Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

ATCL YAKUMBUKA WATOTO YATIMA

$
0
0
Na Said Mwishehe,  Globu ya jamii
SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) limetoa msaada wa vyakula , mafuta , sabuni, nguo,sukari na madaftari kwa Kituo cha Mwandaliwa ambacho kinaelea watoto yatima.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa ATCL, Christina Tungaraza amesema thamani ya msaada huo umegharimu sh.milioni tano ikiwa ni kutambua umuhimu wa jamii kusaidia wasiojiweza na hasa watoto yatima.

"Tumeanza mwaka mpya kwa kusaidia watoto walioko kwenye kituo hiki na mbali ya kuleta msaada huu, tunataka kuzungumza na uongozi kuona ni maeneo gani tunaweza kuendelea kusaidia" amesema Tungaraza.

Amefafanua msaada ambao wameutoa kwa watoto hao ni ule ambao unatumika na kwisha na sasa wanachotaka ni kutoa msaada ambao utadumu zaidi.

Tungaraza amesema shirika lolote la biashara mteja lazima awe namba moja kwao na wanatoa kipaumbele kwa mteja na kurudisha sehemu ya faida kwa wananchi.

Akiuzungumzia msaada huo Mwanzilishi na Mkurugenzi wa kituo hicho, Halima Mpeta ametoa shukrani kwa msaada huo wa ATCL na kuiomba jamii kuiga mfano huo kwa kusaidia watoto walioko hapo.

Amesema kuna vitu ambavyo si lazima kuvifanya lakini la kusaidia watoto yatima lina umuhimu wake na ndio maana tunaomba wenye uwezo wasaidie.

"Tunawashukuru ATCL kwa msaada wao, tunauthamini sana na tunathamini wafanyakazi wote na walichotoa Mungu atakirejesha na kulifanya shirika hilo kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha,"amesema Mpeta.
Meneja Masoko wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Bi. Christina Tungaraza akikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali kwa Bi. Halima Ramadhani Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Mbweni jijini Dar es salaam wakati wafanyakazi wa shirika hilo walipotembelea na kuwafariji watoto Yatima katika kituo hicho leo, Msaada uliotolewa una thamani ya shilingi milioni tano
Meneja Masoko wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Bi. Christina Tungaraza akishiriki kuimba wimbo na watoto wa kituo hicho pamoja na wafanyakazi wenzake.
Wafanyakazi wa ATCL wakicheza pamoja na watoto wa kituo hicho.

mvua kubwa yakwamisha safari barabara ya Dodoma-Morogoro

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Dodoma.
 Mvua Kubwa zinazoendelea kunyesha nchini zimesababisha adha Kubwa kwa watumiaji wa barabara  ya Dodoma -Morogoro kutokana na eneo kubwa la  barabarani kufunikwa na maji kuanzia Mtanana mpaka Kibaigwa. 
Maji hayo ambayo yamesababisha adha ya mabasi ya abiria na binafsi kushindwa kupita  kutokana na kufanya wasafiri kuendelea  kukaa hapo kwa zaidi ya Saa  nne kusubiri maji yapungue.
Wenyeji wa eneo hilo wamesema kuwa Maji hayo yamekuwa yakitoka milimani ambapo mvua zimenyesha kuanzia saa saba usiku











Kamishna wa Maadili awataka viongozi kutoa ushirikiano wakitakiwa kuwasilisha benk statement.

$
0
0
Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji (Mst) Harold Nsekela amewataka viongozi wa umma kutoa ushirikiano kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi pindi watakapotakiwa kuwasilisha pamoja na nyaraka nyingine “bank statement zao” kama sehemu ya tamko la raslimali na madeni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo  Alhamisi January 11, 2018 ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Kamishna Nsekela amesema Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na 13 ya mwaka 1995 inampa mamlaka ya kumuagiza kiongozi kuwasilisha nyaraka za mali anazomiliki zikiwemo hati za mashamba, viwanja, kadi za magali na benk statement kama sehemu ya tamko la raslimali na madeni ya kiongozi.
“Nikiwaandikia barua viongozi kuwataka kuwasilisha benk statement na nyaraka nyingine za mali wanazomiliki watoe ushirikiano kwasababu ni matakwa ya kisheria,” amesema.
Kamishn Nsekela ameeleza kuwa baada ya zoezi la kupokea tamko kukamilika tarehe 31 Desemba, 2017, zoezi linaloendelea kwa sasa ni kuchambua matamko hayo ili kuona ni viongozi wapi wataanza kuhakikiwa mali zao.
“Tukifikia wakati wa kuhakiki mali za viongozi baada ya uchambuzi wa matamko yao, watatakiwa kutoa ushirikiano. Tutataka wathibitishe mali hizo walizipataje?,” amesema na kuongeza kuwa viongozi hawatakiwi kuwa na hofu pindi wanapotakiwa kuhakikiwa mali zao kwasababu sheria ya maadili haiwazuii kumiliki mali, isipokuwa wathibitishe walivyozipata.
Kwa mujibu wa Kamhsina Nsekela, Sekretarieti ya Maadili haipokei tamko kuwatunzia viongozi bila kulifanyia kazi ndio maana lazima zoezi la uhakiki lifanyike.
“Hatupokei matamko ya viongozi kuwatunzia, lazima tuthibitishe waliyoandika ndani vinginevyo hatuna sababu ya kuwepo,” amesema.
“Viongozi wa Umma lazima waelewe kuwa tukienda kuhakiki mali zao, lengo ni kutaka kuthibitisha mali walizonazo nan ni jukumu letu kufanya hivyo sio kuwatuhumu.”
 Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji (Mst.) Harold Nsekela akiongea na waandishi wa habari kuhusu mali zinazotakiwa kutangazwa na viongozi wa Umma katika tamko lao. Ufafanuzi huo umetolewa leo tarehe 11/1/2018 katika ofisi za Sekretarieti ya Maadili jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji (Mst.) Harold Nsekela akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari waliofika ofisini kwake tarehe 11 Januari, 2018 kutaka ufafanuzi kuhusu matakwa ya kisheria ya kuwataka viongozi wa umma kuwasilisha bank statement zao katika tamko la Raslimali na Madeni. Picha zote na Joseph Ishengoma.

PUBLIC NOTICE

$
0
0


The Geological Survey of Tanzania (GST) wishes to remind all Mineral Right Holders to submit exploration, research and mining data/information to GST. This is according to Section 27F (3) and (4) of the Mining Act No. 14 of 2010 as amended by “The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act No. 7, 2017ʺ. The section requires as follows:-

27F.-(3) The mineral right holder shall submit to the Geological Survey of Tanzania    the following accurate mineral data:
  1. geological maps and plans;
  2. geophysical and geochemical raw data;
  3. processed and interpreted data or maps;
  4. technical reports;
  5. core samples and its mineral exploration database; and
  6. any other information as may be required.
(4)The mineral right holder shall give copies of data generated under subsections (2) and (3) to the Geological Survey of Tanzania free of charge.

In this regard, all Mineral Right Holders are required to submit the data and information to the Geological Survey of Tanzania on quarterly basis from October 2017.  

Issued on 10th January 2018 by:

Chief Executive Officer,
Geological Survey of Tanzania,
Kikuyu Avenue, Building Nu.8
P.O. Box 903, DODOMA,
TANZANIA.

Tel: +255 26 2323020/0754497533
Fax: +255 26 2323020
Website: http:www.gst.go.tz

Portal: www.gmis-tanzania.com

Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa Muhimbili

$
0
0
Na John Stephen wa Muhimbili
Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa Muhimbili leo limefanya kikao chake cha 18 na kujadili agenda mbalimbali katika kikao hicho ikiwamo maslahi kwa wafanyakazi.
Katika kikao hicho ambacho kimefanyika  Jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti wake Profesa Lawrence Museru, baraza limepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/17.
Kabla ya kuwasilishwa kwa taarifa hiyo, Katibu wa TUGHE mkoa  Bw. Gaudensi Kadyango amezungumzia umuhimu wa majadiliano mahala pa kazi kuhusu mwajiri na chama cha wafanyakazi ili kuondoa malalamiko na kufanya kazi kwa tija.
Amesema majadiliano ni sehemu ya kazi  hivyo pande zote mbili zinatakiwa kuwa na busara kwa kila mmoja kusikiliza hoja ya mwenzie.
Mada nyingine iliyowasilishwa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira , Vijana na wenye ulemavu ni umuhimu wa utamaduni katika kuinua viwango vya utendaji wa kazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akielezea mada hiyo Bi.Tulia Msemwa amesema utamaduni wa taasisi unatakiwa uangaliwe kwa makini hasa katika Dunia hii ya utandawazi ili kuruhusu tamaduni nyingine mpya kama zile zinazohusika na ufumbuzi, udadisi na ubora wa kazi na kuwajali wateja.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akifafanua jambo kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Muhimbili. Kushoto ni Katibu wa Baraza hilo, Eneza Msuya na kulia ni wawakilishi kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Zaria Mmanga na Pascal Magesa.

 Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakifuatilia mkutano huo ambao umejadili mada mbalimbali yakiwamo maslahi ya wafanyakazi na utekelezaji wa shughuli za hospitali.
 Mkurugenzi  wa Rasilimali Watu katika hospitali hiyo, Makwaia Makani akieleza jambo kwenye mkutano huo. Kushoto ni Katibu wa Baraza hilo, Eneza Msuya na wengine ni wajumbe mkutano huo.
 Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo, Dkt. Frank Masao akiuliza swali.

Wajumbe wakifuatilia mkutano huo Leo

DC HAPPI- WALIOVAMIA HIFADHI YA BARABARA WAONDOKE KWA HIYARI YAO

Uzalendo wa Kweli ni Kupenda vya Kwetu

BARABARA ZA HATARI KULIKO ZOTE DUNIANI


HOTELI 10 ZA MAAJABU DUNIANI, ZIKIONGOZWA NA YA TANZANIA

RAIS MAGUFULI AMEAMUA KUSAFISHA NYUMBA HAKUNA MENDE ATAKAYEBAKI: KHERI JAMES

$
0
0
Na Mathias Canal, Arusha 

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa umesifu utendaji wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kutokana na uwajibikaji wake katika kuimarisha chama pamoja na serikali kwa maslahi ya watanzania.


Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor akiwa ziarani Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.


Kheri alisema kuwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa CCM Taifa ameamua kusafisha nyumba ambayo ni nchi ya Tanzania hivyo hakutegemewi mtu yeyote kusalia kama mende wa kumkwamisha katika umaridadi wa usafi huo wa maslahi ya Taifa.


Mjumbe huyo wa kamati kuu ya CCM Taifa aliwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi tarehe 13 Januari 2018 kupiga kura kwa wingi zitakazompa ushindi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt Steven Kiruswa ili kutekeleza ilani ya ushindi wa chama hicho ya Mwaka 2015-2020 ambayo ni mkataba muhimu kati ya wananchi na CCM.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido. Picha Zote Na Mathias Canal
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akionyesha fimbo ya kimasai baada ya kupewa cheo cha kiongozi wa kimila Olaigwanani rika ya Korianga akizungumza na wakazi wa akiwa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akisalimiana na wananchi wakati akiwasili Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akiwasili Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.


KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

KWANDIKWA AWATAKA ‘TAA NA TPDC’ KUHAMISHA BOMBA LA GESI UWANJA WA NDEGE MTWARA

$
0
0
Naibu Waziri wa ujenzi, Elias Kwandikwa, ameiagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), kulihamisha bomba la gesi lililopitishwa katika maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara kabla ya bomba hilo halijaleta madhara kwa watumiaji wa Uwanja huo.

Akizungumza mkoani Mtwara, mara baada ya kukagua uwanja huo, ikiwa ni siku kadhaa baada ya kutokea kwa tukio la ajali ya bomba la gesi katika maeneo ya Buguruni kwa Mnyamani mkoani Dar es salaam na kusababisha madhara kwa wananchi, Naibu Waziri huyo amesema kuwa uwepo wa bomba hilo katika uwanja huo si salama na huenda ikapelekea watoaji huduma za usafiri wa anga kusitisha au kutokuleta kabisa huduma zao kutokana na hofu, hali itakayopelekea Serikali kukosa mapato.

“TAA, TPDC na wataalam wa Wizara hakikisheni mnafanya kikao kuona namna ya kulihamisha bomba hili kwani jambo hili si salama na pia baadhi ya mashirika ya ndege ya kimataifa yakibaini kama kuna uwepo wa bomba la gesi katika uwanja huu wanaweza kusitisha huduma zao”, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Ametoa rai kwa watendaji wa Taasisi mbalimbali za Serikali kutochukua maamuzi ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali kabla ya kushirikisha uongozi wa wilaya au mkoa kwa pamoja ili kupata ushauri wa maeneo ambayo yanafaa kwa ujenzi wa miundombinu hiyo.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoka kukagua kivuko cha MV. Kilambo kinachotoa huduma kati ya kijiji cha Kilambo, mkoani Mtwara na Namoto, Msumbiji.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akikagua moja ya maboya kwa ajili ya usalama kwa watumiaji wa kivuko cha MV. Kilambo, kinachotoa huduma kati ya kijiji cha Kilambo na Namoto – Msumbiji. wakati alipofanya ziara yake mkoani Mtwara.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akishiriki katika zoezi la uchanganyaji wa zege katika ujenzi wa barabara ya Tangazo-Kilambo yenye urefu wa KM 9.3, Mkoani Mtwara.

INTRODUCING "TUNASAFISHA" BY EDDU BOY FT BELLE9, AMBER LULU

DKT. NDUGULILE AING’ARISHA PROGRAMU YA KIKUNDI MLEZI KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI MKOANI KATAVI

$
0
0
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) ameing’arisha programu ya ‘Kikundi Mlezi’ katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi yenye lengo la kuwawezesha wanawake wajasirimali kuwezeshana wenyewe katika kuanzisha na kuendeleza miradi ya biashara zao.

Dkt. Ndugulile ameitambulisha programu hiyo wakati alipofanya ziara ya siku mbili katika manispaa ya Mpanda mkoani Katavi katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi kuibua miradi na kuanzisha shughiuli za uzalishaji kawa kuzingatia fursa, mazingira na soko.

Dkt.Ndugulile amesema kuwa ili kufanikisha kufikiwa kwa Tanzania ya viwanda Serikali itaendelea kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo hasa wanawake katika kuwawezesha kuanzisha vikundi vitakayoanzisha viwanda vidogo vidogo na vya kati.

Ameongeza kuwa lengo la kuzindua Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ ni kuwashirikisha wanawake wajasirimali waliokomaa katika biashara kuwasaidia wanawake wajasiriamali wanaoanza shughuli hizo kwa kuwapatia uelewa wa soko, mbinu za biashara, upatikanaji wa mikopo na mahitaji ya kiufundi.

“Niseme programu hii itasaidia kwa asilimia kubwa kuibua wanawake ambao hawakuwa na uwezo katika kuanzisha biashara zao na kufanya wanawake kujiunga na vikundi na hatimaye kuanzisha viwanda vidogo na vya kati”alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia moja ya bidhaa ya mvinyo inayotengenezwa na Kikundi cha Wanawake wajasiriamali cha Humbaji kilichopo katika Manispaa ya Mpanda alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsaha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo ili kuchangia azma ya kufikia uchumi wa kati na wa viwanda.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akishona sweta kwa kutumia mashine maalum wakati alipotembelea Kikundi cha wanawake wajasiriamali kilichopo katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kuanzisha shughuli za maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia sweta lililotengenezwa na moja ya kikundi cha wanawake wajasiliamali wakati alipotembelea Kikundi cha wanawake wajasiriamali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda katika ziara yake ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akizungumza na vikundi vya wanawake wajasilimali wa Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.

Mazishi ya Marehemu Said Abdallah Natepe Zanzibar

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amekaa pamoja na Mama Siti Mwinyi mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili (kushoto) pamoja na Huda Karume mke wa Balozi Ali Karume kwenye msiba wa Bw. Said Abdallah Natepe aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Utawala Bora.
Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiwasili Mazizini kuhudhuria msiba wa Said Abdallah Natepe.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Idd akiwasili Mazizini kuhudhuria msiba wa Said Abdallah Natepe.
Mwili wa marehemu Said Natepe ukibebwa tayari kwenda kupumzisha kwenye makaburi ya Mwache

MAZISHI YA MAMA PERAS NGOMBALE MWIRU MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru (Mama Kinje), Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru ukiwasili kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam, alikopumzishwa kwenye nyumba yake ya milele. Mama Peras (Mama Kinje) amezikwa jioni ya leo kwenye makaburi Kinondoni, huku viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Vyama vya siasa wakishiriki mazishi hayo.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na familia ya Marehemu, wakishuhudia Jeneza lenye mwili wa Mama Peras Ngombale Mwiru likishushwa kaburini, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jioni ya leo kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Mtoto wa Marehemu Mama Peras, Kinje Ngombale Mwiru aliyeambatana na mkewe.
 Mume wa Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akiweka udongo kwenye kaburi ya Mke wake mpendwa, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jioni ya leo kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
 Mtoto wa Marehemu Mama Peras, Kinje Ngombale Mwiru na Mkewe Anitha wakiweka udongo kwenye kaburi la Mama yao. 
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akiweka udongo kaburini.
Askofu akiweka msalaba kaburini.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina wakiweka shada ya maua kwenye kaburi la Mama Peras Ngombale Mwiru (Mama Kinje), Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru
 Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba na Mkewe wakiweka shada ya maua kwenye kaburi la Mama Peras Ngombale Mwiru (Mama Kinje), Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru
Mama Anna Mkapa akiweka shada ya maua kwenye kaburi la Mama Peras Ngombale Mwiru (Mama Kinje), Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru.

Article 8

HALMASHAURI YA MJI WA BABATI YAJIZATITI KUKAMILISHA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
Halmashauri ya Mji wa Babati inaendelea na zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea; ambapo wananchi wamehamasika na kujitokeza kwa wingi kusajiliwa.

Akizungumzia zoezi hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Babati Ndg. Fortunatus Fwema amesema kiujumla zoezi la Usajili katika Halmashauri yake linaendelea vema isipokuwa changamoto za hapa na pale.

Amezitaja baadhi ya changamoto ni ushiriki hafifu wa wananchi kutokana na msimu wa kilimo asilimia kubwa ya wananchi kuwepo mashambani, mvua na uelewa mdogo wa wananchi katika masuala yanayohusu umuhimu wa Vitambulisho.

Amewataka Wananchi kugawa muda wa kilimo na wa kujiandikisha ili waweze kutumia fursa hii kujisajili na kuagiza watendaji wote walio chini yake kuhakikisha wanatoa ushirikiano katika kufanikisha zoezi hili.
Wananchi wa Kata ya Babati mkoani Manyara wakiwa wamepanga foleni ya kuingia katika chumba cha Usajili wa Vitambulisho vya Taifa.
Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Babati Ndg. Fortunatus Fwema akielezea umuhimu wa Kitambulisho cha Taifa kwa wananchi ikiwa ni kutambulika na kupata huduma za kijamii kirahisi pamoja na kuwezesha Halmashauri yake kuwa na takwimu sahihi zitakazowasaidia kupanga maendeleo kwa wanannchi wao kwa urahisi alipohojiwa na waandishi wa Radio Manyara. 
Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Babati Ndg. Fortunatus Fwema akifanya mazungumzo juu ya maendeleo ya zoezi wakati Afisa Msajili Mkoa wa Manyara kutoka NIDA alipofika ofisini kwake kwa mazungumzo hayo.

DKT. NDUGULILE AWAONGOZA MADEREVA BODA BODA KULA KIAPO CHA KUWALINDA WATOTO DHIDI YA MIMBA ZA UTOTONI MKOA WA KATAVI

MWENYEKITI WA CUF TAIFA PROF.LIPUMBA AHIMIZA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA ELIMU

$
0
0
Na Jumbe Ismailly SINGIDA Jan,11,2018 Kuwekeza 


CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimesema kuwa pamoja na serikali ya awamu ya tano kufuta ada katika shule za msingi hadi kidato cha nne,lakini sekta ya elimu bado haijawekeza ipasavyo kwenye sekta hiyo kutokana na changamoto mbali mbali zinazoendelea kuikabili sekta hiyo mpaka sasa.

Mwenyekiti wa CUF Taifa,Prof.Ibrahimu Lipumba aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Singida wakati wa kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho,Delphina Mngazija uliofanyika katika Kijiji cha Ughandi,wilaya ya Singida vijijini.

Alifafanua kiongozi huyo wa kitaifa kwamba serikali inapowekeza kwenye sekta ya elimu kwa sasa ni lazima pia iwekeze kwenye matumizi ya kompyuta kwenye shule zilizopo na kuongeza kuwa elimu ya siku hizi inakwenda sambamba na mitandao ya kompyuta.

Kwa mujibu wa Prof.Lipumba nchi nyingi pamoja na nchi maskini zimewekeza mara tu watoto wanapoanza hujifunza pia kutumia kompyuta na kwamba matumizi ya kompyuta ni sawa kama vile kujifunza lugha.
“Mtoto mdogo ni mwepesi kujifunza lugha kuliko mtu mzima,hata mtu mzima ukiwa na simu mwanao anaweza kujua kuitumia ile simu kuliko wewe mtu mzima.

Na kuongeza pia kuwa wataalamu wa mambo ya watoto wanasema kuwa mtoto anapokuwa ndani ya tumbo la mama yake na kwa miaka miwili ya kwanza ndizo zinazompa mtoto fursa ya kujenga maungo yake,ya kujenga ubongo wake,ya kujenga kinga ya mwili.”alisisitiza Prof.Lipumba.
Prof.Lipumba hata hivyo alitumia fursa hiyo kuishauri serikali kuangalia uwezekano wa vituo vya afya vilivyopo kuwa na virutubisho muhimu na kwamba kutokana na taarifa za serikali kuna tatizo kubwa la akina mama wajawazito kutokuwa na damu ya kutosha.

“Kwa mujibu wa taarifa za serikali kuna tatizo kubwa la akina mama wajawazito kutokuwa na damu ya kutosha,hawana madini ya chuma ndani ya damu yao hii inasababisha watoto wasipate lishe bora na watoto wa Tanzania wamedumaa.”alibainisha Mwenyekiti huyo.

Naye Katibu wa CUF Mkoa wa Singida,Selemani Ntandu aliwatahadharisha wanachama wa CUF pamoja na wale wa CCM waishio katika Kijiji na kata ya Ughandi kwa ujumla kwamba endapo watamchagua mgombea wa CCM,Justine Monko wakae wakijua kwamba makao makuu ya wilaya hiyo yatahamishwa kwenda Kijiji cha Sagarumba badala ya Ilongero.

Aidha katibu huyo alisisitiza kwamba wananchi wa jimbo la Singida kaskazini wanahitaji huduma bora za kijamii zinaboreshwa na kuonyesha masikitiko yake kwamba hivi sasa miundombinu ya barabara kwenye maeneo mengi hairidhishi kabisa jambo ambalo halishughulikiwi na watu waliokabidhiwa dhamana ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho.
Mwenyekiti wa CUF Taifa,Prof.Ibrahimu Lipumba akiwasilimia wananchi pamoja na wanachama wa chama hicho katika Kijiji cha Ughandi,wilaya ya Singida vijijini alikwenda kumnadi mgombea ubunge wa chama hicha,Delphine Mngazija.
Mwenyekiti wa Taifa wa CUF,Prof.Ibrahimu Lipumba akiwasisitiza wananchi wa vyama vyote vya siasa kumpigia kura mgombea wa chama hicho,Delphina Mngazija kwa kuwaonyesha mfano wa karatasi la kupigia kura
Mwenyekitti wa CUF Taifa,Prof.Ibrahimu Lipumba akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Singida kaskazini,Delphina Mngazija kwenye mkutano wa kampeni uliofanyia katika Kijiji cha Ughandi,Singida vijijini.
Mgombea ubunge wa CUF,Delphina Mngazija alipokuwa akiomba kura kwa wananchi wa kijiji na kata ya Ughandi kwa ujumla na kuwaahidi kwamba endapo wataampaa ridhaa ya kuwa mwakilishi wao atakwenda kupigania hadi kuondoa kero zinazowakabili wanawake wajawazito za kununua beseni,ndoo na mipira ya kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma vuilivyopo kwenye maeneo yao.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ughandi wakimsikiliza mwenyekiti wa taifa wa CUF,Prof.Ibrahimu Lipumba alipokuwa nakiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Ughandi kumuombea kura mgombea wa ubunge wa chama hicho ili aweze kuchagulia ifikapo jan,13,2018.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images