Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 209 | 210 | (Page 211) | 212 | 213 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0


  Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo, akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ukumbi wa Kivukoni, Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa maonyesho ya siku tatu ya Vodacom Elimu Expo, yanayotarajia kuanza Agosti 30, mwaka huu katika Viwanja vya Michezo vya Chuo cha Posta, Kijitonyama jijini. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama (kushoto) ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa. 


   Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo (katikati) Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama (kulia) na  Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa, wakigonganisha glasi, kama ishara ya uzinduzi wa maonyesho hayo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo.
   Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo leo, Katikati ni   Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo, na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa.
  Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo leo, Katikati ni   Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo, na Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama.
   Sehemu ya waandishi wa habari, waliohudhuria mkutano huo.
  PICHA NA SUFIANIMAFOTO.

  0 0  Licha ya Taifa Stars kushindwa kufuzu kucheza katika mashindano ya CHAN mwakani baada ya kufungwa na Uganda Cranes 3-1, wadhamini wa Stars, Kilimanjaro Premium Lager wamesema hawajakata tama nab ado wana imani na timu nzima na kocha Kim Poulsen.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya Stars kuwasili, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema licha ya habari hizi kutokuwa njema kwa watanzania, ni vizuri kukubali matokeo na kuangalia picha kubwa na malengo ya muda mrefu.

  “Ni vyema tukumbuke kuwa kwenye mpira kuna kushinda na kushindwa,” alisema Bw Kavishe na kuongeza, “Tunapenda kuwahakikishia watanzania kuwa sisi kama wadhamini hatujakata tama na bado tuna imani na timu hii na kocha Kim Poulsen kwa hivyo tunawaomba watanzania wasife moyo.”

  Alisema wakati walipoanza kuidhamini Taifa Stars mwezi Mei mwaka jana na kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa mwaka, kwa muda wa miaka mitano, walikuwa na malengo kadhaa ikiwemo kuinua hadhi ya Timu ya Taifa, kuhakikisha wanaingia kambini kwa muda unaotakiwa, wanalipwa vizuri, wanakula na kulala vizuri na kusafiri vizuri.

  “Tumejitahidi kufanya mambo haya kwani wachezaji sasa hivi wana DVD zenye maelezo yao, tumewapa suti mpya na za kisasa na pia tumewapa basi jipya la kisasa. Mambo haya yote pamoja na mambo wanayofundishwa na Mwalimu Kim Poulsen yamesaidia kuleta mabadiliko kwa timu ya Taifa,” alisema.

  Alisema kuna mafanikio mazuri ya timu ya taifa ambayo watanzania lazima wayakumbuke kama kuzifunga timu kama Zambia, Cameroon, Morocco na Kenya .

  Kwa mujibu wa Meneja huyo walipoanza udhamini Tanzania ilikuwa katika nafasi ya 145 kwa mujibu wa FIFA lakini sasa imesogea hadi 109. “Haya ni mafanikio makubwa kwani tumesogea hatua zaidi ya 40,” alisema.


  Alisema safari ya mafanikio katika mpira ni ndefu na inahitaji uvumilivu wa hali ya juu na kuongeza kuwa Kocha Kim Poulsen anafanya kazi nzuri ya kuibua vijana.

  “Kocha anahitaji kuungwa mkono na sisi sote kuanzia kwa TFF, sisi wadhamini na watanzania wote. Tunahitaji kuangalia picha kubwa,” alisema na kuongeza,”Nawaomba watanzania tuwe wazalendo wakati huu hii ni timu yetu na tunatakiwa kujivunia. Vyombo vya habari pia viwe mstari wa mbele kuonesha uzalendo.”

  Alisema mechi dhidi ya Gambia itakayochezwa mwezi wa 9 ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia ni muhimu hata kama Tanzania haisongi mbele kwani itasaidia katika ngazi za FIFA.

  0 0

  Hili ni moja ya maeneo maarufu yaliopo ndani ya jiji la Dar,Je waweza jua ni wapi hapa??

  0 0
 • 07/29/13--08:21: CCM YAKOMALIA SERIKALI MBILI


 • 0 0
 • 07/29/13--10:07: mambo ya gado
 • Egypt-Who will bink first

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelefu ya wananchi wa mkoa wa Kagera waliofurika katika uwanja wa michezo wa Kaitaba kumsikiliza siku ya mwisho ya ziara yake ya siku sita mkoani humo. PICHA NA IKULU
  Rais Jakaya Kikwete baada ya kutawazwa kuwa Omukama (Chifu) wa Missenyi wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Kagera akiwa na  kiongozi wa wazee wa Missenyi, Mzee Ernest Babeiya.
  Rais Jakaya Kikwete akitawazwa kuwa Omukama (Chifu) wa Missenyi wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Kagera. Anayemsimika ni kiongozi wa wazee wa Missenyi, Mzee Ernest Babeiya.
  Omukama Kikwete akihutubia wananchi Missenyi
   Rais Jakaya Kikwete akitawazwa kuwa Omukama (Chifu) wa Missenyi wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Kagera. Anayemsimika ni kiongozi wa wazee wa Missenyi, Mzee Ernest Babeiya.

  0 0

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima (kulia) akimkabidhi tunzo Rais wa Chama cha Wadau wa Magari (AAT), Nizar Jivani kwa ajili ya chama chake kutoa mchango mkubwa kwa kutoa mafunzo ya uendeshaji kwa madereva 2500 wa pikpiki, ambao tayari wamehitimu mafunzo hayo yaliyotolewa jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2012 hadi Julai 2013. Makabidhiano hayo yalifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi leo. Kulia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima (kulia) akiwafafanulia waandishi wa habari, jisni Chama cha Wadau wa Magari nchini (AAT), kilivyokuwa kinatoa mchango wake kwa kutoa mafunzo ya uendeshaji pikpiki kwa jina maarufu bodaboda. Madereva 2500 wa pikpiki walihitimu mafunzo hayo yaliyotolewa jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2012 hadi Julai 2013.      
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima (wapili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Wadau wa Magari (AAT) Nizar Jivani na Yusuf Ghor. Kulia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga.  Naibu Waziri Pereira alitoa tunzo kwa uongozi wa AAT kwa ajili ya  kutoa mafunzo ya uendeshaji pikpiki kwa jina maarufu bodaboda. Madereva 2500 wa pikpiki walihitimu mafunzo hayo yaliyotolewa jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2012 hadi Julai 2013. Picha zote na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

  0 0


   Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge akipokea taarifa kuhusu ziwa Chala lililoko wilayani Rombo kutoka kwa afisa wa Bonde la maji la Pangani Mtoi Kanyawana.

   Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge akichukua taswira ya ziwa Chala lililoko wilayani Rombo wakati wa ziara kutembelea miradi mbalimbali ya maji katika wilaya hiyo.
  Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa mamlaka ya maji wa mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara yake kutembelea ziwa Chala.Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi.

  0 0

  Baada ya tambo za hapa na pale hatimaye vigogo wa soka la wazee hapa Dar es Salaam wanategemea kukutana siku ya Jumamosi katika uwanja wa bora, pale kijitonyama, jijini Dar es salaam.
  Ni mechi yenye kila aina ufundi maana timu hizi mbili zinasifa tofauti kabisa. Kijitonyama ni timu maarufu sana kwenye vyombo vya habari huku Golden Bush ikiwa na sifa ya kutoa vipigo kwa timu pinzani, ni timu pekee iliyopoteza mechi chache sana toka ianzishwe. Ni kutokana na umuhimu wa game hii ya jumapili tunalazimika kuweka Camp Bamba Beach ili timu iwe sawasawa kabisa. 
  Tumewatafuta kwa muda mrefu sana ndugu zetu hawa lakini tunamshukuru mmoja wa viongozi wa Kijitonyama Veterans bwana Majuto Omary amekubali game bila kusita. 
  Tunaomba mashabiki mfike kwa wingi ili kuona burudani ya watu wazima walioacha mpira huku wakiwa bado kwenye kiwango cha juu kabisa. Maandalizi ya game yamekamilika na uwanja umefungwa kwa muda ili siku ya mechi pitch iwe sawasawa kabisa. 
  Tumeamua kutoa habari hii mapema ili watu wa mkoani na nchi za jirani wapeta muda kujiandaa kuja kuangalia game hii siku ya tarehe 04/08/2013.

  Asanteni. 
  Onesmo Waziri “Ticotico” 
  Msemaji wa timu na mchezaji 
  mwandamizi Golden Bush FC

  0 0

  Imekuwa ni mazoea kwa jamii yetu kupuuza na kutokuzipa uzito kauli na mawazo yanayolenga kujenga taifa letu. Badala yake tumekuwa tukitumia muda mwingi kushabikia na kuongelea mambo yasiyo na tija kwa taifa. Kwa sababu hii CHADEMA UK tuko mstari wa mbele kuzipigia mbiu na kuzipa umuhimu na uzito wake kauli za waTanzania zenye nia ya kulijenga taifa tukianza na kauli nzito iliyotolewa na Shekh Mkuu wa Baraza la Waislamu nchini (BAKWATA). 
  Kwanza kabisa Tunampongeza kwa dhati kabisa kwa ujasiri mkubwa kuzungumzia maswala mabayo viongozi wetu wengi katika ngazi mbali mabli kitiaifa wanalikwepa aidha kwa makusudi au kutokana nan nidhamu ya uoga. Shekh Shaban Simba amegusia swala muhimu sana kuhusiana na mustakabali wa siasa na dini ndani ya nchi yetu. Kwa uwazi mkubwa na kwa nia njema kabisa katika juhudi za kuliepusha Taifa  letu na migangano ya kiimani katika misingi ya malumbano ya kisiasa, ametutahadharisha WaTanzania wapenda amani kuwa makini na baadhi ya wanasiasa wanaojenga utamaduni wa kupenyeza siasa katika nyumba za ibaada kwa kasi kupitia iilimradi wapate majukwaa ya kuendeleza matakwa yao ya kisiasa. 
  Na zaidi ameelezea mpango wa kuanzisha vikundi vya usalama ili kulinda amani ndani ya BAKWATA.
  Hivi karibuni tumeona jinsi ambavyo baadhi ya wanaiasa wamejikita kwenye nyumba za kuabudu kwa kile ambacho ni dhahiri katika kuendeleza (to pursue) ndoto zao za kisiasa. Cha kusikitisha ni kwamba baadhi ya viongozi hawa kwa nyakati tofauti wameshawahi kuhikilia nyadhifa mbali mbali za kisiasa na ndani ya serikali. 
  Kwenye nyadhifa zao ungetegemea wangetumia nafasi zao kuonesha ufanisi na na kudhihirisha uwezo wao wa kuongoza na kujenga imani kwa wananchi. Badala yake wanatumia nyumba za kidini kutaka tena nafasi za kuongoza. Cha kusikitisha zaidi ni jinsi ambavyo baadhi ya viongozi wa dini wanavyokubali kurubuniwa na kutumiwa vibaya na wanasiasa. Alichozungumzia Shekh Mkuu ni ukweli usiopingika kwamba nyumba za dini si majukwaa ya kisiasa. 
  Kama waTanzania wenye mapenzi na nchi yetu, tunapenda kusisitiza na kukazia kauli ya Shekh Mkuu. Nyumba za kuabudu zitumiwe kwa madhumuni hayo na si vinginevyo.

  Shekh Mkuu pia ametoa agizo la kuundwa kwa kamati za ulinzi ndani ya BAKWATA nchi nzima ili kulinda amani. Alisema mpango huu ni katika kutekeleza maagizo yaliyopendekezwa na kiongozi mkuu wa jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema. Nia ni kugundua viashiria vya uvunjaji wa amani na kuzipeleka kwenye vyombo vinavyohusika. 
  Kwa mukhtasari tu, IGP ametoa maelekezo haya kwa kuwa uwezo wa jeshi la Polisi kulinda na kuzuia matukio ya kijangili ni mdogo na hauwezi kufika kila mahali hivyo ni jukumu la viongozi wa taasisi mbali mbali kuweka mikakati ya ulinzi kwenye mikusanyiko yao. Kwa mantiki hii Shekh Mkuu ana kila sababu ya kujipanga na taasisi nyingine zina kila sababu ya kujipanga.

  Ni jambo la ushujaa na lenye kuonesha ukomavu kuona kiongozi mkuu wa dini akiweka bayana hisia zake kuhusu mustakabali wa siasa na dini ndani ya nchi. Na kwa sababu hiyo CHADEMA UK tunampongeza Shekh Mkuu kwa kuonyesha mfano wa kuigwa na viongozi wote wa dini kukemea bila staha utamaduni huu wa kujaribu kuingiza siasa katika nyumba za ibada. 
  Kila kiongozi angekumbuka wajibu wake kama shekhe Shaban Simba, tuna imani kuwa mambo mengi ya kijami yaliowashinda wanasiasa kukemea kwa kukosa (moral authority), yange fanyiwa kazi kwa ufanisi kwa wale wanoaminiwa na jamii kwa kiwango kikubwa. 
  CHADEMA UK itaunga mkono kwa nguvu zote MTanzania yeyote atakaye simamia msingi mikubwa ya amani kitaifa kama Shekh Shaban Simba. Kwa upande wa kauli ya IGP kuhusu vikundi vya ulinzi katika taasisi mbali mbali,  tuna kila sababu ya kuamini kwamba mapendekezo haya ya IGP kuwataka viongozi wa taasisi mbali mbali kuanzisha vikundi vya ulinzi ili kusaidiana na vyombo vya dola katika kulinda mikusanyiko yao , yamekuja wakati muafaka hasa baada ya kiongozi huyo mkuu kukiri uwezo mdogo wa Polisi katika kulinda amani nchi nzima.


  MUNGU IBARIKI TANZANIA


  CHADEMA UK


  0 0

  Kumekuwa na uvumi kwamba mtandao wa uombaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (OLAS) ulikuwa na hitilafu ya kiufundi na hivyo Wanafunzi wanaondelea na masomo ambao walikuwa tayari wameshahakiki taarifa zao wanapaswa kurejea kujaza upya ama kuhakiki iwapo taarifa zao zipo mtandaoni.
  Bodi inatumia fursa hii kuwajulisha Wanafunzi husika, Vyuo vya Elimu ya Juu na Umma kwa ujumla kuwa taarifa za Wanafunzi hao zilizopokelewa ziko salama na hawapaswi kujaza tena na hivyo taarifa hizo za uvumi zipuuzwe.
  Aidha Bodi inasisitiza  kwamba kesho tarehe 31 Julai, 2013 ni mwisho wa kupokea maombi ya mikopo ya waombaji wote wanaotarajia kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2013/2014 na wale wanaoendelea na masomo na kwamba hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.
  Bodi inawapa nafasi ya mwisho waombaji wapya na wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao hawajaomba mikopo kwa njia ya mtandao, kuhakikisha wanatumia muda uliobaki kukamilisha taratibu zote za maombi kupitia anuani ifuatayo: http://olas.heslb.go.tz au kupitia tovuti: www.heslb.go.tz 
  Tangazo hili limetolewa na:
  Mkurugenzi Mtendaji
  BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

  0 0


  Kwa maelezo zaidi na maelekezo tafadhali piga simu 
  0713602898 or 0758870007.
   
   
   
   
   

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto)  akimkaribisha Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas  katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja wao jijini  Dar es Salaam
   Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili  kushoto) akiwakaribisha baadhi  ya wateja wao katika hafla ya futari  iliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya.
   Baadhi ya wateja wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania  wakichukua mlo wa futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar es  Salaamu
   Wateja wa Airtel Tanzania wakipakua  futari iliyoandaliwa  na kampuni hiyo jijini Dar se Salaam
   Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications, Bakari Machumu  (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil  Kolaso (kulia kwake) wakichukua mlo wa futari iliyoandaliwa na Airtel  kwa wateja wake jijini Dar es Salaam
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Azam,  (wa pili  kushoto),  akichukua mlo wa futari pamoja na baadhi ya wateja wa  Airtel katika hafla iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa wateja wake
  jijini Dar es Salaam
  Baadhi ya wateja wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania  wakifuturu katika hafla iiliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar es  Salaamu

  0 0

  (From right to left) Honorable Fatma Abdulhabib Fereji, Minister of State at the First Vice President's Office, Zanzibar Government of National Unity, Dr. Abdallah O. Kigoda, Tanzania's Minister of Industry, Trade and Marketing and guest of honor, United States Ambassador to Tanzania Alfonso E. Lenhardt and Mr. Ali Mzee Ali the former chairman of the “Committee of Six” that spearheaded the transition to the Government of National Unity (GNU) in Zanzibar, during a reception hosted by Ambassador Lenhardt (second from left) at his residence in Dar es Salaam in celebration of the 237th anniversary of American Independence recently.
  During the reception which was attended by approximately 500 people including Tanzanian government, business and cultural leaders, members of the diplomatic corps and other guests, Ambassador Lenhardt thanked his guests for the friendship and partnership they have extended to him and his team for the past four years adding that he was especially proud that President Barack Obama and First Lady Michelle Obama visited Tanzania early this month to personally convey America's message of friendship with Tanzania. (Photo courtesy of the American Embassy).

  0 0

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri ya CCM wa Wilaya za Dimani, Mfenesini na Mkoa wa Magharibi Kichama katika mkutano maalum wa kukaribishwa kwake kuwa Mlezi wa Mkoa Magharibi Kichama.
  Balozi Seif akikabidhi mchango wa shilingi Milioni 1,000,000/- kununulia Mabati kwa ajili ya uwezekaji wa Tawi la CCM la Kilima Matange liliopo Jimbo la Muyuni kutekeleza ahadi aliyoitoa Mwezi Machi mwaka huu wakati wa ziara yake Mkoa Kusini Unguja.
  Wajumbe wa Halmashauri ya CCM wa Wilaya za Dimani, Mfenesini na Mkoa wa Magharibi Kichama wakimsikiliza Mlezi wa Mkoa huo Balozi Seif Ali Iddi alipokuwa akikaribishwa rasmi kuwa mlezi wa Mkoa huo katika Mkutano uliofanyika katika Tawi la CCM Kiembe Samaki.

  0 0

  Wageni kutoka CDC/ATLANTA (waliopo katikati) wakiwa katika Picha ya pamoja na Dkt. Zubeda Suleiman wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (wa kwanza kushoto), wa pili kushoto ni Dkt. Ahmed Makata ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya HVIT Foundation inayoshughulika na Elimu ya Usalama Barabarani na uvaaji wa Kofia ngumu(wa tatu kulia) ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya HVIT Foundation, Bw. Alpherio Nchimbi.
  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Ann Dellinge( wa kwanza kulia) na Dkt. Erin Parker (wa pili kushoto) na mwenyeji wao Dkt. Zubeda Suleiman wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii walipomtembelea ofisini kwake katika ziara hiyo ya tarehe 25/07/2013.

  Mkuu wa Utawala wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania Kamishna Msaidizi wa Polisi Johansen Kahatano (wa kwanza kulia akiwa na wageni kutoka CDC/ATLANTA walipomtembelea ofisini kwake.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili Kigogo Mburahati, jijini Dar es Salaam, leo Julai 30, 2013 nyumbani kwa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Juma Haji Mkima, kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa famili ya mhasibu huyo aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Aga Khan. Marehemu Juma, anatarajia kuzikwa leo kijijini kwao, Rufiji.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu Juma Haji Mkina, Kibibi Juma Mkina, aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais alifika nyumbani kwa marehemu Kigogo Mburahani leo Julai 30, 2013 kwa ajili ua kutoka mkono wa pole, kabla ya marehemu kusafirishwa kwenda kuzikwa kijijini kwao Rufiji.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika pamoja na waombolezaji nyumbani aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Juma Haji Mkina, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam. Makamu alifika nyumbani kwa marehemu Kigogo Mburahati, leo Julai 30 kwa ajili ya kutoa mkono wa pole na kuwafariji wafiwa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka Kigogo Mburahati, jijini Dar es Salaam, leo Julai 30, 2013 nyumbani kwa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Juma Haji Mkima, baada ya kufika kutoka mkono wa pole na kuwafariji wafiwa kutokana na msiba huo. Marehemu Juma, anatarajia kuzikwa leo kijijini kwao, Rufiji. Picha na OMR.

  0 0

  Mtafiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Pasience Mtowe (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Julai 29, 2013. wakati akitoa taarifa ya nusu mwaka ya kuanzia Januari hadi Juni 2013 ya kituo hicho kuhusu mambo mbalimbali yaliyotokea nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji wa Kituo hicho Imelda Urio.
  Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji wa Kituo hicho Imelda Urio, akizungumza katika mkutano huo.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliodhuria mkutano huo.

  0 0

  Na. Luppy Kunga’lo Polisi Dodoma

  Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu wawili wenye asilia ya kiarabu na watanzania watatu kwa tuhuma za kufanya utapeli na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu katika vituo vya kuuzia mafuta (sheli) na maduka ya kubadilishia fedha. Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Bw, David Misime alisema Tukio hilo lilitokea juzi katika Sheli ya Camel Iliyopo karibu na Chuo Cha Mipango katika manispaa ya Dodoma.

  Kamanda Misime alisema watu hao walifika katika sheli hiyo ambapo kulikuwa na duka na kuagiza soda kisha baadae kutoa dola ya kimarekani ya USD 50, ambapo muuzaji aliwaambia kuwa habadilishi pesa, hivyo kuamua kumdanganya kuwa wanahitaji pesa ya kitanzania kwa ajili ya kwenda kuonyesha Misri kama sehemu ya maonyesho.

  “Wateja hao waliomba wapatiwe noti za 10,000/= za zamani ili wao wampatie noti mpya za 10,000/=, muuzaji huyo alichambua noti za zamani zipatazo shilingi 470,000/= na kuwapa kisha wao kumwambia wanazotaka kumbadilishia ziko kwenye gari na kujifanya kwenda katika gari na matokeo yake waliondoka kwa kasi” alieleza Kamanda David Misime.

  Mkuu huyo wa Polisi Mkoa wa Dodoma alisema baada ya watu hao kuondoka kwa kasi ndipo muuzaji huyo kugundua kwamba ameibiwa na kupiga simu Polisi ambao waliwasiliana na vituo vyote vya mjini na nje ya mji na kufanikiwa kuwakamata matapeli hao katika kituo/barrie ya Chanene liyopo wilayani Chamwino pori la Mtungutu.

  Kamanda Misime aliwataja watuhumiwa hao waliokuwa wakitumia gari aina RAV 4 T. 872 CGE la rangi ya damu yam zee kuwa ni mwanamke Ahlam d/o Hassan, miaka hamsini mwarabu na mkazi wa Tanga, mwanaume Daoud Esam@Abdelgawad , miaka 39 , msudani dereva na mkazi wa misri ambaye alikuwa na passport ya kuiingia nchini tarehe 19/07/2013 na ana Visa ya kukaa Tanzania kwa muda wa Miezi mitatu.

  Wengine ambao baada ya kuhojiwa, Kamanda alisema walikiri kufanya utapeli huo ni Matata Laurence, miaka (38) dereva na mkazi wa Gongo la Mboto, Rahma Mahamoud, miaka (26) Mkazi wa Dar es Salaam pamoja na Salehe Hamad Mnene , miaka 40 na mkazi wa Manzese Dar es salaam.

  Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kwa wanachi kuwa makini na ya watu wanaofanya vitendo vya namna hii na kuwataka kutoa taarifa mapema pindi wanapotia shaka kwa watu wa aina hiyo, ili hatua za kuwadhibiti zichukuliwe mapema.

older | 1 | .... | 209 | 210 | (Page 211) | 212 | 213 | .... | 3278 | newer