwenda vizuri.

Alieleza kwasasa amekuta wanaendelea na kazi ya kusimamisha nguzo na maeneo mengine yanatarajiwa kutandaza nyaya ."Mkandarasi Sengerema yupo Mkoa wa Iringa na Pwani ,ameanza kazi vizuri na ndivyo tunavyohitaji ,tunaomba aendelee na kasi hii ili wananchi wapate huduma hii ya umeme haraka" alisisitiza Mgalu.

Naibu waziri huyo,alitoa tahadhali kwa wakandarasi wengine wa mradi wa REA kwenda na kasi inayotakiwa na serikali ya awamu ya tano,na atakaefanya kazi chini ya kiwango hatakuwa na masihala nae.
 Naibu Waziri Wa Nishati ,Subira Mgalu mwenye kitambaa chekundu kichwani ,akiwa ameambatana na mbunge wa jimbo la Bagamoyo.dk.Shukuru Kawambwa wa pili kushoto na wengine ni viongozi mbalimbali wa kijiji cha Kongo na kata ya Yombo wakati alipokwenda kutembelea maeneo yanayotekelezwa mradi wa umeme vijijini (REA )awamu ya III ,ambapo amejiridhisha na kasi anayoendelea nayo mkandarasi Sengerema.(picha na Mwamvua Mwinyi)
 Nguzo 60 za umeme zilizotelekezwa ndani ya miaka mitatu huko kijiji cha Visezi Kata ya Vigwaza pasipo kufanyiwa kazi ,jambo linaloelezwa ni uzembe uliofanywa na mkandarasi MBH aliyepewa kazi awamu ya pili ya mradi wa umeme vijijini (REA )ambapo ameitia hasara serikali na kuchelewesha huduma ya umeme kwa jamii.
Naibu Waziri Wa Nishati ,Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Visezi kata ya Vigwaza kuhusiana na masuala ya huduma ya umeme.
 Mbunge wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete akizungumza jambo kuhusiana na changamoto ya nishati ya umeme huko kijiji cha Visezi kata ya Vigwaza. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

JAJI MKUU AWATAKA VIONGOZI WA SERIKALI NA VYAMA VYA SIASA KUTOINGILIA MUHIMILI WA MAHAKAMA

$
0
0

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma amewataka viongozi  wa serikali na vyama vya siasa kuacha mara moja kuingilia  muhimili wa Mahakama kwani ndio yenye mamlaka ya kutoa haki.
Jaji Profesa Juma ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Sheria.
Amesema kuwa  viongozi wengi hawaheshimu amri zinazotolewa na mahakama hivyo kusababisha muingiliano wa mihimili na kuwashauri kila mtu abaki katika maeneo yao waliyopewa mamlaka ya kikatiba.
JAJI Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma 

KIVUKO CHA SERIKALI CHA MV MISUNGWI KIKIPIGA MZIGO

$
0
0
Kivuko cha serikali cha MV Misungwi, Busisi jijini Mwanza, kikitokea mjini kupeleka wananchi maeneo ya Sengerema, mkoa wa Geita. Kivuko cha MV Misungwi kina uwezo wa kubeba mizigo yenye uzito wa tani 250 na ndicho kivuko kikubwa kuliko vyote katika Ziwa Victoria, kinabeba abiria 1,000 na magari madogo 36 na maroli makubwa 14.
Muonekano wa kivuko cha zamani cha MV Sabasaba kilichokuwa kikitoa huduma ya kuvusha magari na abiria katika Ziwa Victoria kikiwa kimepaki.
Kivuko cha MV Sengerema kikiwa katika gati la Busisi wilayani Sengerema kikisubili abiria kuele Kigongo Mwanza Kivuko hicho ni moja ya vivuko vinavyovusha magari na abiria kati ya Kigongo na Busisi mkoani Mwanza. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii - Geita.

Rais Dkt. Shein Azungumza na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan JIJINI ABU DHABI

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE)wakiwa katika ukumbi wa makadhi ya Kiongozi huyo Nchini Abu Dhabi.
VIONGOZI wa Ngazi za juu wa Serikali ya Abu Dhabi wakihudhuria hafla hiyo katika ukumbi wa makaazi wa Mfalme wakati wa mkutano huo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE)wakiwa katika ukumbi wa makadhi ya Kiongozi huyo Nchini Abu Dhabi. kulia Balozi wa Tanzania Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) Mbarouk Nossor Mbarouk.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na mwenyeji wake , Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE), baada ya mazungumzo yao katika ukumbi wa makadhi ya Kiongozi huyo Nchini Abu Dhabi. 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE) wakitoka katika Jumba la Kiongozi huyo baada ya kumaliza mazungumzo yao
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE) baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika makaazi ya Kiongozi hiyo Nchini Abu Dhabi. Picha na Ikulu

MAMBO YA RUNGWE AVOCADO COMPANY

BREAKING NEWZZZZ: "NABII" TITO ATIWA MBARONI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Marlin Komba amesema hamtambui mtu anayejiita nabii Tito na kwamba hajasajili kanisa lake katika ofisi ya msajili wa taasisi za dini, na kwamba Serikali imeona vitendo anavyovifanya ‘nabii’ huyo kupitia mitandao ya kijamii na imeanza kuchukua hatua.
“Ninachoweza kusema ni kwamba hakuna mtu anayezuiwa kuongea hapa nchini, mwache aongee anavyoweza ila Serikali imeshaona anachokifanya na yanayoendelea mitandaoni hatua zinachukuliwa dhidi yake,” amesema Komba.
Kauli hii imekuja kufuatia kusambaa kwa video mbalimbali zikimuonyesha ‘nabii’ huyo akitoa mafundisho yake huku akinywa vilevi pamoja na kufanya matendo ambayo ni kinyume cha maadili ya dini, jambo ambalo limeonekana kuwakera wadau wengi wa dini.

Kwa upande wao viongozi mbalimbali wa dini wameonyeshwa kukerwa na kulaani vitendo anavyovifanya mtu huyo anayejiita ‘nabii’ na kusisitiza kuwa hakuna dini inayoruhusu hayo.
Askofu Msaidizi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Chediel Lwiza amesema kuwa, kutokana na vitendo anavyofanya, mtu huyo hapaswi kujiita mtumishi wa Mungu.
“Huyo hawezi kuwa mtumishi wa Mungu na wala hafanyi huduma ya kanisa. Ni vyema watu kama hawa wafuatiliwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. Natumaini Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo ndani yake ina ofisi ya msajili wa taasisi za dini itafanya kazi yake,” amesema Mchungaji Lwiza.
Naye Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Rajab Katimba amesisitiza Serikali na viongozi wa dini kuingilia kati suala hilo na kueleza kuwa, hakuna kitabu chochote cha dini kinachohamasisha ulevi na ukosefu wa maadili.
“Hilo suala linakwenda tofauti na dini na mila na desturi zetu pia. Dini zinatakiwa kuleta amani na kuhamasisha watu waheshimiane si kuzungumza mambo yanayokiuka maadili yetu. Naona ipo haja ya viongozi wa dini na Serikali kuingilia suala hili na waende mbali zaidi kwa kuongea naye huenda hafahamu anachokifanya,” amesema Rajab Katimba.
Source- JF
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akimsikiliza mhubiri wa kujitegemea ajiitaye Nabii Tito ambaye ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kutoa maneno yaliyo kinyume na maadili. Nabii Tito anashikiliwa nan a jeshi hilo kituo cha kati mjini Dodoma. Taarifa kamili itafuata baadaye.

Nabii Tito akiwa chini ya ulinzi Central Police Dodoma leo. Ifuatayo hapo chini  video iliyopigwa mwaka 2013 wakati "akihubiri" mitaani jijini Dar es salaam.

DC MHANDO AELEZEA HATUA KWA HATUA MAENDELEO YA WILAYA YA TANGANYIKA

$
0
0
*Amshukuru Rais ,Dk. Magufuli kwa uamuzi wa kuanzisha wilaya hiyo

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando amesema kwa kushirikiana na wananchi wameendelea kutatua changamoto zilizopo wilayani humo huku akielezea hatua kwa hatua miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayoendelea kufanywa.

ASHUKURU UAMUZI WA RAIS

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na Michuz Blogu, leo kwa njia ya simu , Mhando amesema wanamshukuru Rais ,Dk.John Magufuli kwa uamuzi wake wa kuanzisha Wilaya ya Tanganyika kwani imesaidia kusogeza mamlaka karibu, hali iliyochangia kutatuliwa kwa changamoto na kuboreshwa kwa miundombinu ya kimaendeleo.

"Tunamshukuru Rais uamuzi wake wa kuanzisha Wilaya ya Tanganyika iliyoanzishwa rasmi Julai Mosi mwaka 2016.Uwepo wa wilaya hii kumesaidia kwa sehemu kubwa kusogeza huduma kwa wananchi."Uwepo wa wilaya hii kumesaidia kuimarika kwa mindombonu hasa kwa kuzingatia ni wilaya ambayo ipo mpakani.Kwa sehemu kubwa tunampongeza Rais kwa uamuzi wake wa kuona haja ya kuwa na wilaya ya Tanganyika kwani inasukuma kwa kasi maendeleo ya wananchi,"amesema Mhando.

UMEME WILAYANI TANGANYIKA 

Kuhusu nishati ya umeme katika Wilaya hiyo, Mhando anasema kuwa kuna mikakati mingi inayoendelea ya kufanikisha nishati ya umeme inakuwepo katika maeneo yote na kufafanua tayari umeme umefika makao makuu ya wilaya."Wilaya ya Tanganyika ilianza kupata umeme mwaka 2017 baada ya kuanza kusambazwa kwa nguzo za umeme na sasa makao makuu ya wilaya tuna umeme, pia taasisi kadhaa pamoja na kaya 62 tayari nazo zimeanza kupata umeme.

"Malengo yetu ni kuendelea kuweka mikakati ambao utatusaidia kusogeza nishati ya umeme kwa wananchi wa Wilaya ya Tanganyika na hakika tunakwenda vizuri kwani Serikali Kuu nayo imekuwa ikituangalia kwa jicho la aina yeke."Imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya kuendelea na miradi ya kimaendeleo na hasa inayohusu kutatua changamoto zilizopo ikiwamo hii ya umeme,"amesema Mhando.

MIUNDOMBINU YA BARABARA

Akizungumzia miundombinu ya barabara, Mhando anasema Wilaya ya Tanganyika imeendelea kufunguka, kwani wanaendelea kuboresha barabara zilizopo ndani ya wilaya hiyo na zile ambazo zinatoka nje ya wilaya yao."Tunaendelea na ujenzi wa miundombinu ya barabara , kwa kueleza tu tayari barabara za Mpanda hadi Kalema na ile ya Mpanda Uvinza zimekamilika.Pia kuna mradi wa ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 35 kutoka Vikonge hadi Mpanda.

"Tumedhamiria kuhakikisha tunakuwa na barabara za uhakika zitakazopitika wakati wa wote yaani masika na kiangazi na tumeanza kufanikiwa kwenye hili,"amesema Mhando.
MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando akishirikiana na Wananchi katika kazi ya ujenzi wa wilaya mpya ya Tanganyika ,mkoani Katavi ."Tumeanzisha ujenzi wa Sekondari ktk Kata 5 kati ya 8 ambazo hazina kabisa Sekondari za Kata,Lengo ni kuhakikisha ifikapo Disemba 2018 kata zote 8 zinakuwa na Sekondari"alisema DC Mhando
MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando akishirikiana na Wananchi katika kazi ya ujenzi wa wilaya mpya ya Tanganyika ,mkoani Katavi ."Tumeanzisha ujenzi wa Sekondari ktk Kata 5 kati ya 8 ambazo hazina kabisa Sekondari za Kata,Lengo ni kuhakikisha ifikapo Disemba 2018 kata zote 8 zinakuwa na Sekondari"alisema DC Mhando.

COMRADE NGEMELA LUBINGA AKAGUA MIRADI YA TASAF MARA

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, Tarime

Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Comrade Ngemela Lubinga jana (22/01/2018) ameanza ziara ya ukaguzi wa miradi ya TASAF mkoani Mara.

Ziara hiyo ni sehemu ya kufuatilia (monitoring) utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika mkoa wa Mara.Comrade Lubinga ameanza kwa kutembelea Wilaya ya Tarime ambapo alikutana na wanufaika wa Mpango wa TASAF wa kunusuru Kaya masikini katika Vijiji vya Gamasala Kata ya Nyandoto na Remagwe katika Kata ya Regicheri.

"Watendaji wa TASAF na wote wenye dhamana Serikalini, timizeni wajibu wenu na jitumeni zaidi katika kutatua changamoto za Wananchi wanyonge hawa na masikini ili nao wapate nafuu ya maisha," alisisitiza.

Vilevile, Comrade Lubinga amekemea tabia za ubadhilifu wa mali ya umma na kuonya kuwa watendaji wa aina hiyo hawana nafasi katika Serikali ya awamu ya tano chini ya Jemedari, Rais Dk John Magufuli."Serikali ya awamu tano iliyoundwa na CCM imedhamiria kuleta mabadiliko makubwa ya utumishi na kujenga nidhamu ya kazi katika kuwahudumia wananchi wa Tanzania na hasusan wanyonge," alisema.

Ziara hiyo ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa CCM katika kuisimamia Serikali yake kutekeleza Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2015. "CCM katika utaratibu wake wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa Ilani yetu, tumebaini changamoto katika mpango wa kupunguza umaskini na tumekuja kusikiliza kero za wananchi wetu ili kuzipatia majawabu," alisema Lubinga.

CCM mpya chini ya Mwenyekiti wake Dk John Pombe Magufuli, imeazimia kufuatilia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali ili kuharakisha maendeleo ya wananchi wake wakiokipa dhamana ya kuwaongoza, alisema. Ziara hiyo inaendelea leo.

NEWS ALERT: Mwanamuziki mashuhuri wa Afrika Kusini Hugh Masekela afariki dunia

$
0
0
Mwanamuziki mashuhuri wa kimataifa wa Afrika Kusini Hugh Masekela amefariki dunia leo jijini Johannesburg baada ya kushindwa vita dhidi ya tezi dume aliyopigana kishujaa kwa miaka kadhaa. 

Bendi yake imetoa taarifa ikisema kwamba marehemu Hugh Masekela amekuwa akipambana na ugnjwa huo tangia mwaka 2008, na kwamba mnamo Machi 2016 alifanyiwa upasuaji wa jicho baada ya saratani kusambaa ikabidi akafanyiwa upasuaji mwingine mwezi Septemba mwaka huo huo. 
 Hugh Masekela, aliyezaliwa mji wa KwaGuga huko Witbank, alianza kuimba na kucheza piano tangia akiwa mtoto. Na baada ya kuona filamu ya ‘Young Man with a Horn’ akiwa na umri wa miaka 14, Masekela akaanza kupuliza tarumbeta, ambapo Archbishop Trevor Huddleston ndiye alimpa tarumbeta yake ya kwanza. 
 Haukuchukua muda Masekela aliweza kuitawala trumpet hiyo na mwaka 1956 akajiunga na kundi lz jazz la Herbert’s African Jazz revue. Enzi za uhai wake alisema alitumia muziki kama silaha ya kusambaza mageuzi ya kisiasa enzi hizo za ubaguzi wa rangi, na alifanikiwa sana.

VIONGOZI WA SERIKALI, WANASIASA ACHENI KUIINGILIA MAHAKAMA-PROF JUMA

$
0
0
Na Karama Kenyunko-Globu ya jamii.

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma amewataka viongozi wa Serikali na wanasiasa wenye mamlaka ya kikatiba na kisheria kutoingilia muhimili wa Mahakama badala yake waongoze katika misingi yao.

Amesema kumekuwa na uvunjwaji na kudharauliwa kwa amri zinazotolewa na Mahakama  ambayo imepewa mamlaka ya kikatiba ya kutoa haki.Jaji Profesa Juma amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ya wiki ya sheria itakayoanza Januari 27 mwaka huu. 

Amesema,  suala la utoaji haki ni la Mahakama pekee na kwamba viongozi hao wajiepushe kuingilia maeneo yaliyondani ya haki na hadhi ya mamlaka ya kikatiba ya Mahakama.

Amefafanua ibara ya 107A (1) ya Katiba inayozungumzia mamlaka ya utoaji haki inakumbusha kwamba ‘Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Mahakama ya Tanzania na Mahakama ya Zanzibar,hivyo hakuna chombo cha Serikali wala Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki.

 Amesema kuwa vyombo vya habari vimekuwa vikiwapa taarifa kuhusiana na uvunjwaji wa haki ya kikatiba na kwamba mahakimu ndio wenye hadhi ya kulinda haki hiyo.Amesisitiza kuwa amri zinazotolewa na mahakimu zinavunjwa na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa, hivyo ni wakati wa kuwa kama Bunge ambalo watu wake wanapokiuka taratibu wanachukuliwa hatua.

Amesema, mtu yeyote akajivika nguvu za Mahakama atachukuliwa hatua kwani watakuwa wakali kwa watu wataoingia katika anga za mahakama, na kuomba Katiba ifuatwe na sheria ipewe nguvu na wale wote waliopewa mamlaka wabaki katika maeneo yao, 

Akizungumzia wiki ya sheria, Jaji Profesa Juma ameeleza kuwa maadhimisho ya wiki ya Sheria yataanza Januari 27 hadi 31, mwaka huu na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete atayazindua  katika viwanja vya Mnazi Mmoja mpaka  yatakapohitimishwa Februari Mosi ambayo itakuwa ni siku ya Sheria.

Amesema, katika wiki hiyo, kutakuwa na utoaji wa elimu ya sheria na msaada wa kisheria kwa wananchi watakaoshiriki  maadhimisho hayo  kwa kuzifahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mahakama na wadau wa sekta ya sheria.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya wiki ya sheria leo jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia tarehe 27 hadi 31,Januari 2018.  Kushoto ni Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Wambali na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Hussein Kattanga.

WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA COMORO

$
0
0

BALOZI wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Comoro,  Sylvester Mabumba ameupokea ujumbe wa Clouds Media Group uliowasili visiwani humo Januari 20 mwaka 2018.

Upo kwenye ziara maalumu ya siku tatu ikiwa na lengo la kushirikiana na ubalozi kuzitangaza fursa mbalimbali zinazopatikana visiwani humo kwa Watanzania. Ujumbe huo wa Clouds Media Group ukiongozwa na Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji, Ruge Mutahaba uliwasili Comoro kutokana na mualiko wa Ubalozi wa Tanzania hapa Comoro

Ambapo lengo lake lilikuwa ni kuja kufanya tathamini ya kuzindua Jukwa la Fursa (FURSA EXPO) Visiwani Comoro kama sehemu ya kuendeleza kampeni za kuwapatia vijana wa kitanzania taarifa muhimu kuhusu fursa za uwekezaji na biashara.

Ubalozi wa Tanzania Visiwani Comoro kwa kushirikiana na Ujumbe wa Clouds Media Group umelenga ifikapo Aprili mwaka 2018 kupanua mianya ya uwekezaji nchini Comoro na kuhakikisha masoko ya uhakika yanapatikana kwa ajili ya bidhaa za Tanzania hasa katika kipindi hiki ambapo Uchumi wa Tanzania unaelekea kuwa ni uchumi wa Viwanda. 
Balozi wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe, Sylvester Mabumba (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji wa Comoro, Bw. Said Mohamed Omar (wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group pamoja na wajumbe waliofuatana nao katika ziara maalum ya kufungua na kuzitangaza fursa zilizopo Tanzania na Comoro.
Balozi wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya comoro pamoja na Wajumbe kutoka clouds Media Group wakiwa katika mazungumzo ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Comoro, Bw. Mouzamildine Youssouf.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI HAITAMUONEA MTU HURUMA, SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE-ULEGA

$
0
0
NAIBU Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega ameteketeza zana haramu katika Ziwa Victoria.Baadhi ya zana hizo zipo nyavu za Makila zilizounganishwa 21710 zenye macho madogo,makokolo ya Sangara 695,Timba 690,makokoro ya dagaa 90 pamoja na Pikipiki tano zilizokuwa zikitumia katika kusafirisha Samaki haramu.

Akizungumza leo na wananchi wa Mwembeni wilayani Chato mkoani Geita, Ulega amewata kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli kuwafichuwa waharifu hao ili wachukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kupigwa faini au kwenda jela.''Serikali haitamuonea mtu huruma awe kiongozi au raia wa kawaida sheria itachukuwa mkondo wake.

"Nia yetu ni kuona samaki wanaongezaka ziwa Victoria na watu wavue kwa kufuata sheria ili Taifa lipate mapato pamoja na ajira kwa wananchi mbalimbali" amesema Ulega.Aidha amewaonya baadhi ya wafanyakazi wa hifadhi ya Lubondo kuacha tabia ya kupewa rushwa na wavivu haramu kwani wamekuwa wakiwaruhusu kuingia kwenye hifadhi na kuwafichia zana zao wanapomaliza kuvua na kuwapatia fedha laki mbili hadi tatu.

Amefafanua kuwa kwa sasa kuna oparesheni ya kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu ambayo inaendelea maeneo ya Ziwa Victoria ikiwa na lengo la kuondoa uvuvi haramu na mitandao ya wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia ,biashara ya samaki wachanga na utoroshaji wa samaki na mazao ya yake,kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.

Aidha kiongozi wa oparesheni Gabriel Mageni ameongeza kuwa katika operesheni hiyo ambayo ina siku 13 baadhi ya mambo ambayo wameyabaini ni pamoja na baadhi ya viongozi wa vijiji na maofisa pamoja na madiwani wanaosimamia maeneo ya uvuvi kuwapa hifadhi raia wa kigeni wanaofanya shughuli za uvuvi wakiwa hawana kibali na kusababisha hasara Serikali ikiwemo kukosa mapato

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Chato, Chato,Shaban Ntalambe ,amewatahadharisha watendaji ambao wanashirikiana na wavuvi haramu kuwa endapo kuna mtu akibainika na kitendo hicho Serikali itahakikisha inamchukulia hatua kupitia oparesheni hiyo hatabakia hata mtu mmoja anayejihusisha na shughuli hizo awe kiongozi mkubwa ama mtu wa kawaida.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega  akiteketeza nyavu haramu  zilizounganishwa zipatazo 21710 zenye macho madogo,makokolo ya Sangara 695,Timba 690,makokoro ya dagaa 90 wilayani Chato.
 Baadhi ya wananchi wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa zana haramu za uvuvi wilayani Chato mkoani Geita.
 Naibu waziri wa Mifungo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega akisisitiza jambo kwa wale ambao ni watumishi na viongozi kuacha kuendelea na tabia ya kushirikiana na wavuvi haramu.
 Mkuu  wa Wilaya Chato,Shaban Ntalambe akishiriki zowezi  la kutekeeza nyavu haramu
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega akiwa ameambatana na  Mkuu  wa Wilaya chato,Shaban Ntalambe wakielekea katika kisiwa cha hifadhi ya Lubondo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega akizungumza na Wafanyakazi wa Hifadhi ya Lubondo juu ya kuacha kushirikiana na wavuvu haramu kwani wamekuwa wakiwaruhusu kuingia kwenye hifadhi na kuwafichia zana zao wanapomaliza kuvua.

MASHINDANO YA BAISKELI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA NCHINI TANZANIA

$
0
0
Mwenyekiti wa Michezo ya Jumuiya za majeshi ya Afrika ya Mashariki, Brigedia Jenerali Martin  Kemwanga amesema kuwa mashindano ya baiskeli yanajenga umoja kwa nchi za afrika Mashariki. 

Kemwanga ameyasema hayo alipokuwa anawakabidhi bendera ya nchi za Afrika Mashariki pamoja na kutangaza mshindano ya baiskeli yatayofanyika April 13 Mjini Zanzibar na Kumalizika wilayani Masasi mkoani Mtwara, amesema kuwa mashindano hayo kwa kauli mbiu ya Amani na Usafi wa Mazingira yanajenga umoja kati ya nchi wanachama. 

Amesema kuwa mashindano hayo yamekuja wakati wa mwafaka wa kutangaza fursa ya viwanda kwa nchi zitazoshiriki mashindano hayo pamoja na kutangaza umoja na  pamoja na  wananchi kuingia kwenye nchi hizo bila vikwazo vya aina yoyote. 

Rais wa Chama cha Mchezo wa Baiskeli Tanzania, Godfrey Mhagama amesema kuwa katika mashindano hayo nchi zitazoshiriki za Afrika Mashariki ni Tanzania ambaye ndie mwenyeji ,Kenya , Uganda , Rwanda , Burundi pamoja na Sudan Kusini na nchi wa Waalikwa ni Zambia na Ufaransa na nyingine zitajitokeza. 

Amesema kuwa wadau wa wajitokeze katika kufadhili mashindano hayo kwani muda bado wa kutosha ili waweze kufanikisha mashindano
Mwenyekiti wa Michezo ya Jumuiya za majeshi ya Afrika ya Mashariki, Brigedia Jenerali Martin  Kemwanga  akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya kuwakabidhi viongozi bendera ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa ajili ya mashinano ya mchezo wa baiskeri yatakayofanyika nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Afrika Mashariki Fest, Kisembo Ronex Tendo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mashindano ya baiskeri yatakayofanyika nchini Tanzania ili kuhamasisha Amani kwenye nchi za Afrika Mashariki.
Rais wa Chama cha Mchezo wa Baiskeli Tanzania, Godfrey Jax Mhagama akizungumza na kuhusu ujio wa nchi mbalimbali za Afrika mashariki kwenye mashindano ya Baiskeri yatakayofanyika nchini Tanzania
Mwenyekiti wa Michezo ya Jumuiya za majeshi ya Afrika ya Mashariki, Brigedia Jenerali Martin  Kemwanga akimkabidhi bendera ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa Rais wa Afrika Mashariki Fest "Tanzania Chapter", Peter Nzunda wakati wa mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UJENZI WA RELI YA STANDARD GAUGE WA AWAMU YA KWANZA KUTOKA DAR ES SALAAM HADI MOROGORO WAENDELEA KWA KASI

$
0
0
Muonekano wa leo wa tuta la kutandazia reli ya kisasa (Standard Gauge) katika eneo la Soga mkoa wa Pwani takriban kilomita 37 kutoka Pugu mkoa wa Dar es salaam ulivyo sasa, ikiwa ni hatua iliyofikiwa katika muendelezo wa ujenzi wa reli hiyo ulioanza  mwezi Desemba mwaka jana katika mradi unaotarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu na utajengwa kwa awamu nne. 
Kampuni Hodhi ya rasilimali za reli nchini (RAHCO) ndiyo inatekeleza mradi huo kutoka Dar es salaam kwenda Isaka na Mwanza imegawanyika katika awamu ndogo nne ikiwemo Dar es salaam hadi Morogoro, Morogoro hadi Makutupora, Makutupora hadi Tabora na Tabora hadi Mwanza. 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Injinia Masanja Kadogosa jumla ya makandarasi  wanne wanaendelea na kazi usiku na mchana ili kukamilisha  ujenzi wa reli hiyo yenye upana wa mita 1.345 na ambao utaruhusu treni kutembea kwa spidi ya kilomita 160 kwa saa. 
Mradi huu mkubwa unatarajiwa  kuchochea maendeleo katika sekta ya kilimo, biashara, madini na viwanda hususan maeneo ambapo reli hiyo itapita ikiwemo  nchi  jirani ya Rwanda ambayo imekubali kujenga aina hiyo ya reli toka Isaka hadi Kigali. Mtandao mzima wa reli nchini unaotegemewa kujengwa kwa kiwango cha standard Gauge una jumla ya kilometa 2,561 ukitarajiwa kugharimu Dola za Marekani Bilioni 7.6i Bilioni 7.683.  
 Eneo la Soga mkoa wa Pwani takriban kilomita 37 kutoka Pugu mkoa wa Dar es salaam
 Tuta linavyoonekana katika eneo la Soga mkoa wa Pwani takriban kilomita 37 kutoka Pugu mkoa wa Dar es salaam
 Sehemu ya tuta la kupitishia reli eneo la Soga mkoa wa Pwani takriban kilomita 37 kutoka Pugu mkoa wa Dar es salaam
 Sehemu ya tuta la kupitishia reli eneo la Soga mkoa wa Pwani takriban kilomita 37 kutoka Pugu mkoa wa Dar es salaam
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images