Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AFANYA ZIARA JIMBO LA NZEGA VIJIJINI

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la Nzega,Dkt Hamisi Kigwangalla,ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii mapema leo mara baada ya kuwasili kwa ziara fupi ndani ya jimbo la Nzega.kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasuvi pamoja na Katibu wa CCM Wilaya Ndugu Shaibu Ngatiche.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo na Mbunge wa jimbo la Nzega,Dkt Kigwangalla,mapema leo walipokuwa wakishuhudia ngoma ya asili iliyokuwa ikitumbuiza nje ya Ofisi kuu ya chama  ya wilaya ya Nzega mara baada ya kuwasili kwa ziara fupi kufuatia mwaliko wa Mbunge wa jimbo hilo Dk Hamisi Kigwangalla.kushoto kwake ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasuvi
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasuvi akimkaribisha  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ndani ya Ofisi kuu ya chama  ya wilaya ya Nzega na kuitambulisha kamati kuu ya siasa ya Wilaya mapema leo kabla ya kwenda kwenye mkutano wa ndani wa jimbo hilo.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mbele ya Kamati kuu ya Siasa Wilaya ya Nzega,mkoani Tabora mapema leo,mara baada ya kupokea taarifa fupi za chama ndani ya Ofisi kuu ya chama  ya wilaya hiyo 
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nzega Ndugu Amos Kanuda na viongozi wengine wa chama wakielekea kuweka jiwa la msingi la ujenzi wa Ukumbi utakaotumika kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za kijamii,liliojengwa kando kando ya Ofisi kuu ya chama  ya wilaya
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria uwekaji rasmi wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ukumbi mkubwa na wa kisasa utakaotumika kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za kijamii,uliojengwa kando kando ya Ofisi kuu ya chama  ya wilaya hiyo,kulia kwake ni  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nzega Ndugu Amos Kanuda pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo Dkt Hamisi Kigwangalla (aliyevaa mawani katikati).
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nzega Ndugu Amos Kanuda pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo Dkt Hamisi Kigwangalla  wakipiga makofi mara baada ya kuwekwa jiwe la msingi la ujenzi wa ukumbi . 
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Mbunge wa Jimbo hilo Dkt Hamisi Kigwangalla,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nzega Ndugu Amos Kanuda pamoja na  Katibu wa CCM Wilaya Ndugu Shaibu Ngatiche wakikagua ujenzi wa ukumbi huo . PICHA NA MICHUZI JR -NZEGA
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mapema leo mbele ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Nzega mkoani Tabora.Ndugu Kinana amefanya ziara wilayani humo mapema leo kwa Mwaliko wa Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla,aidha katika ziara hiyo Ndugu kinana amewapongeza viongozi mbalimbali waliochaguliwa katika ngazi ya chama ya wilaya na pia kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa ukumbi mkubwa wa kisasa ambao utatumika kwa matumizi mbalimbali.PICHA NA MICHUZI JR -NZEGA
 Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM na Wananchi wakishangilia jambo walipokuwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mapema leo  wilayani Nzega mkoani Tabora.Ndugu Kinana amewasili Wilayani humo kwa ziara fupi ya Mwaliko wa Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla,aidha katika ziara hiyo Ndugu kinana amewapongeza viongozi mbalimbali waliochaguliwa katika ngazi ya chama ya wilaya na pia kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa ukumbi mkubwa wa kisasa ambao utatumika kwa matumizi mbalimbali.PICHA NA MICHUZI JR -NZEGA

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE AZINDUA JUKWAA LA WANAWAKE WILAYANI HUMO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Temeke
Felix Lyaniva azindua jukwaa la wanawake Kiwilaya katika viwanja vya Mwembe Yanga. Katika uzinduzi huo DC Lyaniva asisitiza wanawake kupendana,kuwa na umoja ili kujiletea maendeleo ya kweli,hata kufikia uchumi wa kati.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akiwa akishuhudia wakina mama wakipiga na mabanho yenye ujumbe tofauti katika uzinduzi wa jukwaa la wanawake Wilaya ya Temeke.

Wanawake hao ambao wamejitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo, huku sherehe hizo zikipambwa na shamrashamra za maandamano ya vikundi mbalimbali vya wanawake wajasiriamali.
Pia wanawake wajasiriamali walionesha kazi za mikono na ubunifu ufanywao na vikundi vyao.
Katika uzinduzi huo ulifanyika uchaguzi wa mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Kiwilaya ambapo Johari Maulid Mkonde alichaguliwa rasmi kuwa mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilayani Temeke.
Hata hivyo wanawake wa Temeke wamepewa fursa kushiriki uchumi wa viwanda ili waweze kufika malengo ya maendeleo endelevu ya 50/50 ya dunia kufikia mwaka 2030.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

YANGA KUANZA NA WASHELISHELI KLABU BINGWA, SIMBA WADJIBOUT

$
0
0
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara timu ya soka ya Yanga wamepangwa kuanza na timu ya St Lous ya Seychelles katika mchezo wa raundi ya kwanza katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Endapo Yanga kama itafanikiwa kufuzu katika mchezo huo wa raundi ya kwanza itakuwa na kibarua kingine cha kucheza na mshindi kati ya El Merreikh ya Sudani au Township Rollers ya Botswana.

Yanga imefanikiwa kucheza kombe la klabu bingwa barani Afrika baada ya kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara msimu wa mwaka 2017/18.

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika timu ya soka ya Simba imepangwa kuanza na timu ya Gendermerie Tnale ya Djibout katika mchezo wa raundi ya awali ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Endapo kama wekundu hao wa msimbazi watafuzu katika mchezo huo wa raundi ya awali basi wakuwa na kibarua kingine cha kucheza na mshindi kati ya El Masry ya Misri au Green Button Aloes ya Zambia.

Simba imefanikiwa kupata nafasi ya kucheza kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kuwa mabingwa wa kombe la Azam Sports Federation.

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR APOKEA MSAADA WA MADAWA

$
0
0
Waziri wa Afya Mhe,Mahmoud Thabit Kombo katikati akipokea msaada wa madawa aina mbalimbali kutoka Serikali ya Oman uliokabidhiwa na Balozi wa Oman anaefanyia kazi zake Zanzibar Dk,Ahmed Hamood Al-Habsi (kulia yake )hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Zanzibar kushoto yake ni Naibu Balozi wa Oman Ahmed Mohammed Al-Muzaini mwengine ni Mfamasia Mkuu wa Wizara ya Afya Habib Ali Sharif na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Maulid Salum.
Waziri wa Afya Mhe,Mahmoud Thabit Kombo kulia akizungumza na Viongozi pamoja na Waandishi wa Vyombo mbali mbali vya Habari katika hafla ya Upokeaji wa Msaada wa ar.Madawa kutoka Serikali ya Oman hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Mwandishi wa Habari wa ITV Farouk Kariym akiuliza maswali kwa Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo hayupo pichani baada ya kupokea Msaada wa Madawa kutoka Serikali ya Oman hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANIZBAR.

AGGREY&CLIFFORD YATOA MSAADA KWA KITUO CHA WATOTO WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU, DAR

$
0
0
Kampuni ya Aggrey&Clifford imetoa msaada wa fedha kusaidia kununua mahitaji kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Sadeline Health Care Trust kilichopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Mbali na msaada wa fedha, imetoa vifaa vya shule na vyakula ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kusherehekea sikukuu ya Krismasi ambapo pia wafanyakazi wa kampuni walijitolea muda wao kucheza na kufurahi pamoja na watoto hao kwa ajili ya kuwapatia faraja.
 Meneja Uhusiano wa kampuni ya Aggrey&Clifford, Martha Majura (kulia) akimkabidhi mkurugenzi wa kituo cha Sadeline Health Care Trust, Sara Kitanda (kushoto) mfano wa hundi ili kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu. Wanaoshuhudia kutoka wa pili kushoto ni wakurugenzi watendaji wa Aggrey & Clifford, Luke Smit, Tel Akuku na Ryan Goslin.
 Wafanyakazi wa Aggrey&Clifford wakigawa zawadi na kufurahi na watoto hao.
 Baadhi ya watoto wakiwa na furaha baada ya kupatiwa zawadi na kuonyeshwa faraja na upendo.
Wafanyakazi wa Aggrey&Clifford katika picha ya pamoja na watoto hao wanaolelewa katika kituo cha Sadeline.

Rais Magufuli Aiagiza BOT kuharikisha Sera ya Riba

$
0
0
Na: Beatrice Lyimo,MAELEZO-DODOMA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameihimiza Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuharakisha uandaaji wa Sera ya Riba ambayo zitaifanya taasisi za kifedha kuwa na riba zinazowiana na nafuu.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Mjini Dodoma wakati wa akizundua tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo jengo la LAPF Makole ambalo ni tawi kubwa kwa mkoa wa Dodoma.

“Serikali imechukua hatua mbalimbali za kukabiliana na changamoto za mabenki kutolipwa na wakopaji kwa kuanzisha mfumo wa kuhifadhi taarifa za mkopaji ambazo zitawezesha benki zote kuwatambua wakopaji na kuweza kuchukua tahadhari stahiki, pia itaendelea kutoa vitambulishio vya Taifa ambavyo kwa sasa vina taarifa zote muhimu za mwananchi,” amefafanua Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli ametoa wito kwa BOT kudhibiti matumizi ya dola na fedha nyingine za kigeni hapa nchini kutokana na kuharibu uchumi wa nchi. Dkt. Magufuli ametolea mfano wa fedha zilizoshikiliwa Airport ya Dar es Salaam ambazo ni zaidi ya Dola Bilioni Moja zikiwa hazijulikani zilipokuwa zikipelekwa.

SERIKALI YAWEKA MIKAKATI YA KUWAONDOA VIJANA KATIKA MAZINGIRA HATARISHI ILI WASHIRIKI SHUGHULI ZA KIJAMII

$
0
0
Na EmanuelMadafa,Mbeya ,JamiiMojaBlog.

Serikali inayo wajibu wa kuhakikisha kuwa inawaondoa vijana kwenye mazingira hatarishi na kuhimiza ushiriki wao kwenye shughuli za kijamii na kiuchumi ili kuleta maendeleo katika ngazi zote.

Imeelezwa kuwa takribani asilimia 56 ya nguvu kazi ya Taifa ni vijana wenye umri  kati ya miaka 15 hadi 35  kwa mujibu wa ripoti ya nguvu kazi ya mwaka 2014 .

Akizungumza jijini Mbeya wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya stadi za maisha kwa wawezeshaji kanda ya magharibi,Mkurugenzi wa maendeleo ya vijana Ofisi ya Waziri Mkuu ,kazi,Vijana ,ajira na wenye ulemavu Ndugu Jemsi Kujusi amesema serikali mara baada ya kubaini hali hilo iliamua kutengeneza  viwango vya ufundishaji wa stadi za maisha kwa vijana nje ya shule kwa kuandaa muongozo sanifu.

Amesema muongozo huo ulinzinduliwa mwaka 2011 na baada ya hapo iliendelea na jitihada za kuhakikisha kuwa kunakuwa na wawezeshaji wa kitaifa ambao jukumu lao linakuwa ni kutoa mafunzo kwa waelimishaji rika katika mikoa yao ili kuwafikia vijana wengi zaidi kwa ngazi zote.

Mkurugenzi huyo amesema kazi ya kuwaanda vijana kuwa wawezeshaji kitaifa ilianza Kanda ya Ziwa mwaka 2015  ambapo serikali iliendelea na jitihada za kuendeshav mafunzo kwa wawezeshaji kitaifa kutoka mikoa ya kanda ya kati ,Pwani na mashariki.
Amesema hadi Agosti 2017 jumla ya wawezeshaji kitaifa 60 walikuwa wamefikiwa ambapo lengo la serikali ni kuwa na wawezeshaji 78 kwa nchi nzima .

Mkurugenzi huyo amewataka washiriki wa mafunzo hayo kwa kanda ya magharibi ambo ni ,Ruvuma,Kigoma,Songwe,Mbeya,Katavi kuhakikisha kuwa wanatambua kuwa wanajukumu kubwa kwani serikali kupitia wao inataka kuona vijana wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi na kuachana tabia za kukaa vijiweni.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana ,Ajira na Wenye Ulemavu Ndugu Jemsi Kujusi akifungua mafunzo ya stadi za maisha kwa wawezeshaji kitaifa kanda ya Magharibi katika ukumbi wa Hospital ya Rufaa Mbeya Desemba 13 .

Washiriki wa Mafunzo  ya stadi za maisha kwa wawezeshaji kitaifa kanda ya Magharibi  wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana ,Ajira na Wenye Ulemavu  (hayupo Pichani )Ndugu Jemsi Kujusi  katika ukumbi wa Hospital ya Rufaa Mbeya Desemba 13 .

Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya katika  mafunzo hayo Ndugu George Mbigima akizunngumza katika mafunzo hayo

Washiriki wakifuatilia kwa makini mafunzo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAKULIMA WA PAMBA MKOANI TABORA WATAKIWA KUUZIA KAMPUNI ZILIZOWAKOPESHA MBEGU WAKATI WA MAVUNO

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT

WAKULIMA wa Pamba mkoani Tabora wametakiwa kudiriki kuuza  mazao yao kwa Kampuni ambazo hazikuwakopesha mbegu na viuawadudu ili kuzidisha imani kwa waliosaidia kuwapa mbegu kwa utaratibu wa kulipa baada ya mavuno.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati alipokuwa akikagua mashamba mbalimbali ya wakulima wa pamba Wilayani Igunga ili kujionea maendeleo ya kilimo cha zao hilo.

Alisema kuwa uaminifu ambao watauonyesha mara baada ya kuvuna na kuuza pamba katika Kampuni zilizowakopesha mbegu na viuawadudu itawajenga Imani kwa wakopeshaji kuangalia uwezekano wa kupanua wigo wa kuwasaidia wakulima ,hata ikiwezekana kuwakopesha mbolea kwenye kilimo msimu mwingine.

 “Nawaombeni wakulima wangu wazuri mjitahidi kuwa waaminifu kwa Kampuni zilizowakopesha mbegu na viuawadudu …kwani uaminifu wenu utawasaidia viongozi wenu kukaa meza moja na Kampuni  ili kuziomba ikiwezekana katika kilimo cha mwakani wawakopesha na mbolea” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

“Lakini mtakapovuna pamba yenu na kuitorosha kwa kubadilisha majina wakati wa uuzaji inaweza kusababisha Kampuni zikakataa kuwasaidia tena” alisema Mwanri.

Alisema kuwa mkulima atakayekamatwa kutaka kutorosha pamba ili kukwepa gharama za mbegu na viuawadudu atachukuliwa hatua ili ije fundisho kwa wakulima wengine wenye tabia hiyo. Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwaagiza Maofisa Ugani washirikiane na Maofisa Watendaji wa kuanzia Kata hadi Kata kuhakikisha wanaorodhesha wakulima wote waliokopeshwa mbegu za pamba ikiwa ni pamoja na kiwango walichochukua na eneo walilolima ili kuwa na uhakika.

Mwanri alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuepusha udanganyifu na ukwepaji unaoweza kufanywa na baadhi ya wakulima wachache ambao sio waaminifu kwa kudanganya majina au kutumia jina tofauti na lile ambalo hatalitumia wakati wa mauzo. Alisema kuwa vitendo vya aina hiyo ndivyo vilisababisha baadhi ya vyama vya msingi kufa kwa sababu ya kuwa na wakulima wenye tabia ya kutaka kukopesha lakini hawapendi kulipa mkopo.

Mwanri alisema kuwa ni vema viongozi wakawa makini wanakamilisha haraka kabla hata wakulima hawajaanza kuvuna pamba yao.

Naye Mkaguzi wa wa Pamba wilayani Igunga George Kihimbi alisema kuwa tayari wameshaanza kukusanya takwimu za wakulima wote na ukubwa mashamba waliyolima ili kupata usahihi wa pamba ambayo inatarajiwa kuvuna.


RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA NYUMBA ZA MAKAZI ZA NHC IYUMBU DODOMA LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisaidiwa na viongozi wengine kufunua kitambaa kuashiria kufunguliwa kwa nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisaidiwa na viongozi wengine kukata utepe kuashiria kufunguliwa kwa nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyuma la Taifa (NHC) Mama Blandina Nyoni, Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu wakikagua moja ya nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na NHC eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017
Muonekano wa baadhi za nyumba nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na NHC na kufunguliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017.

MBUNGE WA JIMBO LA NZEGA VIJIJINI DKT KIGWANGALLA AKABIDHI PIKI PIKI 19 MBELE YA KATIBU MKUU WA CCM DNUGU KINANA KWA WATENDAJI NA VIONGOZI WA KATA WA JIMBO HILO

$
0
0


Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla leo amekabidhi piki piki 19 kwa Viongozi na Watendaji wa kata 19 ndani ya jimbo hilo,makabidhiano hayo yalifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Check Pointi mara baada ya mkutano Mkuu wa jimbo kufanyika.Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana (Wa tatu kushoto) na kulia ni Katibu wa CCM wilaya Nzega Ndugu Janath Kayanda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nzega,Mh.Godfrey Ngapula . Picha na Michuzi Jr-Nzega.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpongeza mmoja wa Watendaji Kata kwa kukabidhiwa Piki Piki na Mbunge wao wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla,jioni ya leo katika ukumbi wa Checki Point,mjini humo mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa cha cha Mapinduzi (CCM ) Ndugu Abdulrahaman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa jimbo la Nzega vijijini mapema jioni ya leo katika ukumbi wa mikutano wa Check Point,wilayani humo mkoani Tabora.Ndugu kinana amewapongeza Wana CCM wa jimbo la Nzega kwa kushinda uchaguzi wa marudio wa madiwani,viongozi mbalimbali walioshinda nafasi mbalimbali za uongozi kwa ngazi ya Wilaya na kuwataka kuwa wamoja sambamaba na kushirikana katika kuhakikisha wanawaletea maendeleo wananchi na sii kulumbana tena.
Picha na Michuzi Jr-Nzega.
Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla akizungumza mbele ya Viongozi na wajumbe mbalimbali wa jimbo hilo waliojitokeza kwa wingi,katika Mkutano wao Mkuu wa jimbo ambao mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana .Dkt Kigwangalla amekabidhi piki piki 19 kwa Viongozi na Watendaji wa kata 19 ndani ya jimbo hilo. Mkuu wa Wilaya ya Nzega,Mh.Godfrey Ngapula kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Tabora,akitoa salamu mbele ya Viongozi na wajumbe mbalimbali wa jimbo la Nzega Vijijini kabla ya Mkutano Mkuu wa jimbo hilo kuanza.
Viongozi na wajumbe mbalimbali wa jimbo la Nzega Vijijini wakishangilia jambo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwasalimia kabla ya kuanza rasmi mkutano mkuu wa jimbo hilo,ambapo Mbunge wa jimbo hilo Dkt Hamisi Kigwangalla amekabidhi piki piki 19 kwa Viongozi wa Kata na Watendaji ili kuwasaidia kupambana na chanagamoto za usafri wakati wakiendelea kusikiliza na kutatua matatizo ya Wananchi wa jimbo hilo.
Viongozi na wajumbe mbalimbali wa jimbo la Nzega Vijijini wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia mapema leo katika ukumbi wa Checki Point,mjini humo wakati wa mkutano mkuu wa jimbo hilo,ambapo Mbunge wa jimbo hilo Dkt Hamisi Kigwangalla amekabidhi piki piki 19 kwa Viongozi wa Kata na Watendaji ili kuwasaidia kupambana na chanagamoto za usafri wakati wakiendelea kusikiliza na kutatua matatizo ya Wananchi wa jimbo hilo.

TANZANIA'S POSITION ON THE STATUS OF JERUSALEM

RC Wangabo asimamisha shughuli za uvuvi Ziwa Rukwa Kujikinga na Kipindupindu.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesimamisha shughuli za uvuvi katika ziwa Rukwa hadi hapo wataalamu wa afya watakapojiridhisha kuwa hakuna ugonjwa wa kipindupindu katika kambi za uvuvi zinazozunguka ziwa hilo na Mkoa kwa jumla.

Amesema kuwa athari inayopatikana katika kambi hizo za uvuvi zitawaathiri wala samaki unaotokana na uvuvi wa ziwa hilowaliopo na kuongeza kuwa wale wote wanaovua samaki waliopiga kambi katikakati ya ziwa waache kuvua mara moja na wasiruhusiwe kuingia katika ili kuweza kuudhibiti ugonjwa huo.

“Kuanzia leo tunapiga marufuku shughuli zote za uvuvi, mpaka tutakapojiridhisha kwamba tuna mazingira safi na salama, na kwamba maisha yetu hayapo hatarini tena na hao mnaosema wanakuja hawatapata maeneo ya kuuzia samaki wao tena watatafuta pa kwenda na tutaweka kambi ya kudhibiti wagonjwa wanaotoka huko wataishia hapa hawatakwenda popote,” Alisisitiza.

Ameyasema hayo alipofanya ziara katika kambi ya mererani iliyopo katika kijiji cha Ilanga, Kata ya Muze Wilaya ya Sumbawanga katika bonde la Ziwa Rukwa ambapo mpaka anafiak hapo palikuwa na wagonjwa 9 wa kipindupindu..
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilanga, katika kambi ya wavuvi Mererani, Wilayani Sumbawanga (hawapo kwenye picha) mara baada ya kufanya ziara katika kambi hiyo ili kujionea mazingira ya kambbi hiyo na hali ya kipindupindu.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilanga, katika kambi ya wavuvi Mererani, Wilayani Sumbawanga , mara baada ya kufanya ziara katika kambi hiyo ili kujionea mazingira ya kambbi hiyo na hali ya kipindupindu.

MAGAZETI YA ALHAMIS LEO DECEMBER 14,2017

WILAYA YA KISHAPU YATEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA SEKTA YA ELIMU YA MSINGI KUTOKANA NA FEDHA ZA TEA

$
0
0
Na Robert Hokororo, Kishapu DC

Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imeendelea kutekeleza miradi yake ya maendeleo katika sekta ya elimu ya msingi kutokana na fedha zilizotolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Itakumbukwa hivi karibuni ilitoa fedha kwa Halmashauri hiyo kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ambapo pamoja na nguvu za wananchi imepiga hatua katika utekelezaji.

Baada ya kupokea kiasi cha sh. milioni 25 ujenzi wa nyumba ya walimu wawili pamoja na matundu 18 ya vyoo katika shule ya msingi Idisanhambo ulianza mara moja na tayari umefikia hatua ya umaliziaji.Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga wakati akielezea miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema pamoja na kupokea fedha kutoka TEA, katika mwaka wa fedha 2017/2018, Halmashauri ya Kishapu imetenga jumla ya sh. milioni 90 kupitia mapato yake ya ndani kujenga nyumba sita za walimu.Magoiga alibainisha kuwa Halmashauri hiyo pia iliweza kupokea Ruzuku ya Maendeleo (LGDG) sh. milioni 88 zitakazotumika kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 11 za walimu.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Halmashauri imetenga jumla ya sh. milioni 48 kupitia mapato yake ya ndani kujenga matundu 24 ya vyoo kwa shule zake za msingi.Pia, Ruzuku ya Maendeleo (LGDG) sh. milioni 75 zitakazotumika katika ujenzi wa matundu 50 ya vyoo pia katika shule za msingi wilayani humo.

Fedha hizo kwa ujumla zinatarajiwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili katika sekta ya elimu ya msingi hususan upungufu wa nyumba za walimu na matundu ya vyoo.Aidha, pamoja na Halmashauri ikishirikiana na wadau kutekeleza miradi mbalimbali bado inaendelea kuhamasisha jamii kuchangia shughuli za maendeleo.

Pia kutokana na uelewa mdogo wa baadhi ya wazazi kuhusu masuala ya elimu, imeendelea kuelimisha jamii kuhusiana na suala hilo ili iendelee kupiga hatua wilayani humo.
Viongozi kutoka Idara ya Elimu ya Msingi wakiangalia maendeleo ya mradi wa nyumba ya walimu katika shule ya msingi Idisanhambo ambao umefikia katika hatua za umaliziaji.
Afisa Elimu Ufundi katika Halmashauri ya Kishapu, Moshi Balele (kushoto) akitoa maelezo kwa viongozi wengine katika idara hiyo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa choo katika shule ya msingi Idisanhambo.
Mojawapo ya vyoo katika shule hiyo ya msingi kikiwa katika hatua ya umaliziaji kabla ya kukabidhiwa na kuanza kutumika rasmi na wanafunzi.

AfCHPR ziarani Jamhuri ya Cape Verde

$
0
0
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) yenye Makao yake makuu jijini Arusha inafanya ziara ya kikazi katika Jamhuri ya Cape Verde ili kukutana na kuelimisha wadau mbalimbali nchini humo kwa lengo la kuiitangaza Mahakama hiyo.

Uelimishaji huo ni miongoni mwa juhudi zinazofanyika na Mahakama hiyo ili kuongeza uelewa wa wadau husika kuhusu jukumu na ujumbe wa AFCHPR katika suala zima la kulinda haki za Binadamu baranni Afrika na pia kuzihimiza nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kuridhia itifaki iliyounda Mahakama hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 34(6) na kutoa tamko rasmi la kutambua na kukubali Mamlaka ya AfCHPR kupokea kesi za Watu binafsi na Mashirika yasiyo ya kiserikali.

Katika ziara hiyo ya siku tatu inayoanza leo,13/12/2017 Jumatano wajumbe wake ambao ni pamoja na Majaji watatu na baadhi ya maofisa wa ofisi ya Msajili wa Mahakama hiyo watakutana na Rais wa Cape Verde,Waziri mkuu na Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo na wadau mbalimbali wakiwemo wanasheria na wawakilishi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali.

Rais wa Mahakama hiyo ya Afrika ya haki za Binadamu na Watu Jaji Sylvain Ore’ alisema ziara hiyo ya uelemishaji kuhusu Mahakama hiyo ni wan ne kufanyika kwa mwaka huu na kwamba juhudi hizo zitaendelea mwaka ujao wa 2018.

“Ili kufanikisha malengo ya AfCHPR na pia kuimarisha mfumo wa Haki za Binadamu barani Afrika nchi za umoja wa Afrika hazina budi kuridhia itifaki iliyounda Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kwa mujibu wa kifungu husika” alisema Jaji Ore’.

Tayari kwa mwaka huu uelimishaji huo umefnayika katika nchi za Jamhuri ya kiarabu ya Misri,Tunisia na Guinea Bissau.

Aidha hadi sasa ni nchi 30 tu kati ya 55 wanachama wa umoja wa Afrika ikiwemo Tanzania ndiyo zimeridhia itifaki iliyoanzisha AfCHPR na kati ya hizo ni nchi 8 tu ndiyo zimekwisha toa tamko la kuitambua Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.

BENKI YA CBA TANZANIA YAZINDUA VISA CARD MPYA MAHUSUSI KWA WATEJA WAKE MSIMU WA SIKUKUU

$
0
0
Mkurugenzi wa Mkuu Mtendaji wa Benki ya CBA Tanzania,Gifty Shoka (kushoto)akimkabidhi VISA Card mpya ya benki hiyo Mkurugenzi wa mauzo na masoko wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,Seraphin Lusala wakati wa hafla ya uzinduzi wa kadi hiyo itakayowawezesha wateja wa benki hiyo kufanya manunuzi mbalimbali kwa kipindi hiki cha Sikukuu,Wanaoshuhudia ni baadhi ya wateja wa benki hiyo, Nursiye Marhoon na Majda Mohamed.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Benki ya CBA Tanzania, Gifty Shoka akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa benki hiyo,Hyasinta Mwimanzi wakiongea na wateja wa benki hiyo jijini Dar es Salaam, Nursiye Marhoon na Majda Mohamed wakati wa hafla ya uzinduzi wa VISA Card mpya ya ambayo itawawezesha wateja wa benki hiyo kufanya manunuzi mbalimbali kipindi hiki cha Sikukuu.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya CBA Tanzania,wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa hafla ya uzinduzi wa VISA Card mpya ya benki hiyo itakayo wawezesha wateja wa benki hiyo kufanya manunuzi mbalimbali kipindi hiki cha Sikukuu.

SERIKALI IMETUMIA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 500 KUKAMILISHA MRADI MKUBWA WA UMEME WA KV 400 KUTOKA IRINGA HADI SHINYANGA

$
0
0
Na Jumbe Ismailly 
SERIKALI imetumia zaidi ya shilingi bilioni 500 kugharamia mradi wa usambazaji wa nishati ya umeme wa msongo wa KV 400 ulioanza kutekelezwa mwaka 2016 na kukamilika mwaka 2016  kutoka Mkoani Iringa kupitia Dodoma, Singida, Tabora hadi mkoani Shinyaga.

Meneja Njia kuu za umeme, Amosi Kaihula alisema kiasi hicho kikubwa cha fedha kilichotumika kusambaza miundombinu hiyo ya nishati ya umeme, haina budi kuhakikisha inalindwa na kila mwananchi na inakuwa salama kwa wakati wote ili huduma hiyo iweze kuendelea kupatikana.

Aidha meneja huyo aliweka bayana kwamba kwa hiyo inapotokea mhalifu mmoja anapokwenda kuchukua na kuangusha nguzo ulipopita umeme huo wa msongo wa taifa na kuanguka chini, serikali huingia hasara kubwa sana na kwamba idadi kubwa ya wananchi hukosa huduma hiyo ya umeme.

Kwa mujibu wa Kaihula gridi ya taifa imeungana na kwa hali hiyo endapo njia moja itaanguka na kuchangia kukosekana kwa umeme, itasababisha pia mikoa yote iliyoungamishwa katika gridi ya taiafa kukosa pia huduma hiyo ya umeme pia.
 Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, Emmanueli Luhahula akitoa maelezo ya jitihada zinazofanywa na wilaya hiyo kwa kushirikiana na TANESCO kukabiliana na wizi pamoja na uharibifu wa miundombinu ya umeme katika wilaya hiyo.
 Afisa usalama wa TANESCO Mkoa wa Singida,John Chilali (wa kwanza kutoka kushoto) akibadilishana mawazo nje ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Iramba na afisa mahusiano wa shirika hilo Mkoani Singida, Witness Msumba (wa pili kutoka kushoto). 
 Meneja Njia kuu za umeme, Amosi Kaihula akitoa maelezo kwa waandishi wa Habari juu ya fedha zilizotumika kukamilisha mradi huo mkubwa wa KV400 na mikakati ya kukabiliana na wizi pamoja na uharibifu wa miundombinu ya umeme katika njia kuu ya kusambazia nishati hiyo.
Nyaya za kusambazia umeme katika njia kuu ya kutoka Mkoa wa Iringa hadi Shinyanga yenye msongo wa KV400(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

Barclays awards University of Dar es Salaam students with full scholarships

$
0
0
Barclays Bank Tanzania Limited invests in Education 24 University students from the University of Dar es Salaam receive full scholarships to study.

Speaking during the announcement, which took place at the Barclays Head office, Barclays Managing Director, Abdi Mohamed said “As a business, we focus much of our efforts on education and skills. As an employer, we are well aware that Tanzania needs a thriving private sector that is investing in productive capacity. youth unemployment is a significant national challenge, we aim to play a role in providing young people with the tools and readiness needed to find meaningful employment and business opportunities. The availability of skills in any country is critical to drive economic growth and development”.

Barclays Bank Tanzania’s shared growth strategy is committed to enhance socio-economic growth in Africa. As a continent we can only be successful if we connect positively and create value with the society in which we operate. Shared growth means having a positive impact on society while delivering shareholder value.

He continued, “Our #BaloziMwanafunzi programme is one example aimed at upskilling young people education and skills. This scholarship programme is in partnership with the University of Dar es Salaam – Tanzania’s oldest and largest university. This year alone, 24 undergraduate students have been offered full scholarships,This initiative will help us build a real connection with the students, customers and clients, and other important stakeholders. It is our belief that the programme will have positive implications for our own talent pipeline”

Abdi concluded, “As a leading bank in Tanzania, and as part of a leading financial services group in Africa, we will continue to use our substantial resources and expertise to develop solutions to the various challenges facing Tanzania, as well as build partnerships to create a more prosperous Tanzania for the next generation”. 


Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (sixth from right, seated), posing for a souvenir picture together with 24 students awarded the Barclays full sponsorships at University of Dar es Salaam (UDSM), Barclays and UDSM officials during a media conference in Dar es Salaam yesterday. Fifth from right is UDSM Deputy Vichancellor, Academic, Prof. Bonaventure Rutinwa.
 

KHERI APOKELEWA KWA KISHINDO MKOANI DODOMA

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ndg:Kheri D James akizungumza na Vijana wa mkoa wa dodoma katika hafla ya kumkaribisha iliofanyika makao makuu ya CCM DODOMA.

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi ndg:Thabia Mwita akizungumza na vijana wa Umoja wa Vijana wa chama cha mapinduzi katika viwanja vya makao makuu ya ccm dodoma.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg:Kheri D James (katikati) akiwasili Ofisi za Makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa kushoto kwake ni Ndg Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka.
Ndg:Rodrick Mpogolo Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi akimpokea Mwenyekit wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi alipowasili Makao makuu ya chama cha mapinduzi.
Vijana wakisikiliza kwa umakini hotuba ya mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ndg:Kheri D James.
PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MSHAURI WA ELIMU BEATRICE :WALIMU WENYE UWEZO WANATAKIWA KUFUNDISHA WANAFUNZI WA DARASA LA AWALI

$
0
0
Na Said Mwishehe
MSHAURI wa elimu nchini kutoka Shirika la Maendeleo la Canada, Beatrice Omari amesema walimu wenye uwezo mkubwa kufundisha na walio na hekima, busara na uvumilivu ndio wenye kustahili kufindisha wanafunzi wa elimu ya awali,darasa la kwanza na pili.

 Akizungumza Dar es Saalam leo baada ya kutolewa matokeo ya utafiti wa Kiufunza awamu ya pili wa motisha kwa walimu uliofanyika katika kipindi cha mwaka 2015/2016 katika shule120 nchini.

 Amesema kwa maoni yake na uzoefu alionao kwenye elimu ,ni vema walimu wenye uwezo mkubwa wa kufundisha ndio wawe wanafundishi wanafunzi wa elimu ya awali,darasa la kwanza,pili na tatu kwani ndio ujenzi wa msingi bora wa elimu.

 Ametoa majibu hayo baada ya kuulizwa kwanini miaka ya zamani waliokuwa wanafundisha darasa la kwanza na pili walikuwa wenye umri mkubwa ambapo alisisitiza ilitokana na uzoefu wao wa kufundisha na kuwavumikia wanafunzi ambao ndio wameanza kujengwa kielimu.

 "Elimu ya awali, darasa la kwanza na pili inahitaji walimu wenye uwezo mkubwa wa kufundisha maana ndipo ambapo mwanafunzi anaandaliwa kielimu,ndio eneo ambalo mwaamnafunzi anafundishwa kuandika maumbo ya herufi.

 " Wanapoandaliwa na walimu wazuri mwanzoni,walimu wa madarasa ya mbele jukumu lao inakuwa ni kuwajaza maarifa ya kielimu.Wasipoandaliwa vema matokeo take ndio wanapatikana wanafunzi wanaohitimu darasa la saba lakini hawajui kusoma na kuandika,"amesema.

 Kuhusu motisha amesema Serikali inafanya jitihada kubwa kuboresha maslahi ya walimu nchini lakini no vema kukawa na mfumo rasmi ambao utasaidia kujenga mazingira bora ya walimu.

 Pia badala ya motishi,jamii inatakiwa kutambua thamani ya mwalimu ambaye ndio anayepika wataalamu wa fani mbalimbali. Amesema zamani nyumba nzuri kijijini ilikuwa ni ya mwalimu na walikuwa kimbilio la wananchi kwani walitambua thamani yao lakini sasa jamii imeshindwa kutambua umuhimu wa mwalimu.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images