Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro ofisini  kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro ofisini  kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro  mara baada ya kufanya mazungumzo ofisini  kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro  mara baada ya kufanya mazungumzoleo ofisini  kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Waziri wa Kilimo Dkt.Tizeba akagua usafirishwaji wa Korosho-Mtwara.

$
0
0
Waziri wa Kilimo Dkt.Charles Tizeba ametembelea Bandari ya Mkoa wa Mtwara na kukagua Usafirishaji wa Zao la Korosho Ghafi zinazokwenda nchi za India na Vietnam.
Kufikia Januari 10 mwaka huu Jumla ya Tani Laki 190 za Korosho tayari zimesafirishwa, ambapo lengo ni kusafirisha Tani 230 katika Msimu huu.
Waziri wa Kilimo Charles Tizeba akiwa na Mkuu wa Bandari ya Mtwara Nelson Mlali wakikagua mizigo ya Zao la Korosho inayosafirishwa kwenda katika Nchi za India na Vietnam. 
Waziri wa Kilimo Charles Tizeba akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Bandari Nelson Mlali na Kulia kwake Kaim Mkurugenz Bodi ya Korosho CBT Hassan Jarufu Mara baada ya kuingia Eneo la Bandari ya Mtwara.
 Kaimu Mkurugenz wa Bodi ya Korosho CBT Hassan Jarufu akimtambulisha Meneja Mkuu wa TANECU Mohammed Mwinyuku kwa Waziri wa Kilimo Charles Tizeba Mara baada ya Kuwasili katika Uwanja wa Ndege Mkoani Mtwara,Waziri wa Kilimo Charles Tizeba yupo Ziara ni Mkoa wa Mtwara kukagua Uuzwaji wa Zao la Korosho.

TRL YATANGAZA RATIBA USAFIRI WA TRENI KUANZIA DODOMA, WALIOKATA TIKETI DAR WARUDISHIWA NAULI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.

KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL) imesema imeamua kuhamishia huduma ya usafiri wa treni kutokea Dodoma kuanzia kesho.Uamuzi huo unakuja kipindi ambacho TRL imesitisha huduma za usafiri huo kutokea Dar es Salaam baada ya miundombinu ya reli kuharibika kati ya stesheni za Kilosa na Gulwe kutokana na mafuriko ya mvua zinazonyesha maeneo hayo kuharibu miundombinu. 

Akizungunza Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu Msaidizi (uendeshaji) kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuuu wa kampuni hiyo, Focus Sahani amesema wakati wanaendelea na matengenezo ya miundombinu iliyohariviwa na mafuriko eneo hilo wameona ni vema usafiri huo ukaendelea kwa kuanzia Mkoa wa Dodoma. 

Amesema uongozi baada ya kutathimini hali ya miundombinu ya maeneo mengine yaliyo salama imeamua kuhamishia huduma ya usafiri huo wa treni kutokea Dodoma. Sahani amesema ratiba ya huduma ya muda wa kuanzia Dodoma ni kwamba treni ya abiria itaondoka saa moja usiku kesho Jumanne na Ijumaa kwenda Kigoma, Mwanza Name Mpanda ambako inatarajiwa kuwasili Mwanza saa 12 jioni siku ya Jumatano na Mpanda saa 12 jioni na Kigoma saa 12 jioni. 

"Treni kutoka Mpanda, Mwanza na Kigoma zitatoka huko siku za Jumapili na Alhamis tu. Mpanda inatoka saa moja asubuhi, Mwanza inatoka saa mbili asubuhi na Kigoma inatoka saa1:30 asubuhi.Treni hizo zinafika Dodoma siku ya Jumatatu na Ijumaa saa 1:00 asubuhi, "amesema. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi (Uendeshaji) wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Focus Sahani akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu uamuzi wa kampuni hiyo kutangaza ratiba ya usafiri wa treni kuanzia Mkoa wa Dodoma kwenda mikoa mingine baada ya huduma ya usafiri huo kusitishwa kwa stesheni ya Dar es Salaam.Pichani kushoto ni wengine ni maofisa wa kampuni hiyo.

Johari Mussa, mshindi wa Milioni 10 Mlimani City.

$
0
0
MSHINDI wa Promosheni ya Mlimani City katika kipindi cha msimu wa siku kuu ya Krismass na Mwaka mpya ya fanya manunuzi Mlimani City na ushinde ijulikanayo kama “Mlimani City Grand Shopping Fest” amepatikana mwishoni mwa wiki mara baada ya kuchezesha droo kubwa na ya mwisho ambaye ni Johari Mussa mkazi wa Makongo juu jijini Dar es Salaam.

Johari aliibuka mshindi jana kajishindia vocha yenye thamani ya Shilingi milioni moja na zawadi zake tayari zimesha nunuliwa na ziko tayari kwa kukabidhiwa rasmi.
Johari aliibuka mshindi katika droo kubwa iliyohudhuriwa na mgeni rasmi Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora aliwapongeza uongozi wa Mlimani City kwa ubunifu wa hali ya juu wa kuwajali wapangaji wao pamoja na wateja wanaofanya manunuzi Mlimani City na kuwaomba waendelee na Kampeni za ubunifu kama hizo kwani zinammfanya mpangaji na mteja ajisikie vizuri kuwa anathamani na mchango wake unathaminika afanyapo manunuzi yoyote Mlimani City.

Profesa Kamuzora alisema Serikari inatambua mchango wa Mlimani City na inauthamini sana kwani huduma bora na za kimataifa zitolewazo na Mlimani City sifa ni kwa Taifa pia.
Aidha pia aliwapongeza washindi 100 wote waliopatikana katika kipindi cha promosheni ya kila wiki kwa wiki tano mfululizo ambao walijishindia vocha yenye thamani ya Shilingi laki moja kila mmoja, lakini pia aliwapongeza washindi watano(5) waliojishindia vosha yenye thamani ya shilingi milioni moja kila mmoja na zaidi alimpongeza mshindi mkubwa, Johari Mussa mkazi wa Makongo kwa kuibuka mshindi wa vocha yenye thamani ya milioni kumi ambapo alitoa wito kwa washindi na ambao hawakushinda kuwa mabalozi wazuri wa Mlimani City.

Nae Meneja wa Mlimani City, Pastory Mroso aliwapongeza washiriki wote waliofanikwa kuingia kwenye ushindani wa kupata bahati ya kujishindia zawadi na kuwaomba wasikose kushiriki tena awamu nyingine. 
 Meneja Mkuu wa Mlimani City Mall, Pastory Mroso(kushoto) akimuonyesha Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora(katikati), zawadi za mshindi wa kwanza wa promosheni maalumu ya siku kuu ya Krissmas na Mwaka mpya zenye thamani ya Shilingi milioni kumi.Droo ya kumpata mshindi ilifanyika Mlimani City mwishoni mwa wiki.Kulia ni Oparasheni Meneja wa Mlimani City, Girish Kumar.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora(kashoto) akisoma kuponi ya mshindi wa kwanza wa promosheni maalumu ya siku kuu ya Krissmas na Mwaka mpya yenye thamani ya Shilingi milioni kumi.Droo ya kumpata mshindi ilifanyika Mlimani City mwishoni mwa wiki.Kulia ni Mwakilishi kutoka Gaming Board, Abdalah Singano.

WAZIRI UMMY ASHTUSHWA NA MSONGAMANO WA WAGONJWA TEMEKE

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Waziri wa Afya Wanawake,Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  ameshtushwa na wingi wa wagonjwa waliopo katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke na kuagiza katibu Mkuu wa Wizara hiyo kufanya utaratibu wa kuongeza madaktari ili kutoa huduma kwa ufanisi.

Waziri Ummy ametoa maagizo hayo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kutembelea Hospitali zote za Mikoa za Rufaa ambazo Rais Magufuli ameagiza zianze kuhudumiwa na Wizara ya afaya badala ya halmashauri husika.

"Nimetembelea hapa nimejionea mwenyewe kuwa  na msongamano mkubwa sana hapa kiasi cha Daktari mmoja kuweza kuhudumia wagonjwa 300 kwa siku kwa mujibu wa maelezo ya Mganga mkuu wa hospitali hii jambo ambalo  linahitaji kushughulikiwa mapema hivyo namuagiza katibu mkuu kuweza kuongeza madaktari hapa hili waweze kuwahudumia Wananchi kwa wakati"amesema Ummy.

Waziri Ummy pia alimwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kuhakikisha kuwa anaweka X Ray katika hospitali zilizopo chini yake hili kuweza kupunguza wimbi lka wagonjwa wengi amabo ukimbilia katika Hospitali hiyo.
 Waziri wa  Afya Wanawake Jinsia Wazee na  Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na Mmoja wa Wanawake  waliojifungua katika Hospitali ya  Rufaa ya Temeke na kubaini kuwepo kwa idadi kubw aya wagonjwa kuliko kawaida kutokana na Daktari mmoja kihudumia wagonjwa zaidi ya 300 katika OPD.
 Waziri wa Afya Wanawake Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizunguma na watu waliojaa katika Mapokezi ya Hospitali ya  Rufaa Temeke amabo wanahudumiwa na madkatari wachache.
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke, Dk Amani Malima akitoa maelezo kwa  Waziri wa Afya Wanawake Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  kwanini hospitali hiyo ina wagonjwa wengi .
 Sehemu ya Umati wa Wagonjwa waliofurika katika Hospitali ya Rufaa Temeke.
 Waziri wa Afya Wanawake Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa Habari.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke Dr. Amani Malima akizungumza na Waandishi wa Habari.

WAKATI Album lunch on Tuesday 23.1.2018, 7:30pm at the Geoethe-Institut Dar es salaam

$
0
0
The Wakati album lunch is also a charitable fundraiser to support the renowned visual artist – Augustino Malaba – who is one of the oldest Makonde masters. During his life, Malaba has produced amazing  artwork and contributed to the cultural development and creative industries scene in Tanzania. 
The album WAKATI would like to make a statement that we must take care of the older generation of artists and show our appreciation for their creative work. Therefore, proceeds from the sale of all CDs at this event, will go towards supporting his medical and living expenses.

As you know Wakati means “time” in Kiswahili. The songs on this album portray the essence of daily life from for local Tanzanians, with messages to encourage people to appreciate that time is precious and to live the moment.  We should not wait until the last tree has been cut down, before realizing the importance of the environment for our sustenance. We should not wait until loved ones are gone, before appreciating the beauty of their presence. We should not wait until losing a job, before remembering how difficult it is to find another job. “Yesterday is the past, tomorrow is the future, but today is a gift - that’s why it’s called the present.” You only get one chance to appreciate and that time is now, it is your time, it is my time - let us not wait until time has past us by, only to discover what we have missed.

This album is the result of a creative process, traversing the musical combinations of afro-pop, bongo-fusion, reggae, and other local styles.

MKURUGENZI WA TPA AKUTANA NA BALOZI WA CHINA

$
0
0
Balozi wa China Nchini Tanzania Bi. Wang Ke akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko mara baada ya kumtembelea ofisini kwake. Balozi Wang amefanya ziara hiyo ya kuja kutoa shukuruni zake kwa Mkurugenzi Mkuu kwa jinsi TPA ilivyohudumia meli yao ya Kichina yenye Hospitali. Pamoja na shukurani hizo, viongozi hao pia walizungumzia maendeleo ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo pamoja na jinsi Treni ya TAZARA inavyohudumia mizigo ipitayo bandarini.

SERIKALI YATOA UFAFANUZI WA MATUMIZI YA FEDHA ZA KIGENI

$
0
0
Na:  WFM.

Serikali haijazuia matumizi ya fedha za kigeni nchini bali imechukua hatua ya kudhibiti matumizi ya fedha hizo ili kulinda thamani ya Shilingi ya Tanzania.

Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) alipokutana na wawakilishi wa wafanyabiashara mkoani Arusha kujadiliana mambo mbalimbali kwa ajili ya kukuza sekta ya  biashara nchini. 

Amesema kuwa sheria haijazuia matumizi ya fedha za kigeni nchini lakini inasisitiza kuwa watu wanapaswa kutambua kuwa sarafu ndiyo fedha halali kwa malipo ndani ya nchi.“Tatizo kubwa tunalokumbana nalo ni uhuru ulioachiwa ambao unasababisha kushuka kwa thamani ya Shilingi yetu kwani kila mmoja anaweza kutumia fedha za kigeni pia watumiaji wa fedha za kigeni hawafuati thamani ya fedha iliyoko sokoni kila mmoja anakuwa na kiwango tofauti cha thamani ya kubadili fedha za kigeni”. alifafanua Dkt. Kijaji.

Ili kuondoa changamoto hizo Serikali imeamua kurekebisha sheria ya matumizi ya fedha za kigeni na sheria ya Benki Kuu huku ambayo inazitaka  bei zote hapa nchini zitangazwe kwa Shilingi ya Tanzania. Bei hizi zinajumuisha kodi za nyumba za kuishi na ofisi, bei za ardhi, gharama za elimu na afya, bei za vyombo vya usafiri na vifaa vya kielektroniki. 

“Bei ambazo walengwa wake wakuu ni watalii au wateja ambao sio wakazi zinaweza kutangazwa kwa fedha za kigeni na malipo yake yanaweza kufanyika kwa fedha za kigeni. Hata hivyo kama mlengwa akitaka kulipa kwa Shilingi ya Tanzania asilazimishwe kulipa kwa fedha za kigeni” alieleza Dkt. Kijaji.

Aidha, viwango vya kubadilishia fedha vitakavyotumika katika kuweka hizo bei katika sarafu nyingine vimetakiwa kuwekwa wazi na visizidi vile vya sokoni. Mkazi yeyote wa Tanzania au mtu wa nje anayeishi Tanzania  asilazimishwe kufanya malipo yoyote kwa kutumia fedha za kigeni kama ana Shilingi ya Tanzania mkononi mfano gharama za shule na hoteli.

Aidha Serikali imeagiza vyombo vya dola kuchukua hatua za kisheria kwa wote watakaokiuka maagizo hayo yaliyotolewa na Serikali.Naibu Waziri Dkt. Kijaji alitoa rai kwa wafanyabiashara nchini kuhimiza matumizi ya sarafu ili kuweza kukuza thamani ya Shilingi hivyo kusaidia kuinua uchumi wa nchi. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akifafanua kuhusu matumizi ya fedha za kigeni ambapo alieleza kuwa Serikali imedhibiti matumizi ya fedha hizo ili kulinda thamani ya shilingi wakati wa Mkutano wa Naibu Waziri huyo na Wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango).
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) pamoja na meza kuu wakimsikiliza kwa makini mmoja wa wafanyabiashara (hayupo pichani) aliyekuwa akiuliza kuhusu matumizi ya fedha za kigeni wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri huyo na Wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha.
 Baadhi ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha wakiwa katika mkutano na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) kuhusu ukuzaji wa Sekta ya Biashara Jijini Arusha.

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 11 ajali ya Kagera

TUTAKAMILISHA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MUSOMA -MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha inakamilisha ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara iliyoanza kujengwa mwaka 1980.

Atoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Januari 15, 2018) wakati alipokagua ujenzi wa hospitali hiyo baada ya kuwasili mkoani Mara kwa ajili ya ziara yake ya kikazi.

Waziri Mkuu amesema Serikali itakamilisha ujenzi wa jengo hilo kwa awamu, ambapo wataanza na eneo la mapokezi na vyumba vya madaktari.

Amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya nchini, hivyo amewaomba wananchi waendelee kuiamini na kushirikiana nayo.

Waziri Mkuu amesema tayari Serikali imetoa sh. bilioni 1.4 ili ujenzi uendelee. Ujenzi huo ulianza mwaka 1980, ulisimama mwaka 1987 kuanza tena 2010.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amekagua uwanja wa ndege wa Musoma mkoani Mara ambao unatarajiwa kukarabatiwa na kuwekwa lami.

Amesema kukamilika kwa ukarabati huo wa kiwanja hicho kutafungua fursa za utalii ndani ya mkoa huo ambao umezungukwa na vivutio vingi.

Amesema Serikali imedhamilria kukarabati viwanja mbalimbali vya ndege nchini kikiwemo cha Musoma ili kuboresha huduma za usafiri wa anga.

Viwanja vingine vinavyotarajiwa kukarabatiwa ni Iringa, Kilwa Masoko, Lake Manyara, Lindi, Moshi, Njombe, Tanga, Simiyu, Singida na Songea.
Waziri Mkuu amesema viwanja hivyo kwa sasa vinakarabatiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), ambao wanajenga kwa gharama nafuu na kwa viwango vinavyostahili.

Awali, Meneja wa TANROADS, mkoa wa Mara Mhandisi Mlima Ngaila alisema ukarabati huo utafanyika kwa awamu tatu ambapo ya kwanza itahusisha upanuzi wa uwanja na ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege.

Alisema barabara ya kuruka na kutua ndege ina urefu wa km. 1.6 na upana wa mita 33 ni ya changarawe, hivyo kusababisha baadhi ya ndege kushindwa kutua.

Pia, Waziri Mkuu alikagua ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Musoma na kwamba ameridhishwa na ukarabati wa miundombinu ya shule hiyo.

“Shule hii ilipewa sh bilioni 1.28 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu. Nimekagua jengo la utawala, madarasa, mabweni, jiko, maabara na bwalo, nimeridhika na kazi iliyofanyika.”

Shule hiyo ni miongoni mwa shule 10 kongwe ambazo Serikali iliamua kuzikarabati ili ziweze kurudi kama zamani na kuendelea kutumika.

Hata hivyo Waziri Mkuu aliuagiza uongozi wa Manispaa ya Musoma kushirikiana na uongozi wa shule hiyo katika kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili.

Miongoni mwa changamoto hizo ni malipo ya watumishi wasaidizi wakiwemo wapishi, walinzi na madereva, ambapo aliitaka kuchukua jukumu la kuwalipa watumishi hao badala ya kuacha jukumu hilo kwa Mkuu wa Shule.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATATU, JANUARI 15, 2017.

IGP SIRRO ATETA NA KUSAINI MKATABA NA MWENZAKE WA MSUMBIJI KUKOMESHA UHALIFU

MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI ZENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2 WILAYANI UKEREWE

$
0
0

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina ametaifisha na kuteketeza zana haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2 zilizokamatwa wakati zikitumika kwa shughuli za uvuvi katika visiwa vidogo vilivyopo ndani ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza huku Shilingi milioni 120 zikikusanywa kama sehemu ya adhabu kwa wavuvi na wafanyabiashara waliokutwa na zana haramu pamoja na makosa ya utoroshaji samaki na mazao yake nje ya nchi.

Waziri Mpina aliwaonya watu wanaotumia majina ya wavuvi kutishia kufanya migomo isiyoisha na kuandamana baada ya uamuzi wa Serikali kuanza kuchukua hatua stahiki za kudhibiti uvuvi haramu, na kwamba msimamo uliowekwa na Serikali ni thabiti na usiyoyumba hivyo migomo na maandamano ya watu wenye lengo la kukwamisha vita dhidi ya uvuvi haramu haitasaidia chochote na badala yake operesheni kali isiyo na mwisho itaendelea hadi pale uvuvi haramu utakapokoma ndani ya Ziwa Victoria.

“Rasilimali zilizopo ndani ya ziwa hili ni mali ya wananchi sisi viongozi mliotupa dhamana ya kuongoza kazi yetu ni ulinzi tu na endapo tutakomesha uvuvi haramu nyie ndio mtakaonufaika hivyo ni itashangaza tajiri aliyempa kibarua cha ulinzi, na mlinzi huyo akafanya kazi vizuri ya kulinda mali za bosi wake alafu tajiri akamlalamikia kibarua wake sisi na watendaji wa Serikali ni vibarua tu wenye mali ni ninyi hatua tunazochukua zitaleta manufaa makubwa kwenu”alisema.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani) baada ya kuwasili kwenye kambi ya Uvuvi ya Kisiwa cha Galinzila leo na kuongea na wavuvi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estomiah Chang’a (mwenye kofia) na kulia zaidi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ukerewe Frank Bahati leo. Mhe. Mpina alichoma moto nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni mbili. (Na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akiwahutubia wavuvi kwenye kambi ya wavuvi katika kisiwa cha Galinzila Wilayani Ukerewe ambapo baadaye alichoma moto nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni mbili katika kijiji Kakukuru.
Umati wa wavuvi kwenye kambi ya wavuvi ya Kisiwa cha Galinzila wilayani Ukerewe wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (hayupo pichani) ambapo baadaye alichoma moto nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni mbili katika kijiji cha Kakukuru zilizokamatwa katika operesheni maalum ya siku tano ya kutokomeza uvuvi haramu katika Wilaya ya Ukerewe leo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akiwa katika picha ya pamoja na kikosi kazi kilichofanya operesheni ya kutokomeza uvuvi haramu katika Wilaya ya Magu na Busega mara baada ya kuteketeza kwa kuchoma moto zana haramu za uvuvi zenye thamani ya Tsh 457,075,000/= katika kijiji cha Kageye wilayani Magu leo. 


RAIS KARIA AMPONGEZA DAMAS NDUMBARO UBUNGE SONGEA MJINI

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Ndugu Wallace Karia kwa niaba ya Shirikisho anatoa pongezi kwa mwanamichezo daktari wa Sheria Dr.Damas Ndumbaro kwa kushinda kiti cha Ubunge Jimbo la Songea Mjini.

Rais Karia amesema ushindi wa Dr.Ndumbaro unaongeza wanamichezo zaidi katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wanaweza kuwa chachu ya maendeleo ya michezo ikiwemo mpira wa miguu.

Amesema uzoefu wa Dr.Ndumbaro katika mpira wa miguu utasaidia katika nyanja hiyo na itasaidia kupaza sauti kupitia bunge katika harakati za kushirikiana kuusogeza mbele mchezo wa soka.

“Tunaamini uwezo wa Dr.Ndumbaro katika uongozi tumemuona katika mpira wa miguu akiongoza katika sehemu mbalimbali hakika uwezo wake wa uongozi ni mkubwa na atasaidia sana kukua kwa sekta hii ya michezo,sisi TFF tunamtakia kila la kheri kwenye majukumu yake mapya na tutampa ushirikiano wote kuhakikisha tunafikia mafanikio,kwetu ni faraja kubwa kuona wana familia wa mpira wa miguu wakishinda nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Ubunge”.Alisema Rais Karia.

Rais Karia ameongeza kuwa anaamini Dr.Ndumbaro jimbo lake la Songea Mjini litakuwa moja ya majimbo yenye mfano wa kuigwa katika maendeleo ya mpira wa miguu.Dr.Ndumbaro amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwenye mpira wa miguu na hivi karibuni Rais Karia alimteuwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya rufaa ya leseni za klabu.

Akigombea kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dr.Ndumbaro amejizolea kura 45762 akiwazidi wagombea wengine 7 kutoka vyama mbalimbali.

CAF YATEUA WANNE TFF KUSIMAMIA MECHI

$
0
0

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF limepitisha majina manne ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kuwa makamishna wa michezo mbalimbali inayoandaliwa na CAF.

Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zilizotoa Makamishna wanne ambayo ni idadi ya juu hakuna nchi iliyozidisha idadi hiyo ambayo ni kwa kipindi cha kutokea mwaka 2018 mpaka 2020.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF waliopata nafasi hiyo ni Makamu wa Rais Michael Wambura,Ahmed Mgoyi,Amina Karuma na Sarah Tchao.

Wambura kwa upande wake amechaguliwa kutokana na kufanya vizuri katika aiku za nyuma wakati Mgoyi amepata nafasi hiyo kwa kufanya vizuri kama mechi kamishna wa michezo ya CECAFA nao Karuma na Tchao wameipata nafasi hiyo kutokana na mkakati wa CAF kuanza kuwajengea uwezo viongozi wanawake vijana.

Kuteuliwa kwa viongozi hao wa TFF ni muendelezo CAF kuteua viongozi wa TFF kwenye kamati mbalimbali itakumbukwa hivi karibuni Rais wa TFF aliteuliwa kuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya fainali za Africa kwa wachezaji wa ndani CHAN inayoendelea nchini Morocco lakini pia akiteuliwa kuwa Kamishna wa mechi ya ufunguzi iliyowakutanisha wenyeji Morocco na Mauritania.

MCB YAZINDUA BIDHAA ‘TUKUTANE JANUARI’

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Benki ya ya Mwalim Commercial (MCB) imezindua bidhaa ya Tukutane Januari kwa ajili ya mkakati wa kuboresha maisha ya watanzaia.

Akizungumza na waandishi habari katika uzinduzi wa bidhaa hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa MCB , Ronald Manongi amesema kuanzishwa kwa bidhaa hiyo ni kwa ajili kuwasaidia watanzania wasipate shida kila inapofika Januari.

Manongi amesema kuwa mteja ataweza kujiwekea akiba kidogo kidogo wakati wowote katika kipindi chote cha hadi Januari.Amesema akaunti hiyo ina riba ya kuvutia ambayo mteja atalipwa riba kila robo ya mwaka pamoja na kumfanya mteja kukopa wa hadi asilimia 30 ya amana yake katika kipindi cha mwaka husika.

Aidha amesema faida ya akaunti hiyo itamuondolea usumbufu wa kutatua mahitaji muhimu ya kipesa katika kipindi cha mwanzo wa mwaka husika ikiwa ni pamoja na ada za shule , vyuo , vifaa vya shule , kodi za nyumba .

Manongi amesema amewasaa watanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba mara kwa mara kwani husaidia kutatua matatizo mengi yanayowakabili.
Mkurugenzi Mkuu wa Mkuu wa Mwalimu Commercial Benki (PLC), Ronald Manongi (katika)akizungumza na waandishi habari kuhusiana na uzinduzi wa bidhaa mpya ya Tukutane Januari leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Meneja wa Tawi la Samora, Leticia Ndogole na kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji wa Biashara na Masoko Valence Luteganya

UDSM WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI

SERIKALI YARIDHIA UAMUZI WA KAMPUNI YA IPP KUHUSU GAZETI LA NIPASHE JUMAPILI

Article 1

MWALIMU COMMERCIAL BANK PLC YAZINDUA BIDHAA KWA AJILI YA KUBORESHA MAISHA YA WATANZANIA.

$
0
0

Mwalimu Commercial Bank PLC (MCB) imezindua bidhaa iitwayo Tukutane Januari Akaunti, ikiwa ni moja ya mkakati wake katika kuboresha maisha ya Watanzania kwa ujumla. 

Akizungumzia Kuhusu akaunti hii mpya ya akiba ya ‘Tukutane Januari’, Mkurugenzi Mkuu wa MCB, Bwana Ronald Manongi alisema, mteja ataweza kujiwekea akiba kidogo kidogo wakati wowote katika kipindi chote cha hadi kufikia Januari. Akaunti hii ina riba ya kuvutia ambayo mteja wetu atalipwa kila robo ya mwaka. 

Vilevile inamuwezesha mteja wetu kupata mkopo wa hadi asilimia 30 ya amana yake katika kipindi cha mwaka husika. Hivyo Mteja atakapoweka akiba zaidi atafaidika zaidi, na atakuwa na uwezo wa kukopa kiasi kikubwa kulingana na akiba ya akaunti yake. 

Akaunti hii ya akiba itamuwezesha mteja kujiondolea usumbufu wa kutatua mahitaji muhimu ya kipesa kipindi cha mwanzo wa mwaka husika ikiwa ni pamoja na ada za shule na vyuo na manunuzi mengine ya vifaa vya shule, pia kodi za nyumba hivyo kuondokana na dhana ya Januari kuwa ni mwezi mgumu. 

Mkurugenzi huyo pia aliwaasa watanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba mara kwa mara kwani husaidia sana kutatua matatizo mengi yanayoikabili familia na jamii kwa ujumla. “Mara nyingi watu wamejikuta wakiingia katika madeni makubwa na fedheha pale wanaposhindwa kulipa madeni hayo”, alisema Ndugu Manongi. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Mwalimu Commercial Plc,  (MCB) Ronald Manongi (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi ya akaunti mpya ya ‘Tukutane Januari’ yenye lengo la kuhamasisha moyo wa ujiwekea akiba kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja wa Tawi la Samora, Leticia Ndongole, Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko, Valence Lutegenya na Meneja Mahusiano kwa Wateja, Charles Shadrack. Akaunti hii itakuwa mkombozi kwa wateja kuweza kujiwekea akiba itakayowawezesha kumudu mahitaji muhimu yanayojitokeza  mwanzoni mwa mwaka.  
 Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko wa Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), Valence Luteganya (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi ya akaunti mpya ya ‘Tukutane Januari’ yenye lengo la kuhamasisha moyo wa kujiwekea akiba kwa wateja wake na kwa watanzania kwa ujumla. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja wa Tawi la Samora, Leticia Ndongole, Ofisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Ronald Manongi, Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko, Valence Lutegenya na Meneja Mahusiano kwa Wateja, Charles Shadrack. Akaunti hii itakuwa mkombozi kwa wateja kuweza kujiwekea akiba itakayowawezesha kumudu mahitaji muhimu yanayojitokeza  mwanzoni mwa mwaka.  

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAMA SHEIN AFUNGUA KONGAMANO LA AFYA NA MAISHA BORA

$
0
0
  MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman, wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Inaya Zanzibar Limited Cheherazade Cheikh akitoa maelezo ya bidhaa za kampuni yake katika Maonesho ya Tamasha la Nne la Biashara Zanzibar linalofanyika katika viwanja vya mpira maisara.(Picha na Ikulu)
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akitembelea maonesho Tamasha la nne la Biashara katika viwanja vya mpira vya maisara Zanzibar akimsikiliza Mjasiriamali wa Kikundi cha ZAIDAT cha Chukwani Tatu Suleiman, wakati akitembelea maonesho hayo.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman, wakimsikiliza Mjasiriamali wa Kikundi cha ZANAP Nassor Hamad Omar, akitowa maelezo ya bidhaa zinazozalishwa na kikundi chao wakati wa maoenesho ya Biashara katika viwanja vyaa maisara Zanzibar.
 WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amani Salum Ali akizungumza wakati wa Kongamano la Afya na Maisha Bora, wakati wa Tamasha la Nne la Maenesho ya Biashara katika viwanja vya maisara Zanzibar.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images