Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Waziri Profesa Mbarawa avamia bandarini Usiku, abaini madudu...!

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa jana usiku amefanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam na kubaini mawakala wa meli wanaotoa huduma katika bandari hiyo hawafanyi kazi saa 24 kama Serikali ilivyoelekeza.

Prof. Mbarawa ameiagiza Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA) kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria kwa mawakala wote waliokiuka agizo la Serikali la kutoa huduma bandarini kwa saa 24.

"Kati ya Mawakala wa Meli nane ambao tumewatembelea usiku huu ni wakala mmoja tu ndiye tuliyemkuta akitoa huduma kwa saa 24 hivyo SUMATRA katika kipindi cha siku saba hatua za kinidhamu na kisheria zichukuliwe kwa wote wanaokiuka utaratibu huu na nipewe ripoti ya hatua zilizochukuliwa," alisema Waziri Prof. Mbarawa.

"Katika ukaguzi huu tumegunduwa kuwa mawakala wengi wanaacha watoa huduma wasiostahili, wakiwemo walinzi kufanya kazi nyakati za usiku ambao hawawezi kutoa huduma inayostahili usiku na kuendelea kutoa huduma asubuhi jambo ambalo sio sahihi," amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza kwa simu na mmoja wa maofisa wa Bandari ya Dar es Salaam baada ya kutembelea ofisini kwake.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), Giliadi Ngewe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), wakishuhudia moja ya wakala wa meli akiwa amefunga ofisi kinyume cha maelekezo ya Serikali ya kufanya kazi saa 24.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Jalada la kesi ya Vigogo, Six telecom latua kwa DPP

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

JALADA la kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani milioni 3.7, sawa na Sh.bilioni nane, dhidi ya vigogo wanne wa Kampuni ya Six Telecoms Limited na kampuni yenyewe limetua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP).

Mwendesha mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.

Hatua hiyo imefika baada ya Kishenyi kuieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Kutokana na taarifa hiyo, wakili wa utetezi Alex Mgongolwa aliomba kujua upelelezi dhidi ya kesi hiyo umefikia wapi.

"Mheshimiwa, jalada la kesi hii liko kwa DPP, tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa", amedai Kishenyi.

Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 19, mwaka huu kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mhandisi  na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya  Six telecoms,   Hafidhi  Shamte, Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mwanasheria na Mhadhiri na Mkurugenzi wa hiyo kampuni Dkt ,Ringo Tenga,  Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms Limited.

Wote kwa pamoja wanadaiwa kuhujumu miundombinu ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa kutoza garama chini ya kiwango, kushindwa kulipa ada za udhibiti na kutakatisha 3,282,741.12.

Pia washtakiwa hao wanadaiwa kuisababishia TCRA hasara ya USD 3,748,751.22, sawa na Sh 8 bilioni  za kitanzania.

HAZINA YANG’ARA TENA MATOKEO DARASA LA NNE

$
0
0
SHULE ya  Msingi Hazina ya jijini Dar es Salaam imeng’ara kwenye matokeo ya darasa la nne kwa kufanikiwa kuwa ya kwanza Mkoa wa Dar es Salaam na kutoa wanafunzi saba kati ya 10 walioingia kumi  bora kitaifa.

Katika matokeo yaliyotangazwa jana na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), shule hiyo pia imefanikiwa kutoa wanafunzi wa kike saba bora kitaifa miongoni mwa wasichana 10 walioingia kumi bora kitaifa na mwanafunzi bora kitaifa.

Wanafunzi waliofanikiwa kuingia 10 bora kitaifa ni Rahma Khatibu (Hazina), Fildaus Abbas (Hazina),  Martha Shayo (Hazina), Momy Lawrence (Hazina), Zayyana   Nassoro (Hazina), Kokudyness Rweyemamu (Full Gospel), Jesca Nenula (Hazina), Lailaty Nurdin (Hazina), Sharp Gabukambwe (Mungu Bariki) na Muhamed Hoti (Mudio Islamic).

Wasichana walioingia 10 bora kitaifa ni Rahma Khassan (Hazina), Fildaus Msafiri (Hazina), Martha Shayo (Hazina), Momy Laurence (Hazina), Zayyana Nassoro (Hazina), Kokudyness Rweyemamu (Full Goaspel), Jesca Nenula (Hazina), Lailaty Balii (Hazina), Sala Elias (Mwilamvya), Veneranda Richard (Mwilamvya).

Akizungumza, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Patrick Cheche, alisema kwenye kundi la wanafunzi chini ya 40 shule ya Hazina imekuwa ya kwanza kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema shule hiyo imefanikiwa pia kuwa ya tatu kitaifa na ya kwanza kwa upande wa Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Alisema kwa miaka zaidi ya 10 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo wamekuwa wakipata mafanikio makubwa mwaka hadi mwaka kwenye matokeo ya kitaifa.

Alitoa mfano kuwa shule imekuwa ikipata matokeo mazuri kitaaluma kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na hadi Taifa na kumekuwa na mabadiliko chanya.

Cheche alisema malengo yao ni kuendelea kufundisha kwa bidii sana ili kuendelea kushika nafasi za juu katika mitihani ya kitaifa na kusaidia watoto wengi wa Tanzania kupata elimu bora.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD LOWASSA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe  Magufuli akimsindikiza Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe  Magufuli akifurahia jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe  Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akiwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA IKULU

RC TELACK AFANYA ZIARA KUKAGUA KILIMO CHA PAMBA NA MTAMA WILAYANI KISHAPU

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack amefanya ziara ya kukagua kilimo cha zao la Pamba na Mtama wilayani Kishapu kwa ajili ya kuendelea kuhamasisha wakulima kulima mazao hayo kwa wingi kwa njia za kitaalamu ambayo yatawafanya wakue kiuchumi na mkoa kwa ujumla. 

Telack amefanya ziara hiyo leo Jumatatu Januari 8,2018 wilayani Kishapu kwa kukagua baadhi ya mashamba ya pamba na mtama ambayo yamelimwa na wakulima kwa njia ya kitaalamu na kuwataka wakulima kuendelea kutii magizo ya serikali kwa kulima mazao hayo ya biashara na chakula ambayo yatabadili mfumo wa maisha yao pamoja na kuacha kuishi kwenye nyumba za tembe.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara baada ya kutembelea mashamba ya wakulima katika kijiji na kata ya Shangihilu Telack amewataka wakulima kijijini kuendelea kujikita kulima mazao hayo ya pamba na mtama kwa njia ya kitaalamu ambayo itawafanya kupata mavuno mengi na kuinuka kiuchumi. 

“Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli imejipanga kumuinua mkulima kiuchumi kupitia kilimo na ndiyo maana changamoto zote zilizokuwa zikimkabili mkulima zinatatuliwa ili muweze kunufaika na kilimo chenu , hivyo nawasihi mlime mazao ya pamba na mtama kwa wingi kwani soko lake lipo”,alisema Telack. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack mwenye ushungi akiwa na mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Taraba (katikati mwenye nguo ya njano) na aliyepo mkono wa kushoto ni Diwani wa Kata ya Shangihilu Mohamed Hamadi pamoja na wataalamu wa kilimo na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Steven Magoiga wakikagua shamba la pamba hekali 22 la mkulima Kazimiri Masunga -Picha na Marco Maduhu- Malunde1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akiwa katika shamba la pamba na viongozi mbalimbali
Mkulima wa zao la Pamba Kazimiri Masunga akimuonyesha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack ukubwa wa eneo alilolima shamba hilo hekali 22, na kutarajia kwenye mavuno kumuinua kiuchumi huku akiomba serikali kuwapatia dawa ya kuua wadudu waharibifu ili wasipate hasara.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akiangalia wadudu wanavyolishambulia zao hilo la pamba na kutoa maagizo kuhusu ufumbuzi upatikane wa kuwateketeza kwa kupulizia dawa yenye nguvu ya kuua wadudu ili kutowapatia hasara wakulima.

RAIS MAGUFULI AMEMSIFU LOWASSA KWA KUFANYA SIASA ZA KISTAARABU

$
0
0
*Asema ni mwanasiasa wa tofauti na wengine
*Amuahidi kumpa ushirikiano,apokea ushauri wake

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amemuelezea Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kuwa ni mwanasiasa mstaarabu na kuahidi kumpa ushirikiano.

Ameongeza hata wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, Lowassa hakuna mahali popote ambapo amemtukana na kutumia nafasi hiyo kusema mzee huyo ni tofauti na wanasiasa wengine nchini.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu mstaafu Lowassa ambapo wamezungumza mambo mengi. Akimuelezea Lowassa, Rais, Magufuli amesema ni mzee huyo ni moja kati ya wanasiasa ambao wamekuwa wakifanya siasa za kistaarabu tofauti na wengine.

" Wakati wa uchaguzi mkuu hakuna mahali popote akiwa kwenye kampeni mzee Lowassa amenitukana au kutukana mtu yoyote.

"Kikubwa niseme tu nampongeza .Labda wale wapambe wake ndio walikuwa wanatukana na naamini hakuwatuma. Etii mzee Lowassa uliwatuma? Lowassa akajibu "hapana sijawatuma".

Rais Magufuli akafafanua kuwa "Wapambe ndio walikuwa wanaropoka na kufanya mambo mengi lakini kwa mzee Lowassa amekuwa akifanya siasa za kistaarabu."

Hivyo ndio maana anampongeza na kumtakia maisha mema na yeye Rais akiwa kiongozi wake ataendelea kutoa ushirikiano kwake. Amesema akiwa na mzee Lowassa wamezungumza na kushauriana mambo mengi ambayo hawezi kuyasema.

"Tutaendelea kushirikiana na naamini ataendelea kunishauri kwa maslahi ya nchi yetu,"amesema.

Amumelezea Lowassa kuwa amefanya mambo mengi mazuri kwa nyakati tofauti na aliyoyafanya lazima mchango wake utambulike. "Namshukuru na kumtakia heri ya mwaka mpya".

LOWASSA AIONA TANZANIA YA MATUMAINI

Kwa upande wake Lowassa pamoja na mambo mengi ameelezea namna anavyoiona Tanzania ya miaka mitano ijayo.

"Naiona Tanzania yenye matumaini mapya kwa Watanzania,"amesema Lowassa wakati anajibu swali ambalo ameulizwa anaionaje Tanzania ya miaka mitano ijayo?

MATUNDA SAFI NA SALAMA YAPO HAPA..

MICHUZI TV: WAZIRI LUKUVI ATATUA MIGOGORO PAPO KWA HAPO KWA WAKAZI WA DAR


WACHEZAJI SIMBA WAREJEA DAR NA VIFURUSHI MKONINI

$
0
0

 Wachezaji wa Simba SC, Nicolaus Gyan na Asante Kwasi wakiwasili leo jijini Dar es Salaam kutokea visiwani Zanzibar baada ya kuondolewa katika Michuano ya  Kombe la Mapinduzi kwa kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi A.
 Mshambuliaji wa Wekundu wa Msimbazi,  Shiza Ramadhani Kichuya akizungumza na waandishi wa habari bandarini hapo mara baada ya kuwasili leo Jijini Dar es salaam akitokea visiwani Zanzibar. Simba imendolewa katika Michuano ya  Kombe la Mapinduzi .
 Baadhi ya washabiki wa Simba SC wakishangilia pindi timu hiyo iliporejea Dar baada ya kuondolewa katika Michuano ya  Kombe la Mapinduzi.
Mshabiki wa Simba SC, Willium Mazoba akizungumza na Michuzi Blog amesema kuwa amesikitishwa kwa timu yake kupoteza michuano hiyo na kuwataka walimu kujipanga kwa ajili ya ligi kuu Tanzania Bara. (Picha na Agness Francis wa Globu ya Jamii)

BALOZI POSSI AJITAMBULISHA RASMI KWA RAIS WA AUSTIA

$
0
0
 Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani anayehudumia pia Austria, Balozi Abdallah Possi akiwasili katika Ikulu ya Viena, nchini Austria kwa kujitambulisha rasmi kwa Rais wa nchi hiyo, Dkt. Alexander Van der Bellen. Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani unahudumia pia Austria, miongoni mwa maeneo yake ya uwakilishi.
 Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani anayehudumia pia Austria, Balozi Abdallah Possi akiwasilisha hati ya utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Dkt. Alexander Van der Bellen katika hafla fupi ya kujitambulisha iliyofanyika Ikulu ya nchi hiyo, leo.
 Rais wa Jamhuri ya Austria, Dkt. Alexander Van der Bellen akizungumza jambo na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani anayehudumia pia Austria, Balozi Abdallah Possi, aliyefika Ikulu hapo kujitambulisha.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani anayehudumia pia Austria, Balozi Abdallah Possi akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Austria, Dkt. Alexander Van der Bellen.

Wanafunzi 26 IFM wahitimu shahada ya uzamili

$
0
0
 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WANAFUNZI 26 wamehitimu shahada ya uzamili ya Teknolojia ya habari  na Uongozi  wa katika chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Profesa Thadeo Satta amesema shahada ya uzamili  ya Teknolojia ya habari  na Uongozi inayotolewa kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Avinashillingam cha nchini India.

Amesema kuwa shahada tangu imeanza kutolewa imekuwa na mwitikio kutokana na mabadiliko ya dunia ya teknolojia ya habari.

Satta amesema kuwa kuanzishwa kwa shahada hiyo nchini kwa ushirikiano chuo kikuu cha nchini  India kumewapunguzia gharama wahitaji wa shahada hiyo ambapo walitakiwa wakasome nchini India lakini wanapata kupitia Chuo cha IFM.

Aidha amesema kuwa kuwa wanashirikiana na vyuo mbalimbali katika kutoa kozi nchini kupitia chuo cha IFM.
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Avinashillingam cha nchini India. Dk. Premavathy Vijayan akizungumza katika mahafali ya 11 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Thadeo Satta akizungumza katika mahafali ya 11 ya shahada ya uzamili waTeknolojia ya Habari na Uongozi leo jijini Dar es Salaam.
 Wanafunzi 26 wakitunukiwa shahada ya uzamili waTeknolojia ya Habari na Uongozi katika mahafali ya 11 Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), leo jijini Dar es Salaam.
 Mhitimu wa shahada ya uzamili waTeknolojia ya Habari na Uongozi,     Edwin Owawa akitunukiwa cheti  katika mahafali ya 11 Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Avinashillingam  cha  nchini India.Dk. Premavathy Vijayan akiwa katika picha ya pamoja ya Watendaji wa IFM na Wahitimu 26 katika mahafali ya 11 ya Chuo cha IFM leo jijini Dar es Salaam.

Hazina yang’ara tena matokeo darasa la nne

$
0
0
SHULE ya  Msingi Hazina ya jijini Dar es Salaam imeng’ara kwenye matokeo ya darasa la nne kwa kufanikiwa kuwa ya kwanza Mkoa wa Dar es Salaam na kutoa wanafunzi saba kati ya 10 walioingia kumi  bora kitaifa.

Katika matokeo yaliyotangazwa jana na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), shule hiyo pia imefanikiwa kutoa wanafunzi wa kike saba bora kitaifa miongoni mwa wasichana 10 walioingia kumi bora kitaifa na mwanafunzi bora kitaifa.

Wanafunzi waliofanikiwa kuingia 10 bora kitaifa ni Rahma Khatibu (Hazina), Fildaus Abbas (Hazina),  Martha Shayo (Hazina), Momy Lawrence (Hazina), Zayyana   Nassoro (Hazina), Kokudyness Rweyemamu (Full Gospel), Jesca Nenula (Hazina), Lailaty Nurdin (Hazina), Sharp Gabukambwe (Mungu Bariki) na Muhamed Hoti (Mudio Islamic).

Wasichana walioingia 10 bora kitaifa ni Rahma Khassan (Hazina), Fildaus Msafiri (Hazina), Martha Shayo (Hazina), Momy Laurence (Hazina), Zayyana Nassoro (Hazina), Kokudyness Rweyemamu (Full Goaspel), Jesca Nenula (Hazina), Lailaty Balii (Hazina), Sala Elias (Mwilamvya), Veneranda Richard (Mwilamvya).

Akizungumza, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Patrick Cheche, alisema kwenye kundi la wanafunzi chini ya 40 shule ya Hazina imekuwa ya kwanza kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema shule hiyo imefanikiwa pia kuwa ya tatu kitaifa na ya kwanza kwa upande wa Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Alisema kwa miaka zaidi ya 10 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo wamekuwa wakipata mafanikio makubwa mwaka hadi mwaka kwenye matokeo ya kitaifa.

Alitoa mfano kuwa shule imekuwa ikipata matokeo mazuri kitaaluma kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na hadi Taifa na kumekuwa na mabadiliko chanya.

Cheche alisema malengo yao ni kuendelea kufundisha kwa bidii sana ili kuendelea kushika nafasi za juu katika mitihani ya kitaifa na kusaidia watoto wengi wa Tanzania kupata elimu bora.

MOGELA, KAYUNI WAMZUNGUMZIA MAREHEMU ATHUMAN JUMA CHAMA "JOGOO" ALIYEZIKWA LEO

Naibu Waziri Mpya wa Madini, Doto Biteko aanza kazi

$
0
0
Naibu Waziri wa Madini, Doto Mashaka Biteko ambaye ameapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Madini tarehe 8 Januari, 2018 ameanza kazi rasmi kwa kufanya kikao na Viongozi na Watumishi wa Wizara husika. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Wizara jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Katibu Mkuu, Profesa Simon Msanjila.

Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Waziri huyo alieleza kuhusu umuhimu wa kuwepo kwa ushirikiano kati ya viongozi na watumishi wa Wizara ili kwa pamoja wasimamie ipasavyo Rasilimali Madini na kuhakikisha kuwa inafaidisha Taifa. “ Ili kutimiza malengo ya Rais wetu ya kuhakikisha kuwa Rasimali Madini inaendelezwa ipasavyo, hatuna budi kushirikiana na kushikamana ili kuwe na umoja utakaoleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu kwani sisi sote ni watumishi wa watanzania,” alisema Biteko.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema kuwa Uteuzi wa Naibu Waziri wa Pili katika Wizara ya Madini unaonesha namna Rais John Magufuli anavyoichukulia kwa umuhimu wa pekee Sekta ya Madini ambayo ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa nchi. “ Tutashirikiana kwa pamoja na watumishi wa Wizara ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa mbele zaidi,” alisema Nyongo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila alisema kuwa viongozi hao na watumishi kwa pamoja watafanikisha mategemeo na malengo ya Rais John Magufuli ya kuhakikisha kuwa Rasimali Madini inalinufaisha Taifa.

Aidha alitumia fursa hiyo kuwaeleza watumishi kuhusu uamuzi wa Rais John Magufuli wa kutengua uteuzi wa Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka na kumteua Profesa Shukrani Elisha Manya kuwa Kamishna wa Madini na pia kukaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Madini na hivyo kuwaasa watumishi kumpa ushirikiano Kamishna huyo mpya.
Naibu Waziri Mpya wa Madini, Doto Biteko (katikati) akizungumza katika kikao chake na watumishi wa Wizara ya Madini. Kulia kwa Naibu Waziri Doto Biteko ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo. .
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza katika kikao kati ya Naibu Waziri Mpya wa Madini, Doto Biteko (katikati) na watumishi wa Wizara ya Madini. Kulia kwa Naibu Waziri Doto Biteko ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (aliyesimama) akizungumza katika kikao cha Naibu Waziri Mpya wa Madini, Doto Biteko (katikati) na watumishi wa Wizara ya Madini. kushoto kwa Naibu Waziri, Doto Biteko ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Madini, wakimsikiliza Naibu Waziri Mpya wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) wakati alipowasili katika Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam.

MWIGULU AONGOZA KIKAO CHA WIZARA NA IDARA ZAKE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba akiongoza kikao cha kujadili utendaji kazi wa wizara na Idara zilizopo chini ya wizara.Kushoto  meza kuu ni Katibu Mkuu wa wizara, Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Hassan Simba Yahya.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira, akizungumza  na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama(hawapo pichani), wakati wa kikao cha kujadili utendaji kazi wa   wizara na idara zilizopo chini ya wizara.Kulia ni Waziri wa wizara hiyo, Dk. Mwigulu Nchemba. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Utawala na Fedha  wa Jeshi la Polisi, Kamishna Albert Nyamhanga,  akiwasilisha taarifa ya utendaji wa idara ya polisi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba(hayupo pichani), wakati wa kikao cha kujadili utendaji kazi wa wizara na Idara zilizopo chini ya wizara. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kamishna Musa Ali Musa. 
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dk. Juma Malewa akiwasilisha taarifa ya utendaji wa idara ya magereza  kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba (hayupo pichani), wakati wa kikao cha kujadili utendaji kazi wa wizara na Idara zilizopo chini ya wizara. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage akiwasilisha taarifa ya utendaji wa idara yake  kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba(hayupo pichani), wakati wa kikao cha kujadili utendaji kazi wa wizara na Idara zilizopo chini ya wizara. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Mkuu wa  Idara  Uzalishaji Vitambulisho wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(Nida), Alphonce Malibiche, akiwasilisha taarifa ya utendaji wa idara yake  kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba(hayupo pichani), wakati wa kikao cha kujadili utendaji kazi wa wizara na Idara zilizopo chini ya wizara. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam. 

WAZIRI AAGIZA KUFUFULIWA KWA MNADA IFIKAPO FEBRUARI ILI KUDHIBITI UPOTEVU WA MAPATO YA KILA MWEZI

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye kofia) akipata maelezo ya hali ya sekta ya mifugo na Uvuvi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Denis Mwila (mwenye suti nyeusi) alipotembelea kituo cha mpakani cha Mutukula leo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye kofia) akipokea maelezo ya changamoto za ukaguzi mazao ya mifugo na Uvuvi kutoka kwa Afisa Uhamiaji Konstabo, Rahabu Joel alipotembelea kituo cha mpakani cha Mutukula leo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye kofia) akiangalia mabondo ya samaki aina ya Sangara yaliyokamatwa katika kituo cha mpaka cha Mutukula mkoani Kagera. Kulia ni kaimu Mkurugenzi wa Idara ya maendeleo ya Uvuvi Mwanaidi Mlolwa katikati Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Missenyi Limbe Maurice. Kilo120 zilikamatwa katika kituo hicho.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akifungua mlango wa gari lililokamatwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara likiwa limepakia samaki kilo 2,000 aina ya Sangara na kilo 530 wa aina ya Sato zenye thamani ya shillingi 20,850,000/= kwenye mpaka wa Mlusagamba wilayani Ngara tarehe 03/12/2017.

Na John Mapepele

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Joelson Mpina ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kuhakikisha inafufua mara moja mnada wa Mlusagamba ifikapo mwezi Februari mwaka huu ili kudhibiti zaidi ya milioni mia moja zinazopotea kwa wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi ya Serikali ya kusafirisha mifugo nje ya nchi kwa kupita njia za panya.

Waziri Mpina aliyasema haya leo alipokutana na uongozi wa Halmashauri hiyo pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara katika kituo cha mpaka cha Rusumo baina ya Tanzania na Rwanda kukagua shughuli mbalimbali za sekta za Mifugo na Uvuvi baada ya kutokea katika kituo cha Mutukula mkoani Kagera ambapo pia alifanya ukaguzi kama huo na kukamata kilo 120 za mabondo ya samaki aina ya Sangara yaliyokuwa yakitokea nchi jirani ya Uganda bila kufuata utaratibu.

“Mimi kama Waziri mwenye dhamana ya sekta ya mifugo na uvuvi naelekeza kwamba ifikapo Februari mwaka huu nataka miundo mbinu yote iwe imeboreshwa na mnada wa Mlusagambo uwe unafanya kazi katika kiwango cha mnada wa upili na mimi mwenyewe nitahakikisha ninakuja kuuzindua”lisisitiza Mpina

BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

HEKARI 2,737 ZA MAZAO ZALIWA NA KUHARIBIWA NA PANYA HUKO CHALINZE, WAKULIMA WALILIA MAZAO YAO

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Globu ya Jamii - Chalinze

HEKARI 2,737 za mazao hasa mahindi katika halmashauri ya Chalinze, mkoani Pwani ,zimeliwa na kuharibiwa na wimbi la panya ambalo limejitokeza tangu mwezi Novemba mwaka 2017 hadi sasa. Kutokana na tatizo hilo, wakulima wa kata tano za Kibindu, Miono, Mandela, Pera na Mbwewe wamepata hasara kutokana na kuliwa mazao yao.

Akielezea kuhusiana na panya hao wanaoathiri mazao ya wakulima, afisa kilimo wa halmashauri ya Chalinze, Jovin Bararata alikiri kuwepo kwa tatizo hilo. Alisema walifikishiwa taarifa hiyo miezi miwili sasa ambapo walienda kwenye mashamba ya wakulima na kujionea athari kubwa iliyopo .

Hata hivyo Bararata alisema ,zipo hatua walizozichukua kwani inapotokea tatizo kama hilo ,hulazimika kupeleka taarifa kitengo maalumu cha wizara ya kilimo kinachojishughulikia kuzuia na kudhibiti baa la panya kilichopo Morogoro.

Alieleza ameongea na wataalamu wa kitengo hicho na kuelezwa kuwa kinaendelea na jitihada za kupata sumu itakayosaidia kuua na kuondoa panya hao. Afisa kilimo huyo wa halmashauri ya Chalinze ,alisema wakati wakisubiri kupelekwa kwa sumu hiyo, wamewashauri wakulima kutumia mbinu za asili  zitakazowasaidia kupunguza kero hiyo .

Bararata alisema ,wanachotakiwa kufanya kwasasa ni kuchimba mashimo makubwa kwenye mashamba yao ,kisha wanaweka ndio na kujazaa maji ,pamoja na mahindi,mpunga ama chakula chochote ambapo panya wakiingia watakufa .

"Hiyo ni njia rahisi ya asili ambayo inatumika kusaidia kupambana na baa la panya endapo likijitokeza kama hivi " alifafanua Bararata.

Nae Diwani wa kata ya Kibindu Ramadhani Mkufya ,alisema wakulima walio wengi wamelima kwa wingi msimi huu, lakini limejitokeza wimbi la panya ambapo kwa uhakika, baadhi ya wakulima hakuna watakachovuna.


Alisema uongozi wa kata umefikisha taarifa ya jambo hilo katika Idara ya kilimo ,halmashauri ya Chalinze ,ambapo wataalamu walifika kujionea hali halisi ya uharibifu uliopo na kusema watapeleka taarifa kitengo husika kinachoshughulika na baa la panya kilichopo Morogoro. Mkufya alisema tangu hapo hawajui kinachoendelea , hivyo wanasubiria kupelekwa sumu ili kuzuia panya wasiharibu maeneo mengine .


Baadhi ya wakulima wa kata ya Kibindu ,walishangaa kuona ni kipindi kirefu kimepita tangu kutolewee kwa taarifa hizo na majibu yakiendelewa kutolewa kuwa jitihada zinaendelea za kupeleka sumu.

 ,"Lakini hatujaletewa hiyo sumu ,hivyo haijulikani hiyo sumu huwa haipo,kwenye kitengo hicho hadi kutokee tatizo la aina hiyo ndipo wahangaikie kutafuta sumu ilipo"walihoji.

Kwa mujibu wa afisa kilimo,sekretarieti ya mkoa wa Pwani ,George Kapilima alipokea taarifa ya tatizo la panya katika maeneo ya Kibiti na Chalinze lakini Kibiti hakuna athari kubwa kama iliyotokea Chalinze.

Kutokana na athari iliyojitokeza Chalinze aitaka halmashauri ya Chalinze kufanya tathmini ya tatizo la panya na kuchukua hatua ya kununua sumu hiyo wakati kitengo husika kikiendelea kulifanyia kazi. Kapilima alisema ameshazungumza na afisa kilimo wa halmashauri ya Chalinze na kumtaka aandike barua na kuipelekea kitengo cha kuangamiza panya Morogoro ili waweze kuelekezwa mahali inaponunuliwa sumu ama dawa zinazotumika kuua panya hao.

Alisema ,endapo inabuka tatizo la panya ,zige na viwavijeshi jukumu la kutoa dawa huwa ni la wizara ya kilimo hivyo wakati wakiendelea na mchakato ni lazima ichukuliwe hatua mbadala itakayowasaidia kwa sasa.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU USALAMA WA SEKTA YA KIBENKI NCHINI

$
0
0
Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kuwa taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu sekta ya kibenki nchini kutokuwa salama si sahihi na zinapaswa kupuuzwa. Sekta ya kibenki nchini ipo salama na Benki Kuu ipo makini kuhakikisha kuwa sekta ya kibenki na mfumo wa fedha kwa ujumla ni salama na stahimilivu.

 Benki Kuu inaendelea kuzisimamia benki zote kwa ukaribu kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006. Taarifa zinazosambaa kuhusu kufungwa kwa benki zenye viwango vikubwa vya mikopo chechefu (non-performing loans) hazina ukweli wowote. Taarifa hizo zina lengo la kupotosha umma na kusababisha taharuki kwa wananchi. Benki Kuu inawakumbusha wananchi kuwa benki ndiyo sehemu salama ya kuhifadhi fedha zao. 

Benki Kuu inapenda kuuhakikishia umma kuwa haina lengo la kufuta leseni za benki bila sababu za msingi kama inavyopotoshwa kwenye mitandao ya kijamii. Ni lengo la Benki Kuu kuona kuwa benki zote zilizopewa leseni zinafanya vizuri. Aidha, ieleweke kuwa Benki Kuu hufuta leseni ya benki pale tu benki husika inaposhindwa kuzingatia vigezo ambavyo vimewekwa kisheria. Miongoni mwa sababu za msingi zinazoweza kusababisha kufutwa kwa leseni ya benki ni kuwa na mtaji chini ya kiwango kinachotakiwa kisheria, upungufu wa ukwasi na ukiukwaji wa sheria mbalimbali za kibenki, na si vinginevyo.

 Benki Kuu itaendelea kusimamia shughuli za kibenki kwa ukaribu na kwa mujibu wa Sheria ili kuhakikisha amana za wateja zinakuwa salama muda wote. Hivyo, wananchi wanaombwa kuwa na utulivu na kuondokana na taharuki inayosababishwa na watu wachache. Pia Benki Kuu inawakumbusha wananchi kutoziamini taarifa zisizo rasmi kuhusu usalama wa sekta ya kibenki nchini Tanzania. 

Taarifa rasmi kuhusu sekta ya kibenki hutolewa na Benki Kuu ya Tanzania ambayo kisheria ndiyo msimamizi wa sekta hiyo nchini. Wananchi wanakumbushwa kuwa usambazaji wa taarifa zisizo rasmi ni kinyume cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 na hatua kali zitachukuliwa kwa atakayebainika kufanya hivyo.

 Imetolewa na: Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki
 info@bot.go.tz
 Januari 9, 2018 
 BENKI KUU YA TANZANIA

KAMATI YA MAADILI YA BUNGE YAAGIZWA KUMHOJI OLE SENDEKA

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZINDUZI WA STUIO MPYA ZA ZBC ZANZIBAR LEO

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kuifungua Studio ya Kisasa ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) ikiwa ni shamra shamra za sherehe za Mapinduzi kutimia Miaka 54.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar(ZBC Aiman Duwe akitowa maelezo wakati wa kutembelea Studio ya kurikodia baada ya uzinduzi huo, uliofanyika katika jengo la ZBC mnazi mmoja Zanzibar leo.
KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan King akitowa maelezo ya vifaa vipya vilivyofungwa katika Studio hizo wakati wa ufunguzi wake uliofanya na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza wakiwa katika Studio ya kurikodia katika jengo la ZBC.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mfanyakazi wa ZBC Chumba cha kurushia matangazo ya ZBC Fatma Abubakari akitowa maelezo jinsi ya urushaji wa picha wakati wa ufunguzi wa Studio Mpya za ZBC uliofanyika leo katika jengo lao Mnazi Mmoja Zanzibar.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images