Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110019 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI NISHATI AAGIZA UTEKELEZAJI REA III UANZE HARAKA

$
0
0
Serikali imeagiza utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) uanze mwezi huu wa Januari, 2018 sambamba na utekelezaji wa Mradi wa Densification ambao upo kwenye utekelezaji. Naibu Waziri Nishati, Subira Mgalu ametoa agizo hilo Januari 6, 2018 wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ambayo Mradi wa Umeme Vijijini unatekelezwa Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya.

Mgalu alizungumza na baadhi ya wananchi Wilayani humo ambao walimueleza kero mbalimbali zinazohusu masuala ya Nishati ya Umeme ambayo ni kukatika kwa umeme mara kwa mara bila taarifa, kucheleweshwa kuunganishwa na huduma ya umeme kwa ambao tayari wamelipia, baadhi ya Taasisi (shule, zahanati, vituo vya afya na visima vya maji) kurukwa wakati wa utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA II).
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) alipofanya ziara kwenye Bandari ya Itungi ya Wilayani Kyela ambayo ni moja ya maeneo yaliyonufaika na Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA II). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Claudia Kitta na kulia ni Saleh Songoro ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd inayojenga Meli ya Abiria kwenye Bandari hiyo.

Baada ya kuzungumza na wananchi hao kwa nyakati tofauti, akijibu kero zao, Naibu Waziri Mgalu aliagiza Mradi wa REA III uanze kutekelezwa ndani ya Mwezi huu wa januari, 2018 bila kuchelewa. “Utekelezaji wa Mradi wa Densification ambao unafanyika hivi sasa, uende sambamba na utekelezaji wa Mradi wa REA III kuanzia Mwezi huu wa Januari, 2018,” aliagiza Mgalu. 

Akizungumzia suala la kucheleweshwa kuunganishwa na huduma ya umeme kwa wananchi waliolipia, Mgalu aliliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha wateja wote waliolipia umeme wanaunganishwa mara moja bila kuwepo visingizio. “Tulikwisha agiza maombi yote ya wateja kuunganishiwa umeme yatekelezwe ndani ya Siku Saba baada ya kulipia,” alisema Naibu Waziri Mgalu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) akimsikiliza Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wilaya ya Kyela, Mhandisi Matei Mshana (kulia) alipofanya ziara kwenye Kituo cha Kuwashia na Kuzimia Umeme (Switch Yard) kilichopo katika Kata ya Nkuyu Wilayani humo.

Aidha, kuhusu suala la baadhi ya maeneo kurukwa hususan maeneo ya huduma za kijamii zikiwemo shule, zahanati, vituo vya afya na visima vya maji, Naibu Waziri Mgalu alisisitiza kwamba wakati wa utekelezaji wa Mradi huo wa REA III, maeneo hayo yapewe kipaumbele.

“Tunakiri utekelezaji wa REA II, ulikuwa na mapungufu ikiwemo ya kuruka baadhi ya maeneo, ninawahakikishia kasoro hii haitojirudia kwenye REA III,” alisema. Aliongeza kuwa TANESCO itoe taarifa mapema kwa Wananchi kama kutakuwa na ukataji wa umeme kutokana na sababu mbalimbali na kwamba iongeze ubunifu katika utekelezaji wa shughuli zake ikiwemo kuwafuata wateja na kufungua Vituo maeneo ya Vijijini ili kuwarahisishia wananchi wa maeneo hayo upatikanaji wa huduma.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akionyesha kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) kwa wananchi wa Kata ya Ibanda (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Wilayani Kyela. Kifaa hicho hutumiwa na wananchi wenye nyumba ya vyumba vichache ambao hawahitaji kufanya wiring.

Aidha, baadhi ya maeneo ulikopita Mradi wa Umeme Vijijini wa REA aliyotembelea Naibu Waziri Mgalu katika ziara hiyo Wilayani Kyela ni Bandari ya Itungi; Kata ya Kajunjumele; Kata ya Nkuyu; Kata ya Ibanda na Kata ya Kasumulu.

Bandari ya Itungi ni mnufaika wa Mradi wa REA II ambapo baadhi ya shughuli zake hutekelezwa kwa kutumia Nishati ya Umeme ikiwemo shughuli inayoendelea hivi sasa ya Uundaji wa Meli ya abiria inayofanywa na Mkandarasi ambaye ni Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Naibu Waziri Mgalu yupo Mkoani Mbeya kwa ajili ya ziara ya kukagua utekelezaji  Miradi ya Umeme Vijijini na Miradi mingine ya umeme Mkoani humo.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) akigawa vipeperushi kwa wananchi wa Kata ya Ibanda, Wilaya ya Kyela vya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) vyenye maelezo mbalimbali kuhusiana na huduma ya umeme ikiwemo suala la gharama ya kuunganishiwa umeme.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kata ya Ibanda (kulia) wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Wilayani Kyela.

Wingi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza wapelekea kuanzishwa shule mpya

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo ameishauri Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kuona namna ya kuanzisha shule mpya ili kuleta uwiano wa waalimu katika shule hizo unaoendana na idadi ya wanafunzi ambao wanatarajiwa kuongezeka kila mwaka mpya wa masomo. Ameyasema hayo aliposhiriki kwenye songambele ya ujenzi wa madarasa nane ya Shule ya Sekondari Kirando yanayotarajiwa kutumiwa na wanafunzi 422 waliofaulu kuingia kidato cha kwanza kwa mwaka 2018 katika shule hiyo inayobeba wanafunzi kutoka katika kata mbili zilizopo wilayani Nkasi.

“tunapoangalia kutatua changamoto ya shule hii ya Kirando tuangalie ufumbuzi wa kudumu zaidi, muangalie uwezekano wa kujenga shule nyingine, huo ndio utakuwa ufumbuzi, shule hii ina O – level na A – level, sasa kama kutakuwa na shule nyingine ya O – level peke yake na hii mkaipunguzia mzigo wa kuchukua wanafunzi wengi na walimu wengi katika shule moja”
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo akishiriki kwenye Songambele ya Ujenzi wa madarasa nane katika Shule ya Sekondari Kirando iliyopo Wilayani Nkasi kwaajili ya kutayarisha mazingira kwa wananfunzi 422 wa Kidato cha kwanza kuanza masomo yao Januari 2018.

Ametoa rai kuwa kwa eneo la ekari 60 linalomilikiwa na shule hiyo ya Sekondari Kirando inawezekana kugawa walau ekari 20 kwa shule hiyo mpya jambo litakalowapelekea kupewa waalimu wapya kwa shule mpya na kuleta uwiano wa waalimu kuliko hali ilivyo sasa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda aliyapokea maagizo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi kuanzia ngazi ya Kijiji hadi ngazi ya halmashauri ya Wilaya na kuongeza kuwa suala hilo litawekwa katika bajeti ya mwaka 2018/2019 na kuongeza kuwa wananfunzi wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza watasoma.
Mkuu wa Mkoa wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda (track ya bluu) akishiriki pamoja na wananchi wa kijiji cha Kirando kwenye Songambele ya Ujenzi wa madarasa nane katika Shule ya Sekondari Kirando iliyopo Wilayani Nkasi kwaajili ya kutayarisha mazingira kwa wananfunzi 422 wa Kidato cha kwanza kuanza masomo yao Januari 2018.

“wanafunzi waliofaulu kuingia kidato cha kwanza katika shule hii ya Kirando ni 422 na tumekubaliana kuwa hadi kufungua shule wananfunzi wote hao wanatakiwa wawe madarasani, lakini tumekubaliana na wazazi kuwa kama serikali tutanunua meza zote 422, lakini tumewahamasisha kuchangia walau mchango wa kiti ili mwanafunzi anapokuja akute meza na kiti ili tulimalize jambo hilo,”

Awali Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari kirando, Erneo Mgina akitoa taarifa fupi ya shule hiyo alisema kuwa shule ina wanafunzi 677 na kutaraji kupokea wanafunzi 422 na upungufu wa madara nane ambayo matatu tayari na mengine yapo katika hatua ya msingi na kutaraji kurekebisha vyumba vitatu vya maabara ili kuwahifadhi wanafunzi kwa muda hadi madarasa yatakapokamilika.

Hili limekuja ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI kuitaka mikoa iliyokuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018 ukiwemo mkoa wa Rukwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata madarasa ya kusomea, madawati na vyoo pale shule zitakapofunguliwa tarehe 8/1/2018.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo akitoa maelekezo ya kufanya kazi hiyo ya Songambele muda mfupi kabla ya kuanza kwa kazi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda (track ya bluu) akishiriki na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kirando kubeba jiwe kwaajili ya kuendeleza msingi wa madarasa matatu yanayoendelea kujengwa.
Baadhi wa wananchi wa kijiji cha Kirando wakisaidia kuweka kenchi kwenye moja ya madarasa yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji hicho kwaajili ya maandalizi ya watoto wao waliofaulu kuingia kidato cha kwanza kuanza masomo mwaka 2018 kupata sehemu za kusomea.

DKT. NDUGULILE AWASILI MKOANI KIGOMA KWA ZIARA YA SIKU MBILI YA KIKAZI

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile( katikati) akisalimiana na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Dkt Paul Chaote(kulia) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Kigoma kwa ajili ya ziara ya siku mbili ya kikazi kufuatilia utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na Wizara yakekatika ngazi ya Mikoa na Halmashauri. kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinisa, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akijadiliana jambo na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Dkt Paul Chaote(kulia) na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi(kushoto) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Kigoma kwa ajili ya ziara ya siku mbili ya kikazi kufuatilia utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na Wizara yake katika ngazi ya Mikoa na Halmashauri.

UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA SONGEA MJINI WAZIDI KUIMALIZA KAMBI YA UPINZANI

$
0
0
Moses Machali akimnadi Dkt Damas Ndumbaro
Na Nathan Mtega,  Songea

Wakati kampeni za kuelekea uchaguzi mdogo wa jimbo la Songea mjini mkoani Ruvuma zikiendelea katika kata mbalimbali za manisipaa ya Songea mkoani Ruvuma kwa ajili ya kumpata mbunge wa jimbo hilo ambaye chama cha mapinduzi kimemteua Dkt Damas Ndumbaro kupeperusha bendera ya chama hicho waliokuwa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani nchini wamezidi kujitokeza kwenye kampeni hizo na kutangaza kuachana na vyama vyao vya awali.

Miongoni mwa viongozi hao wa vyama vya upinzani ni pamoja na waliokuwa wajumbe watatu wa serikali ya mtaa wa Majengo mjini Songea kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo ambao walitangaza uamuzi huo wa kukihama chao hicho na kujiunga na chama cha Mapinduzi baada ya hotuba ya siku mbili mfululizo kwenye kampeni hizo za kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chama cha mapinduzi iliyotolewa na aliyewahi kuwa mwanachama wa chama na kingozi pia cha Demokrasia na maendeleo Moses Machali.

Katika hotuba yake ya kumnhadi mgombea huyo Machali alieleza sifa alizo nazo mgombea Dkt Damas Ndumbaro ambazo alizifahamu muda mrefu tangu akiwa kwenye kambi ya upinzani ambazo alisema hazina mashaka yoyote ya kumfanya asichaguliwe kuwa mwakilishi wa wananchi wa jimbo hilo na kuwataka wananchi wa jimbo la Songea mjini kwa ujumla kuitokeza kwa wingi siku ya Januari 13 mwaka huu kumpigia kura mgombea huyo na kuacha kuendelea kusikiliza na kufuata propaganda za wagombea wa vyama vya upinzani ambao walio wengi hawajui kilichoko kwenye vyama hivyo vya upinzani kwa sababu yeye alikuwepo huko na anajua kulivyo.

Viongozi wengine wa kambi ya upinzani waliopanda jukwaani katika viwanja vya mikutano vya Majengo na kutangaza kujiunga na chama cha mapinduzi ni pamoja na aliyekuwa katibu wa chama cha ACT Wazalendo mkoa wa Kigoma Sharon Msanya ambaye kabla ya kutangaza kujiunga na chama cha mapinduzi aliwataka wapiga kura wa jimbno la Songea mjini kutokuthubutu kulifanya jimbo hilo kuwa kambiya upinzani kwa sababu kufanya ni kurudisha nyuma jitihada za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo ambayo wameyahityaji kwa muda mrefu kurtoka serikalini na serikali ya awamu ya tano inaendelea kuonesha dhamira ya dhati kuwafikishia wananchi maendeleo hayo.

Alisema yeye amekuwa kiongozi mkubwa wa chama cha ACT Wazalendo katika ngazi ya mkoa lwa Kigoma akini amefikia uamuzi huo wa kusafiri kutoka mkoani Kigoma mpaka mjini Songea ili aweze kupata fursa ya kuwaeleza wananchi wa Songea umuhimu wa kukiunga mkono chama cha mapinduzi na mgombea wake Dkt Dams Ndumbaro kwa ajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla kwa sababu mgombea huyo amekuwa mpigania maendeleo ya taifa kwa muda mrefu hata kabla hajafikia uamuzi huo wa kugombea nafasi hiyo ya kuwawakilisha wananchi wa jimbo lake.

Huku naye Edna Sunga aliyekuwa katibu wa kamati ya maendeleo ya jamii taifa na mjumbe wa kamati kuu na halmashauri kuu taifa wa chama cha ACT Wazalendo akizungumza baada ya kukihama chama hico na kujijnga na chama cha mapinduzi amesema kwa sababu yeye ni muumini wa kuzingatia miiko na vita dhidi ya rushwa na kuwaletea maendeleo wananchi ameona hana sababu ya kuendelea kuwa kwenye upinzani badala ya kuongeza na kujnganisha nguvu ya kuwajhudumia wananchi walio wengi.

Amesema kiongozi au mwananchi yeyote mwenye dhamira ya dhati ya maendeleo ambayo wananchi walio wengi wanayahitajihana budi kukiunga mkopno chama cha mapinduzi na mgombea wake ambaye amevaa taswira ya chama hicho na taifa kwa ujumla huku naye mgombea wa jimbo hilo kwenye uchaguzi huo akiendelea kuwaomba wananchi wa mji wa Songea kujiktokeza kwa wingi siku hiyo ya uchaguzi kwa ajili ya kupiga kura kwa chama cha mapinduzi.

MKUBWA NA WANAWE PRESENTS TO YOU KISAMAKI | NEW VIDEO & AUDIO | NANENEPA

IGP SIRRO AONGOZA MAOFISA NA ASKARI SHEREHE ZA KUUKARIBISHA MWAKA 2018

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akiwaongoza Maofisa Wakuu Waandamizi na askari wa vyeo mbalimbali wa Jeshi hilo pamoja na wawakilishi kutoka vyombo vya usalama katika sherehe za kuuaga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018 iliyofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Dar es salaam, katika salam zake za mwaka mpya IGP Sirro, amewataka askari kufanya kazi kwa uzalendo kwa kulitetea taifa lao kwa kulinda usalama wa raia na mali zao.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akiwaongoza Maofisa Wakuu Waandamizi na askari wa vyeo mbalimbali wa Jeshi hilo pamoja na wawakilishi kutoka vyombo vya usalama katika tendo la kugongesheana glasi kama alama ya upendo wakati wa sherehe za kuuaga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018 iliyofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Dar es salaam, katika salam zake za mwaka mpya IGP Sirro, amewataka askari kufanya kazi kwa uzalendo kwa kulitetea taifa lao kwa kulinda usalama wa raia na mali zao.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro (kulia), akikata keki kwenye sherehe za kuuaga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018 iliyofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Dar es salaam, sherehe ambayo iliwakutanisha Maofisa Wakuu Waandamizi na askari wa vyeo mbalimbali wa Jeshi hilo pamoja na wawakilishi kutoka vyombo vya usalama.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro (wa pili kulia), akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu (IGP) Said Mwema (kulia), wakati akitoa neno mbele ya Maofisa Wakuu Waandamizi na askari wa vyeo mbalimbali wa Jeshi hilo pamoja na wawakilishi kutoka vyombo vya usalama wakati wa sherehe za kuuaga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018 iliyofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Dar es salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akifurahia jambo na baadhi ya askari wa Jeshi hilo wakati wa sherehe za kuuaga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018 iliyofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Dar es salaam, katika salam zake za mwaka mpya IGP Sirro, amewataka askari kufanya kazi kwa uzalendo kwa kulitetea taifa lao kwa kulinda usalama wa raia na mali zao.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akiongoza kucheza wa muziki wa dansi kwenye sherehe za kuuaga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018 iliyofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Dar es salaam. Picha na Jeshi la Polisi.

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA NAIBU WAZIRI WA MADINI MHE. DOTTO MASHAKA BITEKO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimmkabidhi nyenzo za kazi Mhe. Dotto Mashaka Biteko baada ya kumuapisha kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakimsikiliza Mhe. Dotto Mashaka Biteko akila kiapo cha Uadilifu cha Viongozi wa Umma baada ya kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUA KAMIMSHNA MPYA WA MADINI

$
0
0
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Shukrani Elisha Manya kuwa Kamishna wa Madini na pia kukaimu nafasi wa Msimamizi Mkuu wa Madini.

Rais ametangaza uteuzi huo leo Jumatatu Januari 8, 2018 alipokuwa akitoa hotuba fupi baada ya kumuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini.

“Nimesikia tatizo ni kamishna wa madini, sasa nimeamua kumteua kamishna mpya wa madini, jina lake linaanza na Prof. Shukrani Elisha, huyo atakuwa ndiye mtendaji na msimamizi mkuu wa madini.

“Mambo ya hovyo ni mengi mno, nilipotembelea bandarini niliunda katume kasirisiri hivi, kwa kulihusisha Jeshi la Wananchi, TISS na Polisi. Yanayogundulika huko ni ya ajabu, kuna hadi simenti za zamani sana, yapo makontena bandarini na pale Ubungo.

“Mimi sio mwanasiasa mzuri wa kubembelezabembeleza, nikitoka mimi mtapata wakubembeleza, ila mimi nataka kabla ya Ijumaa regulations (kanuni za sheria ya madini) ziwe zimesainiwa. Pro Kabudi nendeni mkazifanyie kazi, tafuta watu wa kukusaidia na mkamalize hayo,” alisema Magufuli.

TRA YAVUKA LENGO LA UKUSANYAJI WA KODI KATI YA JULAI NA DESEMBA 2017

NEWS ALERT: GAVANA WA SABA WA BENKI KUU YA TANZANIA, PROF. FLORENS LUOGA, AANZA KAZI RASMI

$
0
0
 Gavana wa saba wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Profes Florens Luoga akiwasili katika ofisi za BoT makao makuu jijini Dar es salaam leo tayari kuanza rasmi. Alipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji wa BoT, Bi Aziza Hamis (hayuko pichani)
Prof. Florens akizungumza katika mahojiano mafupi ofisini kwake mara baada ya kuanza rasmi kazi ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania

MATOKEO YA DARASA LA NNE NA KIDATO CHA PILI YATANGAZWA

$
0
0
BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba mwaka jana, huku idadi kubwa ya wanafunzi wakifaulu vizuri katika mitihani hiyo.

Akitangaza matokeo hayo leo Jumatatu, Januari 8, Katibu Mtendaji wa baraza hilo,  Dk Charles Msonde  (pichani) amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu  kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo.

Amesema  wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D wakati wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha.

Kuhusu matokea ya upimaji wa kidato cha pili, Dk Msonde  amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa  kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea  na kidato cha tatu.
Dk Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili  51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.

MVUA ILIVYOATHIRI BAADHI YA MAENEO JIJINI DAR ES SALAAM LEO

AMISI TAMBWE AREJEA JIJINI DAR KWA MATIBABU

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BAADA ya kushindwa kucheza katika michuano ya kombe la Mapinduzi kutokana na kuwa na Malaria, mshambuliaji wa kimataifa kutoka Burundi Amisi Tambwe  amereja Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi.

Tambwe  amepanda boti mchana huu visiwani Zanzibar kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.Daktari wa Yanga SC, Edward Bavu amesema Tambwe amelazimika kuondoka kambini mjini Zanzibar kurejea Dar es Salaam kwa  ajili ya matibabu zaidi ya Malaria.

“Ana Malaria, kwa siku zaidi ya nne sasa amekuwa na wakati mgumu, tumelazimika kumrejesha Dar es Salaam ili apatiwe matibabu zaidi,” amesema Dk. Bavu.

Tambwe anaondoka wakati Yanga leo inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar kuvaana  na Singida United  katika mchezo wa mwisho wa kundi B utakaoanza Saa 2:15 usiku.

Mrundi huyo amekuwa katika msimu mgumu, akianza kukaa nje tangu Agosti kutokana na maumivu ya goti kabla ya kurejea Desemba, lakini mapema Januari hii tena anaondolewa kambini kwa sababu ya Malaria.

Na hii inazidi kuipunguzia nguvu safu ya ushambuliaji ya Yanga kipindi hiki ambacho inawakosa wakali wake wengine wazoefu, Mzimbabwe Donald Ngoma na Mzambia, Obrey Chirwa. 
Yanga sasa itaendelea kumtegemea Ibrahim Ajib, Mateo Antony,Juma Mahadhi na Yohana Mkomola.

TRA yakusanya trioni 7.87 kwa kipindi cha miezi sita Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

$
0
0


Mamlaka ya Mapito nchini(TRA) imekusanya sh.Trioni 7.87 kwa kipindi cha miezi ya mwaka wa fedha 2017/2018 ikilinganishwa na sh.Trioni 7.27 kwa kipindi kama hicho katika mwaka wa Fedha 2016/2017 ambacho ni sawa na ukuaji wa asilimia 8.45.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo amesema katika miezi ya Desemba 2017 pekee TRA ilikusanya jumla ya sh.Trioni 1.66 ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha Desemba makusanyo yalikuwa sh.Trioni 1.41 ambacho ni sawa ukuaji wa asilimia 17.65.

Amesema watanzania waendelee kulipa kodi ili kuweza kupatikana kwa huduma mbalimbali za kijamii pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

Aidha amesema katika taarifa za mapato zinatolewa kila baada ya miezi mitatu hiyo ni kuwezesha wananchi kuwa taarifa za kodi ya nchi yao.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari juu ya ukusanyaji kodi kwa miezi sita ya 2017/2018 leo jijini Dar es Salaam.

MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI DESEMBA 2017 UMEPUNGUA NA KUFIKIA ASILIMIA 4.0-NBS

$
0
0

NA Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwenzi Desemba 2017 umepungua hadi kufikia asilimia 4.O ikilinganishwa na asilimia 4.4 ilivyokuwa mwezi Novemba 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Epharaim Kwesigabo amesema kupungua huko kumetokana na mfumuko wa bei wa mwezi Desemba 2017 ,na kumechangiwa na kupungua kwa bei kwa baadhi ya bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Desemba 2017 ikilinganishwa na bei za mwezi Desemba , 2016.

Amesema baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei huo ni unga wa muhogo kwa asilimia 1.9,Nyama asilimia 3.4, Samaki asilimia 15.1, Karanga asilimia 3.5 ,Mbogamboga asilimia 2.9, Njegere asilimia 7.5 , Viazi Mviringo asilimia 6.7.Mihogo Mibichi asilimia 16.8 pamoja na Viazi Vitamu asilimia 12.6.

Kwesigabo amesema mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaofanana na nchi nyingine Afrika Mashariki ambapo Kenya Mfumuko wa bei wa mwezi Desemba 2017 umepungua hadi asilimia 4.50 kutoka asilimia 4.73 mwezi Novemba 2017, Uganda Mfumuko wa bei wa mwezi Desemba 2017 umepungua hadi asilimia 3.3 kutoka asilimia 4.4 mwezi Novemba 2017.

Aidha amesema Mfumuko wa bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Kwesigabo amesema NBS ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa sheria ya kufanya uratibu upatikanaji wa takwimu rasmi.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Epharaim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari juu ya mfumuko wa bei wa Mwezi Desemba 2017 leo jijini Dar es Salaam.

RAIS DK.SHEIN AZUNGUMZA NA GAVANA WA BENKI YA TANZANIA ( BOT) ANAYEMALIZA MUDA WAKE PROFESA NDULU IKULU ZANZIBAR

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Gavana wa Benki ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu, alipofika Ikulu Zanzibar kumuaga rasmin kwa kumaliza muda wake wa Kazi BOT, hafla hiyo imefanyika leo IkuluZanzibar 8-1-2018
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na mgeni wake Gavana wa Benki ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu, wakitoka katika ukumbi baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Zanzibar kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa Kazi BOT
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Gavana wa Benki ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu na maofisa wa BOT aliofuatana nao .

Picha na Ikulu

WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAUNDA TIMU YA WATAALAMU 15 KUFUATILIA UTEKELEZAJI ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA KATIKA MIKOA 26 TANZANIA BARA

$
0
0
NA MWANAHAMISI MSANGI, WMVU 

WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imeunda timu ya wataalamu 15 iliyopo katika mikoa 26 ya Tanzania bara ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Mifugo) Dk. Maria Mashingo kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa mifugo yote nchini kabla ya kufika tarehe ya mwisho ya muda wa nyongeza wa Januari 31 mwaka huu. 

Timu hiyo ya wataalamu imeanza kutekeleza majukumu yake Januari 4 mwaka huu ambapo kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Maria Mashingo wilaya 30 ambazo bado hazijaanza zoezi la chapa na zimetiliwa mkazo katika ufuatiliaji ikiwemo Monduli, Kilwa, Liwale, Ruangwa, Mafia. 

Aidha, Wilaya nyingine ni Sikonge, Tabora, Urambo, Mwanza, Ilemela Manispaa, Magu, Ukerewe, Buchosa, Tarime, Kyerwa, Ngara, Newala, Newala Mjini, Tandahimba, Nanyamba, Mtwara, Mikindani Manispaa, Masasi, Masasi Mjini, Nanyumbu, Moshi DC, Hai, Same, Rombo, na Kigamboni. 

Dk. Mashingo amesema suala la upigaji chapa mifugo lipo kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa mifugo Namba 12 ya Mwaka 2010 ili kudhibiti magonjwa ya mifugo pamoja na wizi wa mifugo, kuimarisha usalama wa afya na mazao ya mifugo pamoja na kudhibiti usafirishaji na uhamaji holela wa mifugo. 

Amesema jumla ya ng’ombe millioni 19, 219,487 sawa na theluthi mbili ya ng’ombe wote milioni 28, 829,231 walioko nchini ambapo mpaka sasa jumla ya ng’ombe milioni 7, 701,661 sawa na asilimia 38.5 ndio wamepigwa chapa ambapo wamechangia kiasi cha shs. Bilioni 3, 700,830,500 kwa malipo ya Tsh 500 kwa kila ng’ombe.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Maria Mashingo akipiga chapa ng’ombe katika Kijiji cha Igalula Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu 15 ya Wizara hiyo walioko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatilia na kusimamia kikamilifu zoezi la upigaji chapa ambapo Dk Mashingo alisema mifugo itakayokuwa haijapigwa chapa hadi kufikia Januari 31 mwaka huu haijulikani Serikali nini kuhusu mifugo hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo) Dk. Maria Mashingo akiwaonesha wafugaji sehemu sahihi ambayo ng’ombe anatakiwa kupigwa chapa ili kuepuka kuharibu ngozi baada ya kushiriki zoezi la upigaji chapa katika Kijiji cha Igalula wilayani Tanganyika mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu 15 iliyoundwa na Wizara hiyo kufuatiliaji na kusimamia upigaji chapa kabla ya Januari 30 mwaka huu .


NIDHAMU YA KUAHIDI NA KUTEKELEZA, MATUMIZI SAHIHI VYAONGEZA KASI YA UTEKELEZAJI MIRADI

$
0
0
NIDHAMU mpya katika ukusanyaji na matumizi ya fedha za umma na dhamira ya dhati ya kutekeleza ahadi kubwa kwa faida ya wananchi vimesaidia Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kutekeleza kwa mafanikio miradi mbalimbali mikubwa ya kitaifa. Baadhi ya mambo yaliyotekelezwa na kufafanuliwa leo kwa wanahabari ni kama ifuatavyo: 

Hali ya Uchumi

Kama alivyoeleza Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango siku chache zilizopita, tunawahakikishia watanzania kuwa hali ya uchumi wa nchi yetu inaendelea kuwa imara kwa kiasi cha kuziridhisha taasisi mbalimbali za kimataifa.

Ripoti za Shirika la Fedha Duniani (IMF), Benki ya Dunia (WB) na Taasisi ya Goldman Sachs ya Marekani zimetabiri kuwa wakati uchumi wa dunia utakua kwa wastani wa asilimia 3.0 hadi 4.0, ukuaji wa uchumi wa Tanzania unatajwa kuendelea kuwa kati ya nchi tano bora za Afrika ukitarajiwa kukua kwa asilimia 6.5 hadi 7.0 katika mwaka 2018.

Ahadi ya Kuhamia Dodoma

Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuonesha nidhamu ya kuahidi na kutekeleza ahadi ya kuhamia makao makuu, Dodoma. Kufikia mwishoni mwa Desemba, 2017, viongozi waandamizi wa Serikali wameshahamia Dodoma. Rais mwenyewe akitarajiwa mwaka huu.

Mbali na viongozi, jumla ya wafanyakazi 3,671 kutoka wizara na taasisi mbalimbali za umma wameshahamia makao makuu Dodoma. Awamu inayofuata baadaye mwaka huu itahusisha wafanyakazi wengine 2,460. Sekta binafsi ichangamkie fursa za Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakati alipotoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kutolea ufafanuzi wa masuala kadhaa, Pichani kushoto  Mkurugenzi Msaidizi upande wa usajiri wa Magazeti Ndugu Patric Kipangula  na Kulia Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo, Rodney Thadeus 
Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari mapema leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO,alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli. Pichani kushoto ni  Mkurugenzi Msaidizi upande wa usajiri wa Magazeti Ndugu Patric Kipangula  na Kulia Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo, Rodney Thadeus .PICHA NA MICHUZI JR.



DKT. NDUGULILE ASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA KIJIJI CHA NYANGANGA KATIKA ZOEZI LA KUAMSHA ARI YA WANANCHI KUCHANGIA SHUGHULI ZA MAENDELEO MKOANI KIGOMA

$
0
0

Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) ameshiriki ujenzi wa Shule ya Kijiji cha Nyanganga iliyoko kata ya Kazuramimba, wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ikiwa ni jitihada za wananchi wa kijiji hicho kuharakisha upatikanaji wa huduma ya elimu kijijini hapo.

Akiwa katika Kijiji hicho Naibu Waziri Dkt. Ndugulile ameshiriki zoezi la kumimina zege kwa ajili ya kufunga ‘rental’ ya vyumba vya madarasa ya shule hiyo.

Dkt. Ndugulile amesema lengo la kuwepo ziara hiyo ni kufuatilia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii (1996), na Sera nyingine za Wizara amabzo zinasisitiza ushiriki wa jamii katika kuibua mahitaji, kupanga, kuamua, kutekeleza, kufuatilia na utathmini shughuli za miradi ya maendeleo ikiwemo uboreshaji wa huduma ya miundo mbinu ya kufundishia na kujifunzia katika maeneo ya mijini na vijijini.

Mhe. Ndugulile ameongeza kuwa Ili kurejesha ari ya wananchi kushiriki katika maendeleo yao kuelekea uchumi wa kati na wa viwanda, Wizara imeamua kufuatilia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi za Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuhamasisha jamii kushiriki na kuchangia shughuli za maendeleo yao kwa kufanya kazi za bega kwa bega, kuchangia nguvu zao, rasilimali fedha, rasilimali vifaa na ufundi kwenye utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundo ya elimu, afya, kilimo, mifugo, barabara na viwanda vidogo vidogo. 

“Nimeambiwa kuwa mradi wenu wa ujenzi wa shule ya sekondari katika kijiji cha Nyanganga utasaidia kusogeza huduma ya elimu jirani na wananchi, na nimevutiwa na hamasa mliyonayo katika maendeleo name nimekuja kushirikiana nanyi kuendeleza ujenzi wa madarasa ya shule kazi amabyo ni kigezo thabiti cha cha dhamira ya dhati yawananachi wa kijiji hiki katika kutoa haki ya msingi ya kumwendeleza Mtoto katika ngazi ya kijiji na jamii kwa ujumla” alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akishirikiana na wananchi wa Kijiji cha Nyanganga kuchanganya zege kwa ajili ya kuweka ‘rental’ kwa ajili ya madarasa manne ya Shule ya Kijiji hicho katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi kujitolea katika kufanya shughuli za maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akikabidhi mifuko 37 ya Saruji kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za wananchi wa Kijiji cha Nyanganga wa kujitolea kwa nguvu zao kujenga shule ya Sekondari ya Kijiji chao.
Baadhi ya wananchi wakifanya kazi ya kumwaga ‘rental’ katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kijiji cha Nyanganga kilichopo Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.


WATENDAJI WA SERIKALI TIMIZENI WAJIBU WENU-DKT.ABBAS

$
0
0

Said Mwishehe, Blogu ya jamii

SERIKALI imewataka watendaji na watumishi wa umma kuhakikisha wanakwenda na dhamira ya Rais, Dk.John Magufuli ya Hapa Kazi Tu, kinyume na hapo watachukuliwa hatua za kiutendaji.

Hayo yamesemwa leo, Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi wakati akifafanua mambo mbalimbali yanayoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kwa maslahi ya Watanzania wote.

Dk.Abbas amesema ni vema watendaji wa Serikali wakaenda sawa na dhamira ya Rais ya Hapa Kazi Tu, hivyo lazima wafanye kwa bidii na kufafanua kila mtendaji wa umma ajitafakari namna ya utendaji kazi wake kama unaendana na kasi ya Rais.

“Watendaji wa umma wajitafakari kuhusu kazi wanazofanya kama zinaenda na dhana ya Rais wetu ya Hapa Kazi Tu.Watendaji watimize majukumu yao na kufuatilia kila jambo kwani wasipofanya hivyo wapo watakaowafuatilia.

“Kuna mabadiliko makubwa ya kiutendaji kwa Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo lazima twende nayo.Tuhakikishe tunafanya kazi ili kufanikisha maendeleo ya Watanzania,”amesema

Dkt.Abbas ameamua kueleza hayo baada ya kuulizaa bado wapo watendaji ambao hawaendani na dhamira ya Rais ya Hapa Kazi Tu, Je wanawafanya nini watendaji kama hao.Wakati huohuo Dkt.Abbas ameendelea kuviomba vyombo vya habari kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia taaluma ya habari inavyotaka.

Amesema yeye kama mlezi wa vyombo vya habari nchini anayo nafasi ya kuendelea kushauri waandishi wa habari nchini kufanya kazi yao kwa kuzingatia misingi ya taaluma ikiwa pamoja na kuandika habari sahihi na iliyokamilika.Amefafanua njia pekee ya kuwa salama kwa vyombo vya habari ni kuandika ukweli badala ya kuandika mambo ya kuzusha au kuandika uongo kwani madhara yake ni makubwa.

”Binafsi kama mlezi wa vyombo vya habari lazima nikumbushe yale ambayo najua ni muhimu kuyazingatia.Pale ambapo kuna chombo kitakosea lazima tukiite na kukionya na tunafanya hivyo zaidi ya mara moja.
Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakati alipotoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kutolea ufafanuzi wa masuala kadhaa, Pichani kushoto  Mkurugenzi Msaidizi upande wa usajiri wa Magazeti Ndugu Patric Kipangula  na Kulia Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo, Rodney Thadeus .PICHA NA MICHUZI JR.
Viewing all 110019 articles
Browse latest View live




Latest Images