Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

TANESCO "YALIA" NA WAHARIBIFU WA MAZINGIRA MITO INAYOLISHA BWAWA LA MTERA

$
0
0
 Taswira ya daraja la Mtera, ambalo pia hutumika kama milango ya kupitishia maji ya kusukuma mashine za kufua umeme. picha hii imepigwa Desemba 20, 2017.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mtera


UHARIBIFU wa mazingira unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi na shughuli za kibinadamu kwenye bwawa la Mtera sio tu unaathiri kiasi cha maji kwa matumizi ya Kituo cha kufua umeme cha Mtera bali pia unaathiri pakubwa kituo kingine cha kufua umeme cha Kidatu mkoani Morogoro, Mtaalamu wa Mazingira wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, Bw. Yusuf Kamote amewaambia waandishi wa habari waliotembelea Kituo cha Kufua Umeme wa Maji cha Mtera, kilichoiko mpakani mwa mikoa ya Dodoma na Iringa.

Ukiachilia mbali mabadiliko ya tabia nchi, shughuli za kibinadamu kandokando ya mito, kunachafua mazingira ya mito hiyo na kupunguza kiasi cha maji na hivyo kuathiri uzalishaji umeme wa maji.

“Tatizo hili ni kubwa watu wanaingilia mito hii, kuna wakulima na wafugaji wanathiri sana, shughuli za kilimo na ufugaji zinaleta mchanga mwingi kwenye maji na hivyo kupunguza kina cha mto na maji yenyewe tunaita siltation, na hiyo ikitokea ujio wa maji kwenye mitambo unapungua na hivyo uzalishaji unapungua kama hivi sasa mnavyoona maji yamepungua.” Alisema.

Bw. Kamote aliwaasa wananchi kuacha kuaharibu mazingira kwani athari zake ni kubwa katika kuendesha mitambo ya kufua umeme ambao ni muhimu kwa uchumi wanchi.“Yawezekana wanafanya shughuli hizo kwa kutokujua athari zake katika uzalishaji umeme, kwa hivyo tunashauri wananchi waelewe kwamba hilo ni tatizo na waache.” Alisetoa rai Bw. Kamote.
Mtaalamu wa Mazingira wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, Bw. Yusuf Kamote, akielezea jinsi mabadiliko ya tabia nchi na shughuli za kibinadamu zinavyoathiri bwawa la Mtera. Kushoto ni Mhandisi Myumbilwa
Daraja la Mtera, ambako pia ndiko iliko milango ya kupitishia maji ya kufua umeme
Kaimu Meneja wa Kituo cha kuzalisha umeme wa maji Mtera, Mhandisi David Myumbilwa, akielezea jinsi mashine za kufua umeme zinavyotegemea maji.
Wahariri wakiangalia jinsi moja kati ya mashine mbili za kufua umeme wa maji inavyofanya kazi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAKOSA YA JINAI YAZIDI KUPUNGUA: DCI ROBERT BOAZ

MVUA KUBWA YA UPEPO MKALI YASABABISHA MAAFA VIJIJI VYA UKENYENGE NA NEGEZI WILAYANI KISHAPU MKOANI SHINYANGA

$
0
0
Na Robert Hokororo, Kishapu

Mvua kubwa ya upepo mkali imesababisha maafa katika vijiji vya Ukenyenge na Negezi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ambapo imeezua paa za nyumba 37 pamoja na majengo Serikali.

Tukio hilo lilitokea saa 12 jioni ambapo majengo yaliyopatwa na maafa hayo ni ya pamoja na ofisi ya tarafa ya Negezi, ofisi ya afisa kilimo, ofisi ya TCRS.

Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Sahadrack Kengese alitembelea eneo hilo yalipotokea maafa akiwa amembatana na wataalamu kutoka halmashauri kwa ajili ya kufanya tathimini ya tukio hilo.Mratibu wa Maafa Wilaya, Ponsian Kuhabwa na Mwesiga Katunzi kutoka Idara ya Ujenzi waliungana na viongozi wa tarafa na kata na kufanya tathimini hiyo ambapo bado hasara iliyotokea haijafahamika.

Kwa mujibu wa maelezo ya Afisa Tarafa, David Isanga mara baada ya tukio hilo uongozi wa tarafa na kata ulishirikiana na wananchi kuhakikisha wanawasaidia wenzao walioathirika ili kurudisha hali.Tathimini inaonesha kuwa hali ya maafa sio ya kutisha na ipo katika uwezo wa jamii kusaidiana na kuwa katika jengo la tarafa inaonyesha mahitaji mbalimbali ili kulirudisha katika matumizi.

Hatua zinazotakiwa kuchukuliwa ni pamoja na ukarabati kufanyika haraka ili watumishi wapate sehemu za kufanyia kazi kwani sasa hivi wanabanana katika vyumba viwili vilivyosalimika.Aidha, timu ya tathmini ilishauri kuendelea kupanda miti mbele ya jengo hilo ili kupunguza kasi ya upepo na kutunza mazingira katika eneo hilo. Pia wananchi wameshauriwa kupanda miti na kujenga nyumba imara ambazo zitasitahimili mitikisiko ya matukio kama haya.
Picha mbalimbali zikionesha nyumba zilivyoezuliwa paa baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha katika vijiji vya Ukenyenge na Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu.

MASHEHA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA WAPEWA TAARIFA YA UJENZI WA BARABARA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Mustafa Aboudjumbe kushoto akijibu maswala mbalimbali yalioulizwa katika Kikao Maalum cha kutoa taarifa kwa Masheha kuhusiana na Ujenzi wa Barabara inayoanzia Chuini,Mfenesini,Mahonda hadi Mkokotoni inayotarajiwa kuanza mwezi wa January hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Sheha wa Shehia ya Matemwe Denge Khamis Silima akiuliza maswali katika Kikao Maalum cha kutoa taarifa kwa Masheha kuhusiana na Ujenzi wa Barabara inayoanzia Chuini,Mfenesini,Mahonda hadi Mkokotoni inayotarajiwa kuanza mwezi wa January hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A Hassan Ali Kombo akiliza maswali katika Kikao Maalum cha kutoa taarifa kwa Masheha kuhusiana na Ujenzi wa Barabara inayoanzia Chuini,Mfenesini,Mahonda hadi Mkokotoni inayotarajiwa kuanza mwezi wa January hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

ANTU MANDOZA KUTIMIZA NDOTO YAKE YA KUIGIZA NA RAMSEY NOAH KUTOKA NCHINI NIGERIA

$
0
0
 
 Antu Mandoza akiwa katika picha ya pamoja na Muigizaji nyota wa Filamu kutoka nchini Nigeria Ramsey Noah wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwigizaji nyota wa filamu na Mkongwe wa tasnia hiyo kutoka nchini Nigeria ,Ramsey Noah ametamani kufanya kazi na nyota mwingine wa movie anaechipukia kwa kasi katika tasnia hiyo hapa nchini,ambae ameng'ara vilivyo katika filamu ya 'KIUMENI' , Antu Mandoza wa Tanzania . 
 
"Anaonekana ni binti mweye kipaji,anaejiamini,kwa hakika natamani nipate muda wa kubaini kipaji chake zaidi kwa kufanya nae angalau hata filamu moja,itaweza kumsaidia zaidi kujitanua na kutambulika Kimataifa",alisema Ramsey huku akimtazama Antu kwa tabasamu laini la ucheshi.
 
Antu Mandoza ni Binti wa makamo hivi,lakini amejaaliwa kuwa na kipaji cha uigiza wa filamu na mwenye uthubutu wa kufanya jambo.Antu Mandoza na Ramsey Noah walikutana katika Warsha fupi iliyoandaliwa na Sahara Group iliyofanyika hotel ya Hyatt Dar Es Salaam mnamo Desemba 16 2016,ambayo pia iliwahusisha wasanii mbali mbali wa bongo movie .
 
 Ikiwa ni movie yake ya kwanza 'KIUMENI', Antu Mandoza amefunguka na kusema kuwa mwaka ujao utakua ni mwaka wa kazi tu, kama ilivyo Slogan ya Raisi Dkt John Pombe Magufuli,na anategemea kufanya kazi na Ramsey Noah na wasanii wengine wengi wa Ndani na Nje ya Tanzania. 
 
Antu alijipatia Umaarufu katika filamu ya Kiumeni aliyocheza na Ernest Napoleon,ambayo lishinda tuzo 2 ZIFF mwaka 2017.

YALIYOJIRI KATIKA ZIARA YA KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR, MKOA WA KASKAZINI PEMBA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Bwana Omari Khamis Othman Akizungumza na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (kulia) na Ujumbe aliofuatana nao alipomtembelea ofisini kwake, wakati akiendelea na ziara ya kikazi Mkoani humo tarehe 20 – 21 Disemba, 2017. Mkuu huyo wa Mkoa aliahidi kushughulikia kwa karibu ombi lilitolewa na Kamishna Sururu, la kupatiwa Viwanja kwenye maeneo yaaliyotengwa na Serikali ili kujenga Nyumba za Makaazi ya Askari wa Jeshi la Uhamiaji Mkoani humo. 

 Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akisikiliza maelezo yanayotolewa na Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Iddi A. Iddi wa Kituo cha Uhamiaji Bandari ya Wete, kuhusu ukaguzi wa Watu wanaotumia Bandari hiyo, ambapo vyombo vyake havijaruhusiwa kisheria kusafirisha abiria. Ilielezwa kuwa hiyo ni changamoto kubwa katika Bandari hiyo kwani abiria wengi wanaotumia Bandari hiyo hudai kuwa wanakwenda kwenye visiwa vya jirani vya Fundo, Uvinje na Kokota, badala yake wakifika Bandari bubu zilizoko kijiji cha Mtambwe wanabadili chombo kuelekea Visiwa vya Mombasa, Kenya. Yalisemwa hayo wakati wa ziara ya kikazi Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe 20 – 21 Disemba, 2017. 

 Mkuu wa Bandari ya Wete, Bwana Hassan Hamad Ali akimpokea na kumkaguza maeneo mbali mbali ya Bandari hiyo Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa pili kushoto) na Maafisa Waandamizi wa Uhamiaji aliombatana nao katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe 20 – 21 Disemba, 2017. Kamishna Sururu alimtaka Mkuu huyo kushughulikia kwa karibu changamoto iliyopo ya baadhi ya vyombo vya Usafiri “Majahazi” bandarini hapo kupakia abiria kinyume cha Sheria.  

 Mkaguzi wa Uhamiaji, Omari Saidi Mohamed akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (katikati) na Maafisa Waandamizi wa Uhamiaji Aliombatana nao Nyumba za Makaazi ya Askari wa Uhamiaji zilizoko mtaa wa Mtemani, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati wa ziara ya kikazi Mkoani humo tarehe 20 - 21 Disemba, 2017. Kutokana na uchakavu wa nyumba hizo, Kamishna Sururu aliagiza nyumba hizo zifanyiwe ukarabati haraka iwezekanavyo, huku akiahidi kwamba, Idara yake kwa kushirikiana na Serikali 
 Sheha wa Shehia ya Gando, Bw. Jafari Suleiman Said (wa pili kulia) akizungumzia uwepo wa Bandari bubu ya Chokaani, Shehia ya Gando Wilaya ya Wete inayotumiwa na baadhi ya watu kuingia na kutoka Visiwani humo kwenda visiwa vya Mombasa, Kenya. Hayo yalielezwa kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu wakati akiendelea na ziara yake ya kikazi Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe 20 – 21 Disemba, 2017. 

 Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa pili kulia) akiwa mbele ya Jengo la Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba iliyofanyiwa ukarabati mkubwa na kujengwa uzio hivi karibuni, akifafanua jambo kuhusu mkakati wa Idara wa kuboresha Majengo ya Ofisi na Makaazi ya Askari wa Uhamiaji kwa Mikoa yote Unguja na Pemba. Huo ni muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani humo tarehe 20 – 21 Disemba, 2018. 

 Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa pili kushoto) akipokea salamu za Wananchi wa Shumba Mjini, akiwa katika ziara ya kikazi tarehe 20 Disemba 2017, akitembelea Bandari Bubu iliyopo Shumba Mjini, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, ambayo ni maarufu kwa shughuli za Uvuvi na Biashara.  

Mkuu wa Diko “Bandari Bubu” ya Shumba mjini Bwana Hussein Rashid Omar, akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari M. Sururu wakati alipofanya ziara ya kikazi Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe 20 Disemba, 2017, baadhi ya Majahazi (hayapo pichani) yanayofanya safari zake kupitia Bandari bubu hiyo. Huku wananchi waliowazunguka wakisisitiza kuwa wao wanuafata Sheria na Taratibu zote za Nchi wanapotoka ama kuingia nchini ikiwemo matumizi ya Pasipoti na kuiomba Idara ya Uhamiaji kusukuma mbele juhudi za Serikali kurasimisha Bandari hiyo 
 Sheha wa Shehia ya Kiuyu Mbuyuni, Bw. Ali Hamad Sharifu (wa pili kulia) akimueleza Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (kushoto kwake), jinsi wanavyoshirikiana na watendaji wa Idara ya Uhamiaji kwa kutoa taarifa zinazosaidia kuwadhibiti baadhi ya Watu wasio waaminifu wanaojaribu kuingiza wageni bila ya kufuata Sheria na Taratibu za Idara ya Uhamiaji Nchini. Yalielezwa hayo wakati Kamishna akiendelea na ziara ya kikazi, Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe 20 – 21 Disemba, 2017. 

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi ya bandari Bubu za Kiuyu na Mbuyuni, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati alipofanya ziara ya kikazi maeneo mbali mbali, Mkoani humo tarehe 20 – 21 Disemba, 2017. Wilaya ya Micheweni ina Bandari Bubu zaidi ya 80 Zinazotumiwa kuvuka mpaka wa majini kuingia Visiwa vya jirani pamoja na Shimoni, Mombasa, Kenya ambapo wakaazi wa maeneo hayo wana muingiliano mkubwa katika shughuli za kiuchumi na kijamii. 

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUAHIRISHWA KWA FAINALI ZA MISS TANZANIA 2017

$
0
0
Kampuni ya Lino International Agency Limited, waandaji wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania tunapenda kuwajulisha wapenzi, mashabiki na wadau wa tasnia ya urembo kwamba hakutakuwa na Fainali za Taifa za shindano la Miss Tanzania kwa mwaka 2017.
Sababu kubwa za kuahirishwa kwa Fainali hizi ni ukosefu wa Wadhamini ambao kwa njia moja au nyingine huwezesha kufanyika kwa mashindano hayo kwa kulipa gharama mbalimbali ikiwemo zawadi za washiriki n.k.
Aidha kuchelewa kupata kibali cha kuanza mchakato wa Miss Tanzania 2017 pia kumechangia kukosa Wadhamini kutokana na muda kuwa mfupi. Kibali cha kuendesha mashindano ya Miss Tanzania 2017 kimetolewa na Basata mwezi Septemba 2017.
Washindi wa Mikoa na Kanda ambao tayari wameshinda katika sehemu mbalimbali ambao wamefanya mashindano yao kwa mwaka 2017 watashiriki Fainali za Taifa kwa mwaka ujao wa 2018 katika tarehe na mwezi ambao tutawajulisha hapo baadae.
Baadhi ya Mikoa na Kanda mbalimbali ambao hawakuweza kufanya mashindano yao kwa mwaka 2017 kutokana na changamoto za udhamini, tunawapa muda wa kujipanga upya hadi mwezi Mei 2018 wawe wamefanya mashindano yao ili kutoa nafasi kwa Fainali za Taifa kufanyika.
Aidha tunapenda kuchukua fursa hii kuwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kudhamini mashindano ya Miss Tanzania 2018  ili kutoa fursa kwa wasichana washiriki ambao ndio walengwa wa mashindano haya.
Kamati ya Miss Tanzania inawataka Mawakala wote wa Miss Tanzania kufuata Kanuni, Sheria na Taratibu za Mashindano ikiwa ni pamoja na kusajiliwa na kulipa ada husika Baraza la Sanaa la Taifa, kuandaa shindano lenye hadhi na  kutoa zawadi kwa wakati.
Mawakala pia wanatakiwa kuwa na ofisi na mawasiliano yanayoeleweka.
Wakala ambaye hatotimiza masharti hayo, shindano lake halitotambuliwa na hivyo kuwanyima fursa washiriki wa mashindano haya.

Uongozi wa Kampuni ya Lino International Agency Limited tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa ushirikiano wao ambao wamekuwa wakitupatia kila mara tunapohitaji kufanya hivyo.

HIDAN .O. RICCO.
AFISA HABARI.
0673 019112

WAFANYAKAZI WA ZANTEL WASHIRIKI KUFANYA USAFI NA KUKABIDHI VIFAA KWA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA, ZANZIBAR.

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel wakishiriki kufanya usafi katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, zoezi ambalo lilifanyika hivi karibuni mjini Zanzibar. Tofauti na kufanya usafi, Zantel ilikabidhi vifaa vya usafi ikiwemo mifagio, ndoo na mafyekeo vyenye jumla ya thamani ya Sh. 400,000/= kwa ajili ya kuimarisha mfumo wa usafi na kuzuia maambukizi kwa watu wanaofika hospitalini hapo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Dk. Msafiri Marijani (Mwenye fulana ya bluu kushoto) akitoa neno la Shukrani kwa Mkuu wa Zantel, Zanzibar Mohamed Mussa Baucha (kulia) na wafanyakazi wote wa Zantel mara baada ya wafanyakazi hao kufanya usafi na kukabidhi vifaa vya usafi vyenye jumala ya thamani ya Sh.400,000 hospitalini hapo hivi karibuni mjini Zanzibar.
Mkuu wa Zantel, Zanzibar Mohamed Mussa Baucha (kulia) akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Dk. Msafiri Marijani mara baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi katika eneo la hospitali hiyo iliyopo Zanzibar hivi karibuni. Zantel ilikabidhi vifaa vyenye jumala ya thamani ya Sh.400, 000 hospitalini hapo.

NAIBU WAZIRI SHONZA AFUNGA MICHEZO YA VYUO VIKUU TANZANIA (TUSA) MJINI DODOMA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza na washiriki wa Michizo ya Vyuo Vikuu (Hawapo Pichani) wakati akifunga fainali za Michezo hiyo iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dododma leo Tarehe 20/12/2017. Waliokaa kulia kwake wa kwanza ni Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde,Wa pili ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Idris Kikula na Mtangazaji wa Clouds Fm Ndg. Shafii Dauda.  
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akijiandaa kufunga kikapu wakati wakufunga Michezo ya Vyuo Vikuu kwenye Mchezo wa Fainali ya mpira wa kikapu kati ya timu ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Tanzania (OUT) na Chuo Kikuu cha Dododma (UDOM) iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dododma leo Tarehe 20/12/2017, wa Pili kushoto ni Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde. OUT waliibuka washindi wa mchezo wa kikapu kwa wanaume.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akimvisha medali golikipa wa timu ya mpira wa miguu ya Chuo Kikuu cha Zanzibar Ahmad Suleiman wakati wa kufunga fainali za Michezo ya Vyuo Vikuu iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dododma leo Tarehe 20/12/2017. Chuo Kikuu cha Zanzibar waliibuka washindi wa mpira wa  miguu kwa wanaume.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) wakati wa kufunga fainali za Michezo ya Vyuo Vikuu iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dododma leo Tarehe 20/12/2017. OUT waliibuka washindi wa mchezo wa kikapu kwa wanaume dhidi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

SELCOM YAUNGA MKONO BENKI YA EXIM TANZANIA KUBORESHA HUDUMA ZA KIFEDHA NCHINI.

$
0
0
 Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Tanzania, Selemani Ponda na Mkurugenzi wa Mikakati wa kampuni ya Selcom, Benjamin Mpamo wakizindua Cashpoint ATM ambayo itawawezesha watumiaji wamobile money, Visa na Master Card wa ndani ya nchi na wa kimataifa kutoa fedha kwa kutumia kadi au bila kutumia kadi.

KATIKA kuendelea kuboresha huduma za kifedha kwa watanzania, Benki ya Exim Tanzania kwa kushirikiana na Selcom imezindua rasmi Cashpoint ATM zinazowawezesha wateja wa Selcom, Exim benki watumiaji wa mobile money, Visa na Master Card wa ndani ya nchi na wa kimataifa kutoa fedha kwa kutumia kadi au bila kutumia kadi.

Huduma hii inawawezesha wateja wa Tigo Pesa, M-pesa, Airtel Money, Selcom Card, Halopesa na wateja wanaotumia huduma za kibenki kwa njia ya simu kutoa fedha kwa njia ya token. Mteja atatumia simu yake kutoa fedha na kisha kuingiza token namba atakazopkea kwenye ATM, namba ya simu na kiasi anachohitaji kutoa na kufanikiwa kutoa fedha bila kutumia kadi. Kwa wateja wa Visa Card na Master Card, wao wanaweza kutoa fedha lakini kwa kutumia kadi zao kupitia Cashpoint ATM yoyote kwa urahisi zaidi.
“Tukiwa kama benki ya nne inayoongoza Tanzania katika mali, tungependa kusisitiza kujitolea kwetu katika kutengeneza mazingira ambayo huduma za kibenki zinapatikana kwa urahisi.” Ushirikiano huu utaokoa watumiaji wengi kwa kuwa wanaweza kutumia ATM moja na inaruhusu matumizi bila kadi.

Ubunifu ni ahadi tunayowapa wateja wetu. Benki imepata mafanikio makubwa kwenye uvumbuzi wa teknolojia yenye kwango cha dunia na bidhaa zinazolenga wateja. Tunajivunia kuwa benki ya kwanza nchini Tanzania kuanzisha kadi za Mikopo, Hati fungani za kubadilisha biashara, na Taasisi ya mafunzo ndani ya benki iliyothibitishwa na ISO. Sisi pia tulitoa ufumbuzi wa vituo rununu vya kutolea fedha (ATM), Huduma ya maasaa 24 kila siku katika matawi kadhaa yenye kuweka hela na mpango wa kipekee wa fedha kwa wanawake nchini Tanzania. Benki ya Exim ni benki inayongezeka kwa haraka yenye ubunifu wa kidigitali ambayo ina bidhaa nyingi na huduma za kuvutia zaidi zilizozinduliwa mwaka 2017 kama kadi zaa benki za kusafiri, Kadi ya benki ya mshahara kabla ya kulipwa, Kadi ya benki ya dola za Kimarekani na huduma za benki kwenye simu.

Hapo awali kumekuwa na changamoto kubwa katika utoaji wa fedha, na kwa kupitia mfumo huu mpya wa Selcom Cashpoint ATM sasa wateja wataweza kuepuka kero na vikwazo mbalimbali walivyokuwa wakikutana navyo hapo kabla na kufanya miamala hiyo kwa haraka, urahisi na salama zaidi. Kwenye ushirikiano huu Selcom hutoa usimamizi wa vifaa wakati Benki ya Exim hutoa usimamizi wa fedha, leseni ya benki ya kuendesha ATM pamoja na MasterCard / Visa ili kuwezesha wateja kupata huduma za utoaji wa fedha kwa njia ya haraka, rahisi na salama.

Mkurugenzi wa mikakati, Benjamin Mpamo kutoka Selcom aliongezea kwa ksuema, “Dhamira kuu ya Selcom ni kuwarahisishia maisha watanzania kwa njia ya teknolojia na kuhakikisha huduma za kifedha zinapatikana kwa njia rahisi na haraka kwa watanzania wote. Katika kuhakikisha tunatimiza dhamira hiyo, Selcom kwa kushirikiana na Exim Bank tumewaletea huduma hii mpya ya Cashpoint ATM ili kuwawezesha watanzania kutoa fedha kiurahisi kabisa muda wowote inapohitajika”.

Huduma zingine zitakazopatikana kwenye Cashpoint ATM hivi karibu ni pamoja na kununua LUKU, kulipia bili ya maji (Dawasco), kununua muda wa maongezi, kuangalia salio na kupata taarifa fupi ya miamala ya kadi kwa wateja wa Visa Card na Master Card.

Lengo kuu la Cashpoint ATM ni kuwarahisishia wananchi huduma za kutoa fedha na kuwawezesha kutoa fedha muda wowote kwa haraka, salama na uhakika bila kuwa na wasiwasi wa kukosa huduma hiyo.

JUBILEE INSURANCE YATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WATANO WALIOSHINDA SHINDANO LA UCHORAJI

$
0
0
Wanafunzi watano wa shule za serikali  hapa nchini wameshinda shindano la uchoraji ambazo zinaeleza tukio halisi ambalo limetaribiwa na Jubilee Insuarance. Walioshinda wamepewa zawadi za bima za afya za jubilee insurance pamoja na kuahidiwa kushomeshwa elimu ya sekondari pindi watapofaulu.

Shindano  hilo liliendeshwa kwa mikoa saba ambapo wanafunzi watano wameibuka kidedea baada ya kuchora picha hizo.Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Bima Nyanda za juu kusini wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA), Elia Kajiba ameishukuru Jubilee Insurance kwa kuanzisha shindano hilo ambalo limeweza kuwapa maisha wanafunzi watano kwa kuwa na uhakika wa afya zao pamoja na kusomeshwa elimu ya sekondari watapofaulu darasa la saba.

Amesema kuwa waendelee kuandaa mashindano mengi ambayo yatasukuma wanafunzi kushiriki  kutokana na kuwa na uhakika wa zawadi.Nae Mwenyekiti wa bodi  wa Jubilee Life Corporation na Mwenyekiti wa Msaidizi wa The Jubilee Insuarance Company of Tanzania, Shabbir Abji amesema kuwa Jubilee Insuarance sasa imejikita katika kutoa huduma kwa jamii hasa kwa kaya maskini.

Mzazi wa Joseph Mwakyembe wa Mbozi mkoani Songwe, Joyce Mbuya amesema kuwa mtoto wake amemfanya kufika Dar es Salaam na kuwa na uhakika wa afya kupata bima ya afya ya Jubilee Insuarance. 
Amesema kuwa Jubilee Insuarance imekuwa ya kwanza kuwafikia wananchi wa kawaida kwa kutafuta vipaji vya wanafunzi.
Mwenyekiti wa bodi  wa Jubilee Life Corporation na Mwenyekiti wa Msaidizi wa The Jubilee Insuarance Company of Tanzania, Shabbir Abji akizungumza na wageni waalikwa kwenye utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda kwenye shindano la uchoraji wa michoro inayomuweka mtoto huru lililofanyaka hapa nchini.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Bima Nyanda za juu kusini wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA), Elia Kajiba akitoa shukrani kwa Jubilee Insurance kwa kurudisha fadhira kwa jamii pamoja na na kuwasisitiza wajikite hasa kwa kaya maskini.

 Mkuu wa Kitengo cha Fedha Jubilee Life Insuarence Corparition, Helena Mzena akitoa historia ya ya shindano lililoshirikisha shule za msingi mbalimbali hapa nchini kwenye shindano la uchoraji kwa wanafunzi wa darasa la Tatu wakati wa ugawaji wa zawadi kwa wanafunzi watano waliofanya vizuri. 

MKUU WA JESHI LA POLISI, IGP SIMON SIRRO AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI LINDI KWA AJILI YA KUONGEA NA ASKARI.

$
0
0
 IGP Simon Sirro  akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa  ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mh Shaibu Ndemanga baada ya kuwasili mkoani Lindi katika ziara ya siku moja ya kuongea na Askari.  Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati) akiwa na Askari wa Mkoa wa Lindi baada ya kumaliza kukagua  mazoezi ya ukakamavu na utayari yaliokuwa yameandaliwa na kikosi cha kupambana na uhalifu mkoani  humo.  Picha na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa tatu kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Lindi, kulia kwa IGP Sirro ni Kaimu Mkuu wa Mkoa  Mh Shaibu Ndamanga na kushoto kwake ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Renata Mzinga.  Picha na Jeshi la Polisi.

KONGAMANO LA KWANZA LA KIMATAIFA LA KISWAHILI LIMEFUNGULIWA ZANZIBAR

$
0
0

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohammed Shein  akikunjuwa Kitambaa kinachoonesha Picha ya Mtunzi mahiri wa Vitabu na aloeneza lugha ya kiswahili kwa njia hio Muhammed Said Abdulla (BWANA MSA)mara baada ya kuwasili ndani ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani kwa ajili ya uzinduzi wa Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kiswahili Kikwajuni mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohammed  Shein katikati akiwa katikapicha ya pamoja na Viongozi mbalimbali baada ya kuzindua Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kiswahili katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni Mjini Unguja.
 Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar Mohammed Seif Khatib akitoa hotuba yake katika Uzinduzi wa Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kiswahili katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni Mjini Unguja.
 Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni rasmi  katika Uzinduzi wa Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kiswahili katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohammed Shein akisisitiza jambo alipokuwa akitohotuba yake ya Uzinduzi wa Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kiswahili katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni Mjini Unguja
 Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika Uzinduzi wa Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kiswahili katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni Mjini Unguja

PICHA NA YUSSUF SIAMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

TAKUKURU TANGA YAWAFIKISHA MAHAKAMANI WAHASIBU WAWILI WA OFISI YA MKUU WA MKOA WA TANGA KWA MASHTAKA MATATU YA RUSHWA

$
0
0
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Tanga(Takukuru) imewafikisha mahakamani wahasibu wawili wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga Josiah Mwaipela na Julius Idana kwa mashtaka matatu ya rushwa. 

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya
uchepushaji,ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka kuhusiana na shilingi milioni 276,095,106.9 za mishahara ya watumishi ambaowalikoma utumishi wao wa umma kati ya Machi 3 ,2012 na Novemba 2013. 

Hayo yalisemwa na Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tanga, Christopher Mariba wakati akitoa taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo alisema washtakiwa hao walifikishwa mahakamani jana Desemba 18 mwaka huu. Alisema washtakiwa hao walifikishwa mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Tanga,Crisencia Kisongo na kusomewa mashtaka na waendesha mashitaka wa Takukuru Noel Gabba na Neema Kazoka. 

Alisema washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa ya uchepushaji,ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka kuhusiana na shilingi milioni 276,095,106.9 za mishahara ya watumishi ambao walikoma utumishi wao wa umma kati ya Machi 3 ,2012 na Novemba 2013. 


DK.MABODI ATOA NASAHA KWA VIONGOZI

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dk. Abdulla Juma Mabodi amewataka viongozi wa ngazi mbali mbali waliochaguliwa kwa ajili ya kuwatumikia wanachama  kujiandaa kisaikolojia kufanya kazi kwa weledi na ubunifu kwa lengo la kulinda hadhi na heshima ya chama hicho.

Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza katika mahojiano maalum, amesema njia pekee ya viongozi waliochaguliwa ndani ya chama kuanzia ngazi za mashina hadi taifa kulipa mema kwa wanachama wao ni kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo endeleo kwa taasisi hiyo na kwa mwanachama mmoja mmoja.

Amesema baada ya Chama cha Mapinduzi kusajili rasmi jeshi lake la kisiasa kupitia uchaguzi huru na wa haki uliozingatia vigezo vyote vya kidemokrasia na Kikatiba , kwa sasa kazi iliyobaki ni kuanza mapambano kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika chaguzi za serikali za mitaa mwaka 2019 pamoja na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

“Chama chetu kimepata viongozi wa ngazi mbali mbali ambao tumechaguliwa na wanachama wetu ili tuwatumikie kwa miaka mitano ijayo hivyo mimi nikiwa miongoni mwa waliochaguliwa nakuombeni tutumie uwezo na maarifa yetu kuleta mabadiliko ya kimaendeleo ndani ya chama.

Pia tutafakari kwa kina ni mambo gani ya msingi tunayotakiwa kuyafanyia kazi kabla ya 2020, ili tuyaweke katika mipango mikakati yetu kwa lengo la kuwahudumia wananchi wote.”, alisema Dk. Mabodi.

MIAKA MITANO YA WAKALA KATIKA UTEKELEZAJI WA SERIKALI MTANDAO NCHINI

$
0
0
Serikali Mtandao ni matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika taasisi za umma kwa lengo la kutoa huduma bora kwa haraka, zilizo za gharama nafuu, zinazofikiwa kwa urahisi, zinazopatikana wakati wote (24/7) na kwa wakati mwafaka. Huduma za Serikali Mtandao zimegawanyika katika maeneo makuu manne: kati ya Serikali na Watumishi wake (G2E), Serikali na Sekta ya Biashara (G2B), Serikali na Wananchi (G2C) na Kati ya Taasisi moja na Taasisi nyingine ya Serikali (G2G). 


2.0 Wakala ya Serikali Mtandao 

Wakala ya Serikali Mtandao ilianzishwa 2012 kwa Sheria ya Wakala za Serikali Na.30 ya Mwaka 1997 Sura ya 245 na Kanuni zake. Wakala hii ina jukumu na mamlaka ya kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Serikali Mtandao kwa Taasisi za umma. Lengo ni kuziwezesha Taasisi hizo kutumia TEHAMA katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuongeza ufanisi, uwajibikaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. 

3.0 Malengo ya Wakala ya Serikali Mtandao 


Malengo ya Wakala ya Serikali Mtandao ni pamoja na Kuboresha uwezo wa Taasisi za umma kutekeleza jitihada za Serikali Mtandao, kuwezesha upatikanaji wa huduma mtandao kwa umma, Kuboresha mifumo shirikishi ya TEHAMA, Kuimarisha uratibu, usimamizi na uzingatiaji wa viwango vya Serikali Mtandao katika utoaji wa huduma kwa umma, Kuboresha huduma za ushauri wa kitaalam na msaada wa kiufundi na Kushirikiana na Wadau wa Serikali Mtandao. 

4.0 Mafanikio ya Utekelezaji wa Serikali Mtandao yenye Umuhimu wa kipekee. 

Ndani ya miaka mitano, Serikali imeijengea uwezo Wakala ulioiwezesha kutekeleza jitihada za Serikali Mtandao kama ifuatavyo: 

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao, Dk. Jabir Kuwe, akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo alielezea  kuhusu miaka mitano tangu ulipoanzishwa na namna walivyoweza kuhakikisha taasisi za serikali kuingia katika serkali mtandao.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao, Dk. Jabir Kuwe, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu miaka mitano tangu ulipoanzishwa na namna walivyoweza kuhakikisha taasisi za serikali kuingia katika serkali mtandao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Benki ya TPB yachezesha droo ya pili ya Western Union

$
0
0
Benki ya TPB  Desemba 21, 2017 imechezesha droo ya pili ya Western Union na kupata washindi 7 kutoka matawi mbalimbali . Washindi 5 walipata simu za mkononi na 2 walipata kompyuta mpakato.

Majina hayo yalitajwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa benk hiyo Bw. Mshamma Mshamma na kusimamiwa na Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed.

Washindi waliojishindia simu za mkononi aina ya Samsung J5 ni Bi. Elizabeth Lugendo kutoka Dar es Salaam, Bw.Frank Tetea kutoka Korogwe Tanga, Bw, Jafari Msaki kutoka Arusha, Bi. Rose Maluka kutoka Dodoma na B. Anna Kasoga kutoka Ifakara -Morogoro.

Washindi wawili waliojishindia kompyuta mpakato ni Bw. Justine Muyanza kutoka Mwanza na Bw. Abdul Hurey kutoka Arusha.
 Moja ya mfanyakazi wa benki hiyo akichanganya kuponi  za  droo ya pili Western Union wakati wa kumtafuta mshindi wa droo hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana.
Meneja wa huduma ya Western Union kutoka Benki ya TPB. Editha Lunyungu kushoto akihakiki majina ya washindi kwenye kopyuta  mpakato wakati wa kumtafuta mshindi wa droo ya pili Western Union wakati wa kumtafuta mshindi wa droo hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana.
Kaimu ofisa Mtendaji Mkuu kutoka Benki ya TPB, Bw. Mshamma  Mshamma (kushoto) akisoma jina la mshindi katika droo ya pili ya Western union. kulia anae shuhudia ni  mwakilishi kutoka Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed.
 Picha ya pamoja 

LUKUVI AMALIZA MGOGORO WA ARDHI VINGUNGUTI

$
0
0
Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi ameumaliza mgogoro wa ardhi wa muda mrefu kati ya wakazi wa Mtaa wa Mtambani Vingunguti na mwekezaji wa kampuni ya PMM jijini Dar es salaam. 

Mwekezaji huyo wa Kampuni ya PMM inayojihusisha na uhifadhi wa mizigo alitaka kuchukua eneo la hekari 228 lenye nyumba 4,000 na wakazi 70,000 wa Mtaa wa Mtambani Vingunguti. Waziri Lukuvi amesema Serikali haitambui uwekezaji uliokuwa ufanyike na kwamba, mwekezaji hakufuata utaratibu uliyowekwa na Serikali, hivyo kusababisha mgogoro huo kuwa mkubwa. 

Kwa mujibu wa wananchi wa eneo hilo tangu mwaka 2012 mwekezaji huyo aliwazuia kufanya shughuli zozote za uendelezaji kwa kile alichodai ameshafanya tathmini na anaisubiri Wizara ya Ardhi ambayo inamchelewesha, jambo ambalo Waziri Lukuvi amekanusha. 

Mwekezaji huyo ametakiwa kurejesha nyaraka alizozichukua kwa wananchi hao kinyume na utaratibu na ametakiwa kuwalipa fidia wananchi kwakuwa aliwazuia wakazi hao kufanya shughuli zozote za uendelezaji kwa kile alichodai ameshafanya tathmini. Hata hivyo, hadi sasa hakuna kinachoendelea na malipo hayajafanyika. 

Waziri lukuvi aliwaambia wananchi hao kuwa kuanzia leo haya maeneo ni mali ya wananchi kama anataka kununua aanze upya kufuata utaratibu uliowekwa, na haiwezekani mtu anakuja kuwanunua watu 70,000 kienyeji. 
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na Wananchi wa Vingunguti wakati alipoamua kusitisha zoezi la uuzwaji wa nyumba za Buguruni mpaka Vingunguti kwa Muwekezaji wa kampuni ya PMM ambaye amekuwa na mchakato wa kununua nyumba hizo kinyume cha utaratibu wa Serikali katika kufanya ununuzi huo na Tathmini
Mbunge wa Segerea Bonnah Kaluwa akizungumza na Wananchi wa Vingunguti wakati wa kusikiliza Kero za Wananchi juu ya mradi wa PMM 
Mkuu wa Wilaya ya  Ilala Sophia Mjema akizungumza wakati wa Mkutano wa Waziri Lukuvi na Wananchi wa Vingunguti juu ya mradi wa PMM
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi Akipata
Maelezo ya mradi wa ununuzi wa nyumba za Vingunguti

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtambani juu ya Mradi wa PMM Ulivyowazungusha wananchi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, akishangiliwa na Wananchi wa Vingunguti mara kutangaza kuwa mradi wa PMM Autambuliwa na Serikali
Wananchi waliohudhuria Mkutano wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  juu ya mradi wa PMM.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI KALEMANI AAGIZA WOTE WALIOLIPIA UMEME 2017 WAUNGANISHIWE KABLA YA MWISHO WA MWAKA

$
0
0
Na Veronica Simba .

Serikali imeliagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuhakikisha wateja wote walioomba na kulipia huduma hiyo mwaka 2017 wanaunganishiwa kabla ya Desemba 30 mwaka huu.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alitoa agizo hilo kwa nyakati tofauti hivi karibuni, akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme mkoani Singida na Dodoma.“Agizo hili ni kwa nchi nzima. Hakikisheni wateja waliowasilisha maombi yao na kulipia ndani ya mwaka huu wa 2017 wawe wameunganishiwa umeme siyo zaidi ya Desemba 30 mwaka huu.”.

Aidha, Dkt Kalemani aliwaagiza watendaji wa shirika hilo kutoa elimu kwa umma, hasa wananchi walioko vijijini kuhusu umuhimu wa kutumia umeme ili kuwahamasisha kuunganisha nishati hiyo katika makazi yao.

Akifafanua, Waziri alisema kuwa takwimu zinaonesha kuwa baadhi ya wananchi hawajaunganisha umeme katika makazi yao japokuwa tayari Serikali imekwishawafikishia nishati hiyo katika maeneo yao.“Inawezekana baadhi ya wananchi hawajatambua umuhimu wa kutumia umeme, hivyo ni vema wapatiwe elimu husika. Tuwatembelee mahali waliko, hususan vijijini na tuwapatie elimu hiyo,” alisisitiza.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ibaga, Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, wakati wa ziara yake hivi karibuni kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
 Mbunge wa Iramba Mashariki, Allan Kiula akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani jimboni kwake hivi karibuni, kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
 Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (kushoto), akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, jimboni kwake hivi karibuni kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
 Afisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Innocent Lupenza, akiandika majina ya baadhi ya wazee waliopatiwa zawadi ya kifaa kijulikanacho kama Umeme Tayari (UMETA) na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), alipokuwa katika ziara ya kazi Mikoa ya Singida na Dodoma hivi karibuni.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images