Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

Masogange anendelea kukwamisha kesi yake

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

ANDE wa mashitaka katika kesi ya  kutumia dawa za kulevya inayomkabili Agnes Gerald maarufu kama ‘Masogange’ umeiomba Mahakama kuuonya  upande wa utetezi kwa kushindwa kutoa ushahidi  wao  kwa mara ya tatu mfululizo

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa utetezi, Nehemia Nkoko kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri kuwa Wakili mwenzake anayemtetea Mshtakiwa Msogange, Reuben Simwanza, ndiye aliyeandaa mashahidi lakini ameshindwa kufika kwa kuwa anaumwa.

Nkoko amongeza, atahakikisha anaandaa mashahidi ili ikitokea wakili mmoja wao hayupo, mwengine aendelee na kesi.Wakili wa Serikali,  Constantine Kakula alidai kuwa hawana pingamizi na sababu zilizotolewa na upande wa utetezi lakini wanaomba mahakama itambue kuwa ni mara ya tatu kesi kwa upande wa utetezi inaahirishwa.

"Mawakili wapo wengi lakini wanashindwa kuendelea kutoa ushahidi wao wa upande wa utetezi basi kama hawawezi, waache mshitakiwa aendelee na kesi mwenyewe," alidai Kakula.Pia aliiomba mahakama kutoa ahirisho la mwisho kwa sababu kesi ni ya muda mrefu. Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 26, mwaka huu  kwa ajili ya kusikilizwa.

Masogange ataanza kujitetea baada ya mahakama kumkuta na kesi ya kujibu baada ya kusikiliza mashahidi watatu wa upande wa mashitaka.

Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14, mwaka jana katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).

Pia anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14, 2017 alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.


WAZIRI KAMWELWE AZINDUA MIRADI YA SHILINGI BILIONI 2.76 MTWARA

$
0
0
Na Athumani Shariff- MoWI 

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe leo amezindua miradi miwili ya maji ambayo ipo Halmashauri za Wilaya ya Mtwara na Masasi Mkoani Mtwara ilyogharimu jumla ya shilingi bilioni 2,764,376,293.19 yote kwa pamoja.

Mradi wa maji wa Mayaya katika Halmashauri ya Mtwara uligharimu shilingi 973,022,925 una vituo 37 vya kuchotea maji na unanufaisha wananchi wapatao 4,997.

Katika Halmashauri ya Masasi Waziri Kamwelwe alizindua mradi wa maji wa Shaurimoyo– Mpindimbi wenye thamani ya shilingi 1,791,353,368.19 ambao utanufaisha wakati wapatao 8,400 washio katika vijiji vya Shaurimoyo, Kachepa, Mpindimbi na Kanyimbi.

Wakati wa uzinduzi wa Miradi hiyo, wananchi walishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutekeleza ahadi zake kwa vitendo kwani walikuwa na adha kubwa ya maji ambapo kabla ya mradi walikuwa wakinunua ndoo moja ya lita 20 kwa shilingi elfu moja na baada ya mradi wananunua ndoo moja kwa shilingi hamsini tu.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Lulindi Jerome Bwanausi amemshukuru Wazira wa Maji na Umwagiliaji na serikali ya awamu ya tano kwa kukamilisha ahadi zao, na ana furaha isiyo na kifani kwa kukamilika miradi hiyo ambayo imeondoa kero kubwa ya maji kwa wananchi.

Waziri Kamwelwe kesho ataendelea na ziara ya kikazi Mkoani Lindi ambapo atakagua mradi wa maji wa Ng’apa kisha ataelekea Wilayani Newala Mkoani Mtwara kwa ajili ya uzinduzi mradi wa maji wa Mapili uliojengwa kwa thamani ya shilingi 1,668,826,940.

Baada ya kukamilika kwa ziara hiyo Mhandisi Kamwelwe atarudi Dodoma alhamisi kuendelea na shughuli za bunge. 

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe leo amezindua miradi miwili ya maji ambayo ipo Halmashauri za Wilaya ya Mtwara na Masasi Mkoani Mtwara ilyogharimu jumla ya shilingi bilioni 2,764,376,293.19 yote kwa pamoja. 

WAZIRI MKUU AMKABIDHI MHANDISI WA MAJI KWA NAIBU WAZIRI TAMISEMI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemkabidhi Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya wilaya ya Rorya, Mhandisi Obetto Sasi kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. Josephat Kandege baada ya kutoridhishwa na utendaji wake.

Ametoa uamuzi huo jana jioni (Jumanne, Januari 16, 2018) wakati aliposimamishwa na umati wa wananchi kwenye mji Mdogo wa Shitari alipokuwa njiani kuelekea kwenye kijiji cha Bubombi wilayani Rorya.

“Hatuwezi kuwa na mtumishi wa aina hii ambaye kila eneo tunakutana na changamoto za maji huku kukiwa hakuna hatua zinazochukuliwa licha ya Serikali kutoa fedha, hivyo namuagiza Katibu Tawala wa Mkoa alete mhandisi mwingine wa maji.”

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo kwenda wilayani Rorya na kukagua mradi wa maji katika mji Mdogo wa Shirati na kuona namna ya kuutekeleza.
Amesema kwa sasa Serikali inatekeleza Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo. Kampeni hiyo  inalenga kuwaondolea wananchi tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, hivyo itawachukulia hatua wote watakaokwamisha miradi ya maji.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw. Adam Maliwa alimueleza Waziri Mkuu kwamba changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika mkoa huo inatokana na watendaji wa idara hiyo kutokuwa na uwezo wa kutosha kiutendaji.
Wilaya ya Rorya inatekeleza miradi 11 ya maji ya bomba kupitia Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP) katika vijiji vya Kinesi, Randa, Utegi, Mika,Kirogo, Nyihara, Kisumwa,Nyamkonge, Nyambori, Gabimori na Marasibora.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATANO, JANUARI 17, 2017.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ZANZIBAR ATILIANA SAINI NA BALOZI MDOGO WA CHINA XIE XIAO WU ZANZIBAR

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt,Khalid Salum Mohammed kushoto akitiliana saini na Balozi mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiao Wu kulia Msaada wa Fedha za Kitanzania  Shilingi  Bilioni 34.9 ambazo zitasaidia miradi mbalimbali ya Zanzibar hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga mjini Zanzibar.
 Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt,Khalid Salum Mohammed kushoto wakibadilishana hati na Balozi mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiao Wu kulia baada ya kutiliana saini Msaada wa Fedha za Kitanzania  Shilingi  Bilioni 34.9 ambazo zitasaidia miradi mbalimbali ya Zanzibar hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga mjini Zanzibar.
 Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt, Khalid Salum Mohammed kushoto wakipea na Mikono na Balozi mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiao Wu kulia baada ya kutiliana saini Msaada wa Fedha za Kitanzania  Shilingi  Bilioni 34.9 ambazo zitasaidia miradi mbalimbali ya Zanzibar hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga mjini Zanzibar.
 Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt, Khalid Salum Mohammed kulia akizungumza machache baada ya kutiliana saini na Balozi mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiao Wu Msaada wa Fedha za Kitanzania  Shilingi  Bilioni 34.9 ambazo zitasaidia miradi mbalimbali ya Zanzibar hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga mjini Zanzibar.
 aziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt,Khalid Salum Mohammed akisisitiza jambo alipozungumza machache baada ya kutiliana saini na Balozi mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiao Wu Msaada wa Fedha za Kitanzania  Shilingi  Bilioni 34.9 ambazo zitasaidia miradi mbalimbali ya Zanzibar hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga mjini Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt,Khalid Salum Mohammed wapili kulia akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mdogo alioko Zanzibar Xie Xiao Wu baada ya kutiliana saini Msaada wa Fedha za Kitanzania  Shilingi  Bilioni 34.9 ambazo zitasaidia miradi mbalimbali ya Zanzibar hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga mjini Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MAWAZIRI WA ELIMU NA TAMISEMI, APIGA MARUFUKU MICHANGO MASHULENI

$
0
0



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekutana na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani S. Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce L. Ndalichako Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 17, 2018. Mhe. Rais amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za serikali za msingi na sekondari na amewaagiza mawaziri hao kusimamia hilo. Taarifa kamili inakuja.Picha na IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifafanua jambo kwa msisitizo  mara baada ya kukutana na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani S. Jafo (kushoto) na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce L. Ndalichako (kulia) Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 17, 2018. Mhe. Rais amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za serikali za msingi na sekondari na amewaagiza mawaziri hao kusimamia hilo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukutana na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani S. Jafo (kushoto) na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce L. Ndalichako (kulia) Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 17, 2018. Mhe. Rais amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za serikali za msingi na sekondari na amewaagiza mawaziri hao kusimamia hilo. .Picha na IKULU 

WATOTO YATIMA 150 WAPATIWA MSADA WA VIFAA VYA SHULE

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye nguo ya njano), Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Gairo, Mhe. Andrea Sendeha (wa tatu toka kulia) pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Bethel wa Gairo.

 Katika kujali makundi yenye changamoto za maisha hasa watoto wadogo, Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe amegawa sare za shule na madaftari kwa watoto yatima 150 kituo cha Bethel Wilayani Gairo kinachosimamiwa na Mchungaji Chacha. Hafla hiyo ya ugawaji wa vifaa ulifanyika mapema wiki hii, ambapo Mhe. 

Mchembe amesema kuwa huo ni utamaduni aliojiwekea kila mwanzo wa mwaka wa kuwakumbuka watoto yatima na wale waishi katika mazingira magumu. "Nawakumbusha wananchi kujenga utamaduni wa kusaidiana watu wasiojiweza ili muweze kupata baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu, unajua unapokuwa nacho ukatoa kidogo unabarikiwa zaidi," alisema Mhe. Mchembe. 

Mhe. Mchembe aliwakumbusha watoto hao kuzingatia masomo kwani Serikali ya awamu ya tano ya Dr. John Magufuli inatoa elimu bure hivyo hakuna mtoto wa masikini atakayeshindwa kusoma. Katika kukua kwao wamtangulize Mungu naye ataendelea kuwabariki na kuwatoa katika hali ya kuhisi unyonge wa kukosa wazazi. Mwisho aliwaasa waalimu kuwa na moyo wa upendo kwa watoto yatima. Pia kuweka karibu hasa watoto wa kike kuwaepusha na mimba za utotoni.
 Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akiwaasa watoto yatima wa kituo cha Bethel Wilayani Gairo. Kulia kwake ni baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama walioambatana naye.  Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Gairo, Mhe. Andrea Sendeha akitoa salamu kwa watoto yatima. 

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akigawa zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha Bethel kilichopo wilayani humo. 
Watoto wa kituo cha Bethel Wilayani Gairo wakiwa wamejipanga mstari kupokea zawadi. 

WCF YAWANOA WAAMUZI, WASULUHISHI NA MAKATIBU MUHTASI KUTOKA TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI (CMA)

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), umejipanga vema kuendelea kutoa huduma bora kwa wadau, hususan katika kipindi hiki ambacho Mfuko unategemea ongezeko kubwa la waajiri na wafanyakazi, kutokana na mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kujenga uchumi wa viwanda, ambao utaongeza ajira.

Hayo yamesemwa leo Januari 17, 2018 mjini Morogoro na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa Waamuzi, Wasuluhishi na Makatibu Muhtasi kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), ili kuongeza ujuzi kwenye utekelezaji wa majukumu ya Tume.

“Katika jambo hili la kujenga uchumi wa viwanda,  makampuni mengi yataanzishwa, kutakuwa na waajiri wengi, ongezeko la wafanyakazi, kwa hivyo unategemea kwamba hitajio la utoaji huduma za Mfuko kwa wadau  litaongezeka na Mfuko umekuja wakati muafaka na tupo kwa ajili ya kuwahudumia wale wote watakaopatwa na majanga mahala pa kazi lakini pia kuelimisha.” Alisema Bw. Mshomba.

Bw. Mshomba  alisema, kuanzia Julai, 2016 Mfuko ulianza kupokea madai ya Fidia yanayotokana na kuumia au kuugua mahali pa kazi.

 Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, (kushboto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, (wkawanza kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw.Shanes Nungu, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa Waamuzi, Wasuluhishi na Makatibu Muhtasi kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) mjini Morogoro leo Januari 17, 2018. Bw. Kalonga alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Eric Shitindi.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga,kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Eric Shitindi, akifungua mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba yake.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR ATEMBELEA MAONESHO YA BIASHARA MAISARA MJINI UNGUJA.

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi kulia akipata maelezo kutoka kwa Afisa uhusiano wa Taasisi ya Viwango Zanzibar Aisha Abdulkheir Mohammed wakati alipotembelea Banda hilo katika maonesho ya Biashara Maisara Mjini Unguja.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akiangalia Bidhaa za Vipodozi na kupatiwa maelezo kuhusu matumizi yake na Bitatu Suleiman baada ya kutembelea Banda hilo katika maonesho ya Biashara Maisara Mjini Unguja.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akipatiwa bidhaa ya Sabuni zinazotengenezwa na Mjasiria mali wa Zaidat Product Bi Tatu Suleiman baada ya kutembelea Banda hilo katika maonesho ya Biashara Maisara Mjini Unguja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akiwa amefuatana na Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali baada ya  kutembelea sehemu mbalimbali katika maonesho ya Biashara Maisara Mjini Unguja.
PICHA NA YUSSUF SIAMI/MAELEZO ZANZIBAR.

KATIBU UVCCM IRINGA MJINI ANUSURIKA KUFA BAADA KITU CHENYE MLIPUKO KURUSHWA KITANDANI KWAKE

$
0
0
Aelezea hatua kwa hatua namna nyumba yote ilivyoteketea kwa moto.

Na Said Mwishehe-Globu

KATIBU wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM), Alophance Myunga amenusurika kifo baada ya kitu chenye mlipuko kurushwa dirishani kwake na kufikia kitandani huku yeye akiwa amelela na kisha kusababisha moto ulioteketeza nyumba anayoishi yote.
Amesema kutokana na kurushwa kwa kitu hicho ambacho kilisababisha mlipuko mkubwa chumbani kwake na kisha moto kuanza kuwaka alichofanikiwa ni kuchukua simu yake ya mkononi tu huku vitu vingine vyote vikiteketea kwa moto.
Akizungumza na Michuzi Blogu kwa njia ya simu leo , Myunga amesema yeye ni moja kati ya wapangaji saba wanaoishi kwenye nyumba ambayo wanaishi na chumba ambacho kilianza kuwaka moto ni cha kwake.


ASIMULIA MOTO ULIVYOANZA CHUMBANI KWAKE
Katibu huyo wa UVCCM Wilaya ya Iringa amesema kuwa kwenye mida ya saa saba usiku akiwa amelala chumbani kwake alisikia dirisha lililopo chumbani kwake likivunjwa.Hata hivyo aliogopa kuchungulia kwani hakujua wanaofanya hivy wanalengo gani dhidi yake.

Ameongeza wakati anaendelea kutafakari huku akiwa bado yupo kwenye itanda chake alishangaa kuona amerushiwa kitu ambacho hawezi kukielezea ni cha aina gani lakini ghafla kikaangukia chini na kusababisha kulipuka na moto kuanza kuwaka.

"Naogopa kusema ni kitu aina ya bomu au laa.Maana si mtaalamu wa kutambua aina ya kitu ambacho kimerushwa chumbani.Niseme tu baada ya kitu hicho kurushwa kitandani na kudondokea chini, moto ukaanza kufuka na kisha kulipuka.Nilichofanikiwa ni kuchukua simu na Kompyuta mpakato na kisha kukimbilia nje.

"Nilipotoka nje na wapangaji wenzangu nao wakatoka na kuanza kuulizana nani amefanya tukio hilo.Tayari tumetoa taarifa Polisi jana usiku baada ya nyumba kuungua na hivyo tunasubiri watakachobaini kilichosababisha nyumba kuchomwa na waliohusika kufanya tukio hilo,"amesema.

ANAHISI NINI BAADA YA TUKIO HILO?
Kuhusu swali hilo, amejibu kuwa anachoamini sababu kubwa itakuwa ni mambo ya siasa kwani yeye si mfanyabashara na hana kazi nyingine zaidi ya siasa na siku za karibuni kuna moja ya kiongozi wa kisiasa wa upande wa upinzani alimtishia kwa bastola.

"Mbali ya kunitisha kwa bastola aliniambia kuwa nitakiona na lazima atanihamisha Iringa kwani najifanya mjanja kwa kuwa nimetoa Dar es salaam.Huyu kiongozi(jina tunalo) ndio atakuwa adui yangu namba moja na ndio namhisi atakuwa kafanya tukio hilo.

"Inaonesha kabisa walikuwa wamedhamiria kuniuua mimi na ndio maana walvunja dirisha la chumbani kwangu na kurusha kitu hicho ambacho kilisaabisha mlipuko uliofanya moto kuanza kuwaka.Hata hivyo acha Jeshi la Polisi Iringa nalo lifanye kazi yake ya kuchunguza na ukweli utapatikana,"amesema.
 Baadhi ya vitu vilivyoteketea kufuatia mlipuko huo.
 Hivi ndivyo huo mlipuko ulivyoteketeza vitu hivyo
 
Baadhi ya ndugu jamaa na majirani wakishuhudia tukio hilo

MICHANGO SHULE ZA SERIKALI KUONDOKA NA MLOLONGO WA VIONGOZI

$
0
0

*Rais Dkt.Magufuli apiga marufuku, asema asisikie mchango wa aina yoyote shuleni

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Rais Dkt.John Magufuli kusema ni marufuku watoto walioko shuleni kuchangishwa mchango wa aina yoyote na akisikia kuna shule katika wilaya fulani ambayo watoto wanafukuzwa kwa kutochangia basi huyo Mkurugenzi ajihesabu hana kazi.

Ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kukutana na Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Sulemani Jaffo na Waziri wa Elimu ,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako ambapo ameagiza mawaziri hao ambao wanahusika na elimu kusimamia hilo na ni kuanzia leo.

"Kwa taarifa hii mkawaeleze wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi nikisikia kuna shule katika wilaya fulani ambapo watoto wanarudishwa kwa sababu ya kukosa michango, Mkurugenzi wa wilaya hiyo ajue hana kazi.Na haya maagizo yanaanza leo.Nimemueleza Waziri na Waziri mwenzake kusimamia hili,maofisa elimu wote nao wasimamie hili kwani wanalipwa kwa ajili hiyo,"amesema.

Rais,Dk.Magufuli amesema haiwezekani kutoa elimu bure halafu kero zikawa zinaongezeka na anatambua idadi ya wanafunzi imeongezeka lakini hiyo changamoto inatakiwa kubebwa na Serikali na kwamba hicho kisiwe kisingizio."Haiwezani tutoe elimu bure halafu kero zinaongezeka,"amesema.

Amesema sasa hivi watoto wanaacha kwenda shule kwa sababu michango inayotolewa tolewa, hivyo mawaziri hao wasimamie hilo na asisikie watoto wanarudishwa kwa sababu ya michango.

Dkt.Magufuli amesema hataki kusikia mahali popote wananchi wanalalamikia michango huku akitumia nafasi hiyo kuwawaambia walimu ni marufuku kushika mchango wowote.

"Ni marufuku mwanafunzi kurudishwa kwasababu ya kukosa mchango wa maabara,ni marufuku mwanafunzi kurudishwa kwasababu ya mchango wa madawati.Ni marufuku kuchangisha mchango wowote.Kama kuna anayetaka kuchangia iwe kwa hiyari yake anapeleke kwa Mkurugenzi.

"Nikisikia wanafunzi wanachangishwa kwasababu ya michango kuanzia mkuu wa mkoa , mku wa wilaya na mkureugenzi wa eneo husika wote wataondoka,"amesema Rais Dkt.John Magufuli

DK.MABODI AIPONGEZA SMZ

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar kimesema mafanikio yliyofikiwa na Serikali ya awamu ya Saba chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ni kielelezo tosha cha kuenzi kwa vitendo Mapinduzi hayo ya Januari 12, mwaka 1964.

Udhibitisho huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Saadalla ‘Mabodi’ wakati akitoa tathimini yake juu ya hotuba ya Rais wa Zanzibar Dk.Shein aliyoitoa katika kilele cha wamaadhimisho ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi zilizofanyika Uwanja wa Amaan Mjini hapa.

Dk. Mabodi alisema mambo yaliyotajwa katika hotuba hiyo ni sehemu ya mafanikio ambayo kila mwananchi anatakiwa kujivunia kwani ni hatua ya maendeleo yanayotokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi CCM ya mwaka 2015/2020 kwa wananchi wote.

Alisema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetekeleza mambo mbali mbali ya kimaendeleo bila kujali changamoto na vikwazo vya kisiasa kwa lengo la kurahisisha upatanaji wa huduma za msingi kwa wananchi waliopo mijini na vijijini.

Alieleza kuwa mambo yaliyotolewa ufafanuzi wa kina ndani ya hotuba hiyo ya Dk.Shein ni pamoja na kuimarika kwa sekta ya uchumi ambapo makusanyo ya mapato yamefikia shilingi bilioni 548.571 kwa mwaka 2017 ikilinganishwa na shilingi bilioni 487.474 zilizokusanywa katika mwaka 2016.

Mahakama kwenda Kidijitali

$
0
0
Na Mary Gwera, Mahakama

Mahakama ya Tanzania imedhamiria kufanya malipo yote ya huduma zake na ukusanyaji wa mapato kielektroniki ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia na vilevile kuboresha huduma kwa manufaa ya wananchi.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Msaidizi, Mipango na Bajeti-Mahakama ya Tanzania, Bw. Erasmus Uisso Januari 16, alipokuwa akifungua mafunzo ya Siku tano ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali ‘Government Electronic Gateway (GEPG) yanayofanyika katika Ukumbi mpya ya Mikutano uliopo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi-Kisutu jijini Dar es Salaam.

“Mahakama kama ilivyo kwa Taasisi nyingine za Serikali imejiunga katika Mfumo huu ili kufanya ukusanyaji wa Mapato na malipo yote ya Huduma za Mahakama kufanywa kwa njia ya Kieletroniki, kwa hiyo ili kuwezesha matumizi ya mfumo huu yameandaliwa mafunzo haya maalum kwa Watumiaji katika ngazi mbalimbali za Mahakama kuwapa ujuzi wa kuwawezesha kufanya kazi hii,” alifafanua Bw. Uisso.

Alitaja kuwa kwa kuanzia mafunzo hayo ya awamu ya kwanza yameshirikisha jumla ya Watumishi 35 wa Mahakama kwa Mkoa wa Dar es Salaam, akitaja watumishi hao kuwa ni pamoja na Wahasibu, Maafisa TEHAMA, Makarani kutoka Makao Makuu na ngazi zote za Mahakama kwa mkoa huu.

“Tunatarajia kuendelea kutoa elimu hiyo katika mikoa mingine kwa awamu, ili kuiwezesha Mahakama nchi nzima kutumia mfumo huu,” aliongeza Bw. Uisso.

 Afisa TEHAMA kutoka Wizara ya Fedha na Mipango-Kitengo cha Usimamizi wa Mifumo ya Fedha, Bi. Penina Henjewele akitoa Mada ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali ‘Government Electronic Gateway (GEPG) kwa Washiriki wa Mafunzo hayo (hawapo pichani) 
 Mkurugenzi Msaidizi, Mipango na Bajeti-Mahakama ya Tanzania, Bw. Erasmus Uisso akiongea jambo na Washiriki katika mafunzo ya Siku tano ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali ‘Government Electronic Gateway (GEPG) yanayofanyika katika Ukumbi mpya ya Mikutano uliopo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi-Kisutu jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Sehemu ya Wahasibu na Makarani wa Mahakama wakiwa katika mafunzo ya Siku tano ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali ‘Government Electronic Gateway (GEPG) yanayofanyika katika Ukumbi mpya ya Mikutano uliopo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi-Kisutu jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

FINLAND YAONESHA NIA KUWEKEZA SEKTA YA NISHATI NCHINI

$
0
0
Na Veronica Simba – Dodoma.

Ujumbe kutoka Kampuni ya Fortum ya Finland umemtembelea Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na kueleza nia yao kuwekeza kwenye sekta ya nishati nchini.Ujumbe huo ukiongozwa na Balozi wa Finland nchini Tanzania, Pekka Hukka, ulimtembelea Waziri ofisini kwake mjini Dodoma, Januari 16 mwaka huu.

Akiwatambulisha maafisa aliombatana nao, Balozi Hukka alisema ni wawakilishi kutoka Kampuni ya Fortum inayotoa huduma za nishati ya umeme nchini Finland, ambayo hisa zake nyingi zinamilikiwa na Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi yenye hisa chache.

“Tunatambua umuhimu wa sekta ya nishati katika kuleta maendeleo hususan katika kuwezesha uchumi wa viwanda, ndiyo maana tungependa kuwekeza katika sekta hii,” alisema Balozi Hukka.

Kwa upande wake, Waziri Kalemani aliueleza Ujumbe huo kuwa Serikali ingali inahitaji wawekezaji makini katika sekta ya nishati hususan katika uzalishaji na usambazaji wa umeme.“Kiasi cha umeme tulichonacho kwa sasa kinaweza kuonekana kutosheleza mahitaji yetu lakini tunajipanga kuzalisha umeme zaidi kwani mahitaji yanazidi kuongezeka siku hadi siku.”

Waziri aliongeza kufafanua kuwa, umeme mwingi zaidi unahitajika hususan kipindi hiki ambapo Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha nchi inaingia kwenye uchumi wa viwanda.Aliwataka wawekezaji hao kukutana na wataalam kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ili kujadiliana na kuainisha maeneo mahsusi yanayohitaji uwekezaji.

Hata hivyo, Waziri aliainisha baadhi ya maeneo muhimu ya sekta ya nishati ambayo yanahitaji uwekezaji kwa sasa ambayo alisema ni pamoja na njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 400 kutoka SomangaFungu hadi Dar es Salaam.Nyingine ni uzalishaji wa umeme kwa kutumia makaa ya mawe. “Tunayo hazina ya kutosha ya makaa ya mawe huko Magharibi mwa nchi yetu. Hii pia ni fursa nyingine nzuri ya uwekezaji,” alisisitiza.

Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeendelea kuweka mikakati madhubuti inayolenga kuongeza uzalishaji wa umeme na usambazaji katika maeneo yote nchini.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Finland nchini Tanzania, Pekka Hukka (kulia) aliyeongoza Ujumbe wa wawekezaji kutoka Kampuni ya Fortum wakati wa kikao baina yao Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Januari 16 mwaka huu. Kampuni hiyo imeonesha nia kuwekeza kwenye sekta ya nishati nchini.
 Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga na Meneja wa Uendelezaji Biashara kutoka Kampuni ya FORTUM ya Finland, Steve Hawes wakijadiliana jambo mara baada ya kikao baina ya Kampuni hiyo na Waziri wa Nishati, kilichofanyika  Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma hivi karibuni.


Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akimsikiliza Balozi wa Finland nchini Tanzania, Pekka Hukka na Ujumbe Ujumbe wa wawekezaji kutoka Kampuni ya Fortum (kushoto) wakati wa kikao baina yao Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Januari 16 mwaka huu. Kampuni hiyo imeonesha nia kuwekeza kwenye sekta ya nishati nchini. Kulia ni baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Nishati na TANESCO.

MAKAMU WA RAIS AKAGUA UJENZI UKUTA BAHARI YA HINDI DAR

$
0
0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa ukuta wa bahari Kigamboni wenye urefu wa mita 500. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Meneja wa Mradi na Miundo Mbinu wa UNOPS Bw. Bernard Odhuno wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa ukuta wa bahari Kigamboni wenye urefu wa mita 500. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameketi kwenye moja ya sehemu za kupumzikia pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba(kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa ukuta wa bahari Kigamboni wenye urefu wa mita 500. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Waziri nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifafanua jambo mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa ukuta wa bahari Ocean Road. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Ujenzi wa Ukuta wa bahari katika eneo la umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WANAOOMBA UFADHILI WA MASOMO CHINA, JAPAN WATAHADHARISHWA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MKURUGENZI Mtendaji wa Elimu Solutions (T) Limited Neithan Suedy amesema ni vema Watanzania hasa wanafunzi nchini kuwa makini na matapeli wanaochukua fedha za wanafunzi kwa kigezo cha kuwatafutia vyuo vikuu nje ya nchi. 

Amesema wanaungana na Balozi wa Tanzania nchini China kuonya tabia ya baadhi ya mawakala kuchukua fedha za wanafunzi na kisha kushindwa kuwapeleka Kwenye vyuo ambavyo wanaahidi kuwapeleka au kuwapeleka na kusababisha wanafunzi wakifika huko kukosa malazi na makazi. 

Akizungumza Dar es Salaam leo, Sissy amesema wenye tabia hiyo wanasababisha matatizo kwa wanafunzi na wanaokwenda huko nchini China wanasababisha mzigo kwa vyuo husika.

"Wanafunzi wanatapeliwa sana na watu hao ambao wanajiita mawakala wa kutafutia ufadhili wanafunzi wa Tanzania kwa vyuo vikuu vya nchini China. 

"Ni vema Serikali yetu ikasaidia kudhibiti utapeli huu ambao unafanywa kwa wanafunzi wanaotaka kusoma nchini China, "amesema Suedy. 

Akizungumzia kwa upande wao amesema wamekuwa wakitafuta ufadhili kwa wanafunzi wanaohitaji kujiendeleza kielimu nchini China na wanachozingatia wao ni kufuata taratibu ambazo zinatambulika kisheria.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu Solutions Tanzania Ltd, Neithan Swedy akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa zoezi la kutuma maombi ya udahili wa masomo kwa wanafunzi wa nje ya nchi (China, Japan na Korea Kusini) pamoja na taratibu mbalimbali zinazopaswa kuzingatiwa na waombaji. Kushoto ni Afisa Tawala wa Taasisi hiyo, Irene Kigwangwa  leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu Solutions Ltd, Neithan Swedy akionyesha kwa waandishi wa habari nyaraka ya Namba ya Utambulisho Mlipa Kodi (TIN) inayotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) na kupaswa kuwa nayo kila kampuni ya uwakala wa utafutaji wa nafasi za masomo katika vyuo vya nchi za nje ya Tanzania. Wengine ni Afisa Tawala Irene Kigwanga na Meneja mwendeshaji wa Elimu Solutions, Ibrahim Swedy leo Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KAMATI YA RAIS KUCHUNGUZA TANZANITE YAANZA MAZUNGUMZO NA TANZANITE ONE

$
0
0
Kamati iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuchunguza biashara ya madini ya Tanzanite imeanza kufanya mazungumzo na kampuni ya Tanzanite One.

Kwa mujibu wa taarifa ya Bw. Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amesema mazungumzo hayo yaliyoanza tarehe 16 Januari, 2018 yanalenga kuhakikisha Tanzania inanufaika ipasavyo na rasilimali ya madini hayo ambayo yanachimbwa nchini Tanzania pekee.

"Prof. Kabudi amesema mazungumzo yameanza vizuri ambapo pande hizo mbili zinapitia matatizo yote yanayohusu biashara ya madini ya Tanzanite, utekelezaji wa sheria na kanuni mbalimbali za madini na mapato ya rasilimali hiyo, ili hatimaye zikubaliane namna bora itakayohakikisha Tanzania inanufaika ipasavyo" imesema taarifa hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanzanite One Bw. Faisal Juma Shahbhai amesema Tanzanite One ipo tayari kwa majadiliano hayo na inaunga mkono juhudi za kuhakikisha madini hayo yanainufaisha Tanzania tofauti na ilivyo sasa ambapo yanazinufaisha zaidi nchi nyingine ambazo hazizalishi Tanzanite.

Bw. Shahbhai ameongeza kuwa Tanzanite One itatoa taarifa zote zinazohitajika na wakati wote itatoa ushirikiano wenye lengo la kufanikisha mazungumzo hayo. 
Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuchunguza biashara ya madini ya Tanzanite ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi   akisalimiana  jijini Dar es salaam leo Januari 17, 2018   na wawakilishi wa kampuni ya Tanzanite One kabla ya kuanza na mazungumzo ambayo yanalenga kuhakikisha Tanzania inanufaika ipasavyo na rasilimali ya madini hayo ambayo yanachimbwa nchini Tanzania pekee. 
Picha na IKULU

UCHAGUZI WA BFT KUFANYIKA TAREHE 24 MWEZI FEBRUARI MWAKA HUUA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BARAZA la Michezo la Taifa  (BMT) limetangaza uchaguzi wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 mwezi februari mwaka huu.

Akizungumzia kuanza kwa uchukuaji wa fomu hizo leo Jumatano Januari 17, Afisa habari wa BMT, Najaha Bakari amesema kuwa uchaguzi huo utafanyika Mkoani Dodoma na mwisho wa kuchukua fomu utakuwa ni Februari 15.

Najaha amesema kuwa, nafasi zinazogombaniwa ni nafasi ya rais,makamu wa rais, katibu mkuu, Mweka hazina na Wajumbe 9 watakaochaguliwa katika uchaguzi mkuu.

"Uchaguzi utakuwa ni katika nafasi za rais,makamu wa rais, katibu mkuu,mweka hazina na wajumbe 9 watakaochaguliwa kwenye uchaguzi mkuu ambapo kabla ya kuingia katika uchaguzi watapita kwenye usajili,"amesema Najaha. 

Najaha ametaja vigezo vya wagombea hao katika nafasi mbalimbali ni kuwa mgombea haruhusiwi kugombea nafasi yoyote kama yeye ni mchezaji wa mchezo huo, mgombea awe na umri usiopungua miaka 25, asiwe ametenda kosa lolote la jinai, elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea.

Kwenye nafasi ya mweka hazina mgombea lazima awe na cheti cha uhasibu pia wajumbe wanaogombea nafasi hiyo lazima wawe na uzoefu na ngumi za ridhaa.
Kwa upande wa Rais wa Shirikisho la Ngumi BFT Mwita Rwakatare amesema kuwa ana imani uchaguzi huo utakaofanyika Februari 24 utakuwa wa amani pia amewasihi wadau wa mchezo wa ngumi kujitokeza kwa wingi kuja kuchukua fomu zitakazokuwa zinapatikana ofisi za BMT na BFT huku wagombea wote watachukua fomu na kulipia kupitia akaunti ya benki ya BMT.
Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) Mwita Rwakatare akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu uchaguzi wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu Mkoani Dodoma.
 Afisa wa Habari wa Baraza la Michezo la Taifa ( BMT) Najaha Bakari akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya JKCI wakifanya upasuaji kwa wagonjwa

$
0
0
  Madaktari  Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia mgonjwa ambaye mshipa mkubwa unaosambaza damu upande wa kushoto  wa moyo umeziba upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting). 
 Madaktari  Bingwa wa Usingizi na wagonjwa mahututi  wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiangalia jinsi moyo wa mgonjwa unavyofanya kazi (mapigo ya moyo)  kwa kutumia mashine maalum wakati mgonjwa huyo akifanyiwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting).

Madaktari  Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto Godwin Sharau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Benjamin Bierbach wa nchini Ujerumani wakimfanyia upasuaji wa kuziba matundu ya moyo mtoto mwenye  umri wa mwaka mmoja na mwezi mmoja. 

TAASISI YA ELIMU SOLUTIONS TANZANIA LTD YAMWAGA FURSA ZA MASOMO KWA WAFANYAKAZI NA WAJASIRIAMALI CHINA

KIPINDI MAALUM CHA RAIS DKT. ... N MAGUFULI KUHUSU ELIMU BURE

Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images