Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 16, 2018


ATAKAYEBAINIKA KUTAFUNA SH. MILIONI 320 ZA IMARA SACCOS ACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA-MAJALIWA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Musoma Bibi Yunia Wiga kufuatilia upotevu wa sh. milioni 320 za Imara SACCOS na atakayebainika kuhusika ashughulikiwe.

Alitoa kauli hiyo jana jioni (Jumatatu, Januari 15, 2018) alipopokea malalamiko ya wanachama wa SACCOS hiyo kupitia mabango waliyoyawasilisha katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mukendo mjini Musoma.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Mara kwa ziara ya kikazi ya siku sita, alimuagiza ofisa huyo kukutana na uongozi na wanachama wa SACCOS hiyo leo mchana na kisha kumpa majibu juu ya upotevu wa fedha hizo pamoja na sh. milioni 40 za hisa ifikapo Januari 20, 2018.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma Bibi Fidelica Myovella kuhakikisha anatenga fedha kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi mbalimbali waliopisha miradi ya maendeo katika Manispaa hiyo.

Waziri Mkuu alisema siyo vizuri kwa halmashauri kuchukua maeneo ya wananchi kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo kama barabara, standi na kisha kukaa muda mrefu bila ya kuwalipa fidia zao.

Aliyasema hayo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi waliopisha ujenzi wa kituo cha daladala cha Bweri ambao hawajalipwa fidia zao tangu mwaka 2013. Mkurugenzi huyo aliahidi kuanza kulipa madeni hayo kuanzia mwezi Januari, 2018.

Awali, Mbunge wa jimbo la Musoma Mjini, Bw Vedastus Mathayo aliishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kutekeleza baadhi ya ahadi alizozitoa wakati wa kampeni ikiwemo ya upatikanaji wa maji safi na salama.

Bw. Mathayo alisema wananchi wa jimbo hilo kwa muda mrefu walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, hivyo alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa utekelezaji wa ahadi hiyo.

Mbali na mradi wa maji pia Serikali inatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo ikiwemo ya ujenzi wa barabara za mitaa kwa kiwango cha lami pamoja na ukarabati wa kiwanja cha ndege unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Waziri Mkuu alisema ahadi zote zilizopo kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 na zile zilizotolewa na Rais Dkt. Magufuli zitatekelezwa, hivyo wananchi waendelee kuwa na imani na Serikali yao.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMANNE, JANUARI 16, 2017.

TIMU YA USIMAMIZI WA HUDUMA YA AFYA WILAYA YA LINDI YAAGIZWA KUSIMAMIA UKARABATI WA VITUO VYA AFYA

$
0
0

Angela Msimbira- OR-TAMISEMI LINDI.

Mganga Mkuu wa Mkoa  wa Lindi Bw. Ganchwele Makenge ameiagiza timu ya usimamizi wa huduma ya afya Wilaya ya Lindi kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia  ukarabati wa vituo vya afya ili vijengwe kwa ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.

Ameyasema hayo kwenye kikao cha pamoja kati ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushiriana na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri ya Lindi mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya  cha  Nyangamara kilichopo kata ya Nyangamara, Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi.

Bw. Makenge amesema Kamati ya Usimamizi wa Huduma ya Afya inalojukumu kubwa la kusimamia shughuli zote za afya katika Mkoa wa Lindi hivyo hawana budi kuhakikisha Miradi inayotekelezwa na Serikali inasimamiwa kikamilifu ikiwepo Ya ukarabati wa vituo vya afya nchini.

Amesema kuwa Kamati hiyo inahitajika kusimamia wahudumu wa afya katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa kufuata kanuni taratibu na sheria za utumishi wa umma kwa kuwahudumia wananchi ipasavyo na kuondoa malalamiko yaliyopo  katika sekta ya afya.

Ameiagiza kamati hiyo kusimamia utendaji bora katika vituo vya afya vya Mkoa wa Lindi kwa kuwahimiza wafanyakazi kutumia lugha nzuri kwa wagonjwa na kutoa huduma stahiki kwa jamii ili kuondoa kero mbalimbali ambazo wananchi wamekuwa wakizituhumu katika sekta ya afya nchini.
  Baadhi ya Wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) pamoja na wataalam kutoka Mkoa wa Lindi wakikagua Ujenzi wa jengo la maabara lililojengwa katika  kituo cha afya cha Nyangamara Mkoani Lindi.
Mwonekano wa Nyumba ya Mtumishi iliyojengwa katika kituo cha afya cha Nyangamara kilichopo katika Kata ya Nyamara, wilaya ya Lindi Mkoa wa Lindi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WANANCHI WA MBAMBA BAY WATAKA BARABARA YA LAMI

$
0
0
Wananchi wa Mbamba Bay wilayani Nyasa, mkoani Ruvuma wameiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay (km 67), kwa kiwango cha lami ili kutatua changamoto za usafirishaji wa abiria na mizigo wanazozipata hususan katika kipindi cha masika.

Wananchi hao wametoa kero hiyo mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, alipofika wilayani hapo kukagua barabara hiyo ambapo wamefafanua kuwa licha ya wilaya hiyo kuwa na maliasili nyingi, wawekezaji na wafanyabiashara hushindwa kufika kutokana na changamoto ya barabara, hivyo kupelekea uchelewaji wa maendeleo katika wilaya yao.

"Uduni wa barabara hii unapelekea kutopata maendeleo ya haraka, pia usafiri kutoka hapa kwenda maeneo mengine ya jirani huwa mgumu hususan katika kipindi cha mvua kwani madereva wengi hupandisha nauli", amesema mmoja wa wakazi wa Mbamba Bay, Bw. Bahati Ndege.

Aidha, wananchi hao wameipongeza Serikali kwa hatua zinazofanya katika utatuzi wa kero mbalimbali zinazowakabili, hivyo wamefafanua kuwa Serikali kuamua kujenga barabara ya lami kutaboresha uchumi katika wilaya yao na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (mbele), akishuka ngazi wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa unaojengwa na Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Ruvuma na kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo.
Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Edwin Nunduma, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (hayupo pichani), kuhusu hatua na changamoto wanazozipata katika miradi ya ujenzi wa jengo la ofisi na nyumba ya makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani humo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kukagua miradi ya ujenzi wa jengo la ofisi na nyumba ya makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma. Miradi hiyo inajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Muonekano wa hatua ya awali ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma. Mradi huo unajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (katikati) akizungumza na Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Ruvuma, Eng. Lazeck Alinanuswe (kulia), wakati akikagua barabara ya Mbinga-Mbamba Bay yenye urefu wa KM 67 inayotarajiwa kujengwa hivi karibuni kwa kiwango cha lami na mkandarasi CHICO. 
 Muonekano wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay yenye urefu wa KM 67 inayotarajiwa kujengwa hivi karibuni kwa kiwango cha lami na mkandarasi CHICO. Mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo ulisainiwa tarehe 11 mwezi Disemba mwaka jana.
 

POLISI ARUSHA YADHIBITI UVUNJAJI MARA DUFU

$
0
0
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limeweza kudhibiti matukio ya uhalifu kwa 17.9% mwaka jana 2017 tofauti na mwaka 2016 ambapo kulikuwa na matukio 2,817 wakati  mwaka 2017 kulikuwa na matukio 1,963 pungufu ya matukio 854, huku matukio ya uvunjaji yakipungua toka 604 hadi 294 ikiwa ni zaidi ya mara mbili ya mwaka 2016.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda Polisi wa mkoa wa Arusha, Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema kwamba, matukio hayo ya uhalifu yamezidi kupungua mwaka hadi mwaka ambapo mwaka 2016 matukio yalipungua kwa 6.8% ikilinganishwa na mwaka juzi 2015, na kuongeza kwamba hayo yote yanatokana na ushirikiano mzuri kati ya wananchi na Jeshi hilo.

Makosa mengine ambayo yamepungua ni pamoja na Unyang’anyi wa kutumia nguvu ambayo mwaka 2016 yalikuwa 86 na mwaka jana 2017 yameshuka hadi 40 huku makosa ya kutupa watoto yalikuwa 38 lakini mwaka 2017 yameshuka hadi kufikia 13.

“Matukio ya Mauaji nayo yalipungua kutoka 65 hadi 58 kwa mwaka 2017, wizi wa Watoto yalikuwa 20 na yamepungua hadi matukio mawili, na yalioongezeka ni Ubakaji na Ulawiti ambapo mwaka 2016 matukio ya Ubakaji yalikuwa 144 na mwaka jana yameongezeka matukio matano wakati makosa ya Kulawiti yalikuwa 58 yameongeza kufikia 62”. Alisema Kamanda Mkumbo.

MICHUZI TV: WIMBO MPYA MTAANI, MANYOTA - USIKATE TAMAA

BEI YA BIDHAA ZA MATUNDA NA VYAKULA MBALIMBALI SOKO LA MABIBO JIJINI DAR LEO.

$
0
0
Wafanyabiashara  wakiwa katika biashara zao katika soko la Mabibo jijini Dar es Salaam mapema leo kama walivyokutwa na Mpiga picha wetu wa Globu ya jamii.
Tikitiki maji katika soko la mabibo ambalo linauzwa kwa bei ya jumla kati ya shilingi 1500 hadi 1800.
Viazi vitamu kwa gunia katika soko la mabibo vinauzwa kati ya Shilingi Elfu 55,000 hadi Elfu 60,000 na kwa rejareja ni sh. 1,000/= kwa fungu.
Ndizi katika soko la mabibo zinauzwa kati ya shilingi 25000 hadi 50,000 kwa mkungu kwa siku ya leo.
Ndizi mbivu katika soko la mabibo kwa kila moja inauzwa kati ya shilingi 80 hadi 200 kwa bei ya jumla kwa siku ya leo.
Nanasi katika soko la mabibo kwa bei ya jumla yanauzwa kati shilingi  Elfu 1000/= hadi elfu  1,800/=.
Biashara zikiendelea katika soko la mabibo katika kila pilikapilika za kutafuta mkate wa kila siku.Imetayarishwa na Chalila Kibuda-Globu ya Jamii.

MAKONDA APONGEZA KASI YA MATENGENEZO MAGARI YA POLISI,MAGEREZA,JWTZ

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepongeza hatua ambayo kampuni ya kutengeneza mabodi ya magari ya Dar Coach Ltd imefika y'all kutengeneza na kukarabati mabasi 11ya vyombo vya ulinzi na usalama.

Kati ya magari hayo magari matano yatakabidhiwa mwishoni mwa mwezi huu na mengine sita yatakabidhiwa. 

Makonda amesema mmiliki wa kampuni hiyo amethibitisha uzalendo wake na mchango wake katika kusaidia Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam  inayotaka kuona vyombo vya ulinzi na usalama wanakuwa na usafiri wa kisasa na uhakika ili kutekeleza majukumu yao. 
Jumla ya Sh milioni 830 mmiliki wa kampuni hiyo anatumia katika kukarabati magari yote 11ambapo baadhi yamenfenezewa mabodi mapya kwani yalikuwa yameharibika sana. 

Akizungumza leo baada ya kukagua magari hayo katika kampuni hiyo iliyopo Mwandege wilayani Mkuranga mkoani Pwani,Makonda amesema hatua ya ukarabati magari hayo umefikia pazuri na ameahidiwa kukabidhiwa baadhi ya magari hayo mwishoni mwa mwezi huu.

Amesema wakati matengenezo ya magari hayo unaendelea wapo watu kwenye mitandao ya kijamii wanalalamika kwanini yasinunuliwe magari mapya kwa madai gharama kubwa. "Wanaosema gharama ya kutengeneza magari ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ni kubwa wafahamu tu gharama za kutengeneza magari haya amejitolea mmiliki wa Kampuni ya Dar Coach Ltd,

"Ameamua kutoa mchango wake kupitia utalaam alionao wa kutengeneza mabodi ya magari ya majeshi yetu ambayo tumemletea. Ni mlipa kodi mzuri na kazi anayofanya ipo katika ubora unaokubalika,"Hao wanaolalamikia ukubwa wa gharama pengine  hawalipi hata kodi zaidi ya maneno tu.  Huyu ametusaidia na tunathamin mchango wake kwetu,"amesema. 
 Baadhi ya magari ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo yanaendelea kutengenezwa ambayo yalipelekwa yakiwa yameharibika kabisa 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza leo wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakati alipoenda kukagua magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama yanayotengenezwa na Kampuni ya  Dar Coach. 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipewa maelezo leo na Mkurugenzi wa kampuni ya Dar Coach Manmeet Lal kuhusu hatua waliyofikia katika kufanya matengenezo ya magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikagua magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo yanatengenezwa mabodi yake yaliyokuwa yameharibika.Matengenezo hayo yanafanywa na Kampuni ya Dar Coach Ltd
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikagua moja ya gari la Jeshi la Magereza leo inayofanyiwa matengenezo na Kampuni ya Dar Coach Ltd.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


MICHUZI TV: WAZIRI WA AFYA ASEMA SWALA LA MADAKTARI NI CHANGAMOTO

NEC yawakumbusha wasiamamizi wa Uchaguzi kuzingtia Sheria

$
0
0
Na Hussein Makame -NEC.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewakumbusha wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika kusimamia uchaguzi ili kufanikisha Uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Februari 17, 2018.

Hayo yamsemwa na Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Uchaguzi Kanda ya Pwani kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Stephen Elisante wakati akifungua mafunzo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo la Kinondoni na Kata za jimbo hilo la jiji la Dar es Salaam.

Alisema wasimamizi wa Uchaguzi wanapaswa kutambua kuwa Uchaguzi ni mchakato unaohusisha taratibu mbalimbali kwa mujibu wa katiba, sheria, kanuni, taratibu, maelekezo na miongozo iliyotolewa kisheria.

“Hivyo mnapaswa kuzisoma sheria hizo ili kuweze kutekeleza majukumu yenu kwa mujibu wa sheria,tufanye maamuzi yetu kwa kujitambua, kujiamini na kutoogopa na kuchukua hatua za haraka katika kushughulikia changamoto zinazojitokeza” alisema Elisante.
 Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Uchaguzi Kanda ya Pwani kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Stephen Elisante akizungumza na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wa ngazi ya Jimbo la Kinondoni na Kata za jimbo hilo kwenye mafunzo ya maandalizi ya Uchaguzi Mdogo wa Februari.
 Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Kinondoni Boniface Lihamwike akiwaapisha wasiamamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni na kata zake wakati wa mafunzo ya maandalizi ya Uchaguzi Mdogo.

Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni, Victoria Wihenge, akiwasilisha Mada ya Maelekezo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata kwa wasiamamizi wa Kinondoni.Picha na Hussein Makame-NEC

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KOKA ATOA MILIONI MBILI KUCHANGIA UJENZI WA MADARASA YALIYOUNGU ASHULE YA MSINGI KONGOWE

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

MBUNGE wa jimbo la Kibaha Mjini, Silvestry Koka, ametoa kiasi cha shilingi milioni mbili zitakazosaidia kutumika kuezeka madarasa yaliyojengwa baada ya kuungua katika shule ya msingi Kongowe.

Mwaka 2016 vyumba vitatu vya madarasa na ofisi, shuleni hapo viliungua kutokana na kutokea shoti ya umeme .

Koka alitoa mchango huo, wakati alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara ,Miembesaba 'A'kata ya Kongowe katika muendelezo wa ziara yake ya jimbo.Aliomba fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo pamoja na kukamilisha ujenzi wa shule hiyo zisimamiwe na kutumika kwa matumizi lengwa.

Akizungumzia changamoto za kielimu kijumla ,alisema kwasasa maeneo mengi yanakabiliwa na tatizo la upungufu na uchakavu wa miundombinu .
Koka aliitaka jamii ,wadau ,kamati za shule na viongozi mbalimbali kushiririkiana kuongeza vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo mashuleni .

"Kulikuwa na kero kubwa ya uhaba wa madawati na kusababisha watoto wetu kusoma huku wakiwa wamekaa chini na kupata vifua kutokana na vumbi""Lakini tumejitahidi tumemaliza kero hiyo ,kilichobaki kwasasa ni tatizo la miundombinu,ambapo tushikamane kumaliza ama kulipunguza ili watoto waondokane na mlundikano wa kusoma kwenye darasa moja ama kusoma kwa awamu" alifafanua Koka.

ZFA KUKUTANA NA WADAU WA SOKA VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0
 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kamati Tendaji ya chama cha soka Wilaya ya Magharibi A Unguja inatarajia kukutana kwa siku 2 na makundi mbalimbali ya wadau wa soka wilayani humo ili kujadili mambo yanahusiana na msimu wa ligi wa 2017/18.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa ZFA hiyo Zainab Omar Mussa, Kamati itakutana na waamuzi waliochezesha ligi hiyo kabla ya kwenda katika mapumziko na wajumbe wa Kamati ya waamuzi kitakachofanyika Jumamosi ya Januari 20, 2018 kitakachofuatiwa na mkutano wa vilabu vyote wilayani hump kitakachofanyika Jumapili Januari 21, 2018.

Alisema vikao hivyo ni utekelezaji wa uamuzi wa vikao vya Kamati Tendaji na Sekretarieti ya ZFA hiyo ambavyo vilielekeza kufanyika vikao hivyo ili kujadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika kipindi kilichopita.

Akizungumzia mwendelezo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 31 katika daraja la pili na 12 za daraja la tatu, Zainab alisema ligi hiyo itaendelea kuanzia Januari 27, 2018 na ratiba kwa ajili ya ligi hiyo itatolewa siku ya kikao na vilabu na kuvitaka vilabu vyote kuhudhuria sambamba na kuanza maandalizi ya Timu zao kwa ajili ya ligi hiyo.

Msimu wa ligi katika wilaya ya Magharibi A ulianza rasmi mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2017 na kusimama mnamo mwezi wa 12 ili kupisha mashindano ya kombe la Mapinduzi na dirisha dogo la usajili lililomalizika hivi karibuni.

MICHUZI TV: WANAOTUHUMIWA KUJIUNGANISHIA BOMBA LA MAFUTA WAFIKISHWA KORTINI

$
0
0

 Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

WATU saba akiwemo aliyekuwa fundi wa bomba la mafuta la Tazama, Samwel Nyakirang'ani (63) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka saba ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia bomba la mafuta.

Nyakirang'ani anashtakiwa pamoja na Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Ufukoni, Nyangi Matoro (54), washtakiwa wengine,
Mfanyabiashara Farijia Ahmed (39), Malaki Mathias (39), Kristomsi Angelusi(25), Henry Fredrick (38) na fundi ujenzi Pamfili Nkoronko(40).
Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao leo mahakamani hapo na Wakili wa Serikali  Tulumanywa Majigo akisaidiana na Wakili wa Serikali Mkuu Peter Maugo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba.Wanadaiwa kutenda makosa yanayowakabili chini ya sheria petrol kinachoenda pamoja na sheria ya uhujumu uchumi.

Akiwasomea hati ya mashtaka, Wakili Majigo alidai kuwa kosa la kwanza ni kujiunganishia isivyo halali katika bomba la mafuta ya Dizeli.

Imedaiwa, washtakiwa wote  katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2015 na Januari 8, mwaka huu, huko maeneo ya Tungi Muungano katika Wilaya ya  Kigamboni jijini Dar es Salaam walijiunganishia bomba la upana wa inchi moja kwenye bomba la inchi 24 la  diesel material yasiyoshika kutu bila kuwa na kibali cha Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Katika shtaka jingine la kuharibu miundombinu ( kifaa kinachotumika kwa ajili ya utoaji huduma muhimu)  imedaiwa katika tarehe na maeneo hayo hayo, washtakiwa kwa pamoja walitoboa na kuharibu bomba la Inchi 24 linalotumika kusambaza mafuta ya Dizeli mali ya TPA.

Washtakiwa hao wanadaiwa pia kuwa, kati ya 2015 na January 8, 2018 maeneo ya Tungi Kigamboni, walitoboa bomba la inchi 28 la mafuta linalotumika kwa ajili ya usambazaji wa  Crude Oil likiwa ni mali ya TPA.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Wakili Majigo alidai Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amewasilisha hati ya kuzuia dhamana kwa washtakiwa hao.

Washtakiwa hawaruhusiwi kujibu lolote kwa kuwa kesi inayowakabili ni ya uhujumu Uchumi ma imeahirishwa hadi Januari 30,2018.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi bado haujakamili, washtakiwa wamerudishwa rumande.

YANGA YAPATA SHAVU LA BILIONI 2/-

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya jamii 
KLABU ya Yanga ya Dar es Salaam imesaini mkataba wa miaka mitatu na Kampuni ya Macron kutoka  Itali kwa lengo la kutengenezewa jezi za kimataifa zenye thamani ya Sh.bilioni 2.

Makubaliano ya utiaji saini mkataba huo umefanywa leo Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Yanga Boniphace Mkwasa na Mkurugenzi Kampuni ya Macron Tanzania Suleiman Karimu.

Akizungumza baada kusaini mkataba huo, Mkwasa pia amesema kwa wale wanaouza jezi mitaani kwa manufaa yao binafsi ambayo  hayanufaishi klabu yao waache mara moja.

"Kwa wataoendelea na biashara hiyo watachukuliwa hatua,"amesema Mkwasa.

Kwa upande wa Mkurugenzi kampuni ya Macron Tanzania, Suleiman Karimu ameishukuru klabu ya Yanga kwani  makubaliano hayo  yataleta mapinduzi ya mpira wa miguu hapa nchini.
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa akisaini makubaliano ya mkataba na Mkurugenzi wa MACRON Tanzania Suleiman Karim wenye thamani ya Bilion 2 kwa ajili ya vifaa vya michezo uliotiwa saini leo Mbele ya waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.

MAAFISA HABARAI, MAWASILIANO, UHUSIANO NA ITIFAKI SERIKALINI KUKUTANA MACHI 12-16, 2018 JIJINI ARUSHA


MICHUZI TV: RAIS DKT MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABOLOZI SITA IKULU JIJINI DAR LEO

WATEJA WA UMOJASWITCH WAIBUKA NA MAMILIONI KUPITIA BAHATI NASIBU

$
0
0
Kampuni ya UmojaSwitch leo imechezesha droo yake ya bahati nasibu ya Shinda na Umoja kwa wateja wake zaidi ya 32,222 waliotumia kadi za UmojaSwitch kati ya tarehe 1- 8 Januari mwaka huu ambapo zaidi ya wateja 25 wameibuka washindi katika droo ya leo UmojaSwitch ilianzisha bahati nasibu hiyo ya Shinda na Umoja mwezi Desemba mwaka jana kwa lengo la kutoa hamasa kwa wateja wao kupitia kampeni yao ya kubadili kadi za UmojaSwitch kutoka kwenye mfumo wa zamani na kwenda kwenye mfumo mpya wa ‘Microchip’ Katika makundi matatu yaliyo chezeshwa leo kundi la kwanza limetoa washindi 25 waliojishindia T-Shirt za UmojaSwitch, Mzunguruko wa pili umetoa washindi wa tano wa Simu za Mkononi (Smart Phone), mzunguruko wa tatu umepata washindi wawili wa fedha taslimu mara mbili ya fedha walizokuwa wanatoa kwenye Akaunt zao kupitia kadi za UmojaSwitch na Mzunguzuro wa nne umepata mshindi mmoja aliejishindia kiasi cha Shilingi Milioni Moja Taslimu 
Akiendesha Droo hiyo Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Bi Beatrice Emmanuel Chini ya Mkaguzi wa Bodi ya Michezo yakubahatisha Bakari Maggid amewapongeza washindi wa zawadi hizo na kudai kuwa watafanya mawasiliano na Benki husika wanazotumia washindi wao ili kuweza kuwapatia zawadi zao muda mchache kuanzia leo Aidha Beaterice amewataka wateja ambao bado hawajabadilisha kadi zao za awali kufika kwenye Benki ao husika ili kubadili kadi zao na kuwea kuingia katika bahati nasibu hiyo ya Shinda na UmojaSwitch kwenye droo inayofuata. 
Kampuni ya UmojaSwitch inaunganisha mabenki zaidi ya 27 Tanzania kwa lengo la kushirikiana kutoa fedha kwa njia ya kilectronic ya ATMs

BITEKO AWATAKA STAMICO KUTATHIMINI UTENDAJI WAO

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

NAIBU Waziri wa Madini, Dotto Biteko amelitaka Shirika la Taifa la Madini (Stamico) kujitathini kuhusu utendaji wao wa kazi kwa Taifa kutokana na kuwa deni kubwa kuliko uzalishaji wa shirika hilo.

Biteko ametoa kauli hiyo alipotembelea Shirika la Taifa la Madini (Stamico) leo, Dar es Salaam,ambapo amesema Stamico imekuwa na madeni yanayofanya kudidimiza shirika kutokana na miradi wanayoiendesha ya uchimbaji kushindwa kuzalisha faida.

Amesema baada ya watu kujua changamoto sasa ndio wameona sehemu kujengea hoja katika taarifa mbalimbali.Biteko amesema Stamico ilitakiwa kuwa sehemu ya kujifunzia kwa wachimbaji wadogo lakini wachimbaji wadogo hawawezi kufika Stamico kwa sababu hakuna cha kujifunza.

Stamico inadeni zaidi ya Sh.bilioni moja pamoja na deni la Stamigold la Sh.bilioni 54 na Serikali inatakiwa kulipa deni hilo na kuacha kununua madawati katika shule.Biteko amesema kuwa kunahitajika kuwepo ubunifu kwa Stamico kwa kujiona wana kazi ya ziada ya kusaidia Taifa kupiga hatua.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Stamico, Alex Rutagwelela amesema kuwa maagizo watayafanyia kazi katika uendeshaji wa shirika hilo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza jambo wakati akizungumza na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akikagua mtambo wa uchongaji mashimo kwa ajili ya utafiti wakati alipotembelea Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza wakati wa kikao cha pamoja na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza wakati wa kikao cha pamoja na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akiwa katika picha ya  pamoja na Uongozi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.

DK. KIGWANGALLA APONGEZA USHIRIKIANO WA FINLAND KATIKA UHIFADHI WA MISITU NCHINI

$
0
0
Na Hamza Temba - Dodoma

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla ameipongeza Serikali ya Finland kwa ushirikiano na misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiitoa kuunga mkono juhudi za Serikali katika uhifadhi wa maliasili na uendelezaji wa misitu nchini.


Dk. Kigwangalla ametoa pongezi hizo leo Januari 16, 2018 kwa Balozi wa nchi hiyo hapa nchini, Mhe. Peka Huka ambaye amemtembelea ofisini kwake mjini Dodoma kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo katika uhifadhi na maendeleo ya misitu nchini.


“Napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa Serikali ya Finland,  mmekuwa washirika wetu wakubwa wa maendeleo kwa muda mrefu ambao mmetusaidia mambo mbalimbali ikiwemo kuendeleza misitu nchini, kuendeleza Chuo cha Mafunzo ya Misitu Olmotonyi na hata mapitio ya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998, ni matumaini yetu kuwa mtaendelea kudumisha ushirikiano huu”, alisema Dk. Kigwangalla.


Alimueleza balozi huyo kuwa Tanzania inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika uhifadhi wa misitu nchini ikiwemo uhaba wa rasilimali fedha na teknolojia kwa ajili ya kuwezesha uhifadhi endelevu. Alisema changamoto nyingine ni uvunaji haramu wa mazao ya misitu ambayo husababisha eneo la hekta 372,000 za misitu kupotea kila mwaka.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Peka Huka ofisini kwake mjini Dodoma leo alipotembelewa na balozi huyo kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo katika uhifadhi na uendelezaji wa misitu nchini. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimkaribisha Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Peka Huka ofisini kwake mjini Dodoma leo alipotembelewa na balozi huyo kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo katika uhifadhi na uendelezaji wa misitu nchini.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Peka Huka ofisini kwake mjini Dodoma leo alipotembelewa na balozi huyo kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo katika uhifadhi na uendelezaji wa misitu nchini.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MJI MDOGO WA SHIRATI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa mji mdogo wa Shirati wilayani Rorya  akiwa katika ziara a mkoa wa MKara Januari 16. 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images