Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live

ELIMU BURE YAWABANA WAZAZI WALIOKUWA WAKIOZESHA WATOTO KATIKA UMRI MDOGO WILAYANI BAHI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii - Dodoma

Serikali Wilaya ya Bahi  imeahidi kuendelea kushirikiana na Taasisi ya Msichana Initiative katika Mapambano yake ya kupinga ndoa za utotoni na  ukatili wa kijinsia kwa watoto wa Wilaya hiyo  ili waweze kufikia malengo kama ilivyo katika sehemu zingine hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Afisa  Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma , Daudi Kisagure alipotembelea mradi wa Msichana Cafe unaoendeshwa na taasisi ya Msichana Initiative katika kata kumi za wilaya hiyo.

"lazima niwaeleze ukweli tangu mradi huu wa Msichana Cafe uanzishwe na Msichana Initiative umesaidia kwa kiasi kikubwa sana kwani tangu mwaka jana mara baada ya watu kupata elimu na kuelewa kesi za watoto kuolewa katika umri mdogo zimepungua sana kwani kwa tathmini ya awali kutoka kwa walimu wakuu wanasema elimu iliyotolewa imepunguza kwa kiasi kikubwa kwa watoto wa kike kupata mimba wakiwa shuleni "amesema Kisagure.

Ametaja kuwa, uwepo wa taasisi hiyo umeweza kusaidia sana kutoa uelewa kwa wazazi juu ya elimu kwa mtoto na kuwaelimisha juu ya haki za mtoto kuliko ilivyokuwa hapo awali ambapo watoto wengi walikuwa wakiripotiwa kuolewa na kushindwa kuendelea na masomo.

Ametaja kuwa taasisi hii imeweza kufanikiwa zaidi kwani kutokana na mpango wa elimu bure ulioanzishwa na Rais Dk. John Magufuli umeweza kuondoa visingizio ambavyo hapo awali vilikuwa kikwazo kwa watoto wa kike kwenda shule na badala yake kuozeshwa ili wazazi wapate mali.

Kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa Msichana Cafe, Paulina Mbabala amesema kuwa mradi huo wa kupinga mimba za utotoni umewasaidia sana mara baada ya kufanyiwa semina na kuchaguliwa kama wawakilishi wa kutoa elimu hivyo wameweza kuifikia jamii kubwa na kwasasa wameanza kupata kuelewa umuhimu wa mtoto wa kike kuendelea na masomo.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Daudi Kisangire akizungumza jambo na wajumbe wa Msichana Cafe mara alipowatembelea katika eneo lao la kukutania kwa ajili ya kujadili changamoto zinazowakabili katika mapambano ya ukatili wa kijinsia na ndoa za utotoni katika kata ya Kigwe.
Katibu wa mradi wa Msichana Cafe katika kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma, Miraji Adam akisoma taarifa kwa afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo namna walivyofanikiwa kuwafikia wanafunzi na taasisi mbalimbali kutoa elimu juu ya kupinga Mimba za utotoni.
Baadhi ya Wajumbe wa Mradi wa Msichana Cafe kutoka kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi wakisikiliza kwa makini nasaha kutoka kwa afisa maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo.

MPINA ATAKA KUHAKIKI USHURU WA MIAKA MITANO KATIKA MASOMO YA SAMAKI YA KIMATAIFA.

$
0
0
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameamuru kufanyika ukaguzi mpya wa hesabu za fedha kwenye masoko yote ya kimataifa ya samaki na mazao yake yaliyoko katika Ziwa Victoria ili kuhakiki uhalali wa mapato ya Serikali yaliyokusanywa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Masoko hayo yatakayohusika na ukaguzi huo ni pamoja na Kirumba Mwanza, Nyakalilo Buchosa Mwanza ,Kasenda Chato Geita, Magalini Muleba Kagera, Kemondo Bukoba Kagera na Mwigobero Musoma Mara ambapo wafanyabiashara watakaobainika walihusika kufanya udanganyifu wa mapato watatakiwa kurejesha fedha hizo walizoiibia Serikali kwa kipindi hicho ambapo Watumishi wa Umma nao waliohusika kuhujumu mapato hayo watasakwa popote walipo na kufikishwa kwenye vyombo vya dola kukabiliana na mashtaka ya kuhujumu wa rasimali za nchi .

Hatua hiyo ya Waziri Mpina imekuja kufuatia kubaini kuwepo udanganyifu mkubwa katika biashara ya samaki, dagaa,mabondo, na mapanki akibainisha kuwepo tabia ya kupunguza uzito na idadi ya magunia,kubadilisha matumizi ya vibali,kuchanganya mizigo ya ndani na nje ya nchi kwenye malori, kuanzishwa kwa masoko ya kimataifa yasiyo rasmi na wafanyabiashara wakubwa wa mazao ya uvuvi kutolipa kodi za mapato kutoka TRA.

Pia Waziri Mpina ameamuru kufutwa kwa masoko yote yasiyo rasmi yaliyopewa hadhi ya kimataifa ikiwemo soko la Nyakalilo na Magalini ambapo amemuagiza Katibu Mkuu Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Yohana Budeba kuwaondoa na kuwapangia vituo vingine vya kazi watumishi waliokuwepo kwenye masoko hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Chato Shabani Ntarambe (aliyesimama) akimweleza jambo Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye kofia) wakati wa mkutano wa hadhara kwenye soko la kimataifa la samaki la Kasenda wilayani Chato leo, ambapo Waziri ameamuru kufanyika ukaguzi mpya wa hesabu za fedha kwenye masoko yote ya kimataifa ya samaki na mazao yake yaliyoko katika Ziwa Victoria ili kuhakiki uhalali wa mapato ya Serikali yaliyokusanywa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.Kulia ni Diwani wa kata ya Kasenda Muganza Mwita. 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye kofia katikati) akiwa kwenye moja ya boti inayotumika kwa Uvuvi wa samaki kwenye soko la kimataifa la samaki la Kasenda wilayani Chato leo, Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chato Bathromeo Christiani, Kushoto ni Diwani wa kata ya Kasenda Muganza Mwita. (Picha na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye kofia) akiwahutubia wananchi kwenye soko la kimataifa la samaki la Kasenda wilayani Chato leo,  ameamuru kufanyika ukaguzi mpya wa hesabu za fedha kwenye masoko yote ya kimataifa ya samaki na mazao yake yaliyoko katika Ziwa Victoria ili kuhakiki uhalali wa mapato ya Serikali yaliyokusanywa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. (Picha na John Mapepele) 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye kofia) akikagua ofisi za soko la kimataifa la samaki la Kasenda wilayani Chato leo, Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi bi Mwanaidi Mlolwa. Nyumba niYohana Mikumbe Mtekinolojia wa samaki katika soko la Kasenda. . (Picha na John Mapepele)
Umati wa wananchi waliohudhuria mkutano wa Waziri Luhaga Mpina kwenye soko la kimataifa la samaki la Kasenda wilayani Chato leo, ameamuru kufanyika ukaguzi mpya wa hesabu za fedha kwenye masoko yote ya kimataifa ya samaki na mazao yake yaliyoko katika Ziwa Victoria ili kuhakiki uhalali wa mapato ya Serikali yaliyokusanywa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. (Picha na John Mapepele) 

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JANUARI 11, 2018

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI ATEUA MABALOZI WAWILI

WAFANYABIASHARA WA WANYAMAPORI HAI NJE YA NCHI WAIOMBA SERIKALI IWASAIDIE

$
0
0
Chama cha wasafirishaji wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara (TWEA) kimeiomba serikali isitishe zuio la kusafirisha nje wanyamapori hao ili wanachama wake waweze kujikwamua na hali ngumu ya maisha inayaowakabili.

Wakizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kwenye kikao cha Wizara na wawakilishi wa Wafanyabiashara hao waliiomba serikali isikilize kilio chao.

Kwa upande wake , Mwenyekiti wa Chama hicho, Enock Balilemwa alisema baadhi ya wanachama wakiwemo walemavu waliokuwa wamechukua mikopo benki wamefukuzwa kwenye nyumba zao baada ya kushindwa kufanya marejesho ya mikopo hiyo kufuatia zuio la biashara hiyo.

Alieleza kuwa baadhi ya wanachama wake wamejikuta kwenye hali ngumu ya kupoteza mali zao na kuingia kwenye mifarakano na wateja wao kwa vile wafanyabiashara hao walichukua pesa toka kwa wateja kama malipo ya awali hivyo wakati wa zoezi la kusimamisha biashara linafanyika liliwakuta wafanyabiashara hao wameshachukua pesa za wateja wao kama malipo ya awali.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akifungua kikao cha Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Nebbo Mwina
Mwenyekiti wa Chama cha wasafirishaji wanyamapori hai nje ya nchi, Enock Balilemwa akizungumza kwenye kikao cha cha Wizara ya Maliasili na Utalii na Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Nebbo Mwina akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kufungua kikao cha Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wasafirishaji wanyamapori hai nje ya nchi, Fatuma Hamisi akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (hayupo pichani) kwenye kikao cha cha Wizara ya Maliasili na Utalii na Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai kilichofanyika jana mjini Dodoma ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara.

TATU MZUKA YAKABIDHI MABATI YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI TANO UJENZI WA KITUO CHA POLISI MBANDE

$
0
0
Mchezo wa kubahatisha wa Tatu Mzuka  kupitia mshindi wa wiki iliyo pita kutoka Temeke Erinisha Kilango aliyeshinda milioni 50,wamezawadia Wilaya ya Temeke mabati ya thamani ya milioni 5 kusaidia kujenga kituo cha polisi cha Mbande.

 Tatu Mzuka inasemaga kuwa "ukishinda na Tanzania inashinda. Kwenye wilaya ambayo mshindi anatoka, Tatu Mzuka wanazawadia wilaya milioni 5  kusaidia maendeleo ya wilaya hiyo. 

Ukicheza Tatu Mzuka , unaweza kushinda hadi milioni 6 kila lisaa, milioni 10 kila siks na jumapili hii kuna jackpot ya milioni 70 ya kuzawadia. 
  Afisa wa mawasiliano Bi. kemi Mutahaba akikabithi mabati ya thamani ya millioni 5 kwa Katibu Tawala wa Temeke Mh.  Hamisi Komba kusaidia kujenga kituo cha Polisi Mbande, wilaya ya Temeke.
 Mafundi wa ujenzi  wakiwa wana kabidhiwa mabati yenye thamani ya milioni 5 na Afisa ya Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bi Kemi Mutahaba.
Mhe Hamisi Komba, Katibu tawala wa wilaya ya Temeke akikabidhiwa fedha tasilimu milioni 5 na Bi . Kemi Mutahaba  wa Tatu Mzuka kwa ajili ya kununua  mabati yatakayo tumika kujenga kituo cha Polisi Mbande, Temeke.

SALAMU ZA RAMBI RAMBI

KAZI ZA MIKONO ZAWASAIDIA WAKIMBIZI WANAWAKE KUPUNGUZA MAKALI YA MAISHA KAMBINI

$
0
0

Baadhi ya wanakikundi Wanawake waishio katika kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli iliyopo Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma wakifinyanga vyungu mara baada ya kupata mafunzo kutoka shirika la IRC Ambalo linafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) Wanawake hao licha ya kufanikiwa kufinyanga vyungu hivyo, huviuza kwa shilingi 200 kwa kila kimoja, hali ambayo imekuwa haileti tija na faida katika kazi yao.
Mmoja wa wanakikundi wa ufinyanzi katika Kambi ya wakimbizi ya Mtendeli Wilayani Kibondo mkoani Kigoma,ambaye amepata mafunzo kutoka taasisi ya IRC kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR), ambayo yanamuwezesha kutumia muda wake katika shughuli za mikono za uzalishaji. 
 
Ili kuhakikisha uendelevu wa vikundi mbalimbali vya wajasirimali ndani ya Kambi za wakimbizi, kipato hafifu wanachopata baada ya kuuza bidhaa huingizwa katika mfuko wa kuweka na kukopa (VICOBA) wa kikundi ambao umeanzishwa kwa lengo la kuwawezesha wanakikundi kujiwekea akiba pamoja na kugawana faida inayopatikana kila mwisho wa mwezi. Kutokana na wateja kuwa ni watumishi/wadau mbalimbali wanaotembelea kambi hizi faida yao huwa ni finyu.
Mmoja wa Wakimbizi katika Kambi ya Mtendeli Wilayani Kibondo mkoani Kigoma Ambaye amepata mafunzo kutoka taasisi ya IRC kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR). Wanawake hawa wenye uwezo wa kufinyanga vyungu hutumia baadhi ya siku kuwafundisha wanawake wenzao waishio ndani ya kambi hii ya wakimbizi na kwa njia hii elimu inawafikia wanawake wengi. Shughuli za uzalishaji mali/ujasiriamali husaidia kuwajengea wanawake uwezo wa kujikimu kimaisha. Elimu hii itawasaidia hata watakaporejea nchini mwao.

Wanawake wa Kambi ya wakimbizi Mtendeli wakionesha baadhi ya nguo za Watoto ambazo wamezifuma kutokana na uzi kwa kutumia mkono mara baada ya kupata mafunzo kutoka IRC. “Kabla hatujapata haya mafunzo kutokana na mazingira tnayoishi kwa sasa shughuli pekee tuliyoweza kufanya ni kupika na kufanya usafi wa maeneo ya nyumba/mahema lakini sasa tunatumia muda katika kujifunza vitu vya maendeleo.”


NAIBU WAZIRI AAGIZA HALMASHAURI, MANISPAA KUZIPA BMUs KAZI YA KUSIMAMIA UTOZAJI USHURU.

$
0
0
Na Mwandishi wetu
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amezitaka Halmashauri na Manispaa zote nchini kuzipa kazi  ya kukusanya ushuru wa samaki na mazao yatokanayo na samaki BMUs ili ziweze kujiendesha na kusimamia ipasavyo Rasilimali za Uvuvi.

Ulega ameyasema hayo katika Mkutano wa kuzungumza na Jamii ya wavuvi  Kilwa - Kivinje. 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa ameahidi kuzipa kazi  hiyo ifikapo Mwezi Machi, 2018 baada  ya kukamilisha zoezi la  Upitishaji wa Kanuni ndogondogo kwa kila BMUs ambapo kwa wilaya ya Kilwa zipo sita (6).

Aidha, Mhe. Ulega amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa kuhakikisha kuwa Mtambo wa Kuzalisha barafu katika mwalo wa Kilwa - Masoko unafanya kazi  ndani ya siku 14.

Akijibu maswali na hoja za wananchi huku akishangiliwa, Mhe. Ulega, amewaahidi wananchi  katika Wilaya hiyo kurudi mwezi Machi kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa.

Katika kuhitimisha ziara yake  Mhe. Ulega ameshiriki zoezi la  Upigaji Chapa Mifugo katika kijiji cha Mpara, eneo la  magereza ambapo kwa siku ya leo  tu tarehe 10/01/2018 Jumla ya Ng'ombe 198 wamepigwa Chapa. Jumla ya ng'ombe  40,000 wanatarajiwa kupigwa Chapa katika wilaya ya Kilwa.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wavuvi katika soko kuu la samaki la mkoa wa Lindi.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na watendaji mbalimbali, wavuvi ambapo amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa kuhakikisha kuwa Mtambo  wa Kuzalisha barafu katika mwalo  wa Kilwa - Masoko unafanya kazi  ndani ya siku 14. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwaelekeza  namna bora ya kupiga chapa mifungo ya watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akishiriki zowezi la upigaji cha mifungo kijiji cha Mpara mkoa wa Lindi.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa,Zabron Bugingo(katikati) akishiriki zowezi la upiji chapa mifungo, kushoto ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akishuhudia zowezi hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kilwa,Zabron Bugingo (wakwanza kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega kuhusu mkakati wa Halmashauri wa  kuongeza uzalishaji wa Mikorosho katika kituo cha Mpara.

TUMIENI TAMASHA LA BIASHARA KUKUZA BIASHARA YA UTALII-MAJALIWA

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko ya Zanzibar kuhakikisha inatumia Tamashara la Biashara la Zanzibar kama chachu ya kukuza biashara ya Utalii kama ilivyo kwa Dubai Shooping Festival na matamasha mengine Duniani.

“Natambua kwamba kazi ya kulipandisha hadhi zaidi tamasha letu hili si ndogo , hata hivyo ninayo imani kubwa kwamba  si tu uwezo wa kufikia malengo hayo mnayo bali pia mnaweza.”

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumatano, Januari 10, 2018) wakati akifungua Tamasha la Nne la Biashara la Zanzibar lililofanyika kwenye viwanja vya Maisara katika mkoa wa Mjini Magharib, wilaya ya Mjini.

Tamasha hilo lilifunguliwa jana ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kuelekea katika sherehe za kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambayo yalitokea Januari 12, 1964.

Alisema Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko inatakiwa kutumia fursa ya uwepo wa tamasha hilo katika kuhakikisha inakuza biashara ya Utalii kwa kuwa linajumuisha wafanyabiashara kutoka mataifa mbalimbali.

Waziri Mkuu alisema Tamasha la Biashara ni nyenzo muhimu ya kukuza biashara na huduma pamoja na kukuza uchumi wa nchi, pia linatoa fursa ya kuwakutanisha wafanyabiashara au watoa huduma na wateja wao.

”Hali hii humuwezesha mzalishaji kupata mrejesho kuhusu namna bidhaa yake inavyokubalika kwenye soko, mapungufu yaliyopo kwenye bidha husika pamoja na kuelewa maboresho anayotakiwa kuyafanya katika bidhaa au huduma.”

Waziri Mkuu alisema kuwa tamasha hilo linaweza kutumika kama nyenzo muhimu katika kuanzisha mahusiano mazuri ya kibiashara kati ya mteja  na mfanyabiashara, hivyo kuwawezesha wajasiriamali kuwa na masoko ya uhakika.

Pia Waziri Mkuu alisema kufanyika kwa tamasha hilo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 katika ibara ya 84 (f).

“Ilani imeweka wazi azma ya Serikali ya kuanzisha na kuendeleza ujenzi wa kiwanja cha maonyesho ya biashara cha kimataifa na kuhakiisha ushiriki wa wajasiriamali wa Zanzibar  katika maonyesho ya biashara ya kimataifa ndani na nje ya nchi.”

Baada ya kufungua tamasha hilo Waziri Mkuu alitembelea mabanda mbalimbali katika viwanja yakiwemo ya taasisi za umma pamoja na wajasiriamali ambao wanatoka Zanzibar, Tanzania Bara, Kenya, Uturuki, Misri, Uganda na Burundi.

Awali, Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali alisema tamasha hilo lenye washiriki zaidi ya 200 limeandaliwa na wizara yake pamoja na TanTrade.

Balozi Amina aliseka kauli mbiu ya tamasha hilo kwa mwaka 2018 ni ‘wekeza kwenye viwanda kwa uchumi na ajira’ inalengo la kuhamasisha wadau kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya falsafa na dhima ya ujenzi wa viwanda.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
ALHAMISI, JANUARI 11, 2018.

Rais wa Simba ashindwa kutokea Mahakamani.

$
0
0
Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha wa USD 300,000 ameshindwa kufika katika Mahakamani kwa sababu ana matatizo ya figo.

Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa kuwa kesi hiyo leo imekuja kwa ajili ya kutajwa kwa kuwa upelelezi bado haujakamilika lakini amepewa taarifa kuwa Aveva anaumwa.

Mbali ya Aveva mshtakiwa mwingine ni katibu wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu'  Swai ameeleza kuwa amepewa taarifa kutoka Magereza kuwa Aveva hakufika mahakamani kwa sababu ana matatizo ya figo.

Aliongeza kudai kuwa bado hawajapatiwa nyaraka walizoziomba kutoka ofisi ya Aveva na pia aliiomba mahakama iwaruhusu wakamuhoji mshtakiwa Kaburu.

Baada ya hayo, Hakimu Nongwa alikubaliana na maombi ya kutaka kumuhoji mshtakiw kaburu na kuwataka wafuate utaratibu. kesi hiyo imeahirishwa hadi January 25,2018.

Aveva na makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha USD 300,000.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa walikula njama ya kughushi fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya Machi 15,2016 wakionesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa USD 300,000 kwa Evans Aveva wakati si kweli.

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AWATAKA TEMESA KUPELEKA KIVUKO LINDI

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, ameuagiza Uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) makao makuu kusaini haraka mkataba kwa mkandarasi atakayebeba kivuko kipya  kutoka eneo kinapotengenezwa wilayani Pangani mkoani Tanga hadi mkoani Lindi.

Akizungumza mara baada ya kukagua maegesho ya kivuko hicho ambacho kinatarajiwa kutoa huduma za usafiri kutoka Lindi Mjini - Kitunda mkoani humo, Naibu Waziri huyo amewahakikishia wananchi kutegemea kupata huduma nzuri za usafiri kwani ujenzi wa kivuko na  maegesho  yake  kwa sasa umefika katika hatua nzuri.

"Naagiza Mamlaka husika kusaini haraka mkataba kwa mkandarasi atakayebeba kivuko hiki kutoka Tanga hadi hapa ili wananchi waone kwamba kivuko kimefika na kipo tayari kwa ajili ya kutoa huduma", amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Aidha, Naibu Waziri huyo ameridhishwa na ujenzi wa maegesho hayo ambayo kwa sasa ujenzi wake umebakia asilimia 10 na hivyo kutarajiwa kukamilika muda wowote.
 Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mkoa wa Lindi, Mhandisi Grayson Maleko akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, kuhusu ujenzi wa maegesho ya kivuko kitakachotoa huduma kati ya Lindi Mjini na Kitunda, alipokuwa akikagua ujenzi wake mkoani humo.
 Muonekano wa ujenzi wa maegesho ya kivuko kitakachotoa huduma kati ya Lindi Mjini na Kitunda, ambapo mkataba wa kukikokota Kivuko hiko kutoka Pangani mkoani Tanga kuja Lindi upo katika hatua za mwisho.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, na Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Lindi, Mhe. Hamida Abdallah, wakikagua ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Lindi inayojegwa na SUMA JKT chini ya uangalizi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), katika ziara ya kikazi mkoani humo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Rc wangabo atoa mwezi mmoja kuzuia uvuvi haramu ziwa tanganyika

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kalambo pamoja na kamati yake ya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kukaa pamoja na kuandaa mkakati wa kuzui uvuvi haramu unaoendelea katika mwambao wa ziwa Tanganyika ili kuokoa viwanda vilivyopo katika mwambao huo.

Amesema kuwa uvuvi haramu unaoendelea katika mwambao huo unahatarisha maendeleo ya viwanda vya samaki vilivyopo na hatimae kudhoofisha ajira za wananchi waliopo karibu na viwanda hivyo na hatimae kurudisha nyuma juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuibua na kuimarisha viwanda vilivyopo.

“Mwisho wa mwezi huu nataka taarifa ya namna mlivyojipanga kupiga marufuku uvuvi haramu ikiwa ni pamoja na kutoa elimu na kuwakamata wale wanaokaidi na kuendesha uvuvi haramu, uvuvi haramu ukiendelea hiki kiwanda hakitakuwepo, kwasababu ya kuua samaki na watoto wake, achene uvuvi haramu, mnamaliza samaki katika ziwaletu hili,” RC Wangabo Alisisitiza

Ameongeza kuwa samaki ndio rasilimali pekee inayowaajiri pamoja na kuendesha kiwanda na kuwataka wananchi kuungana pamoja kuhakikisha wanatunza rasilimali hiyo, na kupiga marufuku aina zote za uvuvi haramu na kuonya kutosikia kiwanda kimefungwa kutokana na kukosa samaki amabao wamekwisha kwasababu ya uvuvi haramu.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo (wa tatu kutoka kulia) akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Mikebuka Fisheries Tanzania Ltd Azim Premji (wa pili kutoka kulia) katika kiwanda cha Mikebuka Fesheries Tanzania Ltd.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo akipiga marufuku uvuvi haramu katika ziwa Tanganyika ili kuokoa viwanda vilivyopo katika mwambao wa Ziwa hilo, (kushoto aliyekaa) Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura.  
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo (wa tatu kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Mhandisi Mshauri, Martin Hossey (wa pili kushoto) kuotoka Kampuni ya Nicholas O'Dwyer inayosimamia ujenzi wa Barabara ya Sumbawanga - Matai - Kasanga yenye urefu wa Km 112 ya thamani ya Bilioni 133 iliyomalizika kwa kiwango cha Km 71.5. 

Mwonekano wa Kiwanda cha Akwa Fisheries Tanzania Ltd kilichosimamisha uzalishaji. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

DKT. TULIA AKABIDHI TV SITA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE

$
0
0
 Naibu Spika wa Bunge Mhe.  Dkt.  Tulia Ackson akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Fedha Agnes Kuhenga Televisheni moja kati ya nne zilizotolewa na Taasisi ya Tulia (Tulia Trust Fund) kwa ajili ya watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Jumla ya TV sita zimetolewa na Tulia Trust ambazo zimefungwa  katika wodi na kliniki za watoto.
  Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Delila Kimambo akimweleza  Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt.  Tulia Ackson maendeleo ya afya za pacha walioungana Maria na Consolata waliolazwa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya Matibabu.
 Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt.  Tulia Ackson akiwajulia hali pacha walioungana Maria na Consolata waliolazwa  katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)kwa ajili ya Matibabu.
 Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwajulia hali watoto waliolazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu.  Mhe. Dkt. Tulia kupitia Taasisi ya Tulia (Tulia Trust Fund) ametoa TV sita kwa JKCI ambazo zimefungwa  katika wodi na kliniki za watoto. Picha na JKCI 

Jalada kesi ya Malinzi larudi Takukuru.

$
0
0
Jalada la kesi ya  utakatishaji wa fedha inayomkabili aliyekuwa rais wa (TFF), Jamal Malinzi na wenzake limerudishwa Takukuru  kwa maagizo ya kurekebisha vitu vichache ili kukamilisha iuchunguzi.

Mbali ya Malinzi, wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Msiande Mwanga. Wakili wa serikali kutoka Takukuru, Leornad Swai amedai hayo leo mbele ya Hakimu  Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, pindi shauri hilo lilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa.

Swai alidai jalada la kesi hiyo limesharudishwa Takukuru likitokea kwa mkurugenzi wa mashtaka  DPP na kudai wamepewa maelekezo ya kukamilisha baadhi ya uchunguzi.Hata hivyo, wakili wa Utetezi Nehemia Nkonko aliomba upelelezi dhidi ya kesi hiyo ukamilike kwa haraka kwa sababu washtakiwa wapo ndani.

Hakimu Mashauri amahirisha kesi hiyo hadi January 25, 2018 kwa ajili ya kutajwa.Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 28, yakiwemo ya kughushi na utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418.

WANAFUNZI WANAOJITOLEA KUFUNDISHA WAIOMBA SERIKALI KUWASAIDIA

$
0
0
   Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Dar es Salaam (DUCE), wanaotumia muda wao wa ziada kujitolea kufundisha katika shule za Msingi na Sekondari wameiomba Serikali kuwapa ushirikiano ili waweze kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi.

Ombi hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwanzilishi na Mratibu Mkuu wa zoezi hilo, Emijidius Cornel alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na kazi hiyo wanayoifanya hususani katika Wilaya ya Temeke.

Cornel amesema kuwa wameamua kuisaidia Serikali ya Awamu ya Tano katika kuendeleza sekta ya elimu nchini kwa kujitolea kufundisha masomo ya sayansi na hesabu katika shule mbalimbali ili waweze kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuyapenda, kuyasoma na kuyapa kipaumbele masomo hayo.

“Tumeamua kutumia muda wetu wa ziada kuwafundisha wadogo zetu nao waweze kufikia au kuzidi tulipokuwa sisi lakini tunakumbwa na changamoto nyingi hasa nauli za kutufikisha na kuturudisha vyuoni kutoka katika shule tunazojitolea kufundisha hivyo tunaiomba Serikali na wadau wengine kutusaidia katika hili,”alisema Cornel.

Cornel ameongeza kuwa kwa yeyote atakayekuwa tayari kuwawezesha fedha kwa ajili ya nauli atume katika akaunti ya NMB ya Shule ya Sekondari Kibasila ambayo ni moja ya shule wanayojitolea kufundisha kwa namba 20701100005.

Mmoja wa wanafunzi wanaojitolea kufundisha, Nambo Nicodemu ametoa rai kwa wanafunzi wenzie wa vyuo vyote nchini kujenga tabia ya kujitolea katika shughuli mbalimbali zitakazoiletea nchi maendeleo.

“Kama Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli anavyosisitiza wananchi kufanya kazi kwa uzalendo basi tunaomba vijana wenzetu kujitolea kwa wingi kushirikiana na Rais katika kuendeleza gurudumu la maendeleo.” alisema Nicodemu.

Jumla ya wanafunzi 400 kutoka DUCE wanaojitolea walianza kazi hiyo mwezi Februari mwaka 2017, wanafundisha katika shule 10 zilizopo jijini Dar es Salaam na wana mpango wa kuendelea kujitanua katika shule nyingi zaidi.
Mratibu wa Walimu wa Kujitolea Manispaa ya Temeke, Emijidius Cornel akizungumza na waandishi habari kuhusu huduma wanayofanya katika kujitolea ya kufundisha wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari leo jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI, LOWASSA WAMETOA FUNZO KWA VIJANA-RC GAMBO

$
0
0
Na Said Mwishehe, Blogu ya jamii.

MKUU wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa kitendo cha Rais, Dot. John Magufuli kufanya mazungumzo na waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa kumetoa funzo kwa vijana. 

Gambo ametoa kauli hiyo wakati anazungumza na Michuzi Blogu, jijini Dar es  Salaam ambapo amesema kitendo cha Lowassa kuomba kwenda kuonana na Rais Ikulu na kukubaliwa kuna funzo kubwa ndani yake na hasa vijana kutambua siasa si uadui. 

Amesema Rais, Dkt.Magufuli amethibitisha kuwa yupo kwa ajili ya watanzania wote bila kujali dini, kabila au itikadi za kidini na kubwa zaidi ameonesha mamba ambavyo ni msikivu kwa anaowaongoza. 

Amesema hata Lowassa wakati anazungumza akiwa Ikulu amesema amefarijika kukutana na Rais Magufuli na kufanya mazungumzo. 

"Kuna some kubwa la kujifunza hasa kwetu vijana kutambua siasa si uadui. Na unapokuwa kiongozi unastahili kumsikiliza kila mtu.Kwangu naona kuna kitu ambacho Kama kijana lazima tujifunze kutoka kwa Rais wetu,"amesema. 

Kuhusu wanaomshambulia Lowassa kwa uamuzi wake wa kwenda Ikulu amesema hao ni wachanga wa siasa.

"Nimemsikiliza Mwenyekiti wa  Chadema Freeman Mbowe pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema lakini nachokiona kutoka kwako wanasumbuliwa na uchanga wa siasa tu,amesema Gambo. 

DIAMOND AFANYA KWELI....

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI JOHN KIJAZI APOKEA KWA NIABA YA RAIS KANUNI ZA SHERIA YA MADINI NAMBA 7 YA MWAKA 2017

$
0
0
  Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akimpa muhtasari Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi kabla ya kumkabidhi vitabu vya Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 ambaye anapokea kwa niaba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyeagiza kuandaliwa kwa kanuni hizo ndani haraka ili sheria iweze kufanya kazi. Hafla hiyo ndogo, iliyohudhuriwa pia na Manaibu Waziri wa Madini  Mhe. Doto Biteko na  pamoja na Katibu Mkuu  wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018
 Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akimsikiliza  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi baada ya  ya kumkabidhi vitabu vya  Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 ambaye anapokea kwa niaba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyeagiza kuandaliwa kwa kanuni hizo ndani haraka ili sheria iweze kufanya kazi. Hafla hiyo ndogo, iliyohudhuriwa pia na Manaibu Waziri wa Madini  Mhe. stanslaus Nyongo na Mhe. Doto Biteko na  pamoja na Katibu Mkuu  wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018

 Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akimkabidhi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi  vitabu vya Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 ambaye anapokea kwa niaba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyeagiza kuandaliwa kwa kanuni hizo ndani haraka ili sheria iweze kufanya kazi. Hafla hiyo ndogo, iliyohudhuriwa pia na Manaibu Waziri wa Madini  Mhe. Doto Biteko na  pamoja na Katibu Mkuu  wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi  akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kitabu cha Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 baada ya  Balozi Kijazi kuvipokea kwa niaba ya Rais Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018. Wengine ni Manaibu Waziri wa Madini  Mhe. Stanslaus Nyongo na Mhe. Doto Biteko, pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James na Katibu Mkuu  wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila.
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi  na Manaibu Waziri wa Madini  Mhe. Stanslaus Nyongo na Mhe. Doto Biteko, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James pamoja na Katibu Mkuu  wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, wakiwa na vitabu vya  Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 baada ya  Balozi Kijazi kuvipokea kwa niaba ya Rais Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018. Picha na Ikulu

KIGWANGALA ATAKA KAULI MBIU YA KUTANGAZA UTALII

$
0
0
Na Said Mwishehe
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangala amesema ipo haja ya kuwa na kauli mbiu ambayo itatumika kuutangaza utalii wa Tanzania katika mataifa mbalimbali duniani.

Amesema Tanzania imejaaliwa kuwa na maeneo mengi ya utalii lakini hayajafahamika kutokana na nguvu ndogo ya kuyatangaza kwake, hivyo kusababisha watalii wengi kufanya utalii katika maeneo machache ya utalii ukiwamo Mlima Kilimanjaro.

Dk.Kigwangala ametoa kauli hiyo jijini  Dar es Salaam leo wakati anazindua Kamati ya Utambulisho wa Utalii Tanzania na kufafanua kuna vivutio vingi na sasa ipo haja kuendelea kuvitangaza kwa nguvu zote.

Amesema wajumbe wa kamati watakuwa na jukumu la kuweka mikakati sahihi ya kuhakikisha utalii wa Tanzania unaendelea kutangazwa kwa lengo la kuongeza watalii wa ndani na nje ya nchi.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Khamis Kigwangalla akisisistiza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya Utambulisho wa Utalii wa Tanzania leo hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es Salaam leo. Kamati hiyo yenye wajumbe 22 imeundwa na Mhe. Waziri kwa lengo la kupitia na kubuni mkakati mbadala wa namna ya kutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Utambulisho wa Utalii wa Tanzania Bibi. Devotha Mdachi akielezea jambo mbele ya wajumbe wa kamati hiyo (hawapo pichani) mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Kamati hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo Richard Rugimbana. Kamati hiyo yenye wajumbe 21imeundwa na Mhe. Waziri kwa lengo la kupitia na kubuni mkakati mbadala wa namna ya kutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Utambulisho wa Utalii wa Tanzania wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Khamis Kigwangalla wakati wa hafla ya uzinduzi wa kamati hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo yenye wajumbe 21 imeundwa na Mhe. Waziri kwa lengo la kupitia na kubuni mkakati mbadala wa namna ya kutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Khamis Kigwangalla (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Utambulisho wa Utalii wa Tanzania lmara baada ya uzinduzi wa kamati hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo yenye wajumbe 21 imeundwa na Mhe. Waziri kwa lengo la kupitia na kubuni mkakati mbadala wa namna ya kutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.
Picha na Frank Shija – MAELEZO

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live




Latest Images