Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

PROF. KABUDI AMUWAKILISHA WAZIRI MKUU

$
0
0

 Leo Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Waziri wa Katiba na Sheria amemuwakilisha Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Ibada ya kuwekwa Wakfu Askofu wa Pili wa Dayosisi ya Shinyanga, Rev. Can. Capt. Johnson Japheth Chinyong’ole.

Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Stefano, Shinyanga na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Mheshimiwa George Huruma Mkuchika (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Viongozi wa Serikali ya Mkoa ikiongozwa na Mheshimiwa Josephine Matiro, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Viongozi wa Madhehebu mbalimbali ya Dini, Viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Shinyanga na Waumini wa Dayosisi hiyo

Pamoja na kumpongeza kwa kuwekwa Wakfu, Mhe. Prof. Kabudi amemuomba Askofu Chinyong’ole awe kiungo thabiti baina ya waumini na kati ya waumini na Maaskofu katika kuzitatua changamoto zilizopo katika Kanisa na kwamba utumie vipawa na karama alizopewa na mwenyezi Mungu kuwaunganisha viongozi na waumini ili waweke mipango madhubuti ya kulijenga Kanisa na kuijenga Dayosisi ya Shinyanga.

Prof. Kabudi amemuhakikishia Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Kanisa la Anglikana Tanzania katika ustawi wa Taifa kiroho, kisiasa, kiuchumi na kijamii na kwamba mchango huo umeiwezesha nchi yetu kupiga hatua katika nyanja zote; Kwamba Serikali itaendelea kushirikiana na madhehebu yote nchini katika kuweka misingi ya kila raia kuabudu kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Nchi.

Kabla ya kuchaguliwa Mwezi Oktoba, 2017 Askofu Chinyong’ole alikuwa Katibu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania kwa miaka mitatu. Askofu Chinyong’ole anakuwa Askofu wa Pili kuiongoza Dayosisi ya Shinyanga iliyoanzishwa Novemba, 2005 baada ya Dayosisi ya Victoria Nyanza kugawanywa.

Mhe. Prof. Palamagamba J. Kabudi (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria akisoma hotuba wakati akimuwakilisha Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kuwekwa Wakfu Askofu wa Pili wa Dayosisi ya Shinyanga Rev. Can. Capt. Johnson Japheth Chinyong'ole.
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria akiwa kwenye picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania mara baada ya kuwekwa Wakfu Askofu wa Pili wa Dayosisi ya Shinyanga Rev. Can. Capt. Johnson Japheth Chinyong'ole.
Pro. Kabudi akimpongeza Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga Rev. Can. Capt. Johnson Japheth Chinyong'ole mara baada ya kuwekwa wakfu.

ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI KUKAGUA MIRADI YA MAJI YA DAWASA

HOTUBA YA RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI ALIPOKUTANA NA RAIS PAUL KAGAME,IKULU JIJINI DSM JANUARI 14,2018

Reli ya ‘Standard Gauge” Sasa kutandazwa kutoka Dar es salaam Mpaka Kigali, Rwanda

$
0
0
Na. Judith Mhina 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Tanzania na Rwanda zimekubaliana kuunganisha Reli ya Kisasa (Standard Gauge) kutoka Isaka mkoani Shinyanga mpaka Kigali nchini Rwanda, ili kukuza biashara na uchumi wa nchi hizi mbili.
Rais Magufuli ameeleza hayo leo Ikulu Jijini Daar es Salaam muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame aliyekuja nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja.“Mimi na Rais Kagame kumeongea mambo mengi ya ushirikiano na kwa pamoja tumekubaliana kuanza ujenzi wa Reli ya Standard Gauge kutoka Isaka mpaka Kigali,” ameeleza Rais Magufuli.
Ameeleza kuwa ili kuharakisha ujenzi wa reli hiyo, kwa pamoja wamewaagiza Mawaziri wanaohusika na sekta ya ujenzi na wale wale wa Mambo ya Nje wa nchi hizi mbili kukutana haraka wiki ijayo kusughulikia masuala kadhaa yanayohusu ujenzi wa reli hiyo ikiwa ni pamoja na kujadili namna ya upatikanaji wa fedha za ujenzi.
Akielezea umuhimu wa kukuza uchumi na biashara baina nchi hizi mbili, Rais Magufuli amesema mpaka sasa mwenendo wa biashara kati ya nchi hizi umekuwa wa kusuasua na kwamba reli hiyo itasaidia kuimarisha biashara na ushirikiano wa Tanzania na Rwanda.
“Tunataka ikifika mwezi Desemba mwaka huu, mimi na Rais Kagame tuwe tayari tumeweka mawe ya msingi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa reli hii,” alisisitiza Rais Magufuli.
Amesisitiza kuwa mbali na kuimarisha uchumi, ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa takribani kilometa 400 pia utatoa ajira kwa vijana wengi na kusaidia usafirishaji wa madini ya Nickel kutoka nchi za Rwanda, Burundi na Tanzania ambapo madini hayo yanashindwa kuchimbwa kutokana na kukosekana usafiri madhubuti wa reli.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amesema kwamba Tanzania inamuunga mkono Rais Kagame kwa asilimia mia moja katika kuchukua Uenyekiti wa Umoja wa Afrika na kwamba itafanya kila linalowezekana kuzishawishi nchi marafiki pia zimuunge mkono Rais huyo wa Rwanda.
Kwa upande wake, Rais Paul Kagame amemshukuru Rais Magufuli na Watanzania kwa kumuunga mkono katika nafasi ya Uenyekiti wa Umoja wa Afrika na kwamba atafanya kila linalowezekana kuzishawishi nchi za Afrika kuongeza uwekezaji na kila nchi kuweka kikakati ya kuongeza ajira ili kuwafanya vijana waachane na dhana ya kukimbili nchi za Ulaya kutafuta maisha bora.

RAIS DKT MAGUFULI AONGEA NA KUAGANA NA RAIS KAGAME BAADA YA ZIARA YAKE YA SIKU MOJA NCHINI

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mazungumzo rasmi na Rais Paul Kagame wa Rwanda na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018


 Rais Paul Kagame wa Rwanda akiongea na vyombo vya habari baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akiongea na vyombo vya habari baada ya mazungumzo yake  rasmi na Rais Paul Kagame wa Rwanda  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake  Rais Paul Kagame wa Rwanda baada ya ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  leo Januari 14, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake  Rais Paul Kagame wa Rwanda baada ya ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  leo Januari 14, 2018
Rais Paul Kagame wa Rwanda akiagana na viongozi mbalimbali  baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018
Rais Paul Kagame wa Rwanda akiagana na viongozi mbalimbali  baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  mgeni wake  Rais Paul Kagame wa Rwanda baada ya ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  leo Januari 14, 2018.PICHA NA IKULU

Mwanamke wa Kiislam na yeyote unaependa vazi la Hijab,karibu ujumuike na wenzako siku ya PINK HIJAB DAY

$
0
0
 Tupia vazi la Pink,Peach ama Red kuendana na siku yenyewe halafu tukutane DIAMOND JUBILEE HALL tarehe 03 - 02 - 2018,kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku.

kutakuwa na maonyesho ya bidhaa za kijasiriamali,maonyesho ya mavazi,elimu ya mwanamke kujitambua bila kusahau michezo ya wototo.
Kiingilio ni Tshs.5000/= tu.( toka na ziada tuunge mkono bidhaa za kitanzania).
Kwa wajasirimali nafasi yako ya kuongeza wigo wa wateja kibanda cha kuuzia bidhaa zako utakipata kwa Tshs.50,000/=
Kwa mawasiliano zaidi.
0655 445105
Instagram:@pink_hijabtz.


Global TV: Sherehe ya Ndoa ya Shilole na Uchebe yafana jijini Dar es salaam

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 15, 2018


JOTO, MSONGAMANO, KUCHELEWA KWA HUDUMA JNIA KWASABABISHA MAWAZIRI WANNE KUKUTANA

$
0
0
Said Mwishehe,Globu ya jamii

MAWAZIRI wa wizara nne tofauti wameamua kufanya jitihada za kuondoa changamoto ya utoaji huduma kwa muda mrefu na kusababisha msongamano wa wageni wanaiongia na kutoka nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijijini Dar es Salaam.

Pia kuondoa changamoto ya joto katika eneo la kuchukulia mizigo pamoja na kushughukikia hati za kusafiria kwa wageni wanaoingia nchini pamoja na changamoto ya ufinyu wa eneo la kusubiri huduma uwanjani hapo.

Mawaziri hao ambao wamekutana leo katika uwanja huo na kukagua shughuli za utoaji huduma ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala,

Wengine ni Waziri wa Mambo ya Ndani Dk.Mwigulu Nchemba na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dk.Susan Kolimba na Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye. Akizungumza baada ya kufanya ziara hiyo,Waziri wa Mambo ya ndani Ndani Dk.Nchemba amesema kuwa jitihada mbalimbali zinafanywa kutatua changamoto hizo.

Ametaja hatua ambazo wizara yake inachukua ni kuharakisha utoaji huduma wa hati za kusafiria kwa njia ya kieletroniki. Pia wameamua kuongeza idadi ya madawati ya kutolea huduma kwa wageni ikiwa sambamba na kuongeza watoaji huduma ili kurahisisha utoaji huduma wa muda mfupi.

“Taarifa zinaonesha kuwa kwa sasa kuna unafuu mkubwa wa kutoa huduma kwani badala ya saa tatu ambazo zilikuwa zinatumia awali hivi sasa muda wa utoaji huduma umeshuka hadi saa moja.Lengo letu ni kushuka zaidi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto) wakati walipofanya ziara ya kukagua Changamoto mbalimbali zilizopo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es salaam leo. Wengine ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala (katika) na kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba wakisikiliza.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba akizunumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa ziara ya kukagua changamoto mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es salaam leo kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt.Anna Peter Makakala
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala (katikati) akiongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba (kushoto) na, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) 
Kutoka kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Richard Mayongela wakitafakari jambo wakati wa ziara ya kukagua changamoto mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kukagua changamoto mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam leo wengine ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba.

MBUNGE LUSHOTO AWATAKA MAAFISA UGANI KUACHA KUKAA OFISINI

$
0
0
MAAFISA Ugani wa Kata na Vijiji wilayani Lushoto mkoani Tanga wametakiwa kuacha tabia ya kukaa ofisini badala yake wahakikisha wanakwenda kwa wakulima ili kuwapa elimu ya namna ya kulima kilimo cha kisasa ambacho kitakuwa na tija kwao hali itakayosaidia kuongeza uzalishaji wa mazao yao. 

Kauli hiyo ilitolewa na Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia wakati wa ziara yake wa kuwatembelea wananchi katika vijiji mbalimbali iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kujikita kwenye shughuli za uzalishaji na kusikiliza kero zinazowakabili.

Akiwa kwenye kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola, Mbunge huyo alisema wapo baadhi ya maafisa ugani wamekuwa wakikaa ofisini badala ya kwenda wa wananchi ambao wanajishughulisha na kilimo ili waweze kuwapa elimu ya namna ya kulima kisasa jambo ambalo limekuwa likichangia kurudisha maendeleo yao nyuma. 

“Ndugu zangu maafisa ugani tambueni kuwa mnajukumu kubwa la kuhakisha mnakwenda kwa wananchi kuwaelimisha juu ya kulima kilimo chenye tija kwao kwani hiyo itawasaidia kuweza kupata mafanikio kuliko wanavyofanya sasa lakini pia acheni kukaa ofisini “Alisema.
“Kwani elimu ambayo mnaweza kuitoa inaweza kuwa chachu ya wakulima kuweza kulima mazao mazuri yatakayokuwa ya ushindani na soko la kisasa hivyo jambo hilo ni muhimu sana “Alisema. 

TBA YATAKIWA KUHAKIKISHA MAENEO YAO YANA HATI

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, ametoa agizo kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kuhakikisha wanazitambua na kuzisajili nyumba zote na viwanja vya Serikali zinazomilikiwa na Wakala huo katika maeneo mbalimbali nchini.

Agizo hilo amelitoa mkoani Mtwara, mara baada ya kukagua nyumba na viwanja vinavyomilikiwa na Wakala huo na kusisitiza kwa Mameneja wa mikoa wa Wakala huo kuhakikisha wanafanya matengenezo na ukarabati wa majengo hayo ili kuvutia wapangaji wao.

“Wasimamizi wa nyumba hizi hakikisheni nyumba hizi mnazitambua na mnazifanyia matengenezo ya mara kwa mara, nimetembelea Halmashauri mbalimbali na kuona baadhi ya nyumba za Serikali haziridhishi baada ya kuwa zimetelekezwa muda mrefu”, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Aidha, Naibu Waziri huyo amemtaka Kaimu Meneja wa TBA mkoani Mtwara, kuhakikisha nyumba na viwanja vyote anavyosimamia vinakuwa na hati ili kidhibiti changamoto ya wananchi kuvamia viwanja vya Serikali.

Amekemea tabia ya baadhi ya wapangaji wa nyumba za Serikali kutozitunza wala kuzijali nyumba hizo hali inayoipelekea Serikali kuingia gharama kubwa katika kufanya marekebisho ya nyumba hizo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Mtwara Edward Mwangasa, wakati alipokuwa akikagua nyumba zinazomilikiwa na Wakala huo, mkoani humo.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Mtwara Edward Mwangasa, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, katika ukaguzi wa nyumba zinazomilikwa na Wakala huo ambao unamiliki jumla ya nyumba 76 mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, wakati alipokuwa akikagua nyumba zinazomilikiwa na Wakala wa Majengo (TBA), mkoani humo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WANANCHI WA MKOA WA SONGWE WAANZA ZOEZI LA MAPINGAMIZI DHIDI YA WASIO RAIA KUPATA VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
Pamoja na zoezi la Usajili linalohusisha ujazwaji wa fomu za maombi pamoja na kuchukuliwa alama za Kibaiologia pamoja na Picha, Mkoa wa Songwe umeanza zoezi msingi la Mapingamizi ambapo wananchi wanapata fursa ya kuhakiki taarifa zao pamoja na kuweka mapingamizi kwa mtu yoyote wanayehisi si raia au si Mkazi wa eneo husika na amefanya udsajili wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa, ambapo Bi. Coletha amewasihi Wananchi wa katanganyifu kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa.

Zoezi hili lililoanza sambamba na kuendelea kwa usajili kwa Kata ambazo hazijakamilisha linahusisha Kata za ichenjezya, vwawa na mlowo Wilayani Mbozi mkoani Songwe baada ya kukamilisha hatua ya awali ya usajili.

Kwa mujibu wa Afisa Usajili Wilaya ya Mbozi Bi. Bi. Coletha Peter amesema zoezi hilo litahusisha wananchi wote wa mkoa wa Songwe na kuwataka kujitokeza kwa wingi kwenye mbao za matangazo ambako picha zote za waombaji wa Vitambulisho vya Taifa zimebandikwa pamoja na majina yao.

Amesema kama Mamlaka wamejipanga kuhakikisha wanapokea mapingamizi ya watu wote watakao bainishwa kwa njia ya wazi na siri na kuhakikisha Mamlaka inayafanyia kazi majina hayo mapema sambamba na kuanza uchakataji wa taarifa za waombaji wote waliokamilisha taratibu za Usajili ili vitambulisho vianze kutolewa kwa wakati.
Afisa Usajili Mamlaka ya Vitambilsho vya Taifa akichukua alama za Vidole vya mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Mbonji waliofika Katika moja ya Vituo vya Usajili ili kupatiwa huduma ya usajili na Utambuzi.
Wananchi wa Kata ya Itaka Kijiji cha Itaka wengi wao wakiwa ni akina Mama, wakijificha Mvua nje ya moja ya Kituo cha Usajili wakati wakishiriki zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa linaloendelea kwenye Kata hiyo
Wananchi wakiendelea na zoezi la kuchambua fomu nje ya Kituo cha Usajili katika kijiji cha Nsani Kata ya Itaka Wilaya ya Mbozi kabla ya kwenda kupatiwa huduma ya Usajili na Utambuzi uliohusisha uchukuaji wa alama za kibaiologia, saini ya kielektroniki pamoja na Picha.
Wananchi wa Kijiji cha Mbonji kata ya Itaka Wilaya ya Mbozi wakiwa katika foleni kuelekea kupata huduma ya usajili na utambuzi zoezi linaloendela katika kata nzima ya Itaka.


MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA) YASHIRIKI TAMASHA LA NNE LA BIASHARA VIWANJA VYA MAISARA – ZANZIBAR

$
0
0
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ofisi ya Zanzibar inashiriki kwa mara nyingine tena Tamasha la Nne la Biashara linaloendelea viwanja vya Maisara mjini Unguja Zanzibar kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.

Miongoni mwa huduma ambazo Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa inatoa kwenye Banda la Maonesho ni kutoa elimu kuhusu Vitambulisho, Kutoa taarifa za Usajili kwa Wananchi ambao wamesajiliwa na hawajapata Vitambulisho vyao, kuanisha matumizi ya Vitambulisho na huduma ya Usajili kwa wageni (foreigners)

Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa Tanzania Zanzibar umekamilika kwa asilimia 99.7 na kwa wale wananchi ambao hawajasajiliwa Usajili unaendelea kwenye Ofisi za Wilaya zilizonguliwa kwenye kila Wilaya Unguja na Pemba.



Wafanyakazi wa NIDA ofisi ya Zanzibar pamoja na Kaimu Mkurugenzi Ofisi ya NIDA Zanzibar (Mwenye Kaunda) wakiwa katika Banda la maonyesho katika viwanja vya Maisara
Wafanya kazi wa NIDA wakijiandaa kumpokea mgeni rasmi kwenye banda lao lililopo viwanja vya Maisara Zanzibar.
 
Wafanyakazi wa NIDA wakiwahudumia wananchi waliofika katika banda la maonyesho katika viwanja vya Maisara.

MRADI WA BILIONI 1.8 KUONDOSHA SHIDA MAJI KATA YA MTWANGO HALMASHAURI YA MUFINDI

$
0
0

Na Afisa Habari Mufindi

Hatimaye Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imetiliana saini na Kampuni ya Siha Enterprises Limited, kutekeleza ujenzi wa mradi mkubwa wa Maji Sawala, wenye thamani ya shilingi bilioni 1.8, utakao wanufaisha wananchi wa Vijiji vine vya Kata ya Mtwango baada ya kuikosa huduma ya Maji safi na salama kwa miaka mingi.

Hafla ya kihistoria ya kusaini kandarasi hiyo ya miezi 12, imefanyika katika kijiji cha Sawala mbele ya viongozi wa Vijiji vinne vya Sawala, Mtwango, Lufuna na kibao vinavyotarajiwa kunufaika na huduma hii muhimu kwa uhai wa binadamu.

Akizungunza mara baada ya kusainiwa kwa Mkataba huo, kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, ambaye pia ndiye Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Jamhuri William, amemtaka Mkandarasi huyo kutekeleza mradi huo kwa ubora, kukamilisha kwa wakati kadri ya mkataba aliosaini bila kuongeza gharama na ameahidi kuufuatilia mradi huo kwa kila hatua ya ujenzi.

Mh. Jamhuri pia, amewataka wananchi wa kata ya Mtwango kumpa shirikiano Mkandarasi katika kipindi chote cha utekelezaji wa Mradi, huku akikemea tabia ya uwizi kwa Vijana watakaopata ajira kwa kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huo uliosubiriwa kwa muda mrefu na wananchi wa kata ya Mtwango.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. Festo Mgina, amesema Ofisi yake inaimani kubwa na Mkandarasi huyo na akamtaka aanze kutekeleza ujenzi wa mradi kwa wakati kwani shauku pekee ya watu wa Kata ya Mtwango, ni kupata huduma ya Maji baada ya Mkandarasi wa awali kushindwa kukukidhi shauku yao.

Ujenzi wa mradi wa Maji Sawala, utakelezwa na kampuni wa Siha Enterprises Limited na utasimamiwa na Ofisi ya Maji Mjini Iringa (Iruwasa), Ofisi ya Maji ya Katibu tawala Mkoa pamoja na Ofisi ya Maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa muda usizidi miezi 12. Aidha, baadhi ya shughuli kubwa zinazotarajiwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa Matenki manne ya ujazo wa lita 450,000, kusambaza mabomba kwenye Vijiji husika pamoja na kujenga vituo 122 vya kukinga Maji.
 Afisa mipango wa Halmashauri isaya Mbenje, akimwonesha Mkandarasi Maeneo mbalimbali  ya kuyafanyia kazi katika chanzo cha Maji cha Sawala.
 Mkurugenzi Mtendaji Profesa Riziki Shemdoe na Mwenyekiti wa Halmashauri Festo Mgina wakisaini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kwa gharama ya shilingi Bilioni 1.8
Mkurugenzi Mtendaji Profesa Riziki Shemdoe na Mwenyekiti wa Halmashauri Festo Mgina, kushoto wakimkabidhi Mkataba Mkandarasi Siha Enterprises kulia mara baada ya kusainiwa.

MICHUZI TV:AMSHA KIPAJI CHAKO NA TBREAKER.


WAGONJWA 64,093 WATIBIWA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KWA MWAKA 2017

$
0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mwaka wa 2017 imeona jumla ya wagonjwa 64,093 kati ya hawa wagonjwa wa nje ni 60,796 na waliolazwa 3297. Wagonjwa waliolazwa 3010 waliruhusiwa baada ya hali zao kuwa nzuri na wagonjwa 287 walipoteza maisha hii ikiwa ni sawa na asilimia 8.7.

Wagonjwa 225 walifanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua ambapo wagonjwa 200 waliruhusiwa na wagonjwa 25 walifariki Dunia hii ikiwa ni sawa na asilimia 11 (wastani wa kimataifa ni asilimia 13). Kati ya wagonjwa 225 waliofanyiwa upasuaji wa kufungua kifua wagonjwa 105 walifanyiwa upasuaji na madaktari wetu bingwa wa magonjwa ya moyo watoto wakiwa ni 60 na watu wazima 45.

Upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab ulifanyika kwa wagonjwa 800 kati ya hao 798 wanaendelea vizuri na wagonjwa wawili (2)walifariki hii ikiwa ni chini ya asilimia 1.6. Kati ya wagonjwa 800 waliotibiwa wagonjwa watu wazima 631 walifanyiwa upasuaji na madaktari wetu wa ndani.

Tulikuwa na jumla ya kambi za matibabu 15. Tumefanya matibabu ya pamoja na washirika wetu kutoka mabara ya Asia, Australia, Ulaya na Amerika. Katika kambi zote hizo kambi za watoto ni tano na kambi za watu wazima 10. Jumla ya wagonjwa 120 walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua kati ya hao watoto 80 na watu wazima ni 40. Wagonjwa 169 walifanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kati ya hao watoto 92 na watu wazima 77.

Kwa wagonjwa wote hao 1025 kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua hapa nchini Taasisi imeweza kuokoa zaidi ya bilioni 29 (Tshs. 29,725,000,000/=) ambazo Serikali ingezilipa kama wagonjwa hawa wangefanyiwa upasuaji wa moyo nje ya nchi. Gharama za mgonjwa mmoja anayetibiwa nje ya nchi ugonjwa wa moyo ni zaidi ya milioni 29.

Tulifanya upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu (AVF- Arterio Venous Fistula) kwa ajili ya kusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (Hemodialysis) 52.

SERIKALI YAANZA KUTUMIA MFUMO WA NYOTA KATIKA KUVIPIMA VITUO VYA AFYA NA HOSPITALI NCHINI.

$
0
0
Na WAMJWW. RUKWA-NKASI 

Serikali yaanza kutumia mfumo wa nyota kupima huduma zitolewazo na Vituo vya Afya, Hospitali na Zahanati nchini ili kupima utendaji kazi wa watumishi wa Sekta ya Afya katika kutoa huduma kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Kituo cha Afya cha Nkomolo Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa, ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya kukagua shughuli za utoaji wa huduma za Afya na kuamsha hali kwa wananchi katika kujihusisha na shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

“Tumeanza utaratibu wa kutoa nyota katika vituo vya Afya, imeanzia nyota sifuri mpaka nyota tano, sifuri maana yake kituo hicho hakifai kutoa huduma ya Afya na nyota tano maana yake kinafanya vizuri sana” Alisema Dkt. Ndugulile.

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile aliridhishwa na hali ya upatikanaji wa Dawa katika kituo hicho, hivyo kuwatoa hofu wananchi na kusisitiza kuwa hawapaswi kuuziwa dawa zote muhimu kwani Serikali imeboresha hali ya upatikanaji wa Dawa katika vituo vyote vya Afya nchini.
 Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akikagua Bin Kadi ambayo inaonesha idadi ya Dawa zilizoingia na zilizobaki katika stoo ya dawa ya Kituo cha Afya Nkomolo Mkoani Rukwa.

 Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akikagua jokofu la Chanjo wakati alipotembelea katika Kituo cha Afya cha Nkomolo kilichopo Nkasi Mkoani Rukwa wakati wa Ziara yake ya kukagua Huduma za Afya Mkoani Rukwa.

 Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akikagua Idadi ya watu waliohudhuria Kituoni hapo kupitia mfumo wa Kompyuta katika stoo ya dawa ya Kituo cha Afya Nkomolo Mkoani Rukwa.
 Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akipokea maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Majengo Mhandisi Mwakyembe kutoka Ofisi ya Mkoa wa Rukwa.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI KALEMANI ATOA MAAGIZO MAZITO KWA WANAOTEKELEZA MIRADI YA UMEME VIJIJINI

$
0
0
- Mkandarasi asiyeanza kazi ifikapo Machi 2 kukiona cha moto
- Viongozi TANESCO, REA wawasilishe taarifa kila robo mwaka

Na Veronica Simba – Dodoma.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amekutana na watendaji mbalimbali wanaosimamia na wanaotekeleza miradi ya awamu ya tatu ya kusambaza umeme vijijini na kutoa maagizo mazito yanayolenga kufanikisha mradi huo kikamilifu.

Mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa Juma, Januari 13 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, ulihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri Kalemani alitoa maagizo kwa wajumbe ambao ni wazalishaji na wasambazaji wa nguzo, transfoma na nyaya za umeme, wakandarasi wanaotekeleza mradi husika katika maeneo mbalimbali nchini na wataalam wanaosimamia utekelezaji wa mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA); kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake ipasavyo.
Kwa upande wa wakandarasi, Dkt. Kalemani aliwaagiza kuhakikisha kila mmoja anaanza utekelezaji wa kazi halisi (physical work) kabla ya tarehe 2 Machi mwaka huu vinginevyo Serikali itawachukulia hatua za kisheria. “Asiwepo mkandarasi yeyote ambaye atakuwa hajaanza kazi baada ya tarehe hiyo, alisisitiza.”
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akisisitiza jambo wakati akiongoza kikao baina yake na wadau mbalimbali wanaotekeleza miradi ya usambazaji umeme vijijini awamu ya tatu. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Haji Janabi.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (aliyesimama) akizungumza wakati wa Mkutano na wadau mbalimbali wanaotekeleza miradi ya usambazaji umeme vijijini awamu ya tatu. Kushoto kwake ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
 Wakandarasi mbalimbali wanaotekeleza miradi ya usambazaji umeme vijijini awamu ya tatu, wakielezea hatua waliyofikia katika utekelezaji wake katika kikao baina yao na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Dodoma mwishoni mwa Juma.

SEKTA YA MADINI LAZIMA IWE NA MCHANGO MKUBWA KWENYE PATO LA TAIFA: MHE DOTTO BITEKO

$
0
0
Na Mathias Canal, Dodoma

Sekta ya Madini inachangia kati ya asilimia 3.5 mpaka 4 katika Pato la Taifa ukilinganisha na sekta zingine ambazo zimejitutumua kwa kiasi kikubwa katika mchango mahususi wa pato la Taifa nchini Tanzania.

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko amebainisha kuwa kiasi cha kati ya asilimia 3.5 mpaka 4 ni kidogo sana ukilinganisha na umuhimu wa sekta hiyo nchini hivyo Wizara ya Madini imekusudia kuongeza tija katika mchango wa pato la Taifa kupitia sekta hiyo muhimu ya Madini.

Mhe Biteko amebainisha hayo Leo Januari 15, 2018 wakati akizungumza na wakuu wa idara na vitengo pamoja na watumishi wa Wizara ya Madini ofisi Kuu Mjini Dodoma huku akiwataka watumishi wote kufanya kazi kwa bidii, nidhamu na uzalendo mkubwa kwa manufaa ya Taifa.

Alisema kuwa sekta ya Madini ni muhimu nchini kutokana na rasilimali Madini ilizonazo hivyo watumishi wote wanapaswa kufikiria namna ya kufanya kazi kwa tija ili kuwa na ongezeko la mchango mkubwa katika pato la Taifa.

"Natamani nione kwenye taarifa ya robo mwaka ya BOT ikisoma kwamba sekta ya madini inachangia angalau asilimia 10 ya Pato la Taifa kuliko ilivyo hivi sasa na hilo naamini linawezekana kwa ushirikiano wa pamoja" Alisisitiza Mhe Biteko
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akizungumza na wakuu wa idara na vitengo pamoja na wafanyakazi wote wa wizara ya madini mara baada ya kuwasili ofisini Mjini Dodoma, Leo Januari 15, 2018. Picha Zote Na Mathias Canal.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakuu wa idara na vitengo pamoja na wafanyakazi wote wa wizara ya madini mara baada ya kuwasili ofisini Mjini Dodoma, Leo Januari 15, 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Stanislaus Nyongo akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri mwenzake katika Wizara hiyo Mhe Dotto Mashaka Biteko kuzungumza na wakuu wa idara na vitengo pamoja na wafanyakazi wote wa wizara ya madini mara baada ya kuwasili ofisini Mjini Dodoma, Leo Januari 15, 2018.

NEWZ ALERT :AJALI YAUA WATU 11 MKOANI KAGERA

$
0
0
Na Ripota wa Globu ya Jamii Kagera.

WATU 11 wamefariki Dunia na wengine sita kujeruhiwa kutokana na ajali ya gari aina ya hiace kugongana na malori matatu iliyotokea mnamo majira ya saa tano usiku wa kuamkia leo,katika kijiji cha Mubigera kata ya Nyantakara wilaya ya biharamulo mkoani kagera ,wakati wakisafiri kutoka wilaya ya kibondo kuelekea kahama mkoani Shinyanga.

Mganga mkuu wa hospitali teule ya Biharamulo Dr Grasmus Sebuyoya amethibitisha kupokea miili ya watu hao wakiwa maiti na majeruhi sita na kwamba kati ya majeruhi hao wawili hali zao ni mbaya na waliofariki wa jinsia ya kiume ni saba na jinsia ya kike ni watatu

Dr Sebuyoya amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Juma Samo (25) Joseph Otieno (30), Oscar Leonard Sebastian (27), Baseke Mashinga Nyabashiki (31), Mahalulo Charles (25) na majeruhi wa sita hajafahamika kwa kuwa hajajitambua na kwamba maiti waliofia eneo la tukio ni Tisa na wawili wamefariki baada ya kufikishwa hospitalini hapo.

Awali Mwenyekiti wa kijiji cha Mubigera Bw Mapunda Kayuki amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya Saa 11 jioni ambapo hiece ilitaka kukwepana na roli kwenye barabara ya biharamulo kwenda kahama kwenye kijiji hicho na kugongana ambapo dereva wa hiece na tingo wake ni miongoni mwa waliofariki

Bw Kayuki amesema hiece hiyo yenye  namba za usajili T.542 DKE ilikuwa ikitokea kibondo kwenda kahama ambapo maroli yaliyohusika kwenye ajali hiyo ni T.860CGS, T.103 DUJ na T.147 DUJ magari  yako chini ya usalama wa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi amesema hajakamilisha taarifa kamili ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kutambua majina ya waliopoteza maisha mpaka ajiridhishe na taarifa,  zitatolewa kwa umma bila kutia mashaka ili ndugu wa marehemu waweze kujua na kufuatilia kwa uhakika
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images