Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Waziri Mahiga awaasa Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne (4) la Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa Wazalendo na kusimamia maslahi ya Jumuiya

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga(katikati) akiongea katika kikao cha uongozi wa Wizara hiyo na Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne (4) la Jumuiya ya Afrika Mashariki, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Disemba 2017. Pembeni yake kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba na kulia ni Mwenyekiti wa Wabunge wateule wa Bunge la Afika Mashariki, Mhe. Abdullah Makame. 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda (kulia) akiongea katika kikao hicho ambapo aliwakaribisha Waheshimiwa Wabunge wateule pamoja na kuwaeleza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ipo tayari kuwapa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao. Pembeni yake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi. 
Mwenyekiti wa Wabunge Wateule wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Abdullah Makame akiushukuru uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kikao kizuri cha utangulizi kabla ya kuanza kwa Bunge hilo na pia akaahidi kuwa wataenda kuliwakilisha Taifa vizuri sambamba na kusimamia maslahi ya Jumuiya kwa maendeleo na ustawi wa wananchi wake. 
Sehemu ya Waheshimiwa Wabunge Wateule wa Bunge la Afrika Mashariki wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na Mhe. Waziri Mahiga (hayupo pichani) 
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Wabunge wakifuatilia kikao hicho. 


Kaimu Mkurugenzi TAA, Ataka Madereva Wa Magari Ya Zimamoto kuyatunza

$
0
0
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela amewataka madereva wanaoendesha magari ya zimamoto na uokoaji kwenye viwanja vyote vya ndege Tanzania kuyathamini na kuyatunza magari hayo kwa kuwa wameaminiwa kufanya kazi hiyo.

Bw. Mayongela alitoa kauli hiyo kwenye Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), alipokwenda kujitambulisha na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili, ambapo alisema magari hayo yamenunuliwa kwa gharama kubwa, hivyo yanapaswa kutunzwa.

Alisema uthamini wao kwa magari hayo kutayafanya kudumu na kuyafanya kazi kwa muda mrefu bila kuharibika, jambo ambalo litachangia ufanisi wa kazi, ya uokoaji na usalama kwenye viwanja vya ndege, ambapo mbali na miundombinu pia lazima miundombinu ipewe kipaumbele.

“Najua wapo wenzenu wachache sio waaminifu wamekuwa wakitengeneza manunuzi hewa ya vifaa na hata mafuta kwa manufaa yao binafsi, lakini ninawaomba mujione nyie ndio wenye thamani kwa kuaminiwa kuendesha magari haya ya mamilioni ya fedha, kwani ni nyie tu mnayoweza kuyaendesha kutokana na kuwa na mitambo ya kisasa tofauti kidogo na mengine, hivyo basi tuyatunze ili tuisaidie serikali yetu isiingie gharama za mara kwa mara za kununua vifaa au magari mengine mapya,” alisisitiza Bw. Mayongela.

Hatahivyo, alisema zimamoto ni moja ya mambo ya msingi hivyo amewahakikishia kuwapeleka kozi za mara kwa mara za ndani na nje ya nchi, kutokana na mambo mbalimbali yanayobadilika duniani, na kwa kuanzia ataanza na askari wawili hadi wanne, kulingana na mafunzo wanayostahili kushiriki, na atahakikisha washiriki ndio wanaokwenda kufanyia kazi kwa vitendo katika utendaji wao na sio kupeleka mabosi ambao hawahusiki.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (aliyesimama mbele), akiongea na askari wa zimamoto na uokoaji wa kituo cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). Mbele kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa JNIA, Bw. Johannes Munanka na (kulia) ni Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji wa Viwanja vya Ndege nchini, Kamishna Msaidizi, Christom Manyologa.

Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka (aliyesimama mbele) akitoa maelezo mbalimbali kwa askari wa zimamoto na uokoaji katika kikao kilichoitishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela.
Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji wa Viwanja vya Ndege Tanzania, Kamishna Msaidizi, Christom Manyologa (aliyesimama) akiongea na askari wa kituo cha zimamoto na uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, katika mkutano ulioitishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela.

YANGA WAPANGWA KUNDI MOJA NA SINGIDA UNITED KOMBE LA MAPINDUZI

$
0
0
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara timu ya soka ya Yanga imepangwa kundi moja na Singida United katika ushiriki wa michuano ya kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu huko visiwani Zanzibar.
 
Yanga imepangwa katika kundi B lenye jumla ya timu sita huku kundi A lenye timu za Simba na Azam FC lina jumla ya timu tano.

Bingwa Mtetezi wa kombe hilo ni Azam ambao wapo kundi moja na mabingwa wa kombe la Shirikisho Simba sambamba na URA kutoka Uganda,Jamhuri na Mwenge zote za Zanzibar

MAPINDUZI CUP JANUARY 2018

GROUP A
1.Azam FC
2.Jamhuri SC
3.Mwenge SC
4.Simba SC
5.URA

GROUP B
1.JKU
2.Mlandege FC.
3.Singida United
4.Taifa ya Jang'ombe
5.Yanga SC na
6.Zimamoto

MSAMA AMSHUKURU RAIS DKT. MAGUFULI KWA UAMUZI WA KUWASAMEHE WASANII BABU SEYA NA PAPII KOCHA

$
0
0
Na Kajunason/MMG. 
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Action Mart, Alex Msama amshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kitendo cha kutoa msamaha kwa wanamuziki maarufu nchini, Papii Nguza (Papii Kocha) na baba yake mzazi, Nguza Viking (Babu Seya) aliyekuwa akitumikia kifungo cha maisha katika gereza la Keko jijini Dar es Salaam.
 
 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaama, Msama ambaye ni alikuwa ni mjumbe wa Bodi wa BASATA na mpigania haki zawasanii na vile vile ni mlezi wa wasanii mbali mbali amesema jambo alilolifanya ni jema sana na ametekeleza maagizo ya Mungu ambayo anatushauri tusamehe.
 
 "Ukisoma hata kwenye vitabu vya biblia suala la kusamehe alishalisema, katika Mathayo 18:21-22... Ndipo Petro akamjia Yesu na kumwuliza, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami nimsamehe? Je, hata mara saba?” Yesu akamjibu, ''Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.' alisema Msama. 
 
Msama aliongeza kuwa jambo hilo ni kubwa na halina kipingamizi chochote maana kila kona ya Tanzania maamuzi hayo yamepokelewa kwa mikono miwili. Aliongeza kuwa wafanyabiashara wote wanaofanya kazi za sanaa ni vyema wakafuata taratibu kwa kuuza kazi halali zilizo na stika za TRA ambazo zitawanufaisha wasanii na serikali kwa ujumla. 
 
Hata hivyo, zoezi laukamataji Kazi feki za sanaa litaendelea katika Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni zoezi la nchi nzima. 

KUMBE UNGA WA MUHOGO HUTENGENEZEA KIWASHIO MOTO CHA KIBIRITI?!!

$
0
0
Na Richard Mwaikenda, Mkuranga 

UNGA wa muhogo unatumika kutengenezea kishungi cha kuwashia moto katika vibiriti.

Jambo hilo lilithibitishwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha kusaga muhogo cha Ukaya, Mkuranga, Ibrahim mbele ya uongozi wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) uliotembelea kiwanda hicho.

Alisema kuwa miongoni mwa wateja wakubwa wa unga wao ni Kiwanda cha kutengenezea vibiriti cha Kasuku kinachoutumia kwa kutengenezea kishungi cheusi cha njiti ya kibiriti kinachotumika kuwasha moto.

Uongozi wa Mkikita ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Kissui S. Kissui na Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao huo, Adam Ngamange ulitembelea kiwanda hicho kwa lengo la kuingia nao mkataba wa makubaliano ya kukitumia kusaga mihogo ya wanachama wao kupata unga utakaouzwa na katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Ibrahim alisema unga pia hutumika kutengenezea dawa ya kuzuia kuhara, pombe, mafuta, chakula cha wanyama na binadamu.meandaliwa na Richard Mwaikenda;Kamanda wa Matukio Blog 0715-264202
Uongozi wa Mkikita ukiwa na uongozi wa kiwanda cha Unga cha Ukaya, Mkuranga, Pwani, ulipotembelea kiwanda hicho ambacho wako mbioni kuingia mkataba wa kusaga mihogo ya wanachama wao kupata unga wa kuuza katika masoko ya ndani na nje ya nchi.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui S. Kissui, Mkurugenzi wa Kiwanda, Ibrahim, Meneja wa Kiwanda, Matanga na Mkurugenzi wa Mkikita, Adam Ngamange.

WACHIMBAJI WA JASI WALILIA SOKO LA UHAKIKA

$
0
0
Wachimbaji wa Madini ya Jasi Mkoani Singida wametakiwa kufanya shughuli zao kwa uaminifu ili kujihakikishia soko la uhakika.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ametoa wito huo Desemba 11, 2017 Wilayani Itigi mara baada ya kuzungumza na Wachimbaji wa madini hayo wakati wa ziara yake kwenye maeneo yenye uchimbaji wa madini ya Jasi Mkoani Singida. 

Wachimbaji wa Madini hayo walimueleza Naibu Waziri Nyongo changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa soko la uhakika.
Mara baada ya wachimbaji hao kuelezea changamoto zinazowakabili, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi, Ali Minja alimueleza Naibu Waziri Nyongo kwamba tatizo la soko la Madini ya Jasi yanayochimbwa Singida linasababishwa na wachimbaji wenyewe kwa kuchanganya madini hayo na udongo.

Alisema wakati mwingine wachimbaji wenyewe wanasababisha kupotea kwa soko, kwani mnunuzi akinunua Madini ya Jasi yaliyochanganywa na udongo hawezi kurudi tena kununua.“Baadhi ya wachimbaji wa Jasi Mkoani hapa sio waaminifu kwani wanachanganya madini na takataka ikiwemo udongo, na hii inakimbiza wanunuzi,” alisema.

Kufuatia hali hiyo, Naibu Waziri Nyongo aliwaasa wachimbaji hao kuwa wakweli kwa kufanya shughuli zao kwa uadilifu na ubunifu mkubwa wa utafutaji wa masoko ili kuvutia wanunuzi wengi zaidi na hivyo kujiongezea kipato. 
 Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Singida, Sosthenes Massola (kushoto) akizungumza na Wafanyakazi, Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini ya Jasi (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia aliyesimama) Mkoani Singida.
 Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Mapambo ya majumbani cha RSR kilichopo Singida Mjini, Rashid Rashid (kushoto) akimuonesha Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) baadhi ya bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo zitokanazo na Madini ya Jasi yanayochimbwa Itigi mkoani humo.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (aliyesimama) akizungumza na Wafanyakazi, Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini ya Jasi (hawapo pichani) wakati wa ziara yake Itigi Mkoani Singida. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Pius Luhende.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akitembelea Kiwanda cha kutengeneza Chaki cha Furaha, kilichopo katika Kata ya Tambukareli, Itigi. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Pius Luhende na kushoto ni Meneja wa Kiwanda hicho, Peter Nolasco.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

OFISI NZIMA YA MKIKITA WAHAMIA SHAMBANI VIKINDU KUPANDA MCHAICHAI

$
0
0

Na Richard Mwaikenda.

OFISI nzima ya Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Livinggreen), umehamia shamba Vikindu kuanza kampeni ya kupanda mchaichai.

Katika kampeni hiyo ya aina yake iliwashirikisha wakurugenzi, maofisa na wafanyakazi wa mtandao huo ili kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya Back to The Land.

Walipofika Block Farming hiyo ya mchaichai, waligawanyika katika makundi mbalimbali ambapo wengine kazi yao ilikuwa kubeba mbegu ya mchaichai, baadhi walisombelea mbolea, kufyeka majani, kuchanganya mbolea kwenye mashimo na wengine kupanda.

Kazi hiyo ilipamba moto hasa baada ya kuhamasishwa na viongozi wakuu ambao pia walishiriki bega kwa bega kubeba mbolea, mbegu na kupanda pia. Hakuna aliyeruhusiwa kukaa bila kazi akiwemo pia mwandishi wa habari hizi, Richard Mwaikenda.

Viongozi walioshiriki kwenye kampeni hiyo ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,  Dk. Kissui S. Kissui, Mkurugenzi Mtendaji,  Adam Ngamange, Mkurugenzi wa Utawala na Mashamba, Catherina, Mkurugenzi wa Fedha, Elizabeth na Mhasibu Mkuu wa mtandao huo, Mshashu na msaidizi wake Samson.

Ofisi kwa siku nzima ilibidi zifungwe kwa siku nzima, ambapo walifanya kazi ya shamba kwa siku nzima ya jana hadi majira ya saa jioni saa 12.

Mkurugenzi wa Fedha, Elizabeth akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui S. Kissui wakibeba miche ya mchaichai wakipeleka kupanda shambani Vikindu. Shmba hilo ni la wanachama wa Mkikita. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Meneja Uhusiano wa Mkikita, Neema (kulia0 akiwa na Ofisa wa Mradi wa Kuku, Rose wakati wa shughuli ya kupanda mchaichai
Wakichambua miche ya mchaichai
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mkikita, Dk Kissui (kulia) akiwapongeza wafanyakazi kwa moyo wao wao wa kujitolea kupanda mchaichai.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

PROF. MBARAWA ATAKA UJENZI RELI YA KISASA KUHARAKISHWA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa wito kwa mkandarasi Yapi Merkezi na Motaengil Africa wanaojenga reli ya kisasa (Standard Gauge Railway), kufanya kazi kwa uadilifu, kulingana na vipimo vilivyo kwenye mkataba ili kuwezesha mradi huo kukamilika kwa wakati.

Aidha, ameitaka Kampuni Hodhi ya Rasilimali za reli (RAHCO), kuhakikisha kuwa inafuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo kwani wananchi wamekuwa wakisubiri kukamilika kwake na kuanza kupata huduma za usafiri wa treni zitakazorahisisha shughuli zao za kibiashara na kijamii.

Akizungumza leo mara baada ya kukagua mradi huo katika kijiji cha Soga mkoani Pwani, Waziri Mbarawa amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya wakandarasi hao na kuagiza kuongeza spidi zaidi ili ifikapo mwaka 2020 mradi huo uwe umekamilika.“Kasi mnayoenda nayo sio mbaya, ila naomba RAHCO mhakikishe mnasimamia kwa karibu kuhakikisha spidi inaongezwa ili kazi ikamilishwe haraka na kwa viwango”, amesema Profesa Mbarawa.

Akiwa katika kijiji hicho, Waziri Mbarawa amemwagiza Kaimu Mtendaji Mkuu wa RAHCO, Masanja Kadogosa, kukutana na uongozi wa kampuni hizo kujadili na kuangalia fursa za upatikanaji wa ajira kwa watanzania hususan wakazi wa eneo inapopita reli hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali ya Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa (kushoto), kuhusu kusimamia kwa karibu mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge), wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo katika kijiji cha Soga Mkoani Pwani na Ngerengere mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali ya Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa (kulia), alipomweleza hatua za ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge), wakati Waziri huyo alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo Mkoani Pwani.
Muonekano wa moja ya kalvati linalojengwa kwenye Reli ya Kisasa (Standard Gauge), katika eneo la Kisarawe Mkoani Pwani. Mradi huo unajengwa kwa awamu mbili ambapo sehemu ya kwanza inajengwa kutoka Dar es Salaaam mpaka Morogoro ambapo sehemu ya pili itajengwa kutokea Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma.
Mafundi wa Kampuni ya Yapi Merkezi wakiendelea na kazi ya kujaza zege kwenye moja ya kalvati linalojengwa kwenye Reli ya Kisasa (Standard Gauge), katika eneo la Kisarawe Mkoani Pwani.

Tingatinga likiendelea na kazi ya kuchenjua tabaka la chini la Reli ya Kisasa (Standard Gauge), katika eneo la Soga, Mkoani Pwani.

RC PWANI AFUNGA MAFUNZO YA SUMA JKT RUVU

$
0
0
 MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kampuni ya ulinzi ya Suma JKT kwenye kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha 832 Kj cha Ruvu Mlandizi - Kibaha.
 Mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi ya Suma JKT, Meja Alfred Mwaijande  akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kampuni ya ulinzi ya Suma Jkt kwenye kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha 832 Kj cha Ruvu Mlandizi - Kibaha.
Wahitimu wa mafunzo ya kampuni ya ulinzi ya Suma JKT wakiwa kwenye kufunga mafunzo ya kampuno ya ulinzi ya Suma JKT kwenye kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha 832 Kj cha Ruvu Mlandizi - Kibaha.(picha na Mwamvua Mwinyi)

DC MUFINDI: MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA UTASAIDIA KUTOKOMEZA RUSHWA KWENYE OFISI ZA UMMA NCHINI

$
0
0
Na Afisa Habari Mufindi

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Jamhuri William amesema, endapo Ofisi za Umma hazitodhibiti ipasavyo mifumo na urasimu uliowekwa kwenye Ofisi za Serikali, masuala hayo yanaweza kuwa kichocheo kikubwa cha kuendelea kukua kwa tatizo la rushwa katika ofisi hizo.

Mkuu huyo wa Wilaya ametoa kauli hiyo wakati akifunga maadhimisho ya siku ya Maadili na haki za Binadamu, iliyoadhimishwa kiwilaya katika chuo cha maendeleo ya jamii Rungemba kilichopo Mjini Mafinga Wilayani Mufindi.

Mh. Jamhuri amesema, urasimu uliyowekwa kwa nia njema ya kuthibiti utendaji kazi ukitumiwa vibaya, unaweza kuwa chanzo cha rushwa, hivyo akatoa rai kwa taasisi zote za umma kuhakikisha zinazingatia suala la kuwa na mkataba wa huduma kwa wateja na kusisitiza kuwa, hiyo ni moja kati ya njia kuu za kuondoa suala la rushwa katika Ofisi za umma.

Awali Mkuu wa taasisi ya kuzui na kupambana na rushwa Wilayani Mufindi bw. Orest Mushi, ametanabaisha kuwa tafiti za hivi karibuni zinazoonesha kupungua kwa rushwa nchini, zinatokana na utashi wa kisiasa uliopo, chini ya Rais John Pombe Magufuli, huku akibainisha malengo ya maadhimisho hayo, kuwa ni pamoja na kuiwezesha Serikali kufuatilia na kufahamu hali ya rushwa nchini, kubainisha madhara ya rushwa na kutambua umuhimu wa kuendelea kupambana nayo, kutambua changamoto za mapambano dhidi ya rushwa, kuweka mikakati ya kupambana na rushwa, sanajari na kuisaidia nchi kutathimini ushiriki wake dhidi ya mapamabano ya rushwa kimataifa.

Mwaka 2005 serikali iliamua kwamba maadhimisho haya yawe yanafanyika disemba 10 ambapo, nchi yetu huungana na mataifa mengine duniani kuiadhimisha kama siku ya maadili na haki za binadamu. Kaulimbiu ya mwaka huu ni wajibika piga vita rushwa, zingatia maadili na haki za binadamu, kuelekea uchumi wa kati.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Jamhuri William, akiwahutubia wanafunzi wa chuo cha Rungemba pomoja na wananchi wakati maadhimisho ya siku ya Maadili na haki za Binadamu, iliyoadhimishwa kiwilaya katika chuo cha maendeleo ya jamii Rungemba kilichopo Mjini Mafinga Wilayani Mufindi.
Sehemu ya Wanachuo wa Chuo cha Rungemba pamoja na Wananchi wakisikiliza hotuba ya mgeni wa heshima wakati wa kufungwa kwa maadhimisho ya siku ya Maadili na haki za Binadamu, iliyoadhimishwa kiwilaya katika chuo cha maendeleo ya jamii Rungemba kilichopo Mjini Mafinga Wilayani Mufindi.
Mkuu Takukuru Wilaya ya Mufindi Bw. Orest Mushi, akiwasilisha mada wakati wa maadhimisho ya siku ya Maadili na haki za Binadamu, iliyoadhimishwa kiwilaya katika chuo cha maendeleo ya jamii Rungemba kilichopo Mjini Mafinga Wilayani Mufindi.

TAARIFA YA MNADA WA TATU WA KIMATAIFA WA MADINI YA TANZANITE

MAGAZETI YA JUMATANO LEO DECEMBER 13,2017

HOTUBA YA RAIS DKT MAGUFULI UFUNGUZI WA MKUTANO WA 9 WA UMOJA WA WAZAZI WA CCM

UTELEKEZAJI FAMILIA 'WASHAMIRI' KATA YA SARANGA JIJINI DAR

$
0
0
  KESI za wanaume kutelekeza familia zao zimejitokeza kwa wingi Kata ya Saranga eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam kwenye kituo maalumu cha muda kilichoendeshwa kutoa huduma za pamoja kwa waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’.

Akizungumza katika kituo hicho kilichoratibiwa na Kituo cha Usuluhishi – CRC, kilichopo chini ya Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Mwanasheria wa Kituo cha CRC, Bi. Suzan Charles alisema idadi kubwa ya wateja waliowahudumia kwa siku mbili ni akinamama waliotelekezwa na waume zao au wanaume waliowazalisha.

Zoezi hilo la utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia 'One Stop Center’ lililoendeshwa kuanzia Desemba 11 na 12 eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam tangu majira ya asubuhi hadi jioni lilishirikisha huduma za msaada wa kisheria, Ushauri nasihi pamoja na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi.

Akifafanua zaidi Mwanasheria wa CRC, Bi. Suzan Charles alisema licha ya uwepo tatizo la utelekezaji watoto, lakini walikuwepo pia akinamama wajawazito ambao nao walitelekezwa wakiwa na hali hiyo jambo ambalo lilikuwa na changamoto kubwa kwao, kwani hali zao ni dhaifu hawawezi hata kufanya kazi kujipatia kipato kwa sasa.

Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii wa Kituo cha Kituo cha CRC, Bi. Violeth Chonya mbali na kutoa ushauri wa wateja waliojitokeza walishirikiana na vitengo husika vya serikali katika kuwaita wanaolalamikiwa kutelekeza familia na kuangalia namna ya kutatua kesi hizo.

Alisema wateja waliokuja kupata huduma katika kituo hicho pia wamekuwa wakitoa elimu ya uzazi kwa kushirikiana na idara ya afya ili wana jamii kujitambua na kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali.

"..Unajua masuala mengine kwa wateja waliotutembelea kwa siku hizi mbili tumebaini akinamama wengi hawana elimu ya kutosha juu ya masuala ya uzazi, unakuta mama hapewi huduma zozote za msingi toka kwa mwenza wake lakini bado anaendelea kuzaa huku analalamika kutosaidiwa matunzo...hapa utabaini kabisa mama hataki kuongeza idadi ya watoto ila ameshindwa kuzuia mimba anaendelea kuzaa," alisema Bi. Violeth Chonya.

"Naamini mtu kama huyu akipatiwa elimu ya masuala ya uzazi anaweza kuamua kupata mtoto pale tu anapoitaji na kuacha kulundika idadi ya watoto huku akiendelea kukumbana na changamoto ya huduma toka ama kwa mume au wenza wake..," alisema Afisa Ustawi wa Jamii huyo wa Kituo cha KCRC.

Alisema kumekuwa na muamko mkubwa kwa jamii ya Kata ya Saranga, Temboni kuja kupata huduma zilizokuwa zikitolewa kituoni hapo jambo ambalo linaonesha upo uhitaji mkubwa ya kutengenezwa kwa vituo hivyo, ili vihudumie jamii kwa karibu.
 Huduma zikitolewa kwenye Kata ya Saranga eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam kwenye kituo maalumu cha muda kilichoendeshwa kutoa huduma za pamoja kwa waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’.
Huduma zikitolewa kwenye Kata ya Saranga eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam kwenye kituo maalumu cha muda kilichoendeshwa kutoa huduma za pamoja kwa waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’

WAZIRI KALEMANI AKAGUA MIRADI YA UMEME REA III KONGWA NA KONDOA

$
0
0
Na Veronica Simba – Dodoma
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amekagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika Wilaya za Kongwa na Kondoa mkoani Dodoma.

Katika ziara hiyo ya siku moja iliyofanyika Jumatatu Desemba 11, 2017, Waziri Kalemani aliwasisitiza viongozi wa Halmashauri ambako Mradi wa REA III unapita, kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kuunganisha umeme hususan katika Taasisi mbalimbali za umma.

“Siyo vema Taasisi muhimu za umma zikaendelea kukosa umeme kwa kutokuwa na fedha hivyo kuwatesa wananchi. Hakikisheni mnatenga fedha kwa shughuli hiyo muhimu.”

Aidha, alibainisha kuwa, maeneo yanayopewa kipaumbele katika Mradi wa REA III ni Taasisi zote za umma ili kuhakikisha zinatoa huduma bora kwa wananchi.

Pia, aliwataka wakandarasi wanaotekeleza Mradi huo katika maeneo mbalimbali nchini, kukutana na viongozi wa maeneo husika wakiwemo wabunge ili wapewe mwongozo wa sehemu muhimu za kipaumbele zinazotakiwa kuunganishiwa umeme.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (aliyeshika kipaza sauti) akiwasalimu wananchi wa Kijiji cha Pembamoto, Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma, alipofanya ziara kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III)
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akimkabidhi Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, kifaa kinachotumika kuunganisha umeme katika nyumba pasipo kutandaza nyaya, kijulikanacho kama UMETA. Waziri alitoa kifaa hicho kama zawadi kwa baadhi ya wazee katika Kijiji cha Makole, Wilaya ya Kongwa, wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA III) pamoja na kuzungumza na wananchi.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kulia), akifafanua jambo kwa Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (kushoto), alipokuwa katika ziara ya kazi jimboni humo kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III). Wengine pichani ni viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wataalam kutoka wizarani, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

WADAU WA TAKWIMU WAKUTANA KUJADILI NA KUTATHMINI UTEKELEZAJI WA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU NA MPANGO WA PILI WA MAENDELEO WA TAIFA

$
0
0
Na Emmanuel Ghula
WADAU wa Takwimu nchini wamekutana ili kujadili upatikanaji wa Takwimu za msingi na uzalishaji wa takwimu na mapungufu yaliyopo katika kupima na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa.

Akizungumza wakati akifungua warsha ya siku mbili ya wadau hao, Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango Mhandisi Happiness Mgalula amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Maendeleo pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)  wameandaa warsha hiyo ili kujadili namna bora ya upatikanaji wa takwimu zitakazosaidia kufanikisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo.

“Leo tumekutana hapa kwa pamoja ili kujadili namna bora ya upatikanaji wa takwimu kwa ajili ya kupima na kutathmini utekelezaji wa viashiria vya Malengo ya Maendeleo Endelevu na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa katika sekta ya Ukuaji Uchumi, Ajira na Ushindani wa Kiuchumi,” amesema Mhandisi Mgalula.
 Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango Mhandisi Happiness Mgalula akizungumza wakati akifungua warsha ya siku mbili ya wadau wa takwimu waliokutana kuanzia leo jijini Dr es Salaam katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere.
 Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wa hafla ya ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya wadau wa takwimu waliokutana leo jijini Dr es Salaam katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere.
Baadhi ya wadau wa takwimu waliokutana leo jijini Dar es Salaam katika warsha ya siku mbili ili kujadili namna bora ya upatikanaji wa takwimu kwa ajili ya kupima na kutathmini utekelezaji wa viashiria vya Malengo ya Maendeleo Endelevu na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA TAWI JIPYA LA BENKI YA CRDB MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akifungua rasmi Tawi la Benki ya CRDB lililopo katika jengo la LAPF mjini wa Dodoma leo. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu mstaafu Mzee John Samwel Malecela (kulia kwa Rais), Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay (kushoto kwa Rais), Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei pamoja na viongozi wengine wa kitaifa na wa mkoa wa Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua rasmi Tawi la Benki ya CRDB lililopo katikati ya mjini wa Dodoma. Wengine katika picha ni Mke wake Mama Janeth Magufuli watatu kutoka (kushoto), Waziri Mkuu mstaafu Mzee John Samwel Malecela wanne kutoka kushoto pamoja na viongozi wengine wa kitaifa na wa mkoa wa Dodoma.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SIMON SIRRO AKIWA ZIARA MKOANI KIGOMA

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa kwanza kushoto akisalimiana na viongozi  wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kigoma baada ya kumaliza kikao  katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma katika ziara yake ya kikazi mkoani humo.  Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa kwanza kushoto akiwa na Askari wa kikosi cha kupambana na uhalifu katika mazoezi ya viungo mkoani Kigoma (CRT) wakati wa ziara yake ya kikazi.  Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati) na kushoto kwake ni Kamandn cbja wa Polisi Mkoa wa Kigoma  ACP Martin L. Otieno wakiwa katika picha ya pamoja na Askari wa kikosi cha kupambana na uhalifu mkoani Kigoma baada ya kumaliza kukagua mazoezi ya ukakamavu.  Picha na Jeshi la Polisi.

TUWEKE MKAKATI MAALUMU KUFUATILIA VIWANDA VIPYA-MHANDISI MANYANYA

$
0
0
Na Said Mwishehe wa Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mhandisi  Stella Manyanya amesema ipo haja ya kuwa na mkakati maalumu wa kufuatilia viwanda vinavyoanzishwa nchini ili kukomesha vifo vya viwanda.
Manyanya aliyasema hayo wakati wa uhitimishaji wa Maonesho ya  pili  ya bidhaa za viwanda vya ndani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam, amesema kuna idadi kubwa ya viwanda vimeanzishwa nchini, hivyo jukumu lililopo ni kuvisimamia ili viendelee kuwepo.

"Ni wakati muafaka sasa wa kusimamia viwanda vilivyopo nchini vifo vya viwanda vikomeshwe na hii itatoka na ufuatiliaji na usimamizi wa karibu,"anasema.

Mhandisi Manyanya amesema mfumo wa kufuatilia viwanda unawezekana kwani kuna maofisa biashara na wataalamu wengi,hivyo watakuwa na jukumu la kuvisimamia katika  maendeleo yake.

"Kwa lugha rahisi niseme hivi tuwe na zahanati za viwanda kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya ukuaji wa viwanda vyetu,"amesema.

Pia ameonya tabia ya baadhi ya wamiliki wa viwanda kuwa  wadanganyifu kwa Wizara na watakaobainika watachukuliwa hatua.
"Tunazo taarifa kuna wamiliki wa viwanda waliouziwa viwanda na Serikali, wanachokifanya hawazalishi bidhaa na badala yake wanunua kutoka viwanda vya nje na kujifanya wanazalisha hapa nchini,"amesema.
 Naibu Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mhandisi  Stella Manyanya akizungumza katika uhitimishaji wa maonesho ya pili ya bidhaa za viwanda vya ndani katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau wenye viwanda na kampuni mbalimbali walioshiriki maonesho ya pili ya bidhaa za viwanda vya ndani katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live


Latest Images