Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

WANAHABARI WALIOSHINDA TUZO ZA HABARI ZA TANAPA WAENDELEA NA ZIARA YA KUJIFUNZA UTALII NCHINI AFRIKA KUSINI

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mheshimiwa Radhia Msuya akizungumza na wanahabari walioshinda Tuzo za Habari za TANAPA waliomtembelea ofisini kwake jijini Pretoria.
Wanahabari walioshinda Tuzo za Habari za TANAPA katika picha ya pamoja na Balozi Radhia Msuya (wane kushoto). Wengine katika picha ni Jasper Masika Mtanzania anayeishi Afrika Kusini, Phinias Bashaya wa Mwananchi, Pascal Shelutete Meneja Uhusiano TANAPA, Lilian Shirima (TBC) , Alex Magwiza (TBC), Albano Midelo (Nipashe) na Afisa wa Ubalozi.
Wanahabari walioshinda Tuzo za Habari za TANAPA katika picha ya pamoja nje ya Hospitali ya Med Clinic alikolazwa Rais wa Kwanza Mzalendo Nelson Mandela akiendelea na matibabu.
Wanahabari walioshinda Tuzo za Habari za TANAPA katika picha ya pamoja nje ya Kijiji cha Makumbusho cha Lesedi.

Mama Kikwete awataka waislamu kutumia kipindi cha mfungo wa Ramadhani kusali na kutubu dhambi zao

$
0
0
Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi

Waislamu nchini wametakiwa kutumia kipindi cha mfungo wa Ramadhani kuomba na kutubu dhambi zao pia kuwasaidia watu wasiojiweza ili wapate thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Wito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiwafuturisha viongozi wa dini mbalimbali mkoani Lindi. 

Mama Kikwete alisema kuwa kipindi cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani ni kipindi cha kuomba na kutubu dhambi ili yule aliyefunga aweze kujiunganisha na Mwenyezi Mungu.

“Ibada na maombi yenu  viendane na kutoka sadaka, wahudumieni watoto yatima, wagonjwa na watu wasiojiweza, muwe watu wa upendo kwani mahali penye upendo hakuna chuki, vita wala mafarakano”, alisema.

Aliendelea kusema kuwa kila mwaka wamekuwa na utaratibu wa kufuturu kwa pamoja na viongozi wa dini mbalimbali na kuwaombea  kwa Mwenyezi Mungu awajalie funga ya heri na  kuwazidishia huruma, upendo na mshikamano  ndani ya mioyo yao.

Mama Kikwete pia aliwataka viongozi hao wa dini kuhubiri amani kwa waumini wao na kuhakikisha kuwa hawaipotezi  amani kwa mambo yasiyo na tija  kwani kuna nchi waliichezea amani na hivi sasa wanaishi kwa hofu na maisha ya  vita.

“Mjitahidi kila mnapokuwa katika maeneo yenu ya ibada, sherehe na katika huzuni muhubiri juu ya kuwepo kwa  amani kwani pamoja na umaskini wetu Tanzania tumejaliwa kuwa na amani kuna nchi ambazo ni  matajiri lakini hawana amani na wananchi wake wanaishi maisha ya mashaka na hofu”, alisisita  Mama Kikwete.

Kwa upande wake Shekhe na Kadhi mkuu wa mkoa wa Lindi Mohamed Mushangani alimshukuru Mama Kikwete kwa ajili ya futari aliyoiandaa kwa ajili yao na  kusema kuwa kufunga ni moja kati ya  nguzo tano za dini ya Kiislamu na hiyo ni nguzo ya nne.

“Amri ya kufunga  iliyotolewa na Mtume Swalallahu Alayhi Wassalam (S.A.W) akiwa madina mwaka wa pili ndipo ilipoteremka amri hii hivyo basi waislamu wenye afya njema wanatakiwa kufunga”, alisema Shekhe Mushangani.

Aliendelea kusema kuwa mtu anayefunga na kuwa na  hali ya kuamini na kutarajia thawabu anasamehewa makosa ya mwaka wote uliopita nyuma na mfungo mosi anaanza upya kuhesabiwa dhambi zake.

Nafasi za kazi hizo wadau toka SUMATRA

Nafasi ya kazi (for Web Designers).!

EAC Bra Survey team in Uganda

$
0
0
The EAC Brand 2013 survey team embarked on a week-long mission to Uganda on how citizens perceive the regional integration activities, programme and how much they understand of the Community. The survey will be undertaken in all Partner States between 16 July and 27 August. The first two teams set out for Uganda and Burundi. In the picture, the Brand Survey Team poses for a group picture with acting Uganda's Permanent Secretary Steven Niyonzima(with tie) and on his right is the EAC Brand Team leader, Sukhdev Chhatbar., after paying a courtesy call at the Uganda EAC Ministry in Kampala.

MKAZI WA IRINGA ACHUKUA KITITA CHAKE KUPITIA PROMOSHENI YA CHEKA PLUS YA VODACOM

$
0
0
Meneja wa Vodashop Mlimani City jijini Dar es Salaam Bi.Rosemary Maro(kulia)akimuelekeza jinsi ya kutoa Pesa,Anatori E.Chogolo-mkazi wa Iringa,(katikati)ambae ni mshindi kati ya washindi 5 waliojishindia shilingi Milioni 2 kila mmoja katika Promosheni ya Cheka Plus,alizotumiwa kwa njia ya M-PESA kutoka makao makuu ya Vodacom kwa ushindi wake kwenye Promosheni hiyo inayowawezesha wateja kuongea na mitandao yote bila mipaka kwa bei nafuu,anaeshuhudia kushoto ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)na Meneja wa Vodashop Mlimani City jijini Dar es Salaam Bi.Rosemary Maro(katikati)wakimshuhudia Mshindi wa droo kubwa ya Promosheni ya Cheka Plus Bw.Anatori E.Chogolo-mkazi wa Iringa,ambae ni mshindi ,kati ya washindi 5 waliojishindia shilingi Milioni 2 kila mmoja,kwenye Promosheni hiyo inayowawezesha wateja kuongea na mitandao yote bila mipaka kwa bei nafuu,akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)Pesa alizokabidhiwa mara baada ya kuzitoa kwa njia ya M-PESA,alizotumiwa kutoka makao makuu ya Vodacom kwa ushindi wake kwenye Promosheni hiyo,ili kujiunga na promosheni hiyo wateja wanatakiwa kupiga *149*01#.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akimkabidhi Tsh milioni 2 Mshindi wa droo kubwa ya Promosheni ya Cheka Plus Bw. Anatori Emmanuel Chogolo-mkazi wa Iringa,ambae ni mshindi ,kati ya washindi 5 waliojishindia shilingi Milioni 2 kila mmoja,baada ya kuzitoa kwenye M PESA alizotumiwa toka makao makuu ya Vodacom kwa ushindi wake kwenye Promosheni hiyo inayowawezesha wateja kuongea na mitandao yote bila mipaka kwa bei nafuu.Ili kujiunga na promosheni hiyo piga *149*01#.
Mmoja wa washindi wa droo kubwa kati ya washindi 5 wa Promosheni ya Cheka Plus Bw. Anatori E. Chogolo-mkazi wa Iringa(katikati)akihesabu Pesa zake Shilingi Milioni 2 mara baada ya kuzitoa kwa njia ya M-PESA,alizotumiwa kutoka makao makuu ya Vodacom kwa ushindi wake kwenye Promosheni hiyo,wanaoshuhudia kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom,Matina Nkurlu na kulia ni Meneja wa Vodashop Mlimani City jijini Dar es Salaam Bi.Rosemary Maro.

PROGRAMU YA FUTARI LEICESTER UK

$
0
0
Ndugu zetu katika iman, kwanza twamshukuru Allah kwa kutuwezesha kukamilisha hatua za awali za mkakati wa kununua jengo letu wenyewe. Shukrani nyingi pia zikufikieni kwa michango yenu ya kila aina. 

Inshaallah taratibu zetu za Ramdhan zinaendelea na mwaka huu zinafanyikia kituoni kwetu hapo 170a Belgrave Gate, Leicester LE1 3XL. 

Alasiri inasaliwa saa moja jioni (7.00pm) na darsa zinaanza moja na robo jioni (7.15pm) kisha futari inaanza mara baadal Maghrib Tafadhali waweza kuchangia kwa kuwasiliana na Ustadh Farid 07792174408. 

 Siku: kila JMOSI na JPILI. 

 Tafadhali sambaza taarifa Jzkl Lah khayr 
AN NOOR COMMUNITY CENTRE LEICESTER.

TAIFA STARS YAPANGA KUSHAMBULIA MWANZO MWISHO DHIDI YA UGANDA

$
0
0
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen aksisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa Tanzania, mjini Kampala jana kuhusu mechi ya leo ya kufuzu kucheza michuano ya CHAN dhidi ya Uganda Cranes inayotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Namboole mjini humo. Wengine ni Kocha Msaidizi, Sylvester Marsh (kulia) na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura.
Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Sylvester Marsh akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa Tanzania (hawapo pichani) mjini Kampala jana kuhusu mechi ya leo ya kufuzu michuano ya CHAN dhidi ya Uganda Cranes inayotarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Namboole mjini humo. Wengine ni Kocha Mkuu, Kim Poulsen (katikati) na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura. 

Moja ya mikakati ya Taifa Stars kwenye mechi ya kesho (Julai 27 mwaka huu) dhidi ya Uganda kuwania kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Tatu za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini ni kushambulia kwa muda mwingi wa mchezo.

Kocha Kim Poulsen amesema maandalizi ya Taifa Stars jijini Mwanza kwa ajili ya mechi hiyo ambayo Uganda inaongoza kwa bao 1-0 yalikuwa mazuri, lakini mabao ni muhimu hivyo watashambulia bila kusahau kulinda lango lao.

“Unapocheza mechi za aina hii za nyumbani na ugenini, huku mwenyeji akiwa anaongoza mabao yana maana kubwa katika mechi. Mabao yanabadili mchezo na pia wachezaji kifikra,” amesema Kim akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Mt. Zion ambayo Stars imefikia.

Amesema katika mechi ya kwanza walitengeneza nafasi nyingi lakini hawakuzitumia, hivyo wamekuwa wakifanya mazoezi ya kushambulia, jinsi ya kutengeneza nafasi, na jinsi ya kumalizia.

“Hivyo tuko hapa (Kampala) kwa ajili ya kufunga, ni lazima tufunge ili tuweze kuendelea na mashindano. Lakini ngome yetu nayo ni lazima iwe makini ili kutoruhusu bao,” amesema Kim na kuongeza kuwa kikosi chake cha kwanza ni lazima kitakuwa mabadiliko kutoka na Mwinyi Kazimoto kuingia mitini na Shomari Kapombe kwenda kwenye majaribio Uholanzi.

Amesema angalau kutakuwa na mabadiliko kwa kuingiza sura mbili mpya katika kikosi cha kwanza, na kuongeza kuwa wachezaji wanafahamu umuhimu wa mechi hiyo kwani timu ikienda kwenye Fainali za CHAN itakuwa manufaa kwao binafsi.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefanya mazoezi ya mwisho leo jioni Uwanja wa Mandela ulioko Namboole ambao utatumika kwa ajili ya mechi hiyo kesho.

Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki na itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar wakiongozwa na Kanoso Abdoul Ohabee wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Andirvoavonjy Pierre Jean Eric. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Jinoro Velomanana Ferdinand huku Andriamiharisoa Hubert Marie Bruno akiwa mwamuzi wa mezani (fourth official). Kamishna wa mechi hiyo namba 38 ni Ismail Kamal kutoka Ethiopia.

Stars inatarajiwa kupangwa hivi; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, David Luhende, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Salum Abubakar, Frank Domayo, John Bocco, Amri Kiemba na Mrisho Ngasa.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Kampala

TBL YAKABIDHI KISIMA CHA SH. MILIONI 28 KIJIJI CHA ISNURA, MBARALI, MKOANI MBEYA

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gulam Kiffu kulia na Meneja kampuni ya bia (TBL) Nicolaus Kanyamala wakizindua kisima cha kijiji cha Isnura
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gulam Kiffu akiwashukuru TBL kwa kusaidia maji katika kijiji cha isnura na kuahidi kukitunza kisima hicho
Meneja uhusiano wa TBL Dorris Malulu akizungumza na wakazi wa Isnura ambapo amesema kuwa TBL imekuwa na sera ya kusaidia maeneo mbali mbali hapa nchini kupitia faida kidogo inayopata kwa kuamua kurudisha sehemu ya faida hiyo kwa wananchi baada ya kubaini uhitaji wa msaada eneo husika, ambapo pamoja na mambo mengine meneja huyo alitoa rai kwa jamii kuona umuhimu wa kuisaidia serikali hapa nchini.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Isnura  Josphine Ndimilage akisoma risala kwa niaba ya wananchi
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gulam Kiffu akimtwisha maji mwenyekiti wa kijiji cha isnura Josephine ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima hicho
Uchimbaji wa kisima katika Kijiji hicho umefadhiliwa na Kampuni ya Vinywaji ya Tbl kwa gharama ya Shilingi milion 28  ikiwa ni pamoja na Jenereta ndogo kwa ajili ya kupandisha maji katika Tanki kubwa lenye ujazo wa Lita 45,000.

Picha na Mbeya yetu

MAFUNZO YA AWALI YA ASKARI POLISI NA UHAMIAJI YAFUNGWA RASMI LEO

$
0
0
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MH, Dr. EMMANUEL NCHIMBI AKIKAGUA GWARIDE LA WAHITIMU WA MAFUNZO YA AWALI YA ASKARI POLISI WAKATI WA SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO HAYO JANA KATIKA CHUO CHA POLISI MOSHI (CCP). TAKRIBANI ASKARI POLISI ELFU TATU NA TISINI NA MBILI WALIHITIMU MAFUNZO, WAKIWEMO ASKARI WA UHAMIAJI HAMSINI NA MOJA.
ASKARI POLISI WALIOHITIMU MAFUNZO, WAKIONYESHA PIKIPIKI INAVYOWEZA KUSAIDIA KATIKA KUKABILIANA NA WAHALIFU KWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MH, Dr. EMMANUEL NCHIMBI ALIYEKUA MGENI RASMI KATIKA SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO YA AWALI KWA ASKARI POLISI NA UHAMIAJI JANA MJINI MOSHI. TAKRIBANI ASKARI POLISI ELFU TATU NA TISINI NA MBILI WALIHITIMU MAFUNZO, WAKIWEMO ASKARI WA UHAMIAJI HAMSINI NA MOJA.
WASANII WA KIKUNDI CHA NGOMA CHA CHUO CHA POLISI MOSHI WAKITOA BURUDANI JANA MJINI MOSHI WAKATI WA SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO YA AWALI KWA ASKARI POLISI NA UHAMIAJI. TAKRIBANI ASKARI POLISI ELFU TATU NA TISINI NA MBILI WALIHITIMU MAFUNZO, WAKIWEMO ASKARI WA UHAMIAJI HAMSINI NA MOJA. 
MHITIMU WA MAFUNZO YA AWALI YA ASKARI POLISI AKIVUNJA VIGAE KWA KUPIGA NGUMI JANA MJINI MOSHI ALIPOKUA AKIFANYA ONYESHO LA UKAKAMAVU WAKATI WA SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO YALIYOJUMUISHA ASKARI POLISI NA UHAMIAJI. TAKRIBANI ASKARI POLISI ELFU TATU NA TISINI NA MBILI WALIHITIMU MAFUNZO, WAKIWEMO ASKARI WA UHAMIAJI HAMSINI NA MOJA KATIKA CHUO CHA POLISI MOSHI (CCP).
MHITIMU WA MAFUNZO YA AWALI YA ASKARI POLISI AKIJIANDAA KUVUNJA VIGAE KWA KUPIGA NGUMI JANA MJINI MOSHI ALIPOKUA AKIFANYA ONYESHO LA UKAKAMAVU WAKATI WA SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO YALIYOJUMUISHA ASKARI POLISI NA UHAMIAJI. TAKRIBANI ASKARI POLISI ELFU TATU NA TISINI NA MBILI WALIHITIMU MAFUNZO, WAKIWEMO ASKARI WA UHAMIAJI HAMSINI NA MOJA KATIKA CHUO CHA POLISI MOSHI (CCP).
KIKUNDI CHA KARETI NA JUDO CHA WAHITIMU WA MAFUZO YA AWALI YA ASKARI POLISI NA UHAMIAJI WAKIFANYA ONYESHO LA KARETI KWA MGENI RASMI MH, Dr. EMMANUEL NCHIMBI WAKATI WA SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO HAYO. TAKRIBANI ASKARI POLISI ELFU TATU NA TISINI NA MBILI WALIHITIMU MAFUNZO, WAKIWEMO ASKARI WA UHAMIAJI HAMSINI NA MOJA KATIKA CHUO CHA POLISI MOSHI (CCP). PICHA NA HASSAN MNDEME-JESHI LA POLISI.

TAARIFA YA MSIBA

$
0
0
Familia ya Mzee Ndalu inasikitika kutangaza kifo cha kijana wao mpendwa Erick Meshack Ndalu kilichotokea nyumbani kwao Tabata tarehe 24/7/2013 saa 5 usiku, habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu popote pale walipo.

 Mazishi yanategemea kufanyika kesho siku ya Jumamosi tarehe 27/7/2013 katika makaburi ya kinondoni saa 10 jioni.

Bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Amen 

CASTLE na FC Barcelona wasaini mkataba wa kihistoria

$
0
0
wawakilishi wa SABMiller kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wakiwa nje ya ofisi za timu ya FC Barcelona huko Catalonia Hispania leo hii.
Makamu wa Rais wa FC Barcelona,Bw. Javier Faus akimkabidhi jezi yenye jina la Rais Jakaya Kikwete kwa Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Kushilla Thomas ili aweze kumletea Mh. Rais ikiwa ni kwa kutambua mchango wake kwenye swala zima la michezo.
Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Kushilla Thomas akimkabidhi zawadi ya asili kutoka Tanzania Bw. Javier Faus, Makamu wa Rais wa FC Barcelona anayeshughulikia uchumi huko Catalonia Hispania leo hii baada ya kutangazwa kwa udhamini wa Castle Lager kwa Barcelona.
Mkurugenzi wa Masoko wa Tanzania Breweries Limited (TBL),Kushilla Thomas akiwa nje ya ofisi za FC Barcelona huko Catalonia Hispania leo hii baada ya kutangazwa kwa udhamini wa Castle Lager kwa Barcelona.

Barcelona, Hispania, Ijumaa Julai 26, 2013 – Bia ya Castle Lager imeingia makubaliano ya kuidhamini moja ya klabu maarufu zaidi duniani ya FC Barcelona ya Hispania kwa kipindi cha miaka mitatu udhamini utakaokifanya kinywaji hicho kuwa bia rasmi ya FC Barcelona barani Afrika.

Ushirikiano huu, uliyosainiwa kwenye uwanja wa klabu Camp Nou, unaifanya CASTLE Lager kuwa bia rasmi itakayotumika kwa shughuli yoyote ambayo Barcelona itashiriki kwenye bara la Afrika na pia itafungua milango kwa mashabiki wa Barcelona Afrika kuwa karibu na wachezaji wa Barcelona, vifaa, na kumbukumbu. Pia kupata nafasi ya kusafiri kwenda Hispania kushuhudia kwa karibu timu ya Barcelona.

Mkataba huu utakuwa maalum kwa ajili ya CASTLE Lager kwenye nchi nyingi za Afrika isipokuwa kwa baadhi ya nchi chache zilizochaguliwa ambapo itatumika Castle Milk Stout.

Hii ni mara ya kwanza kwa timu ya FC Barcelona kusaini mkataba wa udhamini na kampuni ya bara la Afrika. Kushirikiana na bia bingwa Afrika litaongeza kwa haraka umaarufu wa timu ya FC Barcelona ndani ya bara la Afrika na kufungua milango kwa mashabiki wa klabu hii kupata bidhaa mbalimbali za Barcelona na nafasi za kushinda safari ya kwenda Barcelona kuitembelea klabu hiyo.

“Tumefurahi sana kuingia katika ushirikiano na Castle Lager na Castle Milk Stout, chapa zinayofahamika dunia nzima . Tunafanana na Castle kwa kuwa sote tuna historia ya zaidi ya miaka 100 na utamaduni uliotukuka. Na sote tuna mapenzi na mpira wa miguu pamoja na mashabiki wake katika soko muhimu kama Afrika,” alisema Javier Faus, Makamu wa Rais wa FC Barcelona anayeshughulikia masuala ya uchumi.

“Uamuzi wa Barcelona kuingia ushirika na na bia inayoongoza barani Afrika kutaongeza umaarufu wa bia hiyo kwenye bara hili na kuwawezesha wachezaji wa timu hiyo kufika maeneo amabyo hawajawahi kufika barani Afrika,” alisema David Carruthers Mkurugenzi wa Masoko wa SabMiller Afrika (kampuni mama ya TBL).

CASTLE Lager si bidhaa mpya kwenye udhamini wa mpira wa miguu na vyama, ina miaka mingi ya kujihusisha katika soka barani Afrika kwa kipindi cha miaka 85 kupitia ligi mbalimbali za nchi tofauti kama vile Zimbabwe, Swaziland, Botswana, Lesotho na pia mashindano ya kanda kama COSAFA Kusini mwa Afrika na CECAFA Afrika Mashariki.

Kutokana na soka la Ulaya kupata umaarufu mkubwa na mashabiki wengi barani Afrika, Castle Lager imekuwa ikidhamini urushaji wa matangazo ya ligi hizo kwenye televisheni barani Afrikana kuwapa mashabiki fursa ya kufatilia kila kinachoendelea kwenye ligi hizo maarufu duniani ambazo ni Ligi Kuu ya Ulaya, Ligi Kuu ya Uingereza na La Liga ya Kihispania.

Kufuatia udhamini huu, wanywaji wa Castle Lager na Castle Milk Stout pamoja na mashabiki wa Barcelona barani Afrika sasa watarajie mambo mengi ya kusisimua katika ulimwengu wa soka.

JK awaonya wanaotaka kuichezea Tanzania

KAULI YA JESHI LA MAGEREZA JUU YA MAAFISA WAKE WANNE WALIOKAMATWA NA NYARA ZA SERIKALI

$
0
0
Jeshi la Magereza Tanzania Bara linapenda kuufahamisha Umma kwamba mnamo tarehe 23 Julai, 2013 Maafisa wanne ambao ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza Joseph Kimaro, Sajenti Ketto Ramadhani, Koplo Silyvester Dionice na Wada Richard Barick wa Gereza Kiteto Mkoa wa Manyara walikamatwa na askari wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Kati wakiwa na gari la Jeshi la Magereza pamoja na silaha likiwa limepakia nyara za serikali. 

Dereva wa gari hilo Sajenti Ketto Ramadhan alitoroka na kutelekeza gari hilo na Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu na maadili ya Jeshi la Magereza pamoja na sheria za uwindaji wa wanyama pori. Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Magereza limechukua hatua zifuatazo:-

i - Askari 3 waliohusika wamefukuzwa kazi kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Magereza na watafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi wa Polisi kukamilika.

ii - Afisa Mrakibu Msaidizi wa Magereza Joseph Kimaro amefunguliwa mashtaka ya kinidhamu na kusimamishwa kazi kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Magereza hadi maamuzi ya Mamlaka ya kinidhamu inayomuhusu yeye (Disciplinary authority) itakapotoa maamuzi dhidi yake. Kwa sasa amezuiliwa Kituo cha Polisi Babati kusubiri kufikishwa Mahakamani upelelezi wa Polisi utakapokamilika.

iii - Mkuu wa Gereza Kiteto Mrakibu wa Magereza Ally Ramadhani Sauko kwa kutumia madaraka yake vibaya hivyo amevuliwa uongozi na kuhamishiwa Ofisi ya Mkuu wa Magereza Manyara, akisubiri maamuzi ya Mamlaka ya kinidhamu inayomuhusu yeye (Disciplinary authority) kufuatia mashtaka ya kinidhamu yaliyofunguliwa dhidi yake.

Imetolewa na Kitengo cha Habari 
Ofisi ya Makao Makuu ya Magereza Tanzania Bara

Mkutano wa CPA Barani Afrika wamchagua Spika Makinda kuwa Rais wa Afrika na kumpongeza kwa siku yake ya kuzaliwa

$
0
0
Spika wa Bunge wa Bunge la Tanzania,Mhe Anne Makinda akihutubia kushukuru wajumbe Mkutano wa CPA Barani Afrika kwa kumchagua kuwa Rais wa CPA Afrika.
Mhe Spika Anne Makinda akipongezwa na Mwenyekiti wa CPA na Spika wa Bunge la Gauteng Mhe.Lindiwe Maseko,kwa kuchaguliwa na Mkutano huo wa 44 wa CPA kuwa Rais wa Afrika na Mwenyeji wa Mkutano wa 45 wa CPA utakaofanyika Arusha Tanzanis julai mwakani.
Picha ya pamoja ta Uongozi wa CPA Kanda ya Afrika, kutoka kushoto ni Mhe.Request Muntanga(Mweka Hazina),Mhe Asser Kapere ambae ni Rais aliemaliza muda wake na Spika wa Namibia,Mhe Lindiwe Maseko ambae ni Mwenyekiti na Spika wa Gauteng,Kutoka kulia ni Mr Demetrius Mgalami Naibu Katibu wa Kanda ya Afrika, Mhe Lucia Witbooi wa Namibia na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Afrika, Mhe Spika Sephiri Motanyane wa Lesotho na Mhe Spika Makinda wa Tanzania na Rais wa Afrika wa CPA.Picha na Saidi Yakubu.

OBITUARY

$
0
0
Saidi Ally Masimango: the unsung hero

 It was the morning of Monday July 22, 2013 when I received a brief but chilling email from a close relative. The relative wrote and I quote verbatim:

"Msiba! Saidi Masimango amefariki asubuh hii, TMJ hospital! Innaa Lillah wainnaa ilayhi Raajuun".

This is literally translated as "Misfortune! Saidi Masimango died this morning, TMJ hospital! We are all from Allah and unto Him is our return".

The time was 7.54 am. I was taking my wife and two daughters to Dubai International Airport to catch their flight to Dar es Salaam. We were coming from the UK to attend graduation ceremony of our son Luqman Dau, who the previous Wednesday, earned his BSc (Hons) in Molecular Biology from the University of Sheffield.

As with all sudden deaths, my initial reaction was that of disbelief. I asked myself several questions. Is this the same Masimango who is my Director of IT at NSSF? What might have happened to him? As several questions were racing through my mind, I quickly made an international call to Mrs Chiku Matessa who was taking charge of my office while I was away. At the time, Mrs Matessa was already at the TMJ hospital and confirmed to me that our beloved colleague Saidi Ally Masimango is no more!

In keeping with Islamic teachings and tradition, I knew that the funeral will take place not later than the following day, i.e., Tuesday July 23. I found myself utterly helpless because I was halfway to the airport to drop my family and the flight was only 2 hours away. I didn't have a booking for the flight and didn't have my passport with me at the time. I had no option except to throw the towel because there was no way in those 2 hours I could have catch that flight to escort my colleague to his eternal home. What was left for me was to pray for the departed soul.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL APOKEA MAANDAMANO YA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA VIKUNDI VYA MTANDAO WA WAKULIMA WA TANZANIA (MVUWATA) MJINI MOROGORO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti, mmoja kati ya wachangiaji bora wa kuendeleza Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) Justice Shekilango, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika leo Julai 26, 2013 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Wasanii wa kikundi cha ngoma ya Muhembe cha mjini Dodoma, wakitoa burudani wakati wa sherehe hizo za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri mijini Morogoro.
Wakulima wa Jumuiya ya Mtandao wa Wakulima wa Tanzania (MVUWATA) wakiwasili kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwa maandamano leo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo, yaliyopokelewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, aliyekuwa mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanamtandao wa Jumuiya ya wakulima wa Tanzania (MVUWATA) baada ya kupokea rasmi maandamano ya wakulima ya maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri mijini Morogoro. Picha na OMR.

CAG AHUDHURIA KIKAO CHA 67 CHA BODI YA UKAGUZI YA UMOJA WA MATAIFA (UNBoA)

$
0
0
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S. L. Utouh (Kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon baada ya Mkutano wa 67 wa Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa (UNBoA), Jumanne, 23 Julai, 2013 mjini New York, Marekani.
Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) wakiwa saini ripoti 15 zilizoidhinishwa. Kutoka kushoto walioketi ni Bw. Ludovick S. L. Utouh (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania),Bw. Lui Jiayi (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China) na Bw. Amnyas Morse (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Uingereza).
Wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) wakiwa katika picha ya pamoja. Kuanzania kushoto ni Bw. Ludovick S. L. Utouh (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania), Bw. Amnyas Morse (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Uingereza) na Bw. Lui Jiayi (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China).
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S. L. Utouh (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Bi. Hellen Clark Mtendaji Mkuu wa UNDP (wapili kushoto) baada ya mazungumzo ya pamoja na menejimenti ya shirika hilo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa UN Women Bi. Lakshmi Puri (Kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Bw. Ludovick S. L. Utouh mara baada ya kikao cha pamoja cha kilichofanyika makao makuu ya Ofisi, mjini New York Marekani.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Balozi Tuvako Manongi (Watatu Kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mara baada ya kikao kazi kilichofanyika katika ubalozi wa Tanzania, New York Marekani.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Balozi Modest Mero (Watatu Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipowatembelea, UN Plaza, New York Marekani.

MUSOMA TEXTILE MILLS (T) Ltd EMERGED ‘SOLID WASTE MANAGEMENT WINNER 2013’

$
0
0

The cleaner Production Centre of Tanzania (CPCT) dealing with Resource Efficiency and Cleaner Production (RECP) has conducted training on RECP to all manufacturing industries in Tanzania.


The training was aiming at minimizing of Energy use, Water use, Profitable production, Lowest possible pollution of environment - Particularly Lake Victoria under Lake Victoria Environment Project (LVEMP II).

In this regard CPCT conducted RECP Award Competition for Lake Zone in which 63 manufacturing industries participate among them was Mutex - Musoma Textile Mills (T) Ltd, a subsidiary of MeTL group of Companies.

Out of 63 participants, 10 contestants were short listed for 4 categories, unto which MUTEX emerged SOLID WASTE MANAGEMENT WINNER 2013.

Verification team was comprised of East African members on Cleaner Production, which are Uganda Cleaner Production Centre, Kenya National Cleaner Production Centre, Cleaner Production Centre of Tanzania and OSHA officials.

The ceremony was conducted in Mwanza on 28th June, 2013 by CPCT, under Ministry of Water and Irrigation, headed by Permanent Secretary in the Ministry where the Chief Guest was Hon. Minister of State for Enviornment in the Vice President ‘s Office Hon Dr. Therezya Huvisa.

NEMC and Lake Victoria Environmental Project (East Africa) Officials also attended.

Naibu waziri wa maji afanya ziara katika miradi ya maji Moshi vijijini

$
0
0
Naibu waziri wa maji Dk Bilinith Mahenge akitia saini katika kitabu cha wageni katika ofisi ya kata ya Mbokomu wakati akifanya ziara ya kukagua miradi ya maji katika wilaya ya Moshi vijijini.
Naibu waziri wa maji Dk Bilinith Mahenge akitembelea kukagua miradi ya maji ya Mbokomu wilaya ya Moshi vijijini.
Wakandarasi wa ujenzi wa matangi ya maji katika mradi wa Mbkomu wakibeba nagazi ambayo naibu waziri alitaka kupanda juu ya Tangi hilo kujione ujenzi ni wa kiwango kinachohitajika ama la.
Kisha naibu waziri wa Dk Mhenge akatembelea chanzo cha maji kilichoko mto Whona ambacho maji yake yanatumiwa na wakazi wa mji wa Himo.
Wakazi wa Himo wakichota maji kwa ajili ya matumizi ya Nyumbani na biashara.Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images