Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live

Mzumbe,Brazil wazindua kozi ya kusimamia miradi mikubwa

$
0
0
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Joseph Kuzilwa (kushoto) akizungumza siku ya uzinduzi wa kozi mpya kusimamia miradi mikubwa ya kimataifa iliyoanzishwa na Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Taasisi ya ISAE ya Brazil. Wa pili kustoto ni Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Andrew Mbwambo, Mratibu wa Taasisi hiyo ya Brazil Bi. Rebecca Giese (kulia) na Prof. Wanderlei Marinho da Silva wa taasisis hiyo (wa pili kulia).
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Joseph Kuzilwa (kulia) akipokea nyaraka mbalimbalikwa ajili ya kufundishia kutoka kwa Mratibu wa Taasisi ya ISAE ya Brazil, Bi Rebecca Giese wakati wa siku ya uzinduzi wa kozi mpya kuhusu usimamizi wa miradi mikubwa ya kimataifa jana jijini Dar es Salaam. Kozi hiyo imeanzishwa na Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Taasisi ya ISAE ya Brazil.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Joseph Kuzilwa (kushoto) akifuatilia jambo wakati wa uzinduzi wa kozi mpya na ya kwanza ya kimataifa ya maswala ya kusimamia miradi mikubwa ya kimataifa iliyoanzishwa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Taasisi ya ISAE YA Brazil. katikati ni Profesa Wanderlei Marinho da Silva wa taasisis hiyo ya Brazil na kulia ni Mratibu wa Taasisi hiyo, Bi. Rebecca Giese.

Naibu waziri wa maji atembelea miradi ya maji Kiliwater

$
0
0
Afisa uhusiano wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) Dollah Kilo akifurahia jambo na naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge wakati akitembelea tangi la maji la kampni ya maji ya Kiliwater wilayani Rombo.
Tangi la maji la Kampuni ya Kiliwater linalohifadhi maji kwa ajili ya wakazi wa wilaya ya Rombo.
Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge akipanda katika ngazi ya tangi la maji la kampuni ya Kiliwater kujionea hali ya ujazo wamji ikoje katika tangi hilo.
Naibu wziri wa maji Dk Binilith Mahenge akizungumza na watendaji wa maji wilaya ya Rombo juu ya tangi la maji la kampuni ya Kiliwater.
Naibu wziri wa maji Dk Binilith Mahenge akitizama sehemu ya kuchanganyia dawa katika tangi la maji la kampuni ya maji la Kiliwater.
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji na maji safi mjini Moshi Cyprian Luhemeje akiongea jambo mbele ya naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge mara baada ya kutembelea miradi ya maji katika wilaya ya Rombo. Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jamii ,Moshi.

Ujumbe wa Benki ya CRDB wakutana na Dk.Shein,Zanzibar

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya CRDB Dk.Charles Kimei,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Ujumbe wa Benki ya CRDB,ukiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Dk.Charles Kimei,(wa pili kulia) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

SHUKRANI

$
0
0
Familia ya Marehemu Constantine L.Mavere wa Tabata Chang’ombe Dar Es Salaam,inatoa shukrani kwa wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kumuuguza mpendwa wetu Constantine hadi alipofariki Dunia Tarehe 21.06.2013 na kupumzishwa katika nyumba ya milele Tarehe 24.06.2013 huko Kondoa.

Ni vigumu kuwataja wote lakini shukrani za pekee ziwaendee :

1.Madaktari na wauguzi wa Kinondoni Hospital (Kwa Dr.Mvungi) na kwa namna ya pekee Dr.Ally Mwanga.
2.Watumishi wa kiroho (Mapadre) Parokia ya Kristu Mfalme Tabata DSM na Parokia ya Mt. Paulo wa Msalaba Kondoa.
3.Msajili na wafanyakazi wa Mahakama ya Biashara
4.Majirani,Ndugu,Jamaa na Marafiki wa Dar Es Salaam,Dodoma,Arusha,Singida na Kondoa.

Familia inawakaribisha kwenye Ibada ya Misa ya shukrani itakayofanyika nyumbani kwa Marehemu Tabata Chang’ombe Dar Es Salaam Tarehe 03.08.2013 saa 5.00 asubuhi.

KARIBUNI SANA
BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIPEWE SIFA
AMEN

WADAU WA SOKA SONGEA KUJADILI UREJESHWAJI WA MAJIMAJI LIGI KUU TANZANIA BARA

$
0
0
Kampuni ya Tanzania Mwandi ikishirikiana na Majimaji FC, imeandaa mkutano wa wadau wote wa soka mkoani Ruvuma chini ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Said Mwambungu, mkutano utakaofanyika katika ukumbi wa Centenary tarehe 10. 08. 2013, kuanzia saa 2 asubuhi.

Lengo kubwa la mkutano ni kurejesha makali ya 1985, 1986 na 1998 kwa klabu ya soka ya Majimaji kwa kuiunda upya kiuchumi chini ya mfumo wa Kampuni, kuijengea uwezo wa kimkakati na kiuendeshaji ili iweze kushiriki kwa mafanikio Ligi Daraja la Kwanza na hatimaye kurejea Ligi Kuu msimu ujao.

Itakumbukwa kuwa Majimaji FC ni klabu ambayo imezalisha magwiji wengi wa soka Tanzania kama Abdala Kibadeni 'Mputa', Madaraka Suleimani 'Mzee wa Kiminyio', Peter Tino, Steven Mapunda 'Garincha', Hamis Gaga, Idd Pazi, Omary Hussein 'Machinga' na Mdachi Kombo na ni klabu ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa kwa Simba na Yanga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya Habari na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Mwandi, Bwana Teonas Aswile amewaalika wafadhili na wadau wote wenye mapenzi mema na Majimaji FC kujitokeza na kushiriki katika zoezi la mjadala wa muundo mpya wa Majimaji na hata kununua hisa kwani sasa Majimaji Kampuni haitakuwa na longolongo zozote.

“Binafsi nawahimiza wafadhili wa soka kwamba hii ni fursa adimu nyingine ya kuwekeza fedha zao mahali salama. Majimaji itakuwa ikiendeshwa kikampuni na miradi mbalimbali itaanzishwa na klabu ikiwemo upande wa ukandarasi na kuuza wachezaji nje ya nchi. Kwahiyo atakayenunua hisa atafaidika mara mbili.” alisema Teonas Aswile.

Akizungumzia wachokoza mada wakuu wa Majimaji Revival Conference, Aswile amesema kuwa Wakala wa Kimataifa wa FIFA na Mwanasheria Maarufu nchini, Dkt Damas Ndumbaro pamoja na Bwana Silas Mwakibinga, mhasibu na mdau mkubwa wa michezo ambaye ameshashika nafasi mbalimbali.

Kwa sasa maandalizi kwaajili ya Mkutano wa Wadau wa Majimaji FC “Wanalizombe” yanaendelea vyema na wanaohitaji taarifa wanaweza kuwasiliana na Bwana Nasib Mahinya kwa 0655 468800.

Pia viongozi wa Majimaji FC kama Katibu Mkuu Majimaji FC 0752 622887

WAZIRI MKUU WA THAILAND Yingluck Shinawatra ATUA DAR LEO KWA ZIARA YA SIKU TATU

yale yaleeeeee...uendeshaji hatari mlima kitonga

$
0
0
 Basi la Shining Star likitelemka mlima Kitonga bila kujali usalama barabarani
 Na hii ni baada ya dakika tatu au tano na ikanusurika ajali ya USO kwa USO na basi nyingine. Hapo ni Kitonga vile vile, hawa madereva hawawajibishwi?
Basi namba  T484 AXV  la kampuni ya Hood number 61 Kama Kwenye Picha iki overtake hapo kitonga Leo Majira ya saa Saba mchana na baada ya dakika tatu basi nyingine hapo juu ilifnaya kitendo kile kile na kunusurika ajali USO kwa USO na basi nyingine Hapa ni kitonga

FOR THE FIRST TIME IN TANZANIA… BROADCAST LIVE IN WOGMEDIA

$
0
0

INTRODUCING LIVE WEBCASTING / STREAMING SERVICES

HAVING A SPECIAL EVENT such as …


Corporate Events• Training Seminars • Shareholder Meetings

Marketing & Promotional Campaigns • Press Conferences

Awards Ceremonies • Annual- General-Meetings • Product Launch   • Sports Events • Weddings • Funerals

• Graduation Ceremonies


WATCH EVENTS LIVE FROM 
ANYWHERE EVERYWHERE……

VISIT


WWW.WOGMEDIA.COM or info@wogmedia.com or call 0712617373


WASHINDI WA TUZO ZA HABARI ZA TANAPA WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA KRUGER NCHINI AFRIKA YA KUSINI

$
0
0
Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA wakiwa katika lango la kuingilia Hifadhi ya Taifa ya Kruger kwa ziara ya kujifunza. Kutoka kushoto ni Phinias Bashaya (Mwananchi); Jasper Masika Mtanzania anayeishi Johannesburg; Lilian Shirima (TBC 1); Albano Midello (Nipashe); Alex Magwiza (TBC Taifa) na Festo Sikagonamo wa ITV.
Swala wakivinjari katika Hifadhi ya Kruger.
Twiga Hifadhini Kruger.

FFU wa Ngoma Africa Band Yafanya kweli Jambo Seeheim Festival,Ujerumani

$
0
0
Si nyingine bali ni Ngoma Africa band a.k.a FFU ughaibuni,bendi maarufu yenye ngome yake kule Ujerumani,chini ya kamanda wao Ras Makunja,bendi hiyo imefanya kweli siku ya jumapili 28.08.2013 katika maonyesho ya Jambo Seeheim Festival,yaliyofanyika mjini Jugenheim-Seeheim,nchini Ujerumani kuliko ungua shoka mpini ukabaki,kama kawaida yake Ngoma Africa band ilianza kuwasha muziki mkali na kuwatia kiwewe washabiki waliokuwapo katika onyesho hilo,bendi hiyo yenye utajili wa wanamuziki wenye vipaji akiwemo afande Christian aka Chris-B, na yule kijana Jonathan Souza a.k.a Jo Jo. Usikose kupata burudani za FFU at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com
Ngoma Africa Band Live at jambo seehim,Germany 28.07.2013.
FFU kazini kwao (mwenye miwani) ni kamanda Ras makunja.
Chipukizi wa FFU alikuapo.
Guitarist Matondo Benda.
Mr.Jo Jo, Mkaanga Chips wa Ngoma AFrica.

MAFUNZO ELEKEZI KWA BODI YA WAKURUGENZI YA TBC YAFANYIKA MKOANI MOROGORO

$
0
0
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania ( TBC) kuanziaa Julai 29, mwaka huu wamekutana Mkoani Morogoro kwa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo elekezi ya siku tatu kwa Kamati mbili za Bodi hiyo ambazo ni Kamati ya Ukaguzi na Kamati ya Fedha na Utawala .

Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Clement Mshana, alibainisha hayo Julai 29, mwaka huu alipowakabirisha wajumbe wa Bodi hiyo inayoogozwa na Mwenyekiti wake Profesa Mwajabu Possi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TBC, mafunzo ayo yamekuja wiki mbili baada ya mafunzo mengine kwa wajumbe wa Bodi juu majukumu ya Bodi katika Taasisi hiyo.

Katika mafuno hayo , mgeni rasmi alikuwa ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali , Mohamed Mtonga.
Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Clement Mshana akitoa nasaha zake kwa wajumbe wa Bodi ya TBC wakati wa Mkutano wao uliofanyika kuanzia Julai 29,Mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TBC, Profesa Mwajabu Possi akipokea vitabu vya mwongozo wa ukaguzi kutoka kwa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TBC, Profesa Mwajabu Possi akiwa na vitabu vya mwongozi wa ukaguzi.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara za TBC na wajumbe wa Bodi wa wakimsikiliza mgeni rasmi siku ya kufungua mafunzo elekezi ya siku tatu kuanzia Julai 29, 2013.
Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Clement Mshana ( kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wajumbe wa Bodi hiyo pamoja na Mgeni Rasmi, Mohamed Mtonga ( wapili kutoka kilia).Picha na John Nditi,Globu ya Jamii,Morogoro.

Article 4

MABONDIA WA BIGRIGHT BOXING GYM WAJIFUA KUWAKABILI WAPINZANI

$
0
0
Mabondia wa bigright boxing ya mwananyamala wapo kambini wakiendelea kujifua kwa ajili ya kuwakabili wapinzani wao ambao watazichapa nao katika wakati tofauti na maeneo mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi. 
 Mabondia hao ni issa omar anaetarajiwa kuzipiga katika ukumbi wa Government complex nchini zambia na Pethias Chisonga wa Zambia chini ya uratibu wa Exodus Stable ya nchini humo. Hapa Dar es salaam Friends Corner hotel Mustafa Doto atazipiga na Rajab Mjeshi, Martin Richard na Mbena Rajab wao watakuwa mkoani Tanga huku Zumba Kukwe akizipiga Kibaha na mabondia waliobaki watamsidikiza Daudi Anthony’Odinga’ kuzipiga na Tom-po katika ukumbi wa Eagles pub Bagamoyo. Katika mapambano ya Bagamoyo yameratibiwa na Tan academy chini ya kiongozi wake Japhet Kaseba yatakuwa na ushindani mkali sana kwa wanafunzi watano wa Kaseba watakapozipiga na wanafunzi wa Bigright nje ya mkoa wao
 Baadhi ya mabondia toka kambi ya Bigright boxing club wakiwa  kambini kwenye gym yao Mwananyamala jijini Dar es salaam wakijiandaa kwa ajili ya mapambano yatakayofanyika siku ya idd.
 mabondia wa bigright boxing wakiwa mazoezini katika gym yao iliyoko mwananyamala
 Sparring ya nguvu
 Big right Ibrahim kamwe akiwa na vijana wake gym
 Tizi likiendelea
Vijana wakiwa tayari kwa mapambano

VIJANA WAASWA KUJITAMBUA NA KUTHUBUTU ILI KUJILETEA MAENDELEO

$
0
0
Waziri wa Habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk Fenella Mukangara akizungumza na washiriki wa kambi ya vijana leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua rasmi kambi hiyo ambayo imeanza tarehe 29 na inatarajiwa kumalizika tarehe 2 Agosti.Kambi hiyo ya vijana ya Dunia imeandaliwa na taasisi isiyo ya Kiserikali International Youth Fellowship(IYF) kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Baadhi ya washiriki wa kambi ya vijana wakisikiliza hotuba ya Mheshimiwa Waziri Fenella Mukangara hayupo pichani alipokuwa akifungua rasmi kambi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha sanaa kutoka IYF wakicheza muziki wa kitamaduni kutoka Korea mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk Fenella Mukangara wakati wa hafla ya ufunguzi kambi ya vijana leo jijini Dar es Salaam.
Waimbaji wa Kwaya ya kimataifa kutoka Korea Gracias wakiimba wakati wa hafla ya ufunguzi wa kambi ya vijana l;eo jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha sanaa kutoka Tanzania wakionyesha mchezo wa Tai Kondo leo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Mh. Dr. Seif Rashid Afungua Kongamano la Kujadili Dawa Bandia

$
0
0
Kongamano la siku 3 kujadili dawa bandia limefunguliwa leo na naibu waziri wa afya, Mheshimiwa Dr. Seifu Rashid. Kongamano hili linahudhuruwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali Africa zikiwamo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Botswana, South Africa, Zambia, Eritrea, Ethiopia, Madagascar, Zimbabwa, Namibia na Mozambique. Pia kuna wawakilishi toka USA na makao makuu ya shirika la afya dunia (WHO).

Wajumbe wa kongamano watapata nafasi ya kujifunza mfumo mpya wa kompyuta wa jinsi ya kutoa na kupata taarifa mbalimbali juu ya dawa bandia.

Kongamano linafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wakala wa Serikali wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), uliopo Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Mr Hiiti B. Sillo, Mkurugenzi wa TFDA akitoa utangulizi wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.
Naibu waziri, Dr. Seifu Rashid akifungua rasmi kongamano hio, kulia kwake ni Michael Deats, kutoka makao makuu Shirika la Afya Duniani (WHO)
Sehemu ya washiriki wa kongamano.
Nchi za Africa zinazowakilishwa kwenye kongamano hilo.

MAMA SALMA KIKWETE KATIKA MKUTANO WA HIGH LEVEL GROUP-GABERONE -BOTSWANA

$
0
0
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea ua mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir Seretse Khama jijini Gaberone nchini Botswana kutoka kwa binti Jessica Kissasi, anayesoma darasa la pili, Baobab International School t arehe 29.7.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Bwana Christopher Castle,Mkuu wa Idara ya HIV and Health Education kutoka Makao Makuu ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yaliyoko Paris nchini Ufaransa wakati Mama Salma alipowasiri kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir Seretse Khama huko Botswana tarehe 29.7.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia wajumbe wa mkutano wa sikuk mbili wa “High Level Group” kutoka Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika unaofanyika katika hoteli ya Lansmore Masa Square jijini Gaberone nchini Botswana.

COSTECH, BRELA, JPO, AND WIPO ORGANISE A THREE DAY WORKSHOP ON TECHNOLOGY AND INNOVATION SUPPORT CENTER’S (TISC) at COSTECH BUILDING ON 30TH JULY 2013

$
0
0
Acting Chief executive officer of the Business Registrations and Licensing Agency(BRELA) Leonider Kishebuka (first left) gives the opening remarks during the Technology and Innovation Support Centre (TISC) workshop at COSTECH hall on 30thJuly 2013.Looking on are Minister for Communication, Science and Technology Prof Makame Mbarawa,COSTECH Director General Dr Hassan Mshinda and Dr Gerhard Fischer the representative of the Director General of the World Intellectual Property Organization (WIPO).
Minister for Communication,Science and Technology Prof Makame Mbarawa (centre) follows the opening remarks during the Technology and Innovation Support Centre (TISC) workshop.
COSTECH Director of Finance and Administration, Mr Shaaban Hussein (with a black suit) takes a look at the power point presentation during the Technology and Innovation Support Centre (TISC) workshop.The setting up of the Technology and Innovation Support Centers (TISCs) in Tanzania is one of the strategy to put in place facilities that would give researchers and technology developers access to all technical information available in patent documents as well as to scientific journals.
A cross section of the participants in the Technology and Innovation Support Centre (TISC) workshop.

NBA STAR STEVE CURRY KUENDESHA CLINIC YA VIJANA 100 DON BOSCO OYSTER-BAY 1/Aug, 2013

$
0
0
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania(TBF) Phares Magesa leo asubuhi akiongea na wapenzi wa michezo kupitia Radio kuhusu maendeleo ya Mchezo huo nchini ikiwemo ziara ya mchezaji Nyota wa NBA Steve Curry ambae ataendesha clinic ya vijana wadogo 100 tarehe 1 Aug, viwanja vya Don Bosco Oysterbay, wote mnakaribishwa.

NIDA yaendelea na zoezi la utoaji wa Vitambulisho vya Taifa

$
0
0
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) hivi sasa inaendesha zoezi la uchukuaji alama za vidole, kuweka saini za kielektroniki na kuwapiga picha wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam, ikianzia na wilaya ya Temeke. Hivi sasa zoezi hili linafanyika katika kata za Charambe, Kiburugwa, Mbagala Kuu, Toangoma na Kijichi.

Amani SACCOS ya NDANDA Hospital Masasi yapata mkopo wa Mil 700

$
0
0
Wanachama wa NSSF wa Amani SACCOS ya NDANDA Hospital wamepata Mkopo wa mil 700 chini ya mpango mahsusi wa kukopesha wanachama wa NSSF kwa kupitia SACCOS zao kwa madhumuni ya kupunguza wanachama kujitoa kutoka kwenye Mafao na kuongeza wigo wa wanachama ili kujenga maisha yao ya sasa na Baadae.
Mgeni Rasmi Mhe. Waziri wa Kazi na Ajira Mama Gaudentia Kabaka akikabidhi hundi hiyo kwa Dkt. Peter Shayo Mwenyekiti wa Amani SACCOS katika hafla fupi iliyofanyika MSEMO Hotel and Resort mjini Mtwara.
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live




Latest Images