Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AMESHIRIKI IBADA YA FAMILIA TAKATIFU KATIKA KANISA LA MTAKATIFU PETRO JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na waumini wengine wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay wakishiriki Ibada ya jumapili ya Familia Takatifu katika Kanisa hilo la jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru mara baada ya kushiriki Sakramenti Takatifu katika Ibada ya Jumapili ya Familia Takatifu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitakiana Heri na Masista walioshiriki katika Ibada ya jumapili ya Familia Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Fr. Asis Mendokta mara baada ya Ibada ya jumapili ya Familia Takatifu katika Kanisa hilo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waumini wa Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam mara baada ya Ibada ya jumapili ya Familia Takatifu katika Kanisa hilo jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

WATALII WA NJE NA NDANI WAENDELEA KUMIMINIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

$
0
0
Idadi ya watalii wanaotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Senapa) imeongezeka katika siku za hivi karibuni kutokana na sekta ya utalii kukua huku miundombinu ya barabara na viwanja vidogo vya ndege vilivyopo ndani ya hifadhi hiyo kufanya kazi vizuri.

Afisa Utalii wa Senapa,Evance Magomba alisema kuwa
baada ya kujengwa jengo dogo la wageni wanaowasili na wanaoondoka katika uwanja mdogo wa ndege wa Seronera idadi ya wageni imeongezeka huku wakala wa makampuni ya ndege wakiweka wawakilishi wao katika uwanja huo.

Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa katika kipindi cha
Januari hadi Septemba mwaka huu kumekua na safari za ndege 3,724 katika uwanja  wa Seronera huku uwanja wa Lobo katika kipindi hicho ni safari 349 na uwanja wa Kogatende safari 564.

Alisema ndani ya hifadhi hiyo kuna viwanja vidogo vya ndege saba kikiwemo cha Seronera ambacho ni kikubwa zaidi chenye uwezo wa kupokea ndege
kubwa yenye uwezo wa kubeba abiria 60 ikiwemo ya shirika la Precision
Air inayofanya kazi mara nne kwa wiki.

“Miaka miwili iliyopita hatukua na jengo hili la abiria naamini pamoja na sababu nyingine limekua kishawishi  kwa wageni kuongezeka kwani linawawezesha kuwa na sehemu nzuri ya kupumzika kabla ya kuanza safari zao,”alisema Magomba
Watalii wakiwasili uwanja mdogo wa ndege wa Seronera wilayani Serengeti mkoa wa Mara uliopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti(Senapa) kwaajili ya kutembelea vivutio vya kitalii wakati wa mapumziko ya mwisho wa mwaka.
Watalii wakiwasili uwanja mdogo wa ndege wa Seronera wilayani Serengeti mkoa wa Mara ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,kukamilika kwa jengo la wageni wanaowasili na wanaondoka kumerahisisha huduma za usafiri ndani ya hifadhi hiyo.
Afisa Utalii Mwandamizi wa Hifadhi ya Taifa Serengeti mkoa
wa Mara,Susuma Kusekwa akizungumza na watalii waliotembelea hifadhi hiyo.
Watalii wakimsikiliza Zacharia Mathayo ambaye ni mwongoza watalii wakati akitoa maelezo kuhusu uhamaji wa wanayamapori aina ya Nyumbu kutoka Kaskazini mwa Hifadhi ya Taifa Serengeti hadi Kusini.
Watalii hufurahia kuona wanyama wakubwa wakiwemo Tembo na wengine wanaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti..
Makundi makubwa ya Simba kama hili utayaona ndani ya hifadhi hiyo.


KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AMEHUTUBIA BARAZA LA KUFUNGA MWAKA 2017 NA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2018 JIJINI MBEYA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiongoza Baraza Maalum la kufunga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka mpya 2018. Baraza hilo limehudhuriwa na Maafisa na Askari kutoka vituo mbalimbali vya Magereza Mkoani Mbeya, Chuo cha Magereza Kiwira na Chuo cha Ufundi Mbeya ambapo Baraza hilo limefanyika leo Desemba 31, 2017 katika Viwanja vya Magereza Mkoani Mbeya.
Baadhi ya Askari wa kike wa Jeshi la Magereza kutoka vituo mbalimbali vya Magereza ya Mkoa wa Mbeya wakisikiliza hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(hayupo pichani) katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka mpya 2018.
Wakuu wa Magereza yaliyopo Mkoani Mbeya wakifuatilia kwa umakini mkubwa maelekezo ya Kamishna Jenerali wa Magereza aliyoyatoa katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka mpya 2018.
Mkuu wa Magereza Mkoani Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kijida Mwakingi akitoa taarifa fupi ya Mkoa wake katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka mpya 2018.

WANANCHI WAMIMINIKA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA KAHAMA

$
0
0
Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa 16 ya Tanzania ambayo zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa linaendelea huku mamia ya wananchi wakionekana kuhamasika na zoezi hilo kwa kujitokeza kwa wingi kwenye vituo ambavyo usajili umekuwa ukiendelea.

Akizungumzia zoezi hilo Afisa Usajili wa Wilaya ya Kahama bwana Ibrahim amesema mwitikio mkubwa wa watu katika vituo vya usajili ni kiashiria kwamba uelewa wa wananchi ni mkubwa na kwamba wanatambua vitakavyowasaidia katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Akizungumzia gharama za zoezi afisa huyo ameeleza zoezi ni BURE na kwamba mwananchi hapaswi kutozwa kiasi chochote cha fedha zaidi ya kufika na nakala (photocopy) za nyaraka/viambatanisho muhimu vya kuweza kumtambulisha uraia wake, umri na makazi. Mfano wa nyaraka hizo ni; Kadi ya mpiga kura, cheti cha kuzaliwa, leseni ya udereva, ID ya Mzanzibar mkazi, TIN, Pasi ya kusafiria, vyeti vya elimu nk.

Mbali na Shinyanya mikoa mingine ambayo NIDA inaendesha zoezi ni Iringa, Mara, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Songwe, Njombe, Singida, Manyara, Mwanza, Simiyu, Mara, Geita, Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa akimsajili mmoja wa Wananchi wa Kata ya Kahama Mjini aliyejitokeza kusajiliwa wakati zoezi la usajili likiendelea kwenye Kata hiyo.
Mkusanyiko wa wananchi wa Kata ya mjini Wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakisubiri huduma ya usajili Vitambulisho vya Taifa, zoezi linaloendelea katika Wilaya hiyo na kuhusisha Kata ya Mjini na mitaa yake.

Mkusanyiko wa wananchi wa Kata ya mjini Wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakisubiri huduma ya usajili Vitambulisho vya Taifa, zoezi linaloendelea katika Wilaya hiyo na kuhusisha Kata ya Mjini na mitaa yake.

Mmoja wa wananchi wa Kahama akisajiliwa na kujaziwa fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa na Mtendaji wa Mtaa wa Kahama kabla ya kusajiliwa.

WAZIRI NDALICHAKO ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI MAGUFULI ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA LIPA KWA MATOKEO (P4R)

$
0
0
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Pro.Joyce Ndalichako amefanya ziara fupi Wilayani Chato kwa kuitembelea Shule ya Sekondari Magufuli na kukagua utekelezaji wa miradi ya lipa kulingana na matokeo(P4R) shuleni hapo.

Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa mabweni, Bwalo, vyoo na vyumba vya madarasa Profesa Joyce Ndalichako ameupongeza Uongozi wa Mkoa, Halmashauri ya Chato na Shule ya Sekondari Magufuli kwa kusimamia vizuri fedha za utekelezaji wa miradi hiyo kwa ubora na kiwango kinachotakiwa.''Nafurahi kuona fedha za P4R zinatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa kama tulivyokagua na kujionea kiwango kilichojengwa ndio haswa kinachotakiwa ambacho darasa lazima liwe na silling bodi, umeme lakini pia liwe na madirisha tofauti na madarasa tuliyokuwa tunajenga zamani hivyo nawapongeza kwa dhati kabisa viongozi mmefanya kazi kubwa thamani ya fedha inaonekana''.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondari Magufuli.

Profesa Ndalichako amesema Serikali ya awamu ya tano inajukumu kubwa la kuhakikisha kunakuwa na mazingira bora katika utoaji wa elimu hivyo miradi ya namna hii inatekelezwa katika Halmashauri nchi nzima. Amesema mwezi desemba 2017 serikali imetoa kwa halmashauri zote shilingi bilioni 15 na milioni 900 za kuendeleza jitihda za kuimarisha miundombinu ya sekta ya elimu ili kuongeza na kuimarisha majengo kwa ajili ya kupokea wanafunzi wa darasa la kwanza ambapo zitajenga jumla ya madarasa 415, mabweni 46, matundu ya vyoo 814 na mabwalo 7.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amempongeza Waziri wa elimu kwa kutembelea shule hiyo ili kujionea kazi nzuri iliyofanyika licha ya kuwa na majukumu mengi ya kitaifa. Amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Geita kwa jitihada zao za kushiriki katika ujenzi wa nyumba vya madarasa 8000 kwa shule za msingi na Sekondari ambapo tangu mkoa uzindue kampeni ya ujenzi huo zaidi ya vyumba 900 vya shule za msingi na zaidi ya 130 vya Sekondari vipo katika hatua tofauti. Amesisitiza kuendelea kuunga mkono jitihada zao kwa kuhakikisha kunakuwa na uwazi katika michango inayotolewa na wananchi.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwa na viongozi wa Mkoa wa Geita wakati wa kukagua vyumba vya madarasa.

Mhandisi Robert Gabriel amemhakikishia Waziri wa Elimu kuwa pamoja na kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi walioandikishwa kujiunda na elimu ya awali, darasa la kwanza na Sekondari hakutakuwa na mwanafunzi atakaye kaa nje ya darasa kwa kuwa jitihada za zinafanyika kwa haraka ili kukabiliana na hali hiyo.

Akiwa katika shule hiyo Mheshimiwa Waziri wa elimu alikagua ujenzi wa vyumba 8 vya madarasa, matundu 20 ya vyoo, mabweni 2 ya kulala wanafunzi na bwalo miradi yote hii imetekelezwa na Serikali kupitia mpango wa lipa kulingana na matokeo kwa gharama ya shilingi 570,500,000/=.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bwanga wakati wa Ziara yake katika shule ya Magufuli Sekondari.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi akizungumza jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Magufuli Sekondari.
Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mheshimiwa Shaban Ntarambe akizungumza na wananchi (awapo kwenye picha) wakati wa ziara ya Waziri wa Elimu Wilayani Chato.
Muoenako wa Jengo hilo.

NIDA YATAJA MIKOA INAYOFANYA VIZURI ZOEZI LA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Ndg Andrew W. Massawe ameitaja mikoa ya Mara, Arusha, Iringa, Geita, Lindi, Simiyu, Mbeya na Songwe kuwa mikoa inayoongoza katika zoezi la kuwasajili wananchi kupata Vitambulisho vya Taifa; huku mikoa mingine ikiwa nyuma kiusajili kulinganisha na malengo waliyowekewa.

Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa zoezi la usajili kwa mkoa wa Ruvuma lilofanyika katika viwanja vya Lisaboni-Songea, Ndugu Massawe amemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba kusaidia kuweka msukumo kwa viongozi na wananchi kwenye mikoa ambayo haifanyi vizuri ili iongeze kasi ya usajili kwa lengo la kukamilisha usajili kwenye mikoa yao kwa muda uliopangwa.

Akihutubia wananchi wa Ruvuma waliofurika kwenye viwanja vya Lisaboni vilivyopo nje kidogo ya mji wa Songea, Waziri wa Mambo wa Ndani ya Nchi Mhe.Dkt Mwigulu Lameck Nchemba amewasisitizia wananchi kujitokeza kwa wingi kusajiliwa kwani kuwa na kitambulisho cha Taifa siyo suala la hiyari ni wajibu kwa kila Mtanzania mwenye sifa kuwa nacho.

“ Mhe. Rais wetu ametoa hela za kuwasajili, zoezi ni bure bado kujisajiliwa kwenda kupigwa picha na kuchuliwa alama za vidole ikushinde?” aliuliza Waziri huyo mwenye dhamana kubwa katika kusimamia utekelezaji wa zoezi hilo.
Mhe.Dkt Mwigulu L.Nchemba akikagua baadhi ya Vitambulisho 3470 ambavyo watagawiwa wananchi wa Kata ya Songea ambao Usajili wao umekamilika kufuatia zoezi la Usajili Vitambulisho kuwa kufanyika katika Kata za karibu kabla ya kuanza Usajili wa Umma. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme na Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nida Ndugu Andrew W. Massawe.
Mhe Waziri akimkabidhi Kitambulisho chake mmoja wa wananchi wa Kata ya Songea Bwana Hassan Ally Shomari wakati wa zoezi la ugawaji Vitambulisho kwenye sherehe za uzinduzi wa zoezi la Usajili kwa mkoa wa Ruvuma. Jumla ya Vitambulisho 3470 viligawanywa kwa wanachi wakati wa sherehe hizo.
kikundi cha burudani za asili maarufu kama wana Lizombe wakitumbuiza wakati wa sherehe za uzinduzi wa zoezi la Usajili kwa mkoa wa Ruvuma.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt Mwigulu L.Nchemba akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Ndugu Andrew W. Massawe wakiwasili kwenye viwanja vya Lisaboni –Songea kushiriki sherehe za uzinduzi wa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa mkoa wa Ruvuma.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA KAMPENI YA KITAIFA YA UPANDAJI MIKOROSHO BORA NA MIPYA MILIONI 10 MKOANI LINDI

$
0
0



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Mh Godfrey Zambi alipokuwa akimueleza jambo wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya Upandaji mikorosho Bora na mipya Million10 iliyofanyika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisikiliza Maelezo toka kwa Afisa Ubanguaji Toka Bodi ya Korosho Tanzania CBT Domina Mkangara wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya Upandaji mikorosho Bora na mipya Million10 iliyofanyika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.

KATIBU TAWALA WILAYA YA CHEMBA NYAKIA ALLY AHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UPANDAJI MITI NA UCHANGIAJI DAMU

$
0
0
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Chemba Ndugu Nyakia Ally Chirukile akichangia damu baada ya kushiriki zoezi la Usafi wa kila jumamosi ya mwisho wa Mwezi,zoezi ambalo lilikwenda sambamba na upandaji wa miti zaidi ya 2000 pembezoni mwa barabara ya Dodoma -Babati kuanzia Kidoka mpaka  Kilema.

Akizungumza baada ya shughuli nzima,Ndugu Nyakia aliwaomba wananchi wa wilaya ya Chemba na mkoa wa Dodoma kwa ujumla,kuunga mkono juhudi za Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassani katika suala zima la uhamasishaji wa kupanda miti na kuhakikisha mkoa huo unakuwa wa kijani .
Baada ya kufanyika shughuli ya uchangiaji Damu,pia kulifanyika tukio la usafi na upandaji wa miti zaidi ya 2000 pembezoni mwa barabara ya Dodoma -Babati kuanzia Kidoka mpaka  Kilema,kuhakikisha mkoa wa Dodoma unakuwa wa kijani,kufuatia kampeni maalum ya upandaji miti iliozinduliwa hivi karibuni na Makamu wa Rais,Mama Samia Suluhu Hassan mkoani humo na kushirikisha viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Wadau wengine wa Mazingira.


  Katibu Tawala wa Wilaya ya Chemba Ndugu Nyakia Ally Chirukile akishiriki shughuli ya  upandaji wa miti zaidi ya 2000 pembezoni mwa barabara ya Dodoma -Babati kuanzia Kidoka mpaka  Kilema,baada ya zoezi hio Ndugu Nyakia pia alishiriki tukio la Usafi na uchangiaji wa Damu.

SAME KAYA SACCOS YAWA MKOMBOZI WA WANA -SAME, KILIMANJARO

$
0
0
Same Kaya Saccos yashika nafasi ya pili Mkoa wa Kilimanjaro 2017 kwa kufanya vizuri katika nyanja zote. Hayo yamebainika mwishoni mwa wiki hii wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la SACCOS kata ya Hedaru ambalo ni tawi la 2 ukiacha ofisi ya makao makuu Same. A
 
kizungumza wakati hafla hiyo fupi iliyofanyika Hedaru, Mwenyekiti wa Saccos hiyo, Bw. Kisimbo alisema kuwa kwa sasa wametimiza miaka 15 na tayari wameshapata tuzo siku ya SACCOS dunia mwezi Oktoba 2017. 
 
"Kwa muda ambao tumekuwa tukiwahudumia wanachama wetu tumeweza kupata mafanikio mengi likiwemo la kupata tuzo siku ya SACCOS duniani Mwezi Octoba, 2017," alisema Kisimbo. 
 
Kwa upande wake Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule aliwapongeza kwa juhudi ambazo wamekuwa wakizifanya na pia aliwaomba kuendelea kuongeza wanachama wawe wengi zaidi. 
 

Mhe. Rosemary Senyamule aliwaomba wanachama waendelee kuwa waaminifu kwa kulipa madeni yao kwa wakati, wananchi wengi kujiunga na SACCOS hiyo iliyoonyesha mfano mzuri wa kutunza fedha za wanachama wake.

Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule (kushoto) akionyesha moya ya mashine ya kufulia iliyotolewa na Same Kaya Saccos kwa kituo cha afya cha Hedaru, Kilimanjaro.  
Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule akiwa amenyanyua mikono mara baada ya kukata upete wa kuashiria uzinduzi wa tawi jipya la SACCOS kata ya Hedaru, Kilimanjaro.

Watoto yatima na wa mazingira magumu Hedaru wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Rosemary Senyamule mara baada ya kupatiwa zawadi ya madaftali.

Mhe. Rosemary Senyamule akipanda mti wakati wa hafla hiyo. 
Mhe. Rosemary Senyamule akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Same Kaya Saccos. 

Rais wa Zanzibar Dk. Shein, Ashiriki Katika Zoezi La Usafi Wa Mazingira Katika Nyumba Za Wazee Sebleni Zanzibar

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akishiriki katika zoezi la Usafi wa Mazingira katika eneo la Nyumba za Wazee Sebleni na kujumuika na Wananchi katika zoezi hilo, kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika Nyumba za Wazee Sebleni Unguja, kulia Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe. Maudline Cyrus Castico.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wazee wanaoishi Nyumba za Wazee Sebleni alipofika katika viwanja hivyo kwa ajili ya Uzinduzi wa Usafi wa Mazingira katika eneo hilo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Vifaa vya Usafi Katibu wa Baraza la Vijana Wilaya ya Magharibi A Unguja Farida Juma, kwa ajili ya zoezi la Usafi katika Wilaya yao, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Nyumba za Wazee Sebleni wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Usafi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa meza kuu wakiwa wamesimama kwa dakika moja kuwakumbuka Wazee waliotangulia mbele ya haki.

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Yapongezwa kwa Kuwajali Wateja Wake

$
0
0
Afisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma akikagua fomu ya tamko la rasilimali na madeni iliyowasilishwa na mmoja wa viongozi wa umma katika ofisi za Sekretarieti hiyo Jijini Dar es Salaam leo. . Leo ndiyo siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu hizo ambapo kila kiongozi aliyetajwa katika sheria husika analazimika kuwa amewasilisha fomu yake.(Picha na: Frank Shija -MAELEZO)
Afisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma akimuelekeza jambo mmoja wa viongozi wa umma aliyefika katika ofisi za Sekretarieti hiyo kwa ajili ya kuwasilisha fomu yake ya tamko la rasilimali na madeni leo Jijini Dar es Salaam. . Leo ndiyo siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu hizo ambapo kila kiongozi aliyetajwa katika sheria husika analazimika kuwa amewasilisha fomu yake.
Afisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma akikagua fomu ya tamko la rasilimali na madeni iliyowasilishwa na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Omary Mkumba katika ofisi za Sekretarieti hiyo Jijini Dar es Salaam leo. . Leo ndiyo siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu hizo ambapo kila kiongozi aliyetajwa katika sheria husika analazimika kuwa amewasilisha fomu yake.(Picha na: Frank Shija -MAELEZO)
Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Omary Mkumba akisaini fomu yake ya tamko la rasilimali na madeni mara baada ya kuwasilisha na kukaguliwa na Afisa wa Sektretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. Leo ndiyo siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu hizo ambapo kila kiongozi aliyetajwa katika sheria husika analazimika kuwa amewasilisha fomu yake. (Picha na: Frank Shija -MAELEZO)

TAFUTENI TAKWIMU MPYA, WAZIRI MKUU AAGIZA

$
0
0
“Maafisa kilimo na maafisa ushirika mkisimamiwa na Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi, mshirikiane na kusimamia kwa umakini upatikanaji wa takwimu za wakulima na maeneo yanayolimwa, haiwezekani kila mwaka takwimu ziwe ni zilezile tu,” alisema.

“Afisa kilimo wa wilaya lazima ujue una wakulima wangapi, je hao wakulima wako, kila mmoja analima ekari ngapi? Na katika ekari hizo, ana miche mingapi, na je ana mahitaji ya pembejeo kiasi gani?” alisema.

“Pia nilikwishawaagiza maafisa ushirika na viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) mpaka chama kikuu cha ushirika, kuwa kila mmoja anapaswa atambue ana wanachama wangapi katika chama chake. Hili litawezekana pia kwa kushirikiana na Afisa Mtendaji wa Kata au Mwenyekiti wa Kijiji, kwa sababu wao wana idadi kamili za watu wanaowaongoza,” alisema.

“Ninaamini tukifanya hilo tutamaliza tatizo la takwimu na Serikali itakuwa na uwezo mkubwa wa kuwahudumia wakulima wake, na tutaweza kuweka bajeti ya kutosha kuhudumia mahitaji yao,” alisisitiza.Waziri Mkuu alipanda mche mpya wa korosho ili kuanzisha zoezi la upandaji miche hiyo na kisha akagawa miche kwa wakulima 10 kutoka vijiji vya Likunja, Kitandi, Kilimahewa na Nachingwea ambao waliwawakilisha wenzao.

Mapema, kabla ya kuzungumza na wananchi Waziri Mkuu alikagua vitalu vya miche ya mikorosho vilivyopandwa na Halmashauri ya Ruangwa na kuelezwa kuwa miche hiyo ipo ya aina mbili ambapo aina ya kwanza ni ile iliyotokana na mbegu na ya pili ni ile iliyotokana na vikonyo (grafting).

Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa, yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka jimboni kwake.Sherehe hizo zilihudhuriwa na wakuu wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani na wajumbe wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT). Wakuu wa Wilaya na wataalamu kutoka kituo cha utafiti cha Naliendele walishiriki zoezi hilo.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiangalia Mche Mpya wa Korosho, wakati akikagua kitalu cha miche hiyo, katika kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi. Desemba 31, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipata ufafanuzi wa Miche Mipya ya Korosho kutoka kwa Afisa Ubanguaji Bodi ya Korosho Tanzania, Domina Mkangara, wakati akikagua kitalu cha miche hiyo, katika kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi. Desemba 31, 2017. 
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania, Hassan Jarufu, wakati akikagua kitalu cha miche mipya ya korosho, katika kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi. Desemba 31, 2017. Katikati ni Afisa Ubanguaji Bodi ya Korosho Domina Mkangara 
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Ruangwa wakati wa kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipanda mche mpya wa korosho mara baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi.
aziri Mkuu,Kassim Majaliwa akimwagilia maji mche mpya wa korosho aliyoupanda, baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akimkabidhi mche mpya wa mkorosho Bi. Mwanahamisi Saidi, mkazi wa Kilimahewa, baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi.Desemba 31, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, DKT. JUMA MALEWA ATETA NA VIONGOZI WA KIMILA JIJINI MBEYA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kimila Mkoani Mbeya(kushoto) ni Kiongozi Mkuu wa kimila kabila la Wasafa lililopo Mkoani Mbeya, Rocket Mwashinga(kulia) ni Kiongozi wa Pili wa Wasafa Mkoani Mbeya, George Joto mara baada ya mazungumzo mafupi na Kamishna Jenerali wa Magereza walipokutana katika viwanja vya Magereza Mkoani Mbeya, leo Desemba 31, 2017(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiagana na Kiongozi Mkuu wa kimila kabila la Wasafa lililopo Mkoani Mbeya, Rocket Mwashinga mara baada ya mazungumzo mafupi walipokutana katika viwanja vya Magereza Mkoani Mbeya, leo Desemba 31, 2017. Kamishna Jenerali wa Magereza nchini yupo Jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi ya siku nne ambapo hadi jana amefanya ukaguzi katika Magereza ya Ruanda, Kyela, Tukuyu pamoja na Chuo cha Mafunzo ya Magereza, Kiwira kilichopo Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

NAIBU WAZIRI ULEGA AAGIZA WATENDAJI WA VIJIJI NA WENYEVITI KUWASOMEA MAPATO NA MATUMIZI WANANCHI

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii.

NAIBU waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mbunge) wa Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani Abdalla Ulega ametoa agizo kwa Watendaji wa vijiji na Wenyeviti kuwasomea mapato na matumizi wananchi wao ili kuepuka kurudisha nyumba uchangiaji wa shughili za maendeleo.

Naibu waziri huyo ametoa agizo hilo wilayani humo akiwa katika mwendelezo wa ziara za vijijini ambapo akiwa katika kijiji cha Kiziko, kilichopo Kata ya Mwarusembe baada ya kupokea malalamiko ya wananchi juu ya viongozi wao ngazi ya kijiji kushindwa kusoma taarifa ya mapato na matumizi.

Alisema kushindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi kunachangia kwa asilimia kubwa wananchi kushindwa kuchangia maendeleo katika maeneo hayo hivyo lazima wananchi wajulishe kinachoingia na kinavyotumika.

"Natoa agizo hili kwa watendaji na wenyeviti kusoma mapato na mapato na matumizi na hapa naagizi mtendaji wa Kata ya Mwarusembe kuhakikisha hadi kufika Januari 2 ,2018 niwe nimepata taarifa za kushindwa kusoma mapato na matumizi katika kijiji hiki cha kiziko. "alisema Ulega

Alisema wananchi wanatamani kujitolea kwa lengo la kuchangia maendeleo lakni wanavunjwa moyo viongozi hao huku akisisitiza kupewa ifika January 2 awe amepata taarifa nakuhaidi kulifuatilia jambo hilo kwa ukaribu zaidi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kiziko alipofanya ziara katika jimbo la Mkuranga.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Mkuranga, Juma Abeid akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kiziko juu ya mikakati ya Halmashauri katika uboreshaji wa sekta mbalimbali.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwasili katika kijiji cha cha Kitonga katika ziara ya vijiji jimbo la Mkuranga. 


MKOA WA PWANI UMEUZA TANI 19,815 ZA KOROSHO NA KUPATA BIL.39-RC NDIKILO

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga

MKOA wa Pwani ,tayari umeuza tani 19,815 ambazo zimeingiza zaidi ya bilioni 39 tofauti na msimu uliopita ambapo uliuza tani 13,000 na kupata bilioni 33.##

Mkoa huo umejiwekea lengo la kuuza tani 25,000 hadi 30,000 kwa msimu huu ambao minada yake ya korosho ikiwa bado inaendelea .Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,aliyasema hayo Mkuranga ,wakati akizungumzia changamoto na mafanikio waliyoyapata msimu wa korosho 2017/2018 .

Alieleza ,mbali ya hayo wakulima wa korosho mkoani Pwani wakiwa bado wanadai zaidi ya bilioni tano.Mhandisi Ndikilo alisema ,kuuza tani 19,815 hadi sasa ni mwanzo mzuri wa kufikia malengo yao waliyojiwekea msimu huu.Alisema ,hatua hiyo imetokana na serikali kutoa pembejeo bure katika msimu huu na mfumo wa stakabadhi ghalani.

Alibainisha ,licha ya mafanikio hayo lakini kuna changamoto zimejitokeza tangu kuanza kwa minada mwaka huu ikiwemo uhaba wa magunia .Kero nyingine ni ile iliyojitokeza sasa ya kuchakachua ubora wa korosho unaofanywa na baadhi ya vyama vya msingi vya ushirika (Amcos).

“Changamoto ya magunia inaweza kuwa historia endapo tutakubaliana kwa kukaa na mikoa ya Lindi na Mtwara ili kuhamasisha wawekezaji waje wawekeze kiwanda cha magunia lengo likiwa ni kukabiliana na tatizo hili” alifafanua .Akizungumzia kuhusu tatizo la ubora wa korosho, mhandisi Ndikilo ,alisema baadhi ya Amcos zimejiingiza kwenye kuhujumu minada hiyo kwani baadhi yao wameweka michanga na mawe kwenye magunia ya korosho .
MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani, ambae pia ni mkuu wa Mkoa huo, mhandisi Evarist Ndikilo , akizungumza na baadhi ya wakulima wa korosho wakati alipotembelea ghala moja lililopo wilayani Mkuranga.Picha na Mwamvua Mwinyi



CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) MKOA WA SINGIDA CHAZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO

$
0
0
Na,Jumbe Ismailly SINGIDA 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida kimezindua kampeni zake za uchaguzi mdogo katika jimbo la Singida Kaskazini na kusisitiza juu ya kudumisha amani,utulivu na mshikamano uliopo hapa nchini.

Akizindua kampeni hizo zilizofanyika katika Kijiji cha Mtinko,Singida Vijijini,kwa niaba ya Katibu mkuu wa CCM taifa,Naibu katibu mkuu wa CCM,Tanzania bara,Rodrick Mpogolo alisema idadi kubwa ya wananchi wameendelea kukichagua chama cha mapinduzi kutokana na kuwa na mipango mizuri ya maendeleo.

Alizitaja sababu zingine kuwa ni chama chenye historian a pia kina awamu tano za uongozi na kwamba ni chama kilichokomaa na endapo kitakabidhiwa nchi au ukikabidhi madaraka,watakuwa na uhakika kwamba madaraka hayo yameshikwa na watu waliokomaa.

Kwa mujibu wa Naibu katibu mkuu huyo wakati wote CCM imekuwa ikishughulikia kero za watu na kwa hivi sasa inayo matumaini makubwa ya kubadilisha maendeleo ya nchi na kwamba hivi sasa rais wan chi amekwisha hamisha makao makuu ya serikali yake Mkoani Dodoma,jirani kabisa na Mkoa wa Singida.
Naibu katibu Mkuu wa CCM Tanzania bara,Rodrick Mpogolo akizindua kampeni za uchaguzi mdogo wa CCM katika jimbo la Singida kaskazini zilizofanyika juzi katika Kijiji cha Mtinko,singida vijijini. 
Mgombea wa kiti cha ubunge wa jimbo la Singida kaskazini,Justine Monko akiwa tayari amepokea ilani ya chama kwa ajili ya kutekeleza yaliyoainishwa ndani ya ilani hiyo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Baadhi ya wanachama wa CCM waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Singida kaskazini wakiwa kwenye viwanja vya mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mtinko,singida vijijini juzi.
Baadhi ya wanachama wa CCM waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Singida kaskazini wakiwa kwenye viwanja vya mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mtinko,singida vijijini juzi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Rais Magufuli amtumia salamu za Rambirambi Mhe. Rais Kenyatta kufuatia ajali ya barabarani

SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MHE. NAIBU WAZIRI WA AFYA Dkt. Faustine Ndugulile

$
0
0
SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA MHE. NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO ZIKISISITIZA JUU YA WAJIBU WA WATOA HUDUMA ZA AFYA NA MABARAZA YA KITAALUMA PAMOJA NA HAKI ZA WANANCHI KUPATA HUDUMA BORA ZA AFYA.
Ndugu Wananchi,
Nachukua fursa hii kuungana nanyi nyote kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha salama siku hii ya leo tunapoanza mwaka mpya 2018. Hii ni neema pekee ambayo Mwenyezi Mungu  ametujaalia  kwani kuna wengi walitamani kuifikia siku hii lakini hawakubahatika. Hivyo, nawatakieni nyote kheri na fanaka katika mwaka huu mpya.
Napenda kutumia fursa hii pia kuwashukuru na kuwapongeza Wanataaluma na Watoa huduma za afya wote kwa kuendelea kutoa huduma kwa ari, juhudi, uaminifu na uadilifu licha ya changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika utendaji kazi wa kila siku.  Nami nawatia shime na hamasa ili muendelee na moyo huo wa kuwahudumia na kuwatumikia Wananchi.
Natambua kuwa  Sera yetu ya Afya inataka tuijenge jamii yenye afya bora na ustawi ambayo itachangia kikamilifu katika maendeleo ya mtu binafsi pamoja na yale ya Taifa.  Aidha, Sera na Sheria zetu mbali mbali zinatambua umuhimu na nafasi ya Mabaraza ya kitaaluma katika kuboresha na kusimamia viwango vya maadili ya wanataaluma walio chini ya Wizara yangu. Jambo hili ni muhimu sana hususan tukizingatia ongezeko la minong’ono, manung’uniko na hata malalamiko kutoka kwa wananchi dhidi ya baadhi ya  watoa huduma ambao wanakiuka taratibu au miiko ya kazi zao na hivyo kuathiri ubora wa utoaji huduma.
Nimeona kama sehemu ya salamu zangu za mwaka mpya wa 2018, nitoe maelekezo yatakayoweza kutusaidia kuboresha utoaji huduma katika sekta ya afya kupitia Watoa Huduma za Afya na Mabaraza ya Kitaaluma na pia kuwakumbusha wananchi juu ya haki yao ya msingi ya kupata huduma bora za afya na wajibu wao wa kuhakikisha hilo linatokea.

JK AUKARIBISHA MWAKA MPYA 2018 NA WANANCHI WA MSOGA, MKOANI PWANI USIKU HUU

$
0
0
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa pamoja na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgallu, sambamba na wananchi wa mji wa Msoga Mkoani Pwani kusherehekea kuukaribisha mwaka mpya wa 2018 katika hafla iliyoandaliwa na Dkt. Kikwete kijijini kwake Msoga, usiku huu.
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia fataki angani wakati wa sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2018, iliyofanyika usiku huu kijijini kwake Msoga, Mkoani Pwani.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (aliyemshika mtoto) alikuwa ni mmoja wa wakazi wa mji wa Msoga waliojumuika nyumbani kwa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kulikofanyika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2018.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono wa heri ya mwaka mpya na baadhi ya wageni waliofika kijijini kwake hapo.
 Msanii wa Muziki wa Singeli, Msaga Sumu akitumbuiza mbela ya maelfu ya wananchi wa Msoga katika sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya 2018, iliyofanyika Nyumbani wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, Msoga Mkoani pwani.
 Burudani ya Ngoma ya Asili.

MAGAZETI YA JUMATATU LEO JANUARY MOSI,2018

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images