Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

Tigo Yapata Mamilionea Wapya wa Mwaka Mpya 2018

0
0
Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta (kulia) akiongea kwa njia ya simu na moja wa washindi wa promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde iliyofanyika usiku wa kuamkia mwaka mpya katika ofisi za Tigo ambapo Lugano Thomas Mlimi wa Dar es salaam, Kulthum Salim Ally wa Ruvuma na Maria Josef Maligisa wa Lindi walijinyakulia shilingi milioni 15, milioni 10 na milioni 5 katika promosheni hiyo. Katikati ni Meneja wa Mapato wa Tigo, Arnold Ngakashi na kushooto ni Mwakilisi wa Bodi ya Michezo ya Bahati na Sibu Tanzania, Ally Abdallah.

‘Nimeanza mwaka mpya nikiwa milionea!’ alisema Lugano Thomas Mlini, ambaye ni dereva na mkaazi wa Mbezi Makonde, jijini Dar es Salaam alipotaarifiwa kuwa amejishindia shilingi milioni 15 kutoka Tigo.

Kupitia huduma yake ya Tigo Pesa, kampuni ya simu inayoongoza ya Tigo imewageuza Watanzania watatu kuwa matajiri wapya kwa mwaka 2018.

‘Ndoto zangu za kuanzisha biashara sasa zimetimia! Ahsanteni sana Tigo’ alisema Kulthum Salim Ally, mkulima na mkaazi wa Tunduru, Ruvuma ambaye naye alijinyakulia kitita cha shilinigi 10 milioni katika drooo kabambe ya promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde iliyofanyika siku ya mkesha wa kuamkia mwaka mpya, katika ofisi ya makao makuu ya Tigo jijijni Dar es Salaam.

‘Nilienda kulala nikiwa maskini na sasa nimeamka nikiwa tajiri’ alisema Mariam Josef maligisa, Mkulima na mkaazi wa Nagangu, Lindi aliyeamka kutoka usingizini ili kupokea simu yake na kutaarifiwa kuwa naye amejishindia TSH 5 milioni kutoka Tigo.

Akitangaza washindi katika droo hiyo ya kuukaribisha mwaka mpya, Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema, ‘Tigo pesa ni zaidi ya huduma ya kufanya malipo. Ni sehemu ya maisha. Kwa hiyo leo tumewawezesha wateja wetu kutumiza ndoto zao za msimu wa sikukuu na Mwaka Mpya kupitia huduma ya Tigo Pesa.

Alibainisha kuwa Tigo imetoa jumla ya shilingi 120 milioni kwa watu 153 kutoka maeneo mbali mbali ya nchi. Wateja walishinda zawadi nono za kila siku baada ya kutumia huduma ya Tigo Pesa. ‘Pia tunajivunia mchango wetu katika kufanikisha upatikanaji wa huduma za kifedha nchini. Kupitia Tigo Pesa, tunawawezesha mamilioni ya Watanzania kutuma na kupokea zaidi ya TSH 1.7 bilioni kila mwezi. Hii inawawezesha wateja wenyewe pamoja na jamii, huku ikichangia ukuaji wa uchumi wa nchi,’ aliongeza.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Masoko wa Tigo, Willima Mpinga alisema kuwa,’Tigo inawatakia Watanzania wote Mwaka Mpya wenye furaha na mafanikio. Tigo ni mtandao unaowaelewa zaidi wateja na kujibu mahitaji ya soko. Tulizindua promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde kwa dhumuni kuu la kuwawezesha wateja wetu kushinda pesa zitakazowawezesha kutimiza malengo yao ya mwisho mwaka.’

Tigo Pesa ni huduma ya kifedha kwa njia ya simu ya pili kwa ukubwa nchini. Tigo Pesa ina mtandao mpana zaidi wa wakala na watoa huduma zaidi ya 70,000 waliosambaa nchini kote. Tigo Pesa pia ilikuwa ndio huduma ya kwanza Afrika Mashariki iliyowezesha wateja kutuma fedha kwenda nchi nyingine kwa kutumia viwango na fedha za nchi husika.

Tigo ndio kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ikijivunia huduma bora za sauti, SMS, intaneti yenye kasi ya juu zaidi ya 4G iliyosambaa katika miji 24 nchini, pamoja na huduma za kifedha. Mtandao wa Tigo pia ni maarufu kwa promosheni na ofa zake bunifu kwa wateja. Tigo ilianza kutoa huduma zake Tanzania mwaka 1995 na kwa miaka mitatu sasa ndio kampuni ya simu inayokua kwa kasi zaidi nchini. Kwa sasa Tigo ndio kampuni ya simu ya pili kwa ukubwa nchini ikiwa na wateja zaidi ya 11.6 milioni.

ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO LAONGEZEWA MUDA WA MWEZI MMOJA

0
0
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina(wa pili kushoto) akipiga chapa ng’ombe katika hitimisho la zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa katika Kijiji cha Migato, Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.

Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina ameongeza muda wa mwezi mmoja kwa Halmashauri hapa nchini kukamilisha zoezi la upigaji chapa mifugo na kuwataka watendaji wote wa Serikali wanaohusika kuhakikisha mifugo yote inapigwa chapa.

Waziri Mpina ameyasema hayo wakati wa kuhitimisha zoezi la upigaji chapa Kitaifa katika Kijiji cha Migato wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, zoezi ambalo lilianza rasmi Kitaifa mwezi Desemba, 2016 na kupangwa kukamilika Desemba 31, 2017.

“Kwa kuwa hadi sasa zoezi hili limetekelezwa kwa asilimia 38.5 kutokana na sababu mbalimbali, Mimi Luhaga Mpina Waziri wa Mifugo na Uvuvi kwa Mamlaka niliyopewa chini ya sheria ya Utambuzi, Usajili na ufuatiliaji wa mifugo ya mwaka 2010 na kanuni yake, ninaongeza muda wa kupiga chapa mifugo kutoka tarehe 01/01/ 2018 hadi 31/01/2018”alisititiza.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi (wa tatu kushoto) akipiga chapa ng’ombe katika hitimisho la zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa katika Kijiji cha Migato, Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu ambalo limehitimishwa na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina.

Mpina amesema miongoni mwa changamoto zilizopelekea Halmashauri nyingi kushindwa kutekeleza zoezi hilo kwa asilimia 100 ni baadhi ya halmashauri kutokutenga fedha kwa ajili ya zoezi hilo, kubaini mifugo kutoka nje ya nchi, baadhi ya wafugaji kushindwa kutaja idadi halisi ya mifugo yao na baadhi ya Halmashauri kuwatoza wafugaji zaidi ya shilingi 500 ambayo ndiyo bei elekezi, ambapo ameagiza wafugaji hao waliotozwa zaidi ya shilingi 500 warejeshewe fedha zao.

Ameongeza kuwa hadi kufikia Desemba 31, 2017 Halmashauri 30 hapa nchini hazijapiga kabisa chapa mifugo, halmashauri 23 zimeendesha zoezi hilo chini ya asilimia 10 na akaongeza kuwa orodha ya majina ya viongozi wa wilaya hizo walioshindwa kutekeleza agizo hilo la Serikali ameyawasilisha kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.
Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe.Njalu Silanga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Migato na vijiji jirani mara baada ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa lililofanyika kijijini hapo.

“Halmashauri 30 ambazo hazijapiga chapa kabisa hata ng’ombe mmoja na zile 23 ambazo zimepiga chini ya asilimia 10 majina ya viongozi wote na Halmashauri husika nimekabidhi orodha hiyo kwa Waziri Mkuu, hatuwezi kuendekeza ukaidi wa maagizo ya Viongozi Wakuu wa Nchi” alisema Mpina. Akiwasilisha taarifa ya zoezi la Upigaji Chapa katika Mkoa wa Simiyu, Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa, Ndg.Elias Kasuka amesema zoezi hilo mkoani humo lilianza rasmi mwezi Aprili 2017 ambapo hadi sasa ng’ombe zaidi ya 764, 933 wameshapigwa chapa kati ya ng’ombe 1,500,000.

Milion 6 zatolewa Mlimani City 2017

0
0
Meneja wa Dula la Phone One, Saiyed Shabi lililoko Mlimani City akichagua kuponi ya mshindi wa kwanza wa droo ya tatu ya promosheni ya fanya manunuzi MLIMANI city na ushinde katika msimu wa sikukuu ijulikanayo kama “Mlimani City Grand Fest” iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mlimani City.Wengine waliomzunguka ni mabalozi wa promosheni hiyo.
Moja ya watejawa Mlimani City, Swaibu Swalehe akichagua kuponi ya mshindi wa kwanza wa droo ya tatu ya promosheni ya fanya manunuzi MLIMANI city na ushinde katika msimu wa sikukuu ijulikanayo kama “Mlimani City Grand Fest” iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mlimani City.Wengine waliomzunguka ni mabalozi wa promosheni hiyo.

MWAKA 2017,jumla ya Shilingi milioni 6 zimegawiwa kama zawadi kwa wateja waliofanya manunuzi Mlimani City tangu promosheni ya fanya manunuzi mlimani City na ushinde ijulikanayo kama “Mlimani City Shopping Fest” inayoendelea katika kipindi hiki cha msimu wa siku kuu ya Krismas na Mwaka mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Mlimani City, Pastory Mroso alisema jumla ya wateja 60 mpaka sasa wameshajishindia kila mmoja vocha yenye thamani ya Shilingi 100,000.Tumeshafanya droo tatu mpaka sasa na kila droo tulikuwa tunatoa washindi 20, ambapo kila mmoja alijishindia vocha yenye thamani ya shilingi 100,000 ambapo jumla ya zawadi mpaka sasa ni shilingi milioni 6 tangu kampeni hii ianze.

Alisema Mroso, ni rahisi sana kushinda, ni wewe kuja mlimani City na kufanya manunuzi kwenye duka lolote na kwa bidhaa yoyote ukitumia kiasi cha shilingi 100,000 au zaidi utapewa kuponi ambayo itakuwezesha moja kwa moja kuingia kwenye droo ya kushindania zawadi ya vocha yenye thamani ya shilingi laki moja ambayo itakuwezesha kwenda kufanya manunuzi tena duka lolote la ndani ya Mlimani City.

Wewe ambaye hujashiriki nafasi unayo bado kuna droo mbili mbele njoo ufanye manununuzi Mlimani City katika katika kipindi hiki cha sikuu ya Krismas na mwaka mpya na ushinde.Tunayo droo ya kubwa ya mwisho ambayo mshindi mmoja atajishindia vocha yenye thamani ya milioni 10 na washindi wengine watano watajishindia vocha yenye thamani ya milioni moja kila mmoja.

AMSHA KIPAJI CHAKO NA ZAX 4REAL KWA KUFUNGA NA KUINGIA MWAKA MPYA WA 2018

TAARIFA YA KIFO CHA MTANGAZAJI LIMONGA JUSTINE LIMONGA WA UHURU FM

MAGAZETI YA JUMATATU LEO JANUARY 2,2018

VOA Swahili: Matukio muhimu duniani 2017

NGOMA AFRICA BAND YAWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2018

0
0
 Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani inawatakia wadau wote popote mlipo heri ya mwaka mpya 2018. Inawaombea amani,upendo na mshikamano. Happy New Year  2018.


ASKOFU MKUU WA KANISA LA METHODISTI NCHINI AFARIKI

0
0
Askofu Mkuu wa kanisa la Methodisti nchini, Dk. Mathew Byamungu, amefariki ghafla usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Taarifa iliyotolewa na katibu wa kanisa la Methodisti, Askofu, Yusuf Bundala, ambaye pia ni askofu wa jimbo la Dodoma, imeeleza kuwa alipelekwa hospitali ya Muhimbili akitokea TMJ baada ya kujisikia vibaya kutokana na maradhi ya kisukari ambao alikuwa akisumbuliwa nao kwa muda mrefu na kufariki kabla ya kuanza kupatiwa matibabu. Mipango ya mazishi inaendelea kufanyika katika kanisa kuu la Methodisti la Msasani mkabala na Shoppers plaza atazikwa Januari 4,2018 katika eneo la Kanisa la Methodisti la Boko. 

Marehemu Byamungu alizaliwa mwaka 1954 mkoani kagera , alipata elimu ya msingi katika shule ya Kazilanfuka, sekondari (Kahororo na Mkwawa) , mafunzo ya ualimu katika chuo cha Chang’ombe jijini Dar es Salaam na baada ya kuhitimu alifundisha katika sekondari ya Azania jijini Dar es Salaam. 

Kati ya mwaka 1981-1984 alijiunga na Chuo Kikuu cha Asia Centre for Theological na kupata shahada ya kwanza ya Theolojia na baada ya kuhitimu alirudi nchini na kufanya kazi ya uinjilishaji katika shule za sekondari na vyuoni jijini Dar es Salaam. 

Mnamo mwaka 1987-1989 alikuwa Mchungaji wa kanisa la KKKT ambapo alitoa huduma katika makanisa ya Tabata na Mburahati na akiwa mchungaji wa kanisa hilo alianzisha kituo cha watoto yatima cha Calvary Cross Christian Centre -eneo la Boko jijini Dar es Salaam. 

Mnamo mwaka 1990-1991 alisoma shahada ya pili ya Theolojia katika chuo kikuu cha Hyup Sung. Mnamo mwaka 2009 alitunikiwa Shahada ya Udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Latin California cha Marekani. 

Mwaka 1991 alisimikwa kuwa mchungaji wa kanisa la Immanuel Methodist la nchini Korea na alipangiwa kuja kufanya kazi ya uinjilishaji nchini Tanzania, kazi ambayo aliifanya kwa ufanisi mkubwa na kufanikiwa kulisajili tawi la kanisa hilo nchini na kulibadilisha jina kutoka jina la awali la Tanzania Christian Methodist Church (TCMC) kuwa Tanzania Methodist Church (TMC) na kuongeza idadi ya waumini na makanisa ya Methodisti katika kipindi cha muda mfupi. 

Mnamo mwaka 2003 alisimikwa kuwa askofu wa kwanza wa kanisa hilo nchini nafasi aliyoendelea kuitumikia hadi mwaka 2009 alipoteuliwa kuwa askofu Mkuu nafasi aliyokuwa nayo hadi kifo chake. Ameacha mke Jae-Young Ryu,ambaye pia ni Mchungaji Kiongozi na watoto wawili 

Dk. Bya Mungu ataendelea kukumbukwa kwa kuasisi kanisa la Methodisti nchini na kuliendeleza ambapo chini ya uongozi wake limeweza kukua na kuwa na makanisa zaidi ya 30 nchini pia kanisa linashiriki kutoa mchango wa kuendeleza huduma za jamii kupitia sekta ya elimu na afya ambapo linaendesha shule na vituo vya afya na imekuwa ni kituo cha huduma ya mtoto (Compassion). 

Mbali na kufanya jitihada kubwa za kuendeleza kanisa la Methodisti nchini, Askofu Bya Mungu aliona kuna umuhimu wa kuwa na viongozi wa kanisa wenye elimu na weredi ambapo chini ya uongozi wake kanisa lilianzisha chuo cha kutoa elimu kwa wachungaji na watumishi wa kanisa hilo kilichopo mjini Arusha , Alikuwa ni mhubiri wa kimataifa ambaye amefanya mahubiri katika nchi mbalimbali duniani na ameweza kuliunganisha kanisa na wadau mbalimbali ikiwemo serikali na taasisi mbalimbali za kimataifa za kidini na zisizo za kidini. 

Marehemu katika uhai wake amekuwa ni kiongozi mnyenyekevu, muadilifu mwenye upendo na ushirikiano kwa watu wa ngazi zote. Ameacha ushuhuda na mfano wa Kuigwa. 

Tunamuinua Mungu na Kumrudishia utukufu kwa zawadi aliyotupatia kwa muda tulioishi naye.

WAZIRI MKUU AMEWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA YA KILIMO CHA KOROSHO

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wanaioishi kwenye mikoa ambayo zao la korosho linastawi wachangamkie kilimo cha zao hilo kwa sababu lina fursa nyingi.

“Mahitaji ya korosho ni makubwa duniani, korosho zinatumika mahotelini na kwenye mikutano mikubwa, zinatumika kwenye ndege, kwa hiyo bei yake lazima iwe kubwa,” alisema.

Ametoa wito huo jana (Jumapili, Desemba 31, 2017) wakati akizindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi. Kaulimbiu ya kampeni hiyo ni: “Korosho ni dhahabu ya kijani, tuitunze, itutunze”.

Waziri Mkuu alisema anaamini kuwa kijana yoyote mwenye nguvu ya kufanya kazi hawezi kushindwa kulima zao hilo kwa sababu halihitaji uangalizi mkubwa. “Kijana yeyote anaweza kulima zao hili kwa sababu ekari moja ina miche 37 hadi 40. Kuna mtu atashindwa kuangalia miche 37 hadi ikue?” aliuliza.

Waziri Mkuu alisema kilimo cha korosho ni rahisi lakini pia kilimo cha korosho ni rafiki wa mazingira, kwani miti ikikua inatunza mazingira na inasaidia kuleta mvua. Alisema mbali ya mikoa inayolima korosho ya Lindi, Mtwara, Ruvuma Pwani na Tanga, kuna mikoa mingine ambayo udongo wake umepimwa na kubainika kuwa zao hilo linaweza kustawi bila shida. Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dodoma, Kigoma, Njombe, Songwe na kuongeza kuwa mikoa ya Singida na Manyara iko mbioni kukamilisha uchunguzi wake.

“Leo tumeanza usambazaji wa miche ya bure hapa Ruangwa ambao najua utafuatiwa na wilaya nyingine hapa nchini. Nimeelezwa kwamba mche wenye kutoa mazao mengi ni wa kuanzia miaka mitatu hadi saba, kwa umri huu miche ya korosho inaweza kuchanganywa na mazao mengine kama ambavyo mtashauriwa na maafisa kilimo ili wakati wa palizi ya hayo mazao, shamba lako la korosho libakie kuwa safi,” alisema.

Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa, yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka jimboni kwake. 

Mapema, akitoa taarifa ya taarifa ya uzalishaji wa miche ya mikorosho msimu wa 2017/18 mkoani Lindi, Katibu Tawala wa mkoa huo, Bw. Ramadhani Kaswa alimweleza Waziri Mkuu kwamba katika msimu wa 2016/2017, mkoa huo uliweka lengo la kuzalisha na kupanda miche 1,000,000 ya mikorosho.

“Hadi mwisho wa msimu huu, jumla miche 716,532 ilizalishwa na kusambazwa kwa wakulima sawa na asilimia 71.6 ya lengo lililowekwa. Kati ya hiyo, Halmashauri ya Kilwa ilizalisha miche 55,000, Halmashauri ya Lindi miche 100,000, Manispaa ya Lindi miche 50,000; Halmashauri ya Liwale miche 106,000; Halmashauri ya Nachingwea miche 227,670 na halmashauri ya Ruangwa miche 177,862,” alisema.

“Miche hii iligawanywa kwa wakulima bure ambao walipanda kwenye mashamba yao. Zoezi la tathmini ya miche iliyokua baada ya kupandwa linaendelea kwenye halmashauri zote za mkoa,” aliongeza.

Bw. Kaswa alisema kutofikiwa kwa lengo hilo kumechangiwa na kutopatikana kwa mahitaji yote ya mbegu na vifaa vya uzalishaji, kuchelewa kwa vifaa, na mwamko mdogo wa vikundi vya uzalishaji. Alisema kwa msimu huu wa 2017/2018, mkoa uliweka lengo la kuzalisha miche ya mikorosho iliyobebeshwa na isiyobebeshwa 7,132,000. Kati ya hiyo, Wilaya ya Kilwa walilenga miche 1,122,000, Lindi Vijijini 1,550,000, manispaa ya Lindi 1,000,000, Liwale miche 450,000, Nachingwea miche 1,810,000 na Ruangwa miche 1,200,000.

“Hadi kufikia tarehe 29 Desemba, 2017 tayari miche 4,974,425 ilikuwa imezalishwa na iko tayari kwa kupandwa kwenye mamlaka za serikali za mitaa kama ifuatavyo:- Kilwa miche 772,000, Lindi Vijijini 1,160,455, manispaa ya Lindi 771,440, Liwale miche 266,000, Nachingwea 991,070 na halmashuri ya Ruangwa imezalisha miche 1,013,460,” alisema.

Sherehe hizo za uzinduzi wa upandaji miche mipya zilihudhuriwa na wakuu wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani na wajumbe wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT). Wakuu wa Wilaya, baadhi ya Wenyeviti wa Halmashauri na wataalamu kutoka kituo cha utafiti cha Naliendele walishiriki uzinduzi huo.

UVCCM YAPONGEZA MIRADI YA AFYA TABORA.

0
0

Na Mwandishi wetu,Tabora

Umoja wa Vijana wa CCM umesema umeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya afya inayotokana na ahadi katika ilani ya uchaguzi katika halmshauri za wilaya mji wa Nzega na Nzega vijijini mkoani Tabora. Pia Umoja huo umeeleza kikubwa kasi hiyo inatokana na kuwepo kwa mashirikiano makubwa kati ya viongozi wa chama,halmashauri za wilaya na serikali kuu.

Matamshi hayo yametamkwa jana na Mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM Kheri Denise james mara baada ya kumaliza kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Kazogolo katika halmashauri ya mji wa Nzege .

Kheri alisema kitendo cha serikali ya awamu ya tano kupeleka jumla ya shilingi milioni mia tano toka serikali kuu oktoba mwaka huu kwa ajali ya ujenzi wa kituo hicho ni kielelezo kuwa serikali inajali maisha ya wetu wake .

"UVCCM tumeridhishwa na ujenzi wa miradi ya afya katika halmashauri za mji wa Nzega na halmashauri ya nzega vijijini.Ilani ya uchaguzi ya chama imetekelezwa kwa vitendo. Hii ndiyo tafsiri halisi ya hapa kazi "Alisems Kheir .Aidha alisema kazi ya kuwatumikia wananchi haina mjadala badala yake inamhitaji kila kiongozi dhamana kuwa nafasi yake kuwajibika na kuwatumikia wananchi.

"Kuimarika kwa huduma za jamii na watu kupata huduma bora ndiyo malengo ya kisera yanayotakiwa kufanikishwa. Tuna wajibu kila mmoja kwa nafasi yake kumsaidia Rais na serikali yale "Alisisitiza  Kheri akiwa mkoani Tabora ametembelea mradi mkubwa wa usambazaji maji toka

ziwa Victoria mkoani mwanza kupitia shinyanga hadi Tabora,kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya kazogolo na kuzumgumza na wananchi katika halmashsuri ya mji wa nzega na nzega vijiijini.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Kheri Denice Jameswa tatu toka kushoto akizungumza jambo na M..mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya shillingi billioni 600 utakaotokea Ziwa Victoria na kunufaisha wananchi wapatao milioni 1.1 wa mikoa ya Shinyanga (vijiji 39) na zaidi Tabora (vijiji 89).


Baadhi ya Vifaa vya Ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya shillingi billioni 600 utakaotokea Ziwa Victoria na kunufaisha wananchi wapatao milioni 1.1 wa mikoa ya Shinyanga (vijiji 39) na zaidi Tabora (vijiji 89).
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Kheri Denice James akitunza fedha katika kikundi cha ngoma ya Asili alipowasili Wilaya ya Nzega Vijijini kuzungumza na Viongozi mbali mbali wa chama.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Kheri Denice James akipata maelezo toka kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nzega Ndugu Amos Kanuda na Mkuu wa wilaya ya Nzega Ndugu Godfrey William Ngupula,alipotembelea kituo cha afya cha Zogolo kilichopo Halmashauri ya mji wa Nzega kinachotegemewa zaidi kuhudumia wananchi wa mji wa Nzega yenye watu wasiopungua laki mmoja. Ujenzi unaolenga kuboresha utoaji wa huduma katika kituo hiki ulikadiriwa kugharimu shillingi milioni 500 ukiwa ni ufadhili wa mfuko wa World Bank.

ZAIDI YA BILIONI 1.2 ZIMETENGWA NA WAKALA WA BARABARA NCHINI TANROAD KWA AJILI YA UJENZI WA BARABARA WILAYANI MKURANGA-ULEGA

0
0
ZAIDI ya shilingi bilioni 1.2 zimetengwa na Wakala wa barabara nchini TANROAD kwa ajili ya Ujenzi wa Barabara kutoka Ulanga hadi Kurungu wilayani mkuranga katika Mkoa Pwani.

Akizungumza na wananchi wilayani humo jana katika mkutano wa hadhara wa kufunga mwaka 2017 na kukaribisha 2018 Mbunge wa Jimbo hilo Abdalla Ulega ambaye pia ni Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi,alisema tayari serikali imeshatenga fedha hizo.

Ulega aliwaeleza wananchi wa jimbo hilo kuwa katika miaka miwili ya uongozi wake yapo mambo mengi ambayo ameyafanya, lakini barabara ni kero kubwa kwa wanamkuranga hivyo katika juhudi zake amefanikiwa kupata fedha hizo kwa ajili ya kuaza ujenzi huo.

"Ndugu zangu wanamkuranga mwanenu napambana kwelikweli kwa maana najuwa niliahidi na nyie mlinituma na mmeendelea kunituma nami staki kuwaangusha, hivyo kuazia January hadi Februari mwaka huu 2018 ujenzi wa barabara hii ambayo nimetaja itaaza ujenzi. "alisema Ulega

Pia aliongeza kuwa anajuwa kwamba changamoto ya barabara imekuwepo kwa muda mrefu na viongozi mbalimbali wamepita lakini aliwaeleza wasubiri utekelezaji wake kuanzia miezi hiyo.  Akizungumzia eneo la afya wilayani humo,Ulega  aliwaeleza wananchi hao kuwa kwa muda mrefu hospitali ya wilaya ilikuwa haina kipimo cha X-ray lakini kwa jitihada zake amefanikisha kupata kipimo hicho na kitakabidhiwa hospitalini hapo hivi karibuni.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akikabidhi kadi ya bima ya Afya kwa mmoja wazee waliokatiwa bima ya afya na Naibu Waziri huyo, Salehe Mgonza katika Mkutano uliofanyika Mkuranga.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwa na viongozi wa chama na serikali akikabibidhi mikokoteni kwa kikundi cha Umoja waendesha mikokoteni wilaya ya Mkuranga.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza juu ushirikiano katika ulinzi na usalama pamoja na kuwapeleka shule wanafunzi wa kuanza darasa la kwanza.

Mganga mkuu Wilaya ya Mkuranga Dkt.Steven Mwandambo (kushoto)akijibu swali mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega picha na Emmanuel Massaka,Globui ya jamii.
Baadhi ya Madiwa wani kwakiwa katika mkutano huu
sehemu ya wananchi wakiwa katika mkutano huu.

WAZIRI MKUCHIKA ATEMBELEA TPSC TAWI LA MTWARA

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika (kushoto) akiwasili chuo cha Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Tawi la Mtwara ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kutembelea matawi ya chuo hicho nchini kulia ni Mkurugenzi wa TPSC Tawi la Mtwara Dkt. Emmanuel Shindika,ziara hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika (katikati) akipata maelezo kutoka Mkurugenzi wa TPSC Tawi la Mtwara Dkt. Emmanuel Shindika (kushoto) akiwa katika moja ya madarasa ya chuo hicho tawi la Mtwara ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kutembelea matawi ya chuo hicho nchini, ziara hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki.Wengine pichani ni watumishi wa chuo hicho.
Kwaya ya TPSC tawi la Mtwara ikitoa burudani mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika (Hayupo pichani), aliyefanya ziara fupi chuoni mwishoni mwa wiki sambamba na kupokea taarifa ya tawi na kusikiliza changamoto za watumishi na wanachuo.
Baadhi ya wanachuo wa Chuo cha Utumishi wa Umma TPSC tawi la Mtwara, wakimsikiliza kwa makini waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika (Hayupo pichani), aliyefanya ziara fupi chuoni hapo mwishoni mwa wiki sambamba na kupokea taarifa ya chuo na kusikiliza changamoto za watumishi na wanachuo.

RAIS DKT JPM AOMBOLEZA MSIBA WA MKE WA NAIBU WAZIRI KANGI LUGOLA

0
0

Mhe. Rais John Pombe Magufuli akitia saini kitabu cha maombelezo nyumbani kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Alphaxard Lugola aliyefiwa na Mkewe Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Kikosi cha Polisi Reli Tanzania. Alifariki dunia jana tarehe 01 Januari 2018 katika hospitali ya Rabinisia Memorial Tegeta Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Msiba upo Gerezani Railway Club Jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu.

WAZIRI MKUU ATOA KADI ZA CHF KWA WAZEE 4,000

0
0
*Ahimiza wakazi wa Ruangwa wajiunge na bima hiyo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa wilaya ya Ruangwa wajiunge na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili waweze kumudu gharama za matibabu bila kulazimika kuwa fedha taslimu.

Ametoa wito huo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Ruangwa na vijiji vya jirani katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya CWT, mjini Ruangwa, mkoani Lindi.

“Leo hii nimetoa kadi za CHF kwa wazee 4,000 wa wilaya hii. Ninaishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kutenga fedha na kuwalipia wazee hawa ili wanufaike na bima hii ya afya kama ambavyo imeelekezwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi.”

“Ninatoa wito kwa wananchi wengine walipie sh. 15,000 kwa mwaka ili wapatiwe kadi kwa ajili ya watu sita wa familia zao; yaani mhusika, mwenza wake na watoto wanne. Bima hii inasaidia kwa vile unapata matibabu hata kama huna fedha taslimu,” alisema.

Waziri Mkuu alikabidhi kadi kwa Mzee Issa Juma Ngalapa, mkazi wa kata ya Nachingwea pamoja na Mzee Suleiman Stola Lihepa wa kijiji cha Kilimahewa, kata ya Nachingwea kwa niaba ya wazee wote waliotakiwa kupatiwa kadi hizo.

Akitoa ufafanuzi juu ya mpango huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Bw. Andrea Chezue alisema mpango wa kutoa kadi za bima ya afya kwa wazee wameuita ‘CHF Endelevu’ kwa sababu walifanya tathmini na kubaini kuwa matibabu yao yana gharama, na yasipolipiwa, dawa zitaisha au wazee hao hawataweza kupatiwa huduma.

“Katika Halmashauri tulifanya utambuzi wa wazee wa kuanzia miaka 60 na kuendelea kwenye vijiji vyote na kubaini kuwa kuna wazee 4,000. Tukaamua Halmashauri iwalipie sh. 15,000 kwa kila wazee sita kama ilivyo katika kaya ili tuweze kuchangia gharama za matibabu yao,” alisema.

“Mzee akipatiwa kadi hii, inakuwa ni ya kudumu, anaitumia miaka yote. Si ya kulipia kila mwaka kama zilivyo zile nyingine. Hadi sasa tumeshatoa kadi kwa wazee 2,700 na tunaendelea kutengeza kadi hadi tukamilishe zote. Tumepanga kuwa kila mwaka, tutafanya utambuzi wa wazee katika vijiji vyote ili wale wanaofikisha umri huo, nao pia waingizwe kwenye mpango huu,” alisema.



IMETOLEWA NA:OFISI YA WAZIRI MKUU, JUMATATU, JANUARI MOSI, 2018.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA FAMILIA YA NGUZA VICKING IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0

 Mwanamuziki Nguza Vicking “Babu Seya” na wanae Johnson Nguza “Papii Kocha”, Francis Nguza na Michael Nguza wakiwasili viunga vya  Ikulu jijini Dar Leo Januari 2, 2018 kumshukuru Rais Magufuli kwa msamaha wake alioutoa kwao dhidi ya kifungo cha maisha walichokuwa wakitumikia gerezani tangia walipohukumiwa miaka 13 iliyopita.


Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na Familia ya  Mwanamuziki Nguza Vicking “Babu Seya” na wanae Johnson Nguza “Papii Kocha”, Francis Nguza na Michael Nguza wakipata sala ya pamoja,mara baada kuwasili viunga vya  Ikulu jijini Dar Leo Januari 2, 2018 kumshukuru Rais Magufuli kwa msamaha wake alioutoa kwao dhidi ya kifungo cha maisha walichokuwa wakitumikia gerezani tangia walipohukumiwa miaka 13 iliyopita.

DR. MWAKYEMBE ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA LIMONGA JUSTINE LIMONGA

DK. MNDOLWA AKABIDHIWA RASMI OFISI LEO, AAHIDI KUUNDA KAMATI KUTAFUTA UFUMBUZI DHIDI YA KUMOMONYOKA KWA MAADILI KATIKA JAMII YA KITANZANIA

0
0
Na Bashir Nkoromo.

Mwenyekiti mpya wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa ameahidi kuunda Kamati ya  kutathmini namna Jumuiya hiyo inakavyolishughulia kwa ufanisi tatizo la kuporomoka kwa maadili katika jamii hapa nchini.

Dk. Mndolwa ametoa ahadi hiyo leo, hayo wakati akikabidhiwa rasmi Ofisi na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mstaafu Abdallah Bulembo, hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Jumuiya ya Wazazi Tanzania jijini Dar es Salaam.

"Katika hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli alitutaka sisi viongozi wa Jumuiya hii tusikae kimya wakati vitendo vya kuporomoka kwa maadili katika jamii ikiwemo wasanii wa kike kuonyesha sehemu za miili yao zinazotakiwa kusitiriwa. Sasa hili ni agizo lazima mimi na viongozi wenzangu tulipe kipaumbele katika kulifanyika kazi.

Kwa hiyo baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi leo hii, miongoni mwa mipango yangu Kama Mwenyekiti ni Kuunda Kamati itakayojikita kwa undani kuhakikisha tunapata njia bora za kudhibiti kuporomoka kwa maadili katika jamii ya Watanzania", alisema Dk Mndoldwa.Alisema, pia atahakikisha katika zama za uongozi wake, Jumuiya ya Wazazi inainuka na kujitegemea vya kutosha kiuchumi ili iondokane na adha ya kuwa ombaomba.

"Jumuiya hii ianazo mali nyingi, kinachotakiwa hapa ni kuhakikisha fedha zinazotokana na mali au miradi hii zinaingia kwenye hazina ya Jumuia badala ya kupotelea mifukoni mwa wajanja wachache, tukifanikiwa kuthibiti bila shaka tutakuwa na fedha za kutosha", alisema Dk. Mndolwa.
 Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Abdallah Bulembo (kushoto) akikabidhi nyaraka zenye orodha ya mali za Jumuiya hiyo kwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo, Dk. Edmund Mndolwa, leo Januari 2, 2018, Makao Makuu ya Jumuiya jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Zanzibar  Abdallah Haj Haidar.
 Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Wqzazi Tanzania Abdallah Bulembo akionyesha Katiba ya Jumuiya hiyo kabla ya Kumkabidhi Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hizo Zanzibar Abdallah Haj Haidar
 Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Abdallah Bulembo (kushoto) akikabidhi nyaraka zenye orodha ya mali za Jumuiya hiyo, kwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo, Dk. Edmund Mndolwa, leo Januari 2, 2018, Makao Makuu ya Jumuiya jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Seif Shabani Mohammed na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Zanzibar  Abdallah Haj Haidar. 
 Dk. Mndolwa na Bulembo wakisaini nyaraka za makabidhiano

UBOVU MAGARI MAPYA YA POLISI WAISHITUA WIZARA MAMBO YA NDANI

0
0
 

*Masauni aunda kamati maalumu kufanya uchunguzi upya

Na Said Mwishehe, Blogu ya jamii

NAIBU Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Masauni Yusuph Masauni ameagiza kuundwa kamati maalumu kuchunguza magari 53 ya polisi yaliyopo Chuo cha Polisi jijini Dar es Salaam. Amesema mbali ya kuchunguza kwa kina magari hayo,pia ipo haja kupitiwa kwa mkataba wa ujio wa magari hayo Kwani kuna maswali mengi ya kujiuliza ambayo lazima yapate majibu yake.

Masauni ametoa agizo la kuundwa kwa kamati hiyo leo, baada ya kufanya ziara Katika Bandari ya Dar es Salaam ili kuangalia iwapo agizo la Rais ,John Maguful limetekelezwa la kutaka magari ya polisi yaliyopo bandarini yakabidhiwe kwa Jeshi la Polisi nchini. Masauni amesema kimsingi agizo la Rais limetekelezwa kwa magari 53 kukabidhiwa Polisi lakini amebaini kati ya magari hayo matano ni mabovu kutokana na kuwa na hitilafu mbalimbali licha ya kuwa mapya.

"Baada ya kufanyikaa ukaguzi wa awali kwa magari 53,matano kati ya hayo ni mabovu. Na ukaguzi uliofanywa ni wa waletaji na polisi bado hawajafanya ukaguzi wao."Ukisiliza taarifa kuhusu magari haya kuna maswali yanaibuka. Hivyo Wizara ya Mambo ya Ndani inatoa maagizo ya kuundwa kamati maalumu itakayoshirikisha watalaamu kutoka taasisi tofauti kuchunguza magari yote 53,"amesema Masauni.

Amefafanua mkataba kuhusu magari hayo ya polisi unaeleza idadi ya magari yote kwa ajili ya Polisi ni 777 na yaliyopo hadi sasa ni 53 ambayo tayari yamekabidhiwa na magari 119 bado yapo bandarini."Hivyo niagize pia magari ambayo bado yapo bandarini nayo utaratibu ufanyike na kisha kukabidhi kwa jeshi la polisi kwani tunakabiliwa na uhaba wa magari,lazima tusimamie yatoke haraka wakati ukaguzi wa kina ukiendelea,"amesema.

Amesisitiza ni vema kubaini ubora wa magari hayo na kamati itakayochunguza itakuwa huru na itakapokamilisha itatoa taarifa rasmi itakayokuwa na maelezo muhimu ya ubora na uwezo wa magari hayo ya polis. Alipoulizwa iwapo magari hayo ni mapya, amejibu kwa mujibu wa mkataba magari yanatakiwa kuwa mapya na ndio maana amepata mashaka baada ya kubaini kuna magari yanahitilafu.

Kuhusu thamani ya magari yote kwa mujibu wa mkataba, Kamishna wa Fedha na Lojistiki Albert Nyamhanga amesema ni dola za Marekani 29,606,100.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani Masauni Yusuph Masauni(kulia) akitoa maelekezo kwa maofisa wa polisi wakiongozwa na Kamishina wa Fedha na Lojistiki wa Jeshi la Polisi Albert Nyamhanga(kushoto)baada ya kukagua magari ya polisi leo katika bandari ya Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani akitafakari jambo baada ya kukagua magari ya polisi yaliyopo Chuo cha Polisi Kurasini Dar es Salaam leo baada ya kufanya ziara yenye lengo la kufuatilia kukabidhiwa kwa magari 53 kwa Jeshi la Polisi yaliyokuwa bandarini.
Naibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Masauni Yusuph Masauni (wa kwanza kulia) akipata maelezo kutoka kwa moja ya maofisa wa Bandari ya Dar es Salaam leo kuhusu uwepo wa magari 119 ya Jeshi la Polisi ambayo yanasubiri kukabidhiwa kwa polisi. Masauni amefanya ziara bandarini hapo  kufuatilia agizo la Rais,Dk.John Magufuli la kutaka magari ya polisi ya polisi yaliyopo bandarini yakabidhiwe.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Masaun Yusuph Masauni akiwa mbele ya gari jipya lililopo Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam baada ya kulifanyia ukaguzi. Gari hilo ni moja kati ya magari 53 mapya yaliyokabidhiwa kwa Jeshi la Polisi nchini.

TRA YATOA UTARATIBU WA KUSAJILI WALIPA KODI WADOGO

Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images