Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

SERIKALI KUJADILIANA NA MGODI WA CATA MINING KABLA YA KUURUHUSU KUENDELEA UZALISHAJI

$
0
0
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameuagiza Mgodi wa Dhahabu wa CATA Mining uliopo katika Kijiji cha Kataryo Mkoani Mara kukaa pamoja na Serikali kujadili tofauti zilizopo ili kuruhusu mgodi huo kuendelea na shughuli za uzalishaji.
Alitoa agizo hilo Desemba 28, 2017 kwenye mkutano na wananchi katika Kata ya Tegeruka kufuatia ombi kutoka kwa mmoja wa Wakurugenzi wa mgodi huo, Mahuza Nyakirang’ani  pamoja na wananchi waliokuwa wakifanya kazi kwenye mgodi huo na wananchi wa maeneo ya jirani na mgodi waliokuwa wakinufaika na mgodi kwa namna mbalimbali la kuruhusu uzalishaji uendelee.
Alisema anatambua umuhimu wa mgodi huo kwa wamiliki na wananchi kwa ujumla na hivyo ipo haja ya kukaa pamoja kujadili tofauti zilizosababisha kusimamishwa kwa uzalishaji katika mgodi huo ili uendelee na uzalishaji.
Alisema uangaliwe uwezekano wa kuruhusu uzalishaji uendelee ili wananchi waliokuwa  wameajiriwa mgodini hapo waendelee na ajira zao huku majadiliano yakiendelea kufanyika.
“Kama mlivyonieleza kuna baadhi yenu mlikua mkifanya kazi kwenye mgodi lakini tangu mgodi usimamishwe uzalishaji nanyi hamna kazi, kwahiyo ni vyema wakati mazungumzo yanaendelea na mgodi ukawa unazalisha ili waliokosa ajira warudi kazini,” alisema.
Aidha, akizungumza kwa niaba ya wananchi waishio maeneo jirani na mgodi, Elizabeth Masabu ambaye ni Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Kataryo alimueleza  Naibu Waziri Nyongo kuhusu uhusiano baina ya mgodi na wananchi na pia kumuomba kuingilia kati masuala mbalimbali ikiwemo ajira kwa wananchi wa maeneo husika, fidia, utunzaji wa mazingira na migogoro na mgodi.
Masabu aliongeza kuwa waliingia mikataba ya kirafiki na mgodi huo ambao alisema kuna makubaliano ambayo hayajafanyika na hivyo alimuomba Naibu Waziri kuwasaidia kuhakikisha mgodi huo unarejea makubaliano.
Akijibu hoja za wananchi hao, Nyongo aliuagiza mgodi kuhakikisha unaingia mkataba wa kisheria wa uwajibikaji kwa jamii (corporate social responsibility) ili Serikali ya Kijiji iweze kujipatia haki yake kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba.
Aliuagiza mgodi huo kutoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi wa maeneo ya jirani kwa kazi wanazoziweza na wakati huohuo aliwaasa wananchi watakaonufaika na ajira wafanye kazi kwa uadilifu.
Kwa upande wake Nyakirang’ani  alimuahidi Naibu Waziri Nyongo kwamba mgodi huo utaendelea kuboresha mahusiano na jamii na kwamba watatekeleza maagizo yake kwa wakati ikiwemo suala la ulipaji wa fidia.
 Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Kataryo, Elizabeth Masabu akimueleza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) kuhusu uhusiano baina ya mgodi na wananchi wakati wa mkutano wa Naibu Waziri huyo na wananchi wa Kata ya Tegeruka, Musoma Vijijini.
Baadhi ya Wananchi waishio maeneo ya jirani na Mgodi wa Dhahabu wa CATA Mining wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na wananchi hao uliofanyika katika Kijiji cha Kataryo.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kataryo, Kata ya Tegeruka Wilaya ya Musoma Vijijini (hawapo pichani) wakati wa mkutano wake na wananchi waishio maeneo jirani na Mgodi wa Dhahabu wa CATA Mining.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akitembelea Mgodi wa CATA Mining uliopo katika Kijiji cha Kataryo Mkoani Mara ili kujionea hali ya mgodi huo. Kulia ni mmoja wa Wakurugenzi wa mgodi huo, Mahuza Nyakirang’ani na kushoto ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kushoto) akimsikiliza mmoja wa Wakurugenzi wa Mgodi wa CATA Mining, Mahuza Nyakirang’ani (wa pili kulia) akielezea namna uchenjuaji wa dhahabu unavyofanyika mgodini hapo. Kulia ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina.


MICHUZI TV: DC GODWIN GONDWE AIELEZEA WILAYA YA HANDENI

Mkuchika Awasilisha fomu ya tamka la Rasilimali na Madeni Mtwara leo.

$
0
0
Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Capt Mstaaf George Mkuchika  amewataka Wabunge,madiwani na Viongozi wa Una wanaojihusisha na Biashara Na Halmashauri Kuacha Mara moja kutokana na Kwenda Kinyume na Sheria ya Viongozi Na watumishi wa Uma.

Mkuchika Ameyasema hayo wakati akirejesha taarifa fomu za Rasilimali na Madeni katika Ofisi ya sekretarieti ya maadili ya Uma Kanda ya Kusini Iliyopo Mkoani Mtwara.

Mpaka Kufikia Sasa Jumla ya Viongozi 794 ndio wamerejesha fomu za Rasilimali na Madeni kati ya Viongozi 1246 ambao wanatakiwa kuwasilisha.

Aidha Ofisi Hiyo imetenga Siku ya Jumapili tareh 31 kuanzia Mchana mpaka Jioni Kupokea Taarifa kwa Viongozi ambao hawajawasilisha.
Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Capt Mstafu George Mkuchika Akikabidhi fomu za Rasilimali na Madeni kwa Katibu Msaidizi wa Tume ya serkretariet ya Maadili ya Utumishi wa Uma Kanda ya Kusini Mayina Henjewele.
2.Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Capt Mstaafu George Mkuchika akionesha fomu Mara baada ya kukabidhi fomu zake na Kuhakikiwa.

MTU MMOJA ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUPORWA BAJAJI NA WATU WALIOMKODISHA

$
0
0
Kamanda wa  Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Jonathan Shanna akizungumza na waandishi wa habari 

Na Mwandishi Wetu, Pwani
MTU mmoja nayesadikiwa kuwa ni jambazi amefariki dunia baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kubainika kumjeruhi dereva wa Bajaji  aliyefahamika kwa jina la Looqman Salehe  mkaazi wa Mwanalugali Wilayani Kibaha Mkoani Pwani   katika tukio lililotokea  majira ya saa moja usiku maeneo ya Machinjio ya zamani huku majambazi hayo wakitoweka na Bajaji hiyo.

Imeelezwa kuwa watu hao walimfunga kamba dereva huyo wa Bajaji yenye usajili namba MC 415BSH na kwenda kumtupa eneo la Pangani alikoolewa  na wasamaria wema  waliokuwa wakipita  katika eneo hilo.

Baada ya taarifa kufikishwa katika Jeshi  la Polisi Mkoani Pwani walichukua hatua za haraka za kuweka mitego katika maeneo mbalimbali na kuwashirikisha wananchi na kuendesha msako mkali mtaa kwa mtaa,hatimaye wezi hao waliingia katika mtego, yamesemwa hayo na Kamanda wa  Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Jonathan Shanna alipozungumza na vyombo vya habari katika mkutano uliofanyika kwenye kituo cha Polisi Mapinga Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Kamanda Shanna amewataka wahalifu waliokimbia kujisalimisha  mara moja kwani Jeshi la Polisi limeshapata taarifa za uhakika kutokana na kubaini  maeneo  wanayoishi.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MATUMIZI YA FEDHA ZA KIGENI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

$
0
0


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO


 

 

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MATUMIZI YA FEDHA ZA KIGENI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa maagizo kuhusu matumizi ya fedha za kigeni katika  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusisitiza kuwa utekelezaji wake uanze  tarehe 1 Januari, 2018.  Maagizo hayo ni kama ifuatavyo: -

         i.            Bei zote hapa nchini zitangazwe kwa shilingi ya Tanzania. Bei hizi zinajumuisha kodi ya nyumba za kuishi na maofisi, bei ya ardhi, gharama za elimu na afya, bei za vyombo vya usafiri na vifaa vya kielektroniki.

       ii.            Bei ambazo walengwa wake wakuu ni watalii au wateja wasio wakazi zinaweza kutangazwa kwa fedha za kigeni na malipo yake yanaweza kufanyika kwa fedha za kigeni. Bei hizi zinajumuisha gharama za usafirishaji kwenda nchi za nje kupitia Tanzania, gharama za mizigo bandarini kwenda nchi za nje, gharama za viwanja vya ndege na viza kwa wageni, na gharama za hoteli kwa watalii kutoka nje ya nchi. Walipaji wanaotumia fedha za kigeni watambuliwe kwa vitambulisho vyao kama pasi za kusafiria na nyaraka za usajili kwa makampuni.

      iii.            Viwango vya kubadilishana fedha vitakavyotumika katika kuweka hizo bei katika sarafu mbili viwekwe wazi na visizidi vile vya soko. Ifahamike wazi kuwa ni mabenki na maduka ya fedha za kigeni tu yanayoruhusiwa kupanga viwango vya kubadilisha fedha kutokana na ushindani katika soko la fedha za kigeni.

    iv.            Mkazi yeyote wa Tanzania asilazimishwe kulipia bidhaa au huduma yeyote hapa nchini kwa fedha za kigeni.

Aidha Dkt. Mpango ameviagiza vyombo vya dola viwachukulie hatua za kisheria wale wote watakaobainika kukiuka maagizo haya ya Serikali.


IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI



WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

NAIBU WAZIRI AWESO:HATUTASITA KUWACHUKULIA HATUA WAKANDARASI WAZEMBE

$
0
0

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amesema hatasita kumchukulia hatua mkandarasi yoyote ambaye atashindwa kukamilisha kwa wakati miradi ya maji waliopewa kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kuwasimamisha.

Lakini pia ametoa wito pia wakandarasi wa magengeni kuacha kutumiwa kwenye maeneo mbalimbali kwani wamekuwa ndio chanzo cha kupelekea miradi mingi kushindwa kukamilika kwa wakati hali inayosababisha adha kubwa kwa wananchi.

Aliyasema hayo baada ya kukagua mradi wa maji wa eneo Songea katika mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Momba mkoani Songwe ambao unatekelezwa na Mkandarasi wa Kampuni ya Best One Company ambapo aliwataka kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa waledi mkubwa ili uweze kuwa chachu ya mafanikio kwa wananchi hao.

Katika mradi huo Serikali imetolea fedha bilioni moja kwa ajili ya mradi huo ambapo Naibu Waziri huyo alizitaka zitumike kwa uangalifu mkubwa ili kuweza kuukamilisha kwa lengo la kuondoa kero kwa wananchi .

Hata hivyo alisema iwapo mradi huo utashindwa kukamilika kwa wakati hawasita kumchukulia hatua ikiwamo kumsimamisha kazi kwani hawako tayari kuona uzembe unafanyika wakati wananchi wana uhitaji mkubwa wa huduma hiyo.“Labda niwaambie kwamba sisi kama serikali nia yetu kubwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi kwenye maeneo yao lakini niwaambie kuwa pia hatutamvumilia Mkandarasi yoyote ambaye akishindwa kukamilisha mradi huo kwa wakati hasa huyo ambaye anatekeleza eneo hili “Alisema Naibu Waziri Aweso.

Naye kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Momba,Juma Irando ameitaka idara ya maji wilayani humo kutowapa tenda wakandarasi wanaotuhumiwa kukwamisha juhudi za serikali za kukabiliana na tatizo la maji kuhakikisha linakwisha.Hata hivyo alisema inadaiwa kuwa baadhi ya miradi ya maji wilayani humo inashindwa kukamilika kwa wakati kutokana na uwezo mdogo kitaalamu walionao baadhi ya wakandarasi ambao wanakabidhi miradi (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha).

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso akisaini cha wageni kata ya Songea alipokuwa na mkutano wa hadhara na wananchi wakati wa ziara yake
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso akimwaga mchanga kwa ajili ya mradi huo


Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua mradi huo wa maji 
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akimuagiza Mkandarasi wa Maji mbele ya Wananchi wa Tunduma kuhakikisha mradi wa maji unakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma za maji .

HATUTASITA KUMCHUMKULIA HATUA MKANDARASI YEYOTE ATAKAYEKWAMISHA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI: NAIBU WAZIRI AWESO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesema wizara yake haitasita kumchukulia hatua mkandarasi yeyote endapo atabainika kuwa chanzo cha kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo mbalimbali nchini. Aweso alizungumza hayo wakati akiwa ziarani katika mkoa wa Songwe, akikagua miradi ya maji katika Wilaya ya Momba.

Akiwa kwenye mradi wa Sogea uliopo katika mji mdogo wa Tunduma, amesema endapo mkandarasi wa Kampuni ya Best One aliyepewa kazi ya kujenga mradi huo atashindwa kukamilisha kwa wakati, hawatasita kumchukulia hatua mara moja.

‘‘Serikali inataka mradi huu wa Sogea na miradi mingine yote ya maji nchini ikamilike kwa wakati na wananchi waanze kufaidi matunda ya Serikali yao, ndio maana nipo hapa kufuatilia hilo na wakandarasi waliopewa kazi wahakikishe wanafanya kazi usiku na mchana ili kufanikisha hilo,’’ alisema Naibu Waziri Aweso.

Wakati huo Aweso ameagiza ameagiza Sh. bilioni 1 zilizotolewa na Rais John Magufuli kwa ajili ya ujenzi mradi wa maji Sogea zitumike kwa uadilifu na kukamilisha mradi huo ili kumaliza kero ya maji kwa wakazi wa Sogea na maeneo ya jirani.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Iranda ameiagiza Idara ya Maji wilayani humo, kutowapa tenda wakandarasi waasio na sifa ambao wanatuhumiwa kukwamisha juhudi za Serikali katika kukabiliana na tatizo la maji, na atakayefanya hivyo atakuwa amevunja sheria na atachukuliwa hatua.

Hii inatokana na taarifa kuwa baadhi ya miradi ya maji wilayani Momba kushindwa kukamilika kwa wakati kutokana na uwezo mdogo wa kitaalamu kwa baadhi ya wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akisaini kitabu cha wageni juu ya tenki la maji la mradi wa Sogea uliopo Wilaya ya Momba, mkoani Songwe.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akihutubia wakazi wa Tunduma katika mkutano wa hadhara katika ziara yake katika Wilaya ya Momba, mkoani Songwe.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akishiriki kuchimba sehemu itakayowekwa miundombinu ya mradi wa maji katika Wilaya ya Momba, mkoani Songwe.

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AKAGUA UJENZI WA NYUMBA YA DAKTARI KITUO CHA AFYA NKOWE

$
0
0
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiwa na mganga mkuu wa kituo cha afya Nkowe Dk. Paul Mbinga,wakati akikagua ujenzi wa nyumba ya daktari, Waziri Mkuu yupo Wilayani Ruangwa kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka ambapo aliamua kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake. Desemba 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipewa maelezo ya ujenzi wa maabara katika kituo cha afya Nkowe na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ruangwa, Waziri Mkuu yupo Wilayani Ruangwa kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka ambapo aliamua kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake. Desemba 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Nkowe,baada ya kutembelea na kukagua kituo cha afya Nkowe Wilayani Ruangwa,. Desemba 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea wanachama wapya 60 wa Kata ya Nkowe Wilayani Ruangwa, kutoka Chama cha Wananchi (CUF) ambao wameamua kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM). Desemba 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Sister Nelly Membe wa Shirika la Bikira Maria Msaada wa Wakristu la Ndanda,katika Kata ya Nkowe Wilayani Ruangwa, Desemba 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Sister Mfurahishi Choaji wa Shirika la Bikira Maria Msaada wa Wakristu la Ndanda,katika Kata ya Nkowe Wilayani Ruangwa, Desemba 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akifungua Tawi la vijana wakereketwa wa CCM la Majaliwa Camp,katika Kata ya Nkowe Wilayani Ruangwa, Desemba 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BALOZI SEIF AFUNGUA MKUTANO MKUU WA CCM MKOA WA MAGHARIBI

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi amesema wakati umefika kwa Wananchama wa Chama cha Mapinduzi kutowapa nafasi za Uongozi wanachama wenye tabia ya kuhama Jimbo moja na kuhamia Jimbo jengine.

Alisema Wanachama hao hufikia uamuzi wa kuyakimbia Majimbo yao ya zamani na kutaka kuhamia majimbo mapya baada ya kujibaini kutowatumikia vyema Wanachama na Wananchi wao katika kipindi walichoomba ridhaa ya kuwawakilisha katika nafasi za Ubunge na Uwakilishi kwenye vipindi vya awali.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Magharibi wa kuwachagua Viongozi watakaouongoza Mkoa huo kwa kusaidiana na viongozi wengine katika kipindi cha Miaka Mitano ijayo 2017 – 2022 ambao ulifanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Alisema uzoefu umebainisha wazi kwamba Wawakilishi na Wabunge wanaoendelea na majukumu yao ndani ya Majimbo yao hukumbwa na matatizo ukiwemo ushawishi, fitna na majungu yanayobuniwa na wale wanaotaka nafasi hizo jambo ambalo huchangia kukosekana kwa uwajibikaji.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Viongozi wa CCM Mkoa Magharibi alipofika kuufungua Mkutano wao wa Uchaguzi uliofanyika katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni.
Balozi Seif akiufunguza Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Mkoa wa Magharibi wa kuwachaguwa Viongozi wao wa kuwaongoza katika kipindi cha miaka Mitano ijayo kuanzia 2017 – 2022.
Baadhi ya Wajumbe wa Makutano Mkuu wa CCM Mkoa Magharibi wakiwa katika mchakato wa kuwachagua Viongozi wa Kuuongoza Mkoa huo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Baadhi ya Wajumbe wa Makutano Mkuu wa CCM Mkoa Magharibi wakiwa katika mchakato wa kuwachagua Viongozi wa Kuuongoza Mkoa huo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Mwenyekiti WA CCM Mkoa Magharibi aliyemaliza Muda wake Nd. Yussuf Mohad Yussuf akitoa nasaha na kuwashukuru wanachama na Viongozi wa Mkoa huo alioshirikiana nao na kumuwezesha kutekeleza majukumu yake katika muda wake wa utumishi wa Miaka 15 kwenye nafasi hiyo. Picha na – OMPR – ZNZ.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU AMWAGIZA AFISA MADINI AITISHE KIKAO KESHO SAA 4 ASUBUHI

$
0
0
 *Ni baada ya kupokea mabango ya wananchi wakidai kunyanyaswa
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Kanda ya Kusini, Bw. Ogesa Charles Tale afike eneo la mgodi wa dhahabu wa Namumgo na kuitisha kikao cha wananchi kesho (Jumapili) saa 4 asubuhi.

“Sasa hivi natoka kwenda Matambare, twende wote, lakini kesho saa 4 asubuhi uje hapa Namungo, uitishe mkutano wa hadhara na uwasikilize hawa wachimbaji wadogo na kisha uniletee maelezo ofisini kwangu,” alisema. 

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumamosi, Desemba 30, 2017), wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Namungo, wilayani Ruangwa baada ya kupokea mabango mawili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo. Waziri Mkuu yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka, na ameamua kukagua miradi ya maji, ujenzi wa zahanati na kuzungumza na wananchi katika wilaya hii.

Waziri Mkuu alisema Serikali ya awamu ya tano imejikita kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi na alipomuuliza afisa huyo kama ameshawahi kupata nafasi ya kuwasikiliza wachimbaji wadogo, alijibiwa kwamba hajawahi kufanya hivyo.

“Hawa ndiyo nguvukazi ya mgodi, hawa ndiyo wanaingia kule chini kuchimba udongo, hawa ndiyo wanapata machungu ya kazi ya uchimbaji, kwa hiyo uje uwasikilize na uniletee taarifa kesho mchana,” alisisitiza.

Baada ya kuyasoma mabango yao, Waziri Mkuu aliwaita wakazi ambao waliyaleta mabango hayo na kuwataka waeleze kwa undani ni matatizo gani yanayowakabili. Bango la kwanza lilisema wananchi wananyanyaswa na viongozi kwa maslahi binafsi ya viongozi na la pili lilisema wamekatazwa wasiseme matatizo yao kwenye mkutano huo wa Waziri Mkuu.

Mkazi wa kijiji cha Mtondo, kata ya Nambilanje, Bw. Mussa Omari Kimatilo, alisema wananyanyaswa na uongozi wa kijiji pamoja na uongozi wa wenye machimbo ya dhahabu na kwamba wananyimwa uhuru wa kujieleza kila wanapokutana na viongozi hao.

“Tunanyanyaswa na uongozi wa machimbo, tunanyanyaswa na uongozi wa kijiji na tukilalamika hakuna wa kutusikiliza. Tumekaa na Rajani (mmiliki wa mgodi) amekubali kutulipa lakini wananchi hatuna uhuru wa kujieleza,” alisema.

Alidai hata Naibu Waziri wa Madini alipotembelea mgodi huo mapema mwezi huu, hakupewa fursa ya kukutana na wachimabji wadogo, na badala yake alipitishwa kijijini hapo na kuingizwa mgodini kisha akaondoka.

Naye Bahati Mikael, mkazi wa kijiji cha Namungo alisema kumekuwa na ukiritimba wa kutoa leseni kuhusu mgodi huo na kwamba tangu ilipotolewa rasmi mwaka 2014, bado hawajalipwa malipo yao.

“Hapa pana ukiritimba wa kutoa leseni ya uchimbaji. Mwekezaji amekuwa akichimba kinyemela; tangu mwaka 2006 alikuwa hajapewa leseni hadi mwaka 2014 ndipo alipopewa,” alisema.

Alipoitwa na Waziri Mkuu atoe ufafanuzi juu ya madai ya wakazi hao, Kaimu Afisa Madini wa kanda hiyo alisema eneo wanalodai wakazi hao ni la Mzee Kishor Rajani na inaeleweka hivyo na kwamba miaka ya nyuma walichimba kwa maelewano tu bila mikataba yoyote.

“Yale ya nyuma yalishapita kwa sababu hamkuwa na mkataba naye, mlifanya naye kazi kwa makubaliano ya mdomo tu. Sasa hivi mmeanza kuwekeana mikataba, zamani alikuwa anachukua asilimia kubwa lakini sasa hivi anachukua asilimia 17.5 na inayobaki amewaachia ninyi,” alisema Bw. Tale.
Waziri Mkuu anaendelea na ziara ya jimboni kwake.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMAMOSI, DESEMBA 30, 2017.​

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAKANUSHA TANGAZO LINALOTANGAZA USHIRIKI WA MAKAMU WA RAIS KUPANDA MITI TAREHE 1-1-2018

$
0
0
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakanusha tangazo linalosambaa katika Mitandao ya Kijamii linalomhusisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  kuwa atashiriki zoezi la kupanda miti kwenye Chuo Kikuu Cha Dodoma siku ya tarehe 1-1-2018. Ofisi ya Makamu wa Rais inapenda kuujulisha umma kuwa tangazo hilo si la kweli na Makamu wa Rais hana ratiba ya kupanda miti kwenye chuo hicho kwa tarehe iliyotajwa.

Ikumbukwe kuwa siku ya tarehe 15-12-2017 wakati wa hafla ya kuhamia Makao Makuu ya Nchi, Makamu wa Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alitangaza kampeni ya kupanda miti Dodoma ambayo itaratibiwa na Ofisi yake .

Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka Wananchi kuzingatia matangazo, taarifa na ratiba zitakazotolewa na Ofisi yake kuhusu programu ya upandaji miti Dodoma.

Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dodoma
30 Desemba, 2017.

TRA KUMCHUNGUZA ASKOFU KAKOBE

UFAFANUZI JUU YA MICHANGO KWA WANACHAMA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)

MAGAZETI YA JUMAPILI LEO DECEMBER 31,2017

Vituo vya Afya vinavyojengwa vinahitaji wataalam wa Dawa za Usingizi - Waziri Jafo

$
0
0
Ntegenjwa Hosseah, Mpwapwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amesema vituo vyote 211 vinavyoongezewa miundombinu ya Afya vinahitaji wataalam wa kutoa Dawa za Usingizi ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa watakaofikishwa katika chumba cha Upasuaji pamoja na Wodi ya Kinamama.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya Kikazi Wilayani Mpwapwa na kukagua miradi ya maendeleo iliyompelekea kufika katika ujenzi wa miundombinu ya Afya inayojengwa katika Kituo cha Afya Mima.

Akiwa kituoni hapo alisema ameridhishwa na ujenzi wa miundombinu hiyo ambapo hii ya awamu ya kwanza itakamilika mapema Mwezi Januari 2018 lakini anaona uhitaji wa wataalam wa kutoa Dawa za Usingizi ambao watatoa huduma hizo wakati wa upasuaji na huduma nyingine muhimu.

“Nataka vituo hivi vinapokamilika vianze kufanya kazi mara moja na sio zianze sababu mara wataalamu Fulani hakuna hiki bado sitapenda kusikia hayo ni vyema kwa sasa kila Mkurugenzi wa halmashauri ahakikishe anabainisha wataalam angalau wawili ambao watakwenda kupata mafunzo mafupi ya utoaji wa Dawa hiyo ya Usingizi wakati wa Upasuji”.

Mpaka sasa nimeridhishwa kabisa na kasi ya Ujenzi wa vituo hivi vya Afya na kwa sababu vifaa Tiba pia tunapata kutoka Bohari Kuu ya Dawa sasa kwa pamoja tuangalie maeneo mengine ambayo yataenda sambamba na utoaji wa huduma katika vituo hivi kama wataalamu hawa ambao kwa Takwimu zilizopo kwa sasa bado ni wachache na baada ya ukamilishwaji wa vituo hivi Uhitaji Utakua Mkubwa zaidi alisema Waziri Jafo.

Awali akitoa Taarifa ya Ujenzi Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Space East Africa iliyopewa Kazi ya Kujenga Kituo cha Afya Mima Gaston Francis amesema kampuni hiyo hujenga kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa iitwayo “Pre-Fabricated Material” ambayo ni nafuu zaidi na ina ubora wa hali ya juu hivyo kwa gharama hiyo ya Mil 500 watajengwa majengo saba huku yakiwa na thamani zote zinazohitajika “Full furnished”.

Aina hii ya Teknolojia hutumika sana maeneo yenye vimbunga, upepo Mkali na Dhoruba mbalimbali na kwa sababu eneo hili la Mima linaathiriwa sana na wadudu Material hii tunayotumia itaenda kuwa suluhisho la kudumu la wadudu hao kwa sababu hawataweza kuathiri hata eneo moja na majengo tutakayojenga na ubora wa material hizi tunazotumia zinadumu kwa Zaidi ya miaka sabini alisema Francis.

Awali katika ziara yake Waziri Jafo alianza kwa kutembelea ujenzi wa barabara ya Lami ( Km 1 ) iliyojengwa kuanza NMB Mpwapwa mpaka Stendi ya Mpwapwa, kukagua Mradi wa Maji Mima pamoja na kuzungumza na wananchi wa Mima kwenye Mkutano wa hadhara.
Mbunge wa Mpwapwa Mhe. George Malima Lubeleje(kushoto) akielezea Umuhimu wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa hivi katika sasa kwa Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (kushoto) akimskiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Space East Africa Gaston Francis(Kulia) namna wanavyojengwa kwa kutumia Teknolojia ya “Pre Fabricated Material’.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(kushoto) akikabidhiwa kitendea kazi ili aweze kushiriki kwenye Ujenzi wa Kituo cha Afya kwa kutumia Teknolojia ya “Pre Fabricated Material”.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(aliyeinama) akishiriki kukata chuma kitakachotumika katika ujenzi wa jengo la Maabara kwa kutumia Teknolojia ya “Pre Fabricated Material”.
Hili ni moja ya Jengo lililojengwa katika Kituo cha Afya Mima kwa Kutumia Teknolojia ya “Pre Fabricated Material” linalojengwa na Kampuni ya Global Space East Africa.

KOMBE LA MAPINDUZI: JKU YAICHAPA ZIMAMOTO BAO 1-0 UWANJA WA AMAAN ZANZIBAR

$
0
0
Mshambuliaji wa Timu ya Zimamoto, Hafidh Barik akipokea mpira huku beki wa Timu ya JKU, Ponsiana Malik akijiandaa kumzuiya wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar jana, Timu ya JKU imeshinda bao 1-0.
Wachezaji wa Timu ya JKU na Zimamoto, Ponsiana Malik na Amour Haji, wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya JKU imeshinda bao 1- 0(Picha na Othman Maulid).

BILIONI 1. 8 ZITATUMIKA UJENZI WA MRADI WA MAJI SAWALA – HALMASHAURI YA MUFINDI

$
0
0
Waziri wa Maji na umwagiliaji Mh. Mhandisi Isack Kamwelwe, amewahakikishia wananchi wa kata ya Mtwango halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kuwa, mradi mkubwa wa Maji wa Sawala wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja, utaanza kujengwa mapema mwezi januari mwakani mara baada ya kukamilika kwa taratibu za kutiliana saini na mkandarasi mteule.

Waziri huyo mwenye dhamana ya Maji nchini, ametanabaisha hilo wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Mufindi, iliyokuwa na lengo la kukagua maendeleo ya miradi ya Maji inayotekelezwa Wilayani humo.

Waziri Kamwelwe, amesema baada ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya kukamilisha taratibu zote za manunuzi na kumpata Mkandarasi atakaye tekeleza mradi huo, Ofisi yake inakamilisha uhakiki wa mkataba na ifikapo mwezi wa kwanza mwaka 2018, itatoa kibali kwa Ofisi ya Mkurugenzi ili aendelee na hatua ya mwisho ya kusaini kandarasi hiyo yenye jumla ya shilingi bilioni (1.8).

Mradi wa Maji wa Sawala unatarajiwa kujengwa na kukamilika kwa muda wa kipindi cha miezi (12) huku wakazi wa Vijiji vinne vya Mtwango, Kibao, Sawala na Lufuna ndio watakao nufaika na mradi huu, ikiwa ni utekelezaji wa shabaha ya Serikali inayokusudia kutatua kero ya Maji kwa asiliamia (85) kwa wakazi wa Vjijini ifikapo mwaka 2020.
Waziri wa Maji na umwagiliaji Mh. Isack Kamwelwe, akizungumza na Viongozi wa Wilaya ndani ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi kabla ya kuanza ziara ya kutembelea miradi ya Maji.
Waziri wa Maji na umwagiliaji katikati akilakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William kusho pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mufindi Prof. Riziki Shemdoe kulia, mara baada ya kuwasili Wilayani humo.

DKT MNDOLWA,MAJI MAREFU WAUNGURUMA UZINDUZI WA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA KWAGUDA KOROGWE, WAWATAKA WANANCHI KUIPA KURA ZA KISHINDO CCM

$
0
0
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mkokola Kata ya Kwagunda mara baada ya kuwasili kuzindua kampeni za udiwani kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Korogwe Vijijini.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa akisaliana na wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni hizo mara baada ya kuwasili kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Allan Kingazi
Meza kuu katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa akiangalia vikundi vilivyokuwa vikitoa burudani wakati wa uzinduzi huo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Korogwe Mjini,Charles Emanuel na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu na MNEC na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa akizugumza katika uzinduzi wa kampeni hizo ambapo aliwataka wananchi aliwataka kumchangua mgombea wa CCM kwani anafahamu changamoto zao na hivyo itakuwa rahisi kuweza kuzipatia ufumbuzi.

WATALII WA NJE NA NDANI WAENDELEA KUMIMINIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

$
0
0
Serengeti - Idadi ya watalii wanaotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti(Senapa) imeongezeka katika siku za hivi karibuni kutokana na sekta ya utalii kukua huku miundombinu ya barabara na viwanja vidogo vya ndege vilivyopo ndani ya hifadhi hiyo kufanya kazi vizuri.

Afisa Utalii wa Senapa,Evance Magomba alisema kuwa baada ya kujengwa jengo dogo la wageni wanaowasili na wanaoondoka katika uwanja mdogo wa ndege wa Seronera idadi ya wageni imeongezeka huku wakala wa makampuni ya ndege wakiweka wawakilishi wao katika uwanja huo.

Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa katika kipindi cha Januari hadi Septemba mwaka huu kumekua na safari za ndege 3,724 katika uwanja wa Seronera huku uwanja wa Lobo katika kipindi hicho ni safari 349 na uwanja wa Kogatende safari 564.

Alisema ndani ya hifadhi hiyo kuna viwanja vidogo vya ndege saba kikiwemo cha Seronera ambacho ni kikubwa zaidi chenye uwezo wa kupokea ndege kubwa yenye uwezo wa kubeba abiria 60 ikiwemo ya shirika la Precision Air inayofanya kazi mara nne kwa wiki.

“Miaka miwili iliyopita hatukua na jengo hili la abiria naamini pamoja na sababu nyingine limekua kishawishi kwa wageni kuongezeka kwani linawawezesha kuwa na sehemu nzuri ya kupumzika kabla ya kuanza safari zao,”alisema Magomba

Alisema kutokana na ukubwa wa hifadhi hiyo wanavyo viwanja vingine vilivyosambaa maeneo mbalimbali ili kutoa huduma kwa urahisi na kuwawezesha watalii kupata muda mzuri wa kutembelea vivutio zaidi.

Magomba alivitaja viwanja vingine kuwa ni Kogatenda,Lobo,Ndutu,Kirawira ,Fort Ikoma na Lamai ambavyo hutumika kwa malengo ya kurahisisha kufika eneo husika na kulingana na watalii wanapenda kuona vivutio maalumu.

“Hifadhi ya Serengeti ina uwezo wa kupokea wageni wa aina zote na zipo huduma za malazi zikiwemo hoteli saba,makambi ya kudumu sita na makambi ya muda zaidi 140 yaliyosambaa na kipekee tuwakaribishe wananchi kutembelea hifadhi zetu kwasababu zipo bei maalumu kwaajili yao,”alisema Magomba

Dereva wa kampuni ya kitalii ya Micato Safaris,Emmanuel Lema alisema huduma za kitaalii nchi zimekua kwa kasi baada ya serikali kupitia Bodi ya Utalii(TTB),shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa) na wadau wengine wa utalii kutangaza kwa kiwango kikubwa sekta ya utalii.

Alishauri Tanapa kuongeza ukubwa wa jengo la wanaowasili na kuondoka na huduma zingine muhimu ili kuwawezesha watumiaji wa jengo hilo kupata huduma za kiwango cha juu hasa wakati wa msimu wa utalii.

Watalii wakiwasili uwanja mdogo wa ndege wa Seronera wilayani Serengeti mkoa wa Mara ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,kukamilika kwa jengo la wageni wanaowasili na wanaondoka kumerahisisha huduma za usafiri ndani ya hifadhi hiyo. 
Afisa Utalii Mwandamizi wa Hifadhi ya Taifa Serengeti mkoa wa Mara,Susuma Kusekwa akizungumza na watalii waliotembelea hifadhi hiyo. 
Watalii wakimsikiliza Zacharia Mathayo ambaye ni mwongoza watalii wakati akitoa maelezo kuhusu uhamaji wa wanayamapori aina ya Nyumbu kutoka Kaskazini mwa Hifadhi ya Taifa Serengeti hadi Kusini. 

Watalii hufurahia kuona wanyama wakubwa wakiwemo Tembo na wengine wanaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti.

MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 6.8 KUKAMILISHA UJENZI WA WODI YA WAZAZI ZAHANATI YA SOLWA

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad (CCM) (wa pili kushoto) amekabidhi hundi ya shilingi Milioni 6.8 ( 6,830,000/=) kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi katika zahanati ya kijiji cha Solwa kilichopo kata ya Solwa jimbo la Solwa mkoani Shinyanga. mAkizungumza Jumamosi Desemba 30,2017 wakati wa kukabidhi hundi hiyo kwa kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo, alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa alipotembelea zanahati hiyo mwezi Mei mwaka huu na kukuta changamoto ya uhaba wa vyumba vya kutolea huduma za afya ikiwemo wodi ya watoto na akina mama. 

“Nilifanya ziara katika zanahati hii mwezi Mei mwaka huu wakati natoa vitanda vya kujifungulia na viti vya wagonjwa,baada ya kuingia katika chumba cha akina mama nilikuta vitanda vitatu,niliguswa na jinsi akina mama walivyokuwa wanahangaika,lakini nikaambiwa wananchi wana mpango wa kujenga wodi ya watoto na akina mama,nikaahidi kuchangia mabati 20 pindi majengo yatakapofikia hatua ya upauaji”,alieleza mbunge huyo. 

“Mwezi Septemba mwaka huu, Diwani wa kata ya Solwa alinitumia picha za majengo mawili yakiwa tayari kwa upauaji, nikawaza kuhusu mabati yangu 20, nikaona hayatoshi, ndipo nikaamua kuanza kutafuta watu wa kunisaidia, juzi nikapokea ujumbe kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF kuwa wamekubali ombi langu na wameamua kutoa shilingi 6,830,000/= kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo moja”, alieleza. 

Alisema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kununua mabati na mbao pamoja shughuli zingine katika kukamilisha ujenzi wa jengo la wodi ya akina mama katika zahanati ya Solwa iliyojengwa kwa michango ya wananchi wa kijiji cha Solwa. 

“Niwapongeze sana watu wa Solwa kwa kuamua kuchangishana na kuanza ujenzi, Solwa itajengwa na Wana Solwa,hili ni jibu tosha kabisa kwamba kila kilio kina mwenyewe,mlichokifanya kinapaswa kuigwa katika maeneo mengine,niwashukuru sana pia NSSF kwa kunishika mkono ili kuokoa maisha ya akina mama na watoto”,aliongeza Azza Hilal Hamad. 

Hata hivyo aliwataka wananchi wa Solwa kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili iwe na manufaa kwa wananchi. 

Mbunge huyo alitumia fursa hiyo pia kuwakumbusha wazazi na walezi kupeleka watoto shule badala ya kuwaozesha wangali wadogo kwa tamaa ya mali huku akisisitiza kuwa urithi mzuri kwa mtoto ni elimu pekee. 

“Ni marufuku kuozesha watoto wa kike wanafunzi,matokeo ya darasa saba yametoka,wote waliofaulu wapelekwe shule,waliofeli nao watafutieni kazi zingine za kufanya siyo kuwaozesha,kufeli shule siyo kufeli maisha”,aliongeza. 

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kijiji Solwa, George Bushiya alisema baada ya wananchi kukerwa na adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya walikubaliana kuchangishana fedha ili kujenga majengo ya wodi ya watoto na akina mama ambapo zaidi ya shilingi milioni 36 zimetumika mpaka sasa. 

Kaimu Mganga Mkuu wa halmashauri ya Shinyanga, Dk. Salim Matondo alimshukuru mbunge huyo kwa kusaidia ujenzi wa wodi ya akina mama ambapo pindi ujenzi utakapokamilika itasaidia kupunguza adha ya akina mama kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya katika hospitali ya Nindo na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga. 
Muonekano wa majengo mawili yaliyojengwa na wananchi wa kijiji cha Solwa yatakayotumika kama wodi ya watoto na akina mama katika zahanati ya Solwa iliyopo katika kijiji cha Solwa,kata ya Solwa,jimbo la Solwa mkoani Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati wa kukabidhi hundi ya shilingi Milioni 6.8 ( 6,830,000/=) kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi katika zahanati ya kijiji cha Solwa kilichopo kata ya Solwa jimbo la Solwa mkoani Shinyanga. 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akimsalimia mama aliyejifungua mtoto wa kike mara baada tu ya mbunge kufika katika zanahati hiyo.Mama huyo alikuwa amepewa rufaa ya kwenda kujifungulia katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga,lakini kutokana na Kaimu Mganga Mkuu wa halmashauri ya Shinyanga,Dk. Salim Matondo kuhudhurika kikao cha mbunge,ndiyo ikawa fursa nzuri kwa mama huyo kupewa huduma na Daktari huyo 
Mbunge Azza Hilal Hamad akiwa amembeba mtoto aliyepewa jina la "Azza" 
Mbunge Azza Hilal Hamad akifurahia jambo baada ya kumpatia zawadi ya vitenge mama aliyejifungua mtoto wa kike katika zahanati ya Solwa. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images