Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT) MKOANI DODOMA

0
0





 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wanachama wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kabla ya kufungua mkutano huo  Mkuu wa (CWT )katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma. Wanachama hao wa CWT walisimama na kushangilia  mara baada ya ahadi ya Rais Dkt. Magufuli kuwaahidi kuendelea kutatua kero zao mbalimbali.
 Mamia ya Wajumbe wa Chama cha Walimu(CWT) wakishangilia ndani ya ukumbi wa Chimwaga wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akijibu kero zao mbalimbali walizoziwasilisha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya wajumbe wa Chama cha Walimu CWT mara baada ya kuwahutubia katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na viongozi wa muda wa  CWT, Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako, Spika wa Bunge Job Ndugai, pamoja na mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakiimba wimbo wa mshikamano pamoja na Wajumbe wote wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wakiwa wameshikana mikono wakati wakiimba wimbo wa mshikamano kabla ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhutubia na kufungua mkutano huo wa CWT katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wajumbe wa CWT katika ukumbi wa Chimwaga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza viongozi wa muda wa Chama cha Walimu Tanzania walipokuwa wakiwasilisha hoja zao mbalimbali zinazo wakabili walimu nchini katika mkutano mkuu wa CWT uliofanyika katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma. PICHA NA IKULU 

DIWANI MTARAWANJE AAPA KUWATUMIKIA WANANCHI WA KIJICHI

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii
DIWANI wa Kijichi, Eliasa  Mtarawanje amesema kuwa kazi kubwa ni kuwatumikia wananchi  wa kijichi bila kujali itikadi za vyama.

Mtarawanje ameyasema hayo mara baada ya kuapishwa udiwani wake katika Baraza la Madiwani la Manispaa ya Temeke, amesema  uchaguzi umeisha Novemba 26 kilichobaki ni kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi wa kijiji.

Mtarawanje amesema kuwa Kijichi kuna miradi ya mingi kilichobaki ni kusimamia ili kuweza wananchi kupata huduma bora zinazotokana na miradi hiyo.

“Mimi kama kiongozi nimeamua kuwatumikia wananchi wangu wa kijichi hivyo nilazima nitumike katika kuwasaidia wananchi wenzangu kwa kuniamini kutoa kura zao na kuweza kupata ushindi” amesema Mtarawanje.

Amesema katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano ni kufanya kazi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na si vinginevyo .
 Diwani  wa Kijichi, Eliasa  Mtarawanje akilakiapo cha udiwani katika baraza la madiwani la Manispaa ya Teemeke leo jijini Dar es Salaam.
 Diwani  wa Kijichi, Eliasa  Mtarawanje akizungumza katika baraza hilo mara baada ya kuapishwa leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke, Alimishi Hazali akizungumza juu ya ushindi wa diwani Diwani wa Kijichi, Eliasa  Mtarawanje katika baraza la madiwani la Manispaa ya Teemeke leo jijini Dar es Salaam.
 Diwani  wa Kijichi, Eliasa  Mtarawanje akiwa katika picha ya pamoja na madiwani wenzake mara baada ya kuapishwa leo jijini Dar es Salaam .
Diwani  wa Kijichi, Eliasa  Mtarawanje akiwa katika picha ya pamoja na vongozi wa CCM mara baada ya kuapishwa leo jijini Dar es Salaam .

washindi 12 droo ya pili Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya NBC wapatikana

0
0
 Maofisa wa NBC wakiendesha droo ya pili ya Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Humudi Semvua kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Meneja Masoko wa NBC, Alina  Kimaryo, Meneja Amana za Wateja, Dorothea Mabonye na Meneja Maendeleo ya Biashara wa NBC, Amos lyimo. Jumla ya washindi 12 wakijishindiaa kila mmoja shs milioni 1.
 Meneja Masoko wa NBC, Alina Kimaryo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uchezeshaji wa droo ya pili ya Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana ambapo washindi 12 walijishindia kila mmoja shs milioni 1. Katikati ni Meneja Amana za Wateja wa NBC, Dorothea Mabonye na Meneja Maendeleo ya Biashara wa NBC, Amos Lyimo.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa NBC, Amos Lyimo (kulia) akipiga simu kwa mmoja wa washindi  wakati wa droo ya pili ya Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humudi Semvua, Meneja Masoko wa NBC, Alina Kimaryo na Meneja wa Amana za Wateja, Dorothea Mabonye. Washindi 12 walijishindia shs milioni 1 kila mmoja.

Taasisi ya Tanzania Mortage Refinance Company (TMRC) Yachangia Shilingi Milioni Nane kwa ajili ya matibabu Ya Moyo Kwa Watoto Wanne Wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

0
0
Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya kifedha ya Tanzania Mortage Refinance Company (TMRC) imekabidhi msaada wa shilingi milioni nane kwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuwezesha matibabu ya moyo kwa watoto wanne.

Watoto hao watafanyiwa upasuaji wa moyo wa kuziba matundu na wengine kutibiwa mishipa ya damu ambayo haipitishi damu vizuri katika moyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi wa TMRC Oscar Mgaya alisema wameguswa kuchangia fedha hizo ili kuokoa maisha ya watoto hao wenye matatzo ya moyo ambao ni Taifa la kesho.

“Tumetoa shilingi millioni nane kwa ajili ya upasuaji wa kutibu magonjwa ya moyo kwa watoto wanne, tumeguswa kutoa fedha hizi ikizingatiwa watoto wengi ni wadogo hawajafikisha hata miaka mitano na watalaam wanaeleza ikiwa hawatapatiwa matibabu hasa ya upasuaji kwa wakati muafaka wataweza kupoteza maisha”,.

“Moyo ni kiungo cha muhimu sana katika mwili wa binadamu, unaweza kukosa mguu au mkono ukaishi lakini siyo moyo, binadamu akikosa moyo hawezi kuishi”, alisema.Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi aliishukuru Taasisi ya TMRC kwa kutoa fedha hizo ambazo zitaokoa maisha ya watoto wanne wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo.

Prof. Janabi alitoa rai kwa Taasisi zingine kuiga mfano na kuendelea kujitokeza kufadhili matibabu ya watoto ambao bado wanasubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taaasisi ya Moyo Jakaya Kikwete(JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Mkurugenzi wa Taasisi ya kifedha ya Tanzania Mortage Refinance Company(TMRC) Oscar Mgaya wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wenye matatizo ya Moyo na wazazi wao wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya mfano wa hundi ya shilingi milioni nane ambayo wamezitoa kwa ajili ya matibabu ya watoto hao.
Mkurugenzi wa Taasisi ya kifedha ya Tanzania Mortage Refinance Company(TMRC) Oscar Mgaya akiwakabidhi wazazi wa watoto wenye matatizo ya Moyo mfano wa hundi ya shilingi milioni nane ambazo zimetolea na Taasisi hiyo kwa ajili ya matibabu ya watoto wanne.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taaasisi ya Moyo Jakaya Kikwete(JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Mkurugenzi wa Taasisi ya kifedha ya Tanzania Mortage Refinance (TMRC) Oscar Mgaya wakizungumza baada ya kumaliza makabidhiano ya hundi ya shilingi million nane kwa ajili ya kuwezesha matibabu ya moyo kwa watoto wanne .Picha na JKCI

MWANASHERIA WA GGM MBARONI KWA KUMNYIMA NYARAKA NAIBU WAZIRI

0
0

Na Joel Maduka,Geita

Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo amekamatwa na serikali baada ya kudaiwa kukutwa na nyaraka za serikali .

Mwanasheria huyo amekamatwa kwa amri ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola alipotembelea Mgodi huo ambapo pamoja na mambo mengine amebaini mgodi huo kuwa unaendesha shughuli zake bila kufuata sheria ya mazingira .

Akiwa katika katika ziara ya kikazi ya siku mbili Wilayani Geita,Mhe.Kangi Lugola ameagiza kukamatwa kwa mwanasheria huyo baada ya kudaiwa kukutwa na nyaraka za serikali ambazo hazijawa rasmi kutumika kutoka taasisi ya wakala wa utafiti wa jiolojia Tanzania(GST).

Hata hivyo katika hali isiyo ya kawaida na bila kutarajiwa.Mwanasheria huyo aliyekuwa akiukingia kifua mgodi huo ili usikumbane na rungu la fidia ya uharibifu wa kimazingira kama sheria inavyotamka, alijikuta akimweleza Naibu Waziri kuwa anayo ripoti ya GST aliyodai haijaeleza iwapo mgodi huo unahusika moja kwa moja kwenye uharibifu hivyo mgodi huo usibebeshwe mzigo huo.

Kutokana na hali hiyo,Naibu Waziri Lugola aliomba apatiwe ripoti hiyo ili ajiridhishe,lakini mwanasheria huyo akijibu kwa kujiamnini alimtaka kiongozi huyo wa juu kutumia mbinu zake kuipata Serikalini, lakini yeye hawezi kutoa nyaraka ya serikali, jambo lililomkasirisha Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira na kutoa agizo la kukamatwa mara moja.

Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) David Nzarigo akipandishwa kwenye gari ya Polisi Baada ya agizo la Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola akipokea taarifa ya shughuli zinazofanywa na Mgodi huo. 
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akitazama baadhi ya nyaraka wakati ambapo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola. 
Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo akipelekwa kwenye gari la polisi na askali baada ya agizo la Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola. 


TIA YAJENGEA UWEZO WAHADHIRI WAKE KUFANYA TAFITI KUANDAA MACHAPISHO

Walimu Wapongeza Uamuzi wa Rais Dkt Magufuli Kuhusu Ulipaji wa Madeni.

MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SIRRO AKIWA ZIARANI KUTOKEA KIGOMA KWENDA KATAVI, AWAPA POLE WANANCHI WALIOPATA AJALI PINDI AKIWA SAFARINI

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro akikagua ajali iliyotokea kati ya roli aina ya fuso na basi la kampuni ya Adventure lenye no T 186 AKX, iliyokuwa ikitokea mkoani katavi kwenda mkoa wa Kigoma, ajali hiyo imetokea eneo la Mishamo barabara ya Kigoma – Mpanda mkoani Katavi wakati akitokea mkoa wa Kigoma alipokuwa na ziara ya kikazi siku mbili.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro wa kwanza mkono wa kulia akiangalia ajali iliyotokea kati ya roli aina ya fuso na basi la kampuni ya Adventure lenye no T 186 AKX iliyokuwa ikitokea mkoani katavi kwenda Mkoa wa Kigoma, ajali hiyo imetokea eneo la Mishamo barabara ya Kigoma – Mpanda mkoani Katavi wakati akitokea mkoa wa Kigoma alipokuwa na ziara ya kikazi siku mbili.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro, alievaa nguo ya kijani akishilikiana na wananchi kupata ufumbuzi wa magari yaliokuwa yamepata ajali kati ya roli aina ya fuso na basi la kampuni ya Adventure lenye no T 186 AKX iliyokuwa ikitokea mkoani katavi kwenda mkoa wa Kigoma, ajali hiyo imetokea eneo la Mishamo barabara ya Kigoma – Mpanda mkoani Katavi wakati akitokea mkoa wa Kigoma alipokuwa na ziara ya kikazi siku mbili.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro, akipokelewa na maafisa wa Jeshi la Polisi mkoani katavi baada ya kuwasili mkoani humo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro akiagana na wananchi waliokuwa wamepa ajali baada ya kuhakikisha ufumbuzi wao wa kuondoka umepatikana, ajali hiyo iliyotokea kati ya roli aina ya fuso na basi la kampuni ya Adventure lenye no T 186 AKX iliyokuwa ikitokea mkoani katavi kwenda mkoa wa Kigoma, ajali hiyo imetokea eneo la Mishamo barabara ya Kigoma – Mpanda mkoani Katavi wakati akitokea mkoa wa Kigoma alipokuwa na ziara ya kikazi siku mbili.Picha Na Jeshi La Polisi

VIONGOZI MLIOCHAGULIWA WATUMIKIENI WANACHAMA WOTE KWA UADILIFU -KINANA

0
0
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimewataka viongozi wake wote waliochaguliwa hivi karibuni katika ngazi mbalimbali kuhakikisha wanawatumikia wanachama na wasio wanachama kwa uadilifu na uzalendo ili kuendelea kukijengea imani Chama hicho kwa watu wote. 

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Nzega na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati anakabidhi vitendea kazi (pikipiki 19) kwa viongozi na watendaji wa Chama hicho katika Jimbo la Nzega vijijini vilivyotolewa na Mbunge wao na kuweka jiwe la Msingi kwenye Kitega Uchumi CCM wilaya ya Nzega.
Alisema kuwa uchaguzi umekwisha kilichobaki ni kwa viongozi wapya walichaguliwa kuwatumikia wanachama wote waliowachagua na ambao hawakuwachagua ili kuendelea kukiimarisha Chama chao. 

Kinana alisema kuwa uchaguzi umekwisha kinachofuata ni kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2015 hadi 2020, ahadi za Mgombe wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizitoa wakati akiomba kura na zile zilizotolewa na Wabunge ambazo hakuwa katika Ilani. Alisema kuwa ni muhimu kwa MwanaCCM na watumishi wa umma na wananchi wengine kuhakikisha wanatekeleza Ilani ya Chama hicho ambacho kiko madarakani. 

Aidha Kinana aliwataka viongozi na watendaji waliopatiwa vifaa hivyo kuvitumia kwa ajili ya shughuli za kukiimarisha zaidi Chama na sio kwa ajili ya mambo mengi ambayo sio malengo yake. 

Naye Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala alisema kuwa uchanguzi umekwisha ni vema wakawa wamoja kwa ajili ya kuendelea kujenga Chama chao. 

Alisema kuwa ataendelea kushirikiana na wanachama wote walioshinda na walioshindwa kwa ajili ya kuimarisha mshikamano ndani ya CCM na kwa ajili kuendelea kukipa matokeo mazuri katika chaguzi mbalimbali zijazo. 
Dkt. Kigwangala alisema kuwa pikipiki 19 ni za CCM na sio ya watu waliokabidhiwa na hivyo viongozi na watendaji wa Chama waliopata wanatakiwa kuzitumia katika kuimarisha Chama hicho kwenye maeneo yao ya kazi. Alisema kuwa Jimbo la Nzega Vijiji ni kubwa kwa hiyo usafiri huo utawasaidia kuwafikia wanachama na watu wengi na hivyo kukijenga Chama hicho.

TAMKO LA JUMUIA YA WAZAZI YA CCM KUTENGUA MATOKEO YA UJUMBE WA NEC KUTOKA WAZAZI - BARA

0
0
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Dkt. Edmund Bernard Mndolwa ametengua ushindi wa Ndg. Ngingite Nassoro Mohamed ambaye alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kupitia Jumuiya ya Wazazi (Bara) baada ya kubaini uwepo wa kasoro kubwa katika uhesabuji wa kura wakati wa uchaguzi.

Kufuatia uamuzi huo Dkt. Edmund Mohamed Mndolwa amemtangaza Ndg. Kitwala Erick Komanya kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kupitia Jumuiya ya Wazazi (Bara) .
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Edmund Benard Mndolwa akizungumzia kuhusu kutengua ushindi wa mjumbe mmoja aliyechaguliwa kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi kwa upande wa Tanzania bara.  

WAKIMBIZI WAIOMBA SERIKALI YA TANZANIA KUWAFUNGULIA SOKO LA BIDHAA ZAO

0
0
Mtaalamu wa Masuala ya Ukatili wa Kijinsia na Ustawi wa Jamii kutoka Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Ofisi ndogo ya Kibondo akizungumza na Wanawake wakimbizi wa Kambi ya Mtendeli iliyopo katika Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, juu ya Biashara ya ufumaji wa bidhaa kwa wanawake hao waishio ndani ya kambi hiyo na kupatiwa ujuzi wa kuweza kujiongezea kipato.
Muwezeshaji wa Wanawake wa kutoka Shirika la IRC linalofadhiliwa na UNHCR,Beatrice Emmanuel akitoa maelezo namna kikundi cha wanawake wafumaji wanavyoweza kujiongezea kipato katika familia zao kwa kutengeneza na kuuza bidhaa zao katika soko la pamoja linalojumuisha wakimbizi na Watanzania wanaoishi katika vijiji vya jirani na eneo la kambi ya wakimbizi ya Mtendeli. Pia wageni mbalimbali wanaowatembelea eneo la kambi kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali ikiwemo wahisani na wadau mbalimbali. lengo la mradi huu wa ufumaji ni kuwawezesha wanawake kupata ujuzi utaowawezesha kujiongezea kipato ili pindi watakaporejea  nchini mwao kila mwanamke aweze kuwa na shughuli inayoweza kumuingizia kipato
 Afisa Uzalishaji kutoka IRC, Foibe Julius, akitoa maelekezo ya namna ya kusuka vikapu  kwa mmoja wa Mwanamke Mkimbizi anayeishi katika kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli iliyopo katika Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma 
Msaidizi Mkuu wa Makazi katika kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli- Lulu Malima akiangalia moja ya Bidhaa zilizofumwa na Wanawake wakimbizi wa kambi hiyo ambao wameweza kuuza na kujiongezea kipato ili kuweza kujikimu katika maisha yao.
Wanawake wanaoishi katika kambi ya Wakaimbizi ya Mtendeli ya Wilaya ya Kakonko mkoa wa Kigoma wakipanga bidhaa zao katika hali ya usafi ili kuwawezesha wanunuzikuziona kwa urahisi katika eneo lao na kununua.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU AONGOZA KUAGA MIILI YA ASKARI 14 WA JWTZ WALIOUAWA WAKIWA KWENYE OPERESHENI YA ULINZI WA AMANI CHINI YA UMOJA WA MATAIFA NCHINI DRC

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa askari 14 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  (JWTZ) waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC, kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JWTZ, Upanga jijini Dar es salaam akimwakilisha Rais John Pombe Magufuli, Desemba 14, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017  alikomwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini, Jenerali Venance Mabeyo baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,. Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo  baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete  baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Susan Kolimba baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC. Katikati ni Rais Mstaafu wa Awamu wa Nne, Jakaya Mrisho Kikwete na kushoto Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika - SADC.  
 Askari wa Jeshi  la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba miili ya askari 14 wa JWTZ waliouwa wakiwa kwenye operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo -  DRC,`kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JWTZ Upanga jijini Dar es salaam  Desemba 14, 2017.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari hao.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wafiwa baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC. 

Dk Mwakyembe ateta na Wadhibiti wa Maudhui ya Luninga

0
0
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ameagiza taasisi zote zinazohusika na udhibiti wa maudhui ya luninga nchini kubuni mkakati wa pamoja wa kuboresha udhibiti.

Dk Mwakyembe ametoa rai hiyo baada ya kuzikutanisha taasisi hizo za udhibiti leo jijini Dar Es Salaam.

"Nyinyi nyote ni taasisi za Serikali, hivyo tengenezeni mkakati wa kufanya kazi kwa pamoja kudhibiti maudhui mabovu ili kulinda  maadili ya jamii yetu," alisema.Waziri Mwakyembe alifanya mkutano wa pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)."Kuna hitaji za kuongeza uwezo wa kufuatilia maudhui ya luninga ikiwa ni pamoja na filamu zote ili kubaini maudhui hasi kwa jamii yetu na kuzishughulikia ipasavyo kabla hazijaleta madhara kwa jamii," alisema.

Alisema changamoto za ongezeko la mahitaji ya jamii zinazidi kukua kwa haraka kutokana na kasi ya maendeleo hivyo ni vizuri kuhakikisha  kuwa majawabu yake yanapatikana.Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi Susan Mlawi, alisema Wizara itaangalia jinsi ya kuunganisha majukumu ya taasisi zinazosimamia maudhui ya vyombo vya utangazaji nchini ili kuimarisha udhibiti wa pamoja. 

Akiongea katika mkutano wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dodoma mapema wiki hii, Rais John Pombe Magufuli aliiagiza Wizara ya Habari na TCRA kutosita kuvichukulia hatua vyombo vya utangazaji zinavyokiuka kanuni za utangazaji nchini.
 Dk Mwakyembe akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA,Bi.Valerie Msoka,
 Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi Suzan Mlawi, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Eng James Kilaba na Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Chief Fredrick Ntobi.

MKUU WA WILAYA YA KONGWA AENDELEA NA ZIARA YA KIJIJI KWA KIJIJI KUSIKILIZA NA KUZITAFUTIA UFUMBUZI KERO ZA WANANCHI

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deo Ndejembi, leo ameendelea na ziara katika kata ya Hogoro na vijiji vyote vitano vya Kata hiyo ambavyo ni Mkutani, Banyibanyi, Nyerere, Hogoro na Chamae. Hogoro ni kata ya 11 kati ya kata 22. 

Mpaka sasa DC Ndejembi amefanya ziara katika vijiji 44 kati ya 87 na Kata 11 kati ya 22. Lengo la ziara hii ni muendelezo wa kampeni yake ya Ondoa Njaa Kongwa( ONJAKO) iliyozinduliwa msimu huu wa Kilimo inayohimiza kilimo cha Mtama na Uwele ili kuhakikisha kuna usalama wa chakula wilayani. 

Vile vile akiwa katika vijiji hivyo DC Ndejembi husikiliza kero mbali mbali za wananchi na kutoa maagizo na maelekezo yenye kulenga kutatua kero hizo.Katika majukumu yake DC Ndejembi alikwisha tembelea kata zote 22, ila kwa sasa atatembelea Vijiji vyote 87 katika Wilaya ya Kongwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deo Ndejembi, leo akizungumza na baadhi ya wananchi wa kata ya Hogoro,wilayani humo.Mh Deo ameendelea na ziara yake katika kata ya Hogoro na vijiji vyote vitano vya Kata hiyo ambavyo ni Mkutani, Banyibanyi, Nyerere, Hogoro na Chamae. Hogoro ni kata ya 11 kati ya kata 22.
Baadhi ya wananchi wakimsikilia Mkuu wa wilaya ya Kongwa,Mh Deo alipofanya ziara katika kata ya Hogoro na vijiji vyote vitano vya Kata hiyo ambavyo ni Mkutani, Banyibanyi, Nyerere, Hogoro na Chamae. Hogoro ni kata ya 11 kati ya kata 22. 


JAFO ASHTUKIA MAKUSANYO YA HOSPITALI MISUNGWI

0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo ametilia shaka makusanyo katika hospitali ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza na kuagiza kusimamiwa vyema ukusanyaji mapato.

Jafo ameyasema hayo katika ziara yake ya kikazi ndani ya Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo alisema amegundua kuna kila dalili kwamba mapato ya hospitali hiyo yanavuja kutokana na taarifa nyingi za fedha za Malipo ya wagonjwa kutoingizwa kwenye mfumo wa kielekroniki hivyo kusababisha kukusanya wastani wa Sh.milioni 4 kwa mwezi. 

Katika ziara hiyo, Jafo amezungumza na watumishi wa Halmashauri ya Misungwi ambapo amewasisitiza watumishi na viongozi kuwa na mahusiano mema ili waweze kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya hiyo.Jafo amesisitiza kwamba kila mmoja anapasa kumthamini mwenzake na kushirikiana katika kazi ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha Jafo amewapongeza walimu wa shule ya sekondari Misasi kwa kufanya vyema sana kwani wamefanikiwa kupeleka watoto 45 kidato cha tano kati ya wanafunzi 100 waliomaliza kudato cha nne mwaka jana.

Baada ya ziara hiyo waziri Jafo ameendelea na ziara yake wilayani sengerema mkoani Mwanza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua hospitali ya wilaya ya Misungwi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata taarifa ya miradi ya elimu kutoka kwa viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa maabara katika sekondari ya Misasi.

TIA yahamasisha wahadhiri kuandaa tafiti na machapisho

0
0

Na Said Mwishehe wa Globu ya Jamii
TAASISI ya Uhasibu Tanzania(TIA) imesema kuwa kuna umuhimu wa wahadhiri  kufanya tafiti na machapisho mbalimbali kwa ajili ya kufundishia wanafunzi wao.

Kufanya utafiti huo na kuweka katika machapisho yatasaidia walimu kutoa taaluma ya uhasibu na biashara inayokwenda na wakati.

Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo na Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Dk.Joseph Kahanda wakati anaelezea mikakati yao ni  kuandaa na kuwajenga  wahadhiri kitaaluma  katika kuwaanda wahitimu katika soko la ajira.

“Tumeamua kufanya kongamano ambalo lengo lake ni kujadiliana na walimu wetu na hasa kuwajengea uwezo wa kufanya tafiti na machapisho kwa ajili ya kusaidia  katika majukumu yao ya kupima wataalamu kwenye fani zinazotolewa chuoni kwetu.

“Walimu wasipofanya tafiti na kutoa machapisho kuna uwezekano wa kuendelea kutumia tafiti na machapisho yaliyopitwa na wakati.

“Hivyo tunahimiza walimu wetu kufanya tafiti zitakwenda na wakati na kutowaacha nyuma kitaaluma wanaowafundisha,”amesema Dk.Kihanda.

 Pia amesema wanafunzi wanasoma kwenye taasisi hiyo wamekuwa na soko kubwa la ajira pindi wanapohitimu.

Amesema kuwa kuna mashirika na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikiomba wanafunzi wanapohitimu kuwapatia ajira na hivyo kimefanya kuwa kimbilio la wengi.

Kuhusu mahafali ya 15 ya taasisi hiyo yanayofanyika leo, amesema kwa  Dar es Salaam  wahitimu 3,833 wanatunikiwa vyeti.

Amefafanua mahafali mengine ya taasisi hiyo yatafanyika pia katika tawi lao la mkoani Mtwara.Hivyo jumla ya wahitimu wote wa Dar es Salaam na Mbeya ni zaidi ya 5,840.

RAIS WA MSUMBIJI FILIPE NYUSI AWASILI MKOANI DODOMA NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mjini Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi wakipita kwenye gadi ya Heshima iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi mara baada ya Rais huyo wa Msumbiji kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi wakati wakiangalia vikundi vya ngoma za utamaduni mara baada ya Rais huyo wa Msumbiji kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mjini Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mgeni wake Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi wakati vikundi vya ngoma vilipokuwa vikitumbuiza katika uwanja wa ndege wa Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi katika Ikulu ya Dodoma kabla ya kuanza mazungumzo yao. PICHA NA IKULU

KIPINDI CHA BBCDIRA YA DUNIA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AAGIZA BENKI ZISIZOKIDHI VIGEZO ZIFUTIWE LESENI

0
0

Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa, ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania BOT kuzifutia leseni benki zote za biashara pamoja na benki za wananchi zitakazoshindwa kukidhi vigezo vya kuendesha shughuli za kibenki nchini.

Ametoa agizo hilo mjini Dodoma katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, wakati akifungua Mkutano Maalum wa Wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi Tanzania (COBAT).

“kwa taarifa niliyonayo hadi sasa baadhi ya benki hazijatimiza matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji wa kutosha, hali ambayo haiwezi kuachwa iendelea hata kidogo, kwani haiimarishi sekta ya fedha na haiwasaidii wananchi kuendelea kiuchumi” alisema Waziri Kassim Majaliwa katika hotuba hiyo.Alisema Benki Kuu ilitoa muda hadi mwishoni mwa Desemba 2017, benki za wananchi ziweze kuongeza mtaji na kwamba muda huo hautaongezwa na wala Serikali haitatoa mtaji kwa benki hizo.

“Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania haitasita kuifungia benki yoyote na kufuta leseni yake ya biashara pindi itakapobaini inavunja sheria, ikiwa ni pamoja na kuwa na upungufu mkubwa wa mtaji na ukwasi ambao unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na amana za wateja kama tulivyofanya kwa Mbinga Community Bank PLC kuanzia tarehe 12/5/2017” alisema Dkt. Mpango kwa niaba ya Waziri Mkuu.

Maagizo hayo yamekuja siku moja baada ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kuiagiza Wizara ya Fedha na Mipango wakati akifungua tawi kuu la Benki ya CRDB mjini Dodoma, kuhakikisha kuwa Benki Kuu ya Tanzania-BOT, inazifuta benki zote zinazoshindwa kujiendesha kibiashara hata kama zinamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akihutubia katika mkutano maalum wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi-COBAT, uliofanyika mjini Dodoma ili kujadili masuala ya Mitaji na Mpango wa Kuziunganisha Benki za Wananchi Tanzania.
Washiriki wa mkutano maalum wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mkutano huo uliofunguliwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Mjini Dodoma.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Benard Kibesse (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Benki za Wananchi –COBAT, Bw. Rukwaro Senkoro, wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), mijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akifurahia jambo na Mbunge wa Mtwara Vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia baada ya kufungua mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi-COBAT, uliofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioshiriki mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi-COBAT, nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.

Wasanii watakiwa kutengeneza kazi nzuri zitakazovutia Wadhamini.

0
0
Na Shamimu Nyaki – WHUSM.

Serikali imewataka wasanii kutengeneza kazi nzuri zenye ubora zinazozingatia maadili ya Kitanzania ili kuwavutia wawekezaji wengi wanaotaka kudhamini kazi hizo katika kuziandaa na kuzisambaza.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati akizindua Mfumo wa MaxBurudani ulioandaliwa na Kampuni ya MaxMalipo ambapo ameishukuru Kampuni hiyo kwa kuamua kuchukua dhamana ya kusambaza kazi za wasanii ili kuondoa kero ya muda mrefu ya wizi wa kazi za wasanii hao kupitia njia mbalimbali walizokuwa wanatumia wasanii hao ambazo zilikua zikiwalipa kiasi kidogo.

“Nimefurahishwa sana na Mfumo huu namna ambavyo utaweza kutatua changamoto ya wizi wa kazi za wasanii wetu kwa vile umeonyesha wazi namna ambavyo msanii anaweza kunufaika na kazi yake kuanzia idadi ya kazi zake zilizoenda sokoni,asilimia anazopata kwa kazi yake ambayo ni kuanzia 40-50 pamoja na kumuwezesha kutouza Haki Miliki yake kama walivyokuwa wanafanya hapo awali.”Alisema Mhe.Mwakyembe.

Aidha amewataka Wasanii kutengeneza kazi zenye ubora ambazo zitakidhi vigezo vyinavyotakiwa na Kampuni hiyo ambapo pia ameiagiza Kampuni hiyo kutochukua kazi yeyote ambayo itakuwa haina ubora wala kuwa na maadili.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikata utepe leo Jijini Dar es Salaam kuashiria uzinduzi wa Mfumo wa MaxBurudani ulioandaliwa na Kampuni ya MaxMalipo wenye lengo la kusambaza kazi za wasanii.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) pamoja na viongozi wa Kampuni ya MaxMalipo wakionyesha baadhi ya kazi za wasanii zitakazosambazwa na Kampuni hiyo kupitia mfumo wa MaxBurudani leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mfumo huo.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Wasanii (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa MaxBurudani ulioandaliwa na Kampuni ya MaxMalipo wenye lengo la kusambaza kazi za wasanii.

Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images