Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA SPIKA WA BUNGE LA MOROCCO MJINI DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimkaribisha Spika wa Bunge la Morocco, Mheshimiwa Habib El Malk (kushoto) nyumbani kwake mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa mazungumzo yenye lengo ya kudumisha urafiki baina ya nchi mbili.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akifurahi jambo na Spika wa Bunge la Morocco, Mheshimiwa Habib El Malk (kulia) nyumbani kwake mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akiteta jambo na Spika wa Bunge la Morocco, Mheshimiwa Habib El Malk(kushoto) nyumbani kwake mjini Dodoma ikiwa ni baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru wa Tanzania Bara.

Chuo Kikuu cha SAUT na matawi yake chatoa wahimu 8687

$
0
0
Dkt. Darius Mkiza akitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika fani ya Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Tanzania (SAUT) na Askofu Flaviani Matindi Kassala wa Jimbo Katoliki la Geita kwa niaba ya Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Tercius Ngalekumtwa ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa mwishoni mwa wiki Jijini Mwanza.
Dkt. Judith Adongo Aloo akitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika fani ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Tanzania (SAUT)na Askofu Flaviani Matindi Kassala wa Jimbo Katoliki la Geita kwa niaba ya Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Tercius Ngalekumtwa ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa mwishoni mwa wiki Jijini Mwanza.
Wahitimu wa Shahada ya Uzamivu (PhD) Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Tanzania (SAUT) (mstari wa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo mara baada ya kutunukiwa shahada zao mwishoni mwa wiki Jijini Mwanza. Wa kwanza kulia ni Dkt. Darius Mkiza, wa pili kulia ni Jacob Roman Lubuva, wa kwanza kushoto ni Neema Bhoke Mwita na Judith Adongo Aloo (wa pili kushoto). (Picha na Martin Nyoni, SAUT, Mwanza)

Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Tanzania (SAUT) pamoja na Vyuo Vikuu vyake Vishiriki kimetoa jumla ya wahitimu 8,687 kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kwa kutekeleza azma ya Serikali ya kuandaa wataalamu mbalimbali nchini. Uongozi wa Chuo hicho umeishukuru Serikali kwa kuishirikisha sekta binafsi katika kutoa mchango wao katika sekta ya elimu na umeihakikishia Serikali kuwa kanisa Katoliki litaendelea kuwa mdau muhimu kwa taifa katika kutoa huduma za jamii nchini.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Askofu Mkuu Yuda Thaddeus Ruwa’ichi wa Jimbo kuu la Mwanza, ambaye pia alikuwa Mgeni Rasmi katika mahali ya 19 ya chuo hicho ambapo wahitimu hao wametunukiwa Astashahada, Stashahada na Shahada ya kwanza, shahada ya uzamili pamoja shahada ya uzamivu. Askofu Ruwa’ichi amewataka wahitimu hao wawe wabunifu hatua itakayowawezesha kujiajiri na kuwaajiri watu wengine kwa kuitambua na kuitumia vema fursa ya uwepo wa tecknolojia pamoja na fursa nyingine zilizopo katika mazingira na jamii wanapoishi wakizingatia maadili ya taaluma zao pamoja na maadili ya jamii ili waweze kujiletea maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla.

“Tambueni na onesheni thamani yenu katika jamii kwa elimu mliyoipata hapa SAUT, jamii inatarajia kutumia ujuzi wenu ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili” alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi. Kati ya wahitimu hao, chuo kikuu cha SAUT Mwanza na kituo cha Dar es salaam kimetoa jumla ya wahitimu 2147 ambapo asilimia 55 ni wanaume na asilimia 45 ni wanawake kutoka fani mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo. Fani hizo ni Uandishi wa habari, Mahusiano ya Umma, Mahusiano ya Jamii na Masoko, sosholojia, Falsafa ya Elimu, Uhasibu, Utawala wa Afya, Uchumi, Ugavi, Sheria, Isimu ya Lugha Utawala na Biashara.

Fani nyingine ni, Historia, Utawala wa Elimu na Mipango Usimamaizi wa Maendeleo ya Elimu ya Juu, Uhandisi wa Ujenzi, Sayansi ya Kompyuta, Uhandisi wa umeme, Elimu ya Shule ya Msingi pamoja na Sanaa na Elimu. Miongoni mwa watimu hao wapo wahitimu wane katika ngazi ya shahada ya Uzamivu (PhD) akiwemo Darius D. Mkiza na Jacob Roman Lubuva katika fani ya Mawasiliano ya Umma pamoja na Judith Adongo Aloo na Neema Bhoke Mwita katika fani ya Sheria. Akinukuu maneno ya Rais wa zamani wa Marekani John Kennedy aliyowahi kusema “Usijiulize taifa litakufanyia nini wewe, bali jiulize wewe utalifanyia nini taifa lako”, Askofu Mkuu Ruwa’ichi aliwahimiza wahitimu hao wawe wabunifu ili waweze kuonesha tofauti katika jamii kwa kufanya maamuzi sahihi wakati wa kutekeleza majukumu yao na kuwa mabalozi wazuri wa chuo hicho.

Zaidi ya hayo, Askofu Mkuu Ruwa’ichi amewataka wahitimu hao kuwa wakweli daima wakati wa kutekeleza majukumu yao huku akiwahimiza waichukie rushwa, wasitoe wala kupokea rushwa bali wafanye kazi kwa juhudi na maarifa wakimtegemea Mungu daima. Aidha, Askofu Mkuu Ruwa’ichi amesisitiza kuwa chuo cha SAUT kimekuwa mdau muhimu kwa Serikali ya Tanzania kwa kutoa mchango uliotukuka kwa taifa kwa kuzingatia Sera ya Elimu ya Mwaka 2014 ambayo ilifanyiwa maboresho ktoka Sera ya Elimu ya mwaka 1995.

Lengo la sera hiyo ni kuiwezesha nchi kupata watanzania walioelimika ili waweze kuingia katika mazingira ya ushindani ili wanaweze kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa viwanda na wa kati ifikapo mwaka 2025 kulingana na Dira ya Maendeleo ya taifa. Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo hicho Padre Dkt. Thadeus Mukama amesema kuwa SAUT imetoa mchango mkubwa taifa katika fani wanazotoa wakiongozwa na fani kongwe ya uandishi wa habari inayotolewa chuoni hapo tangu kuanzishwa kwake.

Dkt. amewataja baadhi ya watumishi mbalimbali waliosoma chuoni hapo na kushika nafasi mbalimbali katika taifa na maeneo mbalimbali duniani wakiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas, Emmanuel Buhohela, na Jackson Msangulla ambao wanafanyakazi Ofisi ya Rais katika Kurugenzi ya Mawasiliano.

Dkt. Mukama aliendelea kuwataja watumishi wengine waliosoma SAUT kuwa ni pamoja na Deodatus Balile mwandishi wa habari wa gazeti la Jamhuri, Hoyece Temu anayefanyakazi katika Ofisi za Umoja wa Mtaifa, Tanzania, Zawadi Machibya na Sami Awami, Ester Namhisa, Liisy Masinga ambao wanafanyakazi ya uandishi wa habari katika Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC, Raymondi Nyamwihula anafanyakazi Azam Media, Dotto Bulendu anafanyakazi Radio SAUT, Jonas Songora anayefanyakazi radio Japan pamoja na Maafisa Habari na Mahusiano wengi wanaofanyakazi Serikalini katika Wizara, taasisi, mikoa, majiji na halamashauri na mbalimbali zisizo za kiserikali ndani na nje ya nchi.

Aidha, katika mwaka huu wa masomo wa w 2017/2017 Dkt.Mukama amesema kuwa chuo hicho kimedahili wanachuo pamoja na matawi yake kimedahili wanachuo wapatao 20600 ambapo lengo la chuo ni kudahili wanachuo wapatao 30,000 ifikapo mwaka 2020. Kwa upande wao wahitimu wa fani ya Mawasiliano ya Umma Dkt. Darius D. Mkiza na Dkt. Jacob Roman Lubuza ambao pia ni wahadhiri katika Chuo Kikuu cha Tumaini Tawi la Dar es salaam wamesema kuwa watatumia elimu waliyoipaata katika kwa kufundisha vyuo vikuu, kutangaza utalii wa Tanzania, kufanya utafiti, kuandaa mitaala mbalimbali ya elimu na kutoa ushauri wa kitaalam ikiwa ni mchango wao kwa taifa kuelekea kujenga uchumi wa kati.

Tanga Cement yashinda ushindi wa jumla tuzo za NBAA kwa mwaka wa pili mfululizo

$
0
0
 
 Mhasibu Mkuu wa Serikali, Francis Mwakapalila (kulia), akikabidhi tuzo ya ushindi wa kwanza wa kipengele cha Wazalishaji katika tuzo za Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ya mwaka 2016 kwa Mdhibiti Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Isaac Lupokela, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaamjuzi. Tanga Cement pia iliibuka na ushindi wa jumla katika tuzo hizo hii ikiwa ni mwaka wa pili mfukulizo kuibuka na ushindi wa jumla.  Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, Pius Maneno. 
 Wahasibu wa Tanga Cement, Edgar Mlenge (kushoto), na Isaac Lupokela wakionesha tuzo ya mshindi wa jumla mara baada ya kampuni yao kutangazwa washindi katikaUwasilishaji Bora wa Taarifa za Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2016 jijini Dar es Salaam juzi.
 Wahasibu wa Tanga Cement, Edgar Mlenge (kulia), na Isaac Lupokela (katikati), Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa TCPLC, Mtanga Noor (kushoto), wakionesha tuzo ya mshindi wa jumla na mshindi wa kwanza kipengele cha Wazalishaji mara baada ya kampuni yao kujizolea tuzo hizo katikaUwasilishaji Bora wa Taarifa za Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2016 jijini Dar es Salaam juzi.
Mdhibiti Fedha wa Tanga Cement, Isaac Lupokela (katikati), akisakata rumba pamoja na baadhi ya waalikwa katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa tuzo za uwasilishaji bora wa mahesabu zilizoandaliwa na NBAA jijini Dar es Salaam juzi. 

ALICHOKISEMA BALOZI DR.KAMALA KWENYE ZIARA YA GHAFLA KATIKA KITIO CHA AFYA KABYAILE - ISHOZI WILAYANI MISSENYI

$
0
0

MBUNGE WA JIMBO LA NKENGE BALOZI DR.DIODORUS KAMALA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KITUO CHA AFYA KABYAILE NA KUBAINI CHANGAMOTO YA HUDUMA WATUMISHI,MIUNDOMBINU NA VITENDEA KAZI 

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAIBUKA KIDEDEA TAARIFA BORA YA HESABU KWA MWAKA 2016

$
0
0

Benny Mwaipaja-WFM, Dar es Salaam

Wizara ya Fedha na Mipango Fungu Hamsini (Vote 50)linalohusika na masuala ya utawala, limeibuka kinara kwa kupata tuzo ya mshindi wa kwanza katika utoaji wa Taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 katika kundi la Wizara na Idara za Serikali inayoandaliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).

Tuzo hizo zimetolewa kwa washindi na Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa Mkutano wa mwaka wa Wahasibu nchini uliofanyika katika eneo hilo.

CPA. Mwakapalila alisema kuwa taarifa bora za fedha ni muhimu sana katika maendeleo ya nchi kwa kuwa walipa kodi, wawekezaji na wadau wengine hutegemea taarifa hizo katika kufanya maamuzi.‘Kama taarifa za fedha hazitatolewa kwa ubora unaotakiwa na kwa wakati mwafaka kunaweza kusababisha athari katika uthabiti wa mifumo ya kifedha nchini’, alieleza CPA. Mwakapalila

Aidha Mwakapalila amewapongeza wahasibu kwa kuamua kukaa pamoja na kujadili taaluma ya uhasibu katika maendeleo ya viwanda ambayo ni ajenda ya kipaumbele kwa Serikali ya awamu ya tano.

Amesema suala la Uchumi wa viwanda ni muhimu katika kuongeza kipato na kupata fedha za kigeni kwa njia ya kuuza bidhaa nje na pia kupata mapato ya kodi na yasiyo ya kodi hivyo akatoa rai kwa wananchi kuendelea kujadili masuala ya uchumi wa viwanda na kupata namna sahihi ya kuufikia ili ndoto ya uchumi huo ziweze kuwa za kweli.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA. Pius Maneno amesema kuwa tuzo zinazotolewa na NBAA zinalengo la kuhamasisha uwajibikaji na kuandaa taarifa ya fedha zilizo na viwango vya kimataifa.

Amesema kuwa washindi wa tuzo hizo wanapatikana kupitia mchakato uliosheheni weledi wa hali ya juu kutoka kwa wabobezi wa taaluma ya uhasibu nchini ambao wanaangalia vigezo kadhaa vikiwemo kuwa na hati safi na kuwasilisha Hesabu kwa wakati na pia kufikisha kiwango cha ubora wa taarifa kuanzia asilimia 75.
Wahasibu wa Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50 wakiwa katika picha ya pamoja na Mhasibu Mkuu wa Fungu hilo Bw. Christopher Nkupama (wa pili kushoto) baada ya kupokea Tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 zilizotolewa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam .
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wahasibu wa Wizara hiyo fungu 50 baada ya kuwakabidhi tuzo hiyo katika eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, aliyeshika tuzo ni Mhasibu Mkuu wa Fungu hilo Bw. Christopher Nkupama.
Washindi wa Kwanza wa makundi mbalimbali ya Tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 zinazotolewa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) wakiwa katika picha ya pamoja na Meza kuu baada ya kukabidhiwa tuzo hizo eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mmoja wa wahasibu walioambatana na Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango-fungu 50, Bw. Christopher Nkupama (hayupo pichani) akisalimiana na meza kuu baada ya kupokea tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 iliyotolewa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji l Dar es Salaam.

RC GAMBO AWAASA WATAALAM WA UGAVI NA UNUNUZI KUZINGATIA UADILIFU KATIKA KAZI ZAO

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amewaasa wataalam wa ununuzi na ugavi kuzingatia maadili katika kazi zao za kila siku ili kuleta ufanisi katika maeneo wanayotumikia.Bwana Gambo ameyasema hayo wakati akifunga kongamano la nane la wataalam wa ununuzi na ugavi lililofanyika mkoani Arusha kwa muda wa siku mbili.

Awali akimkaribisha Mhe. Gambo kufunga kongamano hilo mwenyekiti wa PSPTB Sr. Dr. Hellen Bandiyo amemhakikishia mkuu huyo wa mkoa kwamba wao kama wataalam wa ununuzi wanao mchango mkubwa sana katika kuhakikisha malengo ya serikali ya awamu ya tano ya kuelekea uchumi wa viwanda yanafanikiwa.

“Ni jukumu la wagavi kuzingatia maadili katika maeneo ambayo tumeaminiwa ili kumsaida rais wetu Dr. Magufuli kuweza kuifikisha nchi yetu katika uchumi wa viwanda, na sisi kama wataalam wan chi hii ni lazima tujione tuna deni katika ustawi wa chi yetu” alisema Dr. Bandiyo.

Mhe Gambo aliwaasa wataalamu hao kuhakikisha wanazingatia weledi na kuitumia taaluma yao vizuri kwa ustawi wa taasisi zilizowaajiri, “Taaluma ya ugavi na ununuzi ni zaidi ya kwenda dukani na kununua, inakwenda mbali zaidi ya hapo inahitaji weledi na uadilifu ili kuleta matokeo chanya katika maeneo yetu ya kazi kwa ustawi mzuri wa taifa letu” Mhe Gambo alisema.

Aidha moja kati ya changamoto alizozipokea Mhe Gambo ni pamoja na baadhi ya waajiri kuwatumia wataalam wa manunuzi ambao hawajasajiliwa na bodi hiyo ambapo Mhe Gamboa amewataka kwa kuanzia wawasilishe orodha ya waajiri hao waliopo mkoani kwake ili aone namna ya kuwashughulikia kwa kua kufanya hivyo ni kukiuka sheria na taratibu za nchi yetu.
Mhe. Gambo akizungumza na wadau katika kongamano la nane la wataalam wa ugavi na ununuzi lililofanyika jijini Arusha wa muda wa siku mbili.
Mwenyekiti wa bodi ya PSPTB Dr. Hellen Bandiyo akizungumza katika kongamano la nane la wataalam wa ununuzi na ugavi lililohitimishwa jijini Arusha.
Mhe Gambo akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa kongamano la nane la wataalam wa ugavi na ununuzi.

SNS YAPONGEZWA KWA KUWAJALI WATU WENYE MAHITAJI MAALUM

$
0
0

Mratibu wa Elimu Kata ya Kigamboni Bibi. Angelina Ngasaswa akizungumza na wanafunzi wa Elimu ya Watu Wazima na Watu wenye uhitaji maalu wanaofundishwa chini ya uratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Suluhusho la Watu Wenye Mahitaji Maalum (SNS) wakati wa hafla ya kufunga shule hiyo mapema hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Shirika la Suluhusho la Watu Wenye Mahitaji Maalum (SNS) akizungumza na wanafunzi wa Elimu ya Watu Wazima na Watu wenye uhitaji maalum wanaofundishwa chini ya uratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Suluhusho la Watu Wenye Mahitaji Maalum (SNS) wakati wa hafla ya kufunga shule hiyo mapema hivi karibuni. Special Need Salution (SNS) ni shirika lisilo la Kiserikali limeanzisha darasa maalum kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum ili kuwakwamua kielimu, kiuchumi na kimaendeleo huko kauli mbiu yake ikiwa ni “Stawisha watu wenye mahitaji maalum.”
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tua Moyo Bw. Abdul Habibu akisisitiza jambo mbele ya wanafunzi wa Elimu ya Watu Wazima na wenye uhitaji maalum wanaofundishwa chini ya uratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Suluhusho la Watu Wenye Mahitaji Maalum (SNS) wakati wa hafla ya kufunga shule hiyo mapema hivi karibuni. Special Need Salution (SNS) ni shirika lisilo la Kiserikali limeanzisha darasa maalum kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum ili kuwakwamua kielimu, kiuchumi na kimaendeleo huko kauli mbiu yake ikiwa ni “Stawisha watu wenye mahitaji maalum.”

Katibu Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Suluhusho la Watu Wenye Mahitaji Maalum (SNS) Mwl. Sarapendo Urio akionyesha baadhi ya kazi za Wanafunzi wa Elimu ya Watu Wazima na Wenye Uhitaji Maalum wakati wa hafla fupi ya kufunga masomo mapema hivi karibuni. Special Need Salution (SNS) ni shirika lisilo la Kiserikali limeanzisha darasa maalum kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum ili kuwakwamua kielimu, kiuchumi na kimaendeleo huko kauli mbiu yake ikiwa ni “Stawisha watu wenye mahitaji maalum.”
Baadhi ya wanafunzi wa Elimu ya Watu Wazima na wenye uhitaji maalum wanaofundishwa chini ya uratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Suluhusho la Watu Wenye Mahitaji Maalum (SNS) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mara baada ya kufunga shule hiyo mapema hivi karibuni. Special Need Salution (SNS) ni shirika lisilo la Kiserikali limeanzisha darasa maalum kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum ili kuwakwamua kielimu, kiuchumi na kimaendeleo huko kauli mbiu yake ikiwa ni “Stawisha watu wenye mahitaji maalum.”

MAKAMU WA RAIS AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKU MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU KITAIFA

$
0
0
`Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameziagiza Taasisi zote zenye usimamizi kuhakikisha zinasimamia vyema jukumu lao la kutumia nafasi zao kuongeza juhudi katika kuimarisha misingi ya Utawala Bora, Uwazi, Uadilifu na Uwajibikaji. 

Makamu wa Rais aliyasema hayo leo wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa yaliofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mjini Dodoma.

Makamu wa Rais alisema Vita dhidi ya ukiukwaji wa Maadili haiwezi kupiganwa na Serikali peke yake, “Ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kuwa vitendo vya rushwa, ubadhirifu na maovu mengine vinatokomezwa”

Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kisera na kisheria ambayo itahakikisha vijana wanakuzwa kimaadili kwani hakuna Taifa Duniani linaweza kupata maendeleo bila kuwa na utamaduni unaozingatia maadili alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais alisisitiza kuwa ili kujenga Utawala Bora ni lazima kuweka uwiano wa yanayofanyika na serikali kuu hadi serikali ya mitaa nchi nzima.Serikali ilizindua Rasmi mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji Awamu ya Tatu (NACSAP III) Desemba 2016.

Makamu wa Rais alisema kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa baadhi ya Ofisi za Serikali, Serikali imeamua kufuatilia uhalali wa vyeti vya Watumishi, Idadi halali ya Watumishi wa Umma na ulipaji wa Mishahara Hewa na kusisitiza zoezi ili litakuwa endelevu.

Mwisho, Makamu wa Rais aliwaeleza wananchi na Watumishi wa Umma kwa ujumla kuwa Maadili ni nguzo muhimu katika maendeleo ya nchi yetu. “Ni imani yangu kuwa Wakuu wa Taasisi hizi kuwa mtahakikisha misingi ya haki za binadamu, utawala bora na viwango vya Maadili ya Viongozi wa Umma vinasimamiwa ipasavyo ili kuimarisha nidhamu ya Maafisa na Watumishi wa Umma”.

Kuimarishwa na kudumishwa kwa nidhamu ya utendaji, huduma zitolewazo Serikalini, Ukusanyaji wa mapato na matumizi bora ya fedha za Serikali kutaleta mafanikio katika kuelekea uchumi wa kati. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa kwenye Viwanja vya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya  Ndugu Rodgers William Sianga wakati akiwasili kwenye kilele cha maadhimisho ya siku Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa kwenye Viwanja vya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Bahame Tom Nyanduga (kulia) alipotembelea banda lao wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa kwenye Viwanja vya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Sehemu ya wahudhuriaji wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mjini Dodoma(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). 

TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAKE JUU YA MFUMO WA UNUNUZI WA LUKU

$
0
0
 Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Shirika la Umeme Tanzania Tanesco limewatoa hofu wateja wake juu ya mfumo wa ununuzi wa Umeme kwa njia ya luku na kusema kuwa kwa sasa upo sawa na wanaweza kununua katika mifumo iliyozoeleka.


Akizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam Kaimu Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano(TEHAMA)  wa Tanesco, Demetruce Dashina amesema kuwa kulitokea tatizo dogo la mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya Luku kutokana na wataalamu wa shirika hilo walipokuwa wakiamisha mitambo hiyo kutoka ofisi ya Zamani kwenda sehemu nyingine.


“Jana tulikuwa tunafanya uhamisho wa mfumo wa luku kwende katika ofisi zetu mpya hivyo ikawalazimu wateja wetu kupata usumbufu kidogo, lakini kuanzia saa saba mfumo huo umekaa sawa na wateja wanaweza kununua umeme kama walivyokuwa wanafanya hapo awali bila shida yoyote mara baada ya marekebisho ya kiufundi” amesema Dashina


Amesema kuwa shirika lilijipanga kuwahudumia wateja wake kama kawaida wakati wa kuhamisha mitambo hiyo lakini Wananchi wengi wakapata taharuki hivyo kufanya mfumo wa ziada kuzidiwa kutokana na watu kununua umeme kuliko Kawaida.


Kwa upande wake Kaimu Meneja  Uhusiano wa Tanesco Leila Muhaji amewaomba radhi wananchi kwa usumbufu uliojitokeza na kuwasisitiza kuwa sasa wanaweza kununua katika mifumo iliyozoeleka.


Muhaji amesema kuwa Tanesco inatambua umuhimu wa umeme hivyo   kuwataka watanzania kuwa na Imani na shirika lao kwani lipo kwa ajili ya kuwahudumia  kama inavyohitajika.
 Kaimu Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano(TEHAMA)  wa Shirika la Umeme nchini Tanesco, Demetruce Dashina Akizungumza na Waandishi mara baada ya kuimarika kwa mfumo wa kununua Umeme kwa njia Luku 
   Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco, Leila Muhaji akifafanua jambo wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari juu ya kuimarika kwa Mfumo wa Ununuzi wa luku mara baada ya kuhamia sehemu nyingine. 
Waandishi wa habari habari walifika katika mkutano huo wakifatilia kwa Makini.

MAMIA WAMUAGA MWANAHABARI JOYCE MMASI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

VILIO Majonzi na simanzi vilitawala   wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa mwanahabari nguri Joyce Mmasi iliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

Katika ibada hiyo mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wanahabari na wadau wengine walijitokeza katika viwanja hivyo kwa ajili ya kumuaga mpendwa wao Joyce Mmasi ambaye alikuwa akifanyia kazi katika gazeti la Mwananchi.

Mchungaji Kulwa kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambaye aliongoza ibada hiyo aliwaambia watu waliokuwepo kwenye ibada hiyo kuwa wanapaswa kujitayarisha wakati wote kwani hawajui ni lini wataondoka hapa duniani."Mwenzetu Joyce ametutangulia tulikuwa naye pamoja lakini wewe uliye hai leo hii umejiandaeje katika maisha ya kiroho?" alisema Mchungajia Kulwa.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rachel Mhando alisema kifo cha Mmasi kimemshitua kila mtu na wanahabari wamepata pigo la kumpoteza mwenzao.Mhando alihimiza kudumisha upendo kwa watu wote pamoja na wanahabari.

Katika ibada hiyo makundi mbalimbali yalijitokeza kutoa salamu za rambirambi na kuhudhuriwa na viongozi wa dini, siasa, serikali na wadau wengine.Mwili wa marehemu Joyce umesafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro nyumbani kwao kwa mazishi.

Marehemu ameacha mume na watoto watatu, Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu.
 Marehemu Joyce Mmasi enzi za uhai wake.
 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mwanahabari Joyce wakati ukiwasili viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo kwa ibada ya kuuaga kabla ya kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.
 Wanahabari wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Familia ya marehemu ikiwa katika ibada hiyo. Kulia ni mtoto wa kwanza wa marehemu, Lawrence Nicky Mayella.
 Mume wa marehemu Joyce Mmasi, Andrew Kamugisha akizungumza kwenye ibada hiyo.
 Waandishi wa habari wanawake wanaounda kikundi cha Wawata wakitoa neno katika ibada hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

VIDEO: KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AELEZEA NAMNA MSAMAHA WA RAIS KWA WAFUNGWA ULIVYOPOKELEWA

MAGAZETI YA JUMATATU LEO DECEMBER 11,2017

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT MAGUFULI ALIVYOFUNGUA MKUTANO MKUU WA TISA WA UVCCM MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM baada ya kuufungua katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM baada ya kuufungua katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wageni kutoka vyama rafiki toka nchi mbalimbali baada ya kufungua mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akifungua rasmi mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wa meza kuu wakimsikiliza mwanachama mpya Ndg. Alfred Msando akisalimia wajumbe wa mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM baada ya kuufungua katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017
:Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na aliyekuwa mbunge wa Kinondoni na mwanachama mpya Ndg. Maulidi Mtulia baada ya kusalimia wajumbe wa mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo mbele ya wajumbe wa mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi meza kuu wakiimba na kucheza nyimbo za hamasa pamoja na wajumbe wa mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM baada ya kuufungua katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi meza kuu wakiimba na kucheza nyimbo za hamasa pamoja na wajumbe wa mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM baada ya kuufungua katika Ukumbi wa Julius Nyerere mjini Dodoma leo Novemba 10, 2017.

PICHA NA IKULU

IGP SIRRO ATEMBELEA KIKOSI 673 CHA JESHI LA WANANCHI MKOANI DODOMA.

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati) akikagua maandalizi ya JWTZ Kikosi cha 673 katika harakati za maandalizi ya kuamia mkoani Dodoma na alietangulia mwenye nguo nyeusi CEO Meltus Franci akimuonyesha IGP maeneo mbali mbali ya kikosi hicho. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro kushoto akiwa na mwenyeji wake CEO Meltus Franci, akikagua ujenzi wa gharama nafuu katika Kikosi 673 ili kuupata ujuzi huo kutoka JWTZ na Jeshi la Polisi watumie ili kupunguza gharama za Nyumba za Askari mkoani Dodoma katika harakati za kuamia mkoani humo. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro kushoto akiwa na mwenyeji wake CEO Meltus Franci, akikagua ujenzi wa gharama nafuu katika Kikosi 673 ili kuupata ujuzi huo kutoka JWTZ na Jeshi la Polisi watumie ili kupunguza gharama za Nyumba za Askari mkoani Dodoma katika harakati za kuamia mkoani humo. Picha na Jeshi la Polisi.

SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR (ZMCL) LATILIANA SAINI USHIRIKIANO NA KITUO CHA UTANGAZAJI CHA CCTV CHA CHINA

$
0
0
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa CCTV Li Yi (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa ZMCL Muhammed Seif Khatib wakitiliana sainai makubaliano ya ushirikiano baina ya vituo hivyo viwili vya utangazaji katika sherehe zilizofanyika Ofisi za ZMCL Mombasa Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa ZMCL Muhammed Seif Khatib akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar Naibu Mkurugenzi Mkuu wa CCTV mara baada ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano baina ya Taasisi hizo mbili za utangazaji katika sherehe zilizofanyika Ofisini kwao Mombasa Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZMCL) Muhammed Seif Khatib (kati kati kushoto) akiongoza mazungumzo ya ushirikiano baina ya Shirika hilo na Channel ya Televisheni ya China {CCTV) yaliyofanyika ukumbi wa Shirika hilo Mombasa ambapo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa CCTV Li Yin (wa pili kulia) aliongoza ujumbe kutoka China.
Mkurugenzi Mtendaji wa ZMCL Muhammed Seif Khatib akiwatembeza watendaji wa CCTV studio za kutangazia za Redio za shirika hilo kabla ya kutiliiana saini makubaliano ya ushirikiano baina ya Taasisi hzo mbili za utangazaji.Picha na Ramadhani Ali Maelezo Zanzibar

JUMUIYA YA KUKUSANYA ZAKA NA SADAKA (JUZASA) YAANDAA WARSHA KWA WAFANAYABIASHARA ZANZIBAR

$
0
0
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima Mohd Hafidh akifungua warsha ya siku moja ya kuwaelimisha wafanyabiashara wa kiisalamu umuhimu wa kutoa zaka kwa njia iliyosahihi ili kupata radhi Mwenye ez Mungu katika Ukumbi wa Shantimba Mombasa Mjini Zanzibar.
Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu Sheikh Jabir Haidara Jabir akitoa mada ya umuhimu wa kutoa zaka na faida zake katika warsha iliyoandaliwa na Jumuiya ya JUZASA katika Ukumbi wa Shantiba Mombasa Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa JUZASA Sheikh Said Suleiman (Gwiji) akitoa maelezo juu ya malengo ya Jumuiya hiyo katika warsha iliyoandaliwa ya kuhamasisha wafanyabiashara kuelewa umuhimu wa kutoa zaka katika Ukumbi wa Shantiba Mombasa Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.

JWTZ WAZUNGUMZIA VIFO VYA WANAJESHI 14

$
0
0
Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania limesema kikundi chake cha ulinzi na usalama kilichopo DRC kwaajili ya kutekeleza jukumu la ulinzi na amani kilivamiwa na Waasi waliojilikana kuwa ni ADF na kusababisha mauaji kwa wanajeshi 14.

Amesema kwamba tukio hilo lilitokea katika eneo la kambi iliyopo daraja kwenye mto Simulike barabara ya kutokea Oicha kwenda Kamango mpakani mwa nchi ya Uganda Kaskazini Mashariki ya wilaya ya Beni Jimbo la Kivu Kaskazini.

Akithibitisha mauaji hayo muwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania (CDF) Luteni Jenerali James Mwakibolwa amesema shambulio hilo lakuvamiwa lilizusha mapigano baina ya kikundi hicho na kile cha waasi na yalidumu kwa takribani masaa kumi na tatu (13) na kusababisha vifo vya askari wa Tanzania 14 na wengine 44 kujeruhiwa na askari wawili bado hawajulikani walipo ambapo jitihada zaidi za kuwatafuta zinaendelea.

Amesema shambulizi la tarehe 7 kuamkia tarehe 8 Desemba lilikua baya zaidi kuwahi kuitokea tangu vikosi hivyo vianze kushiriki ulinzi wa amani nchini DRC mwaka 2011 kwakua limeleta madhara makubwa, hata hivyo kikundi hicho ambacho bado kipo huko kinauwezo mkubwa wa kutekeleza majukumu husika kwa uhodari wa hali ya juu ,ushupavu, weledi mkubwa na umahiri stahiki.

Kwa niaba ya mkuu wa majeshi Luteni Jenerali Mwakibolwa amewathibitishia watanzania kuwa tukio hilo halitawavunja moyo na kamwe Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania halitatetereka kupeperusha bendera yake ndani na nje ya nchi kwani tukio hilo limewaongezea nguvu, ari ,ushupavu na uhodari zaidi katika kutekeleza majukumu yake.

Aidha amesema nchi pia iko salama na itaendelea kuwa salama na yeyote ambaye anataka kuwajaribu atashughulikiwa ipasavyo kwani historia ya jeshi inadhihirisha uwezo thabiti.

Kuhusu taratibu za kusafirisha miili ya marehemu kuirejesha nchini zinafanyika chini ya utaratibu wa Serikali na umoja wa mataifa na JWTZ na serikali wanaendelea kuchukua hatua stahiki kufuatia tukio hilo ikiwemo kufanya uchunguzi katika eneo husika sambamba na kuangalia taratibu za kuwajulisha familia za wafiwa zimekamilika na ndio maana hawakuweza kutoa taarifa hizo bila kuwaweka sawa familia za mashujaa hao.

Kwa umoja wa watanzania amewataka kuwaombea dua roho za mashujaa hao zipumzike mahali pema peponi kwa amani na majeruhi wote wapone haraka iwezekanavyo ili warejee kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa ulinzi wa taifa na dunia nzima.

mkuu wa mkoa wa Geita atembelea maonesho ya viwanda ya pili jijini Dar es Salaam.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ndugu Robert Gabriel akipata maelezo ya Wizara kutoka kwa Bibi Jane Lyatuu alipotembelea banda la wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika maonesho ya Viwanda vya Tanzania vya Tanzania yanayofanyika Viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es salaam.

 Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ndugu Robert Gabriel akipata maelezo ya namna TANTRADE inavyosaidia sekta ya asali kupenya kwenye masoko ya ndani nan je. kutoka kwa Bi Elizabeth Haule Afisa Biashara wa taasisi hiyo. 

   Mkurugenzi Utumishi Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar ndugu Mohamed Jaffary Jummanne akipata maelezo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bibi. Veronica Ngerageza.

HDIF YAWAWEZESHA WAKAZI WA MAGANZA KISHAPU KUPATA MAJI SAFI

$
0
0
 Mtaalamu wa maji wa Shirika la ICS....linalotekeleza mradi wa kusambaza maji safi na salama kwa kutumia teknolojia ya malipo kabla unaofadhiliwa na HDIF akielezea jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi.Kushoto ni kiongozi msaidizi wa HDIF  Be.Joseph Manirakiza
 Matanki ya maji yaliyojengwa na ICS kwa ufadhili wa HDIF katika kijiji cha Maganzo yanayosambazwa katika vibanda vya maji 25 vinavyotumia teknolojia ya walipo kabla.
Wananchi we Maganzo kata ya Kishapu Shinyanga wakielezea muhimu wa mradi wa kusambaza maji safi na salama kwa kutumia teknolojia ya malipo kabla unaofadhiliwa na HDIF .

TATU MZUKA YAUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA KUBORESHA NA KULINDA USAFI WA MAZINGIRA NCHINI

$
0
0
 kampuni ya The Net Work inayochezesha mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka mwishoni mwa wiki imeadhimisha miaka 56 ya Uhuru kwa kufanya usafi wa mazingira katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kawe Beach,Kinondoni jini Dar Es Salaam.
Akizungumza wakati wa shughuli hizo za usafi,Mratibu wa mawasiliano kutoka kampuni ya The Net Work inayochezesha mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka ,Kemi Mutahaba amesema kuwa wameamua kufanya usafi kwa kushirikiana na baadhi ya Wadau kwa kujitolea,lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika suala zima la kuboresha usafi wa mazingira yetu.
"Tumejitolea kufanya usafi katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kawe Beach,lengo likiwa ni kutunza mazingira na kuweka mazingira yetu safi, lakini pia ikiwa sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika suala zima la kuboresha na kuyaweka mazingira yetu kuwa safi wakati wote",alisema Kemi.
Kemi alisema yote hiyo ni kuhakikisha wanasimamia mlengo wa kampuni yao,waliounzisha katika suala zima la kusaidia kulinda mazingira,ambapo hivi karibuni walichangia kwa kuikabidhi Serikali kiasi cha fedha milioni 100 ili zitumike  katika kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani kupitia mpango maalum ambao Serikali iliishauandaa.
Amesema kuwa Kampuni yake itaendelea kuunga mkono Serikali kwa kuhakikisha kuwa wanachangia katika shughuli za maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo mazingira.
Baadhi ya Wadau na wafanyakazi kutoka kampuni ya
The Net Work inayochezesha mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka wakiadhimisha miaka 56 ya Uhuru kwa kufanya usafi wa mazingira mwishoni mwa wiki katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kawe Beach,Kinondoni jini Dar Es Salaam.
Baada ya kumaliza kufanya usafi wakafurahi kwa pamoja
Shughuli ya usafi ilifanyika kwa umakini kuhakikisha eneo la Fukwe linabaki safi.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images