Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

WAZIRI JAFO-WATAALAMU WA MAJI ZAIDI YA ELFU NNE WANAHITAJIKA TAMISEMI

$
0
0

Nteghenjwa Hosseah, Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amesema mahitaji ya wataalam wa Maji kwa sasa katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Nchini ni kati ya elf nne – hadi elfu saba.

Jafo ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Mji yaliyofanyika Tar 11/01/2018 katika chuo hicho kilichopo Jijini Dar es salaam.

“Taalum hii ni muhimu sana katika ustawi na Afya ya wananchi wetu kote Nchini, uhakika wa kupata maji salama bado ni changamoto kubwa kutokana kutokuwa na miundombinu ya Uhakika na zaidi ni wataalamu wachache waliopo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa” Alisema Jafo.

Aliongeza kuwa Nipongeze chuo hiki cha maji kwa kutoa Shahada kwa mara ya kwanza katika Historia ya Chuo hiki, hapo awali hapakuwa na Ngazi ya Shahada hivyo wataalamu wengi waliishia ngazi ya Stashahada ambapo mara nyingine ilihitajika Utaalamu zaidi kutokana na changamoto za kiutendaji katika maeneo mbali.

“Kwa sasa mmejibu changamoto hii katika Sekta ya Maji kwa kufanikisha kutoa wahitimu wa Ngazi ya Shahada haya ni mafanikio kwa Chuo, kwa Wahitimu na Taifa kwa Ujumla nawapongeza sana na nawakaribishe katika Kulitumikia Taifa hili kwa sababu ujuzi mlioupata unahitajika sana” Alisema Jafo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo(Katikati) akiwasili kwenye Chuo cha Maji tayari kwa kutunuku Shahada na Stashahada katika mahafali ya Tisa ya Chuo hicho.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo akizungumza na wahitimu wa Chuo cha Maji, Wakufunzi na wageni waalikwa(hawapo pichani) wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo hicho.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo akitoa Cheti kwa mwanafunzi wa kike aliyefanya vizuri Kitaaluma katika ngazi ya Astashahada.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo(Katikati aliyekaa) katika Picha ya Pamoja na wanafunzi waliohitimu Shaada ya Uhandisi na Rasilimali za Maji na Umwagiliaji katika Chuo cha Maji.


MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 12,2018

WAWILI WAENDA JELA MIAKA 5 KWA KOSA LA KUSAFIRISHA DHAHABU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii.

WAFANYABIASHARA wawili maarufu Naushad Mohammed Suleiman (63) na Ali Makame Juma (36) wakazi wa Zanzibar, wamehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya jumla ya sh.milioni sita baada ya kukiri mashtaka ya kusafirisha madini ya dhahabu vipande saba vyenye thamani ya Sh milioni 989.7 bila kuwa na leseni.

Hukumu hiyo imesomwa jana jioni na Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mashauri amesema washtakiwa wametiwa hatiani kwa kukiri makosa waliyoshitakiwa nayo ya  uhujumu uchumi ambayo ni kula njama na kusafirisha dhahabu bila kuwa na kibali.
Aidha mahakama imeamuru kuwa, miche saba ya dhahabu pamoja na fedha za nchi 25 ambazo washtakiwa walikamatwa nazo zimetaifishwa na serikali.

Kabla ya kusomwa kwa adhabu, upande wa mashtaka ulitoa niche saba ya dhahabu, fedha za nchi 25 za kigeni zikiwa kwenye mabegi mawili.
 Kabla ya kusomewa adhabu mahakama iliuliza upande wa mashtaka kama wanalolote la kusema ambapo, Wakili  Faraja Nchimbi aliiomba mahakama itoe adhabu Kali kwa washtakiwa ili iwe fundisho kwao na kwa wengine wenye mawazo ya kutenda kosa kama hilo.
Alisema vitendo vilivyofanywa na washtakiwa vinaleta hasara kubwa kwa nchi ya Tanzania na pia vinachangia kwa asilimia kubwa kurudisha nyuma uchumi wa Tainzania.
"Mheshimiwa ni rai yetu, washtakiwa wanastahili kupata adhabu Kali kwa mujibu wa sheria ili pia kulinda rasilimali za nchi yetu, amesema Nchimbi".

Katika utetezi wao washtakiwa wakiwakilishwa na Wakili wao Emmanuel Safari aliomba mahakama kutowapa washtakiwa adhabu Kali kwa kuwa ni wakosaji wa mara ya kwanza na pia wamekiri wenyewe kutenda makosa na wameondoa usumbufu wa kuita mashahidi kwani wamejutia makosa waliyotenda.
Aliongeza kuwa kitendo cha washtakiwa kuachia mali waliyokamatwa nayo ambayo ni mali halali inaonyesha kuwa  wameishajiadhibu. " Tunaomba mahakama izingatie kutokuwa na leseni ni suala ambalo wengi hawalijui hivyo wameishajiadhibu wenyewe" amedai Safari.
Ameongeza, mshtakiwa Mohammed ni mgonjwa hawezi kusimama vizuri pia anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

"Nimezingatia maombi ya upande wa mashtaka na uteezi wenu kuwa ni wakosaji wa mara ya kwanza lakini kitendo mlichofanya ni kosa na kinafanya uchumi wa nchi hii udidimie"

" Mahakama inawahukumu katika shtaka la kula njama kulipa faini ya sh.milioni mbili au kwenda jela miaka miwili na katika shtaka la pili la kusafirisha dhahabu mnatakiwa kulipa faini ya sh.milioni nne na mkishindwa mtatumikia kifungo cha miaka mitatu jela, na ikiwa mtaenda gerezani adhabu zote zitaenda pamoja", alisema Hakimu Mashauri.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI KUVIPA KIPAUMBELE VIWANDA VYA NDANI VINAVYOZALISHA YA VIFAA VYA MAJI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amesema Serikali ya Rais Magufuli kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji imetoa kipaumbele kwa viwanda vya ndani vinavyozalisha bidhaa zinazotumika kutekeleza miradi mikubwa ya maji inayoendelea kujengwa nchini kote.
Aweso ametoa kauli hiyo mjini Kahama alipotembelea kiwanda cha Kahama Oil Mills, mkoani Shinyanga ambacho moja ya shughuli zake ni kutengeneza mabomba na vifaa mbalimbali vinavyotumika kutekeleza miradi ya maji na kutoa angalizo kwamba ni lazima viwanda vya ndani vizingatie ubora wa bidhaa zao na kukidhi mahitaji halisi ya miradi yote ya maji nchini.
‘‘Hatuna sababu ya kutotumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu vya ndani, maadamu vinazingatia ubora wa bidhaa inazozalisha na kukidhi mahitaji ya nchi yetu. Serikali ya Rais Magufuli imetoa kipaumbele kwa wazalendo nchini, hivyo tumieni fursa hii na kutomuangusha,’’ alisema Aweso.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akipokea maelekezo kutoka kwa Meneja Mradi wa Kiwanda cha Kahama Oil Mills, Jiten Divecha (kulia) ambacho moja ya shughuli zake ni kuzalisha vifaa vya maji kilichopo wilayani Kahama, mkoani Shinyanga alipotembelea kiwandani hapo.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akihakiki ubora wa maji yanayozalishwa na mradi wa pamoja (Joint Water Partnership Project) unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu na halmashauri za wilaya ya Shinyanga na Msalala kwa mkoa wa Shinyanga na Nyangh'wale kwa Mkoa wa Geita.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Kakola ambacho ni miongoni mwa vijiji 13 vitakavyonufaika na mradi wa pamoja (Joint Water Partnership Project) unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu na halmashauri za wilaya ya Shinyanga na Msalala kwa mkoa wa Shinyanga na Nyangh'wale kwa Mkoa wa Geita.
 Baadhi ya mabomba yanayozalishwa na Kiwanda cha Kahama Oil Mills kilichopo wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA 

MKUU WA MKOA WA DSM MHE. PAUL MAKONDA NA UJIO WA RAIS PAUL KAGAME WA RWANDA JUMAPILI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUANZA KWA VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE TAREHE 15 HADI 27 JANUARI, 2018, MJINI DODOMA

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA SHEREHE ZA MIAKA 54 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

$
0
0
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani humo.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wakiwa wamesimama  wakati gwaride la heshma(halionekani pichani) lilipokuwa likipita katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani humo.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amani kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akipungia mkono wakati akiwasili katika uwanja wa Amani.
Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la Heshma katika  sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zolizofanyika katika uwanja wa Amani.
 Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Mkapa akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na Rais mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Saluti kutoka kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro mara baada ya kuhudhuria sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.PICHA NA IKULU

LEO NI SIKU YA KUZALIWA KWA MDAU MUGANYIZI BISHEKO

$
0
0
 
Leo January 12, 2018 ni siku ya kuzaliwa kwa Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank of Africa Tanzania, Muganyizi Bisheko. Wote kwa pamoja tunapenda kukutakia heri na fanaka. Mwenyezi Mungu akujalie maisha marefu.

SERA YA VIWANDA HAITAFANIKIWA IWAPO HATUTAENDANA NA MABADILIKO MAKUBWA YA SOKO LA WAKULIMA

$
0
0
Na Jumbe Ismailly,  SINGIDA   
  
MKURUGENZI wa wanawake wa Chama Cha Wananchi (CUF) Taifa, Salama Masudi amesema kuwa sera ya viwanda nchini haiwezi kufanikiwa iwapo hatutaendana na mabadiliko makubwa ya soko la wakulima na ikiwezekana katika mpango mzima wa mapinduzi ya kilimo wenye lengo la kuwawezesha wakulima wa chini kuelekea soko kuu la dunia kuweza kuinua kipato kutoka kwa wananchi maskini kabisa.

Mkurugenzi huyo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wakati wa kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Singida Kaskazini uliofanyika katika Kijiji cha Ughandi, wilaya ya Singida vijijini.

Alifafanua Salama kwamba baada ya wakulima kuwa wamewezeshwa hususani katika maeneo hayo wanayotoka ambapo kilimo ndicho uti wa mgongo,basi kuwezeshwa kwa viwanda hivyo kunawezekana kabisa kutoka maeneo muhimu kulingana na mazao yanayotokana na uwezeshwaji wa viwanda hivyo.

Hata hivyo Salama alisisitiza pia kwamba katika miaka yote wananchi wa jimbo hilo wamekuwa wakipelekewa wagombea wanaume ambao wameshindwa kukidhi haja zao kwa kuwa wanaguswa na matatizo yanayowashika wanawake wenyewe,lakini mwaka huu CUF imewaletea mwanamama huyo mahiri na ambaye wanaamini ndiye suluhisho pekee la matatizo ya wananwake.

“Tunaomba kwa namna ya pekee na utulivu mkubwa tunaomba kura kwa akina mama mtusaidie kuweza kumsaidia mama Delphina Mngazija kwa kuwa ninyi ndio wengi kabisa katika upigaji wa kura na mnatumiwa kuwa chambo cha kuwakandamiza wananchi”alisisitiza Salama.

“Tumewaletea  mama huyo anaguswa na changamoto zinazotukbili sisi wanawake,wengi wetu hapa tunaumizwa na sera mbovu,tumekuja na kampeni pekee  kupitia mgombea wa chama chetu ‘Mwanamke tua ndoo maana yake akiwa sauti ya Bunge kupitia Singida kaskazini anaweza kuongea na serikali kupitia mifuko ya jimbo ili aweze kuleta visima vitakavyosaidia akina mama  kupunguza adha ya maji katika maeneo mnayoishi”alifafanua.
 Wananchi pamoja na wanachama wa CUF wa Kijiji cha Ughandi wakimsubiri kwa hamu Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Prof.Ibrahimu Lipumba kumsikiliza sera za chama na kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho, Delphina Mngazija.
Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof.Ibrahimu Lipumba (wa kwanza kutoka kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa wanawake wa chama hicho, Salama Masudi kwenye viwanja vya mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Ughandi, wilaya ya Singida Vijijini kabla ya kuongea na wananchi hao.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

UVCCM KIBAHA MJINI YAWATAKA VIJANA KUSIMAMIA KWA VITENDO MAPINDUZI

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha.

JUMUIYA ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mjini Kibaha mkoani Pwani imesema Taifa linawategemea vijana katika dhana nzima itakayothibitisha wanasimamia kwa vitendo Mapinduzi katika kuondoa maovu yanayolikabili Taifa hili.

Aidha imekemea tabia ya kujigawa na kuweka makundi baina yao kwani kwa kufanya hivyo ni kudidimiza harakati na juhudi za kuimarisha jumuiya na kupambana kimaendeleo .

Mwenyekiti wa UVCCM Mji wa Kibaha, Azilongwa Bohari aliyasema hayo, mara baada ya jumuiya hiyo kufanya usafi katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya Tumbi pamoja na kuchangia damu units 22 hospitalini hapo katika kuadhimisha miaka 54 ya siku ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hata hivyo ,alisisitiza umoja na mshikamano kwa kundi la vijana.

Azilongwa alisema, serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar ,zinatakiwa kuona vijana wake wanachemchem ya maendeleo badala ya kuwa dimbwi la matatizo mitaani.

Aliwaasa vijana kwa umoja wao kujishughulisha na kuunda vikundi vya ujasiriamali ili kujiinua kimaisha .

"Tukielekea kwenye uchumi wa kati kuna kila sababu ya kupambana na umasikini,tukiwa kama vijana ,tuondokane kuwa matatizo kwenye jamii bali tuwe wapiganaji katika maendeleo na maisha yetu " alisema.

Pamoja na hayo ,Azilongwa aliwaomba wanachama na viongozi wa jumuiya hiyo kuanzia ngazi ya chini kushikamana ili kujidhatiti kwa lengo la kujenga ushindi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020.

Aliwataka viongozi wa chama na jumuiya kuendelea kuongeza wanachama wapya ambao ndio mtaji kwao na wapiga kura halali kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Azilongwa hakusita kusisitiza vikao vya mara kwa mara na kuwataka viongozi wa UVCCM wilayani hapo kushiriki katika vikao muhimu ili kujadili na kubuni njia mbadala za kuongeza wanachama na kuinua maendeleo ya jumuiya.

Akielezea zoezi la kuchangia damu, alishukuru wanachama waliojitokeza kuchangia na kuwezesha units 22 ambazo kwa hakika zitasaidia kuongeza mahitaji yanayotakiwa.

Alisema wamelenga kuchangia damu hospitalini hapo, kutokana na mahitaji makubwa na hospitali hiyo kupokea majeruhi wa ajali nyingi zinazotokea mara kwa mara kwenye barabara kuu ya Morogoro.
Nae katibu wa mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini,Method Mselewa,alisema mbali ya hayo wanatembelea kituo cha watoto yatima kilichopo Mkuza na kutoa misaada iliyotokana na ushirikiano wao na hisani kutoka kwa mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka na mkewe Selina Koka.
Mselewa alimshukuru mbunge huyo na familia yake kwa ushirikiano wao .
Baadhi ya viongozi na wanachama wa jumuiya ya vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kibaha Mjini, Pwani wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanya usafi ,na kujitolea kuchangia damu units 22, katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya Tumbi ikiwa ni sehemu yao ya kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(picha na Mwamvua Mwinyi).

IGP SIRRO ATAKA ASKARI KUHESHIMU WANANCHI.

$
0
0
Mkuu wa jeshi la polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na askari wa vikosi vya Mjini Magharibi, Kusini Unguja na Kaskazini Unguja jana alipokwenda kufanya mazungumzo ya kikazi na maofisa na askari visiwani Unguja. IGP Simon aliwataka askari visiwani humo kuheshimu wananchi wakiwa kwenye kazi zao ili kuendelea kuleta heshima ya jeshi la polisi.

Askari wa vikosi vya Mjini Magharibi, Kusini Unguja na Kaskazini Unguja wakimsiliza  IGP Simon Sirro alipokuwa anazungumza nao

MATUMIZI YA KIKOA CHA DOT TZ NA DOT AFRIKA KUKUZA UCHUMI WA AFRIKA

$
0
0


Na Lilian Lundo na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA
Watanzania washauriwa kusajili na kutumia kikoa cha dot tz (.tz) na dot Africa (.africa) katika matumizi ya intanenti kwa ajili ya kutoa utambulisho wa kitaifa, ki-bara na kukuza uchumi wa Taifa na Bara la Afrika.

 Akizungumza leo Mjini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa Registry.Afrika Lucky Masilela amesema kuwa vikoa hivyo vinafaida mbalimbali ikiwemo kupunguza gharama za mawasiliano na pia kukuza uchumi wa nchi na bara zima la Afrika kutokana na fedha zinazotumika kusajili vikoa hivyo hubaki katika nchi na bara husika.

“Nitoe ombi kwa wale wote wanaotumia mtandao watumie mtandao wa dot tz au dot Afrika kwa sababu vikoa vingine haviwezi kusaidia Afrika, kutokana na fedha zinazotumika kusajili vikoa hivyo hubaki katika nchi husika” ameongeza Masilela.

Aidha, Masilela amefafanua kuwa Umoja wa Afrika (AU) uliridhia maombi ya rajisi ya dot africa kufanya kampeni ya matumizi ya kikoa cha dot Africa, ambapo Rajisi ya dot africa iliainisha maeneo matano (5) ya kufanya kampeni hiyo kwa niaba ya bara lote la Afrika. Maeneo hayo ni Afrika ya Mashariki, Afrika ya Kaskazini, Afrika ya kati, Afrika Magharibi na Afrika ya kusini.

“Lengo kuu la kampeni hii ni kuwahamasisha waafrika wote watumie kikoa cha dot africa na pia kujenga hamasa ya waafrika kujivunia uafrika wao na kujenga uchumi unaotegemea rasilimali ya kikoa hiki pekee kinacho watambulisha na kuwaunganisha waafrika wote” ameongeza Masilela.

Vile vile amesema kuwa kampeni hiyo inaudhihirishia ulimwengu kuwa ucheleweshwaji wa rasilimali pekee ya kuwatambulisha waafrika wote  kwenye mtandao wa Intaneti umefikia hatima yake hivyo Waafrika sasa, kwa kutumia kikoa cha dot africa  wanauwezo wa  kuwasiliana, kutoa huduma, kufanya biashara (taasisi za umma na binafsi) bila bugudha yoyote katika mtandao wa Intaneti.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Network Information Centre Mhandisi Abibu Ntahigiye amesema kuwa rajisi ya dot africa (ZACR) ilipewa mamlaka ya kuendesha rajisi ya dot africa mwezi Februari 2017 ikiwa ni baada ya miaka mitano (5) ya juhudi za kutafuta uhalali wa kufanya hivyo.

“Kufuatia mafanikio hayo, timu ya dot africa ilipewa jukumu na Umoja wa Africa (Africa Union - AU) kuendesha kampeni za kuhamasisha matumizi ya kikoa cha dot africa barani kote kwa kipindi cha miezi sita (6) kuanzia Agosti 2017 mpaka Januari 2018” ameongeza.

Naye Mwanasheria wa Rajisi ya Tanzania (.tz) Sarah Mhamilawa amesema matumizi ya dot tz ni rahisi na panapotokea tatizo la kiufundi muhusika anapiga simu .tz na tatizo hutatuliwa papohapo tofauti na vikoa vingine ambavyo huhitaji kufuata mlolongo uliowekwa kwa ajili ya utatuzi wa tatizo husika ambao huchukua muda kutatuliwa.

Kampeni ya matumizi ya  dot africa imeambatana na kuendesha magari (roadshow) wakiwa na Bendera ya  dot africa kutoka Afrika Kusini ambapo safari ilianza Januari 1, 2017 kuelekea Addis ababa, Ethiopia kupitia Botswana, Zimbabwe, Zambia, Tanzania na Kenya.

Aidha timu hiyo ikiwa Tanzania imeanzia kampeni hiyo Tunduma kupitia Iringa, Dodoma, Arusha na Kilimanjaro ambapo wakiwa Kilimanjaro watapandisha bendera ya dot Africa na dot tz kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro.


  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Network Information Centre Mhandisi Abibu R. Ntahigiye (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kampeni ya msafara kwa njia ya barabara (Roadshow Campaign) inayofanywa na taasisi ya Dot tz na Dot africa kuhamasisha matumizi ya mitandao hiyo ya intaneti kwa Afrika leo mkoani Dodoma. Kulia kwake ni  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Registry.Africa Ndg. Lucky Masilela.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Registry.Africa Ndg. Lucky Masilela(wakwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kampeni ya msafara kwa njia ya barabara (Roadshow Campaign) inayofanywa na taasisi ya Dot tz na Dot africa kuhamasisha matumizi ya mitandao hiyo ya intaneti kwa Afrika leo mkoani Dodoma. Katikati ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Network Information Centre Mhandisi Abibu R. Ntahigiye na mmoja wa wajumbe wa msafara huo Ndg. Ronald Schwaerzler
 Mmoja wa wajumbe wa msafara kwa njia ya barabara (Roadshow Campaign) inayofanywa na taasisi za mitandao ya intaneti za Dot tz na Dot africa kuhamasisha matumizi ya mitandao kwa Afrika Ndg. Ronald Schwaerzler (wapili kulia) akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ratiba ya kupanda mlima Kilimanjaro kama sehemu ya kampeni hiyo leo mkoani Dodoma. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Registry.Africa Ndg. Lucky Masilela na wapili ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Network Information Centre Mhandisi Abibu R. Ntahigiye
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dododma Ndg. Jabera Matogolo(wakwanza kulia) akielezea namna ambavyo mtandao wa intaneti unavyosaidia kukuza kiswahili wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu kampeni ya msafara kwa njia ya barabara (Roadshow Campaign) inayofanywa na taasisi ya Dot tz na Dot africa kuhamasisha matumizi ya mitandao hiyo ya intaneti kwa Afrika leo mkoani Dodoma.
Washiriki wa kampeni ya msafara kwa njia ya barabara (Roadshow Campaign) inayofanywa na taasisi ya Dot tz na Dot africa kuhamasisha matumizi ya mitandao hiyo ya intaneti kwa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma walipokutana na waandishi wa habari leo mkoani Dodoma.

MWANRI AAGIZA WATOTO WASIPORIPOTI SHULE WAZAZI WAO WAKAMATWE

$
0
0
Na Tiganya Vincent
SERIKALI Mkoani Tabora imeagiza kukamatwa mara moja wazazi au walezi ambao hadi kufikia Jumatatu ijayo (15, January 2018) watakuwa wameshindwa kuhakikisha kuwa watoto wao waliochaguliwa kujiunga Kidato cha kwanza mwaka huu watakuwa hajaripoti katika Shule walizopangiwa.

Agizo hilo limetolewa jana mjini Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri baada ya kupata taarifa kutoka kwa Afisa Elimu Mkoa iliyoakuwa ikionyesha kuwa idadi kubwa ya wanafunzi walichaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza mwaka 2018 bado wengi wao hawajaripoti katika Shule walizopangiwa.

Alisema kuwa kufikia Jumatatu ijayo anataka kupata taarifa na majina ya wanafunzi wote waliochangiwa ambao hawako shuleni ikiwa  na majina ya wazazi wao ili hatua za kisheria dhidi yao ziweze kuchukuliwa kwa kosa la kumkoshesha watoto haki ya kupata elimu.

Mwanri aliongeza kuwa viongozi wa kuanzia mitaa, vitongoji, vijiji , Kata na Wilaya ni vema wahakikishe wanawatafuta watoto wote waliochaguliwa ambao hawako shuleni ili kujua walipo na wanafanya nini kwa kuwa inawezekana wapo ambao tayari wameshaozeshwa.

Alisisitiza kuwa wakikuta mtoto yupo nyumbani na mzazi wake hataki kumpeleka Shule wamukamate mzazi wake ili hawawezi kuwajibika kwa uzembe wake.

“Hapa tutakwenda kwa Sera ya mbanano…kama kiongozi lazima umbane mzazi ambaye hadi hivi sasa hajampeleka mtoto shule wakati wenzake wameshaanza masomo na ikibidi mfikisheni katika vyombo vya Sheria ili ajibu mashitaka yake ya kunyima mtoto haki yake ya elima”alisema Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora

RAIS DKT MAGUFULI AREJEA DAR ES SALAAM AKITOKEA ZANZIBAR KWENYE SHEREHE ZA MIAKA 54 YA MAPINDUZI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na viongozi wengine aliporejea kutoka Zanzibar alikohudhuria sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi leo January 12, 2018.Picha na IKULU
 


WAZIRI LUKUVI: SERIKALI IMEDHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kumaliza changamoto ya migogoro ya ardhi nchini. 

Lukuvi ametoa kauli hiyo wakati anazungumza na Globu ya jamii ambapo amefafanua kuna jitihada na mikakati mbalimbali inafanya kutatua migogoro ya ardhi. 

Amesema migogoro ambayo wizara yake inatafuta ufumbuzi mingi ni ile ya kuanzia mwaka 2015 kurudi nyuma kwani tangu Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani hakuna mgogoro wa ardhi. 

"Kwa sehemu kubwa mimi na wasaidizi wangu tunakwenda vizuri katika kuhakikisha tunamaliza migogoro ya ardhi kama ambavyo dhamira ya Serikali hii inavyotaka. 

"Migogoro mingi imeshughulikiwa na hata iliyokuwepo ilitokana na kutoshughulikiwa kwa wakati.Baadhi ya watendaji hawakuwa  wakichukua hatua kwa haraka. 

"Kwa sasa wizarani wanajua nataka nini na ndio maana tunakwenda vizuri maana hatutaki kutumia muda mwingi kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa ardhi,"amesema Lukuvi. 

Ameongeza kwa kutambua namna ya utendaji kazi wa baadhi ya maofisa wake ndio maana anatumia mfumo wa kuita wananchi wenye matatizo ya ardhi na kisha kutafuta ufumbuzi wake tena hadharani. 

Waziri Lukuvi amesema kwa mwenendo wanaokwenda nao anaamini Serikali ya awamu ya tano itafika mahali hakutakuwa na migogoro mingi ya ardhi. 

Akizungumzia migogoro ya ardhi kwa Jiji la Dar es Salaam, Lukuvi amesema kwa siku tatu ambazo amekuwa akitatua migogoro ya ardhi kwa wale waliofika wizarani ameipatia ufumbuzi.

Amesema migogoro ya ardhi ambayo hajaishughulikia ni ile ambayo kesi zipo mahakamani kwani wizara yake haina uwezo wa kuingilia uamuzi wa mahakama. 

Alipoulizwa iwapo migogoro ya ardhi kwa Dar es Salaam ipo siku itakwisha, amejibu ana uhakika wa kuimaliza. 

"Kwa hali ilivyo itafika wakati hata tukiita watu wenye migogoro ya ardhi waje tuitatue hawatakuwepo maana tunakwenda vizuri katika kuishughulikia,"amesema.
Amefafanua kwa sasa atakuwa na ratiba katika wilaya mbalimbali ambapo atakwenda kwa ajili ya kushughulikia migogoro ya ardhi. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Dar es Salaam aliyefika katika wizara hiyo wakati anasikiliza wenye migogoro ya ardhi jana.

MELI YA MV RUVUMA KUFUNGUA FURSA ZA KIUCHUMI NYASA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Nyasa amesema kwamba kuanza kwa safari kwa Meli ya kisasa ya mizigo ya M.V. Ruvuma kutafungua fursa za kiuchumi za mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
Katika salaam zake za kumkaribisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika jimbo lake la Nyasa, Mhe. Manyanya amewataka wakazi wa Nyasa na Wilaya za jirani kutumia fursa ya uwepo wa meli hiyo kujikwamua kiuchumi.
"Kuanza kwa safari ya meli hii ndiyo ufunguo wa kufungua fursa za kiuchumi za mkoa wetu, hivyo napenda kutumia nafasi hii kuwasihi wananchi wa Nyasa watumie fursa ya kuanza safari kwa meli hii kujikwamua kiuchumi," amesema Mhandisi Manyanya.
Mhandisi Manyanya amesisitiza kwamba kama kuna mwananchi yeyote wa Nyasa ambaye ataendelea kulia njaa au hali ngumu ya kiuchumi basi huyo atakuwa amejitakia mwenyewe, aliongeza.
Meli ya mizigo ya MV Ruvuma ambayo ina uwezo wa kubeba shehena ya tani 1,000 za mizigo imefanya safari yake ya kwanza toka bandari ya Kyela hadi Mbambabay ikiwa na shehena ya Saruji.
Naibu Waziri amesema kwamba moja ya manufaa ya kuanza kwa safari za meli hizo ni pamoja na kufungua biashara kati Nyasa na mikoa jirani.
Mbali na kufungua biashara, meli hizo pia zitasadia kufanya bandari zilizo katika Ziwa Nyasa kuamka ambapo pia shughuli mbalimbali za kiuchumi zitakuwa zikiendelea katika bandari hizo.
Kuanza safari kwa meli hiyo na ile ya MV Songea pia kunatarajiwa kufungua milango ya ajira kwa wananchi wa mikoa iliyo pembezoni mwa Ziwa Nyasa.
Meli za mizigo za MV Ruvuma na MV Njombe ni moja kati ya meli tatu zilizotengenezwa na kuendeshwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa ajili ya kutoa huduma kwenye mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Songea na nchi jirani za Malawi na Msumbiji.
Meli hizo za kisasa zenye uwezo wa kubeba shehena yenye uzito wa tani 1,000 kila moja zimekuwa mkombozi kwa wananchi wa mikoa hiyo ambao walikuwa hawana uhakika wa usafiri katika ziwa hilo kwa kipindi kirefu.
Tangu kuzinduliwa rasmi kwa meli hizo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mwaka jana, kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wafanyabiashara na wananchi wa kawaida kutaka kuzitumia meli kusafirisha bidhaa zao.
Bidhaa kubwa zinazotarajiwa kusafirishwa na meli hizo ni pamoja na makaa ya mawe toka Ngaka, Saruji toka kiwanda Saruji cha Mbeya na Dangote pamoja na 'Clinker'.
Ujenzi wa meli hizo mbili za mizigo ulianza Mwaka 2015, ukiwa na lengo la kutoa huduma ya usafirishaji wa shehena ya makaa ya mawe kutoka Bandari ya Ndumbi, pamoja na mizigo mingine katika Ziwa Nyasa. 
Bidhaa nyingine ni pamoja na usafirishaji wa makaa ya mawe kwenda Mbeya kupitia bandari ya Kiwira pamoja na bandari mbalimbali nchini Malawi.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stellah Manyanya ambaye pia ni Mbunge wa Nyasa akishangilia sambamba na Kaimu Mkuu wa Bandari za Ziwa Nyasa, Bw. Ajuaje Msese wakati wa ujio wa meli hiyo ikiwa na shehena ya mzigo wa Saruji toka Kyela.
 Meli ya MV Ruvuma ikishusha shehena ya kwanza ya Saruji katika bandari ya Mbambabay mara baada ya kufanya safari yake ya kwanza ikiwa na shehena ya mzigo kutoka bandari Kyela hadi hapo Mbambabay, mjini Nyasa.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 13, 2018

STAR TV: BODABODA NA BAJAJI ZADAKWA NA NAMBA BANDIA TUNDUMA

STAR TV: KONDAKTA WA BASI ANASWA NA MILIPUKO MJINI TUNDUMA

UPIGAJI CHAPA MIFUGO KATIKA MKOANI SHINYANGA

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa uzalishaji  Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  Dk. Assimwe Rwiguza akipigaji chapa ng’ombe katika Kijiji cha Idodoma Wilaya ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu 15 wa mifugo walioko katika mikoa 26 kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa linalotarajiwa kukamilika January 31 mwaka huu.
 Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Dk  Asimwe  Rwiguza akitoa ufafanuzi wa mahali sahihi panapotakiwa kupiga chapa kwa ng'ombe kwa wafugaji wa Kijiji cha Idodomya wilayani Shinyanga. kushoto ni Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya Shinyanga, Dk. Clement Batisiliko
Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Dk.  Asimwe  Rwiguza akitoa ufafanuzi kwa wafugaji wa Kijiji cha Idomya umuhimu wa kupiga chapa mifugo yao kabla ya muda wa nyongeza uliowekwa na Serikali kumalizika wa Januari 31 mwaka huu ambapo Dk. Assimwe ni miongoni mwa timu ya wataalamu 15 wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi walioko kwenye mikoa 26 ya Tanzania bara kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa.
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images