Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

WAZIRI NCHI OFISI YA RAIS KATIBA SHERIA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA HAROUN ALI SULEIMAN AFUNGUA KITUO CHA AFYA UKONGORONI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala bora Haroun Ali Suleiman akikunjuwa kitambaa kuashiria Ufunguzi wa Kituo cha Afya Ukongoroni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar`
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala bora Haroun Ali Suleiman wakwanza kushoto akipata maelezo kutoka kwa Afisa uendeshaji Timu ya Afya Halmashauri Wilaya ya Kati Salma Bakari Mohammed wakati akitembelea kituo cha Afya baada ya kukifungua Ukongoroni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Naibu katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Maulid Salum akitoa maelezo kuhusiana na Kituo cha Afya cha Ukongoroni pamoja na kuahidi kutatua baadhi ya changamoto zilizopo baada ya kufunguliwa kituo hicho Ukongoroni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Hassan Khatib Hassan akizungumza machache kuhusiana na Kituo cha Afya cha Ukongoroni pamoja na kuahidi kutatua baadhi ya changamoto zilizopo katika Mkoa huo katika ufunguzi wa Kituo cha Afya cha Ukongoroni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Kituo cha Afya cha Ukongoroni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala bora Haroun Ali Suleiman akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Kituo kipya cha Afya Ukongoroni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.kushoto yake ni Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Hassan Khatib Hassan

Baadhi ya waalikwa pamoja na wananchi waliohudhuria katika Ufunguzi wa Kituo cha Afya Ukongoroni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

DC GAIRO AAMURU KUKAMATWA VIONGOZI WALIOKULA FEDHA ZA UJENZI WA SEKONDARI YA KATA IDIBO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe ameagiza kukamatwa kwa viongozi wote waliofuja shilingi milioni 32 za ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata ya Idibo.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa shule hiyo lililokwenda sambamba na ugawaji wa mabati na vifaa mbali mbali kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Kituo cha Polisi Idibo.Mhe. Mchembe aliwaomba TAKUKURU kuwakamata viongozi wote wanaosimamia ujenzi wa shule ili waweze kuhojiwa matumizi ya pesa na wizi uliotokea tokea kuanza kwa ujenzi huo.

"Nimepokea taarifa ya Kamati ya Ujenzi ambayo imebaini wizi wa shilingi milioni 12 na matumizi ya utata yenye thamani ya shilingi milioni 20, hivyo ninawaagiza TAKUKURU na OCD ndani ya siku saba kuwakamata wale wote wanaohusika na sheria ichukue mkondo wake," alisema Mhe. Mchembe.

Aidha mpaka sasa japo kuna dosari Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata Idibo umemaliza madarasa 3, vyoo na jengo la utawala.Wakati huo huo Mhe. Mchembe alikabidhi msaada wa mabati 120 na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kupanua kituo cha Polisi Idibo kilichojengwa kwa nguvu za wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe (kushoto) akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita na OCD - Gairo, Mratibu Mwandamizi Jeshi la Polisi, Ramadhani Kitantu (kulia) wakati alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi Idibo, shule ya sekondari ya kata ya Idibo sambamba na ugawaji wa mabati na vifaa mbali mbali kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Kituo cha Polisi Idibo.
Ukaguzi wa Ujenzi shule ya Sekondari Kata ya Idibo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe (wa kwanza kulia) akabidhi msaada wa mabati 120 na vifaa mbalimbali kwa Jeshi la Polisi na uongozi wa kata ya Idibo kwa ajili ya kupaua kituo cha Polisi Idibo kilichojengwa kwa nguvu za wananchi. 

RC TELACK AFANYA ZIARA KUKAGUA KILIMO CHA PAMBA NA MTAMA WILAYANI KISHAPU

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack amefanya ziara ya kukagua kilimo cha zao la Pamba na Mtama wilayani Kishapu kwa ajili ya kuendelea kuhamasisha wakulima kulima mazao hayo kwa wingi kwa njia za kitaalamu ambayo yatawafanya wakue kiuchumi na mkoa kwa ujumla. 

Telack amefanya ziara hiyo leo Jumatatu Januari 8,2018 wilayani Kishapu kwa kukagua baadhi ya mashamba ya pamba na mtama ambayo yamelimwa na wakulima kwa njia ya kitaalamu na kuwataka wakulima kuendelea kutii magizo ya serikali kwa kulima mazao hayo ya biashara na chakula ambayo yatabadili mfumo wa maisha yao pamoja na kuacha kuishi kwenye nyumba za tembe.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara baada ya kutembelea mashamba ya wakulima katika kijiji na kata ya Shangihilu Telack amewataka wakulima kijijini kuendelea kujikita kulima mazao hayo ya pamba na mtama kwa njia ya kitaalamu ambayo itawafanya kupata mavuno mengi na kuinuka kiuchumi. 

“Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli imejipanga kumuinua mkulima kiuchumi kupitia kilimo na ndiyo maana changamoto zote zilizokuwa zikimkabili mkulima zinatatuliwa ili muweze kunufaika na kilimo chenu , hivyo nawasihi mlime mazao ya pamba na mtama kwa wingi kwani soko lake lipo”,alisema Telack. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack mwenye ushungi akiwa na mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Taraba (katikati mwenye nguo ya njano) na aliyepo mkono wa kushoto ni Diwani wa Kata ya Shangihilu Mohamed Hamadi pamoja na wataalamu wa kilimo na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Steven Magoiga wakikagua shamba la pamba hekali 22 la mkulima Kazimiri Masunga -Picha na Marco Maduhu- Malunde1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akiwa katika shamba la pamba na viongozi mbalimbali
Mkulima wa zao la Pamba Kazimiri Masunga akimuonyesha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack ukubwa wa eneo alilolima shamba hilo hekali 22, na kutarajia kwenye mavuno kumuinua kiuchumi huku akiomba serikali kuwapatia dawa ya kuua wadudu waharibifu ili wasipate hasara.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akiangalia wadudu wanavyolishambulia zao hilo la pamba na kutoa maagizo kuhusu ufumbuzi upatikane wa kuwateketeza kwa kupulizia dawa yenye nguvu ya kuua wadudu ili kutowapatia hasara wakulima.

WAZIRI MPINA AKAMATA KILO 65,600 ZA SAMAKI ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI MIA TATU

$
0
0
Mwandishi Maalum,Bukoba

Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina amekamata kilo 65600 za samaki wachanga aina ya Sangara waliokaushwa kwa chumvi wenye thamani ya shilingi milioni mia tatu katika Kisiwa cha Lubili wilayani Muleba kwenye Mkoa wa Kagera baada ya wamiliki wa samaki hao kukimbia.

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera, Mpina amesema tukio la kukamatwa kwa samaki hao lilifanikiwa baada ya yeye kupata taarifa kutoka kwa raia mwema ambapo aliagiza mamlaka za Wilaya ya Muleba kufuatilia kwa karibu hatimaye kuwakuta samaki hao wakiwa wameanikwa chini katika kisiwa hicho.

Waziri Mpina alisema Sheria ya Uvuvi namba 22 ya Mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 kifungu cha 90(1) inataka samaki wanaovuliwa waandaliwe katika mazingira yanayokidhi vigezo vya usalama kwa mlaji na kwamba ni kosa kisheria kuwavua au kuchakata samaki aina ya Sangara walio chini ya sentimeta 50 kwa kuwa ni wachanga na sentimita 25kwa Samaki aina ya Sato. Pia sentimita 85 kwa Sangara kwa kuwa ni wazazi wanaotakiwa kundelea kuzaa.

Aidha Waziri aliongeza kwamba Sheria hiyo imetoa mamlaka kwa watendaji wa Serikali kutaifisha mali zote zilitumika katika uvuvi haramu kupitia kifungu cha 37(a) (ii) na (iii) pamoja na Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu namba 29 ya mwaka 1994.
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (katikati )akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Bi Mwanaidi Mlolwa akitoa maelezo baada ya kushuhudia shehena ya samaki wachanga aina ya Sangara kilo 65600 mjini Bukoba waliokamatwa katika kisiwa cha Lubili wilayani Muleba leo.Mwenye koti ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu.
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (aliyenyanyua mikono ) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu (mwenye koti) leo, nje ya ghala la kuhifadhia samaki katika ofisi ya Uvuvi mjini Bukoba mara baada ya kushuhudia shehena ya samaki wachanga aina ya Sangara kilo 65600 waliokamatwa katika kisiwa cha Lubili wilayani Muleba.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu (aliyesimama) akisoma taarifa ya mkoa kuhusu sekta ya mifugo na Uvuvi kwa Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (alikaa kulia kwake) leo, mara baada ya kufanya ziara ya ghafla leo ili kushuhudia shehena ya samaki wachanga aina ya Sangara kilo 65600 waliokamatwa katika kisiwa cha Lubili wilayani Muleba. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi nchini, Mwanaidi Mlolwa.
Sehemu ya shehena ya samaki wachanga waliokaushwa kwa chumvi aina ya Sangara kilo 65600 waliokamatwa katika kisiwa cha Lubili wilayani Muleba, wakiwa wamehifadhiwa katika ghala kwenye ofisi ya Uvuvi jijini Bukoba. Samaki hao walikaatwa kufuatia raia mwema kutoa taarifa kwa Waziri Luhaga Mpina hivi karibuni.



MHASIBU HALMASHAURI YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA AJISHINDIA KITITA CHA SHILINGI MILIONI 50 ZA TATUMZUKA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Mh.Luckiness Amlima akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 50 mwishoni mwa wiki kwa Mkazi wa wilaya ya namtumbo mwenye umri wa miaka 31,ambaye ni Mhasibu msaidizi wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma,ndugu Jacob Ndee aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 50 .
Akielezea kwa furaha za kushinda kitita cha milioni 50 za mchezo huo wa kubahatisha wa TatuMzuka,Jacob alisema kuwa ndoto yake kubwa siku akipata fedha za kutosha atazitumia kwa Kilimo,Anasema kwa sasa anaona ndoto yake imetimia baada kupata fedha hizo,hivyo atazitumia katika kilimo.
 Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Mh.Luckiness Amlima akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa Kitita cha Milioni 50 cha TatuMzuka Ndugu Jacob Ndee pamoja na baadhi ya Wadau wengine,ambapo pia walionekana kuuufurahia ushindi wa Jacob,ambaye ni Mhasibu msaidizi wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma.

VOA SWAHILI: Mvua kubwa jijini Dar es salaam zaathiri shughuli za kichumi

Jikinge na Ugonjwa wa Kisukari

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 08.01.2018


WANANCHI MKOANI MBEYA WAZIDI KUJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA USAJILI LICHA YA MVUA KUNYESHA KATIKA MAENEO TOFAUTI

$
0
0
Licha ya Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Mbeya, Wananchi katika Kata na vijiji mbalimbali mkoani humo, wameendelea kuhamasika kujitokeza kwa wingi kusajili kupata Vitambulisho vya Taifa.
Katika Kata ya Ilemi amkusanyiko wa wananchi umekuwa mkubwa; ikidhihirisha ni kwa namna gani wananchi wamekuwa na uelewa mpana wa umuhimu wa Vitambulisho vya Taifa; hususani katika kipindi hiki ambacho zoezi kwa sasa linaendelea.

Afisa Usajili Wilaya ya Mbeya Bi. Alavuya Ntalima amesema katika Kata ya Ilemi zoezi limeanza Jumatano tarehe 3/01/2018 na linahusisha Kata za Iganzo, Isanga, Sisimba, Mabarini, Maendeleo pamoja na Forest.

Wakizungumzia zoezi la Usajili linaloendelea katika Kata zao Watendaji wa Serikali za vijiji wameahidi   kuendelea kushrikiana kwa karibu na Mamlaka kuhakikisha wananchi wote wanaoishi kwenye vijiji vyao na wenye sifa wana sajiliwa na kupata Vitambulisho vya Taifa ndani ya muda uliopangwa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wananchi wamepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) hususani hili la kuwatambua wananchi na kuwapatia Vitambulisho vya Taifa ambavyo vitawapa fursa ya kufanya mambo mengi na kutambulika katika shughuli mbalimbali za kijamii.  

 Afisa Usajili Mamlaka ya Vitambulsho vya Taifa Ndugu Lodrick Hawonga, akiwapatia wananchi wa Kata ya Ilemi huduma ya Usajili kwa kuwajazia fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa. 
 Baadhi ya Wananchi wa Vijiji mbalimbali kata ya Ilemi wakikamilisha usajili wa awali kwa kujaza fomu za maombi kwa wale ambao hawakuwa wamekamilisha zoezi hilo, kushoto ni Mjumbe wa kata hiyo Ndugu Martini Mpwani akiwasaidia kujaza barua za Utambulisho kwa wale waliokosa Viambatisho.

 Mtendaji wa kata ya Ilemi Ndugu Amiri Kassimu, akiwahakiki na kuwatambulisha Wananchi wake kwa kuwagongea Muhuri wa Serikali ya Mtaa ya Ilemi pamoja na kuwaandikia barua za utambulisho zitakazowawezesha kukamilisha hatua muhimu katika zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa ambalo linahusisha uchukuaji alama za Vidole,  Picha na  saini ya Kielktroniki 

 Wananchi wakiwa wamepanga foleni nje ya moja ya Kituo cha Usajili wakisuburi kupatiwa huduma hiyo licha ya Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya. 

Mmoja wa Wananchi waliojitokeza kupatiwa huduma ya Usajili katika kituo cha Usajili cha Mwamfute kata ya Ilemi akichukuliwa alama za Vidole katika zoezi la Usajili lililohusisha uchukuaji wa alama za kibailogia, saini ya Kielektroniki pamoja na Picha.

Jafo ataka Ukarabati wa Ruvu sekondari uwe wa haraka na Viwango

$
0
0
Na Nteghenjwa Hosseah, Kibaha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo amemtaka atakayepewa jukumu la ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Ruvu wilayani Kbaha mkoa wa Pwani wafanye kazi kwa kasi na haraka ili kuboresha mazingira ya shule hiyo. 
Jafo aliyasema hayo leo asubuhi katika shule ya sekondari Ruvu iliyopo mkoani pwani ambapo ni siku ya pili tokea shule  zianze kufunguliwa kwa mwaka huu 2018. Waziri Jafo alitumia siku ya kwanza ya tarehe 08 January ya kufunguliwa shule hapa nchini kwa kuongea na wanafunzi wa mkoa wa mbeya kupitia shule ya sekondari Ilomba iliyopo jiji la Mbeya.
Jafo amesisitiza kwamba Serikali imeamua kufanya ukarabati wa Shule zote kongwe hapa nchini kupitia TEA ili kutengeneza mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia. 
Amesisitiza kwamba Serikali inayo ongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuleta mapinduzi makubwa katika elimu hapa nchini.
Jafo amewaeleza wanafunzi na walimu wa Ruvu sekondari kwamba wakati wa zoezi la ukarabati atatumia muda mwingi kukagua ujenzi wa shule hiyo akiwa pamoja na mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Hamood Abuu Jumaa ili thamani ya fedha ipatikane.
Wanafunzi wa Ruvu sekondari walionyesha furaha kubwa kwa mipango ya Serikali juu ya shule yao kwani uchakavu wa miundombinu umekuwa ukiwaletea shida kubwa kutokana na maeneo mengi ya majengo yao kuvuja wakati wa Mvua.
 
Pia walimu na wanafunzi wa Shle hiyo wameahidi matokea mazuri zaidi katika mitihani inayokuja kwa kuzingatia mangira bora ya kujifunzia na kujisomea watakayokuwa wameyapata baada ya Ukarabati huo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selamani Jafo akikagua miundombinu ya Shule ya Sekondari ya Ruvu wakati alipotembelea shule hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selamani Jafo akikagua mambweni ya  Shule ya Sekondari ya Ruvu wakati alipotembelea shule hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selamani Jafo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ruvu wakati alipotembelea shule hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selamani Jafo  katika picha ya pamoja na walimu wa Shule ya Sekondari ya Ruvu wakati alipotembelea shule hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selamani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ruvu wakati alipotembelea shuleni hapo.

Katibu Mkuu atembele Kiwanda Cha Matrekta Na Kiwanda Cha Viua Dudu

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Elisante Ole Gabriel atembelea kiwanda cha Viua dudu kilichopo Tamco – Kibaha na kukutana na balozi wa Cuba nchini Tanzania Mhe. Lucas Domingo Hernandez Polledo.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Elisante Ole Gabriel, akiagana na na balozi wa Cuba nchini Tanzania Mhe. Lucas Domingo Hernandez Polledo.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa na balozi wa Cuba nchini Tanzania Mhe. Lucas Domingo Hernandez Polledo pamoja na uongozi wa Kiwanda cha Viua dudu Kibaha Mkoani Pwani.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Elisante Ole Gabriel akiendesha trekta la Kiwanda cha URSUS.

MBUNGE MGIMWA ATUMIA MAMILIONI UJENZI WA MADARASA YA SHULE ZA MSINGI, ZAHANATI NA NYUMBA ZA WAFANYAKAZI KATIKA KIJIJI KIBENGU

$
0
0
Na Fredy Mgunda,Mufindi Kaskazini. 

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Kibengu wametumia jumla ya shilingi milioni mia moja kumi na tisa na laki mbili (119,200,000) katika ujenzi wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kijiji hicho lengo likiwa katika kuboresha sekta ya elimu na afya kwa wananchi.

Akizungumza na wananchi katika kijiji hicho mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa alisema kuwa ameamua kuwekeza katika elimu na afya kwasababu wananchi wakifanikiwa kupata vitu hivyo viwili kwa wakati watafanya maendeleo kwa kasi kubwa kulingana na wakati uliopo na kuendana na mazingira wanayoishi.

“Hivi ndio vipaumbele vyangu kwa kijiji hiki kwa wakati huu maana nimegundua kuwa changamoto kubwa ni kuwa shule nyingi za msingi zilijengwa miaka mingi iliyopita sasa zimechakaa na sio rafiki kwa wanafunzi kuwasaidia kupata elimu bora hivyo nimeanza na hilo pamoja na kuchangia maendeleo kwa kuboresha sekta ya afya ili wananchi wakiugua waweze kutibia hapa hapa kijiji kwa kuwa nina uhakika huduma itakuwa inatolewa kwa ustadi mkubwa na yenye ubora unaotakiwa” alisema Mgimwa

Mgimwa alieleza kuwa pesa hiyo itatumika katika maeneo yafuatayo ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Kibengu utatumia gharama ya shilingi milioni thelathini (30,000,000) hadi kukamilika kwake,kuingiza umeme zahanati na kwenye nyumba za waganga imegarimu kiasi cha shilingi 1,200,000/=,ujimbaji wa kisima shilingi 2,00,000/=,ujenzi wa nyumba za walimu mbili kwa moja itagharimu kiasi cha shilingi 25,000,000/= na shule ya msingi Kibengu kutafanyika ujenzi wa madarasa matatu ambayo yatagharimu kiasi cha shilingi 21,000,000/=.
Mbunge wa jimbo la Mufindi KaskaziniMahamuod Mgimwa akitoa mfano wa kufanya kazi kwenye ujenzi wa vyumba vitatu vya shule ya msingi Kibengu ambako nako wananchi wamechangia nguvu zao
Katibu wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM wilaya ya Mufindi akiwa na katibu wa mbunge idara ya uhamasishaji na michezo Lwimbo nao wakijumika na wananchi katika ujenzi wa shule ya msingi Kibengu
Mbunge wa jimbo la Mufindi KaskaziniMahamuod Mgimwa akizungumza na viongozi katika eneo ambalo vyumba vitatu vya madarasa vinajengwa.

WAZIRI JAFO APONGEZA JITIHADA ZA MBUNGE WA MAKAMBAKO

$
0
0

Nteghenjwa Hosseah,Makambako.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amempongeza Mbunge wa Makambako Mhe. Deo Sanga kwa jitihada mbalimbali anazozifanya katika kuboresha Sekta ya Afya katika Jimbo hilo.

Jafo ameyasema hayo wakati alipotembelea Hospital ya Mji wa Makambako na kuona vyumba viwili vya Madaktari ambavyo vimejengwa na Mbunge Mhe. Sanga.

“Kwa dhati kabisa nimpongeze Mhe. Sanga kwa kujitoa kuboresha huduma za Jamiia hii inaonyesha nia yake njema katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa sabababu wananchi wakiwa na Afya Njema wataweza kuendelea na shughuli zao kikamilifu za kujitaftia kipato kisha kupata maendeleo” Alisema Jafo

Kwa kutambua Idadi kubwa ya watu wanaopata huduma katika Hospital hiyo ambayo ina miundombinu Duni ikiwa ni pamoja na ukosefu wa Jengo la kisasa la Kuhifadhia Maiti pamoja na Ukosefu wa wodi mbalimbali.Waziri Jafo amesema Serikali itaangalia jinsi ya kuboresha miundombuni hiyo ili wakazi wa Makambako waweze kupata huduma bora za Afya kama Watanzania wanazopata wengine.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Katikati) alipotembelea Hospital ya Mji wa Makambako.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe.Lucy Msafiri wakati wa ziara yake katika Hospital ya Mji wa Makambako.
Huu ndio Muonekano wa Hospital ya Makambako unavyoonekana kwa hivi sasa


DKT. NDUGULILE ASHIRIKI UJENZI KUAMSHA ARI YA WANANCHI KUCHANGIA SHUGHULI ZA MAENDELEO MKOANI KIGOMA

MWENYEKITI, WAJUMBE WA SERIKALI YA KIJIJI LAMADI WASIMAMISHWA KAZI KUPISHA UCHUNGUZI

$
0
0

Na StellaKalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amemsimamisha kazi kwa muda wa mwezi mmoja Mwenyekiti wa Kijiji cha Lamadi Wilayani Busega Mhe.Nzala Hezron pamoja na Wajumbe wa Serikali ya Kijiji hicho, ili kupisha uchunguzi kufuatia tuhuma mbalimbali zinazowakabili.

Uamuzi huo umekuja kufuatia malalamiko yaliyotolewa na wananchi wa Lamadi dhidi ya Mwenyeiti huyo kwa Mkuu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana Lamadi, kuhusu tuhuma mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za michango ya wananchi katika Ujenzi wa Shule ya Sekondari Lukungu pamoja na kutosoma mapato na matumizi ya fedha za michango mbalimbali ya wananchi.

“Ili tuweze kutenda haki ya uchunguzi na ukaguzi tumeona ni busara Mwenyekiti asiwe Ofisini na wajumbe wanaounda Serikali ya Kijiji wasiwe ofisini ili uchunguzi na ukaguzi wa akaunti uweze kufanyika kwa haki” alisema Mtaka.

Mtaka amesema Mkaguzi wa Ndani kutoka katika Ofisi yake atakayeshirikiana na Mkaguzi wa ndani wa Wilaya ya Busega kufanya ukaguzi katika Akaunti ya Shule kujua namna fedha zilizochangwa na wananchi na zilizotolewa na Halmashauri zilivyofanya kazi ya Ujenzi wa Vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika Shule ya Sekondari Lukungu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akizungumza na wananchi wa Kata ya Lamadi katika mkutano wa Hadhara uliofanyika Lamadi wiayani Busega.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Lamadi Wilayani Busega, Mhe. Nzala Hezron akizungumza na wananchi katika Mkutano wa Hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzitolea ufumbuzi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Boniventure Mushongi akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Lamadi wilayani Busega.



UTARATIBU WA KUSAJILI CHAMA CHA SIASA HUU HAPA.

$
0
0

Na  Bashir  Yakub.


Haki ya  kusajili  na  kuwa  na  chama  cha  siasa  ipo  kwa kila  mtanzania.  Hata  wewe  unaweza  kuwa  na  chama  cha  siasa  ikiwa  utataka  kufanya  hivyo.  Wako  wanaofikiri  kusajili  chama  siasa  ni  jambo  kubwa  mno. Laa  hasha  ni  jambo  la  kawaida    na  utaratibu  wa  usajili  si  mgumu  kama  wengi  wanavyodhani.


Tutaona  hapa  utaratibu  wa  kusajili  chama  cha  siasa.  Sheria  namba  5 ya  1992  Sheria ya  Vyama  vya  Siasa  na  kanuni  zake  za  mwaka  1992 ndizo  zinazoeleza  utaratibu utakaoelezwa  hapa  chini.


USAJILI  HUPITIA  HATUA  KUU  MBILI.


Kwa  mujibu  wa  kifungu  cha8( 1 ) cha  sheria  ya  vyama  vya  siasa  usajili  hupitia  katika  hatua  kuu  mbili.

Kwanza  usajili  wa  muda  na  pili  usajili  wa  kudumu.  Kwahiyo  ili  usajili  chama  cha  siasa  yakupasa  kupitia  hatua  hizi  mbili.


1.      USAJILI  WA  MUDA(PROVISIONAL REGISTRATION).      
  

Usajili  wa  muda  umeelezwa  katika kifungu  cha  9  cha  sheria  hiyo.  Usajili  wa  muda  maana  yake  chama  kitasajiliwa   na  kitaruhusiwa  kufanya  baadhi  ya  kazi  ila  usajili  huo  utakuwa  haujakamilika  mpaka  baada  ya  kutimiza  masharti, sifa  na  viwango  vilivyowekwa  na  sheria   ndani  ya  muda  maalum  ulioainishwa na sheria.  Usajili wa muda ndio  unaoanza  na  utaratibu  wake  ni huu ;

( a ) Andaa  katiba  ya  chama na  hakikisha  unakuwa  nayo. Mnajua  kila  chama  cha  siasa  huwa  na  katiba  yake, basi  hiyo  ndiyo  inayotakiwa hapa.

( b ) Hakikisha  mko  waanzilishi  wasiopungua  wawili.

( c ) Andaa  kanuni  za  chama. Kanuni  na  katiba  ni  tofauti. Kanuni  ndizo  zinazotafsiri  katiba kwahiyo  kanuni  hutokana  na  katiba.



                    KUSOMA  ZAIDI sheriayakub.blogspot.com

MAGAZETI YA JUMANNE LEO JANUARY 9,2018

LUKUVI ATATUA MIGOGORO YA ARDHI PAPO KWA HAPO KWA WAKAZI DAR

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameamua kukutana na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao wanamigogoro mbalimbali ya ardhi kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wake. 

Lukuvi ameamua kutumia siku tatu kuanzia leo hadi keshokutwa kushughulikia migogoro ya ardhi. Hivyo wananchi wenye migogoro ya ardhi wafike Katna Wizara ya Ardhi jijini Dar es Salaam ambako ndiko inafanyika mikutano hiyo. Ambapo ameahidi kusikikiza migogoro yote kwa wale watakaofika kwake. 

Wananchi mbalimbali wenye migogoro ya ardhi ikiwamo viwanja kuvamiwa, kuporwa,kuuzwa bila idhini na malalamiko ya hati kumilikiwa na zaidi ya mtu mmoja, Waziri Lukuvi ametumia nafasi hiyo kutatua mgogoro mmoja baada ya mwingine. 

Kwa leo jumla ya wakazi wa  Dar es  Salaam 250 wamejitokeza kutoa malalamiko yao ya migogoro ya ardhi na anaendelea kuisikiliza . Mmoja ya walitoa malalamiko yao ya mgogoro wa ardhi ni Mohammed Salmin ambaye amesema kuna kiwanja ambacho anayo nyaraka zake lakini kuna mtu mwingine naye anasema ni kiwanja chake na amepewa hati kinyemela. 

"Nimeenda kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kutoa malalamiko yangu lakini hakuna ambacho kimefanyika. Naomba Waziri unisaidie,"amesema. 

Akijibu hilo Waziri Lukuvi amesema kiwanja hicho kina utata kwani Salmin ameambiwa kiwanja kipo eneo la barabara, "Lakini maofisa ardhi wamempa mtu mwingine hati ya kiwanja hicho kinyemela na kuomba wasaidizi wake kulitafutia ufumbuzi,"amesema Waziri Lukuvi. 

Naye Elhau Medikenya amemwambia Waziri Lukuvi kuwa kuna kiwanja ambacho ni cha mama yake eneo la Tegeta kiwanja namba 279 na anayo hati yake  kimevamiwa.

Amesema mvamizi amejenga nyumba na hataki kutoka, hivyo ameomba waziri kusaidia. Akijibu malalamiko ameahidi kuwa atakwenda mwenyewe kusimamia uboaji wa nyumba ya mvamizi. "Kamwambie huyo ambaye amevamia kiwanja chako kuwa Waziri wa Ardhi atakuja kusimamia kuiboa hii nyumba. Mpe salamu hizo ajue kuwa nitakuja mwenyewe,"amesema Waziri Lukuvi.

Mkazi mwingine Yusufu Azalia amemwambia anacho kiwanja na hati Kinondoni jijini Dar  es Salaam lakini ameshanga imejengwa nyumba ya kifahari na hajui nani amejenga. 

Katika hilo Lukuvi amewaagiza maofisa wake kushughulikia kiwanja hicho ili mwenye hati halisi apewe kiwanja chake na nyumba iondolewe. Wapo baadhi ya wakazi hao wameelezea namna nguvu ya feeha inavyotumika kudhulumu wenye hati halali za viwanja kiasi cha wengine kukamatwa na kufungwa bila sababu za msingi zaidi ya nguvu ya  fedha kupindisha ukweli. 
 Waziri wa  Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi aliyeshika kipaza sauti akisikiliza kwa makini kero za migogoro ya ardhi kwa wakazi wa Dar es Salaam leo. 
Mmoja wa wakazi wa Dar es Salaam akitoa malalamiko yake ya ardhi leo jijini kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi.
 Sehemu ya wananchi wa Jiji la Dar  es Salaam wakisubiri kutoa kero zao kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  ambaye ameamua kuanzia Leo hadi keshokutwa kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi.
 Sehemu ya wananchi wa Jiji la Dar  es Salaam wakisubiri kutoa kero zao kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  ambaye ameamua kuanzia Leo hadi keshokutwa kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi. 

GIGY MONEY USO KWA USONA NA BASATA

SHAKA AWASILI SINGIDA LEO,KUMNADI MGOMBEA UBUNGE WA CCM SINGIDA KASKAZINI.

$
0
0
''Tutashinda na tutashinda kwa sababu mtaji wa ushindi tunao lengo ni lile lile kuhakikisha Singida kaskazini inaendelea kuwa ngome ya CCM''Alisema Shaka wakati akizungumza na Viongozi wa CCM Alipowasili katika ofisi za CCM Mkoa wa Singida leo.(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka (Kulia) Akipeana mkono na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Ndg:Peter Monko  Alipowasili katika Ofisi za CCM Mkoa wa Singida leo.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka akisain kitabu cha wageni  katika Ofisi za CCM Mkoa wa Singida (kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Ndg Juma Kilimba.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi  dkt. Denis Nyiraha akimkaribisha  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka alipowasili katika ofisi za CCM Mkoa wa Singida.
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images