Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 207 | 208 | (Page 209) | 210 | 211 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmshauri ya Mji wa Babati Mjini Mkoani Manyara, Bw. Janes Dabare (kulia) akichangia hoja katika eneo la mihimili ya Dola katika Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji huo jana Ijumaa (Julai 26, 2013).
  Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara wakiwa katika mjadala wa kuipitia Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji huo jana Ijumaa (Julai 26, 2013).
  Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmshauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara, Bw. Askari Emeda (kushoto) na Bi Zubeda Iddi wakisoma vipengele vilivyopo katika Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji huo jana Ijumaa (Julai 26, 2013).
  Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara Bw. Simon Mahenge akichangia hoja wakati wa mkutano wa kuijadili Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika jana (Ijumaa Julai 26, 2013). (PICHA NA TUME YA KATIBA)

  0 0
 • 07/27/13--02:51: KONGAMANO LA UONGOZI LAFANA
 • Kongamano la Uongozi linaloandaliwa na Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) limefanyika leo katika hoteli ya Serena na kuhudhuriwa na Jumla ya washiriki wapatao 150, ambao ni viongozi mbalimbali wa sasa na wastaafu walishiriki katika kongamano hilo. Viongozi hao ni pamoja na Wah. Mawaziri Wakuu Wastaafu; Baadhi ya Wah. Mawaziri Wastaafu; Wah. Wabunge; Wenyeviti wa Kamati; Makatibu Wakuu Viongozi Wastaafu; Baadhi ya Wakuu wa Mikoa; Baadhi ya Viongozi wa Halmashauri; Wenyeviti wa Baadhi ya Taasisi za Umma; Watendaji Wakuu wa Baadhi ya Taasisi za Umma; Viongozi Kutoka Sekta Binafsi; Viongozi wa Asasi za Kiraia; Viongozi wa Dini and Wasomi na Watafiti.

  Mgeni rasmi katika Kongamano hilo alikuwa Mh. Mizengo P. Pinda, Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mh. Pius Msekwa, Spika Mstaafu wa Bunge la Muungano, Tanzania ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa kongamano hilo pia lilipata nafasi ya kuwatuza wanafunzi waliofanya vizuri katika shindano la kuandika insha kuhusu uongozi bora na kuwashirikisha wanafunzi toka nchi zote za Afrika Mashariki huku Redemptor Benedict, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akiibuka mshindi.

  Kongamano la uongozi mwaka huu liliongozwa na spika mstaafu, Pius Msekwa ambaye ndiye alimkaribisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda na watoa mada wengine ambao ni viongozi wa kitaifa, wastaafu na wale wa taasisi binafsi ambao wote walielezea changamoto zinazoikabili Tanzania katika uongozi na namna uongozi unavyopaswa kwenda na mabadiliko yanayojitokeza ikiwemo yale ya kisayansi na teknolojia.

  Mgeni rasmi katika Kongamano la Uongozi, Waziri Mkuu Mizengo panda katika meza kuu.

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua rasmi Kongamano la Uongozi liliofanyika Hoteli ya Serena jijini.

  Mkongwe wa siasa nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwilu alikuwa mmoja wa wachangiaji

  Mheshimiwa James Mbatia katika kongamano la uongozi

  Katibu mkuu wa CCM (Mstaafu) Wilson Mukama alikuwa mmoja ya waliotoa changamoto kwa viongozi wa sasa na wajao

  Mbunge wa zamani, Getrude Mongella alipata nafasi ya kuchangia mada katika kongamano kuelezea uzoefu wake

  Alieibuka kidedea katika shindano la uandishi wa insha, Redemptor Benedict akipongezwa na Waziri Mku, Mizengo Pinda na kukabidhiwa cheti cha ushiriki.

  Mshindi wa pili Joan Wanjiku Gichomo akisoma insha yake mbele ya washiriki wa kongamano la uongozi.

  Viongozi mbalimbali walioshiriki katika Kongamano la Uongozi lilioandaliwa na Uongozi Institute katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

  0 0


  0 0

  kikosi cha timu ya taifa 'Taifa Stars' kilichokipiga leo na timu ya taifa ya Uganda.
  kikosi cha timu ya taifa ya Uganda 'Uganda Cranes'
  Mchezaji wa timu ya Taifa "Taifa Stars" Aggrey Morris (katikati) akiwania mpira huku akizongwa na mabeki wa Uganda Cranes wakati wa mchezo wao wa Marudiano uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala Uganda.hadi mwisho wa Mchezo Taifa ilichapwa mabao 3-1
  Amri Kiemba akiambaa na mpira huku akizongwa na beki wa Uganda Cranes, Nicolas Kadada.
  David Luhende akiambaa na mpira huku beki wa Uganda Cranes Said Kyeyune akijaiandaa kumkabili.
  Mrisho Ngasa akiwania mpira na Nicolas Kadada wa Uganda Cranes.
  Washabiki wa Taifa Stars wakishangilia goli la kusawazisha.

  Tanzania (Taifa Stars) imeshindwa kufuzu Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) kwa mara ya pili mfululizo baada ya leo (Julai 27 mwaka huu) kufungwa mabao 3-1 na Uganda Cranes, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 4-1.

  Stars ambayo ilicheza fainali za kwanza zilizofanyika Ivory Coast mwaka 2009 ilimaliza kipindi cha kwanza katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Kampala ikiwa sare ya bao 1-1.

  Wenyeji ndiyo walioanza kufunga bao dakika ya saba katika mechi hiyo iliyochezeshwa na Kanoso Abdoul Ohabee kutoka Madagascar. Frank Kalanda alifunga bao hilo akimalizia mpira uliopigwa ndani ya eneo la hatari la Tanzania.

  Bao hilo halikuonekana kuichangaza Taifa Stars, kwani ilitulia na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 18 mfungaji akiwa Amri Kiemba kutokana na pasi nzuri ya Mrisho Ngasa kwenye kona ya eneo la mita 18.

  Dakika ya 32 nusura Taifa Stars ipate bao, lakini mkwaju maridadi wa Mrisho Ngasa ambao tayari ulikuwa umempira kipa HAmza Muwonge uligonga mwamba kabla ya kuokolewa na mabeki wa Uganda Cranes.

  Mabao mengine ya Uganda Cranes yalifungwa dakika ya 48 kupitia kwa Brian Majwega na lingine dakika ya 63 mfungaji akiwa tenda Kalanda kutokana na makosa ya Salum Abubakar kupokonywa mpira wakati akiwa katika nafasi nzuri ya kutoa pasi kwa mwenzake.

  Kocha Kim Poulsen alifanya mabadiliko dakika ya 43 kwa kumuingiza Simon Msuva badala ya Frank Domayo aliyeumia, na dakika ya 78 akawaingiza kwa mpigo Haruni Chanongo na Vincent Barnabas badala ya David Luhende na John Bocco. Hata hivyo mabadiliko hayo hayakubadili matokeo ya mchezo.

  Kikosi cha Stars kilipangwa hivi; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, David Luhende/Vincent Barnabas, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Frank Domayo/Simon Msuva, Salum Abubakar, John Bocco/Haruni Chanongo, Amri Kiemba na Mrisho Ngasa.

  Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itarejea nyumbani kesho (Julai 28 mwaka huu) saa 4 usiku kwa ndege ya PrecisionAir.

  0 0

  Na Abdulaziz video,lindi

  Mkuu wa mkoa wa lindi Ludovick Mwananzila ameuagiza uongozi wa wilaya ya ruangwa kuwachukulia hatua kali watendaji wa chama cha Msingi na ushirika cha Lucheregwa kwa tuhuma za kuuza pembejeo za ruzuku kwa bei ya juu.

  Agizo hilo amelitoa katika mkutano wa hadhara baada ya wananchi wa wilaya hiyo kuulalamikia uongozi huo kwa mkuu wamkoa wakati alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu wilayani humo.
  Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Mh. Ludovick Mwananzila
  Mwananzila alieleza kuwa kitendo hicho cha viongozi hao kuuza pembejeo hizo kwa bei ya juu kinyume na utaratibu uliopangwa na serikali katk ugawaji wa pembejeo za ruzuku ni ujunjaji wa sheria.

  Mwananzila alisema ili iwe fundisho kwa wafanyabiashara wengine wenye tabia kama hizo ni lazima viongozi hao wachukuliwe hatua kali za kisheria ambapo alitoa agizo kwa uongozi wa wilaya kuwashughulikia viongozi hao haraka iwezekanavyo.

  Kwa upande wake katibu mkuu wachama cha ushirika cha msingi cha kuuza na kununua mazao Lucheregwa Samora fundi alikiri kuuza pembejeo hizo kwa bei ya juu ambapo alieleza kuwa mfuko mmoja wa salfa aliuza kwa shilingi 16500 badala y ash 15000 kama ilivyoagizwa na serikali.

  Fundi alisema uamuzi wa kuuza pembejeo hizo kwa bei hiyo ulitokana na makubaliano ya mkutano mkuu wa chama ukiwa na lengo la kuongeza mapato ya chama kutokana na chama kukosa fedha baada ya kuyumba kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kupitia zao la korosho .

  Aidha Mwananzila aliitaka halmashauri ya wilaya ya ruangwa kuhakikisha inahimiza kilimo cha mbogamboga ili kusaidia kuinua kipato cha wakulima kwa kuwapatia vitendea kazi , kuwajengea Uwezo ili waweze kufanya kazi zao ka ufanisi Na Kipato ikiwemo Halmashauri hiyo kupata Ushuru.

  """wakulima ili muweze kufanikiwa ni lazima mjiunge kwa vikundi na kuunda saccosz itakazo wafanya muweze kutambulika na taasisi za fedha na kukopesheka'''' Alimalizia Mwananzila.

  0 0

  Kambi ya Wasanii wa Filamu na Maigizo pamoja na Kambi ya Waanahabari Makapela Tanzania imepata pigo kubwa baada ya Mwanachama wake Nguli, Simon Simalenga kuamua kuiaga kambi hiyo na kuingia rasmi katika Kambi Tawala ya Wanandoa baada ya kufunga Ndoa na Bi. Neema Inana. Wawili hao wameamua kuingia kambi hiyo ya Upinzani katika mahusiano leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokozi Sinza jijini Dar es Salaam na baadae katika tafrija kubwa inayofanyika usiku huu wa Julai 27, 2013 katika ukumbi qa Grande Hall uliopo ndani ya Hoteli ya Picolo Beach Mbezi. 
  Production: MD Digital Company: +255 373 999/+255 717 002303 
  Whatsapp +255 788 207274.
  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bi. Joyce Mkinga (Kulia) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) alipokutana nao kuzungumzia hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bi. Joyce Mkinga (Kulia) akionesha nakala ya Kijitabu cha Dira ya Taifa ya Maendeleo (TDV 2025), alipokutana na wanahabari kuzungumzia hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Rais Kikwete akiwapungia mkono wakazi wa kijiji cha Rulenge,Wilayani Ngara wakati akiwasili kwenye kiwanja cha kijiji hicho tayari kwa kuzungumza nao ikiwa ni sehemu ya Ziara yake ya Kikazi Mkoani Kagera
  Rais Kikwete akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Rulenge,Wilayani Ngara wakati akiwasili kwenye kiwanja cha kijiji hicho tayari kwa kuzungumza nao ikiwa ni sehemu ya Ziara yake ya Kikazi Mkoani Kagera
  Rais Kikwete akihutubia umati mkubwa wa wananchi wa Wilaya ya Ngara,Mkoani Kagera wakati wa Muendelezo wa Ziara yake ya Kikazi Mkoani Kagera.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Prof Anna Tibaijuka akielezea baraza la ardhi.Kushono ni Rais Kikwete akisikiliza kwa Makini.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha na mawaziri anaoongozana nao pamoja na viongozi wa mkoa wa Kagera wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi kwa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kagoma-Lusahunga wilayani Biharamulo, mkoa wa Kagera
    Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha na viongozi wa CCM wa mkoa wa Kagera wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi kwa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kagoma-Lusahunga wilayani Biharamulo, mkoa wa Kagera
    Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha na mawaziri anaoongozana nao pamoja na viongozi wa TANROADS  wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi kwa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kagoma-Lusahunga wilayani Biharamulo, mkoa wa Kagera
    Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha na mawaziri anaoongozana nao pamoja na wafanyakazi wa TANROADS  wa mkoa wa Kagera wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi kwa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kagoma-Lusahunga wilayani Biharamulo, mkoa wa Kagera
    Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha na mawaziri anaoongozana nao pamoja na viongozi wa kampuni za ujenzi wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi kwa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kagoma-Lusahunga wilayani Biharamulo, mkoa wa Kagera
   Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha na mawaziri anaoongozana nao pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi kwa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kagoma-Lusahunga wilayani Biharamulo, mkoa wa Kagera

  0 0
 • 07/28/13--01:44: Article 16
 • SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD
  WAZEE WA KAZI
  TAARIFA YA ONGEZEKO LA BEI
  MTATUWIA RADHI WATEJA WETU, IMEBIDI TUONGEZE BEI KIDOGO ZA NDEGE
  HII IMETOKANA NA ONGEZEKO LA BEI YA MAFUTA YA NDEGE
  AIR CARGO TO DAR NOW £3.80
  INCLUSIVE CLEARANCE
  STILL THE CHEAPEST AND SIMPLY THE BEST!
  WE PROMISED, WE DID IT AND WE ARE MAKING IT EVEN BETTER!
  KUCHUKUA MZIGO WAKO DAR ES SALAAM 
  MPIGIE AGENT WETU DAR; TORNADO LUKOSI TEL; 0713607116
  MZIGO UNANDOKA KILA IJUMAA UNACHUKUA IJUMAA INAYOFUATA
  FROM NOW ALL OUR CARGO GOES  WITH KENYA AIRWAYS! 
  THIS MEANS A DIRECT FLIGHT TO NAIROBI/DAR EVERY WEEK 
  THIS MEANS NO MORE DELAYS OR EXCUSES!
  THIS MEANS BETTER SERVICE THAN BEFORE!

  ONCE YOU PAY HERE IN UK YOU DONT PAY ANYTHING IN TANZANIA
  UKIISHA LIPA UK UNAKWENDA KUCHUKUA ILALA DAR BILA KULIPA TENA

  FLIGHTS EVERY WEEK

  KWA WALE WANAOTAKA KUNUNUA VITU UK TUTUMIE EMAIL AU TUPIGIE
  MINIMUM WEIGHT IS 40K HANDLING/ADMIN FEE £20
  40' CONTAINER TO DAR/MOMBASA NOW £1,800
  OUR AGENT IN DAR; TORNADO TEL; +255 713607116

  Tupigie kwa namba hizo hapo chini au  tutumie email tafadhali

  HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
  Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Aisha Sururu Fondition, Bi. Aisha Sururu (kulia) akimkabizi mmoja wa vijana wanaojisomea katika kambi ya msikiti wa Idrisa, Muhsin Juma magodoro aliyotoa kwa ajili ya vijana hawo kulalia,pindi wamalizapo masomo yao.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Aisha Sururu Fondition, Aisha Sururu kulia akimkabizi mmoja wa vijana wanaojisomea katika kambi ya msikiti wa Idrisa, Muhsin Juma mashuka pamoja na magodoro aliyotoa kwa ajili ya vijana hawo kulalia.

  0 0

  Kikao cha Viongozi wa Tawi la Chadema Washington DC, Marekani, tarehe 27 July 2013 kimemteua Ndugu Kalley Ammy Pandukizi kuwa Mwenyekiti wa Tawi kuchukua nafasi ya Ndugu Cosmas Wambura.

   Awali Ndugu Kalley Pandukizi alikuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tawi la Chadema DMV linalobeba majimbo matatu ya Washington DC, Maryland na Virginia. Baadae alikuwa Afisa wa Habari wa Tawi na nafasi yake kuchukuliwa na Cosmas Wambura. 

  Viongozi wengine na nafasi  zao ni Katibu wa Tawi niLibearatus Mwang’ombe aliyekuwa  katibu wa kwanza wa Tawi, aliyechukua nafasi ya Isidory Lyamuya. 

  Katibu Mwenezi ni Ndugu Hussein Kauzela na Mweka hazina ni Ndugu Ludigo Mhagama. Mwenyekiti wa Baraza la wanawake ni Ndugu Baybe Mgaza na Katibu wa Baraza la wanawake ni Mariam Khamis. Nafasi nyingine ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Ndugu Amri Maliyatabu na katibu wa baraza la vijana ni Ndugu Stephen Msungu.

   Nafasi nyingine ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee ni Amos Cherehani na Katibu wa baraza la wazee ni Elias Mshana. Nafasi ya Mwisho ni ya Baraza la Washauri linaloongozwa na Prof Nicolas Boaz na Emmanuel Muganda.

  Akizungumza baada ya Uteuzi huo Mwenyekiti wa Chadema Washington DC Ndugu Kalley, Amewashukuru Viongozi wote kwa kumwamini na kumpa nafasi hiyo kwa mara ya pili na kuwaahidi kufanya mambo makubwa ikiwemo kurudisha uhai wa Tawi na kuwaunganisha wanachama kuwa wamoja. 

  Pia ameahidi kushirikiana na Jumuia nyingine ikiwemo Jumuia ya Watanzania DMV, Ofisi ya Ubalozi Wa Tanzania Marekani, Jumuia ya Waislam waishio Washington DC (TAMKO) na Uongozi wa CCM DMV ili kujenga Tanzania Moja yenye mshikamano.

  Pia Ndugu Kalley amesema baada ya kurudi kwenye nafasi hiyo kipaumbele cha kwanza kitakuwa kuvalia njuga mambo makuu mawili ambayo ni Suala la mchakato wa Katiba unaoendelea ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapata Katiba nzuri iliyoridhiwa na Watanzania wote bila kuingiliwa na mtu yeyote kwa nia mbaya. 

  Pili amesema atavalia njuga suala la upatikanaji wa Tume huru ya Uchaguzi ili Uchaguzi Ujao wa Mwaka 2015 uwe huru na Haki.

  Aidha Katika mkutano huo Ndugu Kalley ameelezea kusikitishwa sana na vitendo vya ukiukwaji wa Sheria vinavyofanywa na Jeshi la Polisi kwa kuwabambikizia kesi raia wasio na hatia na hata matukio ya mauaji wanayotuhumiwa baadhi ya Askari Polisi. 

  Ndugu Kalley amesema atapambana vikali kuhakikisha matukio hayo ya ukiukwaji wa haki za raia yanayofanywa na baadhi ya askari Polisi yanakomeshwa, kwani hakuna sheria inayoruhusu askari Polisi kujichukulia sheria mkononi wakati Mahakama ndizo zilizopewa Mamlaka hiyo.

  Tawi la Chadema Washington DC lilianzishwa rasmi tarehe 26 Aprili 2012 chini ya usimamizi wa Mbunge wa viti maalum Mh Leticia Nyerere na Kufunguliwa rasmi tarehe 27 Mei 2012 na Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu katibu mkuu wa Chadema Mh Zitto Kabwe. 

  Sherehe hizo za Ufunguzi ziliudhuriwa Pia na Mbunge wa Iringa mjini Mh Peter Msigwa, Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari, Mbunge wa Viti Maalum Kwimba Mh Leticia Nyerere na Mbunge wa Viti maalum Kutoka Zanzibar Mh Mariam Msabaha.

  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na baadhi ya wananchi wa Lindi aliowaalika kwenye futari mara baada ya kuwafuturisha nyumbani kwake,Lindi Mjini jana.
  Mke wa Rais Mama Salma Kkwete akisalimiana na baadhi ya akinamama aliofuturu nao nyumbani kwake Lindi Mjini,jana.
  Baadhi ya wananchi wa Lindi Mjini walioalikwa kufuturu nyumbani kwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakisikiliza mawaidha yaliyokuwa yakitolewa baada kufuturu.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na Shehe Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Al Haj Mohamed Said Mshangani baada ya kufuturu nyumbani kwa Mama Salma huko Lindi Mjini tarehe 27.7.2013. PICHA NA JOHN LUKUWI

  Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wakazi wa mkoa wa Lindi kuishi maisha ya upendo, ushirikiano, umoja na kuwasaidia watu wasiojiweza kwa kufanya hivyo watapata thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

  Mama Kikwete ametoa wito huo jana wakati wa futari ya pamoja iliyowajumuisha watu wa makundi mbalimbali kutoka mkoa huo.

  Mama Kikwete alisema upendo ukiwepo ndani ya jamii watu wataishi maisha ya furaha na amani huku wakisaidiana kwa kupeana vitu vichache walivyonavyo.

  ‘Tuwe watu wa kuishi maisha ya kumpendeza Mwenyezi Mungu siyo wakati huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani peke yake bali katika maisha yetu yote, tusali swala tano na kuamka usiku wa manane muda ambao Dunia imetulia, kila mtu anakuwa amelala.

  Muombe Mwenyezi Mungu akuamshe muda huo ili uweze kusali bila kusahau kumshukuru kwa kukupa uhai na umri uliofikia na hata kama utakufa muda huo hautakuwa na hofu kwani umeshatengeneza mahusiano yako na Mungu”, alisema Mama Kikwete.

  Aliendelea kusema ni muhimu kwa muumini wa dini ya Kiislamu kukumbuka kusali, kufunga na kusaidia watu wenye mahitaji maalum kwa kufanya hivyo atakuwa anajilinda na kujitengenezea maisha mema pindi atakapokufa.

  Mama Kikwete pia alisisitiza umuhimu wa kutunza amani ya nchi na kuwataka wakazi wa mkoa huo wanapokuwa kwenye mikusanyiko mbalimbali ikiwa ni pamoja na misikitini, makanisani kwenye sherehe na misiba wahubiri umuhimu wa amani kwani mahali penye vita hakuna umoja, ushirikiano na upendo.

  Hivi sasa waumini wa dini ya Kiislamu wako katika kumi la pili la kufunga ambalo ni la msamaha kama alivyosema Mtume Swalallahu Alayhi Wassalam (S.A.W) hivyo basi kwa wale wanaofunga wanatakiwa kujikita zaidi kufanya mambo mazuri kwa watu ikiwa ni pamoja na kulisha wengine kwani ukimpa kula na kunywa mwenzako Mwenyezi Mungu anakulipa zaidi.

  0 0


  0 0

  Baadhi ya wanawake wajasiriamali wadogowadogo wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini wakipatiwa elimu na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania hawapo pichani,kabla ya kupatiwa mikopo yao ya pesa isiyokuwa na riba ya zaidi ya shilingi Milioni 327 iliyotolewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa "MWEI".mikopo hiyo inawawezesha wanawake wajasiriamali wadogowadogo nchini kujiendeleza katika biashara zao,na kurudisha mikopo hiyo kwa njia ya M-PESA.
  Mwenyekiti wa kikundi cha tupendane Bi. Rosena Rashid -Mkazi wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini akisaini kitabu cha orodha ya wakina mama wajasiriamali wadogowadogo waliokuwa wakipatiwa mikopo ya pesa isiyokuwa na riba ya zaidi ya shilingi Milioni 327 toka Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa "MWEI"unaowawezesha wanawake wajasiriamali wadogowadogo nchini, na kurudisha mikopo hiyo kwa njia ya M-PESA.anaeshuhudia kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingwa.
  Mwenyekiti wa kikundi cha tupendane Bi.Rosena Rashid- Mkazi wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini akipokea mkopo wa pesa kutoka kwa wakala wa M-PESA wa Vodacom Morogoro,Bw.Verus Bitahilo(alieketi)Kampuni hiyo inatoa mikopo kwa wanawake wadogowadogo wajasiriamali hapa nchini isiokuwa na riba wanawake hao walipokea mkopo huo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 327 kupitia mradi wake wa "MWEI" na kurudisha mikopo hiyo kwa njia ya M-PESA.anaeshuhudia wapili toka kulia walioketi ni Meneja wa mradi huo Bi.Grace Lyon.
  Mwenyekiti wa kikundi cha Mother support Bi.Veronica Nyemele- Mkazi wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini akionesha na kufurahia pesa zake alizopewa mkopo usio na riba toka Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa "MWEI"unaowawezesha wanawake wajasiriamali wadogowadogo nchini, wanawake 7500 walinufaika na mkopo huo wa zaidi ya shilingi Milioni 327.
  Sehemu ya wanawake wajasiriamali wadogowadogo walionufaika na mkopo huo wa zaidi ya shilingi Milioni 327.

  0 0

  Umoja wa Watanzania ujerumani(UTU) kwa kasi kubwa inaiwakilisha vema Tanzania huko Ughaibuni,kwa kutumia nafasi zote wanazopewa nchi Ujerumani, ni juzi kati tu Umoja huo ulishiriki katika maonyesho ya "Brüderschaft der völker " mjini Aschaffenburg, ambapo wageni wengi walivutiwa sana na shughuli za Umoja huo za kuitangaza Tanzania, Umoja wa watanzania ujerumani (UTU) unatilia mkazo sana katika kuwashawishi wadau wa kimataifa wawekeze katika udumua za jamii kama vile Elimu,Afya n.k Umoja huo umepokea mialiko ya kushiriki maonyesho mengine yakiwemo makubwa kama International African Festival Tubingen 2013 yatakayo anza 8 hadi 11.08.2013 usikose kuwasiliana nao at kamati.utu@googlemail.com
  baadhi ya watanzania na marafiki zao ujerumani.
  wadau wa UTU wakiwa katika moja ya maonyesho ya Aschaffenburg.
  Mdau
  baadhi ya bidhaa katika banda la UTU.

  0 0

    Rais Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga katika wilayani BiharamuloRais Jakaya Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga katika wilayani Biharamulo.
   Rais Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi wa Ngara baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo Jumamosi Julai 27, 2013Rais Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi wa Ngara baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo  Rais Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo wilayani NgaraRais Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo wilayani Ngara Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa (1)Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa.Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu (1)Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Akisulubiwa kwa bakora na mmoja wa watu wenye hasira.
  MTU mmoja aliyetuhumiwa kuwa ni mwizi amenusurika kufa baada ya kundi la wananchi kumpa kipigo cha maana, leo mchana katika eneo la Mbezi-Darajani, Kawe mjini Dar es Salaam. Mtu huyo ambaye jina lake halikueza kupatikana mara moja inadaiwa alikutwa akiruka geti kuingia ndani kwenye nyumba ya mkazi moja wa eneo hilo. Picha zifuatazo ni baadhi ya matukio wakati mtuhumiwa huyo alipokuwa akipata kichapo hicho.  
   Akisulubiwa kwa bakora na mmoja wa wananchi hao wenye hasira.
   Mtuhumiwa wa wizi akiomba kusamehewa wakati mtu mwenye hasira akijiandaa kumtupia tofali kichwani ambalo lilimjeruhi vibaya mtuhumiwa huyo
   Akiendelea kuslubiwa wakati wakipelekwa polisi.
   Mwenye hasira akimsulubu mtuhumiwa huyo kwa kumtandika teke.
  Lakini kutokana na kipigo akaanguka hadi hatua iliyofanya watu hao wenye hasira kutawanyika eneo la tukio, wakidhani mtuhumiwa amekufa. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO. 

  0 0

   Rais Jakaya Kikwete akifunua kitambaa cha jiwe la msingi ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa Ujenzi wa Barabara Kyaka-Bugene,Wilaya ya Karagwe,Mkoani Kagera.
  Rais Jakaya Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na baadhi ya watendaji katika mradi wa Ujenzi wa Barabara Kyaka-Bugene,Wilaya ya Karagwe,Mkoani Kagera mara baara ya kuuzindua.

  0 0

   Bwana Harusi Maneno Mbegu akivishwa pete na mwandani wake, Queen Sendiga walipokuwa wanafunga ndoa hivi karibuni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
                       Maneno Mbegu akiapa mbele Ofisa Tawala  Wilaya ya Kinondoni
                                      Queen akila kiapo
                                  Mbegu akitia saini
   Queen akitia saini


older | 1 | .... | 207 | 208 | (Page 209) | 210 | 211 | .... | 3278 | newer