Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110176 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV: RC MAKONDA APONGEZA KASI YA MATENGENEZO MAGARI YA POLISI, MAGEREZA, JWTZ


RAIA WAWILI WA INDIA WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MIWILI JELA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imewahukumu raia wawili wa India kutumikia kifungo cha kwenda jela miaka miwili ama kulipa faini ya Sh.milioni 64.

Hukumu hiyo ni baada ya kukiri mashtaka saba yaliyokuwa yakiwakabili likiwemo la kuipatia Serikali hasara ya zaidi ya Sh.milioni  694.

Mahakama pia imewaamuru wafungwa hao Kalrav Patel na Kamal Ashar kulipa Sh.milioni 694 ambazo waliisababishia hasara Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA).

 Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ametoa huku hiyo leo ambapo amesema mahakama hiyo imewatia hatiani washtakiwa hao katika makosa saba ya uhujumu uchumi.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mashauri amesema katika kosa la kwanza la kula njama, washtakiwa wanahukumiwa kwenda jela miezi 12 ama kulipa faini ya Sh.milioni 2 kwa kila mmoja.

Aidha katika kosa la pili hadi la saba, Hakimu Mashauri amesema wafungwa  hao  wamehukumiwa kwenda jela miaka 2 ama kulipa faini ya Sh.milioni 5 kwenye kila kosa kwa kila mshtakiwa.

Pia Mahakama hiyo imesema vyombo vyote ambavyo wafungwa hao walivitumia katika kuingilia miundombinu ya TCRA vimetaifishwa na Serikali.

Pia imeelezwa wakiwa maeneo ya Dar es Salaam na Zanzibar walikula njama ya kutaka kusafirisha vifaa vya mawasiliano bila kibali.

Ilidaiwa katika kipindi hicho mwaka 2015, washtakiwa hao walisafirisha vifaa vya mawasiliano kinyume na sheria za TCRA .

Mbali na mashtaka hayo pia wanakabiliwa na shtaka la kuingiza, kusimika nchini kifaa cha mawasiliano aina ya Voice Over internet protocol (Coop) na kukitumia bila ya kuthibishwa, na kusababisha hasara ya Sh.mil 694 kwa TCRA.

BAYIMBA INTERNATIONAL FESTIVAL in Kampala, Uganda, set for new location!

$
0
0

Time for change!
After 10 years in the city centre of Kampala it is time for change. In 2018, the Bayimba International Festival will move from its traditional location at the National Theatre in Kampala to a spacious new home in the midst of a leafy environment at the shores of Lake Victoria.
“We have been thinking about the long-term viability of the festival so that we can continue to go on for another 10 years. We have been exploring different approaches to sustain our annual festival and are extremely excited to have been able to acquire an amazing location,” says festival director Faisal KIWEWA.
The immediate advantage of the new location includes on-site parking, which will eliminate this logistical challenge faced thus far, as well as room for on-site accommodation. Artistic programming will also benefit from the new space, with plenty of room to spread out and an inspirational environment that lends itself for some innovative design and layout, a great opportunity to refresh and revitalise what the festival has been offering its fans.
The festival will however stay truthful to its promise to stimulate and inspire creativity, innovation and collaboration, and thus to contribute to developing the arts sector at large. “In terms of programming we will be very similar to what our audiences are used to – exciting multi-arts programming at various stages for people from all ages and strata – just in a different location with more breathing room,” underlines Faisal KIWEWA.


RAIS DKT JOHN MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABOLOZI SITA IKULU DSM

WAZIRI WA AFYA AKIRI CHANGAMOTO YA UHABA WA MADAKTARI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 

WAZIRI  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu  amesema kuwa kuna changamoto ya uhaba wa madaktari katika Hospitali ya Rufaa ya Amana jijini Dar es Salaam kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika kwa ajili ya kupata huduma katika hospitali hiyo.

Ametoa kauli hiyo leo wakati anamalizia ziara yake kwenye hospitali hiyo ambapo amesema pamoja na kuridhishwa na huduma ambazo madaktari wanazitoa kwa wagonjwa katika hospitali hiyo lakini bado kuna changamoto ya uhaba wa madaktari."Nimeridhishwa na huduma katika hospitali hii na nimpongeze Mganga Mfawidhi na uongozi  wa Wilaya  kwa kazi nzuri wanayoifanya licha ya kwamba bado tunafahamu kuna changamaoto katika sekta ya afya.

"Madaktari wa Amana kwa siku wanahudumia wagonjwa 800 , hivyo tunachangamoto ya uhaba wa madaktari na kwa kuwa kuna nafasi za ajira 52,000 zimetangazwa tunaamini sekta ya afya tutapewa mgao unaostaili ili tuwe na wataalamu wa masuala ya afya wa kutosha,"amesema Waziri Mwalimu.Mbali ya changamoto ya uhaba wa madaktari, Waziri Mwalimu ameendelea kuwasisitiza wagonjwa umuhimu wa kuwa na kadi za bima ya afya kwani humfanya anayekuwa nayo kuwa na uhakika wa kupata matibabu kwa gharama nafuu.

"Ifike wakati kila mwananchi awe na kadi ya bima ya afya kwani milango imefunguka na kilichobaki ni kuendelea kuona umuhimu wa kuwa nayo,"amesema Waziri Mwalimu.Wakati huohuo ametoa onyo kwa watumishi wote wa hospitali za Serikali ambao watabainika kujihusisha na tabia ya kuuza dawa ambazo zimetolewa na Bohari ya Dawa(MSD)ambazo zinatolewa bure waache mara moja.
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu  akizungumza na wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa ajili ya kupatiwa matibabu wakati alipofanya ziara ya kukagua hospitali hizo mara baada ya Rais Dk John Pombe Magufuli kuagiza Hospitali hizo zianze kusimamiwa na Wizara ya Afya.
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Amana, Dr Meshack Shimwela  akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu  akikagua Dawa zilizopo katika Bohari ya Dawa ya Hospitali ya Rufa aya Amana Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu  akizungumza na Madaktari ndani ya Wodi ya watoto katika Hospitali ya Amana.

YANGA ,MWADUI FC KUVAANA KESHO UWANJA WA UHURU, DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Agness Francis,Globu ya jamii 
 TIMU Soka ya Yanga inatarajia kushuka dimbani kesho kuvaana na timu ya Mwadui FC katika mchezo wa raundi ya 13 ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Vodavom Tanzania Bara. Mchezo huo utachezwa saa 10 jioni Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam maarufu kama Shamba la Bibi.
Katika mechi ya raundi ya 12 Yanga walipoteza mchezo wao dhidi ya Mbao FC uliochezwa jijini Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba Mabingwa hao watetezi watashuka dimbani huku wakimkosa mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka nchini Zambia Obrey Chirwa aliyefungiwa mechi tatu na Kamati ya Nidhamu ya TFF. 
Pia watamkosa mshambuliaji wao kutoka Zimbabwe Donard Ngoma ambaye bado hajawa fiti. Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Charles Boniphace Mkwasa amesema maandalizi ni mazuri na wanajua mchezo huo utakuwa mgumu. “Tumejipanga kupambana kuhakikisha tunashinda mchezo wetu wa kesho,” amesisitiza Mkwasa.


Mwadui FC
Yanga

TAARIFA TOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA

YANGA ,MWADUI FC KUVAANA KESHO UWANJA WA UHURU

$
0
0
Na Agness Francis-Globu ya jamii

TIMU Soka ya Yanga inatarajia kushuka dimbani kesho kuvaana na timu ya Mwadui Fc katika mchezo wa raundi ya 13 ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Vodavom Tanzania Bara. 

Mchezo huo utachezwa saa 10 jioni Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam maarufu la Shamba la Bibi.Katika mechi ya raundi ya 12 Yanga walipoteza mchezo wao dhidi ya Mbao FC uliochezwa jijini Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba 

Mabingwa hao watetezi watashuka dimbani huku wakimkosa mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka nchini Zambia Obrey Chirwa aliyefungiwa mechi tatu na Kamati ya Nidhamu ya TFF. Pia watamkosa mshambuliaji wao kutoka Zimbabwe Donard Ngoma ambaye bado hajawa fiti. 

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Boniphace Mkwasa amesema maandalizi ni mazuri na wanajua mchezo huo utakuwa mgumu.

“Tumejipanga kupambana kuhakikisha tunashinda mchezo wetu wa kesho,” amesisitiza Mkwasa.

KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE ZA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA NA KAMATI YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA( PIC) WAENDELEA NA VIKAO VYAKE LEO MJINI DODOMA.

$
0
0
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mheshimiwa Lolensia Bukwimba akizungumza katika kikao cha Kamati hiyo ambapo imekutana na uongozi wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  kwa ajili ya kujadili na kuchambua Taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu uwekezaji na utendaji wa Taasisi hiyo. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.
 Wajumbe wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiwa  katika kikao cha Kamati hiyo ambapo imekutana na uongozi wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  kwa ajili ya kujadili na kuchambua Taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu uwekezaji na utendaji wa Taasisi hiyo. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi  akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC)wakati Kamati ilipokutana na Taasisi hiyo  kwa ajili ya kujadili na kuchambua Taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu uwekezaji na utendaji wa Taasisi hiyo.kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya JKCI, Profesa William Mahalu. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo ambapo leo walikuwa wakijadili ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Shirikisho la wenye Viwanda Nchini (CTI).Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mheshimiwa Sadiq Murad akikisitiza jambo katika kikao cha Kamati hiyo ambapo leo walikuwa wakijadili ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Shirikisho la wenye Viwanda Nchini (CTI).Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma. PICHA NA OFISI YA BUNGE

POLISI KANDA MAALUM YAWAONYA WALIOPATA MSAMAHA WA RAIS

KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE ZA ZAENDELEA NA VIKAO VYAKE LEO MJINI DODOMA.

$
0
0
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mheshimiwa Lolensia Bukwimba akizungumza katika kikao cha Kamati hiyo ambapo imekutana na uongozi wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  kwa ajili ya kujadili na kuchambua Taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu uwekezaji na utendaji wa Taasisi hiyo. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.
 Wajumbe wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiwa  katika kikao cha Kamati hiyo ambapo imekutana na uongozi wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  kwa ajili ya kujadili na kuchambua Taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu uwekezaji na utendaji wa Taasisi hiyo. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi  akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC)wakati Kamati ilipokutana na Taasisi hiyo  kwa ajili ya kujadili na kuchambua Taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu uwekezaji na utendaji wa Taasisi hiyo.kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya JKCI, Profesa William Mahalu. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo ambapo leo walikuwa wakijadili ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Shirikisho la wenye Viwanda Nchini (CTI).Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Mheshimiwa Sadiq Murad akikisitiza jambo katika kikao cha Kamati hiyo ambapo leo walikuwa wakijadili ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Shirikisho la wenye Viwanda Nchini (CTI).Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

SUALA LA AUGUSTINO MREMA LAFIKA POLISI KANDA MAALUM

MICHUZI TV: YANGA YAMNYOOSHEA KIDOLE MZEE AKILIMALI, YASEMA ANAWARUDISHA MWAKA 1947

WAHUJUMU WA MIRADI YA MAJI MARA KUCHUKULIWA HATUA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itawachukulia hatua watendaji wote watakaobainika kuhujumu ujenzi wa miradi ya maji mkoani Mara.

Hatua hiyo imetokana na kutoridhishwa na utekelezwaji wa ujenzi miradi ya maji katika baadhi ya halmashauri za mkoa huo,hivyo kuwacheleweshea wananchi kupata huduma hiyo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Januari 16, 2018) wakati alipokagua mradi wa maji wa Utegi uliopo katika kijiji cha Mika wilayani Rorya.Amesema Serikali inatekeleza Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo. Kampeni hiyo inalenga kuwaondolea wananchi tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.

Waziri Mkuu amesema malengo ya kampeni hiyo ni kuwafikishia wananchi huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.“Nitafuatilia katika maeneo yote ili kujua kama kiasi cha fedha kilichotolewa kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maji kinalingana na thamani halisi ya miradi husika.”

Waziri Mkuu amesema anakerwa na Halmashauri ya wilaya ya Rorya kutosimamia vizuri miradi ya maji inayotekelezwa katika wilaya hiyo, ikiwa ni pamoja na kutozingatia sheria.Wakati huo huo Waziri Mkuu amewataka watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Rorya wanaoshi wilayani Tarime wawe wamehamie Rorya ifikapo Februari 15, 2018.

“Atakayeng’ang’ania kuishi Tarime hadi siku hiyo atakuwa amejiondoa kazini mwenyewe. Lazima watumishi wote waishi kwenye vituo vyao vya kazi Rorya ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.”

Pia Waziri Mkuu aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kutojihusisha na vitendo vya kihalifu ikiwemo ulimaji wa bangi pamoja na uvuvi haramu na badala yake wafanye shughuli halali za kuwaingizia vipato.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMANNE, JANUARI 16, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Nati Hassan mmoja wa wazazi waliojifungua wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya Kituo cha Afya cha Kinesi wilayani Rorya Januari 16, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kukagua Kituo cha Afya cha Kinesi wilayani Rorya Januari 16, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari ya Nyamungo wilayani Rorya, Juma Wilfred baada ya kuzungumza na wananchi wakati alipokagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kinesi Januari 16, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Kituo cha wilaya cha Kipolisi cha Kinesi wilayani Rorya, SSP Juma Wilfred Majula (wapili kushoto) wakati alipotembelea kituo hicho na kuvutiwa na juhudi ziizofanywa na Mkuu huyo wa Polisi za kujenga kituo hicho bila kusubiri fedha za serikali Januari 16, 201.. Waziri Mkuu aliendesha harambee ya papo kwa papo na kufanikiwa kupata shilingi milioni 20 za kumalizia jengo jipya la kituo hicho. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya Tarime na Rorya, David Mwaibambe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Utegi wilayani Rorya wakati alipolazimika kuasimama baada ya kuona umati mkubwa watu waliokuwa na shauku ya kumuona na kuksikiliza Januari 16, 2018.

SALAMU ZA PONGEZI KUTOKA KWA DKT. MWAKYEMBE


Rais wa Zanzibar Dk. Shein Azungumza na Wenyeviti wa Jumuiya za Chama cha Mapimduzi

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dkt. Mndolwa Bernad Edmund alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumza na kujitambulisha baada ya kuchaguliwa kuchukua nafasi hiyo kuiongoza kwa kipindi cha miaka mitano.(Picha Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzu Dk. Ali Mohamed akiwa na mgeni wake Mwnyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dkt. Mndolwa Bernad Edmund, akimshindikiza baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar alipofika kujitambulisha.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka, akitowa maelezo na kumtambulisha Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Kheri James walipofika kwa mazungumzo na kujitambulisha Ikulu Zanzibar leo.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kitaifa wa UVCCM, baada ya mazungumzo yao na kujitambulisha Ikulu Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania (UWT) Thuwaiba Editon Kisasi alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania, baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar walipofika kujitambulisha.(Picha Ikulu)  

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 17, 2018

BASHE AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA MAJI YA ZIWA VICTORIA

$
0
0
Mbunge wa Nzega Mjini, Mhe. Hussein Bashe mapema leo amekagua mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria katika jimbo la Nzega Mjini.

Mradi huu ni moja kati ya miradi mikubwa ya maji nchini huku ukitarajiwa kutumia zaidi ya Bilioni Mia Sita ambazo zilitiliwa saini baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya India mwezi Mei mwaka 2017.
Tayari mkandarasi ameanza ujenzi wa matanki makubwa ya maji na njia za kupitisha mabomba makubwa ambayo yataifanya Nzega Mjini kuwa kitovu kikuu cha Usambazaji wa Maji haya ya Ziwa Victoria.

Katika kuhakikisha mradi huu unanufaisha wananchi wote wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Bashe aliwasilisha maombi binafsi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe  Magufuli fedha kwa ajili ya kupanua mtandao wa Maji Nzega na tayari Rais amekwisha kutoa fedha hizo ili kuboresha upatikanaji wa Maji ya uhakika katika Mji wa Nzega ambao kwa miaka mingi umekua na kilio kikubwa.

Kwa upande mwingine Mhe. Bashe ametembelea eneo la Sagara ambapo kwa pamoja na Halmashauri ya Mji wa Nzega wamekusudia kujenga kisima kikubwa chenye uwezo wa kusambaza maji kwenye maeneo jirani. Upanuzi wa kisima hiki ni katika juhudi mahsusi za kuhakikisha hakuna tena tatizo la maji Nzega.

Aidha, kuhusiana na ajira zitakazotokana na mradi huu Mhe. Bashe amesema "Kipaumbele kwa ajira ambazo zitatokana na mradi huu watapewa watanzania ambao wanaoishi katika maeneo ambayo mradi unapita ili kuhakikisha mzunguko wa fedha na ajira zinakuwepo kwa vijana na wananchi ndani ya Mji wa Nzega"

ALICHOKIZUNGUMZA DKT. NDUGULILE BAADA YA KUWATEMBELEA WANAWAKE WAJASILIAMALI WA MANISPAA YA MBOZI MKOANI SONGWE

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Viewing all 110176 articles
Browse latest View live




Latest Images