Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109935 articles
Browse latest View live

DK. KIGWANGALLA ATEUA WAJUMBE WENGINE WA KAMATI YA KUANDAA MWEZI WA URITHI WA TANZANIA

$
0
0


Na Hamza Temba, Arusha
..............................................................
Wadau wa Utalii Jijini Arusha wamempongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kwa kukubali kuyafanyia kazi mapendekezo yao ya kuwaingiza wajasiriamali wadogo katika utoaji wa huduma za kusafirisha watalii nchini.


Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO), Wilbard Chambulo wakati akichangia mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii zilizowasilishwa kwao na Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini humo.


Chambulo alisema kwa muda mrefu sasa kanuni zinazotumika zinamtaka mfanyabiashara ya usafirishaji watalii awe na magari matatu kwa kiwango cha chini ikiwa ni pamoja na kulipia ada ya leseni ya Dola za Kimarekani 2,000 sawa na wafanyabiashara wengine matajiri jambo ambalo limekuwa likiwabagua wafanyabiashara wadogo.


“Tunakupongeza sana Mhe. Waziri kwa kutupa angalao hilo moja, tuliomba mwenye kagari kamoja nae aruhusiwe na apewe leseni walau ya dola 200 ili afanye biashara kidogo kidogo mwishowe atanunua gari tano na kuendelea, tunataka sisi Watanzania wote tufaidike na rasilimali zetu,” alisema Chambulo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na wadau wa utalii Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya ubora wa nyota. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa utalii Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya ubora wa nyota. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deogratias Mdamu (kushoto).
Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Idara ya Habari (MAELEZO) Yapokea Msaada wa Vifaa Kutoka Ubalozi wa China

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea zawadi ya Krismasi kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini Mhe. WANG Ke  mara baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa kwa ajili ya Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Msaada huo unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za ofisi.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akipokea zawadi ya Krismasi kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini Mhe. WANG Ke  mara baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa kwa ajili ya Idara yake leo Jijini Dar es Salaam. Msaada huo unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za ofisi. 
Waziri Mshauri wa Ubalozi wa China hapa nchini Gou Haodong  akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kutoka kushoto) walipokutana katika hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa vifaa kwa ajili ya Idara ya Habari (MAELEZO) iliyofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa China Jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini Mhe. WANG Ke. Msaada huo unajumuisha Kompyuta mpakato na samani za ofisi. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO) 

SHAKA ATEMA NYONGO,ASEMA YUPO TAYARI KUWAJIBA IWAPO KUNA UFISADI

$
0
0

Na Said Mwishehe,blogu ya jamii

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM)Shaka Hamdu Shaka amesema yupo tayari kuwajibika iwaoi itabainika anefanya ufisaidi wa aina yoyote katika utendaji wake kwenye nafasi aliyonayo sasa.

Shaka ametoa kauli hiyo kwenye ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni jijini Dar es Salaam leo kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Umoja huo Taifa Kheir James Denis ambaye amepokelewa rasmi na kutambulishwa kwa vijana wa mkoa huo.

Amesema katika nafasi hiyo amekuwa akifanya jitihada mbalimbali za kutetea mali za umoja huo na kwa bahati mbaya hatua hiyo imemfanya apigwe vita na kumkwamisha.Amesema chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa,Dk.John Magufuli ataendelea kusimama imara kusimamia rasilimali za umoja huo na hatarudi nyuma.

Amesema amekuwa katika mazingira magumu yanayotokana na kupigwa na ikafika mahali baadhi ya watu wakaanza kumzushia mambo ambayo hayana ukweli wowote.Ametumia nafasi kueleza wazi yupo tayari kuchunguzwa na kuwa tayari kuwajibika iwapo itabainika ameshiriki kufuja mali za umoja huo."Nimeshambuliwa na kupigwa vita kwasababu tu ya kuwa na msimamo thabiti wa kusimamia mali za jumuiya na maadili.

" Naomba niseme leo hii ni siku ya historia kwangu kwani nimetoa la moyoni ambalo nimekuwa nalo muda mrefu,nimeshambuliwa na kupigwa vita bila sababu.Niseme nipo tayari kuwajibika kama nitabainika kufanya ufisadi kwa kutumia bafasi yangu,"amesema Shaka.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KESHO KUFANYA MKUTANO NA WADAU WA PAMBA SHINYANGA

$
0
0
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (pichani) amesema mkutano huo utakaokutanisha pamoja wadau wa pamba utafanyika katika shule ya sekondari Savannah iliyopo katika eneo la Ibadakuli manispaa ya Shinyanga. 

“Mkutano huu utahudhuriwa na watu zaidi ya 1,000 wakiwemo mawaziri,wabunge, watendaji wakuu kutoka ngazi ya wizara,mikoa,wilaya,taasisi ,mashirika ya umma na wadau mbalimbali”,alieleza Telack. 

“Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa wananchi wanalima zao la pamba kwa wingi na kulifanya zao hilo lililokuwa limedorora sasa linakuwa na tija na kuwanufaisha wakulima hivyo mkutano huu utakuwa na majibu kwa wakulima na wadau wote”,aliongeza Telack. 

Mkuu huyo wa mkoa alisema waziri mkuu pia atatembelea kiwanda cha Nyuzi kilichopo katika kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga. 
Aidha alisema pia kutakuwa na maonesho ya biashara na shughuli mbalimbali zinazofanyika mkoani Shinyanga. 

Telack alisema katika msimu huu wa kilimo cha pamba zaidi ya wakazi 80,000 wanatarajiwa kulima zao la pamba na wamepanga kulima katika ekari 67,579.9. 
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa kesho Ijumaa Disemba 22,2017 atafanya mkutano na wadau wa pamba kutoka mikoa 16 nchini. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza na waandishi wa habari leo wakati akitoa taarifa kuhusu ujio wa Waziri mkuu Kassim Majaliwa mkoani Shinyanga .
Waaandishi wa habari wakichukua matukio wakati wa kikao hicho. 
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

SERIKALI YASISITIZA ELIMU YA FEDHA ITOLEWE MASHULENI

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesisitiza kuanzishwa kwa mtaala wa elimu ya fedha mashuleni ili kuwajengea uwezo vijana wa kujua na kutambua kujua matumizi sahihi ya fedha. Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Desemba 21, 2017) wakati akizindua Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

 Akizindua mpango huo unaotarajiwa kutekelezwa kuanzia mwaka 2018 hadi 2022, Waziri Mkuu alisema uwepo wa miundombinu muhimu iliyojengwa na inayojengwa na Serikali; na sekta binafsi katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya vijijini; na ongezeko la watumiaji wa mitandao ya simu na huduma za mawasiliano ni kati ya fursa nzuri iliyotajwa kwenye mpango huo. 

“Kati ya fursa nzuri iliyotajwa kwenye mpango huo ni uwepo wa uchumi imara na unaokua kwa kasi. Tukijenga vizuri juu ya misingi hii tunaweza kupiga haraka hatua za maendeleo katika sekta ya fedha na uchumi kwa ujumla wake,” alisema. 

Alisema ameupitia mpango huo na kubaini kuwa umeainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi hii katika harakati zake za kuongeza matumizi ya huduma za kifedha. Hata hivyo, Waziri Mkuu alikiri kuwa mpango huo umeainisha fursa ambazo zinaweza kutumika ili kukabiliana na changamoto hizo na hatimaye kuongeza matumizi ya huduma za kifedha. 

“Changamoto zilizoainishwa ni pamoja na kuimarisha utawala wa matumizi ya fedha taslimu kwa ajili ya malipo badala ya matumizi ya mifumo ya kielektroniki ya malipo; kukosekana kwa utambulisho wa kipekee (unique identification) kwa Watanzania walio wengi; uhalifu kwa njia za mtandao (cyber-crime); kukosekana kwa mifumo madhubuti ya taarifa za kutosha za watumiaji wa huduma za fedha na dhamana zao; na uelewa mdogo wa masuala ya kifedha,” alisema. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amenyanyua kitabu cha mpango kazi wakati wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, mwingine kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James na Gavana Mpya wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof Florens Luoga. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kitambu cha mpango kazi, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James wakati wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Gavana Mpya wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof Florens Luoga. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kitabu cha mpango kazi, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Benno Ndulu wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Gavana Mpya wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof Florens Luoga. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Benno Ndulu wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.  Picha zote na KAJUNASON/MMG. 

DK. KIGWANGALLA ATEUA WAJUMBE WENGINE WA KAMATI YA KUANDAA MWEZI WA URITHI WA TANZANIA

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI KUIFANYA DODOMA KUWA YA KIJANI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa kampeni ya kupanda na ustawishaji miti isiishie Dodoma mjini tu bali ienee katika Wilaya zote za mkoa wa huo na hatimaye nchi nzima.

Makamu wa Rais aliyasema hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani,alisema upandaji miti si kwa ajili ya kuhifadhi mazingira tu bali ni fursa ya kiuchumi, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi  ambapo alitolea mfano mti mmoja uliokomaa unaweza kunyonya hadi kiasi cha kilo 150 za gesi ya hewa ya ukaa kwa mwaka,husaidia kupunguza joto, kusaidia kuboresha afya zetu za mwili na akili kama tafiti zinavyoonyesha .

“Ni dhahiri, kampeni hii ya kuifanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani ni kuunga mkono uamuzi wa Rais wetu, Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamishia Makamo Makuu ya Nchi kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma kwa vitendo.” Alisema Makamu wa Rais.Makamu wa Rais amewataka Viongozi na Wana Dodoma kuipokea kampeni hii kwa mikono miwili na kutoa kila aina ya ushirikiano ili kufikia lengo zuri lililokusudiwa.

Makamu wa Rais ambaye alihamia rasmi mjini Dodoma siku ya ijumaa tarehe 15 Desemba, 2017 alitoa pongezi kwa Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Ofisi yake kwa kuja na wazo zuri .

Makamu wa Rais alisisitiza kuwa hategemei kuona zoezi la upandaji miti lianze na kuisha leo, na badala yake liwe la kudumu, pia alizitaka manisapaa zitunge sheria ndogo zitakazoelekeza shule, chuo, taasisi na familia kuanzisha bustani ndogo  za miti zitakayomudu mazingira husika,Makamu wa Rais aliendelea kusema kuwa ni vyema kupunguza ukataji wa miti kiholela ambapo alizitaka sheria, kanuni na taratibu zizingatiwe kabla ya kukata miti na kusema tupande miti kabla ya kukata mti.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiandaa mti wake kabla ya kuupanda mara baada ya kuzindua  kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la Makutupora, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipanda mti  mara baada ya kuzinduzi  kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la Makutupora, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akitoa maelezo ya kampeni ya kupanda miti  wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la Makutupora, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAGAZETI YA IJUMAALEO DECEMBER 22,2017


KUMBUKUMBU

Wafanyakazi wa Mgen Tanzania wauaga mwaka kwa hafla fupi na mawakala wake

$
0
0
Mwenyekiti wa Makampuni ya Lawrance Sikutwa & Associates (LSA) Bwana Lawrance Sikutwa akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni Bima ya Mgen Tanzania Insurance Limited katika hafla ya kufunga mwaka iliyowashirikisha wateja na baadhi ya mawakala wa kampuni hiyo hapa nchini ili kufurahi pamoja, Hafla hiyo imefanyika jana katika makao makuu ya kampuni hiyo Masaki jijini Dar es salaam .
Mwenyekiti wa Makampuni ya Lawrance Sikutwa & Associates (LSA) Bwana Lawrance Sikutwa akifurahia jambo mara baada ya kumkabidhi zawadi Hope Kaiza liyefanya kazi kwenye kampuni ya Mgen Tanzania kwa miaka 10 kwa mafanikio makubwa kushoto ni Mkurugenzi wa Mgen Tanzania Insurance Limited Bw. David Tuhoye .
Mwenyekiti wa Makampuni ya Lawrance Sikutwa & Associates (LSA) Bwana Lawrance Sikutwa akifurahia jambo mara baada ya kuwakabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Lumumba Insurance Brokers Limited Bw. Jamal Lardhi kushoto na Tiraib Maghembe Mkuu wa Idara ya Fedha Lumumba Insurance Brokers Limited katikati anayewapongeza ni Mkurugenzi wa Mgen Tanzania Insurance Limited Bw. David Tuhoye
Mwenyekiti wa Makampuni ya Lawrance Sikutwa & Associates (LSA) Bwana Lawrance Sikutwa akimkabidhi zawadi Bw. Sudi Simba Afisa Mtendaji Mkuu wa Zurich Group Ltd kwa ushirikiano wa kampuni hiyo kwa Mgen Tanzania Insurance katikati ni Mkurugenzi wa Mgen Tanzania Insurance Limited Bw. David Tuhoye

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MIKOA YA KUSINI KUPATA UMEME WA UHAKIKA

$
0
0

Na Yasini Silayo

Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limewahakikishia Umeme wa uhakika wakazi wa Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kutokana na uboreshwaji mkubwa wa huduma za Uzalishaji, Usafirishaji na Usambazaji Umeme zinazoendelea katika Mikoa hiyo.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi alipofanya Ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara akiambatana na wajumbe wengine wa bodi pamoja na viongozi waandamizi wa TANESCO Makao Makuu na Kanda ya Kusini.

Akiongea na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali Mkoani Lindi, Dkt. Kyaruzi amesema kuwa tayari TANESCO imefanya matengenezo makubwa katika mitambo ya kuzalisha umeme wa Gesi wa Megawati 18. Mtambo huo unahudumia Mikoa ya Mtwara pamoja na Baadhi ya maeneo ya Lindi kupitia laini mpya ya 132kV Mtwara-Mahumbika iliyokamilika tangu mwezi Julai mwaka huu ikijengwa na mafundi wazawa kutoka ndani ya TANESCO kupitia kampuni Tanzu yake iitwayo ETDCO.

"Mbali na hali ya umeme kuimarika hivi sasa kutokana na matengenezo ya mitambo ya Mtwara, Shirika hivi sasa linaendelea na maandalizi ya ujenzi wa miradi miwili mikubwa ya Uzalishaji Umeme wa jumla ya megawati 540 Katika Mikoa hii pamoja na kuunga mikoa ya Kusini katika Umeme wa Grid ya Taifa kwa Laini kubwa ya Msongo wa Kilovolt 400. 
Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Dkt. Alexender Kyaruzi (katikati) na wajjumbe wa bodi ya Shirika hilo, wakipatiwa maelezo walipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mahumbika mkoani Lindi
Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Dkt. Alexender Kyaruzi akiongea na wananchi wa Mtama Mkoani Lindi wakati wa ziara ya Bodi ya wakurugenzi wa TANESCO Katika mikoa ya Lindi na Mtwara


WILAYA YA KISHAPU YAZINDUA MRADI WA MTOTO MWEREVU UNAOTEKELEZWA NA SERIKALI KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA IMA WORLDHEALTH

$
0
0

Na Robert Hokororo, Kishapu DC

Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imezindua mradi wa Mradi wa Mtoto Mwerevu unaotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la IMA WORLDHEALTH, Pamoja na Chuo cha Cornel.

Lengo kuu la mradi huo ni kupunguza udumavu kwa asilimia 7 kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ambao unatekelezwa katika halmashauri 36 zilizo ndani ya mikoa mitano ya Shinyanga, Mwanza, Geita, Kagera na Kigoma.Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Boniphace Butondo amefungua kikao cha uhamasishaji mbinu za kupambana na udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano kwa madiwani na watendaji kata.

Imeelezwa mradi huo utasaidia kuimarisha mikoa na halmashauri zake kwa kuzijengea uwezo wa watendaji wake wa sekta zote zinazohusika na masuala ya lishe kuhusu kupanga na kufanya ufuatiliaji wa shughuli hizo katika jamii.Pia utachangia fedha za utekelezaji kwenye bajeti na mipango ya mkoa na halmashauri 36 kwa njia ya ruzuku ya uwajibikaji na kuhakikisha fedha zitakazotolewa hazitaifanya mamlaka hizo za Serikali zisitenge fedha kwa ajili ya masuala ya lishe.

Hivyo badala yake utahamasisha ongezeko la bajeti ya shughuli za lishe kupanda katika kipindi chote cha mradi huo unapoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza wakati wa kikao cha uhamasishaji mbinu za kupambana na udunavu kwa watoto chini ya miaka mitano kwa madiwani na watendaji kata. Wengine pichani ni Makamu Mwenyekiti halmashauri hiyo, Mhe. Edward Shigela, Mwenyekiti wa halmashauri, Mhe. Boniphace Butondo na Afisa Lishe Wilaya, Avelina France.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. Boniphace Butondo akifungua kikao hicho.
Washiriki wa kikao hicho wakiwemo madiwani na watendaji kata wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.

TANZANIA NA UGANDA WAUNDA TIMU YA WATAALAMU KUDHIBITI MAGONJWA YA MIFUGO

$
0
0
Na John Mapepele 

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasilano, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (0784 441180).

Tanzania na Uganda leo wamekubaliana kuunda mara moja timu ya pamoja ya wataalamu wa mifugo itakayokuwa ikifuatilia hali ya mifugo ili kudhibiti milipuko ya magonjwa hatari ya Mifugo.

Akizungumza leo mjini Bukoba kwenye mkutano wa wataalam wa mifugo wa Tanzania na Uganda ulioandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi nchini, Balozi wa Uganda nchini bwana Richard Tumusiime Kabonero amesema ushirikiano wa karibu baina ya Tanzania na Uganda kwenye sekta ya mifugo siyo kitu cha hiari bali ni jambo la laziima ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko ambayo ni hatari kwa mifugo ya pande zote mbili.

Balozi Kabonero amesema njia bora ya kudhibiti magonjwa ya wanyama ni kuwa na timu ya pamoja ya wataalam watakaokuwa wakifuatilia hali ya mifugo na kufanya tathmini kila wakati badala ya utaratibu wa sasa wa kila nchi kushughulikia peke yake.“Uganda kama ndugu wa karibu wa Tanzania tuna kila sababu ya kushirikiana ili kuboresha sekta hii” alisisitiza balozi Kabonero

Akizungumzia kwa upande wa Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo anayeshughulikia sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo amesema ushirikiano huo utasaidia kuboresha huduma za mifugo baina ya nchi mbili kwa kuzingatia kuwa taaluma ya udaktari wa mifugo imehuishwa na inadhibitiwa na bodi za taaluma hiyo kidunia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo(aliyeshika fimbo) akipima kina cha KIsima kilitengenezwa kienyeji kwa ajili ya kunyweshea mifugo katika eneo la Kafunjo Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera leo. Waliomzunguka ni wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifana Halmashauri ya Missenyi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo (aliyenyanyua mikono) akiongea na wafugaji wa nchini Uganda leo baada ya kufanya ziara ya kikazi katika eneo la Omwaarogwamabaare. Kushoto ni Mheshimiwa Balozi wa Uganda nchini Tanzania, bwana Richard Tumusiime Kabonero kulia (anayecheka) ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Martin Ruheta. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo (aliyenyanyua mkono)akimweleza jambo Balozi wa Uganda nchini Tanzania Mhe.Richard Tumusiime Kabonero (kulia) walipokuwa katika ziara ya kikazi leo kwenye Mto Kagera katika kijiji cha Kakunyu. Wengine kushoto kwa Katibu Mkuu ni Dkt. Martin Ruheta Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kulia kwa Balozi ni Suleiman Ahmed saleh, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

JUMLA YA KAYA 180,000 KUFIKIWA NA MRADI WA LEAD FOUNDATION

$
0
0
DODOMA: Shirika la LEAD Foundation linalojihusisha na utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu utunzaji wa mazingira limezindua mradi wa Kisiki Hai Mkoa wa Dodoma wenye lengo la kukomboa ardhi iliyochakaa ya mashamba na malisho ili kupambana na baa la njaa na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Akizungumza na wadau mbalimbali wa mazingira wakati wa ufunguzi wa mradi huo Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la LEAD Foundation, Mhandisi Njamasi Chiwanga amesema kuwa lengo la Mradi wa Kisiki Hai ni kuhakikisha wanafikia jumla ya kaya laki moja na themanini (180,000) ambazo zipo katika hali mbaya ya mazingira ziweze kutunza hekta 180,000 kwa kustawisha miti milioni 14 kwa njia ya Kisiki Hai (FMNR - Farmer Managed Natural Regeneration) ifikapo mwaka 2020.

Njamasi amesema kuwa mikakati waliyonayo katika mradi huo ni pamoja na kujenga mshikamano wa wadau wote wa mazingira hususan viongozi wa wilaya, wakuu wa idara na taasisi mbalimbali, madiwani, watendaji wa kata pamoja na viongozi wa dini ili kuweza kushirikiana katika kufanikisha kukomboa mazigira. Kwa kuanzia mradi unatarajia kunufaisha tarafa mbili zilizo athiriwa zaidi na uharibifu wa mazingira katika kila wilaya ili kufikia nusu ya kaya zote za Mkoa wa Dodoma.

Mgeni Rasmi katika ufunguzi huo Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh. Deo Ndejembi amesema anaunga mkono mradi huo na atahakikisha unafanikiwa na kuahidi kutoa ushirikiano kwa mambo mbalimbali watakayo hitaji katika kufanikisha mradi huo.Kwa upande wao baadhi ya wadau waliofika katika ufunguzi wa mradi huo wamesema kuwa mpango wa Kisiki Hai ni mzuri na wana hakika iwapo wananchi wataupokea vizuri baada ya muda mfupi changamoto ya uharibifu wa mazingira katika Wilaya ya Kongwa itakuwa ni historia.

Kisiki Hai ni mradi wa miaka mitatu na unatarajiwa kufikia Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma na kwa sasa umenza katika Wilaya ya Kongwa ambapo umeanza na tarafa ya Kongwa na Mlali za wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deo Ndejembi akifungua rasmi mradi wa LEAD Foundation.

 Mkurugenzi wa Programu - LEAD Foundation Mhandisi Njamasi Chiwanga akiwasilisha mpango wa Programu
Wadau walio hudhuria warsha ya mazingira ya Kisiki Hai


BODI YA WAKURUGENZI, MENEJIMENTI NA WAFANYAKAZI WOTE WA DAWASA WANAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA KRISMAS NA MWAKA MPYA 2018

MAMA SALMA KIKWETE KUZINDUA KAMPENI YA KAMBI YA WANAFUNZI WA MASOMO YA SAYANSI MKOANI IRINGA

$
0
0
Wanafunzi wa shule za sekondari manispaa ya iringa kunufaika na elimu ya masomo ya sayansi kutokana na kuandaliwa kambi maalumu kwa ajili ya kuwafindisha kutoka kwa walimu waliobobea katika masomo hayo kwa wanafunzi wa watakao kuwa tayari kupata elimu hiyo.

Ofisi ya mbunge wa viti maalum Ritta Kabati imeandaa mpango wa kuwaongezea elimua wanafunzi wa shule za sekondari manispaa ya Iringa kwa kuanzisha kambi ya masomo ya sanyasi itakayo kuwa inafanyika bure kwa wanafunzi wa watakao kuwa tayari kupata elimu hiyo.

Akizungumza na Nuru fm Dicksoni Kawovela ambaye ni mratibu wa miradi ya jamii kutoka ofisi ya mbunge RITTA KABATI amesema kuwa wameamua kuja na mpango huo kwa lengo la kuinua elimu ya sayansi kwa wanafunzzi wa shule za sekondari hapa manispaa.

Aidha Kawovela amesema kuwa mafunzo hayo yatakuwa na manufaa kwa walimu na wanafunzi watakaokuwa wanahudhuria masomo haya ambayo yatakuwa yanatolewa bure.Kawovela amewaka wazazi wa wanafunzi kuwaruhusu watoto wao kwenda kwenye makambi hayo ili waongezewe uwezo katika masomo ya sayansi.

Hata hiyo Kawovela alisema kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa mama Salma Kikwete ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na Rais katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MKUU WA WILAYA YA KONGWA AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI WARATIBU ELIMU KATA WAWILI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi Leo amefanya Kikao na Waratibu Elimu  Kata 22 wa Wilaya ya Kongwa na idara nzima ya Elimu. Lengo la Kikao hicho ni kufanya tathimini ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wapya wa darasa la kwanza na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018.

Katika mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na upungufu wa madarasa,madawati na changamoto nyingine mbalimbali.Pia  kuweka mikakati ya kuondoa changamoto hizo ifikapo muda wa usajili.

Katika kikao hicho Mh. Ndejembi alimuagiza Mkurugenzi kuwasimamisha  kazi waratibu wawili wa Kata ya Njoge na Lenjulu ili kupisha uchunguzi juu ya tuhuma zao mbalimbali zinazopelekea kutowajibika vema katika vituo vyao vya kazi.

Mkuu wa Wilaya aliwaasa waratibu hao kuachana na kufanya kazi kwa mazoea (business as usual),  na kuendana na Kasi ya Serikali ya awamu ya tano kwani Mh Rais amewawekea mazingira mazuri ya kazi ikiwemo posho kwa kila MEK Tsh 450,000/= kila mwezi pamoja usafiri. Hivyo wahakikishe  wanatoa huduma bora kwa wananchi.

DC Ndejembi  alieleza kuwa kwa mwaka ujao wa 2018 wanatarajia kusajili wanafunzi wapya wengi sana wa Shule za Msingi na Kidato cha Kwanza kwani Sera ya utoaji Elimu Bure imeamsha Morali zaidi  kwa Wazazi kupeleka watoto Shule.

 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizungumza kwenye Kikao na Waratibu Elimu  Kata 22 wa Wilaya ya Kongwa na idara nzima ya Elimu, Lengo la Kikao hicho ni kufanya tathimini ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wapya wa darasa la kwanza na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018.

USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOA WA MTWARA WASHIKA KASI

$
0
0
Mtendaji wa Mtaa wa Ufukoni – Mtwara akimthibitisha mmoja wa wakazi kwenye Mtaa wake kwa kumgongea mhuri wa Mtaa anakoishi kwenye fomu ya maombi ya Vitambulisho vya Taifa kabla mwananchi huyo hajaingia kwenye hatua ya mwisho ya kuchukuliwa alama za vidole, picha na saini ya Kielektroniki.
Baadhi ya wananchi katika Kata ya Magomeni mkoa wa Mtwara wakichambua fomu zao za Usajili kwa ajili ya kupigwa picha na kuchukuliwa alama za kibaiolojia.
Mkazi wa shule ya Msingi Lilungu mkoani Mtwara akipigwa picha wakati wa zoezi la kuwasajili wananchi kupata Vitambulisho vya Taifa likiendelea.
Mwananchi wa Kata ya Ufukoni akisubiri kupigwa picha wakati wa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa zoezi ambalo kwa sasa linaendekea katika shule ya Msingi ya Ufukoni mkoani Mtwara. Wananchi mkoani Mtwara wamekuwa miongoni mwa wananchi katika mikoa 15 ya Tanzania ambao wanashiriki kwenye zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa lilionza mapema mwezi Novemba mwaka huu. 

 Kwa Wilaya ya Mtwara kwa sasa zoezi hilo linaendelea katika Kata za Magomeni na Ufukoni huku Kata za Shangani, Rahaleo, Tandika, Chikongola, Majengo, Reli na Vigaeni zikiwa zimekamilisha zoezi hilo. Wilaya nyingine ambazo zoezi hilo linaendelea ni Wilaya ya Masasi, Nanyumbu, Nachingwea na Newala.

 Zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa mkoa wa Mtwara linategemewa kumalizika mwezi Februari 2018 kuruhusu kuanza kwa matumizi ya Vitambulisho hivyo huku nchi nzima zoezi hili likikusudiwa kumalizika mwezi Desemba 2018. Mikoa mingine inayoendelea na zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa ni Iringa, Mbeya, Njombe, Songwe, Singida, Manyara, Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara, Kilimanjaro, Arusha na Lindi.

DC SENYAMULE AFUNGUA SEMINA YA KUWAJENGEA UWEZO VIONGOZI WA SERIKALI, DINI NA WASIMAMIZI MPANGO WA PETS

$
0
0
Na Kajunason/MMG.

Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule amewataka wasimamizi wa mpango wa Ufuatiliaji wa Matumizi ya Umma (PETS) kuwa na uadilifu katika kufiatilia matumizi ya fedha za serikali. Hayo ameyazungumza leo wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo uliowakutanisha viongozi wa serikali, dini na wasimamizi wa mpango wa "Public Expenditure Tracking System" (PETS) uliofanyika Same kwa kuwezeshwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT). 

 Mhe. Senyamule alisema ni vyema watendaji hao wakafuata misingi imara itakayowezesha serikali kujua ni wapi wanamatumizi mabovu ya fedha katika halmashauli. Aliagiza halmashauri kushirikiana kwa karibu na watu hao kwani kazi wanayoifanya ni ya halmashauri, hasa ukaguzi na mipango. "Idara ya ukaguzi ina watumishi 3 tu wanaohitaji kukagua kila kitu, sio rahisi wakidhi kwa wakati; lazima tuwashirikishe wadau wa PETS ili taarifa zao ziwe ni moja ya misingi ya ufuatiliaji kwa halmashauri," alisema Mhe. Senyamule. Pamoja na yote Mhe. Senyamule aliomba CCT kuongeza idadi ya kata wanazofanyia kazi kutoka 11 hadi zote 34 zilizopo kwa sasa.
 Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule (wa nne toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali, dini na wasimamizi wa mpango wa "Public Expenditure Tracking System" (PETS) waliohudhuria semina iliyofanyika Same kwa kuwezeshwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT). 

Viewing all 109935 articles
Browse latest View live




Latest Images