Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

. MAGIC FM BAMIZA TOP 20 COUNT DOWN JANUARY 13TH 2018


MICHUZI TV: IDRIS AMKUMBUKA LULU KWA NAMNA YAKE, DIAMOND ANYAKUWA TUZO

UN NEWS KISWAHILI: Ugonjwa hatari wauwa 61, na zaidi ya 700 waathirika Afrika Kusini

UGHAIBUNI MEDIA: Mtanzania arusha Ndege South Africa

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YAJAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE. DKT. FAUSTINE NDUGULILE AZUNGUMZA NA WANAWAKE WAJASILIAMALI WA MKOA WA RUKWA

HAFLA YA KUWAREHEMU NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI YAFANYIKA LEADERS CLUB JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Mtoto wa marehemu Cisco Mtiro na dada yake walijumuika na umati mkubwa uliojitokeza kwenye hafla ya kila mwaka ya kuwarehemu ndugu, jamaa na marafiki waliotangulia mbele ya haki katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam Jumamosi Januari 13, 2018. Siku hii imepewa jina la muasisi wa shughuli hiyi na kujulikana kama Cisco Memorial Day.
 Marafiki wa karibu wa marehemu Cisco Mtiro na ndugu, jamaa na marafiki wengine waliotangulia mbele ya haki wakipata chakula cha mchana baada ya dua
 Kinamama walikuwepo shughulini
 Baada ya dua mpunga ulifinywa
 Viongozi wa dini wakipata chakula cha mchana baada ya kuongoza dua ya kuwakumbuka marehemu
Picha ya pamoja ya kamati ya maandalizi. 

MWENYEKITI WA CCM RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI WA CCM HUMPHREY POLEPOLE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Humphrey Polepole kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Humphrey Polepole Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Humphrey Polepole akizungumza mara bada ya kikao chake na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

OLD SCHOOL REUNION PARTY DMV, MAREKANI

0
0

Its all About Fun, Food, Drinks, Fashion,Sports and Nyama choma

From Fri JULY 6 to Sun JULY 8, 2018 
Oxford Center 
9700 Martin L King Jr Hwy,
Lanham, MD 20706

Friday July 6, 2018 

from 9pm DMV International VIBE
Music by DMV DJ's

Saturday July 7, 2018
From 10 am Basketball Bonanza

From 4 Pm Simba vs Yanga

From 9pm OLD SCHOOL REUNION PARTY Like never before!
Music by the best DJs in North America Dj Luke Joe
Dj Dennis the Funkhouse

Image result for SIMBA YANGA COLUMBUS OHIO
Timu ya Yanga
Image result for SIMBA YANGA COLUMBUS OHIO
Timu ya Simba
Image result for WACHEZAJI BASKETBALL COLUMBUS, OHIO
Wachezaji wa Simba wakiwa na kombe baada ya kuifunga Yanga 2-1 Columbus, Ohio.
Image result for WACHEZAJI BASKETBALL COLUMBUS, OHIO
Timu ya Pazi katika picha ya pamoja
Image result for WACHEZAJI BASKETBALL COLUMBUS, OHIO
Timu ya Vijana ya Columbus, Ohio.




WANANCHI MKOANI MARA WAITIKIA WITO WA MKUU WA MKOA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA

0
0

Wananchi mkoani Mara wamejitokeza kwa wingi kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa Mhe. Adam Kighoma Ali Malimaambaye amewataka wakazi wote wa mkoa huo kuhakikisha wanasajiliwa Vitambulisho vya Taifa ndani ya miezi mitatu ya zoezi hilo linaloendelea katika Wilaya zote za mkoa huo.

Akizungumzia mwitikio wa wananchi katika kutekeleza agizo hilo; Afisa Usajili Wilaya ya Musoma Bi. Ohana Gerald amesema mwitikio mkubwa wa watu ndiyo umepelekea kwa Wilaya ya Musoma Manispaa; zoezi la usajili kuwa  limekamilika na sasa zoezi linaendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Vijijini na tayari Kata za  Bwasi, Makojo na Bukumi zimemaliza Usajili. Kata zinazoendelea na usajili kwa sasa ni Bukima, Suguti na Rusoli.

Aidha amewataka wananchi wa kata nyingine 15 ambazo bado usajili haujaanza kuanza maandalizi na kujitokeza kwa wingi pindi zoezi litakapofika katika kata zao.

Baadhi ya wananchi wameonyesha uelewa mpana wa manufaa ya kuwa na Vitambulisho vya Taifa na kuishukuru Serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kuendesha zoezi bila kulipia gharama zozote.

Pamoja na kuisifu Serikali wamemshukuru Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Malima kwa kuweka msukumo mkubwa wa zoezi la Usajili kwani kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakinyanyasika kwa kukosa utambulisho na hivyo kukosa fursa nyingi na kuwapunguzia kero na usumbufu mkubwa wanaoupata sasa katika kupata baadhi ya huduma.

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa inategemea kumaliza zoezi la Usajili kwa mkoa wa Mara mwishoni mwa mwezi Februari, 2018 na kuendelea na hatua za uchakataji wa taarifa ili kuhakikisha wananchi wote wenye sifa waliosajiliwa mkoani Mara wanapatiwa Utambulisho wa Taifa kabla ya mwezi Desemba 2018.
 Wakazi wa kata ya Bukima Wilaya ya Musoma vijijini mkoani Mara,  wakiwa kwenye foleni wakisubiri kusajiliwa wakati wa zoezi la uandikishaji Vitambulisho vya Taifa.

 Mwenyekiti wa kijiji cha Bukima Ndg. Murungu Murungu akiwasaidia wananchi kujaza fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi la Usajili likiendelea kwenye ofisi ya mtendaji kata ya Bukima.

 Afisa usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bi. Ohana Gerald akimsikiliza mmoja wa wananchi waliojitokeza kusajiliwa wakati wa zoezi la usajili  wananchi wa kata ya Bukima wilaya ya Musoma Vijijini mkoani Mara.

 Bw. Shukrani Kwikalya Mgane mkazi wa kata ya Bukima, akikamilisha hatua ya upigaji wa picha wakati wa zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa. Kulia ni afisa Usajili wa  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bw. Jackson Paulo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

DKT. FAUSTINE AWAAGIZA VIONGOZI WA MKOA WA RUKWA KUTOKOMEZA UDUMAVU UNAOSABABISHWA NA LISHE DUNI.

0
0
Na WAMJWW. RUKWA-SUMBAWANGA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuhakikisha wanapambana na kutokomeza udumavu kwa watoto unaosababishwa na ukosefu wa Lishe bora.

Ameyasema hayo akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua shughuli za utoaji huduma za Afya, na uhamasishaji wa vikundi vidogo vidogo vya wanaweke vya ujasiriamali katika Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.

”Mkoa wa Rukwa haupaswi kuwa na utapiamlo hata kidogo, asilimia 60 ya udumavu ndani ya Rukwa ni kiasi kikubwa sana, katika mkoa ambao una chakula na ardhi yenye rutuba nzuri ni jambo la kushangaza kuona tatizo hili”, Alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile aliendelea kwa kusema kuwa, Siku 100 za mwanzo tangia mtoto anazaliwa ni muhimu na nyeti sana katika kuhakikisha anapata maziwa ndani ya miezi sita, na anapoanza kula ale vyakula vyenye lishe ya kutosha ili ubongo wake ukue vizuri.

Aidha, Dkt. Ndugulile ametoa maelekezo kwa sekretarieti ya Mkoa na viongozi wa kisiasa kushirikiana kwa pamoja katika kutoa elimu ya kutosha kwenye kila mikusanyiko watakayofanya kuhusiana na masuala ya Lishe bora ili kutokomeza janga hili linalosumbua idadi kubwa ya watoto katika Mkoa huu.

Kwa upande wake Mbunge wa Sumbawanga Mh. Aishi Hilaly amemshukuru Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kwa kuwakumbuka katika mgao wa fedha za kuboresha Vituo vya Afya cha Mazwi, pia hakusita kupaza sauti juu ya ombi la gari la kubebea wagonjwa litakalosaidia kupunguza hadha kubwa wanayokumbana nayo inayotokana na kukosekana kwa gari hilo.

Nae Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Boniface Kasululu Mkoa unaendelea kupambana na magonjwa ya mlipuko hasa ugonjwa wa kipindupindu kwa kutoa elimu ya Afya na Usafi wa mazingira kwa wananchi, ili kuhakikisha magonjwa haya yanakuwa historia katika mkoa wa Rukwa.

Aidha, Dkt. Kasululu alimuomba Dkt. Faustine kupunguza hadha ya upungufu wa madaktari bingwa na mabingwa wa fani nyingine, Dkt. Kasululu alisema kuwa hadi kufikia Desemba 2017 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa inajumla ya madaktari bingwa 5 ambao ni sawa na asilimia 21 kati ya madaktari 24 wanaohitajika.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akipitia ramani ya jengo jipya la mama na mtoto linaloendelea kujengwa katika hatua ya kuboresha huduma katika kituo cha Afya cha Mazwi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akiteta jambo na viongozi mbali mbali katika moja ya jengo jipya linalojengwa katika kuboresha kituo cha Afya cha Mazwi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akijiridhisha na uwepo wa Dawa katika stoo ya Dawa katika kituo cha Afya cha Mazwi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akiongoza msafala wa ukaguzi wa jingo jipya katika kituo cha Mazwi Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akikagua Dawa katika stoo ya Dawa katika Kituo cha Afya Mazwi, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mkoa wa Rukwa wilaya ya Sumbawanga, pembeni yake ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Boniface Kasululu.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akiwa ndani ya jengo jipya la wodi ya kina mama wajawazito, katika ziara yake ya kukagua huduma zinazotolewa katika kituo hicho. 

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 14, 2018

SERIKALI YAMCHARUKIA MKANDARASI DOTT

0
0
Serikali imemtaka Mkandarasi Dott Services anayejenga barabara ya Mtwara-Mnivata yenye urefu wa KM 50 kwa kiwango cha lami kuongeza vifaa na kasi katika ujenzi wa barabara hiyo ili kurahisisha huduma za usafirishaji wa mazao na abiria kwa wananchi wa mkoa huo.

Akitoa agizo hilo mkoani Mtwara, Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo na kusisitiza kuwa mkandarasi huyo anatakiwa kuhakikisha ujenzi wa barabara hiyo unaendana sawia na thamani ya fedha zilizotolewa na ubora kwa kiwango cha kisasa.

“Hakikisha unaongeza vifaa na kasi ya ujenzi wa barabara hii, la sivyo tutakutoa na hutapata kazi nyingine ya ujenzi wa barabara hapa nchini”, amesisitiza Naibu Waziri Kwandikwa.Ametoa rai kwa Makandarasi wote nchini kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili, weledi na kuhakikisha kazi wanazopewa zinakamilika kwa wakati na ikiwezekana hata kabla ya muda wa mkataba ili kuweza kuokoa fedha za Serikali.

Aidha ameutaka Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoani hapo pamoja na Mhandisi Mshauri kutoka kampuni ya Kyongdong Engineering, kuusimamia madhubuti mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati na viwango vinavyostahili na hivyo kuweza kufungua fursa za kiuchumi na maendeleo kwa mkoa huo haraka iwezekanavyo.

Naibu Waziri huyo amesema nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri na ya uhakika kupitia miundombinu bora ya barabara vipindi vyote vya mwaka hivyo fedha za kuwalipa makandarasi zipo tayari ni jukumu lao kuikamilisha mapema.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi Dott Service na Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Kyongdong Engineering wanaojenga barabara ya Mtwara – Mnivata yenye urefu wa KM 50 kwa kiwango cha lami na kumtaka Mkandarasi huyo kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo haraka.
Mbunge wa Jimbo la Nanyamba mkoani Mtwara, Mheshimiwa Abdallah Chikota (Wa kwanza kulia), akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, (Wa pili kulia) sehemu yenye mteremko mkali katika mlima wa Nameleche uliopo katika barabara ya Mtwara-Mnivata-Tandahimba-Newala hadi Masasi yenye urefu wa KM 210 ambapo magari husumbuka katika kipindi cha mvua kutokana na mteremko huo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mnivata mkoani Mtwara alipofika hapo kukagua barabara ya Mtwara – Mnivata yenye urefu wa KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Muonekano wa Barabara ya Mtwara – Mnivata yenye urefu wa KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami ambapo Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, amemtaka Mkandarasi Dott Service, anayejenga barabara hiyo kukamilisha ujenzi wake haraka.

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA WATILIANA SAINI MKATABA MPYA WA USHIRIKIANO NA CHUO CHA UKAMANDA DULUTI

0
0
Kushoto ni mkuu wa chuo cha ukamanda na unadhimu Duluti Meja Jenerali H.Masebu akitiliana saini na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha,Dk.Faraji Kasidi mkataba mpya wa ushirikiano (MoU) kati ya chuo cha uhasibu Arusha na chuo cha  unadhimu Duluti .Anayeshuhudiana wa kwanza kulia kwa upande wa chuo cha uhasibu Arusha ni Denson Ndiyemalila,upande wa kushoto ni shuhuda ni Emmanuel Nyivambe kutoka chuo cha Unadhimu Duluti.zoezi hilo lilifanyika katika chuo cha Uhasibu juzi jijini Arusha.(Habari Picha na Pamela Mollel)
Kushoto ni Mkuu wa chuo cha ukamanda na unadhimu Duluti Meja Jenerali H.Masebu akikabidhiana mkataba mpya wa ushirikiano(MoU) na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha,Dk.Faraji Kasidi mara baada ya kutiliana saini kati ya chuo cha uhasibu Arusha na chuo cha  unadhimu Duluti .
Kushoto ni mkuu wa chuo cha ukamanda na unadhimu Duluti Meja Jenerali H.Masebu akizungumza mara baada ya kutiliana saini  mkataba mpya wa ushirikiano(MoU) kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha,Dk.Faraji Kasidi .
Picha ya pamoja ya kumbukumbu mara  baada utilianaji saini huo.

MIGODI YA WACHIMBAJI WADOGO BUHEMBA YAFUNGULIWA

0
0
Hatimaye Serikali imefungua Migodi ya Dhahabu ya Wachimbaji Wadogo iliyopo katika eneo la Buhemba Wilaya ya Butiama Mkoani Mara baada ya kujiridhisha hali ya usalama katika migodi hiyo.

Migodi hiyo imefunguliwa rasmi na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo Januari 13, 2018 na kushuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi.Akizungumza katika tukio hilo, Nyongo alisema jumla ya migodi 10 imefunguliwa kati ya 16 baada ya kujiridhisha usalama wake.

Alifafanua kwamba eneo la Buhemba lina jumla ya Migodi ya Dhahabu 16 ambayo inamilikiwa na Wachimbaji Wadogo hata hivyo iliyokidhi vigezo vya kiusalama ni Migodi 10 pekee ambayo imeruhusiwa kuendeleza shughuli za uchimbaji.

Alisema Serikali ilisitisha shughuli za uchimbaji Madini kwenye eneo hilo la Buhemba Februari 2017 baada ya kutokea vifo vya Wachimbaji Saba na wengine wapatao 15 kujeruhiwa kutokana na kufanya shughuli zao bila kuzingatia taratibu na kanuni za uchimbaji salama.

Alibainisha kuwa Mwezi Desemba mwaka jana alifanya ziara kwenye eneo hilo ili kujionea hali halisi ya machimbo husika pamoja na kuzungumza na wachimbaji waliosimamishwa kuendeleza shughuli zao ambapo aliagiza shughuli za ukaguzi zikamilike ifikapo Mwezi huu wa Januari ili migodi ifunguliwe.
Naibu Waziri wa Madini, Stansalus Nyongo (kulia) akijiandaa kufungua rasmi Migodi ya Dhahabu ya Wachimbaji Wadogo wa Buhemba, Wilayani Butiama Mkoani Mara. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (kushoto) wakati wa kufungua migodi ya wachimbaji wadogo ya Buhemba. Wa pili kutoka kwake ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akijiandaa kufungua rasmi migodi hiyo.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) akifungua rasmi migodi ya Buhemba ya wachimbaji wadogo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima akishuhudia tukio hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima akizungumza wakati wa ufunguzi wa migodi ya wachimbaji wadogo ya Buhemba, Mkoani Mara.

NAIBU WAZIRI KIJAJI AFANYA UZINDUZI WA BARAZA LA WAFANYAKAZI CHUO CHA UHASIBU ARUSHA

0
0

Naibu Waziri wa fedha na mipango Mh.Dkt Ashatu Kijaji(Mb)katikati akinyoosha juu mkataba wa kuunda baraza ambao umehakikiwa na kusainiwa na Kamishna wa kazi,wa pili kulia niKaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha,Dk.Faraji Kasidi,na wakwanza kushoto ni Didas Malekia Mwenyekiti wa tawi la IAA chama kilichounda baraza la wafanyakazi(THTU).

Naibu Waziri wa fedha na mipango Mh.Dkt Ashatu Kijaji(Mb) ambaye  alikuwa mgeni rasmi akizungumza katika uzinduzi wa baraza la pili la Wafanyakazi wa chuo cha Uhasibu Arusha,alisema madhumuni ya baraza hilo ni kuwapa fursa watumishi kupitia wawakilishi wao pamoja na kujadiliana juu ya masuala mbalimbali.(Habari Picha na Pamela Mollel)
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akizungumza katika uzinduzi wa baraza la pili la wafanyakazi wa Chuo cha Uhasibu Arusha

Sehemu ya Baraza la Wafanyakazi Chuo cha Uhasibu Arusha

Baadhi ya wanafunzi chuo cha Uhsibu Arusha wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi kwa umakini ambapo pamoja na mambo mengi Naibu Waziri wa fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji aliwasisitiza umuhimu wa kila mmoja kuwa mshiriki mkubwa wa kupambana na rushwa ambayo inajikita katika kupotosha na kumomonyoa maadili. 


RC MNYETI KUWACHUKULIA HATUA WANASIASA WACHOCHEZI

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ametoa onyo kali kwa viongozi wa kisiasa wa Wilaya ya Kiteto kuwa atawachukulia hatua kali wote watakaosababisha migogoro ya ardhi kwa wananchi. 

Akizungumza kwenye kata ya Njoro, Mnyeti alisema atawachukulia hatua kali wanasiasa hao kwani yeye siyo mkuu wa mkoa wa maboksi anayeogopa kulowanishwa na mvua. Alisema alipata taarifa ya baadhi ya wanasiasa wanaotumia migogoro ya ardhi kwa ajili ya kujinufaisha kisiasa, ila hatawafumbia macho wanasiasa wa aina hiyo waliopo wilayani Kiteto. 

"Tumekuwa na migogoro isiyokwisha, wewe una shamba lako kwenye kijiji cha Bwawani kuna mtu anakuzuia kulima hapa Njoro? au ukiishi hapa Njoro kuna mtu amekunyima kununua nyumba kule Kibaya makao makuu ya wilaya?" alihoji Mnyeti. Alisema atawashughulikia wanasiasa hao wanachochea migogoro ya ardhi baina ya watu na watu na kijiji na kijiji ili iwe funzo kwao na hawatasahau kitendo hicho. 

"Wanasiasa hao wababaishaji, wanaojaribu kuishika serikali sharubu nitakula nao sahani moja, kwani hatuwezi kukubali hali hiyo ijitokeze na kuacha kuchukua hatua kwao bila kuangalia vyeo vyao," alisema Mnyeti. Hata hivyo, alimuagiza mkuu wa wilaya ya Kiteto, mhandisi Tumaini Magessa kuhakikisha vijiji vyote vinawekewa alama za mipaka ili kuondokana na migogoro ya ardhi. 
 Wananchi wa Kata ya Njoro Wilayani Kiteto, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akizungumza nao,  juu ya kuwachukulia hatua kali wanasiasa wanaosababisha migogoro ya ardhi. 
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akizungumza kwenye Kata ya Njoro Wilayani Kiteto juu ya kuwachukulia hatua kali wanasiasa wanaosababisha migogoro ya ardhi, kushoto ni mbunge wa jimbo hilo Emmanuel Papian na Mkuu wa wilaya hiyo mhandisi Tumaini Magessa.
Wananchi wa Kata ya Njoro Wilayani Kiteto, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akizungumza nao,  juu ya kuwachukulia hatua kali wanasiasa wanaosababisha migogoro ya ardhi. 

RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME AWASILI NCHINI NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumpokea katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye Gadi ya Jeshi ya heshma pamoja na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumpokea katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili (hazionekani pichani ) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakielekea Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia frame ya Picha ya Kiasili aliyokabidhiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kumpokea mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU

BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUZINGATIA SHERIA YA USALAMA KWENYE MAENEO YAO YA KAZI.

0
0
Na Joel Maduka-Geita.

Naibu waziri wa madini Doto Biteko amewataka wachimbaji ambao wanamiliki leseni kuhakikisha wanazingatia sheria ambazo wamepewa likiwemo suala la kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi kwenye maeneo yao ya mgodi ili kuepukana na majanga ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara kwenye shughuli za uchimbaji.

Akizungumza wakati alipotembelea na kutoa pole kwenye mgodi mdogokijiji cha Buntubili eneo ambalo hivi karibuni mchimbaji mmoja aliangukiwa na kifusi na kufariki.Naibu waziri Doto alisema ni vyema kwa kila mwenye leseni kuhakikisha usalama unakuwa ni jambo la kwanza huku akimwagiza afisa madini kufuatilia migodi yote kama imewekwa mabango ambayo yanaelekezea suala la usalama kwenye mazingira hayo.

“Hatutaki kuona hata mtanzania mmoja anakufa katika mazingira ya uzembe tunatamani tuone watanzania wote wanachimba wanaendeleza mali na wanabaki kuwa salama kwaajili ya kulihudumia Taifa hili ,Taifa hili linawaitaji watu wote kwa hiyo nitoe wito kila mwenye leseni maali popote alipo ahakikisha kwamba mazingira yake ya kazi usalama kiwe kipaumbele na sasa kuanzia leo afisa madini ninakuagiza wote wenye leseni ambao wanaendeleza migodi waweke mabango yanayoeleza umuhimu wa usalama kila kwenye mgodi unaofanya kazi”Alisisitiza Mh,Doto.

Pamoja na hayo Naibu Waziri wa Madini amewataka wananchi kutokuingia kwenye maeneo ambayo yamesimamishwa na ambayo ni hatarishi kwani kufanya hivyo wanaweza kujisabasha hatari ya kupoteza maisha kutokana na maeneo hayo kutokuwa kwenye hali nzuri ya uchimbaji.
Naibu waziri wa madini Doto Biteko,Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Buntumbili Wilayani Bukombe ambapo kulitokea tukio la mchimbaji kufukiwa na kifusi wakati alipokuwa kwenye shughuli za uchimbaji. 
Naibu waziri wa madini Doto Biteko pamoja na viongozi wa Wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye eneo ambalo ajali ya mchimbaji kufukiwa na kifusi ilitokea 
Baadhi ya viongozi na Naibu waziri wa madini Doto Biteko wakiwa kwenye shimo ambalo ndipo mchimbaji mdogo ambaye alipoteza uhai wakati akiwa kwenye shughuli za uchimbaji.
Naibu waziri wa madini Doto Biteko akipatiwa maelezo ya namna ajali hiyo ilivyotokea mgodini hapo.
Mmiliki wa mgodi huo,akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa madini namna ambavyo wachimbaji hao walivyovyamia eneo hilo na kuanza shughuli za uchimbaji hali ambayo imesababisha mmoja wao kufukiwa na kifusi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akutana na Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Kampuni ya Mkulazi

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Kampuni ya Mkulazi kupata taarifa ya maendeleo ya Uwekezaji katika uzalishaji Sukari Nchini, Ofisini kwake Mlimwa, mjini Dodoma. Januari 14, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Kampuni ya Mkulazi kupata taarifa ya maendeleo ya Uwekezaji katika uzalishaji Sukari Nchini
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Kampuni ya Mkulazi  Ofisini kwake Mlimwa, mjini Dodoma. Januari 14, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU AUVUNJA MFUKO WA WAKFU WA KUENDELEZA KAHAWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuvunja Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza zao la Kahawa (CDTF) na amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuchunguza mwenendo wa mfuko huo tangu ulipoanzishwa.

Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Januari 14, 2018) wakati akizungumza na wadau wa zao hilo kwenye kikao cha kujadili maendeleo ya zao la kahawa alichokiitisha, mjini Dodoma. Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada ya kubaini kwamba uundwaji wa mfuko huo si wa kisheria bali ni wadau wa zao hilo kwa kushirikiana na Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB).

“Wakati Serikali inapambana kupunguza makato ya hovyo kwa wakulima, kumbe huku kuna chombo cha kuwachukulia fedha wakulima hii haikubaliki.”Pia aliagiza kufungwa kwa ofisi za CDTF ili kupisha uchunguzi na baada ya CAG kukamilisha uchunguzi na kukabidhi ripoti, kazi zote zilizokuwa zinafanywa na mfuko huo zitafanywa na Bodi ya Kahawa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameongeza kuwa  majukumu ya kuundwa kwa mfuko huo yanaingiliana na yale ya Bodi ya Kahawa, ambayo ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya zao hilo, hivyo hakuna haja ya kuwa vyombo viwili vinavyofanya kazi moja.Wakati huo huo, Waziri Mkuu amepiga marufuku wanunuzi wa kahawa kwenda kununua kwa wanavijiji na badala yake kahawa yote itauzwa kwa njia ya minada.

“Kahawa itauzwa katika minada tu na utaratibu wa kutoa vibali kwa wanunuzi wa kahawa kwenda kununua kwa wananchi vijijini marufuku kuanzia sasa, kama kuna watu wamepeleka fedha zao wazirudishe kwani hazitafanya kazi.”Amesema Wakuu wa Mikoa na Wilaya wasimamie uuzwaji wa zao hilo na kuwachukulia hatua wote watakaokutwa wananunua kahawa kwa wakulima. 

“Anayetaka kahawa akanunue mnadani na si kwa wanavijiji lengo ni kuhakikisha mkulima anapata tija.”Pia ameziagiza halmashauri zote zinazolima kahawa nchini kuanzisha vitalu vya miche ya kahawa na kisha kuigawa bure kwa wakulima, pia Maofiza Kilimo wawaelimishe walkulima wote wenye miti mikongwe waanzisha mashamba mapya.

Kuhusu suala la utafiti wa zao hilo, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Kilimo itumie vyuo vyake vya kilimo ianzishe vituo vyake vya utafiti vitakavyofanya kazi ya utafiti wa zao hilo.
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images