Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 205 | 206 | (Page 207) | 208 | 209 | .... | 3285 | newer

  0 0

   Treni ya abiria aina ya Alvia 730 iliyokuwa ikisafiri kutoka mji wa Madrid kwenda mji wa bandari ya Ferrol,iliyokuwa imebeba abiria wapatao 218,imepata ajali mbaya sana leo na kusababisha vifo vya watu 88 huku wengine 130 wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana. Ajali hiyo imetokea jioni ya leo nje kidogo ya mji wa Santiago de Compostela.Chanzo cha ajali hiyo inasemekana ni moja ya behewa za Treni hiyo kushindwa kukata kona wakati ikiwa kwenye mwendo mkali.
  Msaada ukiendelea kutolewa.
  Waokoaji wakiendelea na kazi ya uokozi kwa abiria walionasa kwenye treni hiyo.
  Ni huzuni imetawala eneo la tukuo huku miili ya waliopoteza maisha ikiwa imefunikwa.
  Uokoaji ukiendelea.


  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka ngao katika mnara wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera Julai 25, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka mkuki katika mnara wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera Julai 25, 2013
  Rais Jakaya Kikwete akitembelea makaburi ya mashujaa waliopoteza maisha wakati wa vita na Nduli Iddi Amini wa Uganda.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0
 • 07/25/13--15:04: Article 10


 • 0 0

  Makamu wa Rais wa Chama cha Wabunge wa CPA Barani Afrika, Mhe. Spika Anne Makinda akitambulishwa kwa Rais wa Namibia, Mhe. Hifikepunye Pohamba wakati wa sherehe ya ufunguzi wa Mkutano wa 44 wa Chama hicho (CPA) barani Afrika. Katikati ni mwenyeji wa mkutano huo na Spika wa Bunge la Namibia, Mhe. Asser Kapere. Jumla ya Wabunge 500 toka nchi 19 wanachama wa CPA barani Afrika wanahudhuria mkutano huo.
  Spika Makinda akihutubia katika mkutano huo.
  Makamu wa Rais wa CPA, Spika Makinda akiwa na baadhi ya wabunge na maafisa wa Tanzania katika mkutano huo pamoja na watanzania, Balozi Bandora ambae ni mwakilishi mkazi wa UNDP nchini Namibia (kwanza kulia) na Dr. William Shija, Katibu Mkuu wa CPA Duniani (kwanza kushoto).

  0 0

  Ndugu David Shinganya wa Kampuni ya SGC INVESTMENTS LTD akikabidhi cheki ya Kwacha Milioni Nane (ZK 8,000,000.00) kwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace J. Mujuma katika kuitikia wito wa wazo la baadhi ya Watanzania waishio nchini Zambia walilolitoa kuchangia ukarabati wa Jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia. Hafla hiyo ya kukabidhi cheki ilifanyika hivi karibuni Ofisini kwa Balozi Mujuma ikishuhudiwa na Maafisa wawili  0 0

  Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi (MUWSA) Cyprian Luhemeja akichangia jambo katika kikao cha naibu waziri wa maji Dk Mahenge na watendaji wa idara ya maji.
  Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini Dk Cyril Chami akichangia jambo katika kikao hicho.
  Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge(aliyesimama) akizungumza na watendaji wa maji pamoja na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Moshi.waliokaa kutoka shoto ni Suleiman Moshi(RSO),Mkuu wa wilaya ya Moshi Dk Ibrahim Msengi na wa mwisho kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz.
  Mhandisi wa maji wilaya ya Moshi vijijini Brown Lyimo akitoa maelezo mbele ya naibu waziri wa maji Dk Mahenge alipotembelea mradi wa maji wa Mbokomu wilaya ya Moshi vijijini.
  Miongoni mwa mambo ambayo yalionekana kumkera naibu waziri ni pamoja na upotevu huu wa maji kama inavyoonekana hapa huku wahusika wakiweka mti ili kuzuia maji yasitoke badala ya koki.hapa naibu waziri akimuuliza mhandisi wa iwlaya kuhusu tatizo hilo.

  Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi

  SERIKALI imetaka mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira nchini sanjari na halmashauri za miji,manispaa na majiji kuipa kipaumbele miradi ya maji katika maeneo ili kupunguza uwezekano wa kuwapo kwa maradhi ya milipuko yanayochangiwa na ukosefu wa maji safi na salama.

  Naibu waziri wa maji Dk Bilinith Mahenge aliyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa wilaya ya Moshi wakiwamo wakurugenzi wa halmashauri za Manispaa ya Moshi na Moshi vijijini wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Kilimanjaro kukagua utekelezaji wa miradi ya maji.

  Amesema kuna umuhimu kwa mamlaka na miji hiyo kutenga sehemu ya fedha katika bajeti zao kila mwaka kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji huku wizara ikiendelea kutoa misaada katika miradi mikubwa na masuala ya kiufundi.

  “Lazima mtenge fedha za miradi ya maji kila mwaka,msipofanya hivyo, sisi tunajua hilo siyo jambo la kipaumbele, lakini kumbukeni upatikanaji wa maji unawasaidia wananchi kupunguza fedha ambazo wangetumia kwa matibabu baada ya kuugua matumbo na watazifanyia shughuli za kiuchumi”alisema.

  Kuhusu wingi wa maji naibu waziri alipongeza juhudi za mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi(MUWSA) kwa kuvitunza vyanzo vya maji Nsere, uchimbaji kisima cha eneo la longuo, tanki la kuhifadhi maji Kilimanjaro na CCP ambavyo kuna miti yenye kuhifadhi maji.

  Akizungumzia mradi wa vijiji 10 unaofadhiliwa na benki ya dunia, alitaka kila halmashauri kuhakikisha unatekelezeka kwa wakati ili kupunguza idadi ya watu wanaokosa maji.

  Hata hivyo alikiri kuwapo kwa changamoto ya mgawo wa vijiji 10 hata kwa halmashauri ambazo ni kubwa zenye vijiji zaidi ya 100 ambazo nazo zinatakiwa kuainisha vijiji 10 jambo ambalo alidai linatakiwa kutazamwa upya.

  “Lazima tuangalie upya vigezo vya ugawaji wa mafungu ya fedha kwa kuzingatia ukubwa wa wilaya kwani sasa inazingatia idadi ya watu,aina ya teknolojia ya mradi wa maji,maeneo mengine teknolojia mtiririko ambayo ni gharama sana na mengine ni ya visima au mabwawa”alisema.

  0 0
 • 07/25/13--15:19: PAMOJAH NITE!!!!!
 • Pamoja Nite is a get together reggae event, intended to showcase the best reggae DJs, quality sounds and interactive atmosphere. The event aims to gather the youths and everyone who accepts the invitation to come and enjoy quality entertaining moment. The night will also feature the display of handmade crafts which has always blended well with the theme of reggae as a way of networking and acknowledging efforts of our local artists. The event is scheduled to take place on 16th August, 2013 at New Msasani Club from 9pm TILL DOWN!!!!!,

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (RUBADA), Bw. Aloyce Masanja akisisitiza jambo wakati wa semina ya kuwajengea uwezo watendaji na madiwani wa halmashauri ya mji wa Makambako juu ya Mpango wa Uendelezaji wa Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) jana mkoani Njombe.

  Na Mwandishi wetu, Makambako

  Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (RUBADA) imewataka madiwani na watendaji wa idara mbalimbali katika Halmashauri ya Mji Makambako kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake watumie fursa zilizopo ikiwa ni pamoja na rasilimali watu ili kuchoche kasi ya ukuaji wa maendeleo katika halmashauri hiyo.

  Mkurugenzi Mkuu wa RUBADA, Bw. Aloyce Masanja Alitoa kauli hiyo wakati wa semina ya kuwajengea uwezo watendaji na madiwani wa halmashauri hiyo juu ya Mpango wa Uendelezaji wa Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) jana mkoani Njombe.

  “Ndugu zangu naomba tufanye kazi, haya mambo ya kulaumiana hayawezi kutufikisha popote, ni vema kila mtu akatimiza wajibu wake mahala pake pa kazi, ili kufikisha taifa hili kule linakotakiwa kwenda,” alisema.

  Aidha alimewaomba madiwani na watendaji kutoa ushirikiano kwa mamlaka hiyo katika kuanisha maeneo ambayo yanafaa kwa kilimo ili yaweze kutafutiwa wawekezaji watakaowekeza katika sekta hiyo pana hapa nchini na kuleta maendeleo katika mji huo.

  “Mamlaka siku zote inahakikisha wananchi wanafaidika sambamba na uwekezaji unaofanyika katika maeneo yao…nawaomba wana Makambako mlitambue hilo,” alisisitiza Masanja.

  Aliwataka watendaji hao kuwatumikia wananchi wao kwa nguvu zao zote ikizingatiwa kuwa mji huo bado ni mdogo na unahitaji kuendelezwa kwa kiasi kikubwa ili kuubadilishisha tofauiti na ilivyo sasa.

  “Makambako bado inakuwa hivyo ni jukumu lenu kuanza kutumia fursa ambazo mnazo hasa rasilimali watu, nimeona vijana wa hapa wana nguvu na wanajituma katika kufanya kazi za shamba, watumieni hawa mtaona faida yao,” alieleza Mkurugenzi huyo.

  Aliwakumbusha watendaji hao kuwa katika mkakati wa serikali wa matokeo makubwa sasa, (Big Results Now) hakuna kulala na kwamba kasi katika kufanya kazi za kuwatumikia wananchi ndio jambo la msingi.

  “Kila mtu atakuwa akipimwa kutokana na utendaji wake, kama hutaweza kutekeleza yale uliwekewa kuyafanya basi utajikuta unawekwa pembeni…tufanye kazi kujenga nchi na si vinginevyo,” aliongeza.

  Akizungumza kwa niaba ya madiwani na watendaji wa halmashauri ya mji Makambako, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo diwani Chesco Mfikwa alisema halmashauri hiyo imejipanga vema katika kuibua miradi mingi ya maendeleo.

  “Sisi wana Makambako tupo tayari kushirikiana na RUBADA katika mpango wa SAGCOT ili kujenga uchumi wa mji wetu na watu wetu ili tuweze kujitegemea,” alisema Mfikwa.

  Aliongeza kuwa semina waliyopata kutoka kwa mamlaka hiyo imewafungua macho kwa kiasi kikubwa hivyo mkakati wao ni kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuendeleza kilimo hasa kilimo cha umwagiliaji katika eneo hilo.

  “Semina imetujenga kwa kiasi kikubwa mimi nikiwa mwenyekiti nitakuwa mstari wa mbele kuwahimiza vijana kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali ili kukuza kilimo katika halmashauri yetu na kuleta mabadiliko ya kweli,” aliongeza.

  0 0

  Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA wakiwa nje ya nyumba ya Rais wa Kwanza mzalendo Nelson Mandela jijini Johannesburg, Afika ya Kusini. Kutoka kushoto ni Festo Sikagonamo (ITV), Albano Midelo (Nipashe), Phinias Bashaya (Mwananchi), Lilian Shirima (TBC 1) na Alex Magwiza (TBC Taifa).
  Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA wakiwa na mwanahabari kutoka Reuters aliyetega camera yake nje ya nyumba ya Mzee Nelson Mandela.
  Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA wakitembelea Jengo la Mahakama ya Katiba Johannesburg.
  Lilian Shirima wa TBC 1 akiwa amembeba kitukuu cha Mzee Nelson Mandela mara baada ya kutembelea nyumbani kwa Winnie Mandela.
  Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA wakiwa nyumbani kwa Winnie Mandela.
  Festo Sikagonamo akiangalia kwa umakini kitanda kilichokuwa kikitumiwa na Mzee Nelson Mandela.

  0 0


  0 0

  Video na Joshua Mmali.

  Oliver Mtukudzi alitoa burudani bure kwa wakazi wa New York katika eneo la kupumzika  Free Park, maelfu ya wamarekani walifurika katika show yake. Hii inafundisha nini wasanii wa nyumbani Tanzania? Nafikiri kuna jambo kubwa sana la kujifunza toka kwa mkongwe huyu. 
  Oliver si mjinga kutoa burudani ya bure, wasanii wetu toka Tanzania inabidi waige mfano huu ili mziki wao uanze kuwaingia wamarekani na hata mataifa mengine ya nje. Nazungumzia msanii kujulikana na kukubalika katika kiwango cha kimataifa  katika soko la mziki la dunia.

  Namalizia kwa kuwapongeza mapromota wote wanaowatafutia show wasanii toka nyumbani kutoa burudani nje ya nchi. Kwa kweli wanafanya kazi nzuri. Sasa nawaomba waanze kutafuta masoko nje ya jamii zetu za kitanzania na Afrika mashariki kwa ujumla. Hii namaanisha sio kuimba pekee katika klabu za wabongo ama wakenya.

   Mtakubaliana nami wasanii mliowahi kutoka nje ya Tanzania nadhani mnaelewa nachosema. Sisi mashabiki wenu tunataka kuona mkipanda na kushiriki katika majukwaa makubwa yanayoheshimika duniani. Ni furaha yangu nitakapoona msanii wetu anatoa burudani katika viwanja vikubwa hapa Marekani na kwingineko, naamini inawezekana.

  kuona mengi toka Swahili TV Mtaani Kunani tembelea www.swahilitv.blogspot.com


  0 0

  Pichani ni Mather Joseph mwenye umri wa mika 16. ni manfunzi wa Chuo cha ufundi cha Santer Peter Parish aliondoka nyumbani akielekea shuleni huko oysterbay akiwa amevalia ngua za shule sketi ya damu ya mzee na shati jeupe (uniform)

  Tangu siku hiyo hajaonekana wala hatuna taarifa zozote tumemtafuta katika Hospitali zote za jijini Dar es Salaam, ikwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Mwananyamala,Amana na kwingineko lakini bado hatujafanikiwa kumpata.

  Pia taarifa hizi zimeripotiwa katika kituo cha Polisi cha kigamboni ,kwa arb namba ,KGD/RB 5017/2013 kwa yeyote atakaye muona atoe tarifa katika kituo chochote kilicho[po karibu naye.

  Nyumbani kwao ni Kigamboni kota za Jeshi la Wanamaji Kigamboni, Kabila lake ni msukuma.kwa mawasiliano zaidi wasiliana na 0718 038128.

  0 0


  0 0

  Na Mwandishi Maalum 
   Wakati hali ya usalama ikiendelea kuwa tete Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kufuatia kuibuka upya kwa mapigano hivi karibuni. Marekani imetamka bayana mbele ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwamba, inakaribisha na kuunga mkono upelekaji wa Brigedi Maalum ( Force Intervention Brigade) pamoja na mamlaka iliyopewa kupitia Azimio namba 2098 la 2013. 
  Brigedi hiyo Maalum inaundwa na wanajeshi kutoka Tanzania, Afrika ya Kusini na Malawi. Na imepewa mamlaka na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ya, pamoja na mambo mengine, kuyakabili na kuyadhibiti na ikibidi kutumia nguvu za ziada pamoja na kuyapokonya silaha makundi ya wanagambo wakiwamo M23 na FDRL. 
   Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Bw. John Kerry ameyasema hayo wakati alipokuwa akiongoza mkutano wa Baraza Kuu la Usalama katika ngazi ya Mawaziri ulioandaliwa na Marekani ambaye ndiyo Rais wa Baraza hilo kwa Mwezi huu wa Julai. 
  Ajenda iliyoandaliwa na Marekani na kujadiliwa na Baraza hilo siku ya Alhamisi ilihusu hali katika Eneo la Maziwa Makuu na Uungaji mkono Mpango Mpana wa Kisiasa wa Umoja wa Mataifa wa Amani , Usalama na Ushirikiano wa Maendelea katika DRC na eneo la Maziwa Makuu (PSC Framework). 
  Anasema Bw. Kerry “ Marekani inakaribisha upelekaji wa Brigedi Maalum na inaunga mkono mamlaka iliyopewa ya kutangua makundi yote ya wanamgambo yenye silaha, na kuwalinda raia ili hatimaye Amani iweze kutawala” Amesisitiza kwa kusema, Marekani inaunga mkono jitihada zote za kutafuta Amani katika DRC ikiwa ni pamoja na kuziunga mkono nchi 11 na wadhamini wanne (11+4) waliotia saini mpango mpana wa kisiasa na kwamba itashirikiana nao katika utekelezaji wa mpango huo. Hata hivyo amesema ,nchi yake inasikitishwa sana na taarifa mpya na za hivi karibuni zinazoonyesha kwamba bado makundi ya waasi ya M23 na FDRL yanaendelea kupewa misaada kutoka nje. 
  Na kwa sababu hiyo, amesisitiza kwa kuzitaka pande zote zinazohusika kuacha mara moja kuyasaidia makundi hayo na kwamba kila nchi ihakikishe wale wote wanaokiuka haki za binadamu wanachukuliwa hatua na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. 
  Kama hiyo haitoshi Bw. Kerry ametoa changamoto kwa nchi zote ambazo zimetia saini PSC Framework kuheshimu na kutoiingilia DRC katika mambo yake ya ndani ikiwamo mipaka yake. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, Mshauri wake Maalum katika Maziwa Makuu, Bi. Mary Robinson, Mawaziri kadhaa wakiwamo wa kutoka nchi za Maziwa Makuu, SADC, EU, na Umoja wa Afrika na Mkuu wa Bank ya Dunia aliyeongea kwa njia ya Video kutokea Washgton DC. 
   Waziri huyo wa Marekani pia amesema suala la eneo la Maziwa Makuu na DRC ni moja wapo ya vipa umbele vya serikali ya Rais Obama na kwamba kwa kuutambua umuhimu huo, Obama amemteua, Seneta mstaafu, Bw. Russ Feingold anayetajwa kuwa na uzoefu na utaalam mkubwa kuhusu masuala ya Afrika kuwa Mjumbe Maalum wa Marekani katika Maziwa Makuu. Miongoni mwa nchi chache nje ya wajumbe wa Baraza Kuu zilizokaribishwa kuzungumza katika mkutao huo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
   Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Balozi Tuvako Manongi aliweka bayana msimamo wa Tanzania kuhusu suala zima la ushiriki wake katika mchako mzima wa utafutaji wa Amani ya kudumu katika DRC. Katika mchango wake Balozi Manongi alianza kwa kulikumbusha Baraza Kuu la Usalama tamko la Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwamba, suluhu ya upatikaji wa Amani ya kudumu katika DRC haiwezi kuwa kwa njia za kijeshi bali ni kwa mchakato wa kisiasa na ambao nyuma yake kuna utekelezaji wa PSC Framework. 
   Na kwamba suala la kuyahusisha makundi yote katika majadiliano bila ya kubaugua haliepukiki. Na kwa sababu hiyo akasema ndiyo maana Tanzania inaunga mkono na kushiriki juhudi zote za kimataifa na kikanda zikiwamo za utekelezaji wa mpango mpana wa kisiasa, pamoja na utoaji wa wanajeshi wake kushiriki katika Brigedi Maalum kama sehemu ya MONUSCO kwa mamlaka iliyoainishwa katika Azimio namba 2098(2013) la Baraza Kuu la Usalama. 
  Akasema Brigedi hiyo Maalum inahitaji kuungwa mkono na watu wote na hasa kutoka Baraza Kuu la Usalama. Akasisitiza kwamba Brigedi Maalum haipashwi kuvunjiwa heshima kwa tuhuma za uongo na zisizokuwa na ushahidi wowote. 
  Balozi Tuvako Manongi amesema katika siku za hivi karibuni kumeibuka tuhuma dhidi ya uongozi wa juu wa Brigedi Maalum na kwamba tuhuma hizo za kuwapaka matope wale wote ambao wamejitolea kwa nia njema kusaidia katika eneo la Mashariki ya Kongo, zinatia shaka. 
  Na kwa sababu hiyo Tanzania kupitia Mwakilishi wake huyo imelitaka Baraza Kuu la Usalama, lidai ushahidi dhidi ya tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwa Uongozi wa Juu wa Brigedi Maalum Akalikumbusha Baraza Kuu kwamba hata Tanzania iliwahi kupata heshima ya kuwa mjumbe wa Baraza hilo, heshima ambayo iliibeba kwa dhamana kubwa , ikikatekeleza wajibu wake kwa uadilifu wa hali ya juu kwa sababu ilitambua iko ndani ya chombo hicho kuiwakilisha Afrika na Jumuiya ya Kimataifa kwa ujumla na kamwe si kwa maslahi binafsi au kuitumia vibaya nafasi hiyo. Akasisitiza kwamba lazima Baraza Kuu la Usalama lichukue hatua madhubuti za kuwalinda wale ambao wamekabidhiwa jukumu hilo adhimu. 
  Aidha akasema Tanzania inalipongeza Baraza Kuu la Usalama kwa kuendelea kuunga mkono MONUSCO katika utekelezaji wa mamlaka iliyokabidhiwa licha ya mlolongo wa kampeni chafu kutoka kwa makundi ya waasi na waharibifu wengine. 
  Akasema Tanzania inaamini kwamba, kampeni hizo chafu na tuhuma zisizokuwa na ukweli dhidi ya Brigedi Maalum zinalenga kudhoofia utekelezaji wa mpango mpana wa kisiasa na kudhoofidha mamlaka ya MONUSCO. 
   “ Tunaamini jumuiya ya kimataifa itashinda, hakuna nguvu au propaganda chafu zitakazodhoofisha kiu ya kutafuta amani, usalama na ustawi katika eneo la Maziwa Makuu. Huu ndiyo Mpango wa Matumaini ambao Tanzania inaunga na itaendelea kuunga mkono.” Akasisitiza Balozi Manongi. Baadhi ya nchi zilizozungumza zikiwamo Ufarasa na Uingereza zimeunga mkono mchakato wote wa upelekaji wa Brigedi Maalum huku Uingereza ikisema tuhuma za uongo na zisiokuwa na ushahidi dhidi ya Brigedi hiyo hazina maana yoyote na zinalenga kudhoofisha upatikanaji wa Amani. 
  Na ikatakakuharakishwa upekelekaji wa teknolojia ya kisasa ya ndege ambazo haziendeshwi na binadamu ( UAVs) Waziri kutoka Ufaransa yeye alikwenda mbali Zaidi kwa kuitaka FIB ianza kazi haraka iwezekanavyo. Mwishoni mwa mkutano huo ilitolewa taarifa ya Rais wa Baraza Kuu, taarifa ambayo pamoja na mambo mengine ilielezea uungwaji mkono wa Brigedi Maalum, huku ikitaka makundi ya waasi wanaopigana kuacha mara moja mapingano.
    Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza kwaniaba ya Serikali katika mkutano  huo ambapo alilitaka  Baraza Kuu la Usalama  Kudai ushahidi dhidi ya tuhuma na propaganda za uongo  ambazo zimekuwa zikielekezwa  dhidi ya Uongozi wa Juu wa  Brigedi  Maalum ambayo inaundwa na wanajeshi kutoka Tanzania, Afrika Kusini na Malawi.   Akasema  tuhuma hizo  zinazoipaka matope FIB bila  ya sababu zote za msingi zinalenga katika kudhoofisha mamlaka ya Brigedi hiyo na MONUSCO kwa Ujumla katika  kutafuta amani ya kudumu  DRC na kwamba Baraza  Kuu linawajibu wa kuwalinda wale wote ambao siyo tu wamejitolea kusaidia upatikanaji wa amani lakini pia wanabeba dhamana iliyoadhimu.  Tanzania ilikuwa kati ya nchi chache zilizoalikwa kuzungumza katika mkutano huo.
   Waziri  wa Mambo ya Nje wa Marekani, Bw. John Kerry,  alizungumza wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,  uliokuwa ukijadili hali katika eneo la  Maziwa Makuu na  uungaji mkono Mpango Mpana wa Kisiasa wa Umoja wa Mataifa wa  Amani, Usalama na  Ushirikiano wa Maendeleo katika Jamhuri ya  Kidemokrasia ya Kongo na Maziwa Makuu.  Mkutano huo uliokuwa katika  ngazi ya Mawaziri umeandaliwa na Marekani ambaye ni Rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu wa Julai. katika  hotuba yake, Waziri Kerry amesema  Marekani inakaribisha na kuunga mkono  upelekaji wa Brigedi Maalum ( FIB) katika eneo la Mashariki ya Kongo na  pia   inaunga mkono na itashirikiana na  nchi 11 zilizotia saini    Mpango  mpana wa kisiasa  ili  kuhakikisha   unatekelezwa na kufanikiwa.
   Taswira ya Ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  ulivyokuwa siku ya Alhamisi wakati wa mkutano uliojadili hali katika eneo la  Maziwa Makuu, mkutano huo ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon,  Mwakilishi wake wa Maziwa Makuu  Mary Robinson, Mawaziri kutoka  nchi za Maziwa Makuu, SADC , Umoja wa Afrika,  EU, na Mkuu wa Banki ya Dunia aliyeongea kwa njia ya Video kutokea  Makao Makuu ya Banki hiyo jijini Washington.

  0 0
 • 07/26/13--01:17: Article 22
 • "Hongera...Weruweru,umlezi wetuuu...."If this line reminds you of our beloved school,then this is for you.
  In preparations for our big celebrations of Weruweru's Golden Jubilee,we have a meeting on Sunday at Cine Club...Yes,This Sunday from 3pm.

  If you are a Weruweru girl or you know one,please pass the message along. Use the numbers above on the poster to confirm and/or ask for more info.

  Remember to come with a scarf of the color of your skirt during them good days...Or if you still have your Shamba dress :)

  Looking forward to seeing you,

  xoxo
  Missie Popular

  0 0
 • 07/26/13--01:21: Mapigano yatishia wengi DRC
 • Mapigano baina ya majeshi ya serikali na waasi wa M23 yanazidi kuhusu wananchi wa vijiji ambao wanalazimika kupigana kulinda miji yao.

  0 0
 • 07/26/13--01:59: RAIS KIKWETE WILAYANI MULEBA
 • Rais Kikwete akivikwa skafu na skauti baada ya kuwasili Muleba
  Vikundi vya ngoma vikitumbuiza wageni
  Rais Kikwete akisalimiana na mama wa Profesa Anna Tibaijuka
  Waziri wa Ardhi Profesa Anna Tibaijuka akishiriki katika ngoma ya utamaduni wakati wa mapokezi ya Rais Kikwete wilayani Muleba
  Rais Kikwete akiongea na viongozi wa wilaya ya Muleba baada ya kupokea taarifa ya maendeleo, akiwa na mawaziri watano anaoongozana nao katika ziara hiyo.

  TEMBELEA LIBENEKE LA IKULU MAWASILIANO KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na A bdulaziz Video Lindi

  Wakazi wa Manispaa ya Lindi, kwa takribani juma moja sasa, wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa upatikanaji maji safi na salama na kulazimika kutumia maji ya visima vya kienyeji vilivyochimbwa kwenye baadhi ya makazi ya watu.

  Baadhi ya wananchi waliohojiwa na Mtandao huu kuhusiana na tatizo hilo, wameonesha hofu yao ya kutokea kwa milipuko ya magonjwa ya matumbo ikiwemo kipindupindu kwa vile maji ya visima wanayotumia kwa sasa siyo safi na salama kwa matumizi ya binadamu.

  Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Maji safi na Usafi wa Mazingira Lindi mjini(LUWASA), Idrisa Sengulo, pamoja na kukiri kuwepo kwa tatizo hilo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Mamlaka, amewaomba radhi wananchi kwa tatizo hilo ambalo amesema kama mambo yakienda vizuri linaweza kutatuliwa ktk kipindi cha siku mbili zijazo.

  Amesema mahitaji ya maji kwa wakazi wa Manispaa ya Lindi ni lita milioni 5 kwa siku, ikilinganishwa na lita lita milioni 1,340,000 tu kwa siku zinazopatikana kwa sasa.

  0 0

  MBEYA MANAGEMENT CONSULTANTS CERTIFIED ACCOUNTANTS IN PUBLIC PRACTICE

  Tunatangaza nafasi ya kazi ya mwasibu aliyehitimu chuo kikuu na kupata shahada au stashahada ya Accountancy

  Vigezo:
  Awe na GPA isiyopungua 3.2 points
  Awe na Advance Diploma in Accountancy or B.Com in accountancy or Bachelor of Accountancy or Bachelor of Accountancy and Finance.

  Mwombaji atume application letter, CV, Pamoja na attachment za vyeti copy kwenda kwenye email address: swayzlight@yahoo.comor gstanzanie@yahoo.com 

   Mwisho wa maombi ni tarehe 2/08/2013.

  0 0
 • 07/26/13--02:07: Vacancy at SmartCodes

older | 1 | .... | 205 | 206 | (Page 207) | 208 | 209 | .... | 3285 | newer