Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 09.01.2018


NAIBU SPIKA ATEMBELEA BOHARI YA DAWA (MSD)

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu, akizungumza na Naibu Spika, Tulia Akson alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja kutembelea MSD kuona shughuli mbalimbali za uhifadhi dawa na Vifaa tiba jijini Dar es Salaam jana.
Hapa Naibu Spika, Tulia Akson akitembelea ghara la kuhifadhi dawa na vifaa tiba.
Naibu Spika akipata maelezo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu, akiagana na Naibu Spika, Tulia Akson baada ya kumaliza ziara hiyo ya kikazi.

NAPE AFUNGUKA AKIMNADI DK. NDUMBARO ADAI KAMWE HATA IHAMA CCM

$
0
0
Na Gideon Mwakanosya-Songea

MBUNGE wa jimbo la Mtama mkoa wa Lindi Nape Nnauye amefunguka kwa kudai kuwa hawezi kukihama chama cha mapinduzi (CCM) kama baadhi ya watu wakiwemo wa vyama vya upinzani kwa kile alichodai kuwa magari ya upinzani yanaenda kuzama na hayajulikani yataibuka lini.

Uwazi huo ameuweka jana wakati akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Songea mjini mkoani Ruvuma kwa tiketi ya CCM Dk, Damas Ndumbaro kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya bombambili Manispaa ya Songea.

Nnauye ambaye aliwahi kuwa katibu wa hitikadi na uenezi CCM taifa na Waziri wa Habari, Michezo na Sanaa katika serikali ya awamu ya tano alisema kuwa kama kuna watu walidhani atakihama chama cha mapinduzi (CCM) na kwenda upinzani wasahau kabisa .

Akizungumza kwa kujiamini huku akishangiliwa na mamia ya wakazi wa bombambili alisema kuwa kama kuna kuwa na matatizo ndani ya CCM tunaonyana ndani ya chama na kuyamaliza na siyo kuhama chama.
“Naikubali serikali ya awamu ya tano inayongonzwa na jemedali Dk. John Magufuli pamoja na makamu wa Rais na waziri mkuu wake kuwa ipo imara na mimi naapa kufia CCM na siyo vinginevyo” alisema Nape Nnauye.

“Nasikia maneno maneno kutoka kwa baadhi ya watu wakisema Nape anataka kuhamia upinzani jambo ambalo siyo la kweli kuanzia leo watu hao waondokane na mawazo hayo” alisema mbunge wa Mtama Nape Nnauye.
Katika kampeni hizo ambazo uchaguzi wake utafanyika Januari 13 mwaka huu Nape Nnauye na Moses Machali aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Kasulu mkoa wa Kigoma kwa tiketi ya NCCR Mageuzi wamekuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa jimbo la Songea hasa wanapokuwa majukwani.

Walinda amani kutoka Tanzania kuongoza operesheni milimani Sudan

DKT MASHINGO AHIMIZA NG'OMBE WENYE UMRI WA MIEZI SITA NA KUENDELEA KUPIGWA CHAPA

$
0
0
Na Kumbuka Ndatta, KASULU

KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo) Dk. Maria Mashingo ameagiza ng’ombe wote wenye umri wa kuanzia miezi sita na kuendelea kuhakikisha wamepigwa chapa kabla ya kufikia tarehe ya mwisho ya upigaji chapa Januari 31 mwaka huu, kwani zoezi hilo sio la hiari bali ni la lazima na linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria.

Dk. Mashingo ametoa kauli hiyo wakati akishiriki zoezi la upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu wa Wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka huu. 

Dk Mashingo aliwaambia wafugaji hao kutambua kuwa zoezi hilo linasimamiwa kwa mujibu wa Sheria ya utambuzi ,usajili na ufuatiliaji wa mifugo Na. 12 ya Mwaka 2010 na kuwasititiza kuwa haijulikani Serikali itaamua nini kwa mifugo itakayokuwa haijapigwa chapa hadi kufikia tarehe ya mwisho iliyowekwa ya Januari 31 mwaka huu.

Aidha Dk. Mashingo alitumia fursa hiyo kuwaelimisha wafugaji sehemu maalum ambayo ng’ombe anapotakiwa kupigwa chapa mwilini mwake ili kutoharibu ngozi yake inayotegemewa kwa matumizi mengine.
KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo akishiriki upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu wa wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka huu.
KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo akiwaeleza na wafugaji wa Kijiji cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma umuhimu wa zoezi la kupiga chapa ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu wa wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka huu.
KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo akishiriki upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu wa wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka huu. 

WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WA HALIMASHAURI YA WILAYA YA NYASA KUMALIZA TOFAUTI ZAO

$
0
0
Waziri mkuu wa Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania KASSIM MAJALIWA, amewaagiza viongozi wa halimashauri ya NYASA akiwemo mbunge wa jimbo hilo, mkuu wa wilaya na mkurugenzi, kumaliza tofauti zao na madala yake wawaletee wananchi maendeleo. Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza na watumishi na wakuu wa idara mbalimbali wa halimashauri ya wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

VOA SWAHILI: VURUMAI CONGO DRC

LUBINGA AMNADI MGOMBEA WA CCM JIMBOLA SINGIDA KASKAZINI LEO.

$
0
0
Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (kushoto) akimnadi mgombea wa Ubunge jimbo la Singida Kaskazini ndg:Justine Monko (kulia) wakati wa mkutano wa Hadhara uliofanyika kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida Kaskazini Mkoani Singida.
Mgombea Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini Ndg:Justine Monko akijinadi katika mkutano wa Hadhara uliofanyika kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida Kaskazini Mkoani Singida.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini  Bi Grace Shindika Akizungumza katika mkutano wa Hadhara uliofanyika kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida Kaskazini Mkoani Singida
.Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (katikati) akizungumza na Mgombea Ubunge Jimbo ;la Singida Kaskazini ndg: justine Monko (kwanza kushoto) pampoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Ndg:Juma Kilimba.

 (PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


GIGY MONEY UJANJA MFUKONI....

DK.KIGWANGALLA ATEUA KAMATI BONDE LA MTO KILOMBERO

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) ameteua Kamati maalum ambayo itaishahuri Serikali namna ya nini kifanyike katika kushughulikia athari za bonde la Kilombero lililopo Mkoani Morogoro.

Waziri Dk Kigwangalla amebainisha kuwa Kamati hiyo aliyoiteua, ndio itamshahuri juu ya bonde hilo litasimamiwa vipi pamoja na namna bora ya hatua za kuchukua ili kulinda bonde hilo ambalo lina mahitaji makubwa ikiwemo chanzo kikubwa cha maji yanayotengeneza Stiegler’s Gorge ambako Serikali imeamua kuweka mikakati ya utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme unaotarajiwa kufikia megawatts 2100 huku pia bonde hilo likiwa na utajiri wa kuwepo na aina zaidi ya 400 ya ndege pamoja na mnyama anaina ya Puku ama Sheshe ambaye hapatiani duniani kote zaidi ya Tanzania pekee.

"Hii ndio Kamati yangu, itakayonishahuri juu ya bonde ili litasimamiwa vipi. Hii ndio Kamati ambayo itanishahuri mimi na kwamaana hiyo Serikali kwa ujumla wake juu ya namna bora ya uhifadhi hususani katika eneo lile la Pori tengefu.
Waziri wa Maliasili na Utali Dkt Hamis Kigwangalla.


KATIBU MKUU KATIBA NA SHERIA AFANYA ZIARA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome (kulia), akiweka saini kwenye kitabu cha wageni alipowasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa ziara ya kikazi ili kuona namna Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi (Forensic Bureau) inavyofanyakazi zake pamoja kujadiliana namna yakuimarisha eneo la utoaji Haki Jinai pamoja na ubadilishanaji wa taarifa, anayefuatia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, pamoja na Maofisa wa Jeshi hilo wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome (katikati), akitoa neno wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo ili kuona namna Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi (Forensic Bureau) inavyofanyakazi zake pamoja kujadiliana namna yakuimarisha eneo la utoaji Haki Jinai pamoja na ubadilishanaji wa taarifa.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome (kushoto), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro (wa pili kulia) na Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele (kulia) wakiteta jambo wakati walipokuwa kwenye moja ya ofisi ya Uchunguzi wa Kisayansi (Forensic Bureau) Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jana, ili kuona namna Kamisheni hiyo inavyofanyakazi zake.

Picha na Jeshi la Polisi.

GLOBAL TV: MAZISHI YA MCHEZAJI WA ZAMANI WA YANGA

TFC YAPAKIA TANI 200 ZA MBOLEA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS DK. JOHN MAGUFULI

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

KUFUATIA agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli, kwa Wizara ya Kilimo, kuhakikisha ndani ya siku saba kumaliza malalamiko ya mahitaji ya mbolea kwa mikoa ya Katavi na Rukwa, Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC) imeanza mara moja kuteleleza agizo hilo.

Waandishi wa Habari jana na leo wameshuhudia watendaji wa TFC wakihaha kutafuta magari ya kukodi kwa ajili ya kusafirisha mbolea kuipeleka mkoani Rukwa na Katavi, ambapo zaidi ya tani 600 zimeanza kusafirishwa kuanzia juzi siku ya agizo hilo.

Akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TFC, Salum Mkumba, alisema mara baada ya taarifa ya Ikulu juzi, waliamua kuanza kupakia mbolea hiyo, kwa kutumia magari makubwa (malori) ya kukodi pamoja na magari makubwa ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

“Kwa sasa sisi TFC hatuna akiba ya mbolea, lakini hawa wenzetu wa Primium Agro Limited, wanayo akiba ya kutosha, hivyo tunachukua kwao kwa makubaliano maalum,” alisema Mkumba.




Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC), Salum Mkumba (kushoto), akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Premium Agro Chem Limited inayosambaza mbolea alipofanya ziara ya kikazi ya siku mbili jana na leo jijini Dar es Salaam kujionea zoezi la kusafirisha mbolea kwenda mikoani. Kutoka kulia ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Brijesh Barot, Mkurugenzi Mtendaji, Sagar Shah na Oparesheni Meneja, Rhoda Mwita.
Wafanyakazi wa kampuni hiyo na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakipakia mbolea hiyo kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda mikoani.
Malori ya JWTZ yakiwa katika foleni ya kupakia mbolea hiyo.
Shehena ya mbolea hiyo ambayo inasafirishwa kwenda mikoani kwa wakulima.

UTAMU WA BAISKELI KWA KINAMAMA WILAYANI KYELA

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AZINDUWA SOKO LA KISASA KINYASINI MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

$
0
0
 Soko la Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ikiwa ni Shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 WANANCHI wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Soko la Kisasa la Kinyasini Unguja
 JENGO Ljipya la Soko la Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ikiwa ni Shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Soko Jipya la Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja kulia Waziri wa Kilimo Mifungo Maliasili na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid Mohamed na kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu Bunge Kazi Ajira Vijana na Wenye Ulemavu. Mhe. Jenista Mhagama
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi la Soko Jipya la Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkandarasi wa Ujenzi wa Soko hilo Ali Mbarouk, akitowa maelezo wakati wa uzinduzi wake kutembelea jengo hilo.




Jiji la Dar es Salaam kupokea Tuzo ya huduma bora ya Usafiri endelevu

$
0
0

Na Nteghenjwa Hosseah, Dar es Salaam.

Jiji la Dar es Salaam limechaguliwa kupata tuzo ya huduma bora ya Usafiri endelevu barani Afrika kufuatia Mradi wake wa mabasi yaendayo haraka (DART) ambao kwa kiasi kikubwa umeleta mabadiliko katika kutatua changamoto ya msongamano wa Magari uliokuwa ukiikabili Jiji la Dar es Salaam.
Akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa Habari Waziri mwenye dhamana na Mamlaka ya Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amesema Jiji hili la Dar es salaam litapokea tuzo mapema leo tar 09 jan 2018 katika hafla itakayofanyika huko Nchini Marekani katika Jiji la Washington Dc kufuatia utoaji wa huduma huduma hiyo bora ya Usafiri.
“Huduma ya Usafiri katika awamu hii ya kwanza imeonyesha mafanikio makubwa kufuatia uwezo wa kupunguza muda wa kusafiri kwa wananchi kutoka masaa matatu waliyokua wanatumia hapo awali hadi kufikia kutumia dakika 40 kwa watumiaji wa Mabasi haya kutoka Kimara hadi eneo la Katikati ya Jiji la Dar es salaam” Alisema Jafo.

Jafo aliongeza kuwa Tangu kaunzishwa kwa Mradi huu wa Mabasi yaendeyo Haraka(DART) umetoa ajira kwa watanzania kwani zaidi ya watumishi 967 wamepata fursa za kutumikia Taasisi hii hivyo ni fursa pia ya kiuchumi kwa watanzania.
Zaidi hapo Mradi huu huathiri Mazingira kwani Injini zinazotumiwa na mabasi yaendayo haraka kutokuwa na athari kwenye mazingira, Mabasi haya hayotoa Moshi wala kusababisha kelele katika ya Mji hivyo mradi kuwa rafiki kwa  mazingira alisisitiza Jafo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mabasi yanedayo haraka Victor Ndonne akizungumza katika kikao na waandishi wa habari alisema Ujumbe kutoka Tanzania katika halfa ya Upokeaji wa Tuzo hiyo Nchini Marekani unaongozwa na Balozi wa Tanzania katika Nchi za Marekani na Mexico Balozi Wilson Masiling ambaye ameambatana na Naibu Katibu Mkuu(E) kutoka OR-TAMISEMI Bw.Tixon Nzunda, Mwenyekiti wa Bodi ya DART pamoja na Mtendaji Mkuu wa DART.
Mradi wa abasi yaendayo Haraka unatekelezwa katika awamu sita ambapo ujenzi wa miundombinu katika awamu ya Pili ya Mradi katika Barabara ya Kilwa inataraji kuanza mapema mwaka huu.
Hii ni Tuzo ya pili kupokelewa na Wakala wa Mabasi yendayo haraka ambapo hivi  karibuni Taasisi ya C40 YA Marekani iliipa Jiji la Dar es salaam Tuzo ya Usafirishaji endelevu pamoja na Jiji la Newyork ka Marekani.

MTOTO AZUWA GUMZO MITANDAONI, RUBY ASEMA NANDY HAMUWEZI...

SOKO LA SAMAKI MKOA WA LINDI

$
0
0

 Wajasirimali katika Soko kuu la samaki la mkoa wa Lindi wakitayarisha Samaki kwa lengo la kuwauza kwa wateja watakaofika sokoni hapo.
Wajasiliamali katika soko kuu la mkoa wa Lindi wakipanga samaki tayari kwa kuwauza kwa wateja sokoni hapo.
 Wavuvi wakiwa katika jahazi wakiandaa samaki ambao wamewavua kwa ajili ya kuwauza katika soko kuu la samaki la mkoa wa Lindi.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jambii Lindi.
Chombo kikiandaliwa 

Dkt. Abbas Ahamasisha Wanahabari Kushiriki Tuzo za SADC

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amewahamasisha Waandishi wa Habari wa Tanzania kushiriki vema katika kuwania tuzo za wanahabari wa Jumuiya za Mendeleo Kusini mwa Bara la Africa (SADC).

Dkt. Abbas ametoa rai kwa Waandishi wa Habari kushiriki tuzo hizo jumatatu wiki hii wakati akiongea na waandishi wa Habari kuhusu hali ya uchumi na utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyopo nchini. “Tunawaomba wale wote ambao wanadhani wanavigezo basi washiriki tuzo hizi za umahiri ambazo zinahusu waandishi wa habari za magazeti, redio, televisheni na wapiga picha za habari”, alieleza Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali.

Alieleza kuwa maelezo kamili juu ya tuzo hizo yanapatikana katika tovuti ya Idara ya Habari ya www.maelezo.go.tz hivyo wote wenye habari mahiri katika magazeti, vipindi vizuri vya luninga au wapiga picha wahakikishe wanashiriki ili kushindana na waandishi wenzao kutoka nchi za kusini mwa Afrika.

Mbali na tuzo za SADC, Dkt. Abbas pia ameeleza kuwa tuzo nyingine ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inashindaniwa na Wanahabari na maelezo yake yanapatikana katika tovuti ya Idara ya Habari.

Amewataka wanahabari kuandika habari zao kwa umahiri mkubwa ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kukidhi hata kupata tuzo za waandishi bora kama hizo zilizojitokeza. Pamoja na kuwataka waandishi wa habari kushiriki katika tuzo hizo, pia amewataka waandihsi hao kuhakikisha wanapata vitambulisho vipya ya Waandishi wa Habari (Press Cards) vya mwaka 2018 baada ya vile vya mwaka jana kuisha muda wake.

“Kwa kweli mwaka huu tutakuwa wakali kidogo kwa wale ambao hawatokuwa na vitambulisho hivi kwani mchakato wa kuvipata ni rahisi kwa sababu tumeshawapa muda wa miaka mitano wa kwenda kusoma hivyo hatuhitaji vyeti, kinachohitajika ni barua ya mwajiri au chombo cha habari unachofanyia kazi tu.” Alisema Dkt. Abbas.

Aidha, Dkt. Abbas amewakumbusha wanahabari ambao bado kiwango chao cha elimu kipo chini ya kile kilichowekwa katika Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2016 na Kanuni zake za mwaka 2017 kujiendeleza kwani muda uliotolewa wa miaka mitano unaendelea unazidi kuisha.

VIDEO: DKT. NDUGULILE AITAMBULISHA PROGRAMU YA KIKUNDI MLEZI KWA WANAWAKE WAJASILIAMALI MKOANI KIGOMA

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images