Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

Wanafunzi saba wafanya mtihani na kufaulu kupandishwa madaraja ya mkanda mweusi wa Goju Ryu karate

0
0
 Na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii
Wanafunzi waandamizi saba wa  shule za Karate (dojo) mtindo wa Okinawa Goju Ryu  za  Kaizen na Hekalu la Kujilinda  za jijini Dar es salaam na Dodoma wamefanya mitihani na kufaulu kupandishwa madaraja ya mkanda mweusi chini ya Sensei Rumadha Fundi  (BOFYA HAPA KUMJUA) usiku wa Jumatatu Januari 22, 2018.
Wanafunzi hao kutoka Kaizen dojo  iliyopo Shule ya Sekondari ya Jamhuri na dojo dada ya Hekalu la Kujilinda iliyopo katika shule ya msingi ya Zanaki ni pamoja na ma-Senpai Yusuf Kimvuli, Abdulwahud Aghfoul, Bilali Mtenga na Seif Soud ambao wamepanda kutoka mkanda mweusi daraja la kwanza (1st Dan)  kwenda la daraja la pili (2nd Dan) lijulikanalo kama "Nidan".
Wakati ma-Senpai Kimvuli, Maghfoul na Mtenga wanatoka dojo la Kaizen, Senpai Seif Soud anatoka Hekalu la Kujilinda.
Wanafunzi wengine watatu waliofaulu na kupanda daraja la kwanza (1st Dan) ama "Shodan" kutoka mkanda wa kahawia ni ma-Senpai Abdulmajid Khan wa Hekalu la Kujilinda pamoja na  Shaaban Yusuf na Galant Swai ambao wanatoka katika tawi la Hekalu la Kujilinda lililopo mjini Dodoma kwa jina la Miyagi dojo.
Hii ni mara ya kwanza kwa  Sensei Rumadha Fundi  mwenye Dan 4,“Yondan” na  mwenye uzoefu mkubwa wa  mafunzo ya Goju Ryu chini ya walimu wakuu wengi maarufu toka Okinawa, Japan, kuwafanyia mitihani na kuwapandisha madaraja wanafunzi wa Tanzania.
Sensei Rumadha, ambaye alianza mafunzo ya Okinawa Goju Ryu miaka 38 iliyopita  katika Hekalu la Kujilinda la Zanaki amesema anajisikia furaha na fahari kutimiza hilo jukumu lake kwa mara ya kwanza, na kwamba hajutii kufunga safari hii kutoka Houston, Marekani, anakoishi na kuja kuwasaidia ndugu zake.
Na hilo liliwezakana baada ya mwaka jana huko  nchini Poland  Sensei Rumadha kufanya  na kufaulu vizuri mitihani wake wa kupanda ngazi toka Dan ya tatu "Sandan" kwenda ngazi ya nne "Yondan"  chini ya waamuzi (masters) toka Okinawa wakiongozwa na Sensei Yoshihiro Kancho Miyazato, ambaye ni Master au mwalimu mkuu wa Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu Karate-Do huko Okinawa.
Tokea hapo Sensei  Rumadha amekuwa na mamlaka ya kuwasaidia wanafunzi wake wa Tanzania na kuwafanyia mitihani na kuwapa wanafunzi  "Dan" hadi ngazi ya pili " Nidan" sababu katika Goju Ryu Karate  kuanzia Dan ya 3 na kuendelea hutolewa na Master Miyazato pekee.
"Hawa waliofaulu na kupanda daraja la pili hivi sasa wana mamlaka ya kufungua shule zao chini ya uangalizi wangu na wakiendelea kufanya vyema nitatoa idhini ya wao kuwa waalimu ("Sensei") wanaotambulika Okinawa  baada ya muda si mrefu ujao" amesema Sensei Rumadha.
Hakusita kutoa shukran zake nyingi kwa mlezi wake wa mafunzo tokea utotoni,  "Sensei Magoma Nyamuko Sarya akisema chini ya uongozi wake kitengo cha watoto kilichoitwa "Bomani Brigade"  kilichobuniwa  na mwanzilishi wa Okinawa Goju Ryu nchini Tanzania mwaka 1973,  hayati Sensei Nantambu Camara Bomani. 
Alitoa shukurani za pekee kwa viongozi wa sasa wa Hekalu la Kujilinda - Sensei Mohamed Murudker, Sensei Wilfred Melkia, Sensei Geofrey Sawayael “Shoo” na Sensei Rashid Almasi ambao amesema moyo wao wa  kuendeleza Goju Ryu bila kutetereka pale Zanaki ni wa kusifika, na kwamba anawapongeza sana.
Sensei Rumadha pia ameeleza kuwa kabahatika mwaka huu kualikwa kuiwakilisha Tanzania ambayo pamoja na na Angola ni nchi pekee za Afrika zilizoalikwa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 65 tangu kuanzishwa kwa chama cha "Jundokan" na Master Eiichi Miyazato Sensei huko Naha City, Okinawa, mwezi wa Novemba 1918. 
Chama hicho kwa sasa kinaongozwa na mwanawe Yoshihiro Kancho Miyazato, ambaye pia ni Mwenyekiti mkuu dunia wa chama hicho na mwanae Master Eiichi Miyazato, ambaye amewafanyia mitihani ya mkanda mweusi zaidi ya walimu 15 toka ngazi ya pili" Nidan" hadi ngazi ya saba "Nandan". 
Kwa mujibu wa Sensei Rumadha, ngazi hizo zote kwa utamaduni wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu Karate huchukua miaka mingi sana kupandishwa ngazi  tofauti na mitindo mingine. 
 Sensei Rumadha Fundi akiwafanyisha mazoezi wanafunzi saba hao kabla ya kuanza kufanya mtihani wao wa kupanda daraja katika Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam Jumatatu usiku Januari 22, 2018
Viongozi wakuu wa  Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam  wakishuhudia  wanafunzi saba wakifanya mazoezi kabla ya mtihani Jumatatu usiku Januari 22, 2018. Kutoka kulia ni Sensei Wilfred Malekia, Sensei Mohamed Murudker na Sensei Rashid Almasi
  Sensei Rumadha Fundi akiendelea kuwafanyisha  mazoezi wanafunzi saba hao kabla ya kuanza kufanya mtihani wao wa kupanda daraja katika Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam Jumatatu usiku Januari 22, 2018
Sensei Rumadha Fundi akiendelea kuwafanyisha  mazoezi kwa vitendowanafunzi saba hao kabla ya kuanza kufanya mtihani wao wa kupanda daraja katika Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam Jumatatu usiku Januari 22, 2018
 Sensei Rumadha Fundi akitoa mwongozo akiwa na uongozi wa dojo kabla ya  mtihani  wa kupanda daraja wa wanafunzi saba  katika Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam Jumatatu usiku Januari 22, 2018
 Kutoka kushoto Ma-Senpai Abdulmajid Khan wa Hekalu la Kujilinda pamoja na  Shaaban Yusuf na Galant Swai ambao wanatoka katika tawi la Hekalu la Kujilinda lililopo mjini Dodoma kwa jina la Miyagi dojo wakifuatiwa na ma-Senpai Yusuf Kimvuli wa Kaizen dojo na Senpai Seif Soud wa Hekalu la Kujilinda.
Wanafunzi watatu waliofaulu na kupanda daraja la kwanza (1st Dan) ama "Shodan" kutoka mkanda wa kahawia ni  kutoka kushoto ma-Senpai Abdulmajid Khan wa Hekalu la Kujilinda pamoja na  Shaaban Yusuf na Galant Swai ambao wanatoka katika tawi la Hekalu la Kujilinda lililopo mjini Dodoma kwa jina la Miyagi dojo.

Nyumba inauzwa Mbezi Beach, maeneo ya Jogoo, jijini Dar es salaam.

0
0
  Ni ya ghorofa mbili na apartment tatu.
 Bei ni 380m/-  
Dalali haitajiki. 
Kwa mawasiliano piga namba 0626171080
Muonekano wa mbele
 Muonekano wa nyuma
 Muonekano wa pembeni
Muonekano wa ndani

Wakulima na Wasambazaji mbolea Rukwa Waridhishwa na upatikanaji wa mbolea hadi vijijini.

0
0
Wafanyabiashara wakubwa wa mbolea Mkoani Rukwa pamoja na wakulima wameridhishwa na upatikanaji wa mbolea na kusifu juhudi za serikali baada ya kupaza sauti zao na kusikika na Rais Dk. John Pombe Magufuli na jambo hilo kufanyiwa kazi ndani ya muda mfupi.
Wafanyabiashara hao wamesema kuwa wakulima hivi sasa hawapangi tena foleni kusubiri mbolea iliyokuwa ikipatikana kwa taabu na kwa kunyang’anyiana na kuwa foleni hizo zimekwisha na wakulima hawana haja ya kutoka Kijiji kuja mjini kufuata mbolea kwani mbolea hizo zinawafuata huko waliko hasa baada ya marekebisho ya bei elekezi iliyotolewa na Uongozi wa mkoa wa Rukwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo.
Mmoja wa Wafanyabiashara hao wakubwa Mohamed Rashid Mdangwa wa Kampuni ya ETG amesema “Sasa wakulima wameanza kupata mbolea kwa wingi, mwanzo walikuwa wanapanga foleni hapa lakini kuanzia ile Jumatatu agizo la Rais kuwa mbolea iende Mkoa wa Rukwa, sasa hivi population (wingi) ya watu imepungua sana,  sasa hivi mahitaji ya mbolea sio makubwa sana kama miezi miwili iliyopita,na mbolea ipo nyingi njiani inakuja, na bei elekezi aliyoitoa Mkuu wa Mkoa imesaidia mbolea kufika vijijini kupitia wakala wadogo wa mbolea.”
Yamewsemwa hayo baada ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kupitia maghala makubwa ya mbolea yaliyopo Sumbawanga Mjini pamoja na baadhi ya wasambazaji wadogo ili kujionea upatikanaji wa mbolea hizo tangu kutolewa kwa agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli la kusambaza mbolea hizo katika Mikoa inayoongoza kwa uzalishaji wa chakula nchini tarehe 8.1.2018.
Mh. Wangabo aliwasihi wasambazaji wadogo wa mbolea kuendelea kujitokeza na kununua mbolea hiyo ambayo bei iliyopo sasa imezingatia maoni yao na haiumizi, hivyo kufanya hima kuhakikisha kuwa mkulima hakosi mbolea ili kuweza kubaki katika lengo la kuzalisha chakula kwa wingi na kuleta ushindani na mikoa mingine inayozalisha chakula.
“Mimi nitoe wito tu kwa wale Agrodealers (wasambazaji wadogo wa mbolea) wafike kuendelea kununua mbolea, hata bei tumekwishazifikiria tena upya, kila Halmashauri katika Wilaya wamekwisha kaa na kutoa mapendekezo yao halisi ya kiusafirishaji, kwahiyo wafike wanunue mbolea na kutakuwa na faida, bei imezingatia hadi miundombinu iliyoharibika hakutakuwa na usumbufu,” Mh. Wangabo alifafanua.
Mh. Wangabo alitembelea maghala matatu ya wafanyabiashara wakubwa waliopo mjini sumbawanga, TFC pamoja na maduka ya wasambazaji wadogo matatu na kuongea na baadhi ya wakulima ili kujithibitishia upatikanaji wa mbolea hiyo kwa maeneo ya mjini na inayopelekwa vijijini.
Kwa msimu wa 2016/2017 Mkoa wa Rukwa ulilima Hekta zipatazo 556,975.9 na kuvuna tani 1,109,055.6 za mazao ya chakula kati ya hizo mahindi yalikuwa tani 710,602. Kwa msimu huu wa Kilimo wa 2017/18 Mkoa umelenga kulima jumla ya eneo la Hekta 554,310.6 na kuvuna tani 1,669,746.2 za mazao ya chakula.
 Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa, Kamanda wa Zimamoto Mkoani Rukwa akikagua mbolea katika ghala la Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC) lililopo Sumbawanga Mjini.  ​
 Mmoja wa Wasambazaji wakubwa wa mbolea Mkoa wa Rukwa Mohamed Mdanga (Kulia) akitoa maelezo ya upatikanaji wa mbolea Mkoani humo mbele ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo(kushoto) alipokwenda kumtembelea kwenye ghala lake na kukuta mbolea zai ya tani 300.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa mbele wa kwanza kushoto)alipokuwa akipita mtaa kwa mtaa katika mji wa Sumbawanga kujionea biashara ya mbolea inavyokwenda katika maduka ya mbolea (hayapo pichani) huku akiwa ameambatana na Meya wa manispaa ya Sumbawanga Mh. Justin Malisawa (koti la Draft).
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa pili kutoka kulia) akiwa amesimama mbele ya duka la mbolea kuulizia upatikanaji wa bidhaa hiyo katikati ya mji wa sumbawanga, Mkoani Rukwa. 
 Timu ya wataalamu wa Kilimo, Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na Viongozi wa Manispaa ya Sumbawanga,  wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kupita duka hadi duka kujionea upatikanaji wa mbolea katika mkoa wa Rukwa.

MAGAZETI YA JUMATANO LEO JANUARY 24,2018

Dkt. Abbas akutana na kufanya Mazungumzo na Viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari Kanda ya Kati

0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi leo (jana) amekutana na kufanya Mazungumzo na Viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari Kanda ya Kati Mjini Dodoma.

KAIMU MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI (TAA) ATEMBELEA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye kushoto akimkaribisha Kaimu Mkuu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela kulia alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 23/01/2018.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam, wakati alipofanya ziara yake mapema jana  tarehe 23/01/2018.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (aliyeketi mbele) pamoja na Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo wakimfuatilia kwa karibu, Kaimu Mkurugenzi MKuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela, wakati wa mazungumzo yao alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 23/01/2018.
Picha ya Pamoja, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (wa pili kushoto) akiwa na Viongozi Waandamizi wa Jeshi pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela (wa tatu kulia), mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo, Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 23/01/2018.Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

RC NDIKILO-VIGOGO WASIOJULIKANA WALIOVAMIA MSITU WA HIFADHI WA KAZIMZUMBWI WASAKWE

0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Kisarawe

VYOMBO vya ulinzi na usalama,Mkoani Pwani vimetakiwa kuwatafuta baadhi ya watu wanaodhaniwa kuwa ni vigogo,; kuvamia msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi uliopo wilayani Kisarawe na kugawa viwanja.

Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ,alitoa rai hiyo wakati alipotembelea msitu huo kujionea baadhi ya maeneo ambayo yalivamiwa na wavamizi hao.Alisema vigogo hao wamesababisha msitu huo kuingiliwa na kuvamiwa mara nne na kundi la watu ambao wanadai sehemu ya msitu ni mali yao. 

Mhandisi Ndikilo ,alieleza kundi hilo limekuwa likiisumbua serikali kwa kwenda mahakamani na kushindwa .Aidha alisema vyombo hivyo vifanye ufuatiliaji kujua ni vigogo gani ambao wamekuwa wakiwatumia baadhi ya watu kwenda kushtaki mahakamani ili wapewe maeneo hayo kwa ajili ya viwanja .

“Inadaiwa kuna kampuni ilikata viwanja zaidi ya 300 na kuwauzia watu jambo ambalo haliwezekani kwani msitu huo umehifadhiwa kisheria”alisema mhandisi Ndikilo.Mhandisi Ndikilo,alisema kuwa msitu huo ulindwe kwani ni kama mapafu ya kupumulia viwanda na hewa ukaa hivyo endapo msitu huo utaharibiwa itahatarisha afya za watu. 

“Serikali ya mkoa haikibali hili,nimeshangazwa na kusikia kuna tume imekuja hapa Kisarawe na kuwahoji wataalamu mbalimbali juu ya suala la msitu huu wakati hakuna rufaa ya kesi ambayo ilifunguliwa na wavamizi ambao walishindwa”:;
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo (Wa kwanza kushoto)na kaimu meneja wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS)wilayani Kisarawe Mkoani Pwani, Endrew Mwenuo (wa pili kulia)na mkuu wa wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda ( Wa kwanza kulia) wakiangalia namna uvamizi ulivyofanywa na baadhi ya watu na vigogo katika msitu wa Kazimzumbwi wilayani Kisarawe.
Kaimu meneja wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS)wilayani Kisarawe Mkoani Pwani, Endrew Mwenuo (kushoto) akimwelekeza jambo mkuu wa Mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo kuhusiana na uvamizi uliofanywa na baadhi ya watu na vigogo katika msitu wa Kazimzumbwi.Picha na Mwamvua Mwinyi.


RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AZUNGUMZA NA MFALME WA DUBAI, WAFANYABIASHARA, ATEMBELEA BANDARI WA JEBEL ALI PORT NA KUTEMBELEA MRADI WA AKHEEL.

0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na mazungumzo na Mfalme wa Dubai Shaikh Mohammed Bin Rashid Al Maktoum, Vice President, Prime Minister and Ruler of Dubai, alipofika katika makaazi ya Mfalme huyo Nchini Dubai akiendelea na ziara yake ya kiserikali katika Nchi za Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu (UAE ).
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali. Mohamed Shein, Mfalme wa Dubai Shaikh Mohammed Bin Rashid Al Maktoum, Vice President, Prime Minister and Ruler of Dubai, wakibadilisha mawazo na CEO na Rais Shirika la Ndege la Emirates Airline Sheikh.Ahmed Bin Saeed Al Makhtoum,baada ya mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa makaazi ya Mfame Nchini Dubai.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Mfalme Shaikh. Mohammed Bin Rashid Al Maktoum, Vice President, Prime Minister and Ruler of Dubai, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika makaazi ya Mfalme Dubai akiwa katika ziara yake katika Nchi za UAE.




 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Ujumbe wake akizungumza na Wafanyabiasha wa Umoja wa Nchini za Falme za Kiarabu UAE (Business Community Chamber of Commerce Dubai) mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa jengo la jumuiya hiyo Dubai. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA





Wavuvi waaswa kulima pindi Ziwa Rukwa linapofungwa Januari hadi April Kila Mwaka.

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaasa wavuvi wanaozunguka ziwa Rukwa kuhakikisha wanatafuta ardhi kwaajili ya kilimo, biashara pamoja na ufugaji katika kipindi cha kunzia mwezi wa kwanza hadi wanne kila mwaka ili kuwaacha samaki wa ziwa hilo kuzaliana.

Amewaasa kutotegemea shughuli moja tu kwaajili ya kuwaingizia kipato, “Wavuvi msitegemee kuvua tu, jishughulisheni na kazi nyingine za kuwaingizia kipato kama vile kilimo, biashara pamoja na ufugaji, hatufungi kambi hizi kwaajili ya kipindupindu tu lakini pia ili kuweza kuwaacha samaki wazaliane katika kipindi cha kuanzia mwezi wa kwanza hadi wanne,”

Ameyasema hayo alipofanya ziara kwenye kambi ya Nankanga iliyopo katika Kijiji cha Solola Wilayani Sumbawanga ili kujionea hali halisi ya maisha ya wavuvi katika kambi zisizo rasmi na namna ya kuweka mpango salama wa kuweza kuwaepusha na ugonjwa wa kipindupindu ulioenea katika makambi hayo yanayozunguka ziwa Rukwa. 

Tangu ugonjwa huo uingie Mkoani Rukwa tarehe 15/11/2017 tayari watu 210 wanaugua ugonjwa huo na watu nane wamepoteza maisha wote wakiwa wanatokea katika makambi hayo yasiyo rasmi ambapo hadi sasa kambi zisizo rasmi zaidi ya tisa zimefungwa huku zoezi hilo likitegemewa kuendelea hadi hapo Mwezi wa tano.

Nae Diwani wa kata ya Nankanga kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule amesema kuwa katika kambi hiyo kuna watoto 270 walio na umri chini ya miaka 7 ambao wamekosa kwenda shule na hivyo wananchi kujenga madarasa mawili ya shule shikizi katika kitongoji kilichopo Km 9 kutoka kwenye kambi hiyo yaliyofikia usawa wa linta na kumuomba Mkuu wa Mkoa kuwaunga Mkono jambo lililompelekea Mh. Wangabo kutoa bati 50 na kuitaka Halmashauri kuongezea bati 50 ili kukamilisha ujenzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiwaasa wavuvi wa kambi ya Nankanga kujishughulisha na kilimo hasa katika kipindi cha mwezi wa kwanza hadi wa Nne kila mwaka pindi shughuli za uvuvi zinapofungwa ili kuwaacha samaki wazaliane na kutunza Ziwa lisipotee kwa faida ya vizazi vijavyo. 

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELELEA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO NA MAKUMBUSHO YA OLDUVAI GORGE

0
0
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kazi nzuri iliyofanya ya ujenzi wa jengo la makumbusho ya kisasa katika Bonde la Olduvai ya Gorge ambako ni chimbuko la historia ya Binadamu.

Kamati hiyo imesema imeridhishwa na ujenzi wa jengo hilo ambalo litawavutia watalii na wanasayansi wabobezi wa masuala ya Malikale kutembelea Makumbusho hiyo.

Kamati hiyo ilibainisha kuwa Makumbusho hiyo mbali ya kutumika kuingiza pesa kupitia watalii pia inatumika kama kielelezo na utambulisho muhimu wa taifa katika kutangaza utamaduni wa Mtanzania ndani na nje ya nchi.

Hayo yalisemwa jana na Kamati hiyo wakati ilipofanya ziara ya kutembelea Ngorongoro Crater na Makumbusho ya Olduvai Gorge katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo. Kemilembe Luota ameipongeza Serikali pamoja na wataalamu kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kuhakikisha kuwa eneo la Olduvai Gorge linakuwa kivutio bora kwa ajili ya historia ya nchi na kivutio kikubwa cha Utalii duniani.
 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kulia) wakizungumza na Mbunge wa viti maalumu, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Zainabu Mwamwindi wakiwa wameongozana na Wajumbe Kamati hiyo wakati walipotembelea jana Jengo la Makumbusho ya Olduvai ya Gorge ambako ni chimbuko la historia ya Binadamu katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii , Kemilembe Luota ( wa kwanza kushoto) Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa pili kulia) wakiwa na baadhi ya Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa kwenye ‘’View Point’ kituo ambacho hutumika kuangalia bonde la Ngorongoro kabla ya kutelemka katika Bonde hilo jana wakati walipofanya ziara ya kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Huyu ndiye Faru Fausta ni faru kikongwe kuliko wote nchini, akiwa na umri wa miaka 54, na anahitaji matunzo mazuri ili aendelee kuvuta watalii na wanasayansi kutoka kila pembe ya dunia.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiwa katika nje ya ofisi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kuanza ziara.
Kundi la Simba wakiwa wamepumzika walipoonekana jana wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilipofanya ziara ya kutembelea Bonde la Ngorongoro.

RAIS KARIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA KOCHA NTAMBI NA ISMAIL SUMA

0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Ndugu Wallace Karia amepokea kwa huzuni na mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Kocha msaidizi wa Mwadui FC Jumanne Ntambi kilichotokea usiku wa kuamkia leo huko Shinyanga.

Rais Karia kwa niaba ya TFF ametoa pole kwa familia ya kocha huyo ,timu ya Mwadui FC,wanafamilia wa Mpira wa Miguu,ndugu ,jamaa na marafiki.

“Kifo cha Kocha Ntambi kimenishtua sana na kwa niaba ya Shirikisho natoa pole kwa wafiwa nawaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu kwao kumpoteza mpendwa wao,hakika alikuwa kocha aliyejitahidi kuibua vipaji na amekuwa na mchango mkubwa katika mpira wa miguu ambao bado alikuwa anautumikia mpaka kifo chake.” Alisema Rais Karia.

Kocha Ntambi hakuweza kuhudhuria mazoezi ya Mwadui yaliyofanyika jana kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu badala yake alifika mazoezini mwishoni kabla ya usiku mauti kumkuta akiwa nyumbani kwake,Mungu ailaze roho ya marehemu Ntambi mahala pema peponi,Amina.

Enzi za uhai wake Ntambi aliwahi kufundisha timu za Kahama United ya Shinyanga,Mlale JKT ya Ruvuma,Panone ya Kilimanjaro,Timu ya mkoa wa Shinyanga Igembe Nsabo na mpaka mauti yanamkuta alikuwa akiifundisha Mwadui ya Shinyanga akiwa kocha msaidizi.

Wakati huohuo Rais Karia pia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya aliyekuwa golikipa wa zamani wa Yanga na Simba Ismail Suma aliyefariki nchini Burundi.Rais Karia ametoa pole kwa wafiwa kufuatia msiba huo wa Suma aliyefariki kwa maradhi ya ini na figo.

Suma wakati wa uhai wake mbali na kuvitumikia vilabu vya Simba na Yanga pia amewahi kuvitumikia vilabu vya Kariakoo United ya Lindi na African Lyon ya Dar Es Salaam.

Naibu Waziri Kandege avunja mkataba wa TBA na Halmashauri ya Wilaya ya Butiama.

0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege ameagiza kuvunjwa kwa Mkataba wa Tsh Bil 3.2 kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Butiama iliyokuwa ikijengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Mhe Kandege ameyasema hayo kufuatia Ukaguzi aliyoufanya baada ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa aliyekamilisha ziara yake Mkoani hapa kumuagiza kufanya Ukaguzi huo kutokana na kutoridhishwa na taarifa aliyoipokea kutoka kwa Meneja wa TBA Mkoa wa Mara kuhusiana na mradi huo.

Mhe Kandege alisema kuwa katika ukaguzi wake amebaini kuwepo kwa kasi ndogo ya utekelezaji wa Mradi huo na kubadilishwa kwa eneo lililofanyiwa usanifu hapo awali kwa ajili ya ujenzi badala yake kazi hiyo kufanyika katika eneo tofauti na lile la awali hivyo kuiongezea Serikali gharama ya Tsh Mil. 180.

Aidha, aliongeza kuwa taarifa iliyotolewa na Meneja wa Wakala wa Majengo Mkoa wa Mara kwa Waziri Mkuu ilieleza kuwa kati ya Tsh. mil. 600 zilizopokelewa Aprili, 2017 kutoka Serikali kuu, Tsh Mil. 400 zimekwishatumika kujenga msingi na kazi hiyo imekamilika kwa asilimia 60 tofauti na hali aliyoikuta alipotembelea eneo hilo la Mradi.
Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe Josephat Kandege akimskiliza Meneja wa TBA Mkoa wa Mara wakati alipotembelea eneo ya ujenzi wa Ofisi za Halmashauri ya Butiama
Hapa ndipo mradi ulipofikia wa ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Butiama inayojengwa na TBA ambao mkataba wake umesitishwa
Hii ndio Kazi iliyofanyika mpaka sasa kwenye eneo la Ujenzi ilihali taarifa iliyotokewa kwa Waziri Mkuu ni kuwa ujenzi wa Msingi umefikia asilimia 60.

RC Wangabo atoa miezi mitatu kwa wavuvi Ziwa Rukwa kuhama kambi kuepuka kipindupindu.

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa miezi mitatu kwa wananchi wanaoishi katika kambi ya uvuvi ya Nankanga iliyopo kando ya ziwa Rukwa kuhama kwa hiyari baada ya kambi hiyo kuwa katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kipindupindu kwa kutokuwa na vyoo.

Mh. Wangabo amesema kuwa kuondoka huko kwa hiari kuwepo ndani ya mwezi huu wa kwanza hadi wa nne baada ya kuona wingi wa wananchi wanaoishi katika kambi hiyo pamoja na kutokuwepo kwa kipindupindu kwa wakati huu ila zoezi hilo ni la tahadhari ili kujikinga na ugonjwa huo.

“Hatuwezi kuendelea kuishi mahali hapa ambapo vyoo vyenyewe vinaingiliana na maji ya kunywa, na ili kisije hapa kipindupindu ni lazima watu wasifanye shughuli kwenye ziwa ili kuwe salama, lakini mkiruhusu kipindupindu kuingia hapa tutawafurusha, tena tutawasimamia kweli kweli, tutawapiga quarantine (kuwaweka kwenye kizuizi) mkipona tutawaswaga,” Amesisitiza

Ameyasema hayo alipofanya ziara kwenye kambi ya Nankanga iliyopo katika Kijiji cha Solola Wilayani Sumbawanga ili kujionea hali halisi ya maisha ya wavuvi katika kambi zisizo rasmi na namna ya kuweka mpango salama wa kuweza kuwaepusha na ugonjwa wa kipindupindu ulioenea katika makambi hayo yanayozunguka ziwa Rukwa. 

Nae Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule alitoa hadi tarehe 1/5/2018 wananchi hao wawe wameyahama makazi hayo na kujisogeza kwenye vitongoji vya jirani huku akiwasihi viongozi wa vijiji na vitongoji hivyo kushirikiana kuhakikisha wanatoa maeneo kwaajili ya wananchi hao kuhamia.

“Kuanzia tarehe 1 mwezi wa 5 hapa hatutaki kumuona mtu, kama una kibanda chako ama bati lako anza sasa hivi kwa kushirikiana na mwenyekiti wa Kijiji na Mtendaji wa Kata mtafute nafasi katika kitongoji cha Isanga kila mtu ajenge nyumba,” Alisisitiza.

Hatua hiyo imekuja baada ya ugonjwa wa kipindupindu kusambaa kwenye kambi kadhaa za wavuvi pembezoni mwa ziwa rukwa na kusababisha watu 210 kuumwa ugonjwa huo na watu nane kupoteza maisha, ambapo hadi sasa kambi zisizo rasmi zaidi ya tisa zimefungwa huku zoezi hilo likitegemewa kuendelea hadi hapo Mwezi wa tano.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa kwanza mbele kulia) akiwa ameambatana na mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule wakitembelea kambi ya mererani waliyohamishwa wavuvi kwa nguvu ili kuepuka kipindupindu na kulinda mazingira ya ziwa hilo. 
 Moja ya kibanda kilichokuwa katika kambi ya Wavuvi ya Mererani kikiwaka moto ikiwa ni juhudi za kuwaondoa wavuvi waliopo ndani ya Ziwa Rukwa kuwaepusha na kipindupindu na kulinda ziwa lisipotee. 
 Miongoni mwa wananchi waliokuwa wakiishi katika makambi ya wavuvi yalipo ndani ya Ziwa Rukwa yaliyoathiriwa na kipindupindu wakisimamiwa kuhama kambi hiyo ili kujiepusha na kipindupindu na kuliza Ziwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa tahadhari kwa Wavuvi waliohamishwa kwenye makambi (hawapo pichani) kutorudi katika makambi hayo kwa usalama wa afya zao na kuendelea kulitunza ziwa Rukwa. 
 Miongoni mwa Vyoo vinavyotumiwa na Wavuvi wa kambi ya Nankanga waliopewa miezi mitatu kuihama kambi hiyo kabla ya kipindupindu kuwamaliza. 
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alipoongozana na kamati ya ulinzi na Usalama kuangalia moja ya choo kinachotumiwa na wavuvi wa kambi ya Nankanga, choo ambacho si salama kwa matumizi ya binadamu.

MRADI WA MAJI NA JENGO LA UZAZI ZAHANATI YA YOMBO/BAGAMOYO YAKWAMA

0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo.

Wakazi wa kijiji cha Yombo kata ya Yombo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wamelalamikia mradi wa maji uliofadhiliwa na Bank ya Dunia na kugharimu milioni 297, ambao haufanyikazi huku wakiwa hawanufaiki nao tangu ukamilike.

Aidha wamelalamikia kukwama kwa mradi wa jengo la uzazi, katika zahanati ya Yombo,ambalo limetumia kiasi cha sh.mil.55 na kuwekwa jiwe la  msingi na katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa,Abdulrahman Kinana tangu mwaka 2014.

Kilio hicho kimetolewa na baadhi ya wakazi wa kijiji hicho ,wakati wa mkutano wa wananchi uliomwita diwani wa kata ya Yombo ,Mohammed Usinga kwenda kuwaeleza hatua zinazochukuliwa ili kukamilisha miradi hiyo .

Mkazi wa Yombo,Jabir Omary ,alisema inasikitisha kuona serikali na wafadhili wanatumia mamilioni ya fedha kwenye miradi ya maendeleo lakini haiendelezwi na haifanyikazi.

Alieleza mradi huo wa maji umetumia fedha nyingi ,hivyo ni jukumu la serikali kuisimamia ili ilete tija ndani ya jamii.Mkazi mwingine ,Abubakar Harubu alimtaka diwani wa kata hiyo pamoja na bodi ya maji ya kata kufuatilia na kusimamia kero hizo kwa maslahi ya wakazi hao.
 Diwani wa kata ya Yombo wilayani Bagamoyo, Mohammed Usinga akizungumza na wakazi wa kijiji cha Yombo kuhusiana na baadhi ya miradi ya maendeleo isiyofanyakazi na mengine kushindwa kuendelezwa.(picha na Mwamvua Mwinyi)
 Jengo la wodi ya uzazi katika zahanati ya Yombo, Bagamoyo likiwa limekwama kwenye ujenzi na kuwekwa jiwe la msingi na katibu mkuu wa CCM Taifa ,Abdurahman Kinana mwaka 2014 .

Mradi wa maji uliofadhiliwa na bank ya dunia na kugharimu mamilioni ya fedha huko kata ya Yombo Bagamoyo, ambao haufanyi kazi iliyotarajiwa na wananchi hawanufaiki nao tangu ukamilike 2015.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI WA NISHATI ARIDHISHWA NA KAZI YA UJENZI WA NJIA YA UMEME KUELEKEA STIEGLERS GORGE

0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameeleza kuridhishwa kwake na kazi ya ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha Umeme wa msongo wa kV 33 inayojengwa kuelekea eneo litakalotumika kuzalisha Umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (Stiegler’s Gorge).

Dkt. Kalemani aliyasema hayo mkoani Morogoro wakati alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa kazi ya maandalizi ya ujenzi wa mradi wa Stiegler’s Gorge utakaozalisha umeme wa kiasi cha megawati 2100 pamoja na kuzungumza na wananchi katika vijiji vinavyopitiwa na miundombinu hiyo ya kusafirisha Umeme.

Dkt. Kalemani alisema kuwa, maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa Umeme wa Stiegler’s yanajumuisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ya Barabara na usafirishaji Umeme kuelekea eneo la Mradi ili mradi huo mkubwa utekelezwe kwa ufanisi. 
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( wa Nne kushoto) akikagua maeneo ambayo miundombinu ya usafirishaji umeme inajengwa kuelekea katika eneo la Mto Rufiji utakapotekelezwa mradi wa uzalishaji umeme wa megawati 2100. Wa Tatu kulia ni Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo na wengine ni watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kampuni ya  ETDCO ambayo ni kampuni tanzu ya TANESCO.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akizungumza na watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kampuni ya  ETDCO ambayo ni kampuni tanzu ya TANESCO wakati alipokuwa katika kijiji cha Dakawa mkoani Morogoro kukagua miundombinu ya usafirishaji umeme inayojengwa kuelekea katika eneo la Mto Rufiji utakapotekelezwa mradi wa uzalishaji umeme wa megawati 2100.

Kazi ya ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji umeme kuelekea katika eneo la Mto Rufiji utakapotekelezwa mradi wa uzalishaji umeme wa megawati 2100 ikiendelea. Kazi hiyo inatekelezwa na  kampuni ya  ETDCO ambayo ni kampuni tanzu ya TANESCO.


Helioum One yagundua heliamu ya futi za ujazo bilioni 98.9

0
0
Kampuni ya uchunguzi na utafiti wa madini, Helium One, ambayo kwa sasa inafanya utafiti wa gesi ya heliamu mkoa wa Rukwa imegundua kuwapo kwa futi za ujazo bilioni 98.9 za gesi hiyo katika maeneo iliyokwishafanyia uchunguzi. Hayo yalielezwa katika warsha ya siku moja iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, na kuratibiwa na Idara ya Jiolojia ya chuo hicho, Helium One na Chuo Kikuu cha Oxford.

Akizungumza katika warsha hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Helium One, Thomas Abraham-James, alisema kwamba kampuni yao imetafuta leseni 23 za uchunguzi na kwamba nyingine tatu zimeombwa.Alisema kwamba leseni hizo zote zinamilikiwa na kampuni hiyo kwa asilimia 100 na kwamba ina haki za kipekee za gesi hiyo ya heliamu .

Pamoja na kutoa taarifa hiyo,alisema lengo la kuwa na warsha ni kuwaita wataalamu na wadau mbalimbali wa hapa nchini na kimataifa ubadilishana uzoefu na taarifa zilizopo kuhusu gesi hiyo na kuangalia fursa zinazoambatana na uwapo wa gesi hiyo katika harakati za kitaifa za kuwa na taifa la viwanda.

“Helium One inaamini kwamba kuna fursa kupitia utafiti huu kuweza kutengeneza utaalamu wa kiwango cha juu na utaalamu wa hapa nchini juu ya uendelezaji wa gesi hiyo. Tutaendelea kujenga uhusiano na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuweza kubadilishana elimu, kutoa mafunzo kwa wanafunzi na maofisa wizara ya madini na kutengeneza mpango wa ufadhili wa masomo,” alisema.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya utafutajji gesi ya Helium One, Thomas Abraham-James, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa warsa juu ya ugunduzi wa gesi ya Helium iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Idara ya Jiolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Hudson Nkotago akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa warsa juu ya ugunduzi wa gesi ya Helium iliyoandaliwa na kampuni ya utafutaji wa gesi ya Helium One kwa kushirikiana na Idara ya Jiolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Azam FC: Tumejipanga Kuchukua Pointi Tatu dhidi ya Yanga

0
0
Na Agness Francis,Blog ya Jamii. 
  MCHEZO kati ya Timu ya Azam FC dhidi ya Timu ya Yanga unaotarajiwa  kuchezwa Jumamosi saa 1 usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Timu ya Azam imesema   kuwa Timu imeishaingia Kambini kwaajili ya maandalizi ya mchezo huo. 

Akizungumzia kuelekea kuhusu mchezo huo Afisa Habari wa Azam FC, Jaffary Iddy Maganga amesema kuwa  kikosi cha Azam FC iko imara katika kuweza kuwakabili Yanga na matokeo ya mchezo huo ni Dakika 90. 

Azam watashuka dimba ni siku hiyo dhidi ya YangAfricans mchezo utakaokuwa wa kukata na shoka ambapo timu zote mbili zitakuwa na hamu ya kupata Ushindi  wa pointi Tatu siku hiyo. 

"Baada ya Timu kurejea kutokea  Jijini Mbeya ambapo tulikokuwa na mchezo wetu na Tanzania Persons  jana imeingia kambini  na kuanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi dhidi ya YangAfrica. Mchezo huo utakuwa ni mgumu ukizingatia Yanga nayo ni timu nzuri na Ina kikosi kipana lakini na sisi tumejipanga kunyakua pointi Tatu zenye ushindi wa mabao" Amesema Maganga

Mpaka sasa hivi Azam FC anashika nafasi ya pili kwa kwa pointi  30 kwenye misimamo Tanzania Bara akifatiwa na mabingwa watetezi  YangAfrica  mwenye pointi 25, huku wakiingozwa na pointi 33 za timu ya Simba.
Afisa Habari wa AzamFc,  Jafari Iddy Maganga akizungumza na waandishi wa habari mara  baada ya timu kuanza rasmi jana mazoezi kule Chamazi Complex, leo katika ofisi zao zilizopo Mzizima Jijini Dar es Salaam.

Ashtakiwa kwa Kutoa Taarifa za Uongo

0
0

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA

Serikali imemshtaki John Hima (29) kwa kosa la kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu Namba 9 ya mwaka 2015.

Akisoma kesi hiyo namba 9 ya mwaka 2018 katika Mahakama ya Wilaya ya Bahi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Suniva Mwajumbe, Inspekta Msaidizi Amani amesema kuwa mshtakiwa ametenda kosa hilo Januari 7 mwaka huu katika kijiji cha Nghulukano, Kata ya Chikola, Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa ni mwajiriwa wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akiwa ni mkusanya taarifa (mdadisi) katika Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2017/2018 kwa Tanzania Bara.

Hata hivyo baada ya kusomewa mashtaka hayo, Mdadisi Hima alikana mashitaka na kesi hiyo itasomwa tena tarehe 7 Februari, 2018 ambapo amerudishwa rumande baada ya kukosa wadhamini.Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama, Mwanasheria wa NBS Oscar Mangula amesema kuwa, mtuhumiwa Hima aliingia mkataba na NBS kuwa mmoja wa wadadisi wa Utafiti huo unaoendelea hivi sasa ambao ulianza Desemba mwaka jana.

“Kwa mujibu wa sheria akiwa kama mdadisi majukumu yake alitakiwa kuwa katika eneo la kazi kulingana na mkataba na kiapo alichopata ambapo yeye kwa makusudi aliamua kutelekeza majukumu hayo na kuwa nje ya kituo cha kazi hivyo kwa mujibu wa sheria ya Takwimu ametenda kosa la kijinai” amesema Mwanasheria Mangula.

Mwanasheria Mangula ameongeza kuwa, “Mkataba wa kazi ni wa miezi 12 ambapo ulianzia Desemba 2017 hadi Novemba 2018 lakini mdadisi huyu aliacha kutimiza majukumu yake kuanzia tarehe 7 Januari ambapo sisi tulifika pale tarehe 13 na 14 Januari mwaka huu ila hakuweza kufanya kazi yake kama ilivyotakiwa”.

Mwanasheria Mangula alieleza kuwa kesi hiyo inawakumbusha wadadisi waliopewa jukumu la kukusanya taarifa za kitakwimu kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa mikataba yao ya ajira, kiapo na mafunzo waliyopewa ili kuepuka kutenda makossa ya kijinai kama analodaiwa kutenda na mtuhumiwa.

Aidha, inawakumbusha wananchi umuhimu wa kuendelea kutoa ushirikiano kwa wadadisi mbalimbali wanaopewa jukumu la kukusanya taarifa za kitakwimu kwani kufanya hivyo ni kutekeleza matakwa ya Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015.

Waziri Kamwelwe Akutana na Balozi wa Ujerumani Nchini

0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Kamwelwe amekutana na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dkt. Detlef Wachter na kuzungumzia ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika kuinua kiwango cha huduma ya maji na usafi wa mazingira nchini. Katika kikao hicho kilichofanyika Ofisi za Wizara ya Maji na Umwagiliaji jijini Dar es Salaam, kililenga kuimarisha uhusiano mzuri wa Serikali hizo mbili kwa lengo kukuza maendeleo ya Sekta za Maji, ambapo Ujerumani imeendelea kuwa mdau wake mkubwa.

Mhandisi Kamwelwe ameishukuru sana Ujerumani kwa mchango wake mkubwa ambao imekua ikiutoa na kukiri umekuwa na manufaa makubwa sana kwa Tanzania, akitolea mfano utekelezaji wa miradi mikubwa ya maji ya Sumbawanga, mkoani Rukwa ambao umekamilika na Kigoma ambao uko katika hatua za mwisho kukamilika kwa ufadhili wa Serikali ya Ujerumani. Pia, Waziri Kamwelwe amesema Tanzania inategemea kutekeleza miradi mikubwa sita nchini kwa ufadhili wa Ujerumani na kuwakaribisha wawekezaji zaidi kutoka Ujerumani kwa ajili ya kuwekeza kwenye Sekta za Maji na Umwagiliaji.

Aidha, Balozi wa Ujerumani nchini, Dkt. Wachter amesema Sekta ya Maji ni moja ya sekta inayopewa kipaumbele katika ushirikiano huo na kumuhakikishia Waziri Kamwelwe dhamira ya Ujerumani kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuinua kiwango cha huduma ya maji na usafi wa mazingira nchin.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini, Dkt. Detlef Wachter pamoja na ujumbe alioongozana nao.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe akiagana na mgeni wake Balozi wa Ujerumani nchini, Dkt. Detlef Wachter mara baada ya mazungumzo yao jijini Dar es Salaam.

WATOTO 15 WENYE MATATIZO YA MOYO WAFANYIWA UPASUAJI WA BILA KUFUNGUA KIFUA

0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya  Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel na Kituo  cha Moyo  cha Berlin (Berlin Heart Center) cha nchini Ujerumani  wamefanya upasuaji  wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa watoto 15 wenye matatizo ya Moyo.

Upasuaji huo unaotumia  mtambo wa Cathlab umefanyika katika kambi maalum ya matibabu iliyoanza tarehe 20/01/2018 inatarajia kumalizika kesho tarehe 25/01/2018. Matibabu yaliyofanyika ni ya kuzibua matundu kwenye moyo na kutanua mishipa ya moyo kwa watoto wenye umri wa kuanzia mwezi mmoja hadi miaka 18.
Kambi  hii ilienda sambamba na uchunguzi wa moyo kwa watoto 32 ambapo watoto 20 watafanyiwa matibabu katika kambi hii na wengine 12 waliobaki watatibiwa na madaktari wetu wa ndani kuanzia wiki ijayo.
Tumepanga kufanya matibabu kwa watoto 20 tunaamini hadi kambi itakapomalizika watoto wote hawa watakuwa wamepata matibabu. Watoto 15 waliopata matibabu wengine wameruhusiwa na waliobaki hali zao zinaendelea vizuri na wataruhusiwa pindi afya zao zitakapoimarika.
Aidha kambi hii imeenda sambamba na utoaji wa elimu ya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua kwa watoto na jinsi ya kuwahudumia watoto waliofanyiwa upasuaji huo. Mafunzo haya yamewajengea uwezo wafanyakazi wetu wakiwemo madaktari, wauguzi, wataalam wa kutoa dawa za usingizi na wataalam wengine wa chumba cha upasuaji. Mafunzo hayo  yatawasaidia  kuongeza ufanisi katika  kazi zao.
Tangu mwaka 2015 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ilianza kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart- SACH) naBerlin Heart Center hadi sasa jumla ya watoto 46 wamefanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel. Gharama za matibabu ya watoto hawa zinagharamiwa na Taasisi hizi za Israel na Ujerumani kwa makubaliano ya kirafiki na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.
Kwa upande wa watoto waliotibiwa katika kambi maalum za matibabu zilizofanyika hapa nchini ni  79 mchanganuo wake ni kama ifuatavyo: Mwaka 2015 walitibiwa watoto  11, mwaka 2016 watoto 48,  mwaka 2017 watoto 20.
Tunawashukuru sana wenzetu hawa wa SACH na Berlin Heart Center kwa kuona umuhimu wa kutoa huduma ya matibabu bila malipo  kwa watoto wenye matatizo ya moyo.  Watoto waliotibiwa wamepona na wale ambao ni  wanafunzi   wanaendelea na masomo yao.
Kwa upande wa wazazi na walezi tunawaomba wasisahau kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya kumfikisha Hospitali na kufanyiwa vipimo  ndipo inagundulika mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo.

Kwa wamama wajawazito wafanye uchunguzi (Fetal Echocardiography) wa kuangalia kama mtoto aliyeko tumboni anamatatizo ya moyo au la. Kupitia kipimo hiki  mtoto akigundulika kuwa  na tatizo la moyo ataweza kupatiwa  matibabu kwa wakati  na hivyo kuwa na afya njema kama watoto wengine.

Kama mnavyofahamu matibabu ya moyo ni ya gharama hivyo basi tunaendelea kuwahimiza wananchi  kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambao utawasaidia kulipa gharama za matibabu pindi  watakapouguwa na kuhitaji kupata matibabu. Kwa wale wasiojiweza kabisa kambi kama hizi zinatumika na Taasisi kuwahudumia bila malipo yoyote yale.
  
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

24/01/2018
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images