Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 208 | 209 | (Page 210) | 211 | 212 | .... | 3285 | newer

  0 0

   MBUNGE wa Chalinze, wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Saidi Mwanamdogo, akizungumza na wanachama wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanambwewe waishio Dar es Salaam (MNDF), leo katika ukumbi wa Shule ya Msingi Ali Hassani Mwinyi, mjini Dar es Salaam. Wanachama hao walimwalika kwenye kikao chao cha kujadili jinsi ya kuuendesha mfuko huo kwa manufaa ya wananchi wengi.
   Katibu wa wanachama wa Mfuko wa Maendeleo ya wanamtandao wa Mbwewe waishio Dar  es Salaam, Hassani Msonde akizungumza mwanzoni mwa kikao
   Mwenyekiti wa Umoja huo, Rajabu Papa akifungua kikao hicho
   Mjumbe wa Kamati ya Umoja huo, Fatuma Kikwappe akisoma risala huku viongozi wakimsikiliza kwa makini akiwemo Mbunge Bwanamdogo.
  Kisha akaikabidhi risala hiyo kwa Mbunge wa Chalinze, Saidi Mwanamdogo
   Mbunge Saidi Mwanamdogo akiwakabidhi dola za Marekani, viongozi wa umoja huo, ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya kufanikisha usajili.
   Mwenyekiti akimkabidi Mbunge Katiba ya Umoja. NA theNkoromo Blog

  0 0
 • 07/28/13--14:52: Article 4
 • Short Course Announcement – September 2013


  STATISTICAL ANALYSIS USING MS EXCEL 2010


  Duration: 4 days

  Dates: September 17 – 20, 2013

  Price: 300,000 TZS (excluding lunch)

  Place: School of Social Sciences (MRL 4)-UDOM-Dodoma


  Course outline

  This training is organized by the department of Statistics, College of Natural and Mathematical Sciences of the University of Dodoma (UDOM).  


  This is a four days course designed to introduce Excel as a data analysis tool. It is designed for both non-statisticians and statisticians who wish to develop their basic statistical skills and understanding. By the end of the course, participants will be able to acquire some basic knowledge of data management using excel 2010 and understand some basic statistical concepts relating to data analysis. The course will cover;

  ·   Data entry

  ·   Descriptive data analysis

  ·   Creation of pivot tables

  ·   Inferential data analysis (causal-effect relationship among variables) 


  Mode of payment: All payments should be done through;

  Account Name: College of Natural and Mathematical

       Sciences

  Account no:      0150221567000

  Bank:                        CRDB


  Please confirm fee payment and your participation by sending SMS or an email indicating your name using contact below.


  Participants should come with their laptops and bank deposit slip. Certificate of attendance will be awarded.


  Contact person:

  Josephat Peter

  Mobile: 0787288998 or 0717999012  0 0

  Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk.Mohamed Gharib Bilal akifungua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi kwa ujenzi wa jengo la Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Shule ya Msingi Kisiwandui mjini Zanzibar juzi. Kushoto kwake ni Mbunge wa Kikwajuni, Hamadi Yussuf Masauni. Vodacom Foundation imesaidia saruji yenye thamani ya Sh.Milioni 10 kufanikisha ujenzi huo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano,, Dk Mohamed Gharib Bilal akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Shule ya Msingi Kisiwandui katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, mjini Zanzibar juzi. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Kikwajuni Hamadi Yussuf Masauni na Meneja wa Vodacom Hassan Saleh.
  Mbunge wa Kikwajuni, Hamadi Yussuf Masauni akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal (wa pili kulia) kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Shule ya Msingi ya Kisiwandui, mjini Zanzibar juzi.
  Mwenyekiti wa Vodacom Foundation, Hassan Saleh (kulia) akikabidhi moja ya kompyuta kwa Makamu wa Rais wa Tanzania Dk.Mohamed Gharib Bilal kwa ajili ya Shule ya Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Chwaka hafla iliyofanyika wakati wa uzinduzi wa kituo kama hicho katika Shule ya Msingi Kisiwandui Mjini Zanzibar juzi.
  Makamu wa Rais, Mohamed Gharib Bilal (kulia), akiagana na Mbunge wa Kikwauni, Hamadi Yussuf Masauni mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Kituo cha Habari na Mawasiliano katika Shule ya Msingi ya Kisiwandui, mjini Zanzibar juzi.  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akiandika maelezo ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa wakati alipokuwa anachangia mada ya Mustakabali wa Amani na Usalama wa Taifa kwa miaka 50 ijayo. Waziri Nchimbi licha ya kuzijibu hoja mbalimbali katika kongamano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisisitiza kuwa, watakaotaka kufanya maandamano ya aina yoyote ile nchini ni lazima wafuate sheria.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akijibu hoja mbalimbali za washiriki katika Kongamano la Amani na Usalama wa Taifa kwa miaka 50 ijayo. Waziri Nchimbi licha ya kuzijibu hoja mbalimbali katika kongamano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisisitiza kuwa, watakaotaka kufanya maandamano ya aina yoyote ile nchini ni lazima wafuate sheria.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu baada ya kuzijibu hoja mbalimbali za washiriki katika Kongamano la Amani na Usalama wa Taifa kwa miaka 50 ijayo. Waziri Nchimbi licha ya kuzijibu hoja mbalimbali katika kongamano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisisitiza kuwa, watakaotaka kufanya maandamano ya aina yoyote ile nchini ni lazima wafuate sheria.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wapili kushoto) akifurahi jambo wakati alipokuwa akizungumza na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa mara baada ya kufungwa kwa Kongamano la Amani na Usalama wa Taifa kwa miaka 50 ijayo. Waziri Nchimbi licha ya kuzijibu hoja mbalimbali katika kongamano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisisitiza kuwa, watakaotaka kufanya maandamano ya aina yoyote ile nchini ni lazima wafuate sheria. Picha na Felix Mwagara. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Asalaam Alaykum Warahmatu llahi Wabarakatu

  Ama Baada ya Salamu naomba toa Shukran zangu za dhati kwako Kaka Michuzi na Timu Nzima ya Blog ya Jamii kwa kutuwekea Ujumbe huu Pili naomba Niwatakie kheri za Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani Wadau wote pamoja na timu yako.

  Tumuombe M/Mungu azipokee Funga Zetu na Dua zetu kwa Ujumla.

  Dhumuni kuu la kuandika Makala hii Nikutaka kukumbushana Siku hii Muhimu katika Siku ambazo Ndio zimeufanya Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani kuwa Mwezi Mtukufu nayo Ni Siku ya LAYLATUL QADIR (USIKU WA CHEO) ambayo ipo katika Kumi hili la Mwisho ambalo tumelianza.

  LAYLATUL QADIR (USIKU WA CHEO) NI USIKU AMBAO UNAPATIKANA NDANI YA MWEZI HUU MTUKUFU WA RAMADHANI NDANI YA KUMI LA MWISHO MTUME (S.A.W) LILIPOKUWA LIKIINGIA KUMI LA MWISHO ALIKUWA AKIZIDISHA IBADA KWA SANA NA KUWA AMSHA WATU WAKE ( ALHAL BAYTI ) KWA AJILI YA KUFANYA IBADA ZAIDI KATIKA KUMI HILO.

  LAYLATU QADIR SI MWEZI 27 TU ILA WENGI WA WANACHUONI WAMEJITAHIDI KUWA HIYO NDIO SIKU YA LAYLATUL QADIR

  SIKU HII HUENDA IKAPATIKANA NDANI YA MWEZI 21 , 23 , 25 , 27 , 29 , NI JUU YETU NDUGU ZANGU KUITAFUTA SIKU HII KWA KUFANYA IBADA KWA WINGI NDANI YA KUMI LA MWISHO ILI M/MUNGU ATUWEZESHE KUIDIRIKI SIKU AMBAYO UBORA WAKE KWA WENYE KUUDIRIKI USIKU HUU KWA IBADA NI ZAIDI YA MIEZI 1000 NA HUSHUKA MALAIKA NDANI YA SIKU HIYO KWA IDHINI YA M/MUNGU NA MALAIKA JIBRIL HUSHUKA.

  NI JUU YETU KUHAMASISHANA NAKUKUMBUSHANA KUWA SIKU HII NI SIKU MOJA NA NI MUHIMU SANA ILI KUPATA KUMUOMBA M/MUNGU NA KULIOMBEA TAIFA LETU LA TANZANIA KWA M/MUNGU KUEPUKIKA NA KILA AINA ZA FITNA .

  Katika Mambo ambayo yame kokotezwa (Sunnah) katika Kumi hili la Mwisho Ni Kikazi cha Itkafu na Maana ya ITKAFU KI SHAARIA ni Kushikamana na Msikiti na kukaa ndani yake pasina ya kutoka kwa ajili ya kujikurubisha(kuwa karibu) kwa M/Mungu Mtukufu .

  Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu ziwe juu yake alikuwa akikaa itikafu katika kila Mwaka ndani ya kumi la mwisho la Ramadhani na Mwaka alio fariki alikaa itikafu muda wa siku ishirini Kama ilivyo pokelewa na Bukhari.

  Vile vile Maswahaba wa Mtume na Wake zake walikaa nae itikafu na walikaa Itikafu baada ya mtume kufariki.

  M/MUNGU AKIKUBARIKI KUIDIRIKI USIKU HUU WA CHEO SOMA DUA HII KWA MAELEKEZO YA MAMA AISHA alimuliza Mtume Jee? tukiidiriki LAYLATUL QADIR (USIKU WA CHEO) tufanye nini ? Mtume akajibu kithirisha kusema NASH-HADU ANLAA ILAAHA ILLA ALLAHU NASTAGHFIRULLAH NAS'ALUKAL JANNATA WANAUDHUBIKA MINA NNAAR ALLAHUMA INNAKA AFUWUN TUHIBUL AFWAA FA'AFUANNAA YAA KARIYMAL AFWU ". Kama alivyosema Mtume.

  MUNGU NDIYE MJUZI WA HII SIKU NI JUU YETU NA FAMILIA ZETU KUZIDISHA IBADA .

  Kwa Fikra zaidi fatilia katika Ukurasa wetu wa Facebook : Kijana wa Kiislam Tanzania au ID Fb : Kijana wa Kiislam Dsm Whatsapp :+201110189580

  Na:-
  Ghalib Nassor Monero l Azhariy.
  Al- Azhar University.

  0 0


   kocha kwame mkuluma kulia akimwelekeza Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' jinsi ya kutupa makonde mazito mazito.


   Bondia  Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' yupo kambini kwa ajili ya kupambana na bondia Bahati Mwafyela mpambano utakaofanyika siku ya sikukuu ya Iddi pili jijini Dar es salaam,katika ukumbi wa friends Corner Manzese.

   akizungumzia maandalizi ya mpambano huo mtaalishaji wa Mpambano huo,Waziri Rosta amesema mpambano huo wa uzito wa juu umekuwa gumzo katika jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake kwani mabondia hao wanatafutana kwa muda mrefu sana na sasa wamekutana kwa ajili ya mchezo huo.

  Mpambano huo wa raundi 8 siwakukosa kwani ndio mpambano pekee kwa mwaka huu kukutanisha uzito wa juu kwani mabondia wa uzito huu  wanaotamba viwango vyao ni vidogo ukizingatia kuwa wapo wachache nchini.

  aliongeza kuwa mbali na mpambano huo kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia chipkizi na wanaotamba hapa nchini.

  Na kwa upande wa kocha anaemnoa bondia  Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' amesema kuwa bondia wake alikuwa na manyama nyama mengi lakini kwa sasa hakuna kutokana na mazoezi anayompatia kwani kwa sasa dozi yake ni kutwa mara tatu na mpaka siku ya mchezo nahisi mambo yatakuwa safi.

  Mpambano huo utakao sindikizwa na mabondia Hassani Mandula atakae pambana na Twalib Mchanjo na Fadhili Majia atakae menyana na Ally Mahiyo na Mustapha Doto atapambana na Hashimu Mjeshi mapambano yote ya utangulizi itakuwa ni ya raundi sita.

  0 0

  Blogu yako ya 
  inayotoa habari za usafiri wa anga, mazingira, maliasili na utalii, inakuletea kampeni ya ‘Share your experince’.
  Ambapo wadau, watu binafsi na makampuni ya tours mnaombwa ku-share picha zenu za good moments, matukio mbalimbali ya safari za kwenye hifadhi na vivutio vingine vya utalii, picha za safarini kwenye ndege, ushuhuda wa safari zenu (testimonies) na picha za mazingira mbalimbali.
  Share experience yako, kupitia blog yako ya tabianchi, emailkingkahindi@gmail.com, au tupia kwa fb tabianchi
  Asante sana!

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bi. Juliet Kairuki (kushoto) akimsikiliza kwa makini mmoja wa maafisa wa juu toka muungano wa makampuni ya Dangote, Bw. DVG Edwin mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Baadhi ya maafisa wa kampuni hiyo kubwa barani Africa walikua nchini kwa ziara ya kikazi.  Kampuni hiyo inaendelea na ujenzi wa kiwanda kikubwa cha simenti mkoani Mtwara.


  0 0
 • 07/29/13--01:58: TANZIA
 • Bw. Samson Kamalamo anasikitika kutangaza kifo cha Baba yake Mzazi Bw. Samwel Bulimbe Kamalamo kilichotokea Julai 27, 2013 jijini Dar es Salaam. Mipango ya Mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, Mtaa wa Daima jijini Dar es Salaam. 

  Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki popote walipo. Maziko yanatarajiwa kufanyika katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Julai 31, 2013. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, 

   Amen.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho kikwete akiongea mchana huu na viongozi mbalimbali wa kitaifa na wa mkoa wa Kagera wakati wa kikao cha majumuisho baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara yake ya kikazi ya siku sita mkoani humo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, mwishoni mwa wiki uliandaa hafla fupi ya kumuaga Afisa mwenza Bw. Modest Mero na Familia yake, Bw. Mero aliteuliwa hivi karibuni na Mhe. Rais Jakaya Kikwete kuwa Balozi wa Tanzania Geneva, hafla hiyo ilifanyika katika Makazi ya Balozi Tuvako Manongi yaliyoko 86 Jadison. zifuatato ni baadhi tu ya picha ya hafla hiyo iliyoambatana na nyama choma na chakula cha jioni.
  Moja ya Zawadi ambazo wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa waliyomizawadia Bw. Mero kama kumbukumbu, kutoka kushoto ni Balozi Tuvako Manongi na mkewe Upendo, Balozi Modest Mero na mkewe Rose.
  Balozi Modest Mero akitoa shukrani zake kwa niaba ya familia yake nyumayake ni watoto wake na aliyekaa kushoto ni Bw. Ken Kanda Balozi wa Ghana katika Umoja wa Mataifa.
  Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, akizungumza machache wakati wa hafla hiyo ambapo alimuelezea Balozi Mero kama mchapa kazi , anayejituma na wakati wowote alipohitaji au kuulizwa chochote alilkuwa tayari kukifanya au kujibu.
  Balozi Modest Jonadhan Mero akiwa na Mke wake, Bibi Rose Mero.


  0 0

  Ndugu Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam,

  Napenda nichukue fursa hii kuwajulisha rasmi kwamba Nchi yetu imepata heshima ya kutembelewa na Waziri Mkuu wa Thailand ambaye atawasili Nchini tarehe 30/07/2013. Ziara hii ni ya kikazi (state visit) na atawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kumbukumbu ya Mwalimu J. K. Nyerere majira ya saa 6:30 mchana na kulakiwa na mwenyeji wake Mhe. Rais wetu mpendwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatana na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Mkoa.

  Ndugu Wananchi,
  Baada ya kuwasili Mhe. Waziri Mkuu wa Thailand atakagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake na pia atapata fursa ya kukagua vikundi mbalimbali vya ngoma ambavyo vitakuwa vikitumbuiza na kutoa burudani kwa Mgeni wetu na msafara wake.

  Ndugu Wananchi,
  Mgeni wetu baada ya kukagua vikundi vya ngoma na burudani ataondoka kuelekea Ikulu kupitia barabara ya Nyerere, Railway, Gerezani, Sokoine Drive hadi Ikulu. Akiwa Ikulu atasaini mikataba mbalimbali kati ya Serikali ya Tanzania na Thailand. Usiku atashiriki katika dhifa maalumu iliyoandaliwa na Mwenyeji wake.

  Ndugu Wananchi,
  Tunaomba radhi kwamba barabara hizi nilizozitaja zitafungwa kwa muda kupisha misafara ya Viongozi wetu Wakuu watakaoelekea Uwanja wa Ndege wa Kumbukumbu ya Mwalimu J. K. Nyerere kumlaki Mgeni wetu hususan barabara ya Nyerere kuanzia saa 6.00 mchana hadi saa 7.30 mchana.

  Ndugu Wananchi,
  Tarehe 31/07/2013 Waziri Mkuu wa Thailand atatembelea Mbuga za Wanyama za Serengeti.Tarehe 01/08/2013 atarejea Dar es Salaam na kuagwa rasmi katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere na kuendelea na ziara yake huko Uganda.

  Ndugu Wananchi,
  Kama ilivyo ada tunaombwa kumlaki mgeni wetu kwa shangwe na bashasha katika maeneo yote atakayopita. Asanteni kwa kunisikiliza.

  Saidi Meck Sadiki
  MKUU WA MKOA

  DAR ES SALAAM

  0 0

  Wafanyakazi wa Benki ya NBC kitengo cha operesheni, wakipozi kwa picha na watoto wanaolelewa katika kituo cha Ijango Zaidia Orphanage cha Sinza walipokwenda kupeleka msaada wa vyakula, sabuni, mafuta ya kupikia na vyandarua ikiwa ni moja ya mikakati ya NBC kurudisha sehemu ya faida waipatayo katika jamii. Hafla ilifanyika kituoni hapo jijini Dar es Salaam juzi. Wengine ni watumishi wa kituo hicho.
  Mkurugenzi wa Uendeshaji na Huduma wa Benki ya NBC Tanzania, Cornie Loots (kulia) akikabidhi msaada wa vyakula, mafuta ya kupikia, sabuni na vyandarua kwa Mkuu wa kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia Orphanage , Bi. Zaidia Nuru Hasani, vilivyotolewa na NBC kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi.
  Mtoto anayelelewa katika kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia Orphanage, Ramia Mahmoud , akipokea mafuta ya ngozi kwa niaba ya wenzake vyaliyotolewa msaada na Benki ya NBC kutoka kwa mfanyakazi wa benki hiyo, Ernest Paulo Mbepera (kulia) kituoni hapo, Sinza, jijini Dar es Salaam. Benki hiyo pia ilikabidhi msaada wa vyakula, mafuta ya kupikia, sabuni na vyandarua.
  Mfanyakazi wa Benki ya NBC, Mwanaisha Nassoro Ayosi (kulia) akikakabidhi misaada iliyotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia Orphanage, kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi.
  Mtoto anayelelewa katika kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia Orphanage, Amina Twahilu, akipokea moja ya vyandarua kwa niaba ya wenzake vilivyotolewa msaada na Benki ya NBC kutoka kwa mfanyakazi wa benki hiyo, Anyelwisye Enock Mwakatobe (kulia) kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi. Benki hiyo pia ilikabidhi msaada wa vyakula, mafuta ya kupikia na sabuni.

  0 0

  After breaking the rules relating to violence and provocation, tonight (Sunday July 28) saw Big Brother The Chase housemate Nando disqualified from the 91 day reality show.

   This season Big Brother has been issuing strikes to housemates for inappropriate behavior with three strikes resulting in disqualification from the game. 

  The 22-year-old from Tanzania was issued a first strike in week five of the show for carrying a knife to a Big Brother party. Following an altercation with fellow housemate Elikem late on Friday night, today Big Brother issued two more strikes against him – one for provocation and one for concealing a pair of scissors in his bed after the argument. 

  With three strikes, Big Brother tonight disqualified Nando from the game. For his part in Friday’s altercation, Elikem was also issued a strike by Big Brother, his first in the game. 

  Given that M-Net and show producers Endemol, are committed to ensuring the safety of all housemates in the Big Brother house, they view such incidents in a serious light and will continue to take the necessary actions against housemates who break the strict rules prohibiting violence in the Big Brother house.

  0 0

  IMG_1336
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na uongozi wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya iliyopo Msasani Bonde la Mpunga Ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Spika mbili, Vipaza sauti viwili (Microphones) pamoja na Amplifaya ambavyo vitatumika kuendeshea shughuli mbalimbali za kueneza mafunzo ya dini kwa jamii na watoto wanaosoma chuoni hapo. Vifaa hivyo vimetolewa na mdau mpenda maendeleo kupitia kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
  IMG_1339
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa pamoja na Bw. Abdulmalik Ibrahim (kulia) aliyemwakilishi mdau aliyetoa vifaa hivyo (jina kapuni) wakikabidhi Spika tatu, vipaza sauti viwili na Mixer kwa Katibu wa Madrasa hiyo Bw. Salim Amri (wa pili kushoto) aliyeambatana na Ustaadh Nurdin Nassor Abdallah (katikati). Kushoto ni mmoja wa walimu wa madrassatul Munauwaratul Islamiya kilichopo Msasani Bonde la Mpunga Ustaadh Mohamed Kassim.
  IMG_1344
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akikagua moja vifaa hivyo alivyokabidhi leo ofisini kwake .
  IMG_1360
  Ustaadh Nurdin Nassor Abdallah wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya ya Msasani Bonde la Mpunga akitoa shukrani kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa pamoja na mdau alijitolea baada ya kupokea vifaa hivyo ambavyo amesema vitawasaidia katika kazi zao za kueneza neno la Mungu hasa kipindi hichi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwemo kuhubiri Amani nchini.
  IMG_1372
  Uongozi wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya kilichopo Msasani Bonde la Mpunga wakiomba dua za baraka kwa msaada waliopokea leo ofisini kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa.

  0 0

  Ujumbe wa Bandari ya Singapore "Port Authority of Singapore(PSA)" unatembelea Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), pichani ni wakuu wa idara mbalimbali za TPA na viongozi wa PSA wakiwa katika ziara ya Bandari ya Dar Es Salaam. Haya ni matunda ya ziara ya Mhe. Rais Kikwete aliyoifanya nchini Singapore mapema mwaka huu. TPA iko mbioni kuboresha huduma zake kwa kutumia Teknolojia ya kisasa ya TEHAMA (ICT) katika shughuli zote za kibandari, TPA itashirikiana na PSA katika eneo hili pamoja na mafunzo ya marubani, wahandisi na shughuli za utekelezaji(operations).

  0 0

  Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Luteni Kanali Lidwino Saimon Mgumba (kushoto) akimvisha cheo Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Iringa, Mrakibu Msaidizi wa jeshi hilo, Kennedy Komba katika hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji, jijini Dar es Salaam leo. Naibu Kamishna Mgumba aliwavisha vyeo maafisa hao kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Pius Makuru Nyambacha. Picha na Puyo Nzalayaimisi, Afisa Mahusiano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Makao Makuu.
  Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Luteni Kanali Lidwino Saimon Mgumba akiwaasa maafisa wa jeshi hilo waliovishwa vyeo katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es Salaam leo. Mgumba aliwaasa maafisa hao kutumia vyema vyeo na madaraka waliyopewa kwa uhadilifu na kwa kuzingatia sheria. Naibu Kamishna Mgumba aliwavisha vyeo maafisa hao kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Pius Makuru Nyambacha. Picha na Puyo Nzalayaimisi, Afisa Mahusiano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Makao Makuu.
  Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na askari wakimsikiliza kwa makini Naibu Kamishna wa jeshi hilo, Luteni Kanali Lidwino Saimon Mgumba wakati alipokuwa akiwaasa maafisa wa jeshi hilo waliovishwa vyeo katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es Salaam leo. Mgumba aliwaasa maafisa hao kutumia vyema vyeo na madaraka waliyopewa kwa uhadilifu na kwa kuzingatia sheria. Naibu Kamishna Mgumba aliwavisha vyeo maafisa hao kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Pius Makuru Nyambacha. Picha zote na Puyo Nzalayaimisi, Afisa Mahusiano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Makao Makuu.

  0 0


   Wanakijiwe kutoka kushoto ni Dotto Mwallongo, David Ndunguru na Jabir Jongo wakikutayarishia kipindi chako ukipendacho cha KIJIWE CHA UGHAIBUNI kitakachorushwa kesho Jumanne. 
   Wanakijiwe kutoka kushoto ni Libe Mwang'ombe, Kenyatta Mayanga na Mkwavi Mwinyikheri.
   Kruu nzima ya Kijiwe ikimsikiliza David Ndunguru alipokua akisisitiza jambo.

  0 0

  Na Angela Sebastian, Bukoba

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema udhaifu na uzembe unaoendelea kufanywa na watendaji wa Idara ya Uhamiaji umesababisha nchi kuwa na lindi kubwa la wahamiaji haramu kutoka katika nchi zinazotuzunguka.

  Rais Kikwete alitoa kauli hiyo kwa uchungu leo Ikulu ndogo mjini Bukoba wakati akifanya majumuisho ya ziara yake ya siku sita mkoani hapa na kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

  Alisema kwasasa Tanzania ina wahamiaji haramu zaidi ya 52,000 huku mkoa wa Kagera ukiwa na wahamiji haramu zaidi ya 36,000 ambapo ameongeza kuwa hilo ni tataizo kubwa lililosabaishwa na udhaifu wa watendaji wa idara ya uhamiaji na litaigharimu nchi yetu.

  “ Tanzania sio shamba la bibi kila mtu anaingia na kutoka na mifugo yake eti kwasababu kuna sehemu nzuri ya malisho alafu watendaji wa vijiji na wenyeviti wanawapa vibari wahamiajia hao na kuwahonga viongozi hao wa vijiji ng’ombe sana sana hawazidi wawili na nyie uhamiaji mnaona na kuyafumbia macho mnatenda dhambi kubwa asambayo inapeleka nchi yetu katika hali mbaya kwa kipindi cha miaka 50 ijayo”alisema Rais Kikwete kwa uchungu.

  “Hili sijalisema kwa mara ya kwanza,niliisha lisema hata mwaka 2008 nilipokuja Kagera na kuhutubia wilayani Muleba lakini bado mmenyamaza,kuna mtu anaitwa Katongole anaishi kule mpakani Mutukula ndiye anayeingiza wahamiaji hapa nchini ameishajua bei zenu anawahonga anaingiza watu wake,mtu anayetoa rushwa anajulikana ushahidi upo wanaohongwa wanajulikana PCCB mnafanya nini mmenyamaza tu basi kazi imewashinda”aliongeza Rais

  Alisema hili suala la watendaji na wenyeviti wa vijiji kuwapa vibali watu hao,uhamiaji wanalijua na wameliacha kwa muda mrefu na kama wangelitilia maanani pale mnapobaini kuwa viongozi hao wametoa vibali feki mnawakamata na kuwachukulia hatua,nchi isingefikia hatua hii ya kuwa na idadi kubwa ya wahamiaji kiasi hiki.

  Alisema kuwa kutokana na hali hiyo ya ulegevu na udhaifu wenu inawafanya watu wajiulize maswali mengi juu ya utendaji wenu wa kazi na kuwaona kama nyie ndio sehemu ya tatizo; kila siku sisi misako tu mpaka lini?kwanini tusisimamie zoezi hili kwa umakini pale mtu anapoingia tu na kumbaini tunamrudisha mara moja na sio kusubiri wawe wengi ndio mfanye misako,itafikia siku mtataka kuwarudisha watagoma na kukuelezeni kuwa ni kwao na wanahaki ya kuishi hapa jambo ambalo litazua mtafaruku mkubwa kati ya wazawa na hao wahamiajia haramu na mwisho wake ni mapambano.

  Alisema hatuchukii wageni ila mtu anayetaka kuishi Tanzania afuate utaratibu,apeleke maombi uhamiaji na watayafanyia kazi na pale mtu akikataliwa kupewa uraia asihoji kwasabu sio kila mtu atapewa uraia kuna wengine ni majambazi,wauza madawa ya kulevya na makosa mengine hatuwezi kuwapa uraia”mwaka 1982 Hayati mwalimu Julias Nyerere alitoa uraia wa fursa kwa wahamiaji 30,000 wakapata uraia na mimi kwa kipindi cha uongozi wangu nimetoa Fursa hiyo ambapo watu 160,000 wameomba na kupewa uraia kwaiyo ambaye hakuomba huyo hataki kuwa raia wa Tanzania wasakwe na kurudishwa kwao pia kumbuka hao ni binadamu wasiswagwe kama mifugo kama mtu ana mali yake auze na kuondoka msiwadhulumu.

  Aidha Rais amewaasa Watanzania kuacha kutumiwa na watu wenye nia mbaya ya kutaka kuvuruga amani ya nchi yetu kwa kupitia njia ya udini na siasa kwani matokeo yake ni kugawanyika na kupoteza malengo yao.

  Pia ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Bukoba kumpa jibu haraka kuhusu wananchi 800 wa mgogoro wa viwanja wanapewa lini.

  0 0

  Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma limefanikiwa kukamata lita mia sita (600) za pombe haramu ya Gongo, mitambo 11 pamoja na mapipa 134 ya (molasisi) ambayo ni mali ghafi inayotumika kutengenezea pombe hiyo.

  Mafanikio hayo yametokana na operesheni maalumu ya msako iliyofanyika tarehe 27/07/2013 katika wilaya Kongwa, Kijiji cha Kimero –Kiteto Kata ya Lenjulu Tarafa ya Mlali Wilaya ya Kongwa.

  Pia tumefanikiwa kukamata debe kumi za Bhangi, ambazo zimekamatwa huko katika kijiji cha Garigari kitongoji cha Mfiro wilayani Mpwapwa, ambapo debe nane zimeteketezwa.

  Aliyekamatwa na pombe ya gongo, mitambo 11 na mapipa 134 ya molasisi ni TAITA S/O MASHAKA RASHIDI@Rashid, Mchaga,miaka 40, mkulima na mkazi wa Kimero Kiteto Kongwa.

  Waliokamatwa na Bhangi huko Mpwapwa ni;
  1. FREDRICK S/O NGIMBA, Mhehe, miaka 25,mkulima,
  2. EMANUEL S/O NGIMBA, Mhehe, miaka 28,mkulima,
  3. JUMA S/O NGIMBA, mhehe,miaka 46, mkulima wote wakazi wa kijiji cha Garigari.

  Tunashukuru wananchi kwa jinsi wanavyoendelea kutupa taarifa zinazoleta mafanikio kama haya ya kupungufa uhalifu na madhara kwa afya za watu.

  DAVID A. MISIME- ACP
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA

older | 1 | .... | 208 | 209 | (Page 210) | 211 | 212 | .... | 3285 | newer